24 Dec 2014

Awali,kupitia akaunti yake ya Twitter, Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC Swahili) iliripoti ifuatavyoHata hivyo, baada ya kuzongwa na baadhi ya WANAHARAKATI huko Twitter walioonyesha kukerwa na hatua hiyo ya nchi wahisani, Mwenyekiti wa nchi wahisani, Balozi wa Finland nchini Tanzania Sinikka Antila (@SinikkaAntila) alifafanua kwa tweet ifuatayo 


Kwa lugha ya taifa, Balozi huyo anaeleza kwamba "vyombo vya habari havipo sahihi. Asilimia 15 ya msaada ulioahidiwa kwa bajeti ya mwaka 2014/15 ilitolewa kabla ya hotuba ya Rais (Kikwete)."

Hata hivyo, licha ya kauli hiyo ya Balozi Antila kutanabaisha kuwa BBC Swahili waliripoti ndivyo sivyo kuwa wafadhili wameamua kutofa fedha hizo baada ya kuridhishwa na hotuba ya Rais Kikwete, bado kuna swali gumu kuhusu suala hilo, nalo ni JE NCHI WAFADHILI ZILITUHADAA ZILIPODAI KUWA ZIMESITISHA MISAADA HADI HATUA ZITAKAPOCHUKULIWA KUHUSU SUALA LA ESCROW?

Swali hilo linatokana na kauli ya Balozi huyo wa Finland kuwa fedha hizo zilishatolewa hata kabla ya hotuba ya Rais Kikwete, ikimaanisha aidha nchi hizo wahisani zilikuwa zina hakika kuwa Rais Kikwete angechukua 'hatua hizo za kuwaridhisha wafadhili' au 'walituzuga tu' kuhusu kusitishwa misaada hiyo.

Kadhalika, kauli ya Balozi Antila haikanushi kuridhishwa kwa wafadhili na hotuba ya Rais Kikwete, ambayo Watanzania wengi wanaamini kuwa imewalinda mafisadi hasa ikizingatiwa mzigo mkubwa wanaoubeba kutokana na sakata la muda mrefu la IPTL. Kwa Rais Kikwete kushindwa kumaliza sakata hilo, na kuridhia kuwa pesa za Tegeta Escrow ni za IPTL/ PAP, ina maana Watanzania wataendelea kulipa mamilioni ya shilingi kila siku kwa huduma ya umeme ambayo kimsingi ni hewa.

Binafsi ninaguswa na uamuzi wa nchi wahisani kwa sababu kama mkazi wa Uingereza, ninalipa kodi mbalimbali, ambazo sehemu ya kodi hiyo ipo katika misaada inayotolewa na nchi hii kwa Tanzania. Wakati sina kipingamizi kwa nchi hizo kuisaidia Tanzania, siungi mkono kabisa kuendelea kutoa fedha zinazoishia kuwaneemesha mafisadi kwa kunenepesha akaunti zao, kuongeza idadi za mahekalu na magari yao ya thamani na kukuza idadi ya nyumba zao ndogo.

Ufadhili usiozingatia maslahi ya nchi fadhiliwa sio tu ni upuuzi bali pia ni ku-abuse fedha za walipakodi katika nchi wafadhili.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube