Leo nilishiriki katika mahojiano mawili kuhusu kura ya maoni iliyopigwa hapa Uingereza juzi kuhusu hatma ya uanachama wa taifa hilo kwenye Umoja wa Ulaya, ambapo matokeo yalikuwa kwa Uingereza kujitoa. Mahojiano hayo yalikuwa kati yangu na kipindi cha radio cha Dira ya Dunia ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC na baadaye kipindi cha televisheni cha Dira ya Dunia cha kituo hicho.
Hapa chini ni video na audio ya mahojiano hayo. Karibuni