Kuna mengi yanasemwa kuhusu mwelekeo mzuri wa Barack Obama katika harakati zake za kuingia Ikulu ya Marekani baadaye mwaka huu.Lakini,je mafanikio ya Obama yanamaanisha kukubalika kwa asilimia 100 kwa mtu mweusi katika jamii ya Waamerika au ni matokeo ya kukwepa kile "weusi wenzie" kama 
Jesse Jackson na 
Al Sharpton wamekuwa wakikipigia kelele?
Binafsi napenda kumuona mtu mweusi (au hata 
half-caste) akiwa 
White House,na kwa maana hiyo ingependeza endapo Januari mwakani Bush angempokea Obama kama "mkazi mpya" katika jumba hilo maarufu hapo 
1600 Pennsylvania Avenue NW.Lakini sioni dalili ya hilo kutokea.Na kumbe siko peke yangu mwenye mtazamo wa namna hiyo.Naendelea kuamini kuwa 
White America bado haiko tayari kumuona mtu mweusi akiwa Rais wa Taifa hilo.Na pengine ndio sababu muhimu ya 
Republicans "kusherehekea" mafanikio ya Obama (wahenga wanatuonya kwamba ukiona adui yako anasherehekea ushindi wako basi ujue ushindi huo utamnufaisha).Wana sababu kuu mbili,moja,wanafahamu ugumu wa kumzuia Hillary Clinton kuingia Ikulu,na pili,wanafahamu wepesi wa kumwangusha Obama pindi akipitishwa kuwa mgombea wa 
Democrats.Niite 
prophet of doom lakini amin nakuambia,pindi Obama akishinda kuwa mgombea,basi shehena zote za 
White America za kumbomoa mwanasiasa zitaelekezwa kwake.Na atakuwa 
target rahisi kwao:watapigia mstari jina lake la kati la Hussein na kulikuza utadhani linamaanisha ugaidi (baadhi yao walishajifanya kuteleza ulimi na 
kumwita Barack Osama),watakumbushia 
confession yake kwamba zamani hizo 
alishawahi kubwia unga na kuvuta bangi.
Anyway,ndani ya
 The Huffington Post kuna makala inayoelekea kurandana na mtizamo wangu kuhusu Obama.