Showing posts with label Michezo na Burudani. Show all posts
Showing posts with label Michezo na Burudani. Show all posts
3 Mar 2015
6 Feb 2015
YAMOTO BAND COMFIRMED will performing all their major hits including NITAJUTA, NISEME, WAMBEA, NITAKUPWELEPWETA and many more @ The Royal Regency Banquet Hall, Sat 21 Feb 2015 From 8pm to 3:30am, there are limited VIP Tables available book yours now for ultimate VIP treatment or individual place your booking early to avoid disappointment. Table bookings please call 07405824696/ WhatsApp +447557304940
[email protected] or [email protected]
Usiku wa tarehe 21 February 2015 The Royal Regency patakuwa hapatoshi. Kwa kuondosha usumbufu wahi ticket yako mapema
Kiingilio ni:
£25 kwa Ticket ya kawaida
£35 kwa VIP ticket
[email protected] or [email protected]
Ukumbi wa Royal Regency ndio sehemu pekee ambayo utawaona YAMOTO BAND kwenye jiji la LONDON usiku wa 21. Feb 2015
Usiku wa tarehe 21 February 2015 The Royal Regency patakuwa hapatoshi. Kwa kuondosha usumbufu wahi ticket yako mapema
Kiingilio ni:
£25 kwa Ticket ya kawaida
£35 kwa VIP ticket
Kama Unahitaji VIP table for 10 people piga simu 07405824696 kwa maelezo zaidi au tuma email kwenda: [email protected] or [email protected]
YAMOTO BAND will be alongside supported artist such as Sultan King, OJ, Hyper hype And many more,why wait grab your ticket Now!!!!
HOT LINE FOR TICKET 07853482158/07557304940
--
Regards,
Jestina George
Mobile +44 7557 304 940
Email: [email protected]
website: www.jestina-george.com
4 Nov 2014
15 Oct 2014
Dunia yetu imesheheni watu wanaoitwa 'conspiracy theorists,' Sina uhakika wa tasiri ya kiswahili ya neno hilo, lakini nadhani neno la karibu ni 'wazushi.' Hata hivyo, tofauti ya wazushi tuliowazowea ambao mara nyingi huzusha jambo kwa minajili ya kuzusha tu, kwa conspiracy theorist uzushi wao huambatana na 'ushahidi wa kimazingira,' japo si ajabu ushahidi huo nao kuelemea zaidi kwenye uzushi kuliko facts.
Sasa msanii maarufu wa Marekani, Chris Brown, nae ameingia katika kundi la conspiracy theorists baada ya kudai kuwa ugonjwa hatari wa Ebla ni moja ya mbinu za kudhibiti idadi ya watu duniani.
Msanii huyo ali-post mtizamo wake huo kwenye ukurasa wake wa Twitter, ambapo ana 'wafuasi' (followers) milioni 13.7. Hata hivyo, baadhi yao walipingana nae waziwazi
"Wajua mjadala kuhusu ugonjwa wa Ebola ulichokuwa unahitaji? Upuuzi zaidi. Hapa anaingia Chris Brown..." aliandika mmoja wa wafuasi wake.
"Chris Brwon anadai Ebola ni moja ya mbinu za kudhibiti idadi ya watu. Ajaribu ugonjwa." alitwiti mwingine huo akimaanisha msanii huyo ni miongoni mwa watu wanaohitaji kudhibitiwa.
"Chris Brown anadai kuwa Ebola ni njia ya kudhibiti widadi ya watu. Kwa hakika hiyo si kweli, na laiti ingekuwa kweli basi tungempa ugonjwa huo yeye kwanza," aliandika mwingine.
Brown ambaye hivi karibuni alitumikia kifungo cha siku 108 jela kwa kukiuka taratibu za uangalizi wa kimahakama (probation) kufuatia kosa la kumpiga mpenzi wake wa zamani, msanii Rihanna, baadaye alionekana kutafakari upya kauli yake, na kutanabaisha kuwa 'anafunga mdomo wake,' japo si kwa maneno ya kistaarabu.
Lakini muda mfupi baadae 'alipandisha mzuka' na kuwashambulia waliopingana na mtizamo wake huo, na kutwiti maneno makali: "naandika ninachotaka. Kama hutaki nyonya %$*£$ yangu (tusi)
Hata hivyo, licha ya baadhi ya watu kupingana na conspiracy theory hiyo ya msanii huyo, watu kadhaa katika mtandao huo wa Twitter walionekana kuafikiana nae kwa tweet hiyo kupata takriban 'Retweets' 30,000 na 'Favourites' 22,000.
Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola umeshasababisha vifo zaidi ya 4000 huku Afrika ya Magharibi ikiwa ni eneo lililoathirika vibaya zaidi japo tayari kuna wagonjwa wachache waliokumbwa na maradhi hayo huko Hispania na Marekani.
CHANZO: Imetafsiriwa kutoka mtandaoni
24 Aug 2014
Chris Brown akielekea kwenye Lamborghini lake kuondoka katika klabu ya usiku palipotokea shambulio la risasi |
Majeruhi akitibiwa |
Chris Brown 'akijirusha' kabla ya shambulio |
Mastaa wengine waliokuwa kwenye pati hiyo ni pamoja na Justin Beiber na rapa The Game.
Justin Beiber alikuwa miongoni mwa waliohudhuria pati hiyo, kama ilivyokuwa kwa rapa The Game (pichani chini) |
Chrsi Brown akiruka kuelekea eneo la baa baada ya milio ya risasi |
Akimaanisha 'Jamii haiwezi kustarehe au kuburudika pasipo mikwaruzo.'
Majeruhi wakiingizwa kwenye gari la kubebea wagonjwa |
Chris Brown akiwa ametahayari baada ya shambulio hilo
CHANZO : The Mail Online
|
9 Aug 2014
Klabu Bingwa ya Soka hapa Scotland, imepewa ushindi wa bure katika hatua ya awali kuelekea michuano ya soka Ligi ya Mabingwa (Champions League) barani Ulaya, licha ya kutwangwa bao 6-1 na Legia Warsaw ya Poland.
Celtic walifungwa mabao 4-1 katika mechi ya kwanza iliyofanyika Warsaw, Poland, kabla ya kupewa kipigo kingine cha mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano uliofanyika Edinburgh hapa Scotland.
Hata hivyo, timu hiyo ya Poland imeadhibiwa na Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) kwa kunyang'anywa ushindi na kutolewa mashindanoni kwa kuchezesha mchezaji asiyestahili, na badala yake Celtic wamepewa ushindi wa mabo 3-0, na sasa watachuana na Maribor ya Slovenia.
Hii ni mara ya pili kwa mabingwa hao wa Scotland kuangukiwa na bahati kama hiyo. Mwaka 2011, timu hiyo ilirejeshwa katika Ligi ya Europa licha ya kutolewa kwa mabao 3-1 na timu ya Sion ya Uswisi. Kama ilivyotokea hivi, sasa, kosa la Sion lilikuwa kuchezesha wachezaji wasiostahili
24 Jul 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)