Showing posts with label RICHMOND SCAM. Show all posts
Showing posts with label RICHMOND SCAM. Show all posts

10 Dec 2011




Kikwete, Lowassa hapatoshi

Saed Kubenea's picture
Na Saed Kubenea - Imechapwa 30 November 2011
Printer-friendly versionSend to friend
HATIMAYE Edward Lowassa ametoka hadharani na kuonyesha kuwa anataka kupimana ubavu na Rais Jakaya Kikwete.
Ameeleza hadharani kuwa Rais Kikwete anahusika kwenye mkataba tata wa Richmond/Dowans; lakini pia, kuwa hafuati taratibu katika kuongoza chama chake.
Lowassa ambaye alikuwa nguzo muhimu katika mbio za urais wa Kikwete mwaka 2005, ameonekana kumgeuka waziwazi swahiba wake huyo kwa kuanika kile wachunguzi wanaita “udhaifu katika uongozi.”
Ndani ya kipindi cha siku nne, Lowassa ametoa kauli tatu nzito zinazoonyesha dhahiri ameamua kufanya mapambano na Kikwete.
Akiwa ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lowassa alinukuliwa akieleza hatua kwa hatua namna kampuni ya kitapeli ya Richmond Development Company (RDC), ilivyopewa zabuni ya kufua umeme wa dharura nchini.
Lowassa alijiuzulu wadhifa wa waziri mkuu mwaka 2008 kufuatia kashfa ya mkataba wa Richmond, kampuni iliyopewa kwa upendeleo zabuni ya kuzalisha umeme wakati haina fedha, haina uzoefu wala fedha za kufanyia kazi hiyo.
Alikiambia kikao cha NEC mjini Dodoma, “Hakuna jambo nililolifanya ambalo wewe Rais Kikwete hukulifahamu au hukunituma” kuhusu Richmond/Dowans.
Alisema, “…Mwenyekiti, natukanwa kwa ufisadi wa Richmond wakati wewe unafahamu yalichosababisha kashfa ya Richmond ni makosa ya watendaji walio chini yangu? Sasa kosa langu ni lipi? Ni kule kukubali kuwajibika kwa ajili ya serikali yangu na chama chetu? Kwa nini nihukumiwe kwa kosa hilo?”
Huku akimtolea macho Kikwete alisema, “Unakumbuka vema jinsi nilivyotaka kuvunja mkataba ule. Nilikupigia simu ukiwa nje ya nchi, lakini ukasema umepata ushauri wa kamati ya makatibu wakuu, ushauri ambao ulisababisha mkataba usivunjwe?”
Lowassa alisema Kikwete anafahamu kila kitu kwa kuwa ni yeye aliyeridhia Rostam Aziz kutafuta mbia baada ya Richmond kushindwa kuleta umeme.
“Uliponitaka ushauri wa mtu wa kutusaidia ili kuondokana na aibu ya Richmond kushindwa kutimiza mkataba wake, nilipokutajia jina la Rostam, haraka ulikubali na kusema, naona hilo ni sawa,” alieleza Lowassa kwa njia ya kumsuta Kikwete.
Hatua ya Lowassa kumuingiza Kikwete kwenye tope la Richmond/Dowans imezima moja kwa moja kauli yake iliyodai, “Siwajui wala siwafahamu wamiliki wa makampuni ya Dowans Tanzania Ltd na Dowans Holdings SA.”
Akihutubia kwenye maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM, tarehe 5 Februari 2011, mjini Dodoma, Kikwete alikana kufahamu wamiliki wa kampuni hiyo na kwamba hajawahi kuwaona wamiliki wake.
Alisema, “Nataka kuuhakikishia umma kwamba, sihusiki na kampuni hii. Siifahamu na wala sijawahi kuwaona wamiliki wake…Ama kweli akutukanae hakuchagulii tusi.”
Kauli ya Kikwete ya kutoitambua Dowans wala wamiliki wake, ilikuwa ni mwendelezo wa kauli kama hizo zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya wasaidizi wake, zikilenga kumuondoa kwenye kashfa hiyo iliyomlazimu kuvunja baraza lake la mawaziri.
Akizungumzia kwa undani jinsi Richmond ilivyoingia na jinsi yeye na Kikwete walivyokuwa kitu kimoja kuhakikisha mkataba unasainiwa na kutekelezwa, Lowassa alisema, “Hakuna jambo nililolifanya ambalo Rais Kikwete hukulifahamu.”
Akizungumzia kwa undani suala hilo kwa mara ya kwanza tangu ajiuzulu wadhifa wa waziri mkuu, Februari 2008, Lowassa alisema, “Mwenyekiti kwanza napongeza uamuzi huu wa kurejesha jambo hili katika taratibu za kawaida, lakini napenda kufahamu kwa miezi saba nimetukanwa nikiitwa fisadi, watu wamezunguka nchi nzima kwa fedha za chama, hivi hatukujua kama kuna kamati hizo za maadili?”
Lowassa alikuwa akichangia pendekezo la Kamati Kuu (CC) ya CCM lililotaka kurejeshwa kwa suala la “kujivua gamba” kwenye vikao vya chini vya chama hicho baada ya watuhumiwa, isipokuwa Rostam Aziz, kukataa kuachia uongozi katika chama.
Kikwete alikiambia kikao cha NEC kuwa, uamuzi wa kutaka jambo hilo lirejeshwe kwenye vikao vya chini, umetokana na “taratibu kukosewa.”
Hata hivyo, kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya chama hicho aliliambia gazeti hili juzi Jumatatu, uamuzi wa Kikwete kulirejesha suala la kujivua gamba kwenye vikao vya chini ulitokana na hofu ya NEC kujaa wajumbe wengi kutoka kwa kundi la Lowassa.
“Unajua mle NEC, Kikwete hana chake. Mle ndani kuna kundi kubwa la Lowassa, ndiyo maana jamaa ameogopa suala hilo la kuvuana magamba lijadiliwe,” ameeleza kiongozi huyo ambaye ni waziri katika serikali ya Rais Kikwete.
Kanuni za CCM zinaeleza kabla ya tuhuma kufikishwa NEC, sharti wale wanaotuhumiwa wapewe haki na fursa ya kujitetea mbele ya vikao vya kamati ya usalama na maadili.
Akifunga mjadala huo kwa angalizo mwanana, Kikwete aliagiza suala hilo lipelekwe kamati ya maadili ambako alitaka kuwasilishwa ushahidi wa vielelezo na siyo hujuma dhidi ya watuhumiwa.
Wakati Lowassa akishusha tuhuma kwa Kikwete, kiongozi huyo wa nchi alionekana kama amepigwa ngazi. Hakukana hata tuhuma moja miongoni mwa yaliyoelezwa na swahiba wake huyo wa zamani.
Kikwete na Lowassa, wamejitambulisha mara kadhaa kuwa ni marafiki, huku mmoja akisisitiza, “Hatukutana barabarani.”
Haijafahamika mahusiano yao yamefikia wapi kwa sasa baada ya Lowassa kumhusisha mwenzake katika kashfa ya Richmond katika kile wachunguzi wanasema amechukua tabia ya “tufe sote au tukose wote.”
Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanasema kauli ya Lowassa ambayo ilitolewa mbele ya viongozi wake wakuu, akiwamo rais mstaafu, Benjamin Mkapa, ililenga kuonyesha udhaifu wa Kikwete ndani ya CCM kwa kuasisi falsafa ya kujivua gamba na kuikimbiza moja kwa moja kwenye CC na NEC, kinyume cha taratibu na kanuni za chama chake.
Kama hiyo haitoshi, juzi Jumapili akiwa mkoani Singida alikokwenda kusimamia harambaee ya kuchangia fedha za ujenzi wa kanisa, Lowassa alinukuliwa akisema, “Kwa vyovyote vile, nitaibuka mshindi dhidi ya vita vya kuvuana magamba.”
Akitiwa moyo na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dayosisi ya Kati, Ushirika wa Amani, mjini Singida, Eliufoo Sima aliyesema, “suluhu ya mapambano ni kukabiliana nayo,” mwanasiasa huyo alisema, amekuwa akihusishwa na tuhuma ambazo hazina ukweli.
Askofu Sima alisema mapambano katika maisha hayatakwisha na “suluhisho siyo kuyaogopa, isipokuwa kuyatafutia majawabu kwa upole, hekima na utulivu.”
Vita vya magamba viliasisiwa na Kikwete 5 Februari 2011, kabla ya kudakwa na baadhi ya watendaji wa Sekretarieti ya CC ambao kwa miezi saba sasa, wamekuwa wakituhumu Lowassa na wenzake wawili - Rostam Aziz na Andrew Chenge – kuwa mafisadi wanaokidhalilisha chama mbele ya jamii.
Wakati hayo yakiendelea, taarifa kutoka ndani ya CC zinasema kushindwa kwa Rais Kikwete kutekeleza mkakati wake wa kumfukuza Lowassa ndani ya chama chake, kulitokana na upinzani mkali uliotokea kwenye mkutano wa CC.
“Ni kweli kabisa, ndani ya CC, Lowassa alipata uungwaji mkono mkubwa, kiasi ambacho mwenyekiti alilazimika kulipeleka suala hilo NEC. Alipofika NEC na kuona moto umekuwa mkubwa, ndipo alipoamua kuliondoa na kutaka lifanyiwe kazi kwenye vyombo vya chini,” kimeeleza chanzo kimoja cha gazeti hili.
Amesema wajumnbe wa Zanzibar, wakiongozwa na makamu mwenyekiti wa chama hicho visiwani, Amani Abeid Karume, muda wote wa mkutano walisimama imara kuhakikisha Lowassa hafukuzwi kwenye chama.
“Kuna wakati watu kutoka Bara walikuwa wanakaribia kushinda. Lakini baadaye Zanzibar wakapata nguvu pale Karume aliposimama na kusema, shutuma zote hizo hazijafuata taratibu,” ameeleza.



CHANZO: Mwanahalisi

7 Nov 2009


SIKU moja baada ya mjadala wa Richmond kuahirishwa bungeni, baadhi ya wabunge wamesema serikali imechangia kuchelewesha suala hilo ili kukwepa fedheha na kuonya kwamba ujanja huo hautaisaidia.

Wakati wabunge wakitoa kauli hiyo, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), sasa wanajiandaa kuishtaki serikali kwa wananchi ili waihukumu kwa kuikumbatia Richmond.

Wabunge waliozungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi Jumapili jana, walisema licha ya kuendelea kuupiga kalenda mjadala, bado wanaisubiri ripoti ya Richmond kwa hamu na kwamba hawatalala mpaka kieleweke.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini, William Shellukindo alisema hajui kilichotokea hata ripoti hiyo ikaahirishwa tena.

"Siku mbili za mwisho sikuwa bungeni, niko nyumbani nimefiwa na mtoto wangu¦, sijui kilichotokea mpaka waahirishe ripoti hiyo katika Bunge hili, alisema Shellukindo...ENDELEA KUSOMA HAPA

CHANZO: Mwananchi

SABABU NYINGINE YA KUINYIMA CCM KURA HAPO MWAKANI.ZIPO NYINGI LAKINI HII INASUKUMA HATA WALE WALIOKUNYWA MAJI YA BENDERA YA CCM.BUNGE LENYEWE HALINA MENO,MIKWARA MIIIINGI KABLA YA VIKAO (PENGINE KATIKA KUHALALISHA MARUPURUPU YAO MANONO) NA WANAHABARI WETU WANADAKIA KILELE HIZO TO AN EXTENT YA KUKUAMINISHA KUWA SAFARI HII WEZI WA RICHMOND HAW

31 Oct 2009


Sometimes I am left wondering if democracy means anything to a common man on the street.Look at Tanzania.Our elected representatives in the National Assembly have,arguably,made democracy look like a joke.How on earth would they defend accepting (or rather demanding) extra allowances despite their hefty packages in terms of their sitting allowances and salaries?

It's more than ironic when a body entrusted with the task of making laws becomes a champion in breaking the law.Our MPs should understand that it's simply unacceptable for them to demand or receive hospitality allowances not only because it could impact their opinions but also they are already receiving more benefits an ordinary Tanzanian could only imagine about.

I am even more disgusted by the stance taken by the Speaker of the House Samuel Sitta who claims that 'hospitality allowance is offered in accordance with African tradition.Bribe is not an African tradition,and that is exactly what our MPs are doing.It is widely understood that hospitality accorded to MPs when they visit an organisation for a fact-finding mission could very well be an attempt to soften their stance towards it.In other words,our MPs could easily be bribed by lunch allowances simply because they can't have enough.

Of course, I have been one of the strongest critic of PCCB,especially after its Director General Edward Hosea was implicated by a Parliamentary Committee which was investigating the Richmond scam.However,despite "getting it right at a wrong time" PCCB has every right to investigate the said claims against our MPs.

And it is ridiculous for Speaker Sitta to give statements which imply that MPs are above the law,and therefore have a divine right to break the law.Although it could be true that the decision by PCCB ot investigate the hospitality allowances was prompted by the much anticipated House debate on the Richmond scam,it still does not make our MPs,Sitta included,immune to scrutiny on favours accorded to our representatives.

Back to my point about how ironic democracy could look when analysing African politics,it makes one wonder if the 300 plus MPs representing Tanzanians in Dodoma are actually useful.Arguably,the only thing that most of our MPs have been so effective is in demanding improvement in their benefits.They have so far failed to pressurise the Government to act responsibly in dealing with such important issues as the Richmond scandal,stupid mining contracts and the likes.How could they while they rely on the Government for 'improving' their welfare?

It looks as if the Government's trick to bring the hospitality allowance issue ahead of the debate on the Richmond scam has worked perfectly.Our MPs are so busy to justify that they deserve 'bribes' in a form of hospitality allowances that they have completely forgotten about pressing the Government to come clean on the Richmond saga.

As I have frequently written in my previous posts,I strongly believe that despite of what majority of Tanzanians would like to see or hear,the Government will never bring the Richmond farce to an end because most of the key players are still useful for its (the government's) survival.Unless you are dreaming,Lowassa and Co are too important to wanamtandao to have him on the dock to tell us how we ended up signing such a silly contract with Richmond.

21 Oct 2009


DANADANA KUHUSU SUALA LA RICHMOND IMEZIDI KUENDELEA.BINAFSI SIDHANI KAMA SUALA HILI LITAPATIWA UFUMBUZI UNAOSUBIRIWA NA WATANZANIA WENGI.KUPATA UFUMBUZI,KWA MAANA YA KUWEKWA BAYANA UKWELI WA UTAPELI NA UJAMBAZI HUO UTAMAANISHA WATU MUHIMU KUPOTEZA NYADHIFA ZAO.SIO KWAMBA HILO NI BAYA BALI HALIWEZEKANI KATIKA MAZINGIRA YA SIASA ZETU ZA KUJIKOMBA,KUOGOPANA NA BORA LIENDE.


PENGINE HII NI SABABU NYINGINE MUHIMU KWA WAPIGAKURA KUIHOJI CCM COME THE 2010 ELECTION.HEBU SOMA KWANZA HAPA CHINI:


Mazingaombwe tupu Richmond


• Shellukindo anuna, akataa kuulizwa maswali

na Deogratius Temba

KWA mara nyingine tena, serikali jana ilishindwa kuwasilisha maelezo ya utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge kuhusu hatma ya kashfa ya Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

Licha ya kauli thabiti iliyotolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, William Shellukindo mwanzoni mwa wiki kwa waandishi wa habari kuwa, serikali ingetoa maelezo hayo kwa kamati yake jana, hali ilikuwa tofauti baada ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kutotokea katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam, ambako kamati mbalimbali za Bunge zinaendelea na vikao vyake.

Kwa mujibu wa ratiba mpya ya vikao vya kamati hiyo vinavyoendelea katika ofisi hizo, jana kamati ilipanga kupokea taarifa hiyo na kuanza kuijadili kwa muda wa siku mbili, baada ya wiki iliyopita kuahirishwa kwa kile kilichoelezwa kuwa Waziri Ngeleja alikuwa nje ya nchi.

Habari ambazo Tanzania Daima Jumatano lilizipata kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini zilieleza kuwa, walipokea ombi la serikali la kuahirishwa kwa mjadala huo ili ijipange sawasawa.

Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo alieleza kuwa, serikali katika ombi lake kwa kamati, iliitaka kuliweka suala hilo pembeni hadi baadaye itakapoarifiwa, na ilitaka kuendelea na ratiba zake nyingine kama zilivyopangwa.

“Ni kweli leo (jana) tulikuwa tuipokee taarifa ya serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge, lakini haya ni masuala yanayoihusu serikali zaidi, wameomba tuendelee na kazi nyingine, wanaweza kuiwasilisha kesho (leo) au keshokutwa (kesho),” alisema mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo aliyeomba jina lake lisitajwe kwa sababu si msemaji.

Alieleza zaidi maelezo kamili ya kuahirishwa kwa upokeaji maelezo ya serikali yanaweza kutolewa na mwenyekiti wa kamati hiyo, Shellukindo, ambaye ndiye aliyepokea ombi hilo la serikali.

Shellukindo alipoulizwa kuhusu hali hiyo, aligeuka mbogo kwa waandishi wa habari kwa kuwataka wasimuulize maswali kuhusu Richmond. Kwa ukali aliwataka waulize maswali yanayohusiana na kampuni ya kuzalisha umeme wa gesi ya Songas, ambayo ilikuwa ikijadiliwa na kamati yake jana.

“Nataka kuwaeleza tulichozungumza na watu wa Songas, lakini nikimaliza nitakaribisha maswali ambayo yatahusiana tu na suala hili la Songas, nje ya hapo sitajibu,” alisema Shellukindo.

Msimamo huo wa Shellukindo uliwafanya waandishi wa habari waliokuwa na shauku ya kutaka kujua sababu za serikali kushindwa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji maazimio ya Bunge ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na watu wengi, kushikwa na butwaa na kushindwa kuuliza maswali kwa muda.

Baada ya dakika chake, Shellukindo ambaye alionekana kutokuwa katika hali ya kawaida, alieleza kuwa kamati yake imezungumza na uongozi wa Kampuni ya Songas kuhusu utengenezaji wa mashine ya kuzalisha umeme wa megawati 20 iliyoharibika wiki iliyopita na upatikanaji wa gesi nchini.

Hata hivyo katika hali ambayo haikutarajiwa na waandishi wa habari, wakati Shellukindo akiendelea kutoa maelezo, wajumbe wa kamati walianza kusimama mmoja mmoja na kuondoka na walipoulizwa sababu ya kuondoka katika kikao hicho, walidai kuwa wana majukumu mengi ya kufanya.

Kabla ya Shellukindo kuanza kuongea na waandishi wa habari, Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe ambaye ni kinara wa kashfa hiyo, alisimama na kutoka nje. Mwakyembe amekuwa hazungumzi lolote na waandishi tangu kuanza kwa vikao vya kamati hiyo.

Awali Tanzania Daima Jumatano lilielezwa kuwa, taarifa hiyo haitawasilishwa kwa kamati hiyo ikiwa jijini Dar es Salaam kwa sababu za kiusalama na badala yake itawasilishwa mjini Dodoma.

Taarifa hizo zilieleza kuwa, wajumbe wa kamati ya Shellukindo watapata nafasi ya kuijadili wakiwa Dodoma na endapo watairidhia wataruhusu serikali iiwasilishe bungeni katika mkutano wa 17, utakaokuwa ukiendelea. Mkutano huo unatarajiwa kuanza Oktoba 27.

Taarifa nyingine zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa, serikali ina hofu kuwa, iwapo itaitoa taarifa hiyo kwa kamati ya Shellukindo mapema, inaweza kuvuja na kutoa mwanya kwa baadhi ya watuhumiwa wa Richmond kujipanga namna ya kujisafisha au kupoteza baadhi ya vielelezo.

Mmoja wa viongozi wa serikali aliyezungumza na gazeti hili katika eneo la ofisi ndogo za Bunge jana, alisema serikali imekuwa ikisita kuiwasilisha taarifa yake kwa kamati hiyo kwa sababu inaweza kuvuja na kuvuruga mwenendo wa mambo.

“Hofu yetu ni kwamba, serikali ikiwasilisha taarifa hii mapema, hadi kufikia siku ya kuijadili bungeni itakuwa imezagaa mno, taarifa kuenea si jambo jema, watuhumiwa wanaweza kujipanga, inatakiwa iwe ya kushtukizia,” alisema ofisa huyo.

Katika mjadala huo uliokamiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, wajumbe pamoja na mambo mengine wataangalia kama serikali imejibu maswali na maagizo ambayo Bunge liliipa serikali.

Wakati Bunge likitaka watu zaidi waliohusika wawajibishwe, tayari mmoja wa wawakilishi wa Kampuni ya Richmond, Naeem Adam Gire, ameshafikishwa katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam Januari 13, mwaka huu na kusomewa mashtaka matano ya makosa ya jinai.

CHANZO: Tanzania Daima

MAAMUZI YA KUIPA TENDA RICHMOND HAYAKUFANYIKA KWENYE KIJIWE CHA KAHAWA BALI KWENYE OFISI NYETI.SASA KWANINI KILA ALIYEHUSIKA KWENYE MAAMUZI HAYO ASIWEKWE HADHARANI?JIBU JEPESI NI KWAMBA KUFANYA HIVYO KUNAWEZA KUPELEKEA "KUISOGEZA 2010 KABLA YA MUDA WAKE" (READ BETWEEN THE LINES,PLZ).

4 Aug 2009


Mkutano mwingine wa Bunge umamilizika huko Dodoma huku danadana ziliendelea kuhusu ufisadi wa Richmond.Wakati Watanzania wakiendelea kumwagiwa "changa la macho",gazeti la Mwananchi linaripoti kuwa Mwanasheria Mkuu,Johnston Mwanyika,ambaye anahusishwa kwa karibu na ufisadi huo,anatarajiwa kustaafu kabla ya kuanza kwa kikao kijacho cha Bunge.Na akistaafu ndio habari imekwisha!Kama unabisha,jiulize kwanini uamuzi wa Lowassa,Msabaha,Karamagi na Chenge ndio ulikuwa mwisho wa kuhusishwa kwao na tuhuma zote zinazowakabili.Yaani mtu anaiba,au anawezesha wizi,au kwa lugha mwafaka ANAFISADI kisha anajiuzulu!Kwa lugha nyingine,anahitimisha utumishi wake uliotukuka kwa heshima zote.


Kwa wale wanaotarajia jipya kwenye kikao kijacho cha Bunge hapo Novemba wanapoteza muda wao.Ngonjera zitakuwa zilezile za "Bunge kuwaka moto kuhusu Richmond","Wabunge wampania Masha","Ngeleja kuwekwa kitimoto",na uzushi mwingine.Kikao kitaanza,wahehimiwa watalambishwa mamilioni yao ya mishahara (huku Watanzania wenzao waliokodoshwa kwa wahindi wa TRL wakizungungushwa kila kukicha na wawekezaji hao feki),na hatimaye kikao kitafikia ukingoni kwa ahadi kuwa "ishu x,y na z zitajadiliwa katika kikao kijacho"


Na bado itapojiri 2010 utaskia watu wazima na akili zao wamefungiwa baa au shuleni (na mgombea mmoja) ili wasinunuliwe na mgombea mwingine!Wawakilishi wetu wanafahamu kuwa hata wakizembea namna gani bado siasa itaendelea kuwa shughuli yenye mvuto mkubwa miongoni mwa wananchi kuliko jambo lolote lile.


Halafu tunaambiwa eti tuna BUNGE LENYE MENO!Labda ya plastiki!

30 Jul 2009


Tume huru inayochunguza uhusika wa Uingereza katika vita ya Iraki imetangaza kuwa itamhoji Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair.


Atakayenuna na anune,lakini ni dhahiri kuwa Rais wetu mstaafu ( wa awamu ya tatu),Benjamin William Mkapa,amekuwa akiandamwa na tuhuma za ufisadi wakati akiwa jengo takatifu la Ikulu.Hoja kubwa ya wanaomtetea Mkapa ni maneno kama "Mwacheni Mzee wetu apumzike".

Ni wazo zuri kutosumbua wazee wetu,lakini ingeleta maana kama wazee wote,na si Mkapa pekee,wangekumbukwa katika "maombi" hayo kuwa waachwe wapumzike.Mbona "busara" hizo hazijatumika kuwakumbuka wazee (halisi) wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki?Wamesumbuliwa,wamezungushwa,wametishiwa FFU,na kufanyiwa kila aina ya vituko...tofauti na Mkapa-ambaye hajaomba atetewe au ajitetee-wastaafu hao wanadai stahili yao halali.Hawakutumia ofisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kununua japo vifusi vya kokoto au kuanzisha chama cha kuweka na kukopa,tofauti na Mkapa ambaye pamoja na mambo mengine anayetuhumiwa kujiuzia mgodi wa Kiwira kwa bei ya kishkaji na pia kuhusishwa na kuanzisha benki.

Hivi njia bora zaidi ya kumwacha Mkapa apumzike ni kwa wanasiasa kumsafisha katika tuhuma za ufisadi zinazomkabili au kwa mahakama-chombo chenye mamlaka ya kikatiba kutoa haki-kufanya kazi hiyo?Wanasiasa wetu ni wavivu wa kufikiri.Wao ni binadamu,kwa maana hiyo leo wapo kesho hawapo-aidha kiuhai au kimadaraka.Utetezi wao leo unaweza kabisa kuondoka pindi nao watakapoondoka.Uzuri wa taasisi-kama mahakama-ni kwamba inastahili kuwepo kwa muda mrefu au hata milele ikibidi.Na hata ikibadilishwa,misingi yake itaendelea kuwepo.Kwa mantiki hiyo,namna pekee ya "kumwacha Mkapa apumzike" ni kumburuza mahakamani kisha haki itendekee huko.Kupuuza ushauri huu kunaweza kupelekea mzee huyo kuburuzwa kwa nguvu kwenda kujibu tuhuma zake wakati watetezi wake wa sasa hawako madarakani au nao wakiwa wanakabiliwa na tuhuma za kujibu.Hebu chukua mfano mwepesi kama huu.Unadhani Charles Taylor huko aliko anakumbuka flani aliyekuwa anamtetea?Hapo ni kila mtu anabeba mzigo wake.

Sawa,Tanzania sio Uingereza.Na ni kweli kwamba sio kila wafanyalo Waingereza lazima sie pia tulifanye.Lakini mfano wa Blair kufikishwa kwenye tume hiyo ya vita ya Irak inapswa kuwa changamoto nzuri kwa mamlaka zetu kuangalia umuhimu wa kuzingatia sheria na taratibu badala ya kuendekeza ushakaji na kubebana.By the way,si kila mtuhumiwa anayefikishwa kwenye vyombo vya sheria lazima aonekane ana hatia.

Mzee wetu Mkapa hatoweza kupumzika hadi sheria itakapochukua mkondo wake kumsafisha au kumtia hatiani.Kuzembea kufanya hivyo ni kuiachia "mahakama ya umma" (court of public opinion) kumhukumu pasipo kumpatia nafasi ya kujitetea.Na kwa vile mahakama hiyo ya umma haina utaratibu wa kukata rufaa pindi hukumu ikishatolewa,tuhuma dhidi ya Mkapa zitaendelea kuwepo hadi hapo......God knows!Kama wanaomtetea wanampenda kwa dhati (au hata kinafiki) basi ni vema wakamwepusha na hatari ya kuburuzwa mahakamani akiwa na mkongojo wake,say miaka 20 au zaidi kutoka sasa.

Binafsi siamini kuwa wanaomtetea Mkapa wanafanya hivyo kwa vile wanamheshimu sana au wanaamini kuwa tuhuma hizo ni uzushi.Badala yake,wanachelea kwamba wakiruhusu sheria ichukue mkondo wake,kesho wao nao watajikuta wakikabiliwa na hali hiyohiyo kama ya Mkapa.Waadilifu hawaogopi sheria bali wanaiheshimu na kuilinda,lakini wenye mapungufu kwenye maadili yao huiogopa sheria kama kirusi cha mafua ya nguruwe (japo huitumia kuwakandamiza wabaya wao).

Naamini pia kuwa ipo siku Mkapa na watuhumiwa wengine wa ufisadi watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.Inaweza kuwa sio kesho au mwaka kesho lakini siku hiyo itafika.Na hapa nazungumzia mahakama za kidunia na sio ile ya kwenye wimbo niupendao wa "na kila mtu atatoa habari zake mwenyewe mbele ya Mungu,siku hiyo itafika...."

Kuendeleza ushkaji katika mambo yanayopaswa kushughulikiwa kisheria kunaweza pia kusambaza kirusi cha "ah mbona yule fisadi anatetewa na kusafishwa,what's wrong with me kufisadi pia?Si nami nitatetewa kama fisadi X..."Hapo tunafanya reproduction ya ufisadi katika jamii.Yayumkinika kuhisi kuwa kwa namna watuhumiwa wa ufisadi wa EPA,Richmond na maskandali mengine wanavyoendelea kuogopwa,tayari mafisadi hao wameshaambukiza virusi vya ufisadi kwa Watanzania wengine chungu mbovu.Thing is,kama wenye maamuzi wameamua kuhalalisha visivyo halali,then visivyo halali vinageuka kuwa halali.

Na kama kuna mzembe ataona wazo langu la kuchukua hatua dhidi ya Mkapa ni ukosefu wa nidhamu,then they can simply shove it up kunakostahili.


Kizitto Noya, Dodoma


SASA ni wazi kwamba sakata la Richmond limeingia katika hatua nyingine baada ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ofisi Rais kutangaza kwamba, Rais Jakaya Kikwete hahusiki kwa namna yoyote na kashfa hiyo ambayo inaendelea kulitikisa taifa kwa muda sasa.

Hatua ya Rais Kikwete kutotaka kuhusishwa na kashfa hiyo ya Richmond kunazidi kuibua maswali mengi kutoka kwa wananchi kwamba, ni nini hatima ya mjadala huo ambao unazidi kupamba moto kila kukicha nje na ndani ya Bunge.

Wakati Rais Kikwete akijivua kutoka katika sakata hilo, Kamati ya Nishati na Madini imetoa maazimio ya kupinga jinsi serikali inavyotekeleza maazimio ya Bunge kuhusu ripoti ya Richmond. Jana jioni Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ilitoa taarifa ikimuepusha rais na kashfa hiyo.

"Tumepata kusema huko nyuma, na tunapenda kusisitiza kwa mara nyingine kuwa, Rais hana mkono katika Richmond na hata Ripoti ya Bunge iliyotolewa kufuatia uchunguzi katika suala hilo la Richmond, haikumhusisha Rais Kikwete," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa ya Ikulu, imetolewa huku Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba akidai kwamba, Rais Kikwete anahusika na Richmond kwa kuwa maamuzi yalifanyika chini ya serikali anayoiongoza.

Habari kutoka Dodoma zinadai kuwa kutokana na kusuasua kwa utekelezaji wa maazimio ya Bunge kutaka maafisa wa serikali waliohusika kwa njia moja au nyingine na mchakato wa kampuni hiyo kupewa zabuni Tanesco, wachukuliwe hatua.

Kundi mojawapo la wabunge limeeleza kutoridhishwa na ripoti ya serikali iliyotolewa bungeni hivi karibuni kuwasafisha. Kundi hilo limepanga kumchukulia hatua kubwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye ndiye kiongozi mkuu wa serikali bungeni, kutokana na kuwanusuru maafisa waliotuhumiwa kuhusika na kashfa hiyo.

Wakati kamati hiyo ikitoa msimamo huo, wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikutana jana usiku katika Ukumbi wa Pius Msekwa kutafakari sakata hilo.

Ingawa tangazo la Mwenyekiti wa Bunge, Job Ndugai jana mchana halikueleza agenda za kikao hicho, vyanzo huru vya habari vililidokeza gazeti hili kuwa wabunge hao wangejadili ripoti ya Richmond na kuweka mkakati wa kuinusuru serikali.

Mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini ambaye hakutaka kutajwa gazetini akihofia kuvunja Kanuni za Bunge kwa kutoa siri za vikao, alisema kamati haikuridhishwa na ripoti ya serikali hasa katika suala la kuwasafisha Mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hoseah na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika.

"Kamati haikubaliani na ripoti hiyo hasa pale iliposema Dk Hoseah na Mwanyika hawana hatia. Tumekuwa na vikao kwa siku mbili jana (juzi), leo (jana) na bado tunaendelea kesho (leo),”alisema.

Alisema mapendekezo ya kamati ya Bunge kuhusu Richmond yalijitosheleza kimaamuzi na serikali ilitakiwa kuyatekeleza tu na sio kuendesha uchunguzi mwingine.

"Uchunguzi ulishafanywa na Bunge, serikali ilitakiwa kutekeleza tu. Ilikuaje ifanye tena uchunguzi kwa muda zaidi ya ule uliopangwa na Bunge badala ya kufanya utekelezaji?" alihoji.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, William Shelukindo na Makamu wake, Dk Harrison Mwakyembe hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo na simu zao za mikononi kutopatikana kabisa.

Mjumbe wa kamati iliyoundwa na Bunge kuchunguza suala la Richmond, Habib Mnyaa alikiri kuwa na taarifa ya kamati ya kisekta kukutana na kujadili ripoti hiyo, lakini akaeleza kuwa kikao hicho kilichokaa juzi na jana, kinamalizika leo.

"Kikao kimekuwapo, lakini hakijafikia maamuzi hayo unayosema," alisema Mnyaa akirejea hoja ya mwandishi wa habari aliyetaka kuthibitisha taarifa kwamba, kikao hicho kimejenga hoja ya kutokuwa na imani na serikali katika suala la Richmond.

Hata hivyo, habari nyingine zinadai kuwa kamati hiyo leo inatarajia kumweka kiti moto Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja ili awaeleze ni kwanini serikali imeshindwa kutekeleza mapendekezo ya Bunge.

Hata hivyo, mjumbe mwingine, Lucas Selelii alilieleza gazeti hili kuwa vikao vyote vilivyojadili Richmond, vimemaliza kazi na kuwasilisha hoja zake kwa spika wa Bunge Samuel Sitta ambaye leo atatoa mwongozo bungeni.

"Mjadala wa Richmond umemalizika na mambo yote kesho (leo) yako hadharani. Kamati ya kisekta imekaa na kuandaa taarifa ambayo amekabidhiwa spika wa Bunge leo (jana). Kikubwa jamii ijue kwamba, kamati iko makini, haimwonei wala kumpendelea mtu," alisema Selelii.

Alipotakiwa kuthibitisha kama amepokea hoja za kamati hiyo kuhusu Richmond na kwamba ataruhusu mjadala wake bungeni leo, Spika Sita alisema: "Haijanifikia bado".

Alifafanua kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini anatarajia kuwasilisha hoja za Kiwira na Richmond kesho, siku ambayo pia wenyeviti wa kamati za Miundombinu, Ardhi, Maliasili na Mazingira watawasilisha hoja zao.

Alibanwa zaidi aeleze kama endapo angeipata jana jioni angekuwa tayari kuiwasilisha leo kama ilivyoelezwa, alijibu:

"Hata kama nitaipata sasa, siwezi kuitable kesho (leo) kwani nahitaji muda kuisoma na kuielewa".

Awali mbung wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alisema suala la Richmond limeanza kuligawa taifa na njia pekee ya kuirudishia jamii imani na serikali, ni Rais kwa mamlaka ya kuwa mkuu wa nchi kuunda jopo la majaji kupitia upya hoja zote na kutoa maamuzi.

"Suala hili limeonekana kuigonganisha mihimili mikuu miwili ya dola, Bunge na Serikali, dawa yake sasa ili liishe, ni Rais kama mkuu wa nchi nasisitiza, mkuu wa nchi sio serikali kuunda tume ya majaji wapitie Maazimio ya Bunge, utekelezaji wa serikali na watoe maamuzi," alisema.

Alisema: "Inavyoonekana kila upande unavutia kwake, wakati Bunge likitaka serikali itekeleze mapendekezo yake ndani ya miezi mitatu, serikali imetumia karibu mwaka na nusu na bado inakuja na majibu ya kubabaisha.
CHANZO: Mwananchi

16 Apr 2009

Mke wa Lowassa azindua kitabu

Na Mwandishi Wetu,
MTANZANIA, Aprili 15, 2009.

Watu mbali mbali jana jioni walimiminika nyumbani kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kushuhudia uzinduzi wa kitabu kilichotungwa na mkewe Regina, uliofanywa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Regina aliandika kitabu hicho wakati akiwa katika matembezi binafsi inchini Israel, siku chache baada ya mumewe kujiuzulu uwaziri mkuu Februari mwaka jana kutokana na sakata la Richmond.

Kitabu hicho kilichoandikwa kwa lugha ya Kiingereza kiitwacho “Walk The Path With Diary in Israel, The Holy Land” kina kurasa 15 na dibaji yake imeandikwa na Monsinyori Julian Kangalawe kutoka Kanisa la Mtakatifu Joseph la Dar es Salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Kardinali Pengo, bila kufafanua, aliwataka Watanzania waache tabia ya kusulubiana. “Yesu alikuja duniani, akasulubiwa na hadi leo watu wanaendelea kusulubiana. Tuache mchezo huo,” alisema.

Mhubiri maarufu mwenye makazi yake mjini Arusha, Christopher Mwakasege, ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, alisema ni yeye aliyetoa wazo kwa Lowassa na mkewe kutembelea Israel baada ya matatizo yaliyowakuta.

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Malasusa, ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, aliwahimiza watu kujenga moyo wa kupendana ili kujenga nchi yenye maelewano.

Mbali na Mlasasusa, Askofu Mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki ni Pwani, Elinaza Sendoro, pia alihudhuria hafla hiyo, na akatumia nafasi hiyo kuwashawishi watu kutembelea Israel kujionea namna watu wa dini tofauti wanavyoishi.

Akizunmgumza katika hafla hiyo, Lowassa mwenyewe alisema baada ya kupata matatizo nayo, yeye na familia yake waliamua kumgeukia Mungu na kwamba ndio maana wakaamua kwenda Israel kutembelea maeneo takatifu.

LET'S BE HONEST.LOWASSA ALIJIUZULU KUTOKANA NA UFISADI WA RICHMOND.HILO HALINA MJADALA.SINA TATIZO NA HIYO ZIARA YAKE YA KUTEMBELEA ISRAEL.KAMA KWELI ALIENDA KUTUBU AU LA,ANAJUA YEYE NA MUNGU WAKE .LAKINI NASHINDWA KUWAELEWA HAO MAASKOFU WALIOJITOKEZA KATIKA SHUGHULI HIYO.NAELEWA KUWA DINI INAHUBIRI UPENDO NA KUSAMEHE WAKOSAJI LAKINI SIDHANI KAMA HIYO INAMAANISHA VIONGOZI WA DINI KUWA KARIBU NA WATUHUMIWA WA UFISADI.
NA MHASHAMU PENGO ANAPOTOA MFANO WA YESU KUSULUBIWA ANATAKA KUTUELEZA NINI?KWAMBA LOWASSA NAE ALISULUBIWA KAMA YESU?HIVI SIO RICHMOND NA BINAMU YAKE DOWANS ILIYOWASULUBU WALALAHOI WA TANZANIA KWA MAMILIONI YA SHILINGI!YESU ALISULUBIWA MSALABANI ILI KUWANUSUBURU WANYONGE,MASIKINI,WAJANE,YATIMA,NK KUTOKA KWA MINYORORO WANAYOFUNGWA NA MAFISADI.

JAPO NINA HESHIMA KUBWA KWA VIONGOZI HAO WA DINI LAKINI YAYUMKINIKA KUELEZA KWAMBA UHUDHURIAJI WAO HUO KATIKA HAFLA YA MTUHUMIWA WA UFISADI UNAWEZA KUTAFSIRIWA NA WAUMINI WAO KUWA NAO WANASAPOTI UFISADI.
IN A WIDER CONTEXT,UFISADI NI MATOKEO YA KUMOMONYOKA KWA MAADILI YA KIROHO.KITACHOTUPA IMANI KUWA WATUHUMIWA WA UFISADI WAMEAMUA KUMREJEA MUNGU SIO PUBLICITY STUNTS BALI FIRM COMMITMENT KATIKA KUHURUMIA NAFSI NA ROHO ZINAZOANGAMIA KUTOKANA NA MATENDO YA MAFISADI HAO.

23 Mar 2009


KADA maarufu wa Chama cha Mapinduzi, Nape Nnauye, amesema malumbano yanayoendelea sasa nchini ni ishara kwamba mafisadi wamejipanga kuifanya nchi isitawalike.

Nape alitoa kauli hiyo jana alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu hali ya kisiasa nchini, hususani malumbano yanayoendelea sasa kati ya Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe.

Bila kutaja majina ya watu, Nape alisema chimbuko la malumbano hayo aliyoyaita ya kipuuzi ni kashfa nzima ya kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond, iliyosababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na aliyekuwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha, kujiuzulu.

Huku akiwa makini kuchangua maneno ya kuzungumza, Nape alisema malumbano hayo yanaonyesha kuna baadhi ya watu hawakuridhika na taarifa ya Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Dk. Mwakyembe, hivyo kuna ulazima wa hoja hiyo kurudishwa tena bungeni ili kukata mzizi wa fitna.

“Kuna kila dalili kuwa mafisadi wamejipanga kuhakikisha nchi haitawaliki, ndiyo maana mijadala isiyo na kichwa wala miguu inaibuka kila kukicha hata kwa mambo ambayo yamekwishaamuliwa na chombo kikubwa kama Bunge,” alisema.

Katika kuthibitisha kauli yake, Nape alisema ana taarifa za siri kuwa kuna baadhi ya mafisadi wamekuwa wakifanya mikutano ya faragha ambapo pamoja na mambo mengine, wamepanga kuhakikisha nchi haitawaliki kwa kuibua hoja na mijadala kupitia baadhi ya vyombo vyao vya habari.

“Tunakoenda ni kubaya, ila naamini serikali iko imara na CCM kama chama tawala, tutaomba tulizungumze kwenye vikao vyetu kwa nia njema ya kuliokoa taifa linalovurugwa na watu wachache wenye fedha,” alisema Nape.

Nape alisema ili kuhakikisha Tanzania haiyumbishwi, aliwataka wananchi kupuuzia mjadala wa sasa kwa madai kuwa hauna tija na una lengo la kuhatarisha amani na utulivu uliopo nchini.

Kuhusu mjadala wa ununuzi wa mitambo ya kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans iliyorithi kutoka Kampuni ya Richmond, kada huyo wa CCM alisema anashangazwa na uamuzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuomba kibali cha Bunge au kamati zake.

“Kwani TANESCO wanapoenda kununua transfoma na vifaa vingine, wanaomba kibali cha Bunge? Kama si hivyo, kwa nini wanataka kuhalalisha ununuzi wa mitambo ya Dowans kupitia kamati za Bunge? Hata hivyo, Bunge lilishatoa msimamo wake juu ya hilo, kama kuna mtu hakuridhika, alirudishe bungeni na si kuwagawa Watanzania kwa mijadala isiyoisha na vitisho,” alisema Nape.

Mwanasiasa huyo machachari aliwataka mafisadi kutambua kuwa hata wakiibua mijadala ya kuwagawa Watanzania kama ilivyo sasa, hakutabadili ukweli kwamba Richmond na hata mrithi wake Dowans, ndio waliolifikisha taifa hapa lilipo.

Kwa upande wake, Mbunge wa Maswa, John Shibuda, alisema malumbano yanayoendelea sasa kati ya Dk. Mwakyembe na Rostam kumetokana na upepo wa kisiasa ambao wakati mwingine huleta tija katika kukuza demokrasia.

Hata hivyo, Shibuda ambaye hupenda kuzungumza kwa mafumbo, alisema mjadala huo umejikita kwenye hila na visa vya kufunika mema na mazuri ya mtu.

“Mimi naona hayo ni mapepo ya kisiasa na mtenguko wa fikra ambao umeleta mng’atuko dhidi ya dhulma, lakini ni mjadala wa heri kwa maana kuwa unawafanya watu kutoa manung’uniko yao, bila hivyo hali ingekuwa mbaya siku moja, kwa hiyo naona mjadala uendelee,” alisema Shibuda.

Mbunge wa zamani wa Morogoro Vijijini, Semindu Pawa (CCM), aliiambia Tanzania Daima jana kuwa, mjadala huo sasa umechacha na kuwataka waandishi wa habari kuachana nao.

“Mimi sitaki kusema nani yuko sahihi, lakini nasema mjadala huo umechacha, umepitwa na wakati, wanahabari mkiacha tu, hautausikia tena, lakini naweza kusema wanahabari ndio mnaoukuza, waacheni,” alisema Semindu Pawa.

Mwishoni mwa wiki, Dk. Mwakyembe alijibu tuhuma zinazomhusisha na kumiliki kampuni binafsi ya kuzalisha umeme kuwa ni kazi mahususi inayofanywa na majeruhi wa vita ya ufisadi, ambao waliumizwa na matokeo ya kazi ya Kamati Teule ya Bunge ya kuchunguza mkataba wa Kampuni ya Richmond, ambayo yeye alikuwa mwenyekiti wake.


Hatua ya Mwakyembe kujibu tuhuma hizo, ilikuja baada ya magazeti mawili ya kila siku, (si Tanzania Daima) kuchapisha habari zinazomhusisha yeye na umiliki wa hisa 1,000,000 zenye thamani ya jumla ya sh bilioni 1.5 katika Kampuni ya Power Pool East Africa Ltd.

Mbali ya habari hizo kuandikwa katika magazeti hayo mawili; moja la binafsi na jingine la serikali, nyaraka kadhaa zinazomhusisha Mwakyembe na kampuni hiyo, zimesambazwa katika mtandao wa intaneti.

Taarifa hizo pia zinamtaja Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya TANESCO, kuwa miongoni mwa wanahisa wa kampuni hiyo binafsi ambayo wakati fulani Mwakyembe alipata kuwa mtendaji mkuu wake.

Taarifa hizo zinajaribu kujenga hoja zinazojaribu kumuondolea Mwakyembe uhalali wa kuendelea kudai kupambana na ufisadi ndani na nje ya Bunge ilhali yeye mwenyewe akionekana kuwa na ukwasi mkubwa unaotiliwa shaka.

Pia zinaonyesha kuwa, Mwakyembe licha ya kuwa na hisa nyingi katika kampuni hiyo, ameisaidia katika mambo mbalimbali ambayo hata hivyo hayakufafanuliwa, wakati akiwa katika wadhifa wa mtendaji mkuu.

Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, lengo kuu la kusambaza nyaraka hizo ni kujaribu kumnyoshea kidole Mwakyembe na kujaribu kumuondolea uhalali wa kuendelea kupigania sekta ya nishati ilhali yeye mwenyewe akijua kuwa na maslahi.

Mwakyembe ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alisema kuwa katika Kampuni ya Power Pool East Africa Ltd, hakuwezi kukamsababishia akaingia katika mgogoro wowote wa kimaslahi kutokana na ukweli kwamba, kampuni hiyo iliyosajiliwa kwa Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA), bado ipo katika hatua ya awali ya mradi ambao bado haujaanza kuzalisha.

Alipotakiwa kueleza ni kwa nini wakati alipoteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyoichunguza Richmond kuanzia Oktoba mwaka juzi na kuwasilisha ripoti yake mwaka jana, hakueleza lolote kuhusu kuwa na kampuni ya kuzalisha umeme, Mwakyembe alisema asingeweza kufanya hivyo wakati mkakati wao wa kikampuni ukiwa katika hatua ya mradi tu.

‘‘Kwa mujibu wa sheria ya makampuni, majina yanakuwapo mpaka hapo kampuni itakapoanza ‘ku-take off’ (kuanza kazi). Sikuweza kuitaja kuwa ni sehemu ya makampuni yangu, kwa kuwa bado ilikuwa katika hatua ya mradi,” alisema Mwakyembe.

Mwanasiasa huyo alikwenda mbele zaidi na kuwaeleza wanahabari hao ambao miongoni mwao walionekana dhahiri kukabiliana naye kwa njia ya malumbano kuwa, hata wakati akiandikisha mali anazomiliki chini ya sheria ya viongozi kutangaza mali wanazomiliki, hakuitaja kampuni hiyo ya Power Pool kwa sababu hizo hizo za kutoanza kwake kazi.

Akifafanua tuhuma hizo dhidi yake, alimgeukia mbunge mwenzake wa CCM, Rostam Aziz na kumtuhumu kuwa nyuma ya habari zote mbaya zinazoandikwa dhidi yake.

Huku akilitaja jina la Rostam mara kadhaa, Mwakyembe alisema ni jambo ambalo haliingii akilini kwa mtu ambaye amechafuka kuamua kutumia maji taka kujisafisha.


WALA TUSINGEFIKA HAPA TULIPO IWAPO SHERIA INGEFUATA MKONDO WAKE.VINARA WALIOTUINGIZA MKENGE KWENYE UTAPELI WA RICHMOND HAWAJACHUKULIWA HATUA BAADA YA KUJIUZULU,NA SASA WAMEPATA JEURI YA KUTAKA KUTULIZA MARA YA PILI KWA KUTUUZIA MITAMBO MITUMBA ILEILE ILE YA RICHMOND a.k.a DOWANS.HUU MTINDO WA KULINDANA UTALIPELEKA TAIFA MAHALA PABAYA.

HOWEVER,LET IT BE KNOW TO MAFISADI AND THOSE WHO SHIELD THEM THAT IF THEY TURN OUR BELOVED COUNTRY INTO ANOTHER MADAGASCAR THEY TOO WOULDNT BE SAFE!

29 Jan 2009

BONYEZA HAPA kusoma habari hiyo na nyinginezo,pamoja na makala motomoto.

3 Nov 2008

Mitambo ya Richmond ikiwasili kwa mbwembwe.Kampuni hiyo ya kitapeli imerithiwa na Dowans.Picha kwa hisani ya MICHUZI

Kampuni ya Dowans Tanzania Ltd imetangaza rasmi zabuni ya kuuza mitambo yake ya kuzalisha umeme ikiwa ni miezi mitatu baada ya serikali kusitisha mkataba wake na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco). 

Dowans Tanzania Limited ilirithi mkataba wa kuiuzia umeme wa megawati 120 Tanesco kutoka kwa Kampuni ya Richmond Development LLC ambayo baadaye iligundulika kuwa ni kampuni hewa. Serikali ilifikia uamuzi wa kusitisha mkataba huo Agosti mosi mwaka huu baada ya kuridhika kuwa mkataba huo haukuwa halali wala haukuwa na nguvu kisheria. 

Serikali pia ilisema ilibaini iwapo mkataba husika ungekuwa halali, uhamishaji wa mkataba kutoka RDVCO badala ya Richmond Development LLC kwenda Dowans Tanzania Ltd, haukufuata msingi wa mkataba.“Hivyo uhamishaji haukuwa halali na ifahamike kwamba mkataba ulikuwa baina ya Richmond Development Company LLC na Tanesco na siyo na REDVCO na Tanesco,” alisema. 

Tangazo ambalo limetolewa na kampuni hiyo leo kwa vyombo vya habari, limesema watu au kampuni makini ambazo zitakuwa na nia ya kununua mitambo hiyo wanakaribishwa kuinunua. Kutolewa kwa tangazo hilo la kuuza mitambo yake, huenda ikawa ni ishara ya kampuni hiyo kufungasha virago baada ya kimya kingi tangu mkataba huo usitishwe. 

Baada ya kusitishwa kwa mkataba huo, Tanesco imekuwa ikitumia pamoja na vyanzo vingine vya umeme, mitambo yake ya megawati 100 iliyojengwa na Kampuni ya Watsilla ya Finland ili kufidia upungufu uliotokana na kuondoka Dowans. Tanesco pia imekuwa ikinunua umeme kutoka kwa kampuni za Songas na IPTL. 

Siku chache baada ya kusitishwa kwa mkataba huo, mmoja wa maofisa wa Dowans aliiambia HabariLeo kuwa walikuwa na njia nyingi za kufanya na mitambo hiyo ikiwa kuikodisha au kuiuza kwa watu wengine. “Kukatishwa kwa mkataba haina maana hatuwezi endelea na kazi, tutatafuta wateja wengine kama kampuni za migodi na kuwauzia umeme au tunaweza kukodisha mitambo yenyewe,” alisema ofisa huyo. 

Kwa mujibu wa tangazo hilo, mitambo hiyo ina mashine tano za uzalishaji wa umeme ambazo mnunuzi atazinunua kwa bei ya hali yake ilivyo kwa wakati wa kununua. “Vifaa vyote ikiwa pamoja na vipuri na vifaa vingine vya pembeni vipo na vitauzwa kwa pamoja kama bidhaa moja,” lilisema tangazo hilo. 

Mkataba kati ya Tanesco na kampuni ya Richmond Development LLC umekuwa ni mmoja wa mikataba ambayo ilivuta hisia za watu wengi kitu ambacho kilisababisha kuundwa kwa Kamati iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM), ambako kutokana na ripoti hiyo, aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa alijiuzulu. 

Wengine waliojiuzulu ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha ambaye alikuwa Waziri wa Wizara hiyo na kabla ya kuhamishiwa Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kutokana na mapendekezo ya ripoti hiyo, serikali iliahidi kuyafanyia kazi mapendekezo ya ripoti hiyo, ambapo moja ya hatua iliyochukuliwa ni kusitisha mkataba na Dowans.

 CHANZO : HabariLeo

I SMELL SOMETHING FISHY HERE.HII TENDA YA KUTANGAZWA KWA PRESS RELEASE INAZIDISHA SUSPICION YANGU.KWANINI ISIWE TANGAZO LA ZABUNI GAZETINI BADALA YA KU-SEEK ATTENTION KWENYE MAGAZETI,AMBAYO MENGI YAO HUWA HAYANA MUDA WA KU-READ BETWEEN LINES YANAPOPATA STORIES?I SUSPECT KUNA DILI INATAKA KUCHEZWA HAPA.POTENTIAL BUYER WA MITAMBO HIYO ATAKUWA TANESCO (CLICK HAPA NA HAPA KUPATA HINT). ITANUNULIWA KWA UTARATIBU UNAOONEKANA TRANSPARENT (HIVI TRANSPARENCY INA UMUHIMUWOWOTE  KATIKA KUNUNUA BIDHAA BOMU?) KISHA MITAMBO HIYO (AMBAYO "WAMBEA" WANADAI NI INJINI MBOVU ZA NDEGE) ITAISHIA "KUBUMA".DOWANS WAKATI HUO ISHAKUWA KAMPUNI MFU,KAMA MZAZI WAKE RICHMOND.LET'S WAIT AND SEE!

31 Oct 2008


*Yataka sheria ziachwe zifuate mkondo wake
*Yasubiri uamuzi kuhusu sakata la ufisadi
*Yaguswa na usanii wa kampuni ya Richmond
*Yaahidi Rais Obama au McCain kuja nchini

Na Hassan Abbas


BALOZI wa Marekani nchini, Bw. Mark Green amekuwa mwanadiplomasia wa kwanza nchini kumshauri Rais Jakaya Kikwete kuhusu nini anachopaswa kukifanya saa chache kabla hajaamua hatima ya waliokwapua mabilioni kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA). 

Balozi Green aliyesisitiza kuwa mafisadi si watu wa kuachwa hata kama ni vigogo na kutaka sheria zichukue mkondo wake, ameifafanulia Majira jinsi alivyoguswa baada ya kuona kampuni ya kimarekani ya Richmond ilivyohusika katika utata kwenye sekta ya umeme nchini. 

Balozi Green alisema hayo jana katika mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake Dar es Salaam kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu uchaguzi wa Marekani, mtikisiko wa uchumi, hali ya kisiasa nchini na mtazamo wake kuhusu wagombea, maseneta Barack Obama na John McCain. 

EPA na Richmond 

Balozi Green alisema hawezi kujinasibu kuwa Marekani ni Taifa la mfano katika kupambana na rushwa, lakini alisisitiza kuwa katika miaka 232 ya Uhuru wa Taifa hilo, ujenzi wa jamii yenye kuwajibika kwa kufuata utawala wa sheria usiomwogopa mtu ndio msingi. 

"Rais Kikwete anafanya kazi kubwa ya kujenga Taifa. Lakini vita dhidi ya ufisadi inahitaji kutowaacha watu wakatamba. Sheria ichukue mkondo wake hata kama mtu ni mashuhuri kiasi gani. 

"Sisi Marekani tumekuwa na azma ya wazi kuwa kiongozi wa umma akiiba fedha za watu, anachunguzwa na kuchukuliwa hatua. Wamarekani ni wakarimu sana kutoa fedha zao kusaidia watu, lakini ni wakali sana wanapoona inafanyiwa ufisadi. Rais Kikwete akitumia sheria atafanikiwa," alisema Balozi Green na kusisitiza kuwa katika sakata la EPA, waliopoka fedha hizo wanapaswa kuwajibishwa. 

Akifafanua kuhusu hilo, Balozi Green alisema Rais Kikwete alitaja mikakati mizuri alipozungumza bungeni kuhusu namna atakavyowashughulikia mafisadi wa EPA. 

"Rais alitaja mikakati mizuri. Tunasubiri kuona atakavyoitekeleza," alisema. Akizungumza bungeni Agosti 21 mwaka huu, Rais Kikwete aliwapa mafisadi hao hadi Oktoba 30 (jana) wawe wamerejesha fedha hizo, vinginevyo ifikapo Novemba mosi (kesho) wawe wameburutwa kortini. 

Sakata la Richmond, kampuni iliyoshinda zabuni ya kufua umeme wa mamilioni nchini ikijieleza kuwa ilitokea Marekani, ni moja ya matukio yaliyoitikisa Serikali ya Rais Kikwete mwanzoni tu mwa utawala wake. 

Akilizungumzia sakata hilo, Balozi Green alisema Serikali ya Tanzania katika kupambana na rushwa inapaswa kufuata sheria bila kujali mhusika au kampuni husika imetoka nchi gani. 

"Suala la Richmond najua ilikuja ikafanya kazi kupitia kampuni iliyosajiliwa nchini. Lakini bila kujali kampuni hiyo ilitoka wapi, Serikali inapaswa kuchukua sheria haraka inapoona kuna ufisadi," alisema huku akikiri kuwa ukweli kwamba kampuni hiyo ilijieleza kutoka Marekani, ulimsumbua wakati wa sakata hilo, ingawa ubalozi wake hauwajibiki moja kwa moja katika mikataba inayohusu kampuni binafsi. 

Uchaguzi wa Marekani 

Balozi Green alikiri kuwa uchaguzi wa mwaka huu wa nchi hiyo umekuwa na hamasa kubwa hasa kutokana na ushiriki wa Seneta Obama, Mmarekani mwenmye asili ya Afrika wa kwanza kuteuliwa na chama kikuu kuwania urais. 

"Ni kweli kwamba ushiriki wa Seneta Obama umeibua hamasa miongoni mwa Wamarekani wengi, hilo ni suala lisilo na ubishi. Lakini pia hata uteuzi wa Seneta McCain naye umeibua ushawishi katika baadhi ya nchi. 

"Wakati huku Afrika Obama anaonekana kuwa na ushawishi, McCain naye ni kivutio hasa katika nchi za Mashariki ya Mbali ambako kutokana na historia yake ya kushiriki vita ya Vietnamu na kwa miaka mingi aliyokaa kwenye Kamati ya Mambo ya Nje kwenye Bunge la Seneti, alishiriki masuala mengi yanayohusu eneo hilo," alisema Balozi Green ambaye ni mfuasi wa Republican. 

Alisema, akiwatathmini wagombea hao wawili, anaona kuwa wote kwa sera zao, wana uwezo wa kuisaidia Marekani iwapo mmojawapo ataingia Ikulu. 

"Ukiangalia sera zao, hakuna shaka kwamba wote (McCain na Obama) wana mikakati ya dhati kuisaidia Marekani na historia zao zinaonesha wana uwezo mkubwa," aliongeza. 

Akizungumzia somo ambalo nchi za Afrika zinaweza kujifunza kutokana na kampeni zinazoendelea sasa nchini Marekani, Balozi Green alisema kubwa ni umuhimu wa watu kujadiliana masuala ya kitaifa kwa uwazi na mwishowe kila mwananchi akawa na fursa ya kupiga kura na kumchagua kiongozi anayemtaka. 

"Siwezi kusema kuwa Marekani ina demokrasia ya kuigwa, sote bado tunajifunza kutoka kwa kila mmoja. Lakini kama ilivyoonekana, mijadala ya wazi ni kitu muhimu ili kujadili masuala ya kitaifa na mwishowe kuheshimu uhuru wa kupiga kura. Naamini mkiimarisha hili, Afrika na Tanzania zitafanikiwa," aliongeza. 

Msukusuko wa uchumi na Afrika 

Balozi Green alikiri kuwa uchumi wa Marekani umetikisika, lakini akazitoa wasiwasi nchi za Afrika hususani Tanzania, kuwa kiwango cha misaada ya Marekani hakitaathirika kutokana na hali hiyo. 

"Kwa mfano, miradi ambayo tumekubali kuisaidia Tanzania ilishapitishwa na fungu lake lipo, kwa hiyo haitaathirika, sioni sababu ya Watanzania kuwa na wasiwasi," alisisitiza. 

Pia alisema hofu ya miradi mingi iliyoanzishwa chini ya utawala wa chama cha Republican nayo kubatilishwa, iwapo kitaingia madarakani chama cha Democrat haina msingi, kwani wakati wa upitishaji wa miradi hiyo Wamarekani hukubaliana kwa pamoja bila kujali itikadi ya vyama. 

"Kwa bahati nzuri nilikuwa kwenye Baraza la Wawakilishi, ni mmoja wa wawakilishi waliopigania kupitishwa kwa sheria iliyounda shirika la Millenium Challenge Account, linalotoa misaada mbalimbali kwa Afrika ikiwamo Tanzania. 

"Bahati nzuri wakati wa kujadili masuala haya, wabunge walikuwa wamoja bila kujali itikadi. Kwa hiyo hakuna atakayeweza kuzuia miradi hii, iliamuliwa kwa sauti ya Wamarekani wote," alisema.

Obama au McCain kuja Tanzania 

Akizungumzia ushirikiano mzuri baina ya Tanzania na Marekani, Balozi Green aliisifu kazi nzuri iliyofanywa na Rais wa zamani wa Marekani, Bw. Bill Clinton, ambaye ujio wake nchini na kazi za taasisi zake, ziliwafanya Wamarekani wengi kuijua au kuwa na nia ya kuijua Tanzania. 

"Hata ujio wa Bush, watu wanaweza kunipongeza kwa kufanikisha kuja kwake, lakini historia nzuri iliyowekwa na Clinton ndiyo iliyowazindua Wamarekani wengi kisha akaja Bush na baadaye mkutano wa Sullivan, lakini pia wadhifa wa Rais Kikwete kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, vimeifanya Tanzania kujulikana zaidi. 

Akizungumzia uwezekano wa ofisi yake kuhakikisha Rais ajaye wa Marekani anafuata nyayo hizo kwa kufika nchini, Balozi Green alisema: 

"Nitafurahi kuona siku moja Rais ajaye wa Marekani awe Seneta McCain au Seneta Obama anaitembelea Tanzania, kuimarisha uhusiano mzuri uliopo. Niko tayari kushughulikia hilo ili afike hapa. 

"Bahati nzuri Seneta McCain nimeshawahi kukutana naye wakati nikiwa kwenye Baraza la Wawakilishi, Obama hatujaweza kukutana kwa sababu wakati huo nikiwa kwenye siasa, yeye alikuwa bado yuko chini, lakini naamini wote watakuwa tayari kuja kuiona nchi hii nzuri," aliahidi. 

Balozi Green kitaaluma ni mwanasheria aliyepata kujaribu kuwania ugavana wa jimbo la Wisconsin kupitia chama cha Republican mwaka juzi akapoteza.

Chanzo:Majira

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.