Showing posts with label LIYUMBA. Show all posts
Showing posts with label LIYUMBA. Show all posts

23 Sept 2011


Hatimaye mfungwa maarufu kuliko wote nchini Tanzania kwa miaka ya hivi karibuni,Bwana Amatus Liyumba ameachiwa huru leo.Haijafahamika kama amemaliza kifungo,au amepewa msamaha wa Rais au muda wa kipindi cha maigizo umekwisha.

Na kwa vile fisadi huyu ameachiwa,je wewe mlipakodi umenufaika vipi na kifungo chake?Sikuwahi kusikia kuwa fedha alizokwiba zilitaifishwa,ikimaanisha kwamba anaweza kabisa kutumia jeuri ya fedha hizo kwa kufuru ya kukufanya utamani angeendelea kuzeekea jela.

Na kwa vile habari za kifungo chake huko jela zilikuwa za siri,hatuna uhakika kuwa alikuwa mfungwa wa kawaida-kwa maana ya kutopewa huduma za ki-V.I.P au hata kuwa analala nyumbani kisha asubuhi anarejea jela.

Anyway,kwa sasa habari ndio hiyo.

24 May 2010


Hatimaye kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki Kuu,Amatus Liyumba,inafikia ukingoni leo ambapo atasomewa hukumu.Japo zamani hizoo nilishawahi kuwa 'mnajimu/mtabiri wa kizushi' nilipoandikia magazeti ya Sanifu,Kasheshe na Komesha huku nikijiita 'Ustaadh Bonge' (na baadhi ya watu walikuwa wakiamini 'unajimu' huo),siwezi kwa hakika kubashiri lolote kuhusu hukumu hiyo.Kibaya zaidi,upeo wangu wa taaluma ya sheria ni dhaifu kama uchumi wa Somalia.

Lakini kabla ya kuzungumzia kwa undani kuhusu hukumu hiyo,pengine ni muhimu kuangalia kidogo mwenendo wa kesi hiyo inayogusa hisia za wengi (na wengine wakiwa na sababu zao binafsi).Hadi sasa sielewi mantiki iliyotumika katika kumweka Liyumba gerezani muda wote huu ilhali kisheria yeye anabaki kuwa mtuhumiwa hadi itakapoamuliwa vinginevyo na mahakama.Naomba ieleweke kuwa simtetei Liyumba japo ni 'mwana wa pakaya' kwangu.Ninachohoji hapa ni uhalali wa kumweka mtuhumiwa rumande kwa zaidi ya mwaka mzima pasipo kumpatia dhamana.Hii ni mithili ya kuwa na kiji-Guantanamo chetu ndani ya jamii inayodai kuzingatia utawala wa sheria.Hatari iliyopo ni kwamba kama akishinda kesi,Liyumba anaweza kudai fidia kubwa zaidi ya kiwango anachotuhumiwa kukifanyia ubadhirifu.Afungwe au aachiwe huru,kwa kuwekwa gerezani muda wote huo pasipo kupewa dhamana ni kama alishakuhukumiwa kabla ya hukumu ya leo.Badala ya kuwa 'innocent until proven guilty',hii imekuwa 'guilty until proven innocent'.

Tuje kwenye mwenendo wa kesi yenyewe.Kulikuwa na mikanganyiko kadhaa kwa upande wa mashtaka huku baadhi ya mashahidi wake wakimtetea mshtakiwa waziwazi.Pigo jingine kwa upande wa mashtaka ni kutokuwepo kwa mtu ambaye wangeweza kumfanya 'shahidi nyota' (star witness),aliyekuwa Gavana wa BOT,hayati Daudi Ballali (huyu nae alikuwa 'mwana wa pakaya' just like alivyo 'mrithi' wake,Prof Benno Ndulu).Kwa vile haingekuwa rahisi kwa Liyumba kufanya ubadhirifu huo pasipo Gavana kufahamu kinachoendelea kwa kipindi chote hicho,yayumkinika kusema kuwa marehemu Ballali angekuwa na umuhimu wa kipekee katika kesi hiyo.Na japo 'star witness' huyo hakuwepo,ushahidi ulotolewa na Naibu Gavana na watendaji wengine wa BOT unaweza kutafsiriwa kama 'habari njema' kwake badala ya kumkandamiza.

Halafu kuna tatizo jingine,nalo ni udhaifu wa wanasheria wa serikali/ waendesha mashtaka.Mjuzi mmoja wa masuala ya mahakamani aliwahi kuniambia kwamba wahitimu wa sheria waliofanya vizuri kwenye masomo yao hukimbiliwa na kampuni binafsi za sheria,na hivyo kuwaacha 'wale wa kawaida' wakitarajia ajira kutoka serikalini au vyombo vya sheria vya umma.Sote twaweza kubashiri nini kitajiri pindi wahitimu hawa wanapokutana mahakamani,huku wale wa 'daraja la kwanza' wakiwa upande wa washtakiwa au washtaki dhidi ya serikali.Inaelezwa pia kuwa kipato cha mawakili binafsi kipo juu zaidi ya cha wenzao wa serikalini/taasisi za umma.Ni dhahiri mwanasheria anayelipwa kwa saa au mwenye maslahi bora atakuwa katika nafasi nzuri dhidi ya mwenzie ambaye si ajabu wakati akiwa mahakamani atakuwa bize zaidi kupiga mahesabu ya namna ya kumudu maisha hadi siku ya mshahara wake kijungujiko kuliko kutimiza wajibu wake sawasawa.

Kwa wengi tunaofahamu ugumu kwa mtu wa tabaka la juu kama Liyumba kuhukumiwa kifungo,let alone kufunguliwa mashtaka (akina Chenge 'wanapeta' tu huku kesi ya Pro Mahalu ikisuasua na mafisadi wa Kagoda wakiendelea 'kula bata'),kuna hisia kuwa Liyumba 'anafanyiziwa' tu.Yani,si kwamba anachotuhumiwa kufanya hakikupaswa kumfikisha mahakamani bali ni imani inayozidi kushamiri katika Tanzania yetu kuwa mashtaka na vifungo ni kwa wanyonge na wasio na uwezo wa 'kununua au kutetea haki zao.'Wambeya' wanadai kuwa ishu ya Liyumba inaweza kuwa kama ya 'Babu Seya' ambapo inadaiwa kuwa kesi zao ni matokeo ya 'kuingilia maslahi ya watu'.By 'watu' haimaanishi mie na wewe bali vigogo ambao 'kugusa mali zao' ni zaidi ya kosa la jinai.Inadaiwa kuwa mtu anaweza kufisadi atakavyo na asichukuliwe hatua alimradi hagusi 'mali' za 'wenye nchi'.Na kama hujaelewa by 'mali' namaanisha nini,well,huijui vema Tanzania unayoishi au unayotoka.

Ok,tusubirie hukumu lakini kama umesoma vema between lines katika nilichoandika hapo juu basi utakuwa unafahamu bet yangu ikoje.

21 Feb 2009

ULE MCHEZO WA KUIGIZA KUHUSU "KUTOWEKA" KWA LIYUMBA BADO UNAENDELEA.LATEST EPISODE INAHUSU TAKUKURU KUTANGAZA DONGE NONO KWA ATAYEFANIKISHA KUKAMATWA KWA NDUGU LIYUMBA.

Na Boniface Meena

TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini(Takukuru) imetangaza kutoa donge nono kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi (DPA) wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba ambaye hadi hivi sasa hajulikani halipo.

Wakati Takukuru ikifikia hatua hiyo, tayari kuna wananchi ambao wametoa taarifa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa wanaweza kutoa taarifa za alipo Liyumba. Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana Afisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani alisema wameamua kutangaza doge nono ambalo hakulitaja ni kiasi gani cha fedha ili wananchi wasaidie kupatikana kwa Liyumba. Alisema Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Dk Edward Hoseah ,anakaribisha watu ambao wanaweza kutoa taarifa au kusaidia alipo Liyumba ili aweze kukamatwa.

"Kuna wananchi tumesikia wako tayari kuisaidia Takukuru, tunawakaribisha na Dk Hoseah anawakaribisha ili waweze kutusaidia na donge nono litatolewa kwa atakayesaidia kukamatwa kwa Liyumba," alisema Kapwani.

Wakati Takukuru ikifikia maamuzi hayo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema kama Takukuru itahitaji msaada wa Wizara hiyo kumtafuta Liyumba iko tayari kutoa msaada huo.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili Waziri wa Wizara hiyo, Lawrance Masha alisema wakipewa maombi ya kumtafuta Liyumba, watasaidia kumtafuta kwa kuwa wote ni Serikali. "Juzi nilitoa tamko kuwa hatujaletewa maombi ya kumtafuta, lakini Takukuru wakituletea tutafanya hivyo, kwa kuwa sisi ni Serikali," alisema Masha.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilifuta dhamana ya Liyumba Februari 19 na kutoa amri ya kuwakamata wadhamini wake ambao walikamatwa siku hiyohiyo na baadaye kuachiwa. Wadhamini hao ni wafanyakazi wa BoT Benjamin Nduguru (mhasibu wa benki hiyo) na Agaterus Oto (Afisa Usalama wa ndani wa benki hiyo).

Hata hivyo, licha ya mahakama kufuta dhamana kuwakamata wadhamini hao, ilitoa amri ya kumtafuta na kumkamatwa Liyumba.Liyumba pamoja na aliyekuwa Meneja Miradi wa BoT, Deogratius Kweka wameshitakiwa mahakamani kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka yao katika mradi wa ujenzi wa majengo pacha ya benki hiyo na kuisababishia hasara serikali jumla ya Sh221 bilioni.

Liyumba alipewa dhamana na Hakimu Mkaazi wa Kisutu, Hadija Msongo kwa kutumia hati ya nyumba yake iliyoko Mbezi Juu, jijini Dar es Salaam yenye thamani ya Sh800 milioni, ambayo hata hivyo ililalamikiwa na upande wa mashitaka kwamba imetolewa katika mazingira tata kwa kuwa haijafikisha kiwango cha Sh50 bilioni walizotakiwa kutoa

Juzi Wakili wa serikali, Prosper Mwangumila aliileza mahakama kwamba, Liyumba bado hajapatikana. Hakimu alisema amri ya kumkamata Liyumba bado inaendelea na ya kuwakamata wadhamini imesitishwa hadi kesi itakapotajwa Februari 24, mwaka huu.

Katika hatua nyingine Mawakili wanaomtetea mtuhumiwa huyo waliulalamikia upande wa mashitaka kwa kitendo chake cha kuwanyanyasa ndugu wa mtuhumiwa huyo ambapo walidai kuwa uliwanyang’anya baadhi ya mali zao.

Mmoja wa mawakili hao wa utetezi, Majura Magafu aliiomba mahakama kutoa amri ya kuutaka upande wa mashitaka kuacha kuinyanyasa familia ya Liyumba na kwamba warudishe gari ya mmoja wa wadhamini ambayo waliikamata. Akijibu hoja hiyo, Hakimu Msongo aliutaka upande wa utetezi kama una maombi yoyote kuyapeleka kwa utaratibu wa mahakama kwa kuwa juzi haikuwa tarehe ya kesi.

Wakati akitoa dhamana hiyo Februari 17, mwaka huu, Hakimu Msongo alisema mshitakiwa huyo, atakuwa nje kwa dhamana ya Sh882 milioni wakati mahakama inajiridhisha na hati nyingine zilizopingwa na upande wa mashitaka. Alisema mshitakiwa atatakiwa kutimiza masharti ya dhamana ya kiasi kilichobaki cha Sh54,417,344,800.23 endapo mahakama itabaini kuwa hati hizo zina kasoro.

Hata hivyo baada ya kutolewa maamuzi hayo Wakili wa serikali Justus Mulokozi alisema hawajaridhika na maamuzi yaliyotolewa na kwamba watakaa kuyajadili na kuyatolea maamuzi. Upande wa mashitaka ulipinga kupokelewa kwa hati 10 kati ya 11 zilizowasilishwa mahakamani hapo na upande wa utetezi kwa madai kuwa zina kasoro, zikiwemo za kuwa na mali zisizokuwa za kudumu kama mbuzi, ng’ombe na kuku.

Siku mbili baada ya mtuhumiwa huyo kuachiwa huru na mahakama kutokana na kutimiza masharti, mahakama ilitoa amri ya kukamatwa tena jambo lilosababisha wadhamani wake kushikiliwa kwa muda na kisha kuachiwa.

Liyumba na Kweka walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza , Januari 27, mwaka huu kwa tuhuma za kutumia madaraka yao vibaya na kuisababishia hasara serikali kiasi cha Sh 221 bilioni. Kweka bado hajapata dhamana.



TATIZO KUBWA LA VYOMBO VYETU VYA HABARI NI KURIPOTI HABARI AU MATUKIO BADALA YA KWENDA NDANI ZAIDI NA KUCHUNGUZA YALIYOJIFICHA KATI YA MISTARI.KWA MFANO,KWANINI HATUJIULIZI SABABU WA WADHAMINI WA LIYUMBA KUKAMATWA KISHA KUACHIWA?JE WADHAMINI HAO NAO "WAKITOWEKA" SI ITAMAANISHA "KIFO CHA ASILI" CHA KESI HIYO?

HIVI HATUWEZI KUJIULIZA SABABU ZA HAKIMU KUTOA DHAMANA KWA MSHTAKIWA JAPO DHAMANA HIYO ILIKUWA NA MAPUNGUFU?NAFAHAMU NI HAKI KWA MSHTAKIWA KUPATIWA DHAMANA LAKINI SHARTI ATIMIZE MASHARTI YA DHAMANA HIYO.

WIZI MTUPU!

20 Feb 2009

Picha kwa hisani ya KENNEDY.
HUU NI USANII WA MCHANA MWEUPE.UNFORTUNATELY,VYOMBO VYETU VYA HABARI VIMEKUWA MAKINI ZAIDI KATIKA KURIPOTI MATUKIO BADALA YA KUYAFANYIA UCHUNGUZI HABARI.WELL,HII NDIO BONGO BWANA.


PENGINE UTASEMA NI MAPEMA MNO KUWA PESSIMIST,LAKINI YAYUMKINIKA KUAMINI KWAMBA NI VIGUMU SANA KWA MTUHUMIWA MWENYE UWEZO WA KIFEDHA KUHUKUMIWA KWA KOSA LOLOTE ALILOTENDA,HATA KAMA KUNA USHAHIDI WA WAZIWAZI.


HIVI INAINGIA AKILINI KWELI KWAMBA TUHUMA DHIDI YA LIYUMBA NI PAMOJA NA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA KATI YA MWAKA 2001 HADI 2006?KAMA HUJAELEWA MANTIKI YA SWALI LANGU NI KWAMBA HUU NI MWAKA 2009.SO,INA MAANA MATUMIZI HAYO MABAYA HAYAKUWEZA KUGUNDULIKA KWA KIPINDI CHOTE HICHO CHA MIAKA MITANO?HIVI BENKI KUU HAIFANYIWI UKAGUZI WA MAHESABU KILA MWAKA?IF SO,KWANINI WAKAGUZI HAO WASIULIZWE KUHUSU TAARIFA ZA MWAKA 2001-2006?OK,TUACHANE NA WAKAGUZI.VIPI KUHUSU INTERNAL SECURITY NDANI YA BENKI KUU?HAWA WATU WANALIPWA KWA AJILI YA KAZI GANI IWAPO FEDHA ZILIKUWA ZIKITUMIKA KWA MIAKA MITANO MFULULIZO PASIPO WAO KUSHTUKA.


PENGINE JIBU LA SWALI HILO LA MWISHO LINAWEZA KUPATIKANA KWENYE TAARIFA KWAMBA MMOJA YA WADHAMINI WA LIYUMBA NI AFISA USALAMA WA BENKI HIYO.DOES THIS MAKE ANY SENSE?AFISA USALAMA WA BENKI ANAMDHAMINI MTUHUMIWA ANAYAYESHTAKIWA KWA UBADHIRIFU WA FEDHA KATIKA BENKI HIYOHIYO!?


HAYA TWENDE KWENYE SUALA ZIMA LA DHAMANA.KAMA LIYUMBA ALIKUWA HAJATIMIZA MASHARTI YOTE YA DHAMANA KWANINI BASI HAKIMU ALITOA DHAMANA HIYO?INAELEZWA KWAMBA DHAMANA ILIYOTOLEWA ILIKUWA NA MAPUNGUFU YA MAMILIONI KADHAA.HALAFU ETI KWA USANII,WAENDESHA MASHTAKA WALINUKULIWA WAKIDAI HAWAJARIDHISHWA NA DHAMANA HIYO.


HUU NI MCHEZO WA KUIGIZA.NA NDIO MAANA UKISOMA MAGAZETI KADHAA UTAGUNDUA STORI ZINALINGANA.HII BUZZ IS MOST LIKELY ENGINEERED BY SOMEONE WHO'S BEHIND ALL THIS FRAUD.WANATANGAZA KWA SAUTI KUWA LIYUMBA KATOWEKA (JAPO TUNAAMBIWA ETI PASSPORT YAKE ILIKUWA IMEZUILIWA) ILI BAADAE WATANZANIA WASAHAU KAMA WALIVYOSAHAU KUHUSU BALLALI,MAJAMBAZI WA RICHMOND,MAFISADI WA KAGODA,NK.

WANAFANYA HIVI KWA VILE WANAFAHAMU BAYANA KUWA WATANZANIA NI WAPOLE,HAWAKAWII KUSAMEHE NA KUSAHAU MABAYA.

HII NDIO BONGO YETU!AU KAMA WANAVYOSEMA SIKU HIZI, WIZI MTUPU

17 Jan 2008


Gavana mpya wa Benki Kuu,Profesa Benno Ndulu,amefanya mabadiliko kadhaa katika uongozi wa benki hiyo.Katika mabadiliko hayo,Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala (DAP) wa B.O.T,AMATUS LIYUMBA (pichani) ameondolewa katika wadhifa huo.Habari kamili soma hapa.
(Picha hii ya zamani ya Liyumba ni alipokuwa Mkuu wa Chuo cha BoT 1993-2000)

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.