31 May 2009







Glenn Beck is the fastest-rising star on American TV. He's part of a right-wing broadcasting boom that's become the most powerful opposition to the President...CONTINUE.



30 May 2009


MHH,AJALI ZINAZOWAANDAMA WABUNGE "WA AINA MOJA" ZINAWEZA KUZUA MASWALI YA NAMNA FLANI JAPO YAWEZEKANA KABISA KUWA NI AJALI KAMA NYINGINEZO.HEBU SOMA KWANZA HABARI IFUATAYO,KISHA TUJIULIZE MASWALI MAWILI MATATU:

Ally Sonda na Rehema Matowo, Mwanga

MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, Aloyce Kimaro amenusurika kufa baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kuparamia mawe yaliyopangwa barabarani na kupata ajali usiku wa kuamkia jana. Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na Kimaro na polisi zinasema kuwa, ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Mikongeni kata ya Lembeni wilayani Mwanga, Kilimanjaro kwenye barabara kuu ya Moshi-Tanga, akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kwenda jimboni kwake.

Kwa mujibu wa habari hizo, wakati ajali hiyo inatokea, Kimaro alikuwa na rafiki yake Joseph Temu ambaye ndiye aliyekuwa anaendesha gari hilo aina ya Mercedes Benz akiwa na mkewe na watoto wake watatu. Katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa.

Kimaro alisema baada ya ajali hiyo mfanyabiashara wa Mwanga, Shafii Hasanal alitoa msaada wa kulivuta gari hilo hadi kwenye kituo cha mafuta Kisangara.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko alisema kuwa ajali hiyo ilitokea saa 2:30 usiku, chanzo kikiwa ni mawe makubwa na matofali yaliyokuwa yamepangwa barabarani katika eneo lenye kona na mlima.

Kamanda Ng’hoboko alisema kuwa watu wanaosadikiwa kuwa ni wezi, walipanga mawe hayo barabarani kwa lengo la kusababisha ajali ili kuwaibia abiria.

“Gari ya mbunge huyo ilipofika katika eneo hilo likiwa katika mwendo wa kawaida na mbele yao kukiwa na lori ambalo liliweza kuyapita mawe hayo bila tatizo, wao walipojaribu kuyapita tairi la mbele upande wa kulia na ‘sampo’ ya gari hilo vilipasuka wakashindwa kuendelea na safari,” alisema Ng’hoboko.

Kamanda huyo alisema kuwa miaka ya nyuma eneo hilo lilikuwa na matukio mengi ya aina hiyo ambayo yameanza kujitokeza upya, kwa kuwa awali wananchi wa eneo hilo kwa kushirikiana na polisi walikuwa wameyamaliza. Alibainisha kuwa polisi wanafanya operesheni ili kuwadhibiti wezi hao na kuwasaka waliohusika na tukio hilo ili wafikishwe mbele ya sheria.


Kimaro ni miongoni mwa wabunge waliojitokeza hadharani kupambana na vitendo vya ufisadi. Mwaka jana aliibua hoja bungeni kutaka, Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa ashitakiwe kwa kutumia madaraka vibaya ya kufanya biashara akiwa ikulu.

Hii ni ajali ya pili inayohusisha wabunge kutokea ndani ya wiki mbili baada ya ajali iliyomhusisha mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe iliyotokea eneo la Ihemi, Ifunda mkoani Iringa. Dk Mwakyembe, alinusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Kyela kwenda Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka.

Ripoti ya polisi iliyotolewa wiki hii ilieleza kwamba ajali hiyo ilitokana na uzembe wa dereva, lakini mbunge huyo ameiponda na kuifananisha na ripoti ya mpiga ramli kwa vile haikuzingatia vigezo na utaalamu katika uchunguzi.


CHANZO: Mwananchi
NAAMINI WENGI WETU TUNAKUMBUKA AJALI ILIYOMHUSISHA MHESHIMIWA CHEYO a.k.a "Mzee wa Vijisenti" AMBAYO ILIPELEKEA VIFO VYA WATU WAWILI.TOFAUTI KATI YA AJALI YA CHENGE NA HIZI ZA MWAKYEMBE NA KIMARO NI REACTION YA POLISI.BAADA YA GARI LA CHENGE KUUA,SIKUWAHI KUSIKIA RPC AU RTC AKIKURUPUKA KUELEZA CHANZO CHA AJALI HUSIKA (JAPO KATIKA MAZINGIRA YA KAWAIDA,NI RAHISI KUIHUSISHA AJALI YA SAA 10 ALFAJIRI NA STIMU ZA KILEVI).BADALA YAKE ILIUNDWA TUME AMBAYO HADI LEO HAIJATUELEZA MATOKEO YA UCHUNGUZI WAKE (IF AT ALL ILIFANYA UCHUNGUZI).WORSE STILL,INAELEZWA KUWA WAKATI AJALI HIYO INATOKEA GARI LA CHENGE LILIKUWA NA BIMA ILIYOISHA MUDA WAKE.


ALIPOPATA AJALI MWAKYEMBE,RPC AKAKURUPUKA NA KUDAI KWAMBA CHANZO CHA AJALI NI MWENDO MKALI NA SHIMO LILILOKUWA BARABARANAI.BAADAYE TUME YA KAMANDA KOMBE IKAZIDI KUCHANGANYA MADAWA KWA KUTOA FINDINGS AMBAZO SI TU ZIMEINGILIA KAZI YA MAHAKAMA KWA KUWAHUKUMU MWAKYEMBE (kuwa alikuwa amelala wakati wa ajali) NA DEREVA WAKE (kwa uzembe) LAKINI PIA HAZIKUHUSISHA MAELEZO YA MWAKYEMBE KWA VILE HAKUHOJIWA NA TUME HIYO!


KINGINE CHA KUSHANGAZA NI KWAMBA WHILE KWENYE AJALI YA CHENGE,DEREVA WA BAJAJI NA MMILIKI WAKE WALIAMRIWA KUJISALIMISHA POLISI MARA MOJA,HATUJASIKIA KAULI YOYOTE KUTOKA KWA POLISI KUHUSU DEREVA WA LORI LILIOHUSIKA KWENYE AJALI YA MWAKYEMBE!


NA SASA KATIKA AJALI YA KIMARO TUNAELEZWA KUWA MAWE HAYO YALIPANGWA NA WEZI.HOW DID THE POLICE KNOW KUWA WALIOFANYA HIVYO NI WEZI NA SIO WATU WALIOKUWA WANAWINDA UHAI WA MHESHIMIWA KIMARO?KWANINI(ANGALAU KWA KUTUZUGA) ISIUNDWE TUME KAMA ILE YA AJALI YA CHENGE AMBAPO HAKUKUWA HATA HAJA YA KUFANYA SPECULATION LET ALONE KUUNDA TUME?


CALL ME A CONSPIRACY THEORIST,LAKINI NADHANI AJALI HIZI ZINA TAFSIRI KUBWA ZAIDI YA TUNACHOSIKIA AU KUONA KWA MACHO YETU.LET'S WAIT AND SEE!



29 May 2009

ILIKUWA SIKU,WIKI,MIEZI NA SASA UMETIMIA MWAKA TANGU BWANA ALIPOKUCHUKUA MPENDWA WETU MAMA ADELINA MAPANGO (Mama CHAHALI).PENGO ULILOTUACHIA HALITOZIBIKA MILELE.KINACHOTULIWAZA NI MAPENZI YA BWANA.JAPO SIE TULIKUPENDA,LAKINI YEYE ALIKUPENDA ZAIDI,NA NDIO MAANA AKAKUCHUKUA SAA4.30 USIKU WA TAREHE 29/05/2008.JAPO HAUKO NASI KIMWILI,LAKINI TUKO SOTE KIROHO.

KWA NIABA YA FAMILIA YA MZEE PHILEMON CHAHALI,NACHUKUA FURSA HII KUTOA SHUKRANI ZA DHATI KWA WOTE WALIOSHIRIKIANA NASI KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA SALA/DUA WAKATI TUNAMUUGUZA MAREHEMU ADELINA,NA SAPOTI MLIYOTUPATIA KUTUFARIJI BAADA YA MSIBA.BWANA AWABARIKI SANA.

BWANA ALITOA,BWANA ALITWAA.JINA LAKE LIHIMIDIWE MILELE,AMEN.

PUMZIKO LA MILELE UMPE EE BWANA,NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE.APUMZIKE KWA AMANI.AMEEN

27 May 2009





CLICK HERE for more on the nomination including reactions.

24 May 2009


CLICK HERE for more.

CLICK HERE for full story from various sources.

23 May 2009



CLICK HERE for full story

22 May 2009

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.