13 Aug 2016

14026664_162506520845816_426045486_n
Leo ni siku ya kuzaliwa ya mwana-hiphop mahiri na lejendari nchini Tanzania, Fareed Kubanda a.k.a Fid-Q. Na katika kuadhmisha birthday yake, msanii huyu ambaye sio tu amedumu "kwenye fani" kitambo bali pia ni miongoni mwa waasisi wa Swahili Hip-Hop.

 Kwangu, Fid-Q sio tu ni msanii maarufu kabisa huko nyumbani Tanzania na katika Swahii hip-hop duniani, bali ni mmoja wa watu ambao wamkuwa wakinipatia sapoti kubwa katika kazi zangu za uandishi wa vitabu. Na ndio maana kwa kutambua mchango wake huo, alikuwa mtu wa kwanza kupata nakala dhahiri ya kitabu changu kuhusu taaluma ya uafisa usalama wa taifa (ushushushu) kama inavyoonyesha pichani chini.

 Jana niliuliza huko kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuhusu wimbo gani wa Fid-Q unawavutia zaidi mashabiki wake. Jibu jepesi lilikuwa "kila wimbo wake unavutia." Nimesikiliza hii track mpya ya 'SUMU.' Imesheheni kauli nyingi za busara. Nitamwomba Fid-Q anitumie mashairi ya wimbo hu ili kuwaletea ninyi wasomaji uchambuzi zaidi ya wimbo huo. Lakini hata bila uchambuzi, kwa kuusikia tu, utaafikiana nami kuwa umeshehenu busara tele.

 Na hiki ndio kinachomfanya Fareed aendelee kuwa mmoja wa wasanii wachache na adimu kabisa Tanzania sio tu kuwa waasisi wa fani bali pia wasiochuja: kuwa na nyimbo zenye ujumbe usiochuja. Kama ingekuwa ni muziki wa bendi basi tungelinganisha na timeless tunes za kina Mbaraka Mwinshehe, Marijan Rajabu, Bitchuka, Shaban Dede, nk ambao tungo zao zilituvutia tangu tukiwa utotoni (kwa tulozaliwa enzi hizo) na ni tamu hadi leo. Na utamu so wa ladha tu bali pia relevance ya ujumbe uliomo. 

 Basi nisiandike 'gazeti,' bali nimtakie Fareed heri ya siku yake ya kuzaliwa, na kumtakia kila la heri na fanaka maishani, na kumshukuru kwa sapoti yake kwa kazi zangu, na kumpongeza kwa kutupatia 'SUMU.' Isikilize hapa chini

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube