Showing posts with label MUZIKI. Show all posts
Showing posts with label MUZIKI. Show all posts

4 Jul 2013Kutoka kushoto ni Paulyne Zongo, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Joan Matovolwa. 
Wanamuziki hao watatu na wakongwe nchini ndio wanaounda kundi hilo litakalojulikana kwa jina la NDEGE 3


Kundi la Ndege 3 linaloundwa na wanamuziki wakongwe katika Tasnia ya muziki wa dansi na kizazi kipya Joan matovolwa, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Paulyne Zongo, hivi karibuni limeshatoa kibao chake kinachokwenda kwa jina la 'MISUKOSUKO YA MAPENZI' ambacho redio kadhaa nchini zimeanza kukirusha.
MISUKOSUKO YA MAPENZI ni nyimbo ambayo imetungwa kwa umahiri wa hali ya juu, na kuonyesha viwango vya juu katika uimbaji na utunzi.
 
Kwa sasa Joan Matovolwa na Paulyne Zongo ni wanamuziki huru wakati Khadija Mnoga (Kimobitel) ni mwanamuziki anayeimba katika bendi ya Extra Bongo inayoongozwa na Camarade Ally Choki.

5 Mar 2012

Mahojiano mafupi na msanii Linah akizungumzia (japo kwa ufupi) kuhusu historia yake kimuziki, maendeleo katika muziki wa kizazi kipya na ziara yake hapa Marekani kwa mwaka 2012.


26 Feb 2012

Ifuatayo ni taarifa niliyotumiwa kutoka kundi la VINEGA kuhusu maafikiano yalifikiwa hivi karibuni kati ya Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (a.k.a SUGU) na mmoja wa Wakurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.Ninaomba kuiwasilisha kama ilivyo:


Tamko La Vinega Juu Ya Makubaliano Ya Sugu Na Ruge

23 Feb 2012


Chuck D,mwanzilishi na kiongozi wa lilikouwa kundi maarufu la rap huko Marekani,Public Enemy,aliwahi kusema muziki wa rap ndio CNN ya mtaa.Tangu awali,muziki wa rap umekuwa ukizungumzia masuala mbalimbali yanayoikabbili jamii-kutoka ukimwi,mihadarati,ubaguzi wa rangi hadi sera za ndani na za nje.Na sasa tunashuhudia baadhi ya wasanii wetu wakipata mwamko kama huo wa Public Enemy.Ushuhuda ni huu hapa chini.Sahau kidogo kuhusu video na sikiliza ujumbe kwa makiniCHANZO: Dj Choka's Blog

2 Nov 2011

4 Oct 2011


Karibu  Kona ya Mangoma"It's all about East African Flava"
Habari zenu wadau wote... Tunapenda kuchukua nafasi hii ya kipekee kabisa kuwakaribisha katika Libeneke jipya kabisa la KONA YA MANGOMA  Ambapo mtapata kutazama video mpya na nyenginezo nyingi kutoka pande zote Afrika Mashariki yani Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi..Pia tunaomba wasanii wote ambao mnatoa Video mtutumie link kupitia barua pepe hii ([email protected]) ili tuweze wape sapoti ya juu, Kwa pamoja tunaendeleza Muziki wa Afrika. Tunatanguliza Shukrani  zetu za dhati kwenu. Ukiona link hii mpe na mwenzako.


Jina la Blog: Kona ya Mangoma  

10 Sept 2011

 
 "Jinamizi la  Bongo Dansi" LINASUMBUA ULAYA !
 USO KWA USO NA WASHABIKI BREMEN CITY !
 
 
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU,
wanatarajiwa kutumbuiza katika onyesho kubwa la aina yake "AFRIKA MESSE"
mjini Bremen,nchini Ujerumani siku ya ijumaa 16-09-2011 majira ya alhasiri.
Bendi hiyo yenye tabia za kuwadatisha akili washabiki katika kila kona duniani na
mdundo wake "Bongo Dansi" made in Uswahilini.
 
Ngoma Africa band aka FFU imejikuta inapambanishwa tena uso kwa uso na washabiki
wengine katika mji wa Bremen,huko ujerumani Ughaibuni !ambapo maelfu ya washabiki
wamekaa mkao wa kula makombora ya muziki kutoka kwa bendi hiyo inayoongozwa na
kamanda Ras Makunja,bendi hiyo yenye utajiri wa wanamziki wenye vipaji wakiwemo
mwanadada Diva Bedi Beraca aka Princess Bedi Bella,pia yupo yule mcharaza solo
mahili Christian Bakotessa aka Chris-B,aka "Mshenzi wa Gitaa la solo" na wengineo,
Ngoma Africa band kwa sasa wanatamba na nyimbo zao "Supu ya Mawe" na
"Bongo Tambarare" zisikilize at www.ngoma-africa.com

5 Sept 2011

22 Aug 2011BENDI ya mziki ya msondo ngoma imepata TUZO ya the Best Rhumba Group katika East Africa Music Awards mashindano yariyofanyika Nairobi Kenya na kukusanyika kwa bendi za Afrika Mashariki na bendi ya msondo kuibuka Kidedea katika mashindano hayo akisibitisha ushindi uho meneja wa bendi Saidi KIbiriti alipokuwa akiongea na Msemaji wa Bendi hiyo, Rajabu Mhamila , Super D (pichani)

Alisema wameshinda tuzo hiyo na watahakikisha wanaionesha kwa mashabiki wa bendi hiyo ili kudhirisha kuwa bendi ipo ng'ang'ari popote duniani mana bendi imekamilika kila idara alisema Super D
(pichani)

Bendi hiyo itanza mazoezi siku ya jumatatu kwa ajili ya kujiandaa na sikukuu ya Iddi inayotarajia kufanyika wiki ijayo ambapo wanaingia kambini kusuka vibao vipya ikiwemo na kuvifanyia kazi vile vya Zamani

Super D alisema bendi hiyo siku ya Iddi Mosi itapiga katika viwanja vya TTC Chang'ombe ambapo mashabiki watapata kuona tuzo hiyo ya Afrika Mashariki walioitwaa hivi karibuni na kupata fursa ya kupiga nayo picha katika viwanja hivyo

Bendi hiyo inayotamba na vibao vyake vipya vya Suluu uliotungwa na Shabani Dede na Nadhili ya Mapenzi uliotungwa na Juma Katundu

Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times [email protected] www.burudan.blogspot.com
 Mob;+255787 406930
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

18 Jun 2006

KULIKONI UGHAIBUNI:

Asalam aleykum wasomaji wapendwa wa gazeti hili.

Leo tuzungumzie muziki.Muda mfupi uliopita nilikuwa nasoma makala flani kumhusu msanii wa kizazi kipya Albert Mangwea.Yalikuwa ni mahojiano kati ya msaanii huyo na tovuti ya Darhotwire.com.Niliguswa sana na kilio cha msanii huyo ambacho kimekuwa pia kikisikika kutoka kwa takribani kila msanii wa Bongofleva.Kuna wajanja flani,(hapana,hawa si wajanja,bali ni WEZI) ambao wamekuwa wakiwanyonya vijana wetu bila hata chembe ya huruma.Wezi hawa wanafahamika zaidi kwa jina la “wadosi”.Binafsi sijui kwanini wanaitwa wadosi lakini la muhimu hawa sio jina wanaloitwa bali unyonyaji wanaowafanyia wasanii wetu.

Pengine kabla ya kujadili wizi wa mchana mweupe unaofanywa na wadosi hao,tuangalie maendeleo ya Bongofleva huko nyumbani na huku Ughaibuni.Mimi ni mfuatiliaji sana wa mambo yanayotokea huko Bongo. “Ibada” yangu ya kila asubuhi inaanza kwa kutembelea tovuti za ki-Tanzania ili kujua yanayojiri huko.Sasa,kabla ya kuja huko mwaka jana mwishoni mwa mwaka jana nilikuwa nahisi kuwa habari kwamba Bongofleva imeikamata Tanzania kwa “kasi ya tsunami” ni porojo tu.Lakini nilipokuja nilishihudia mwenyewe jinsi gani hatimaye nyimbo zinazotengenezwa na kuimbwa na Watanzania zilivyokamata soko na mioyo ya wapenzi wa muziki.Wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu nilibahatika kushuhudia tamasha la “Piga Kura au Upigike” kwenye viwanja vya Biafra Kinondoni.Licha ya picha kadhaa nilizochukua kwa ajili ya kuwajulisha marafiki zangu hapa,nilijionea jinsi gani watu wa rika mbalimbali wanavyovutiwa na kazi za wasanii wa muziki wa kizazi kipya.Nadiriki kuamini kuwa mashabiki waliofika viwanja hivyo walikuwa wanawakilisha karibu kila kona ya jiji la Dar es Salaam.Kitu kingine nilichobaini ni kwamba jinsi gani wasanii wanavyotumika katika masuala ya muhiu kwa Taifa.

Nakumbuka niliwahi kusoma katika gazeti moja la huko nyumbani kwamba msanii Juma Nature “alimfunika” mwenyeji wake-mgombea aliyemwalika msanii huyo katika kampeni zake.Yaani watu walikuwa na kiu zaidi ya kusikia muziki wa Nature kuliko hotuba ya mheshimiwa huyo.Na pengine umati kubwa uliojitokeza kwenye mkutano huo ulifuata buridani hiyo ya bure.Yayumkinika kusema kuwa mchango wa wasanii katika kufanikisha uchaguzi,na hata kuwapatia ushindi baadhi ya wagombea,ulikuwa mkubwa.Kwa bahati mbaya,au pengine kwa makusudi,baada ya kukamilisha kazi ya kuhamasisha jamii kuhusu uchaguzi na wagombea,wasanii wetu wamerudi kulekule walikokuwa:wamesahauliwa na wanaendelea kunyonywa.

Napenda kuwafumbua macho wasanii wetu kwa kuwaambia kuwa muziki wao huku guhaibuni unauzika sana miongoni mwa watu waliotoka Afrika Mashariki.Wamuulize Banana Zorro aliyealikwa hapo London kwenye pati ya Muungano,wamuulize Mr Nice,Ray C na TID,na Profesa J ambaye nasikia amewachengua vilivyo huko Sweden na Holland.Wasanii wa nyumbani wakija huku wanababaikiwa kama vile akina Shaggy au Sean Paul wanavyobabaikiwa wakija huko nyumbani.Lakini,safari za nje sio jambo la kukurupuka tu,ni kitu kinachotaka maandalizi.Kwa mantiki hiyo si lazima kusafiri ili kunufaika na kazi za sanaa bali hata kutafuta namna ya kupenyeza muziki katika soko la kimataifa kunaweza sana kuwainua wasanii wetu.Hivi wasanii wetu wanajua kuwa CD zao huku zinauzwa hadi paundi 10 (zaidi ya shs 24,000/=)?Nimesoma kwenye internet kwamba tarehe 12/06/2006 kampuni moja iitwayo Townsend Records itatoa CD iitwayo Bongoflava (Swahili Rap from Tanzania) ambayo itauzwa paundi 10.99 (takriban shs 27,000/= kwa exchange rate za leo).Sijui kama na hawa ni wadosi au la,lakini huo ni uthibitisho kuwa Bongoflava ina soko zuri tu kuhu Ughaibuni.Na watu wanapenda kweli kazi za wasanii wa nyumbani.Niliporudi kutoka Tanzania jamaa zangu kibao walikuwa wananiulizia kama nimekuja na CD za Bongofleva.Kila mmoja anasema wanaposikia wasanii wetu wanakumbuka sana nyumbani.

Mheshimiwa Kikwete alinukuliwa akiwataka Watanzania walioko nje kuwasaidia wenzao walio nyumbani hasa katika nafasi za masomo.Ujumbe huo unaweza pia kupanuliwa na kuwahusisha wasanii wa nyumbani,kwa maana kuwa Watanzania walio nje hasa wale wenye upeo na mambo ya muziki wawasaidie wasanii wetu wa nyumbani kwa namna yoyote ile inayowezekana.Lakini ili hilo liwezekane wasanii wetu hawana budi “kuchangamka.”Wanaoitwa “wadosi” wanawanyonya na kuwaibia kwa vile wanajua dhahiri kuwa wasanii hao hawana njia mbadala.Jamani,dunia siku hizi imekuwa kama kijiji (japo ni kinadharia) na unachohitaji ni kwenda tu kwenye internet cafĂ© na kuperuza kurasa za mtandao kujua wapi unaweza kupata huduma au kuuza ulichonacho kwa mtu aliye bara jingine.Hapa ndipo umuhimu wa shule (elimu) unapojidhihirisha.Lakini hata kama shule haipandi,si unaweza kumwomba rafiki yako akusaidie kutafuta soko la kazi zako za sanaa nje ya nchi?

Serikali inapaswa kuwasaidia wasanii wetu kwa kuipa meno sheria ya hatimiliki.Sambamba na hilo ni wasanii wenyewe kusimama kidete kutetea maslahi yao badala ya kuendelea kulalamika au kufikiria kuingia kwenye fani nyingine kukwepa wizi wa kazi zao.Pia wasione aibu kuomba msaada kwa wenzao walio nje.Mwisho naiomba serikali ipanue vita dhidi ya wala rushwa na majambazi na kujumuisha “wadosi” pia.

Alamsiki

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.