Picha kwa hisani ya MJENGWA
27 Apr 2013
22 Apr 2013
Kikwete Anakimbia kivuli Chake? Adai Nchi Haijamshinda, Anaimudu,Adai ni majungu ya wapuuzi wachache

KWA mara ya kwanza, Rais Jakaya Kikwete amewabeza watu wote, wanaodai kuwa ameshindwa kuongoza nchi.
Akizungumza na Watanzania waishio nchini Uholanzi na taarifa yake kurushwa na kituo cha runinga cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), mwishoni mwa wiki, Rais Kikwete alisema kamwe hajashindwa kuongoza na kusisitiza kama angeshindwa angechukua uamuzi sahihi.
“Sijashindwa kuongoza nchi kama watu wengine wanavyosambaza taarifa za kizushi na fitina, nachojua mimi nchi iko katika mikono salama na ninaimudu.
“Msikae na kusikiliza maneno ya wapuuzi wachache ambao wamekuwa wakieneza maneno yao ya umbea katika mitandao na mikutano ya kisiasa.
“Ukiacha matukio machache ya uvunjifu wa amani ambayo Serikali yangu imekuwa ikiyashughulikia, tumefanikiwa kudhibiti hali hiyo na Watanzania wanaendelea na shughuli zao kama kawaida,” alisema Rais Kikwete.
Alisema japo kuongoza watu ni kazi ngumu na nzito, lakini yeye binafsi ameweza kuongoza kutokana na kulelewa na kukulia katika maadili mema ya uongozi.
Alisema kutokana na misingi hiyo, haoni haja ya kupigizana kelele na watu ambao hawamtakii mema katika uongozi wake.
Aliwataka Watanzania waishio nchini Uholanzi, kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri kwa kutangaza vivutio vya utalii na rasilimali zinazopatikana Tanzania ili kuwavutia.
Kuhusiana na migogoro ya kidini ambayo imekuwa ikitokea nchini, Rais Kikwete aliwataka Watanzania kuhakikisha wanaenzi na kulinda tunu ya umoja na amani, iliyoasisiwa na viongozi wake, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na mwasisi wa Zanzibar, Hayati Sheikh Amani Karume.
“Watanzania tumeachiwa tunu ya amani na umoja kutoka kwa waasisi wa taifa letu, tunapaswa kuienzi, kuilinda na kuidumisha kwa maslahi ya nchi yetu na vizazi vijavyo,” alisema Kikwete.
Kwa muda mrefu, baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakimshutumu Rais Kikwete kuwa nchi imemshinda kutokana na kukumbwa na misukosuko mingi.
Miongoni mwa misukosuko hiyo, ni pamoja na mgomo wa madaktari, mgomo wa walimu, mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), mauaji ya watu, kutekwa na kujeruhiwa vibaya.
Tuhuma nyingine, ni tatizo la kuenea kwa udini ambalo limesababisha vifo kadhaa Tanzania Bara na Zanzibar.
Lakini katika matukio hayo yote Rais Kikwete amekuwa akiyakemea na kuwataka Watanzania waishi kama ndugu.
Akizungumza na Watanzania waishio nchini Uholanzi na taarifa yake kurushwa na kituo cha runinga cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), mwishoni mwa wiki, Rais Kikwete alisema kamwe hajashindwa kuongoza na kusisitiza kama angeshindwa angechukua uamuzi sahihi.
“Sijashindwa kuongoza nchi kama watu wengine wanavyosambaza taarifa za kizushi na fitina, nachojua mimi nchi iko katika mikono salama na ninaimudu.
“Msikae na kusikiliza maneno ya wapuuzi wachache ambao wamekuwa wakieneza maneno yao ya umbea katika mitandao na mikutano ya kisiasa.
“Ukiacha matukio machache ya uvunjifu wa amani ambayo Serikali yangu imekuwa ikiyashughulikia, tumefanikiwa kudhibiti hali hiyo na Watanzania wanaendelea na shughuli zao kama kawaida,” alisema Rais Kikwete.
Alisema japo kuongoza watu ni kazi ngumu na nzito, lakini yeye binafsi ameweza kuongoza kutokana na kulelewa na kukulia katika maadili mema ya uongozi.
Alisema kutokana na misingi hiyo, haoni haja ya kupigizana kelele na watu ambao hawamtakii mema katika uongozi wake.
Aliwataka Watanzania waishio nchini Uholanzi, kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri kwa kutangaza vivutio vya utalii na rasilimali zinazopatikana Tanzania ili kuwavutia.
Kuhusiana na migogoro ya kidini ambayo imekuwa ikitokea nchini, Rais Kikwete aliwataka Watanzania kuhakikisha wanaenzi na kulinda tunu ya umoja na amani, iliyoasisiwa na viongozi wake, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na mwasisi wa Zanzibar, Hayati Sheikh Amani Karume.
“Watanzania tumeachiwa tunu ya amani na umoja kutoka kwa waasisi wa taifa letu, tunapaswa kuienzi, kuilinda na kuidumisha kwa maslahi ya nchi yetu na vizazi vijavyo,” alisema Kikwete.
Kwa muda mrefu, baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakimshutumu Rais Kikwete kuwa nchi imemshinda kutokana na kukumbwa na misukosuko mingi.
Miongoni mwa misukosuko hiyo, ni pamoja na mgomo wa madaktari, mgomo wa walimu, mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), mauaji ya watu, kutekwa na kujeruhiwa vibaya.
Tuhuma nyingine, ni tatizo la kuenea kwa udini ambalo limesababisha vifo kadhaa Tanzania Bara na Zanzibar.
Lakini katika matukio hayo yote Rais Kikwete amekuwa akiyakemea na kuwataka Watanzania waishi kama ndugu.
CHANZO: Mtanzania
ANAKIMBIA KIVULI CHAKE?
22.4.13
Evarist Chahali
RAIA MWEMA
No comments
WAKATI Tanzania imetimiza zaidi ya miaka 20 tangu yatokee mageuzi ya kisiasa yaliyosababisha kuruhusiwa kwa siasa za vyama vingi, kuna haja ya kufanya tathmini japo fupi kwa minajili ya kuyafanya mageuzi hayo yawe na manufaa kwa nchi yetu.
Miongoni mwa machapisho mbalimbali yanayozungumzia suala la mageuzi ya kisiasa barani Afrika ni kitabu maridhawa kilichohaririwa na Profesa Adebayo Olukushi, kinachoitwa The Politics of Opposition in Contemporary Africa (yaani, Siasa za upinzani katika Afrika ya sasa).
Katika tafiti zilizofanyika kwenye nchi saba za Afrika (na ambazo zimejadiliwa katika kitabu hicho) masuala kadhaa ‘yasiyopendeza’ yalibainika. Masuala hayo ni pamoja na
Mosi, tawala zilizokuwa madarakani (wakati wa mageuzi) kuridhia kwa ‘shingo upande’ mageuzi hayo, na matokeo yake tawala hizo zimeendelea kuyakwaza, kunyanyasa wapinzani sambamba na kuwadhoofisha na ‘kuwafitini.’
Pili, uungaji mkono wa taasisi mbalimbali (za umma na za binafsi) uliondolewa kwa kila aliyeonekana kuwa karibu au kuwaunga mkono wapinzani, na hii imeathiri uwezo wa kiuchumi wa vyama vya upinzani hususan kwa wafanyabiashara kuchelea ‘hasira za watawala’ pindi wakitambulika kuwa wanawasaidia wapinzani.
Tatu, vyama tawala kupata upendeleo zaidi ya vyama vya upinzani katika maeneo mbalimbali, hususan kutoka kwa vyombo vya habari vya umma na taasisi za usalama (ambavyo licha ya kushiriki ‘kuchakachua’ matokeo ya chaguzi mbalimbali pia vimekuwa vikiwanyanyasa na kuwaonea wapinzani).
Nne, mfumo wa uchaguzi wa ‘mshindi kuchukua vyote’ (winner takes all) umekuwa kikwazo kwa wapinzani ambapo idadi ya viti wanavyoshinda kwenye chaguzi havilingani na mgawanyo wa kura.
Tano, katika kukimbilia kwao kushiriki kwenye chaguzi chini ya mfumo wa vyama vingi, vyama vya upinzani vilijinyima fursa muhimu ya kudai mabadiliko ya Katiba ambayo yangesaidia uendeshaji wa shughuli za kisiasa wakati na baada ya chaguzi.
Sita, harakati za kisiasa za vyama vya upinzani kutegemea mno misaada au uungwaji mkono kutoka nje yao.
Japo kitabu hicho kilichapishwa miaka 15 iliyopita, tafiti husika zilifanywa nchini Kenya, Zimbabwe, Niger, Nigeria, Senegal, Afrika ya Kusini na Uganda, takriban vipengele vyote nilivyotaja hapo juu vinaakisi hali ilivyo huko nyumbani.
Wakati chaguzi mbalimbali zilizofanyika huko Kenya, Nigeria na Afrika Kusini zinaweza kutoa picha tofauti kiasi na inayobainishwa kwenye kitabu hicho, yayumkinika kuhitimisha kuwa kwa Tanzania yetu hali inaelekea kubaya zaidi. Nitafafanua.
Tuweke kando tawala za Awamu ya Kwanza na ya Pili (angalau kwa minajili ya mjadala huu), Awamu zilizofuatia (ya Rais Benjamin Mkapa na ya sasa ya Rais Jakaya Kikwete) kwa kiasi kikubwa zimetawaliwa na harakati na mikakati ya makusudi si tu ya kudhoofisha siasa za upinzani bali pia kuutokomeza kabisa upinzani.
Hata hivyo, tofauti na ilivyokuwa zama za Mkapa ambaye wapinzani wataendelea kukumbuka kwa hotuba zake kali dhidi yao, sambamba na ‘kuwaponda’ mara kwa mara, ni nadra kwa Kikwete ‘kuwapiga vijembe’ wapinzani, na hata anapofanya ni rahisi kumtoa lawamani kwa hoja kuwa “huwezi kuwa kiongozi kamili wa kitaifa wa CCM pasipo angalau ‘kuwapiga madongo’ wapinzani.” Ni kama anatekeleza tu wajibu wake kwani hata ‘tone’ yake huwa sio ya mwanasiasa mwenye chuki au uadui dhidi ya wapinzani.
Lakini kama kuna zama ambazo nchi yetu imeshuhudia siasa hatari kabisa basi ni hiyo ya Mwenyekiti ‘mpole’ wa CCM Taifa, yaani Kikwete. Sasa kama Kikwete ana ‘sura mbili’ (ya upole hadharani lakini mwenye hasira anapokuwa na wasaidizi wake ndani ya CCM na serikali), au amezungukwa na watu wenye chuki kubwa dhidi ya wapinzani, ni vigumu kuhitimisha hilo kwa dhati.
Naomba nisiume maneno. Kuna wanasiasa watatu ambao wote ni wasaidizi wa karibu wa Kikwete huko CCM, wamekuwa sio tu wakijitahidi kufanya kila wawezalo kuteketeza vyama vya upinzani-hususan Chadema bali pia wanaweza kabisa kuliingiza taifa letu matatizoni kutokana na siasa zao za chuki. Hao ni Steven Wassira, Nape Nnauye na Mwigulu Nchemba.
Wassira, maarufu kama Tyson, amekuwa ‘asset’ muhimu kwa CCM dhidi ya wapinzani, pengine kwa vile alikuwa huko kabla ya kurejea CCM. Nafasi niliyonayo katika makala hii haitoshi kuorodhesha matendo kadhaa ya mwanasiasa huyo dhidi ya vyama vya upinzani, lakini kubwa, na pengine la msingi zaidi, ni kauli yake hatari kuwa Chadema itakufa kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao.
Ikumbukwe kuwa Wassira si mnajimu wala hakuna kumbukumbu zozote zinazoonyesha kuwa ana uwezo wa kupiga ramli kubashiri uhai au vifo vya vyama vya siasa. Kauli hiyo ya Wassira ina uzito mkubwa zaidi kutokana na ukweli kuwa nafasi yake serikalini inaweza kusukuma vyombo vya dola kufanikisha utabiri wake huo (ambao kimsingi ni fyongo lakini unaoweza kutimia kwa ‘nguvu za giza.’)
Nape ni mwanasiasa ambaye binafsi ninamwona kama disappointment of the century.Kabla ya kuingia kwenye siasa za ngazi za juu, mwanasiasa huyu kijana alijipambanua kama mtu mwenye maono, ujasiri na msimamo usioyumba. Pasi kuchelea matokeo, alimudu kukosoa vikwazo kwa maendeleo na ustawi wa taifa letu na kupingana waziwazi na wanasiasa wenye mitizamo fyongo ndani ya chama chake.
Kijana huyo 'alilipa gharama’ kubwa ya msimamo wake usioyumba (wakati huo) na akakumbwa na zahma kubwa ya kisiasa. Pengine kwa kutambua kuwa kosa pekee la Nape ni msimamo wake makini, Rais Kikwete ‘alimzawadia’ ukuu wa wilaya (ambapo wachambuzi wa siasa walitafsiri hatua hiyo kama sapoti ya Rais kwa mwanasiasa huyo).
Alipoteuliwa kushika nyadhifa ya juu ndani ya CCM, Nape alikuja na nuru mpya ndani ya chama kilichokuwa kikionekana machoni mwa wengi kuwa kimezama kwenye himaya ya mafisadi, akatangaza dhamira ya kihistoria ya ‘CCM kujivua magamba,’ yaani chama hicho tawala ‘kuwakalia kooni’ viongozi na wanasiasa wake wanaohusishwa na tuhuma za ufisadi. Kwa nyakati kadhaa, Mwenyekiti wake wa CCM Taifa, Rais Kikwete alionyesha kumuunga mkono Nape.
Nikiri kuwa nami ni miongoni mwa ‘tuliongizwa mkenge’ (kughilibiwa) na suala hilo la CCM kujivua magamba. Pengine kilichoniaminisha zaidi kuhusu suala hilo ni kauli za Nape na ukweli kwamba historia yake huko nyuma ilipaswa kumwaminisha yeyote anayemfahamu vema kuwa hakuwa ‘anapiga politiki’ bali alikusudia kwa dhati kukisafisha chama chake.
Pamoja na ‘hasira’ za Nape kutonifuatilia (unfollow) kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter baada ya kumwandama kwa maswali ya/hoja za kichokozi (lengo likiwa kumhamasisha arejee kwenye mstari sahihi), bado ninaamini kwa asilimia 100 kuwa mwanasiasa huyo alikuwa na dhamira ya dhati kuivua CCM magamba, na kilichomkwaza si unafiki bali ukweli kuwa ‘tofauti na nyoka ambaye uhai wake hutegemea kujivua gamba, ukimvua gamba kobe utamuuwa.’
CCM si kama kobe bali ni kama nyoka ambaye kujivua gamba ni sehemu muhimu ya uhai wake. Jitihada zozote za kukitenganisha chama hicho na mafisadi kitakuwa na matokeo ya aina moja tu: kukidhoofisha na hatimaye kukiuwa.
18 Apr 2013

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Frans Timmermans akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika makazi rasmi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo jijijini The Hague na kufanya naye mazungumzo rasmi.
Ina maana Waziri Mkuu wa Uholanzi hakuona umuhimu wa kumkaribisha Rais Kikwete yeye mwenyewe hadi akamtuma Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo? Zingatia maneno yenye herufi nyekundu: tukio hilo limetokea kwenye makazi ya Waziri Mkuu huyo.Hii ni fedheha!
Ikumbukwe hali kama hiyo ilijitokeza katika ziara ya Rais Kikwete nchini Ufaransa ambapo badala ya kupokewa na Rais Hollande, alipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Maendeleo wa nchi hiyo Pascal Canfin.
Bottom line is, hata kama angepokelewa na viongozi wakuu wa nchi hizo, bado ukweli unabaki kuwa Kikwete atabaki kwenye kumbukumbu za Tanzania (na pengine duniani kwa ujumla) kama Rais anayependa mno safari za nje licha ya safari hizo kuwa mzigo mkubwa kwa walalahoi wa Tanzania.
Kwa mujibu wa takwimu za mtandao wa Jamii Forums, hadi kufikia mwezi huu wa April 2013, Kikwete amesafiri mara 365 (sawa na idadi ya siku katika mwaka mmoja) tangu aingie madarakani mwaka 2005.
Mwaka juzi, gazeti lililokuwa mwiba kwa serikali ya Kikwete hadi likafungiwa la Mwanahalisi liliripoti kuwa safari hizo za Kikwete zinachangia mno kukausha fedha huko Hazina.
Kwanini ninasema Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi a.k.a Mzee Ruksa AMELIKOROGA? Hebu soma msimamo wake wa awali kuhusu suala la kuchinja
Mwinyi: Kila mtu ruksa kuchinja • ASEMA IMANI NI NAFSI, HATA KULA CHURA SAWA
na Asha BaniRAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amerejea kauli yake kuhusu mgogoro wa udini akisema kila mtu ana haki ya kuchinja kutokana na imani yake ilimradi tu asivunje sheria za nchi.
Mwinyi alisema anashangaa kuona watu wakigombania kitu kidogo kama kuchinja ilihali Tanzania ina utamaduni wa amani siku zote na kwamba kila mtu ana imani yake ya dini anayoiamini.
Kiongozi huyo mstaafu alitoa msimamo huo jana jijini Dar es Salaam katika kongamano juu ya utamaduni wa Kiislamu Afrika Mashariki ambapo Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji.“Imani ni nafsi ya mtu na haitakiwi kumlazimisha kula nyama iliyochinjwa na mwenzie. Na kama unaona aliyochinja mwenzio ni kibudu basi usile chinja yako, kula hata ukitaka kula chura, mjusi, konokono, kula utakacho ruksa ilimradi tu usiingie katika jinai,” alisema.
Mwinyi alikumbusha kuwa hata wakati wa utawala wake majaribu kama hayo yaliwahi kumtokea, lakini alijitahidi kuweka sawa kwa kumwambia kila mtu ale kile anachofikiri ni chakula bila kumlazimisha mwenzake.
Alisema Watanzania wamezaliwa ardhi moja na kwamba kinachotakiwa ni kuwa na misingi ya kuvumiliana, na kwamba sifa ya Uislamu ni pamoja na kuwa na uvumilivu.Aliongeza kuwa Uislamu si kufanya vurugu kama inayotafsiriwa na makundi ya wanaotaka kuvunja amani ya nchi kwa kutumia jina la dini ya Kiislamu.
Sasa linganisha msimamo huo wa awali na hicho alichoongea Mzee Ruksa kwenye video hapo juu.
Yawezekana Rais huyo mstaafu ameamua 'kulamba matapishi yake' (kusema 'amefafanua' ni kupotosha ukweli kwani alichoongea kwenye video ni tofauti kabisa na alichoongea awali) baada ya kupata shinikizo kutoka kwa Waislam wenzie. Au albda nafsi tu imemsuta.
Nitajadili kwa kifupi suala hili kama Mtanzania na pia kama Mkristo. Kama tunakubaliana kuwa Tanzania haina dini, lakini Watanzania wana dini,basi kila dini inapaswa kuheshimu uhuru na haki za wenzao. Kama sheria za kidini zinawataka Waislam kuchinja, na zile za Wakristo haziwalazimishi kuchinja, basi kila mmoja afuate kile kinachoelekezwa na dini yake.
Mzee Ruksa anaposema Biblia ipo kimya kuhusu suala la kuchinja haimaanishi kuwa ukimya huo unatoa ruhusa kwa Wakristo kulazimishwa kufuata matakwa ya Waislam au wapagani.Msimamo wake wa awali ulikuwa sahihi kabisa: kila mtu afuate imani yake, na hata mtu akitaka kula chura aachiwe uhuru wa kufanya hivyo.
Kimsingi, Mwinyi amechochea moto kwenye mjadala huo japo katika video hiyo anaonekana kama angependa Watanzania waishi kwa amani na umoja. Lakini haiwezekani kuishi kwa amani na umoja iwapo dini moja inafanywa kuwa yenye haki zaidi ya dini nyingine. Haki ya Waislam kuchinja shurti iendane na utambuzi wa haki ya Wakristo kutolazimika kuchinja. Hatuwezi kuzungumzia haki za Waislam lakini wakati huohuo tukapuuza haki za Wakristo.
Hivi ikitokea Wakristo wanataka kuchinja nguruwe itabidi watafute Musilam wa kuwacvhinia ilhali nguruwe ni haramu kwa Waislamu?
Sorry Mzee Ruksa, hii flip-flop imeturejesha kwenye tatizo lile lile la udini: kuangalia upande mmoja wa imani na kupuuza upande mwingine.
17 Apr 2013
Subscribe to:
Comments (Atom)
















.jpg)



















