2 Dec 2010



Nimetumiwa na mdau,nami nawasilisha

Nadhani kwa wakaazi wa Arusha na vitongoji vyake watakuwa wameshaona kwenye mabango mbalimbali barabarani ama kupitia redio ama magazeti ya kuwa iliyokuwa inaitwa Novotel Mount Meru Hotel inafunguliwa tena upya ikijulikana kama New Mount Meru Hotel.

Kikubwa nachotaka kuwafikishia watanzania wenzangu ni kuwa nimestaajabika sana ile maana kamili ya uwekezaji kuendelea kutupwa kapuni. Huwezi amini moderator na watanzania kwa ujumla, Hotel hii hadi maua na mchanga vyote vimetoka South Africa ambapo ndipo ilipo kampuni iliyopewa jukumu la kuindesha hotel hii ijulikanayo kama Zabulan.

Nachokiona hapa ni kuwa wasauzi afrika wao wanathamini vyao hata kama wako nje ya kwao, itakumbukwa watu walishapiga kelele kuhusu bidhaa zipatikanazo shoprite ya kuwa hadi nyanya na vitunguu hata mchicha vinatoka hukohuko SA, sasa ambacho watu watajionea hapa ni kuwa mchanga, maua, mbolea, signboards, tisheti, viatu, sabuni, vitambaa, computer, curtains na vyooote vinatoka sauzi afrika, hivi ina maana hapa hatuna hivyo vitu; vingine itasemekana labda viwango na jee hata mbolea na mchanga??

Kali zaidi ni kuwa Senior staffs woote ni ndani ya sauzi afrika ama asia au kwa watani wa jadi, ina maana hapa hatuna mameneja wazuri wakuendesha hotel? hatuna mashefu wazuri hapa tz?

Ikumbukwe walisema katika ajira wataweka mbele wazawa...hii imefia wapi??

Kama uwekezaji ndo hivi jamani bora tufie na tai shingoni.

Kali nyingine ni kuwa Raisi wetu yuleyule aliyeifunguaga Snow Crest Hotel then kesho yake ikaja kuvunjwa ukuta ndio anakuja tarehe 17 Dec kuifungua hii ambayo ilikuwa mali ya watanzania then Mkapa na Magufuli wakaiuza na sasa watanzania hawana hata percent moja hapa, hilo moja pili ni kuwa wafanyakazi woote ni wametoka kenya ama sauzi afrika ma bara asia na pia waliopewa tenda za ku-supply vyakula ni wakenya tupu na vyote vinatoka hukuhuko kenya kuanzia kuku, maharage hadi matunda, jamani rais hana washauri wakamfungua kwenye hili na jee watanzania tutakuwa wapole hadi lini watu wanakuja kupora malighafi zetu na kukimbia??


Ama ndio kichwa cha mwendawazimu??


TUAMKE WATANZANIA NA TULIANGALIE HILI SWALA LA MOUNT MERU KWA JICHO LATATU.


NGUVU YA UMAA IFANYE KAZI JAMANI............

2 comments:

  1. We are the administration of peliculasonlinecinema.blogspot.com, a blog that has 1000 visits of 110 countrys all over the world, and we are looking to exchange blogroll links. If you are interested in this, please write a comment to us in our blog and let us know that you put our link in your blog. In less than 24 hours we will put your link in our blogroll and let you know immediatly. Thank you.

    ReplyDelete
  2. Mount Meru Hoteli sasa iko wazi.
    Wao wana kazi ya jumla ya wageni 11 (kumi na moja) ina kuvunjika kama ifuatavyo : 1 Kiholanzi, 1 Ireland, 3 Mauritius, 1 ya Afrika Kusini na Wa Kenya 2.
    Uwaino wa wafanyakazi (229) ni wa mtanzania.
    Wafanyakazi ni muhimu sana kwa ajili ya Mount Meru Hotel na wao wame kwisha anza mafunzo kotoka mwezi wa Oktoba 2010.
    Yao wanaamini ni : ‘’ Haijalishi unachouzza, umuhimu wa biashara yako itabaki kuwa watu wako’’

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.