24 May 2013


MKALI WA VODACOM:
Je, unajiamini kuwa na kitu kinachokufanya uwe mkali mtarajiwa? Vodacom inatafuta mtangazaji mpya wa kipindi cha TV kitakachoanza hivi karibuni. Soma namna ya kushiriki na unaweza kuwa mmoja ya watangazaji wa kipindi hiki.
Kazi ni kwako










HEBU JIULIZE, LINI ULISHUHUDIA HALI KAMA HII IKITOKEA TANZANIA?

BADALA YA KUSAKA CHANZO, OUR DEAR LEADER DOKTA KIKWETE ANADAI "ATAKATA MAPEMBE" YA ANAYESABABISHA VURUGU. WELL, YEYE MWENYEWE NI PEMBE PIA KWANI UTAWALA WAKE UMEZIDI KUISUKUMA TANZANIA YETU KUELEKEA MAHALA KUSIKOFAA: UFISADI UMEKUWA KAMA SEHEMU YA MAISHA YA MTANZANIA, UDINI SIO TU UMEONGEZEKA BALI PIA UMEANZA KUWAFARAKANISHA WATANZANIA HUKU BAADHI YA WENZETU WAKIPOTEZA MAISHA YAO, UHUNI USIOELEZEKA MIONGONI MWA WATU WALIOCHAGULIWA NA KUPEWA DHAMANA YA KUWAKILISHA WATANZANIA (WABUNGE), MGAO WA UMEME USIOISHA LICHA YA AHADI KEDEKEDE KUTOKA KWA KIKWETE...MENGINE ONGEZEA MWENYEWE MSOMAJI.

NASEMA HIVI, IFIKE MAHALA KIKWETE AAMBIWE UKWELI KUWA KAMA KWELI ANA LENGO LA KUKATA PEMBE BASI AJIWEKE KANDO YEYE MWENYEWE KWANI YEYE NDIYE PEMBE KUBWA ZAIDI.

21 May 2013

Click image for larger version. 

Name: Prof Jay Ajiunga Na Chadema.jpg 
Views: 0 
Size: 47.5 KB 
ID: 94612
 Profesa Jay akipokea kadi ya unachama wa Chadema kutoka kwa Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) Mh. Joseph Mbilinyi (a.k.a Sugu)
Click image for larger version. 

Name: Prof Jay Na Sugu Na Mnyika.jpg 
Views: 0 
Size: 40.8 KB 
ID: 94613

Profesa Jay akiwa na Mh 'Sugu'  na Mbunge wa Ubungo (Chadema) Mh John Mnyika.

Ni Mtanzania gani kijana (na hata wazee wa kati) asiyemjua Profesa Jay, msanii mahiri wa Bongoflava ambaye jina lake halisi ni Joseph Haule (au Jay wa Mitulinga). Msanii huyo, pengine katika hali ambayo haikutarajiwa kabisa, leo amejiunga na chama cha upinzani cha Chadema.

Uamuzi wa Profesa Jay kujiunga na Chadema unaweza kuwa na manufaa makubwa sana kwa chama hicho hasa kwa vile mabadiliko ya kisiasa huko nyumbani yanategemea zaidi hamasa ya vijana.


Nitaandika zaidi baadaye kuhusu tukio hili muhimu kwa Chadema, muziki wa bongoflava na vijana kwa ujumla, lakini kwa sasa burudika na kibao hiki cha "Nikusaidiaje" cha Profesa Jay akimshirikisha Ferouz


DSC 0043 f478a
DSC 0044 efb36
DSC 0045 6ff67
DSC 0046 1edd5
DSC 0047 b993f

DSC 0048 77783
DSC 0049 06bdd
DSC 0050 95093
DSC 0051 e147b
DSC 0052 6559f
DSC 0053 ac5ac
RATE THIS ITEM

18 May 2013


DSC 0261 1a54f
DSC 0262 5766d
DSC 0263 ef14a
DSC 0264 e160a

DSC 0265 784f3
DSC 0266 58f60
DSC 0267 c101d
DSC 0268 5e9e8
DSC 0269 f7c59
DSC 0270 80e8c
Chanzo: MJENGWA

17 May 2013

Je wewe ni mwanasheria? Je wewe ni mtetezi wa haki za binadamu? Je katika nafasi uliyonayo-hata kama si mwanasheria au mtetezi wa haki za binadamu- unaweza kumsaidia mwananchi huyu asiye na hatia?

Tumekuwa wepesi wa kulaumu zaidi kuliko kutenda. Sote twatambua uonevu unaofanywa na baadhi ya watumishi wa vyombo vya dola hususan Jeshi la Polisi. Lakini kulaumu au kulaani pekee hakuwezi kumaliza tatizo husika, hususan katika nyakati ambazo kuna wenzetu wanateswa pasi hatia. Basi ombi langu kwako ni kutumia nafasi yako-iwe ni mtu maarufu, mfanyabiashara, mwanasiasa, nk-kumsaidia mwananchi huyu.Mie nimeanza kwa kuweka hadharani kilio chake.



16 May 2013


AWALI nilidhamiria makala hii iwe ya hitimisho la makala mbili zilizotangulia kuhusu mageuzi ya kisiasa na kushamiri kwa siasa za chuki huko nyumbani. Nimeliweka kando kidogo hitimisho hilo ili nizungumzie tukio la shambulio la bomu kanisani huko Arusha.
Pasi kuuma maneno, naomba niweke bayana kuwa kwa mtizamo wangu, tukio hilo la kusikitisha na kuogopesha huko Arusha ni matokeo ya jitihada chafu za baadhi ya wanasiasa kutumia dini kwa manufaa yao binafsi, sambamba na  udhaifu wa baadhi ya vyombo vya usalama wetu.
Katika makala hii nitazungumzia hilo la pili, na hilo la ‘siasa chafu’ nitalizungumzia katika makala zijazo. Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na kelele kuhusu utendaji kazi wa wanausalama wetu. Makala hii haitoshi kueleza mlolongo wa masuala na matukio yanayozua hitimisho kuwa wanausalama wetu ni dhaifu.
Ni hivi, ndani ya wanausalama wetu kuna kitengo maalumu cha kupambana na ugaidi. Je, kwa matukio ya hivi karibuni ya kigaidi, lile la mauaji ya padre Evaristus Mushi huko Zanzibar, na hili la shambulio la bomu kanisani, wanausalama wetu wanaweza kujitetea vipi kuwa si tu wanawatia hasara walipa kodi huko nyumbani (wanaobebeshwa gharama za ‘operesheni’ zao). Mara kadhaa nimeandika kuwa tatizo la wanausalama wetu ni kuwa na vipaumbele fyongo (misguided priorities).
Wenzetu Marekani yalipotokea mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, 2001 waliwaweka ‘kitimoto’ mashushushu wa nchi hiyo na kuwahoji kwanini walishindwa kuzuwia janga hilo kubwa kabisa katika historia ya nchi hiyo. Kadhalika, Waingereza nao waliwabana kweli mashushushu wao wa MI5, MI6 na GCHQ baada ya mashambulizi ya kigaidi jijini London Julai 7, 2005.
Lengo la kuwabana wanausalama hao halikuwa ‘kushikana uchawi’ bali kubaini mapungufu yaliyopelekea magaidi kufanikisha mashambulizi hayo na hivyo kutengeneza mazingira ya kuyazuwia huko mbele.
Ninawalaumu wanausalama wetu moja kwa moja kwa vile moja ya majukumu makuu ya Idara yao kwa mujibu wa  Sheria ya Usalama wa Taifa (kama ilivyorekebishwa mwaka 1996) Sehemu ya Pili kifungu namba 5(d) ni “kumfahamisha Rais, au na mtu au taasisi yeyote yenye mamlaka kama Waziri husika atakavyoelekeza, kuhusu maeneo yoyote mapya yenye uwezekano wa kusababisha ujasusi (espionage), hujuma (sabotage), UGAIDI (terrorism) au uzandiki (subversion) ambapo Mkurugenzi Mkuu anaona ni muhimu kufanya ufuatiliaji (surveillance).”
Baada ya tukio la Padre Mushi kuuawa Zanzibar ungetarajia wanausalama wetu wangeamka usingizini na kutambua kuwa kuna tishio halisi la ugaidi huko nyumbani.
Kibaya zaidi, mwezi uliopita Jeshi la Polisi lilitangaza hadharani kupitia Kamishna Mwandamizi Hussein Nassoro Laiseri, kuwa zipo dalili za kuibuka makundi ya kigaidi huko nyumbani yakiratibiwa na Al-Qaeda na Al-Shabaab.
Je, Idara yetu ya Usalama wa Taifa inaweza kutueleza kwanini haikutumia tahadhari hiyo kujipanga vizuri kuhakikisha kuwa inazuwia uwezekano wowote wa ugaidi huko nyumbani?
Pengine udhaifu wa wanausalama wetu unajidhihirisha zaidi kwenye ukweli kwamba baada ya mauaji ya Padre Mushi serikali ililazimika kuomba msaada wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) kusaidia uchunguzi wa tukio hilo. Na sasa taarifa zinaeleza kuwa FBI wameombwa tena kusaidia uchunguzi wa tukio hilo la Arusha.
Hivi kimetokea nini hasa kwa wanausalama wetu ambao huko nyuma walimudu kuwadhibiti majasusi wa Makaburu waliokuwa wanasaidiwa na FBI na CIA haohao ambao leo tunawaomba msaada? Na tutaendelea kutegemea misaada ya kiintelijensia hadi lini hasa ikizingatiwa kuwa hao Wamarekani nao wana vipaumbele vyao muhimu nchi mwao na sehemu nyinginezo duniani?
Binafsi, nimekuwa nikitafsiri kushamiri kwa ufisadi huko nyumbani kuwa uthibitisho wa wazi wa kushindwa kwa wanausalama wetu katika eneo la kupambana na hujuma za kiuchumi (economic sabotage). Nimekuwa pia nikifahamu kuwa uwezo wa taasisi ya wanausalama wetu kupambana na ugaidi unakwazwa na 'kirusi' cha ‘undugunaizesheni’ na kujuana kwenye teuzi za baadhi ya maafisa wanaopelekwa kwenye balozi zetu  badala ya uwezo wao kikazi.
Maafisa hao ni nyenzo muhimu katika kupambana na ugaidi kwani ni jukumu lao kuifahamisha Idara juu ya matishio ya kiusalama kutoka nchi vilipo vituo vyao vya kazi. Wakati mataifa mengi yanajaza mashushushu kwenye balozi zao nje, sisi tunafanya kinyume.
Niliwahi kusimuliwa kuhusu ‘mwandamizi’ fulani ambaye sasa ana wadhifa mkubwa huko nyumbani ambapo taarifa zake za kiusalama zilikuwa vipande vya habari za magazeti ya nchi iliyokuwa kituo chake cha kazi. Baadhi ya taarifa hizo zilikuwa ni mithili ya vichekesho.
Ninatambua makala hii itawaudhi wahusika lakini kwa vile usalama wa taifa letu si hakimiliki ya mtu au kundi flani, bali kila Mtanzania, basi ni muhimu tuambiane ukweli pasi hofu.
Lakini pia inatulazimu baadhi yetu tuseme haya ninayoandika kwa sababu wanausalama wetu wanaogopwa sana kiasi kwamba hakuna wa kuwakosoa hata wakinapoboronga na hilo halina tija sasa na siku zijazo. Tuyajadili mambo haya, maana kosa ni kujadili siri za nchi si kujadili udhaifu wa taasisi inashughulikia siri hizo.
Nini kifanyike? Tuelezane kwa nini wanausalama wetu wameshindwa kuzuia ugaidi uliotokea Zanzibar na huu wa majuzi huko Arusha. Sambamba na hilo, ni muhimu kwa mamlaka ndani ya Idara kujihukumu zenyewe. Maana hivi 
tunavyokwenda tutaliingiza taifa kwenye madhara makubwa.

Haitoshi tu kwa Rais na viongozi wengine wa serikali kukasirishwa na matukio haya ya ugaidi. Tumeshawasikia wakionyesha hisia kama hizo wanapozungumzia majanga kama ya umasikini wetu, rushwa na ajali zinazoweza kuepukika. Lakini sote twatambua kuwa umasikini wetu unazidi kutuumiza, rushwa inazidi kushamiri, na ajali (kama ile ya jengo lililoanguka Dar) zinazidi kutuangamiza.
Mkoloni hakuondoka kwa kuchukiwa pekee, Nduli Idi Amin hakukimbia kwa vile tu aliwachukiza viongozi wetu: dhamira ya dhati na vitendo ndivyo viliwezesha kuwatimua. Pasipo vitendo, udhaifu wa wanausalama wetu utapelekea majanga makubwa zaidi huko mbele.
Watanzania wana NIA ya kuona taifa likiwa na usalama. Pia wana kila SABABU ya kuuhitaji usalama wa taifa lao. Tatizo ni UWEZO dhaifu wa tuliowakabidhi jukumu la usalama wetu.


DSC 0198 b6684
DSC 0199 c9faa
DSC 0200 7985f
DSC 0201 6a9fe
DSC 0202 1be70

DSC 0203 33ab2
DSC 0204 a095b
DSC 0205 15543
DSC 0206 6a929
DSC 0207 fba28
DSC 0208 12c22
DSC 0209 fa0ba
DSC 0211 b7e8a
DSC 0212 df6f9
DSC 0213 2d894

Picha kwa hisani ya MJENGWA


Happy birthday Nathan. Knowing you brought a whole new meaning to the age-old adage "A friend in need is a friend indeed."

Friend is just a word but you give it a meaning.

May God Bless you

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.