5 Mar 2011


Tunaposema kuna ombwe la uongozi kwenye Serikali ya Rais Jakaya Kikwete baadhi ya vichwa panzi wanatuita wachochezi.Sasa unapoona Waziri anauchapa usingizi kwenye mkutano wa kimataifa,huku bosi wake akiwa kando,basi sijui tusemeje!!!

Na tunaposema Kikwete ni kiongozi dhaifu sio kama ni uchochezi,majungu au chuki binafsi.Hivi kama Rais anashindwa kumkemea Waziri wake kwa kulala kwenye mkutano tunaoambiwa una umuhimu mkubwa kwa nchi yetu (hadi imelazimu mkuu wa nchi aende mwenyewe badala ya kuwakilishwa na Makamu wake,Waziri Mkuu au Waziri wa Nishati na Madini)atamudu vipi kukemea wabaka uchumi ambao baadhi yao ni watu wake wa karibu waliochangia harakati zake za kuukwaa Urais?

Na kuna umuhimu gani kwa fedha ya walipa kodi kugharamia safari ya Ngeleja ambaye anaishia kulala mkutanoni badala ya kutuwakilisha?Au Kikwete amelazimika kwenda mwenyewe badala ya kumwacha Ngeleja pekee kwa vile alijua kuwa waziri wake huyo ataishia kuuchapa usingizi mkutanoni?

Kutegemea watu wa aina hii wanaweza kumsaidia Mtanzania kuondokana na umasikini wa kutupa ni sawa na kutegemea kugema damu kwenye jiwe.Na ukiona waziri mzima pasi haya anachapa usingizi huku Rais wake akiwa kando basi ujue wazi kuwa si akina Richmond na Dowans tu waliomudu kutuingiza mkenge bali tutarajie mengi zaidi.Unadhani kama Ngeleja anathubutu kuuchapa usingizi katika mkutano wa kimataifa unaouhusu maslahi ya nchi,hali inakuwaje wakati anashughulikia maslahi ya nchi ofisini mwake?Sintoshangaa kusikia kuna mikataba ya kuhamisha madini yetu ikisainiwa huku waziri yuko fofofo usingizini

Au Ngeleja ameanzisha mashindano ya kuchapa usingizi dhidi ya Mbunge wa CCM Kapteni John Komba,ambaye kama inavyoonekana pichani chini,alifumwa akiwakilisha wapiga kura wa jimbo lake kwa kuchapa usingizi Bungeni DodomaPicha kwa hisani ya Jamii Forums

3 comments:

 1. Kama sikosei, kuna wakati zamani kiasi, Mheshimiwa Spika aliulizwa kwa nini hawadhibiti wabunge wanaotwanga usingizi wakati wa vikao Bungeni. Alijibu kuwa kwa mujibu wa sheria za Bunge, mbunge ruksa kuuchapa usingizi, ili mradi hakoromi.

  Mzee Chahali upo hapo? :-)

  ReplyDelete
 2. Hili lilikuwa ni kongamano ambalo ilikuwa stahiki ya katibu mkuu au mkurugenzi wa kitengo. Ukiangalia mkao wenyewe, unadhihirisha kuwa hawa jamaa walikwenda tu kutalii na ndio maana wote wawili wamekuwa bored- mmoja amepiga usingizi na mwingine anapotezea muda kwa kupitisha macho kwenye kijarida kama sio kipeperushi!! Washiriki wengine wote wanaonekana kusikiliza kwa makini. Nilisoma habari hii katika blogu nyingine nikasikitika sana kuona baadhi ya watoa maoni wanasema (sio kwa makosa yao) "baba tuombee misaada tupunguze makali ya umeme!!!" Hii ni kwa sababu watawala wetu wamewaaminisha wananchi/walipakodi kuwa kodi yao inayotumika kugharamia safari za nje ni kwenda kuwatafutia "maisha bora" kutoka kwa "wenzetu"! Ukikuta wabongo (including wasomi) wakitetea safari za nje za mkuu wa kaya unakaribia kupata BP!!!!

  ReplyDelete
 3. Mimi nahisi huyu mtu wa sengerema haelewi kitu kinachoongelewa labda sasa tatizo ni elimu yake au tatizo ni lugha hilo ni swali lengine na kama haelewi kinachoongelewa kwa nini asilale na bahati nzuri walienda na mheshimiwa kwasaabu mtu aliyelala kikao kizima sijui anarudisha ripoti gani

  ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.