Tunapenda kulitambulisha watanzania wote waishio popote Duniani kwamba kuanzia sasa wanaweza sikiliza Radio kupitia mtandao yani Internet Buree. Tumeona tufanye hivi kwa kutambua kwamba pamoja na kuwa watanzania wengi wapo hapa nchini na wengi wao kwa sasa wanatumia mtandao na wanapenda sikiliza Radio kupitia mtandao, lakini pia tumezingatia na watanzania wenzetu wanaoishi nje ya nchi wapate Burudani, Habari na mambo mengine mengi kutoka Tanzania. Kupitia Tone  Internet Radio watakuwa hawajisikii upweke na kuona kama wapo Tanzania. Pia Tone Radio inawapa wasanii wa Muziki wa aina yoyote Tanzania kuleta nyimbo zao hapa studio na sisi kutangaza kazi zao bure kwa kututumia nyimbo zao kupitia[email protected] . Karibuni sana nyote na pia ukisikiliza Radio mwalike  na mwenzako. Pia tunapatikana katikaFacebook profile yetu Tanzania Online-Radio 


Tunatanguliza Shukurani Zetu za Dhati na karibuni sana... Tone Internet Radio Pamoja Tutafika
Sillah Mbuya