17 Oct 2010

Moja ya mambo yaliyokuwa yakiwaumiza vichwa wafuasi wa Barack Obama wakati wa kinyang'anyiro kati yake na Hillary Clinton kupata mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democrats mwaka 2008 ni theory inayofahamika kama Bradley Effect.Kwa kifupi kabisa,Bradley Effect (au Wilder Effect) ni hali inayoweza kutokea kwenye kura za maoni katika chaguzi nchini Marekani panapokuwa na mgombea Mweupe (White) na asiye mweupe (non-White).Pengine ili wasionekane wabaguzi wa rangi,wahojiwa Weupe katika kura za maoni hueleza kuwa chaguo lao ni mgombea asiye Mweupe au husema kuwa hawajafanya uamuzi kuhusu chaguo lao (Undecided).

Kwahiyo,matokeo ya kura ya maoni yanaweza kuonyesha mgombea asiye Mweupe anapendwa zaidi kuliko mgombea Mweupe lakini inapofika kwenye hatua ya kupiga kura (ambapo mpiga kura anakuwa peke yake),wapiga kura Weupe wanampigia Mweupe mwenzao.

Asili ya Bradley Effect ni katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa uchaguzi wa gavana wa jimbo la California mwaka 1982 ambapo licha ya mgombea Mweusi,Meya wa Jiji la Los Angeles Tom Bradley kuongoza kura za maoni,aliishia kushindwa uchaguzi huo kwa mgombea Mweupe George Deukmejian.

Baadhi ya wachambuzi wa chaguzi nchini Marekani wanaamini pia kuwa Bradley Effect ilijitokeza tena kwenye mchakato wa kumpata mgombea wa chama cha Democrats kwenye jimbo la New Hampshire ambapo licha ya Obama kuongoza katika kura za maoni,Hillary Clinton aliibuka mshindi kwenye jimbo hilo (japokuwa baadaye Obama alifanikiwa kuibuka mshindi wa jumla,na kupitishwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Democrats,na hatimaye kushinda nafasi ya urais).

Katika post hii najaribu kubashiri (hypothesize) namna Bradley Effect inavyoweza kuwa sababu ya mgombea wa CCM,Jakaya Kikwete,kuongoza katika tafiti za  taasisi za Redet na Synovate kuhusu nafasi za wagombea urais katika uchaguzi mkuu wa Tanzania hapo Oktoba 31.Hapa ntawazungumzia wagombea wawili tu,Kikwete na mgombea urais kwa tiketi ya Chadema,Dokta Wilbroad Slaa.

Japo Bradley Effect 'halisi' inahusu mgombea Mweupe na asiye Mweupe,sababu inayopelekea matokeo ya kura kutorandana na mwelekeo wa kura za maoni inaweza kutumika kuelezea kwanini kura za maoni za Redet na Synovate zilimpa Kikwete ushindi na sio Dokta Slaa.Kama ilivyo kwenye chambuzi mbalimbali,kuna mambo flani inabidi 'kupuuzwa' ili kufikia matokeo yanayokusudiwa.Katika uchambuzi huu,naomba 'nipuuze' urafiki kati ya taasisi hizo na CCM na badala yake nikazanie kwenye uwezekano wa Bradley Effect pekee.

Inawezekana kabisa kuwa wahojiwa kwenye tafiti za Redet na Synovate ni wananchi waliotoa majibu 'kuwaridhisha watafiti',yaani walisema wanampenda zaidi Kikwete kuliko Dokta Slaa.Moja ya sababu za kutoa majibu ya aina hiyo ni mazingira halisi ya Tanzania ambapo licha ya 'siasa za mkono wa chuma' za zama za chama kimoja kuonekana kama historia,ukweli unabaki kuwa baadhi ya wananchi wanaamini kuwa kusema lolote lisilowapendeza watawala ni kujitafutia matatizo.

Naomba kufafanua kidogo katika hilo.Nilipokwenda Tanzania mwaka 2005 kufanya fieldwork ya utafiti wangu wa shahada ya uzamifu (PhD) nilikumbana na wakati mgumu kuwahoji baadhi ya maustaadh (mada yangu inahusu masuala ya Waislam na Uislam nchini Tanzania) kwa vile baadhi yao walidhani mie ni wakala wa serikali niliyetumwa kuwachunguza ili 'serikali iweze kuwadhibiti zaidi'.Bahati mbaya,fieldwork hiyo ilifanyika wakati jeshi la polisi lilikuwa linamsaka mwanaharakati wa Kiislam,Sheikh Issa Ponda.Ilichukua kitambo kujenga uaminifu kati yangu na maustaadh hao.

Kuna wanaoilaumu Redet na Synovate kuhusu aina ya watu waliohojiwa wakidai kuwa huenda wahojiwa walikuwa watu walio karibu na CCM (kwa mfano mabalozi wa nyumba kumi).Uwezekano wa Bradley Effect  'yetu' (yaani isiyohusiana na ishu za ubaguzi wa rangi) ni mkubwa kwa vile wahojiwa wanaweza kutoa majibu yasiyoonyesha 'wanambagua mgombea wao' na hivyo kusema huyo ndio chaguo lao japo mioyoni wana dhamira na/au chaguo tofauti.

Of course,inawezekana tafiti hizo za Redet na Synovate 'zilipikwa' ili kuendana na matakwa ya CCM.Inawezekana pia kuwa aina ya watu waliohojiwa ni ambayo isingetoa majibu tofauti na 'ushindi kwa Kikwete'.Lakini,kama makala hii inavyojaribu kubashiri,inawezekana kabisa kuwa wahojiwa 'waliwazuga' jamaa wa Redet na Synivate 'ili isiwe shida'.Nani yuko tayari kuona genge lake au kibanda cha biashara kinabomolewa kwa vile tu amechoshwa na namna CCM inavyozidi kuahidi maisha bora lakini wanaonufaika ni mafisadi pekee?Mtu wa aina hii haoni shida 'kudanganya leo' kisha 'akaungama siku ya kupiga kura' kwa 'kumwadhibu Kikwete na CCM kwenye sanduku la kura ambapo hakutokuwa na wa kumtoa mimacho kwanini hajampigia kura Kikwete au CCM'.

Huu ni ubashiri tu.Unaweza kuwa sio sahihi lakini kama zilivyo bashiri nyingine-hususan zinazoambatana na mifano hai-unaweza kuwa na ukweli ndani yake.Kadhalika,Bradley Effect 'yetu' inaweza kutoa matokeo ya kuwashangaza wote wenye imani kuwa CCM na Kikwete watarudia kupata ushindi wa kishindo kama wa mwaka 2005.

Pengine kuna watakaohoji kwanini Bradley Effect 'yetu' haiwezi kutumika kwenye utafiti mwingine (wa TCIB) unaoonyesha kuwa Dokta Slaa anaongoza.Jibu langu ni kwamba watoa maoni hawana cha kupata (nothing to gain) kuwadanganya watafiti kuwa wanampenda Dokta Slaa wakati ukweli wanayempenda ni Kikwete.Likewise,kwenye tafiti za Redet na Synovate,inawezekana baadhi ya wahojiwa walikuwa na cha kupoteza laiti wangesema hawampendi Kikwete (si unajua kuhusu umoja na mshikamano ndani ya chama?).Vilevile,yawezekana wahojiwa hawakuwa na cha kupoteza (nothing to lose) kwa kudanganya kuwa wanampenda Kikwete (kwa minajili ya kuwaridhishwa watafiti na 'kulinda ugali wao') kisha wakamnyima kura katika usiri wa chumba cha kupigia kura.

Mwisho,naomba kusisitiza tena kuwa hypothesis hii imejaribu kupuuza sababu za 'wazi' kama vile upendeleo wa watafiti,uoga wa wahojiwa,na kubwa zaidi,UCHAKACHUAJI.

7 comments:

  1. KULIKONI hebu jaribu kuwashauri chadema ku-update website yao na kuweka habari zote za kila siku za mambo wanayofanya na yaliotokea kwenye kampeni. wajaribu pia kuweka hotuba za wagombea wote wa chadema wa ubunge na rais mtarajiwa Dr. Salaa. Inakuwa haina maana wanakuwa na website lakini wanaiendesha kama website ya CCM isiyokuwa na habari hata moja mpya. Waambie waweke sera zao kwenye mtandao watu waone jinsi wanavyotaka kubadilisha nchi. Vitu kama katiba kubadiolishwa waambie waonyeshe ubovu wa katiba tuliokuwanayo na waeleze kila kipengere cha kubadilisha na kwanini. Lets be seriou so we can have our country back. Waonyeshe jisni gani CCM isivyothamini maamuzi ya wananchi wanapowachagua wagombea wanaowataka lakini the so called kamati ya NEC inabadilisha majina ya washindi na kuwaweka watu wanaowataka wao kwa sababu zao. Inakuwaje NEC inafanya kazi ya mahakama? Kama kunamgombea anayesadikika kuwa amevunja sheria au kama wanavyodai kuwa baadhi ya wagombea sio raia mara tu baada ya kushinda kura za maoni si kazi ya mahakama kuamua kwa kosa lililotendeka? Inakuwaje NEC wawe nauwezo wakuondoa majina ya watu eti kwasababu inasemekana walitoa rushwa? Kwani kama kutoa rushwa ni kosa kwa sheria za nchi mahakama si ndio ilikuwa inatakiwa kutoa maamuzi badala ya NEC? Unaweza kufikiri ni too late lakini kama chadema wakitumia mtandao vizuri na TV na redio inaweza kubadilisha kabisa matokeo ya uchaguzi ujao. Wanatakiwa wachukue kila hoja ambayo inaubovu na wakuwaonyesha wananchi wa kawaida wao watafanyanini na kwajinsi gani. I have alot to offer i wish i had your direct contact.

    ReplyDelete
  2. Ahaa, sasa nimekuelewa Chahali kutokana na maelez yako hapo juu.Kumbe kwako ni chuki binafsi tu dhidi ya amani iliyodumu nchini, na utawala wa CCM, kwa hiyo kwa namna yoyote ile daktari mtarajiwa unataka kuona CCM inaangushwa madarakani na Chadema inatawala. Sijakusikia ukiitaja NCCR au CUF kwa hiyo nimekuelewa kuwa wewe ni mwana Chadema. ubarikiwe..zimebaki siku 12 tukuonyeshe surprise

    ReplyDelete
  3. Nilidhani Laiza hupo kwenye dozi ya kupna kichaa, naona umerudi huku mtandaoni ungali hajamalizia dozi ya kichaa chako. Au umeshindwa kununua dozi kamili kwa sababu kutkowa na pesa kutosha kupata dozi kamili, na kama sasa ilivyokuwa mazoea kwa watanzania wapenda CCM kama wewe kushindwa kupata dozi kamili ya matibabu na kusingizia dawa zina ubora wa chini hivyo haziponyeshi magonjwa kama huu wa ugonjwa akili unakukabili wewe laiza....Kinachotakiwa siyo chama kikibwa tunachohijitaji watanzania fair and balance political power...na pia kubwa zaidi fedha za umma zitumike kwa ajili aya umma na taratibu zilizopo na siyo familia moja ama kikundi cha watu...Wahalifu wanatakiwa nyumba yao ni jela na siyo ikulu au kuitwa wastaafu wangalia hawastaili kuitwa hivyo. Ni kweli inayoweza kushinda kwa sababu viongozi wake wanaogopa madhambi yao hivyo wapao tayyari kutumia mbinu yoyote ile iwe chafu aua nzuri ili mradi waoneyshe wao ni washindi bila kujalai athari zake katika jamamii, na hiyo ndiyo sifa watenda maovu huwa ahwajali matokeo yake. CCM ndiyo itkayoleta vita Tanzania na siyo mtu mwingine, Wengine wote wanatahadharisha jamii kuwa matendo ya CCM ni mabaya na matokeo yakee ni vita..Mifano imeonekana Ivory Coast, Siera leon, Somalia, Afrika ya kati....Kwa hiyo unazijua hizo nchi na histori ya machafuko yake utaelewa kwa nini wanaoitwa wapinzania wanakemea vitendo na mbinu chafu za CCM kushinda uchaguzi na mdhara yake kw asababu wanafahamu mzuri kuhusu haya.

    ReplyDelete
  4. Nimeipenda hayo maoni anonymous wa 19.10.2010 saa 06.04.

    Ni kweli media is a powerful tool from this morden life. Chadema wake up and make the most of it from media technology point of view to highlite all dirty issues going on....

    God Bless ordinary Tanzanian and purnish all ppl like Laiza and its followers CCM top leaders

    ReplyDelete
  5. Laiza huwezi kumwelewa Chahali wakati hujielewi mwenyewe. Hakuna cha chuki bali uoni wa mbali unaoonekana kuwa utata kwa upogo wako. Kutotaja CUF na NCCR au vyama vingine visivyo na mvuto siyo kuvichukia.

    ReplyDelete
  6. Mzee Mhango hapo hupo sahihi kabisa unachosema, kuuelewa na nayo suala lingine ingawa naamini huyu Laiza anawezxa kusoma kiswahili kama luigha isipokuwa kuupata ujumbe ndiyo hapo anatuonesha uwezo wake kuchanganua mambo ni kiwango cha chini sana.................

    ReplyDelete
  7. Chahali sasa naona umeamua kutochapisha maoni yangu kwa kuwa tu nimekuwa critic wa falsafa zako. Hat hivyo nikuchekeshe kidogo...Tanzania daima toleo la jana limedai ati JK ali-import watu kutoka majimbo mengine kwenda karatu kuhudhuria mkutano wake wa kampeni. Ngoja kwanza tukubaliane na ujinga wenu...halafu tuwaulize..je Dr.Slaa ali-import watu kutoka majimbo mengine kuwaleta karatu? maana population ya karatu sio kubwa kiasi kile...kama jibu ni ndiyo basi kuna ubaya gani na JK kuiga yale aliyofanya Dr.Slaa? Lakini twende kwenye facts and figures...Dr.Slaa atakayeondoa kodi kwenye vifaa vya ujenzi ili wananchi wawe na nyumba bora na za kisasa..ameshindfwa kwa miaka kumi na tano aliyooongoza jimbo la karatu, kubadili mandhari ya mji mdogo wa karatu kuwa wote wenye nyumba za kisasa zilizopangiliwa. Mbaya zaidi ameshindwa kutatua kero ya maji inayowasumbua wana karatu kwa miongo kadhaa sasa. Uhodari wake ni kuanzisha bodi ya maji inayokaa na kulipwa posho lakini maji...kaput...Charity begins.....sasa ndugu yangu kama jimbo limekushinda kwa miaka kumi na tano je nchi utaiweza kwa miaka mitano?....HATUDANGANYIKI...JUMAPILI TWENDE SOTE TUKAMPE JK NA TIMU YAKE KURA ZA NDIYO ZA KISHINDO....Mbuyu hatutafuni...we kaanga sis tunauangalia na kuupuuza....CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.