24 Dec 2010


Majuzi,msomaji mmoja wa blogu hii alinitumia maoni ambapo pamoja na mambo mengine aliashiria kuwa nina chuki dhidi ya Rais Jakaya Kikwete.Msomaji huyo aliyejitambulisha kuwa mkazi wa hapa Glasgow alidai (namnukuu) "...I know you hate JK because whatever happens to him you have a negative view, even a tyre puncture...",yaani kwa Kiswahili,"najua unamchukia JK kwa vile chochote kinachotokea kwake wewe una mtizamo hasi,hata pancha ya tairi".Hii ndio mitizamo ya Watanzania wenzetu ambao licha ya kubahatika kuwa nje ya nchi,hususan nchi zilizoendelea kama hapa Uingereza,bado wana mitizamo mgando ambayo kwa kiasi kikubwa imechangia kutufanya hata miaka 49 baada ya uhuru kutamani mkoloni arejee.

Yah,huwezi kuwalaumu wanaotama mkoloni arejee japo mie si mmoja wao.Hivi tunawezaje kuelezea namna Watanzania wanavypelekeshwa kama watoto wadogo tena yatima siku chache tu baada ya Kikwete na CCM yake kupita huku na kule kuahidi neema,only for madudu and more madudu kuibuka kila kukicha?Unajua,angalau mkoloni alipotupelekesha alikuwa na excuse (japo isiyokubalika) kwamba yeye hakuwa Mtanganyika,na hakuwa na uchungu na nchi yetu.Na kwa wanaokumbuka vizuri somo la historia wanafahamu bayana kuwa ujio wa mkoloni ulikuwa kwa minajili ya kuendeleza nchi zao za asili,yaani kukwapua raslimali zetu kwa ajili ya viwanda vyao,kupata masoko ya bidhaa zao na eneo la makazi kwa nguvukazi ya ziada katika nchi hizo za wakoloni.Sasa ondoa neno mkoloni kisha weka neno FISADI,na yayumkinika kuhitimisha kuwa angalau mkoloni alikuwa na ajenda ya maendeleo huko kwao japo at our expense.Mafisadi nao wana ajenda za maendeleo pia,ila ni katika kutunisha akaunti zao kwenye mabenki ya hukohuko kwa wakoloni,kuongeza idadi ya nyumba ndogo zao (isomeke ufuska au uzinzi),kuongeza idadi ya mahekalu yao na magari ya kifahari,na sasa ajenda mpya ya kuimarisha himaya zao kwa kutumbukiza kila mwanafamilia na ndugu wa karibu kwenye siasa ili pindi baba akiondoka madarakani basi mwana amrithi kuzuia uwezekano wa baba mtu kukaliwa kooni kwa madudu aliyofanya akiwa madarakani.

Nimelazimika kuandika makala hii sio kwa minajili ya kumjibu huyo msomaji wangu wa hapa Glasgow bali ni baada ya kusoma toleo la mtandaoni la gazeti la Mwananchi ambapo kuna habari kuwa Tanesco wametangaza tena mgao wa umeme nchi nzima.Hivi sio majuzi tu shirika hilo lilitangaza mwisho wa mgao wa umeme?Tuwe wakweli,hivi uhuni huu wa Tanesco,ambao mie natafsiri kuwa ni uhuni wa serikali iliyopo madarakani,utaendelea hadi lini?So far,hakuna taarifa za wazi kuhusu athari za mgao wa umeme lakini haihitaji sayansi ya roketi au dissertation ya quantum physics kumaizi kwamba mgao huo una madhara makubwa mno kwa uchumi wa taifa na kwa maisha ya walalahoi kwa ujumla (vigogo licha ya kunufaika na ufisadi unaowawezesha kuuza jenereta kila mgao unapotangazwa lakini pia hawaathiriki kwa vile majumbani na maofisini kwao kuna jenereta zinazoendeshwa na fedha za kodi za walalahoi).

Hatuwezi kuilaumu Tanesco pekee kuhusiana na uhuni huu kwani ni siri ya wazi kuwa shirika hilo na sekta ya nishati kwa ujumla vimegeuzwa kitegauchumi kizuri kwa mafisadi.Majuzi tu tumesikia majambazi wa Richmond wakijiandaa kurejeshewa fedha walizotuibia ambapo watalipwa fidia ya mabilioni kwa mgongo wa binamu zao wa Dowans.Hatuwezi kumwepusha Kikwete na CCM yake na ufisadi huu kwa vile licha ya madudu hayo kushika hatamu wakati wa utawala wake,sasa tunafahamu kuwa amekuwa akiwakingia kifua mafisadi wasichukuliwe hatua za kisheria (thanks to nyaraka za siri za kidiplomasia zilizovujishwa na mtandao wa WikiLeaks).Kwa wale ambao hawajabahatika kusoma habari hizo,kuna nyaraka kutoka ubalozi wa Marekani hapo Dar zilizobeba maongezi kati ya bosi wa Takukuru Edward Hoseah na afisa ubalozi wa Marekani ambapo Hoseah alinukuliwa akieleza bayana kwamba Kikwete alishinikiza baadhi ya mafisadi wasichukuliwe hatua.Japo bosi huyo wa Takukuru amejaribu kuruka kimanga na kukana tuhuma hizo,kila mwenye akili timamu anafahamu kuwa ufisadi unashamiri Tanzania kwa vile Kikwete ameshindwa kuwachukulia hatua mafisadi papa licha ya madaraka lukuki aliyorundikiwa na Katiba.

Baadhi yetu tuliwaasa Watanzania wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita majuzi kwamba kuirejesha tena madarakani serikali ya Kikwete ni sawa na kumwaga chumvi kwenye kidonda kibichi,na matokeo yake ndio haya.Wakati tunaelekea mwezi wa pili tangu Kikwete atangazwe mshindi,hakuna lolote la maana lililokwishafanyika kuashiria kuwa kiongozi huyo ana ajenda mpya tofauti na zile zilizotawala miaka mitano iliyopita,kubwa ikiwa na kushamiri kwa ufisadi na uimarishaji himaya za mafisadi huko nyumbani.

Sawa,makosa yameshafanyika kwa kumrejesha Kikwete na CCM yake madarakani lakini hiyo isiwe sababu ya kuendelea kunung'unika kimoyomoyo huku nchi yetu ikizidi kuteketea.Umefika wakati Watanzania wasikubali kupelekeshwa namna hii.Kwanini Kikwete asibanwe kuhusu tatizo la umeme licha ya ahadi zake za mara kwa mara kuwa tatizo hilo lingekuwa historia?Au alimaanisha kuwa tatizo hilo litaendelea kuwa la kihistoria?

Nimesikia taarifa za mpango wa Chadema kuandaa maandamano ya nchi nzima kupinga kuongezwa bei ya umeme.Yaani licha ya mgao wa kila kukicha bado Tanesco wanataka kuongeza bei?Yayumkinika kuhisi kuwa wazo hilo la ongezeko la bei ya umeme ni la kifisadi lenye lengo la kupata fedha za kuwafidia mafisadi wa Richmond/Dowans.Ni muhimu kwa kila Mtanzania mzalendo kuunga mkono mpango huo wa maandamano ya amani ili kufikisha ujumbe kwa Kikwete na serikali yake kuwa Watanzania wamechoka kupelekeshwa.Hata hivyo,kama maandamano ya kuwapongeza wabunge wa upinzani yalizuiliwa na polisi,sidhani kama serikali itaridhia maandamano hayo ya kupinga ongezeko la bei ya umeme.

Mwisho,tuna choices mbili tu:kuchukua hatua sasa kabla hatujafika mahala ambapo hata tukichukua hatua itakuwa sawa na kutwanga maji kwenye gunia,au tusubiri kusoma rambirambi kuhusu nchi yetu hapo 2015.

5 comments:

  1. Evarist am the guy from Glasgow who you misquoted in this article. You took my words out of context and use them showing as if am supporting JK. The sentence you refer to concerns you supporting your Tabora Boys buddy who got appointed by JK, I was surprised you hate the president and the party you endorsed during election denounce him, still you applauded his ministerial selection.
    For the matter of fact am not one of the people who joins the CCM bandwagon abroad and I don’t have any political affiliation to any party, It seems your pride was hurt a bit when I challenged you and offer constructive criticism on my comments and you decided to come after me. I just gave you my opinion and what do I get, being labelled as JK sympathiser. If you read properly in my comments, the reason I wrote to you was that, you applauded FFU’s actions. That was not right because everyone has a right to demonstrate regardless and we should condone the actions by authorities. You live in UK and you saw student demonstrations in London, they were given routes by police and were escorted through them, trouble started when anarchist started to cause havoc in the streets of London. Most students supported LibDems because of the pledge of not raising tuition fees, what’s your view about that; police should have gone after them as well?
    I hope this time you will admit that you are wrong and not come after me with another article labelling me something else!!
    And this is what I feel about JK, I see the importance of spelling it out so you do not get a chance of taking a sentence and quote in another article of yours.
    I think he is a conman and when he speaks he looks like a dodgy salesman, but this is a character of most politicians in bongo whether in government or opposition. I feel bad everywhere I go here in UK when I see changes that are happening. The roads, power supplies, water supplies, children welfare, public transport compared to TZ. The solutions, all politicians to stop thinking about themselves for once and think about the people they represent and put themselves in their shoes, may be, may be the country will be a better place.

    Mo,Glasgow

    ReplyDelete
  2. WATANZANIA WENZANGU HALI NI MBAYA, NA SIO KWENYE UMEME TU HATA BEI YA PETROLI IMEPANDA, NA MNAJUA BEI YA PETROLI IKIPANDA HATA KAMA HUNA BAJAJI BADO ITAKUKUMBA TU! SASA MFIKIRIE MLALA HOI HAPO! YAANI KWAKWELI KAKA NASHANGAA UMELIONGELEA SWALA LA MKOLONI, HATA MIMI NILISHATAMANI ARUDI TU HUYO MKOLONI, NI BORA MTAWALIWE MJUE MOJA, KULIKO WAZALENDO WENZENU WANAOWADIDIMIZA KUSUDI WAO WAELEE... JAMANI NILISHAJIULIZA SANA HIVI TUNAWANAUME HAPA? MBONA NI MAMBO YA DHARAU HIVI? NDIO HII NCHI YA AMANI? AU UJINGA? WANASIMAMA WAZUNGU MABARABARANI KWA KUONA TUNAVYOIBIWA! SISI WAZALENDO TUNASUBIRI NSHALLAH MUNGU ATATUPA KESHO! TUMEPATWA NA NINI SIJUI! HAKUNA SHERIA YOYOTE INAYOFWATA, TUKIINGIA KWENYE KATIBA NDIO USISEME, ALAFU MIJITU MINGINE OOH MSIWE NEGATIVE HATA PANCHA KWENYE TAIRI MNAKOSOA!! KWELI MTU UTASEMA MANENO HAYO WAKATI NCHI IMEKWISHA HIVI BAADA YA MIAKA 49 YA UHURU! REALLY? NI MBINAFSI KAMA HAO MAFISADI, SHAME ON YOU KABISA, KAA KWENYE KIBARAZA CHA UFISADI SUBIRI KAHAWA NA KASHATA, LAKINI WALAHI PANGA LAJA.

    ReplyDelete
  3. Mo,my sincerest apology for the misunderstanding,and thanks for your comment.

    ReplyDelete
  4. Honestly, After I have made thoroughly research over scandles ang government resources mismanagement...The temporary solution for Tanzanians problems is to make shameful request to Britain get back and coloniesing us for second time untill. We are fully civilised and brain washed into the actual meaning of nationalism...

    ReplyDelete
  5. Kuna tatizo gani watu kunyimwa umeme wakati ndicho walichochagua? Hata pale kura zilipochakachuliwa, si wananchi wala viongozi wao (upinzani) walikuwa tayari kuingia mitaani. Angalia kilivyoumana pale Ivory Coast. Hawa ndiyo watu wenye akili achia mbali misukule na mafisadi wetu. Kwa sasa hatuwezi kumlaumu Mungu wala serikali bali wananchi wetu ambao wengi ni kama kondoo waliochanganyikana na mafisi halafu wakaaminiana kondoo wasijue ni kiama chao!
    Kwa vile walichagua giza basi tusiwalazimishe kutaka mwanga. Kwa vile walikula chao mapema acha na mafisadi wachukue chao mapema kwa kulipana kupitia Dowans.
    Kuna ubaya gani shamba la bibi kuchumwa hata na mabwege? Hivi mlitegemea nini msanii alipoaminiwa na wapwakia udoho udoho? Hapa hakuna anayemdai mwenzake. Kwani Tapeli kawapa dhahabu feki nao wamempa pesa safi wanalia nini? Ila tukumbuke. Katika upuuzi huu, vizazi vijavyo vinazidi kuwekwa pakanga kiasi cha siku moja kukojolea makaburi yetu tusipobadilika.
    Kwa vile nyumbani kwa mfalme hata nyumba zake ndogo wanapata umeme, tatizo liko wapi kwa mende kulala kizani wakazaane na kuzaana hadi wawe kero? Shauri yenu

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.