Ukichanganya "nyomi" kama hilo la kampeni za Dokta Slaa mjini Moshi na matokeo "yaliyominywa" ya Synovate,ni dhahiri Kikwete na mafisadi wako tumbo joto na sasa wanahangaika namna ya kuchakachua matokeo ya Uchaguzi Mkuu ujao.Washindwe na walegee.HATUDANGANYIKI!
Slaa anasa waraka mzito
• NI ULE WA SERIKALI KUIMALIZA CHADEMA
na Janet Josiah na Charles Ndagula, Moshi
MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ametangaza kunasa waraka wa siri ulioandikwa siku nne zilizopita, ambao pamoja na mambo mengine unawaagiza watendaji wakuu wa serikali kufanya kila wawezalo kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinashinda uchaguzi.
Dk. Slaa mwanasiasa mwenye rekodi ya kunasa taarifa mbalimbali nyeti za serikali, alitangaza kuhusu kuuona waraka huo wakati akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza katika Manispaa ya Moshi.
Akizungumzia suala hilo, Dk. Slaa alimtahadharisha mgombea wa urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha anachukua hatua ya kuvidhibiti vyombo vyake vya usalama ili visimwage damu isiyo na hatia kwa sababu tu ya kutaka kushinda urais kwa gharama zozote zile.
Dk. Slaa aliyekuwa akihutubia katika Uwanja wa Mashujaa mjini hapa, alisema dalili zimeanza kujitokeza katika mikoa mbalimbali aliyopita, ambako kumekuwapo na matukio ya watu kuonewa na viongozi wa serikali.
Akifafanua, alisema waraka huo unaokwenda kwa vyombo vya usalama, wakiwemo wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, unawataka wafanye lolote ili kuhakikisha CCM inashinda.
“Ninao waraka ulioandikwa Septemba 19 (Jumapili iliyopita), mwaka huu na leo ni siku ya tatu, unakamilishwa na kusambazwa kwa viongozi hao kuwakumbusha kuwa lazima wahakikishe CCM inashinda, sikuupata hapa hapa, ila tayari umesambazwa nchi nzima,” alisema Dk. Slaa.
Dk. Slaa ambaye ni Katibu Mkuu wa chama hicho, kwa nafasi yake anatoa tamko hilo ili kumtahadharisha Rais Kikwete kuacha mara moja hujuma hiyo, na kuwa dalili zinaonyesha kwamba Watanzania wameamka na wanahitaji mabadiliko.
Alisema pamoja na kupata hujuma hizo, chama chake kimejipanga vyema kukabiliana na mashambulizi ya CCM na serikali yake, kwa kuweka mfumo imara wa ulinzi kwa viongozi wao na wapiga kura wao.
Alivitaka vyombo vya usalama kuacha kuhujumu msafara wake pamoja na watendaji wake, ambao wanatangulia katika vituo ambavyo anafanyia mikutano ya kampeni, kwa kuwa leo serikali ni ya CCM na kesho serikali itakuwa ya CHADEMA.
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo baada ya kupata taarifa za polisi kutaka kuwakamata vijana wa chama hicho, ambao wanapima viwanja vya kufanyia mikutano yao, ambavyo helikopta itaweza kutua kwa urahisi (GPS).
Akizungumza na Tanzania Daima, mmoja wa vijana hao, Gwakisa Gwakisa, alikiri kutaka kukamatwa na polisi hao na kudai kuwa alipowaona alifungua mlango wa gari na kukimbia pamoja na wenzake wachache na kuacha gari la chama hicho, ambalo lilichukuliwa na polisi.
Hata hivyo, Tanzania Daima ilipomuuliza Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko, alikiri kuwa wanalishikilia gari la CHADEMA na kwamba wanamsaka mpima ramani ili wamkamate.
“Bado tunamtafuta mpima ramani wa chama hicho ili baadaye tutoe taarifa kwenu nyinyi waandishi wa habari,” alisema RPC Ng’hoboko.
Akizungumzia tukio hilo, Dk. Slaa amewataka polisi kuwaacha Watanzania wanaotimiza mapenzi yao bila kuwabughudhi na kwamba kero hizo mwisho ni Oktoba 31.
Akiwahutubia wananchi hao mara baada ya kutoa tamko la chama chake, Dk. Slaa aliwaomba wawachague wagombea wa chama chao ili waweze kufufua viwanda ambavyo vimekufa kutokana na sera mbovu za CCM.
“Ndugu zangu wana Moshi, ichagueni CHADEMA kwa kuwa CCM imeshindwa kuwaletea maendeleo, kwa kushindwa kufufua viwanda vyenu kama vile kiwanda cha ngozi, magunia, vyuma na viwanda vingine,” alisema Dk. Slaa.
Mapema akimnadi mgombea huyo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, aliwataka Watanzania kuufanya mwaka huu kuwa wa maamuzi na si wa utani, kwa kuwachagua wagombea makini wa chama hicho.
“Mwaka 2010 hatudanganyiki ndugu zangu wa Moshi…kwa kuwa tutaingia Ikulu na watu makini kama Dk. Slaa, kwa kuwa na nyie ni makini, hivyo mtatuchagua.
“Kwa kuwa CCM ilitumia woga wenu Watanzania kuwatawala na kuwanyanyasa, lakini sasa Watanzania mmeondokana na woga…lakini imani kubwa ipo kwenu wana Moshi, kwa kuwa mmechangia mafanikio ya wana CHADEMA,” alisema Mbowe.
Mkutano huo ulitanguliwa na maandamano makubwa yaliyoanzia katika ofisi za wilaya za chama hicho zilizopo katika Kata ya Majengo na kupita katika barabara za Ghala na Mawenzi, maarufu kama Double Road, Florida hadi katika viwanja vya Mashujaa, huku waandamanaji wakisindikizwa na helikopta iliyokuwa ikiyahamasisha kwa saa nzima.
CHANZO: Tanzania DaimaPICHA KWA HISANI YA Jamii Forums
NAMNA MWAFAKA YA KUMWADHIBU KIKWETE NA MAFISADI NI KWA KUMPIGIA KURA DOKTA WILBROAD SLAA SIKU YA UCHAGUZI HAPO TAREHE 31 OKTOBA.KIKWETE NA CCM YAKE WATAJARIBU KUCHAKACHUA MATOKEO LAKINI HILO LITAWEZEKANA TU KAMA TOFAUTI YA KURA ZA DKT SLAA NA KIKWETE ITAKUWA NDOGO.LA MUHIMU NI KUMPATIA KURA NYINGI MKOMBOZI WETU DOKTA SLAA ILI KIKWETE NA MAFISADI WASHINDWE KUBADILI MATOKEO.KAMA KENYA WALIWEZA KUMG'OA MOI NA KANU BASI HATA SISI PIA TUNAWEZA KUING'OA CCM.
TIMIZA WAJIBU WAKO