Makala yangu katika toleo la wiki hii la gazeti la
Raia Mwema inazungumzia UHURU.Inaanza kwa kuhabarisha kuhusu tangazo la
Uhuru wa Kosovo,kisha inachambua "urafiki mpya" wa
Marekani na China kwa Bara la Afrika na kuhitimisha kwamba urafiki huo ni mithili ya
Mkutano wa Berlin 1884-5 ulioligawa bara la Afrika miongoni mwa wakoloni.Makala hii inakumbushia pia kwamba kuna uwezekano ziara ya
Bush barani Afrika ikabaki kumbukumbu muhimu kwake kutokana na namna alivyonyenyekewa katika kipindi ambacho ni mmoja ya marais wanaochukiwa sana katika sehemu mbalimbali duniani,na
very unpopular nyumbani kwake US of A.Kadhalika makala inawashikia bango
Mwanyika na
Hosea kwamba wajiuzulu haraka sana,sambamba na wale wote waliotajwa kwenye
ripoti ya Tume ya Mwakyembe.Pamoja na makala nyingine zilizokwenda shule ya hali ya juu,bingirika na makala hiyo kwa
KUBONYEZA HAPA.