18 May 2010

Ofkoz,Mtukufu Rais Jakaya Kikwete alikuwa anatania alipotetea rushwa hadharani kwa kudai takrima haikwepeki.Ndio,Rais alikuwa anatania,na ndo maana,Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwa amekaririwa na magazeti kadhaa akimtetea JK kuwa "kauli yake (JK) kuhusu takrima (rushwa) ilikuwa utani tu".Pengine neno 'utani' kwa mujibu Tendwa linaweza kuwa na maana kubwa zaidi tukilitafsiri katika informal English.Kwenye kamusi,'joke' (informal) inamaanisha An object of amusement or laughter; a laughingstock.Kwa Kiswahili,ni 'kituko', 'kioja' au 'kitu cha kuchekwa'.

Lakini kwa namna siasa zetu zilizvyojaa vituko (jokes) si ajabu Tendwa alikuwa serious kumtetea bosi wake JK.Na inawezekana kabisa Msajili huyo wa Vyma vya Siasa anayepaswa kufanya kazi bila upendeleo anaamini kwa dhati kuwa rais wetu alikuwa anataniana tu na viongozi wa dini.Kama ni hivyo,basi nae ni kituko pia.Haiingii akilini kwa kiongozi wa nchi kukutana na watu muhimu katika jamii yetu (viongozi wa dini) na kufanya 'utani mbaya' kama huo.Kulikuwa na umuhimu gani basi wa rais kuhudhuria mkutano huo kama lengo lilikuwa kutoa utani tu?Si angeweza kuwapigia simu kwa wakati wake kisha akawarushia utani huo!

Kwa bahati mbaya,au makusudi,'utani huo mbaya' ushaanza kusahaulika miongoni mwa Watanzania wengi.Siwezi kuwalaumu walalahoi ambao wako bize na kuhakikisha mkono unaenda kinywani,lakini nashindwa kujizuia kuwashangaa Watanzania wenzetu walio katika 'tabaka la kati' (middle class) kwa kuweka umuhimu zaidi kwenye ishu kama tuzo za Kili,ujio wa Sean Kingston,'kujirusha',nk ilhali tabaka la chini linalohitaji sapoti yao likizidi kuangamia.Wengi wa walio katika tabaka la kati wako bize zaidi 'kuishi kama tabaka tawala' (hata kama hiyo itamaanisha wakope kwa ndugu na marafiki au wajihusishe na ufisadi) kuliko kupambana na 'tabaka tawala' (tabaka la juu) 'kusawazisha uwanja' (to level the ground) kwa minajili ya kujenga jamii yenye kukaribia usawa.


Sijui tunaelekea wapi,lakini lililo bayana ni kwamba hatma ya taifa letu iko mashakani.Ukiona mkuu wa nchi anaongea pasi hofu (na kicheko juu,kama kawaida yake) kuwa takrima (ambayo ni jina la kistaarab la rushwa) haikwepeki.Tafsiri pana ya kauli hiyo ya 'Chaguo la Mungu' ni mithili ya kuhalalisha uhalifu kwa vile rushwa ni kosa la jinai.Lakini binafsi sishangazwi sana na kauli hiyo ya 'mwenye nchi' kwa vile alishawahi kutamka bayana kuwa 'anajali haki za binadamu za mafisadi' alipohutubia Bunge Agosti mwaka 2008Kusoma habari kamili kuhusu utetezi wa Tendwa kwa Kikwete BONYEZA HAPA na HAPA.

1 comment:

  1. Huyo ndiyo Rais anategemewa kuleta maendeleo Tanzania kwa kuleta mzahaa katika mambo makini...natambua JK na kundi lake na watu kama Tendwa wanawakejeli hao watanzania milioni arobaini lakini wakumbuke hakuna marefu yasiyokuwa na ncha..

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube