1 Jun 2009


NIMEMALIZA KUSOMA RIWAYA YA KWANZA YA MATUKIO YA KWELI (NON-FICTION) KWA MTUNZI MAHIRI WA RIWAYA ULIMWENGUNI,JOHN GRISHAM.BINAFSI,GRISHAM NA SIDNEY SHELDON NDIO WALIOJAZA KIJIMAKTABA CHANGU CHA VITABU MBALIMBALI.NILIANZA KUSOMA RIWAYA ZA LUGHA YA KIINGEREZA NILIPOKUWA SHULE YA MSINGI,NA SHUKRANI ZIMWENDEE BABA MZEE CHAHALI KWA KUTUSIMULIA WANAWE YALIYOMO KWENYE RIWAYA YA JAMES HADLEY CHASE YA COME EASY GO EASY,KISHA NIKAJITUTUMUA KUISOMA MWENYEWE NA KUFANIKIWA KUELEWA.TANGU MUDA HUO,MIE NA NOVELS TUMEKUWA DAM DAM.KWA UJUMLA MIONGONI MWA INTERESTS ZANGU NI PAMOJA NA KUSOMA VITABU PAMOJA NA UANDISHI BUNIFU (CREATIVE WRITING).

RIWAYA HIYO YA GRISHAM INAITWA THE INNOCENT MAN.PASIPO KUINGIA KWA UNDANI ZAIDI,INAHUSU SHERIA INAPOKWENDA MRAMA.MWAKA 1982 YALITOKEA MAUAJI YA BINTI AITWAYE DEBRA CARTER KATIKA MJI MDOGO WA ADA,PONTOTOC COUNTY JIMBONI OKLAHOMA POLISI WAKASUASUA KUMPATA MUUAJI,"KESI IKABAMBIKWA" KWA RON WILLIAMSON (MHUSIKA MKUU KATIKA STORI HIYO) AMBAYE KIMSINGI ALIKUWA NA MATATIZO YA AKILI,HALI AMBAYO ILIPELEKEA "AKIRI KUWA MUUAJI" LAKINI KATIKA SIMULIZI YA NDOTO ALIYOOTA USIKU MMOJA.RAFIKI YAKE WA KARIBU,DENNIS FRITZ NAE AKAFANYWA MTUHUMIWA NAMBARI MBILI,KWA VILE TU "RAMLI YA POLISI" (KAMA HIYO ILIYOPIGWA KWENYE
AJALI YA MWAKYEMBE) ILIONYESHA KUWA ISINGEKUWA RAHISI KWA MAUAJI HUSIKA KUFANYWA NA MTU MMOJA.HATIMAYE,RON ALIHUKUMIWA KIFO NA KUPELEKWA DEATH ROW NA DENIIS ALIHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA.KUSALIMIKA KWA "WAUAJI HAO" NI TEKNOLOJIA YA D.N.A AMBAYO ILIONYESHA KUWA HAWAKUHUSIKA NA MAUAJI HAYO.

SI LENGO LANGU KUWASIMULIA SIMULIZI KUTOKA KWENYE RIWAYA BALI THE INNOCENT MAN IMENIFANYA NIJIULIZE KUHUSU HUKUMU YA KWENDA JELA MIAKA 11 ALIYOPEWA ALIYEKUWA HAKIMU WA MAHAKAMA YA WILAYA YA TEMEKE,
JAMILA NZOTA.MWANAMAMA HUYO ALIKUTWA NA HATIA YA KOSA LA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA YA SHILINGI LAKI 7 (AWALI ALIDAI MLUNGULA WA SHS MILIONI 4).

HAKI IMETENDEKA.LAKINI KWA UPANDE FLANI INAWEZEKANA HAKI HAIJAONEKANA KUTENDEKA,SI KWA HAKIMU NZOTA BALI WALE ALIOWAHI KUWAHUKUMU WAKATI WA UTAWALA WAKE.HIVI HAKUNA UWEZEKANA KWAMBA TUKIO LILOPELEKEA HAKIMU HUYO KUKAMATWA NA MLOLONGO WA MATUKIO KADHAA KATIKA MAISHA YA UHAKIMU WA JAMILA?MAANA WASWAHILI WANAPOSEMA ZA MWIZI NI 40 WANAMAANISHA PIA KUWA MWIZI ANAENDELEA NA WIZI WAKE HADI ITAPOJIRI HIYO 40

KATIKA MANTIKI HIYOHIYO,KUKAMATWA KWA HAKIMU HUYO KULIKUWA NI SAWA NA 40 YA "WIZI" WAKE,LAKINI PIA KULIASHIRIA MWISHO WA SHUGHULI ILIYOANZA AT A CERTAIN POINT OF TIME.MIMI NA WEWE HATUJUI NI LINI LAKINI YAYUMKINIKA KUAMINI KUWA KUNA HUKUMU ZILIZOTOLEWA NA HAKIMU HUYO AMBAZO ZILIKUWA INFLUENCED NA "MCHEZO" WAKE WA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA.HAPA KUNA MAWILI:KUNA WALITOA RUSHWA ILI WASIKUTWE NA HATIA KATIKA HUKUMU ZA HAKIMU NZOTA,NA KUNA WALIOHUKUMIWA KWENDA JELA LICHA YA KUWA HAWANA HATIA LAKINI WALISHINDWA KUTOA RUSHWA KWA HAKIMU HUYO.

SISHANGAI KWANINI HABARI YA KIFUNGO CHA HAKIMU HUYO IMESHASAHAULIKA.NDIO TANZANIA YETU HIYO.LICHA YA AMANI NA TULIVU,TUNASIFIKA PIA KWA USAHALIFU HATA KATIKA MAMBO YANAYOWEZA KUWA NA MADHARA MAKUBWA MBELENI.TUNGETARAJI VIKUNDI VYA UTETEZI WA HAKI ZA BINADAMU AU TAASISI ZA KISHERIA ZISHIKILIE BANGO KUHUSU MAPITIO (REVIEWS) YA HUKUMU ZILIZOTOLEWA NA HAKIMU HUYO.LAKINI KATIKA UTAMADUNI WA LAISSEZ FAIRE,NDIO "IMETOKA HIYO" KAMA WASEMAVYO WATOTO WA MJINI (ILA SINA HAKIKA KAMA MSEMO HUU BADO UNATUMIKA AS KISWAHILI KINAKUA KWA KASI YA TSUNAMI).

NI UTAMADUNI HUU WA "BORA LIENDE" UNAOIMARISHA UNYONGE WA WATANZANIA NA KUDUMISHA ULAFI WA MAFISADI KATIKA KILA NYANJA.NI UTAMADUNI HUU TUTAKAOUSHUHUDIA TENA MWAKA KESHO WAKATI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI AMBAPO WABABAISHAJI WALEWALE WALIOAHIDI BAKULI ZA MAZIWA NA ASALI HAPO 2005 (LAKINI WAKAISHIA KUTUMWAGIA UJI WA MWAROBAINI NA SHUBIRI) WATAKUJA TENA NA AHADI ZILEZILE,ILA ZIKINOGESHWA NA UONGO KUWA TUMEJIPANGA VYA KUTOSHA.BADALA YA BAKULI ZENYE MAZIWA NA ASILI TUMEAMUA KUWAJENGEA MABWAWA KABISA YATAKAYOKUWA YAKITIRIRIKA MAZIWA NA ASALI 24/7.WATAKAPOULIZWA KWANINI AWALI WALIAHIDI HIVYO NA BADALA YAKE WAKATOA MWAROBAINI NA SHUBIRI,WATAJIBU KISIASA KUWA MCHAKATO WA UTEKELEZAJI ENDELEVU WA BLAH BLAH BLAH NDIO ULIPELEKEA HIVYO LAKINI SASA KILA KITU KIKO TAYARI...TUPENI KURA ZENU ILI MFAIDI UHONDO KWENYE ARDHI YA MAZIWA NA ASALI....NA WATAPEWA.

TUMEROGWA?

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube