Showing posts with label BLOGGING IN TANZANIA. Show all posts
Showing posts with label BLOGGING IN TANZANIA. Show all posts

13 Aug 2011




Bonyeza picha hapo juu kupelekwa moja kwa moja kwenye blogu ya MtotoSix.tk

6 Aug 2011


Nimekutana nayo huko Jamii Forums.Habari hii imenikumbusha mbinu iliyotumiwa na utawala wa mkoloni kuendeleza utawala wake dhalimu.Wakoloni walitugawanya kwa misingi mbalimbali,hususan rangi,na kwa kiasi kikubwa walifanikiwa kuchelewesha jithada za ukombozi wetu.Lakini kama zilivyo mbinu nyingine za ujanja ujanja,mbinu hiyo haikuweza kudumu milele.Kwa hakika hakuna mbinu yoyote inayoweza kuzuwia kiu ya mwanadamu kuleta mabadiliko bora kwake.

Kinachonisikitisha katika habari hii ni namna baadhi ya wanablogu wenzetu wanavyokubali kuuza utu wao (na kuwasaliti mamilioni ya walalahoi) kwa ajili tu ya maslahi binafsi.Wosia wangu kwao ni mwepesi tu: waangalie namna CCM ilivyowatumia wanahabari katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010,na mara baada ya Wanamtandao kufanikiwa kumwingiza Kikwete Ikulu wakawatosa wengi wa wanahabari hao.Kuna wanahabari walibembelezwa kuacha vibarua vyao nje ya nchi,wakawatumikia wanamtandao na baada ya umuhimu wao kwisha,wakatoswa.Ni vema mabloga walioingia mkenge huu wakatambua kuwa nafasi yao walionayo ni mhimili wa nne wa dola.Lakini la muhimu zaidi,wakae wakielewa kuwa,ashakum si matusi watatumika kama kondomu: MUHIMU SANA KABLA NA WAKATI WA TENDO LA NDOA LAKINI HUONEKANA UCHAFU USIOVUMILIKA BAADA YA TENDO HILO.

You have been warned.

Soma habari husika hapa chini


CCM yaanzisha Mtandao wa Friendly Media to CCM

Wana Jf

Nimesoma habari ambayo imenistua na imenibidi niongee na Mhariri wa Gazeti la Mtanzani Ndg Jacton Manyerere na amenithibitishia kuwa habari aliyoandika ni ya uhakika.

Idara ya Uenezi na Itikadi ya CCM ambayo ipo Chini ya Ndg Nape imeanzisha Mtandao wa Vyombo vya Habari na wana Habari Rafiki na Bloggers na amekuwa akikutana nao Mara kwa Mara.

Kutokana Taarifa za Gazeti la Mtanzania (Media House ambao si Rafiki na CCM kwa Sasa), media ambazo hazitahudhuria ktk mkutano wa Tar 13 na 14 mwezi huu utakaofanyika Morogoro ni Mwananchi Communication, New Habari, Hali Halisi na Free Media. Vyombo hivi si Rafiki wa CCM.

Na Bwana Jacton ansema doc ya FCCM inaonyesha uwepo wa Mpango Mkakati wa Kuanzisha FORUM itakayoitwa KWETUFORUM na pia utaanzishwa mpango halisi wa kuimaliza Jamii Forums.

Pamoja na mpango huu awali walikua wakutane Dodoma wakati wa kamati kuu na mnamo mwezi wa Tano Nape alifanya kikao makao makuu ya CCM na akakutana Bloggers na kuwaahidi kuwasaidia lakini waisaidie CCM ktk Mkutano huo alikuwepo Blogger mmoja wa Jinsia ya Kike... kutokana na mahudhurio ya kikao hicho.

Kilichonishangaza ni baada ya kusoma Agenda za Mkutano ktk Gazeti la Mtanzania leo nimeshangaa katibu wa mpango huu ni dada ambaye sisi hapa Nipashe alikuwa haheshimiki na alisimamishwa kazi.

Binafsi hii ninailaani kwakua inaleta Taswira Mbaya na ninatarajia kuona Editors Forum wanalifanyia kazi kama CCM inatugawa wana Habari ktk Makundi ya Rafiki na Adui ni jambo baya kufanywa na chama kikongwe kama Hiki. Nadhani huyu dogo Nape amechanganyikiwa kabisa.

Nimeona niilete hapa Jamvini Tulijadili.

Story ipo ukurasa wa kwanza ktk Gazeti la Mtanzania na inaendelea ukurusa wa nane

CHANZO: Jamii Forums

19 May 2011


JINA LA BLOG: KONA YA MATUKIO

Tunapenda kulitambulisha wadau wote libeneke jipya la KONA YA MATUKIO ambapo nia na lengo kubwa ni kuleta matukio yanayotokea kila siku katika Jamii yetu na Duniani kwa Ujumla..pia kutakuwa na Matukio ya papo kwa hapo yani Breaking News Endelea kuwepo kila muda kujua nini kitatokea

Kama unatukio la aina yoyote tutumie kupitia [email protected] 
Karibuni nyote na asanteni kwa kututembelea.

Pamoja Tunaweza

13 May 2011


Napenda kuwafahamisha badiliko la anwani ya blogu
Blog title: SAUTI YA MNYONGE:

Asante
Malkiory William Matiya,
B.Ed.(Hons) (UDSM); M.Sc, P/Health (UTA, Finland)
Mobile: +358404623776



14 Jan 2011


Katika moja ya maeneo machache ambayo Watanzania tumepiga hatua ya kuridhisha ni fani ya kublogu.Ni vigumu kufahamu idadi kamili ya mabloga wa-na blogu za- Kitanzania (ndani na nje ya nchi) lakini haihitaji sensa kutambua kuwa idadi ni ya kuridhisha.Iwapo idadi hiyo inaendana na matarajio ya wasomaji,hilo ni suala jingine.

Kwa haraka haraka,ni rahisi pia kutambua blogu za picha (zinazoambatana na habari) ndizo zinazotamba zaidi.Pengine ni kwa vile,kama wasemavyo, "PICHA MOJA INAWEZA KUWAKILISHA MANENO ELFU MOJA".Lakini inawezekana pia kuwa wasomaji wetu wengi wako bize,na hawana muda wa kusoma makala ndefu kwenye blogu kama hii.Kadhalika,na hili nalitamka kwa uangalifu mkubwa,huenda kuna kundi dogo la wenzetu ambao kwa mtizamo wao,kusoma ni mithili ya self-inflicted third degree torture.

Blogu hii ina umri wa miaka mitano kasoro miezi mitatu (ilizaliwa mwezi April 2006).Ukiangalia idadi ya wasomaji wanaoitembelea (visitors),unaweza kudhani imeanzishwa miezi michache tu iliyopita.Kuna blogu kadhaa zenye visitors milioni kadhaa,na baadhi yao zina umri haba kulinganisha na wa blogu hii.

Unaweza kudhani inakatisha tamaa.Hapana.Binafsi,naamini nina kundi dogo la wasomaji "tunaoelewana".Yaani namaanisha wasomaji ambao kwa kiasi kikubwa wanaafikiana na dhima kuu ya blogu hii: harakati za haki kwa jamii na mapambano dhidi ya uhujumu uchumi,ukiukwaji haki za binadamu na utawala bora.Haimaanishi kuwa wasomaji hao wanaoiamini blogu hii wanaafikiana na kila nachoandika.Hapana.Kuna nyakati tunatofautiana kimtazamo,na wengi wao huwa huru kunikosoa au kutoa mawazo tofauti na yangu.Of course,kuna nyakati,baadhi ya wasomaji huamua kutumia lugha isiyofaa kuwasilisha ujumbe/mtizamo wao.Hizo ni changamoto katika maisha kwani ukiona kila kitu kinakwenda sawia basi huenda kuna walakini mahala flani.

Of course,ingependeza kuona blogu hii nayo ina visitors milioni 5 au zaidi.Lakini what if kati ya hao,ni asilimia ndogo tu wanaochukulia kwa makini ujumbe uliomo bloguni hapa?Kwangu,idadi ya visitors hainusumbui kwa vile naamini nina kundi dogo la wasomaji makini ambao wanaichukulia blogu hii kama kiwanja chao cha mazoezi kwa ajili ya mapambano ya kusaka uhuru wa pili wa Tanzania,sambamba na kuhabarishana kinachojiri kwenye korido za watawala wetu.

Enewei,kisa cha kuandika post hii ni mfadhaiko nilioupata siku chache zilizopita pale nilipotuma post (niliyoichapisha hapa) kwa bloga mwenzangu wa picha-habari.Kuna nyakati huwa naona umuhimu wa kufikisha ujumbe wangu kwa wasomaji wengi zaidi,hususan wale wapenda picha lakini sio habari.Na kwa kutambua kuwa blogu ya rafiki yangu huyo inatembelewa na wasomaji wengi kuliko hii,na pia kwa vile alishatoa wazo la kumtumia angalau makala moja kwa wiki,nikaona hakuna ubaya wa kumtumia post hiyo.

Cha kusikitisha,sio tu hakuichapisha bali amekuwa akikwepa hata meseji nazomtumia (sio kumkumbushia kuhusu post husika bali mawasiliano yetu ya kawaida tu).Nafahamu kuwa baadhi ya "waswahili" wanapata wakati mgumu sana kuwa wawazi na wakweli kusema "samahani,hii haiendani na hadhi ya blogu yangu".Mhusika anadhani kukaa kimya kutapelekea mie kusahau ombi langu kwake,na ishu itamalizika kienyeji.

Najua kwanini bloga huyo aliogopa kuchapisha post niliyomtumia.Anaogopa mamlaka.Lakini uoga wa nini wakati kilichoandikwa si mawazo yake?Binafsi,kuna nyakati huwa natumiwa habari au matangazo mbalimbali,na ninachofanya ni kuyatundika sambamba na kubainisha chanzo au mtumaji.

Ushirikiano ni muhimu kwa mabloga hasa kwa vile yawezekana mwenzangu hana nilichonacho,nae anacho kile ambacho mie sina.Wingi wa idadi ya visitors isiwafanye  baadhi ya "mabloga wenye majina makubwa" (kama huyu rafiki yangu nayemzungumzia hapa) wajisahau kuwa sisi kama wanadamu ni wanyama tunaohitaji sana ushirikiano (social animals).Na sio lazima ushirikiano huo uwe kwenye kublogu pekee bali mambo mbalimbali yanayotugusa binafsi au jamii kwa ujumla.

Enewei,simlaumu ndugu yangu huyo kwa vile kama ilivyo katika blogu hii,yeye pia ana haki yake ya kikatiba kutochapisha kitu anachoona hakiendani na maudhui ya blogu yake.Lakini,japo pia ni haki yake ya kikatiba,kufanya dharau si jambo la kiungwana.Kunifahamisha kuwa "aah ndugu yangu ile kitu naona inaweza kuniletea matatizo..." sio kauli ngumu,hasa ikitolewa kwa njia ya meseji.

Well,wakati tunaanza mwaka mpya ni vema kufanya inventory ya kuangalia watu walio na umuhimu kwako na wale ambao wanaongeza tu idadi.Namshukuru ndugu yangu huyu kwa kunirahisishia zoezi hilo.



27 Nov 2010


Image and video hosting by TinyPic
Ni matumaini yangu kuwa muwazima na mnaendelea na majukumu yenu ya kujenga Taifa au ustawi wa familia zenu popote mlipo.

Ni kitambo kidogo nilitoweka katika ulimwengu wa Kublog, na hiyo ilitokana na majukumu yangu ambayo yalinifanya nihamie Arusha kwa muda ambapo nilijikuta nikiwa na wakati finyu sana kuutenga kwa ajili ya kublog.

Najua kwa wale wapenzi wa Blog ya VUKANI, watakuwa wame-miss makala zangu ambazo kwa kweli zilikuwa zikiibua mijadala mipana ambayo ilikuwa ikifurahisha kuchangamsha na wakati mwingine kukera kidogo.......lakini yote kwangu yalikuwa ni heri tu... lakini pia kwa wale waliokuwa wakifuatilia maoni yangu popote pale nilipokuwa nikichangia mada mbalimbali nao pia walikuwa wanani-miss kwa kuwa napo huko nilikuwa siishi uchokozi.

UCHAGUZI UMEKWISHA!

katika kipindi kizima cha kampeni za uchaguzi karibu blog zote zilikuwa zimedorora, nadhani sikuwa peke yangu, nawapongeza sana wale walioendelea kutupasha habari mbalimbali wakati wa kampeni hususan kaka zangu Evarist Chahali, Mubelwa Bandio,Prof. Matondo,Prof Mbele, Mzee wa Karibu Iringa, Magid Mjengwa Simon Kitururu, Chacha Wambura, Kamala Fadhy Dada yangu Subi, Yasinta na wengine ambao sikuwataja hapa, lakini nilikuwa napitia blog zenu na kujifunza japo mawili matatu.

sasa baada ya uchaguzi kwisha ni vyema wote turejee na nguvu mpya tukiwa na fikra pevu za kuijenga nchi yetu, kuna haja sasa ya kuwa na sauti moja yaani wanablog na wasomaji wa blog kuwahamasisha viongozi wa serikali wasome blog zetu hizi kwani kuna mawazo mengi yanayotolewa katika eneo hili la blog lakini yameachwa tu yapotee bila sababu.

Ni vyema kuunganisha nguvu zetu bila kujali vyama, maana najua wengi tumeumia mioyoni mwetu baada ya kuona yule tuliyemtegemea hakutangazwa na tume kuwa ndiye mshindi, lakini mimi naamini kuwa kwa kiasi kikubwa vyama vya upinzani vimeshinda uchaguzi wa mwaka huu, kwani kwa nguvu ndogo walizokuwa nazo kwa maana ya nguvu ya kifedha, lakini wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzoa wabunge na madiwani wengi nchini na hivyo kuonyesha kuwa wananchi wamewakubali.

Tunahitaji sasa kuonesha mshikamano, na kumsaidia bwana mkubwa aliyeko madarakani ili aweze kutuvusha katika miaka mitano hii aliyobakiza salama.Tunatakiwa kukosoa kwa nia ya kujenga na kuelekeza na ikibidi kufundisha........katika tasnia hii ya wanablog naamini kuna vichwa vilivyojaa hekima na mawazo mapya, na ninaamini hata wao wanalitambua hilo

Nimerejea lakini sidhani kama nitakuwa na nguvu kama ile ya kipindi kilichopita kwa sababu ya kutingwa na mambo ya kujiimarisha kiuchumi......

nawatakia kila la kheri na mafanikio mema katika kipindi hiki cha kuumaliza mwaka huu wa 2010.

Ni mie Koero Japhet Mkundi

ASANTE SANA DA KOERO.NAMI NAKUTAKIA HERI NA MAFANIKIO MEMA KATIKA KIPINDI HIKI KILICHOSALIA KABLA YA KUMALIZA 2010 NA SIKU ZOTE.

23 Sept 2010


You posted the following comment on this blog.I have tried to reply on your blog but it doesn't seem to work.I know my reply will offer you a rare chance of publicity,but,well,there's nothing I could do about that.Perhaps that's all you wanted: cheap publicity.You wrote (I quote):

you should tellus about your political status and knowledge,sio kuanza kuponda tu,mbona you dont look on the p[ositive side?we are not interested na watu wanaoponda wenzao bila kuchangia mawazo ya nini kifanyike kuiwezesha tanzania kupiga hatua,afu kumbuka bila uzuri hakuna ubaya wa kuzungumziwa,so tell us about uzuri wa jk ili tupime wenyewe siyo unatoa one side tu unless you are apoliticia.”

In reply to your above comment on my blog,I first would encourage you to check a dictionary as to what “political status” means. As a human being, I don’t have any. As to your inquiry on my political knowledge, I’m just a Political Studies research student. However, you could read my full profile HERE

Mheshimiwa Meya, if you were not interested “na watu kuponda ya wenzao” you could have simply not visited my blog. I believe nobody held you at a gun point when you decided to pay my blog a brief visit. And I think you did not do me justice when you lamented that I did not “kuchangia mawazo ya nini kifanyike kuiwezesha Tanzania kupiga hatua”. Of course I did, unless you are allergic to letters. I clearly urged Tanzanians to vote Kikwete out of office. In my view, which you have every right to oppose, economic sabotage (ufisadi) is one of the stumbling blocks which hinder our country from attaining desired progress, and removing their patron, Kikwete, would most likely be a way forward towards achieving that goal.

I’m left speechless on your assertion that “bila uzuri hakuna ubaya wa kuzungumziwa”. I would expect to hear that not from msomi like yourself. Tell me one good thing about Ukimwi, which is a menace to society. Or, tell me just one “uzuri” of ufisadi. You surely know there are things which are absolutely evil, and one couldn’t find any good quality from them. But even if you personally think Kikwete has good and bad qualities, as a msomi you should have acknowledged my point of view. I hope you have been taught there’s no such a thing as a universal point of view. So if I think Kikwete is a hack, I don’t have to convince you to agree with me. And you too don’t have to convince me to believe otherwise.

I don’t have to tell you “uzuri wa Kikwete” if I couldn’t find any. By the way, if you sincerely believe that I did not do him justice,you can now shower him with praises now you have your own blog.Why expect praises for Kikwete from my blog when you could do the same on your own blog?So,be a good blogger,stop forcing other bloggers to write what you want to read,and do just that yourself,instead.And just a polite word of advice,you better write such article in Swahili.

Finally, try to do a little proof reading before you post your articles. You wrote “Guys WORDWIDE i welcome you "instead of "WORLDWIDE”. And you also wrote “For those who are interested in politics especially with the CONCIDERATION...” instead of “CONSIDERATION”. You see, it’s easy criticising someone but hard for yourself to do a simple right thing as getting your spelling right.

Honestly,Honourable Mayor, you are not just a disgrace to Mzumbe University but also a public insult to the entire higher education sector in Tanzania.

10 Jun 2010

Uandishi wa blogu si jambo rahisi kama inavyodhaniwa na wengi.Na ni jambo gumu zaidi kwa akina sie tunaoelemea zaidi katika kuandisha mambo yanayogusa maslahi ya mafisadi na vibaraka wao.Kwa mfano mara kadhaa nimekuwa nikipata comments zenye matusi ya kila aina kutoka kwa baadhi ya wasomaji.Huwa siyachapishi matusi hayo kwa vile naamini wanaotukana wana mtindio wa mawazo na tafakuri.Hoja hujibiwa kwa hoja na wala si matusi.

Ninafahamu matusi hayo yanatoka wapi,na pia natambua kwanini badala ya hoja zangu kujibiwa kwa hoja zao wanakimbilia kutukana.Ni hivi,ukiona mtu anakusema vibaya au kukutukana wakati hujamkosoea lolote ujue mtu huyo hana zuri upande wake,na maneno mabaya au matusi dhidi yako inakuwa kama njia ya mkato ya kupunguza matatizo yake.Watu wa aina hii wanahitaji ushauri nasaha badala ya kuwatukana.Na kibaya zaidi ni kwamba ukimtukana chizi,basi watu watashindwa kutofautisha kati ya nani mzima au mwenye busara na nani chizi.

Lakini wapenda matusi hawa wananipa faraja moja kubwa.Kwamba hadi kufikia hatua ya kutukana kwa njia ya comment kwenye blogu hii inamaanisha walitumia muda wao kusoma nachoandika.Hiyo ni faraja kubwa kwangu kwani walengwa wangu wakuu ni watu makini na sio vichwa panzi kama hao mabingwa wa matusi.

Ujumbe wangu mfupi kwa wazembe hao wa kufikiri ni huu: kasheshe nilizokumbana nazo huko nyuma kutokana na mtizamo wangu ni mara alfu ya hivyo vijimatusi mnavyotuma kama comments.Kwahiyo endeleeni kupoteza muda wenu kutukana lakini mkae mkifahamu kuwa mnachofanya ni sawa na kutegemea damu kutoka kwenye jiwe.

Anyway,nasikitika kupoteza muda wangu muhimu kuwazungumzia wazushi hawa.Lakini yote katika yote,hivi ni vijimambo tu ambavyo once ukiingia kwenye fani ya kublogu lazima utakumbana navyo.

Bring it on!

13 Mar 2010


Wiki hii tumeadimisha siku ya wanawake duniani.Na kesho ni siku ya mama zetu.Ni kipindi mwafaka cha kungalia mchango wa jinsia ya kike katika ngazi ya familia hadi taifa.Tukubali tusikubali,dunia imeendelea kutawaliwa na mfumo dume.Na bara letu la Afrika (na pengine sehemu kubwa ya Dunia ya Tatu) haki za akinamama na mchango wa jinsia ya kike vimeendelea kupuuzwa.Kwa bahati nzuri kwangu,kabla wiki hii muhimu haijamalizika nilipata wasaa wa kuongea na bloga maarufu wa Kitanzania,Sarah Peter,mmiliki wa blogu ijulikanayo kama ANGALIA BONGO. Sihitaji kumpamba kwani ukitembelea blogu hiyo utaafikiana nami kuwa binti huyu licha ya udogo wake wa umri ana kipaji cha hali ya juu katika kuwasilisha ujumbe wake kwa wasomaji wa blog yake na jamii kwa ujumlaNimejijengea mazingira ya kutembelea takriban blogu zote za Watanzania wenzangu kila siku,au angalau mara kadhaa kwa wiki.Licha ya idadi kubwa ya blogu hizo kuwa kwenye blogroll yangu,nina orodha kubwa ya subscription kwenye Google reader,na inanisaidia sana kufahamu kinachoendelea kwenye blogsphere.



Back to Sarah.Nilianza kublog mwaka 2006 na tangu wakati huo blogging imekuwa sehemu muhimu ya maisha yangu.Lakini hadi jana nilikuwa sijakutana na bloga ambaye ndani ya dakika chache alinifumbua macho kwa kiwango kikubwa as to wapi panahitaji marekebisho bloguni mwangu na namna nyingine za kunoresha uwanja huu.Lakini ukidhani hilo ni kubwa zaidi,basi tembelea kwanza hiyo blog ya ANGALIA BONGO kisha utapata picha nzuri zaidi ya nachokieleza.



Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu kuhusu blog hiyo hasa kiu yangu ya kumfahamu vema mmiliki wake.Awali nilidhani kuwa Sarah ni 'mtu mzima' (kiumri) kwani nyingi ya posts zake zimesheheni upeo unaoendana na utu uzima.Tofauti na dhana hiyo,kumbe Sarah ni binti aliyezaliwa miaka ya 80 hivyo ana miaka ishirini na kitu (lakini haifiki 25).Kwa kifupi,ni binti mdogo mwenye akili kubwa na kipaji cha hali ya juu.Na siandiki hivi kwa minajili ya 'kumpa ujiko' (hata ningekuwa nafanya hivyo ingekuwa kazi bure kwani tayari ana 'ujiko' wa kutosha)bali ni katika kutambua mchango wa jinsia ya kike katika fani ya habari hususan kwenye matumizi ya vipasha habari vya jamii (social media) kama blogu.



Hata hivyo,pamoja na mwonekano maridhwawa wa blogu ya ANGALIA BONGO na habari zenye kila ishara kuwa aliyeandika anajua vema anachofanya,kumwelewa vema Sarah kunahitaji uongee nae kama ilivyotokea kwangu jana.Alinipa darasa la chapchap kuhusu mambo mbalimbali ya maana.Na mie ni mwanafunzi mzuri napokutana na mwalimu mzuri.Na haikuchukua muda kwangu kabaini kwamba binti huyu ana akiba kubwa ya akili na kipaji,na hadi sasa kinachotumika ni kiasi kidogo tu cha kipaji na akili hiyo.Sasa kama kiasi kidogo ndio mambo makubwa namna hiyo,ni dhahiri kuwa bloga huyu atakuwa mbali sana akiamua kutumia uwezo wake wote(na anasema atafanya hivyo mbeleni).



Ukiangalia picha zake,unaweza kumhukumu isivyo.Ana mwonekano wa 'kisistaduu' (sina tafsiri sahihi ya neno hili) na ni rahisi kudhani ana 'pozi' (maringo).Lakini hata kama angekuwa hivyo (i.e. sistaduu mwenye pozi),which she is not,character hizo zingefunikwa na kipaji na upeo wake.Sarah anaeleza kwamba yuko into many stuffs japo amebobea zaidi kwenye mambo ya burudani (entertainment).Licha ya background yake kama journalist na radio producer,uwezo wake wa kufikiri na kuandika haraka unachangia sana kuifanya blog yake kuwa mahala pa kumridhisha kila msomaji anayepatembelea.Lakini kingine kinachopendeza katika wasifu wa binti huyu ni imani yake ya kiroho.Anasema kuwa dini ni kitu muhimu sana katika maisha yake,na kwa kuthibiths ahilo ameandika I...always believe in Jesus, Remember İm a pure Christian.Imani thabiti katika dini inasaidia sana kuimarisha vipaji na kutanua upeo,na ni ishara ya karama za Muumba.



Ni dhahiri kuwa bloga huyu ana nafasi ya kufanya mambo makubwa huko mbeleni,na ni matarajio yangu kuwa siku moja Sarah ataitangaza nchi yetu si tu kupitia blog yake bali pia katika fani flani muhimu.Nilimtania kuwa this time in 2012 or so natarajia kumuona akiwa katika delegation ya Mama Asha Rose Migiro,sio kwa vile ni Mtanzania mwenzake bali akiwajibika katika wadhifa flani.Na kama si hilo,basi sintoshangaa akija na chapisho kama Ebony au The Source ya kitanzania.

Kila la heri Sarah!

13 Oct 2009


Hivi karibuni niliandika makala flani kuhusu milipuko ya mabomu huko Mbagala, jijini Dar es Salaam. Kwa kutambua kuwa blogu yangu haina idadi kubwa ya wasomaji (japo nawathamini sana wachache wanaotumia muda wao kuitembelea) niliamua kuisambaza makala hiyo kwa bloga wenzangu wawili ambao “nyumba” zao hupata “wageni” wa kutosha kila siku.

Kwa bahati mbaya, bloga hao waliamua kuiweka makala hiyo kapuni.Siwalaumu,kwa sababu kadhaa. Kwanza, blogu ni mali ya mmiliki, na hilo linampa haki ya kuchagua nini kiwepo kwenye blogu yake na nini kisiwepo.Pili, kila bloga ana mtazamo wake kuhusu mambo mbalimbali yanayotuzunguka, iwe siasa, dini au nyanja nyingine za maisha ya binadamu. Kwa maana hiyo, kama ataletewa makala inayokinzana na mtazamo huo, ana haki ya kuipuuza. Kuna sababu nyingine za kibinafsi lakini sidhani kama zina umuhimu sana.

Makala husika (isome hapa) haikuwa ya matusi, kashfa au utovu wa nidhamu kwa watawala japo ilikuwa ikizungumzia uzembe na kutowajibika kwa baadhi ya viongozi wetu unavyohusika na janga hilo la milipuko ya mabomu.Nilishauri katika makala hiyo kwamba wakati umefika kwa Watanzania kudai haki zao hasa pale zinapopuuzwa makusudi. Kwamba ripoti ya milipuko ya kwanza inaozea katika makabrasha ya Wizara husika, kisha mlipuko mwingine unatokea lakini hakuna anayewajibika, jambo linalohitaji shinikizo la kudai haki na uwajibikaji.

Naamini kwamba laiti makala hiyo ingechapishwa laiti ingekuwa ya kumsifia kiongozi flani au kukumbushia tarehe yake ya kuzaliwa. Au laiti ingekuwa ni tangazo binafsi. Yote hayo ni mazuri kwa vile ni huduma kwa umma. Hata hivyo, harakati tunazohangaika nazo wengine kuboresha future ya nchi yetu ni muhimu pia na hazipaswi kupuuzwa.

Ni rahisi kwangu kuhitimisha kwamba kinachokwanza makala za aina hiyo kuchapishwa ni uoga wa mabloga husika wakihofia kuwaudhi watawala. Japo huo ni uhuru wao kibinadamu, madhara yake kwa jamii ni makubwa kwa vile historia inaonyesha kwamba uoga ni kitalu mwafaka kwa ushamiri wa tawala dhalimu.

Lengo langu si kulaumu bali kushauriana.Kukimbilia kuweka picha za kiongozi akihutubia au akirejea Dar akiwa bukheri wa afya lakini kuchelea kujumuisha maelezo kwamba pia alikumbwa na dhahama ya kiafya ni kutowatendea haki wasomaji wetu. Hapa narejea tukio lililotokea jijini Mwanza hivi karibuni ambapo baadhi ya wenzetu walitonyesha “picha nzuri” za JK lakini “wakabania” maelezo kuhusu mkasa uliomkumba wa kushindwa kuendelea na hotuba yake katika kile kilichoelezwa kuwa “uchovu wa safari.”

Ushirikiano wetu jumuiya iliyojibebesha dhamana ya kuujulisha umma kuhusu mambo mbalimbali usiishie kwenye yanayopendeza machoni pekee bali pia yale yanayoudhi au kukera.

3 Oct 2008

Kuna nyakati huwa napatwa na hisia kwamba baadhi ya makampuni makubwa huko nyumbani (hasa ya kigeni) yanachuma faida kubwa kupita kiasi to an extent of kukurupuka na sherehe zisizo na vichwa wala miguu.Kwa mujibu wa gazeti la Tanzania Daima,kampuni ya Multichoice leo itafanya sherehe za kumpongeza mshiriki wa kwanza kutolewa kwenye Big Brother ya Afrika,Latoya Lyakurwa wa Tanzania.Hivi anapongezwa kwa upuuzi aliofanya ndani ya jumba hilo au kwa kuwa wa kwanza kutolewa katika mashindano hayo?Kama jibu ni ndio kwa swali la kwanza basi huu ni ufisadi wa kimaadili (moral corruption) na kama jibu ni ndio kwa swali la pili basi yayumkinika kuamini kwamba Multichoice wana fedha za kuchezea (pengine kutokana na faida kubwa wanayopata) kupongeza a loser badala ya winner kama ilivyozoeleka.Yaani hata kushindwa nako kunaambatana na sherehe ya pongezi!?

1 Oct 2008

Muhidini Issa Michuzi (left) and Haki Hakingowi
Photo courtesy of MICHUZI

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.