Nani kasema Breaking News lazima iwe ya CNN,BBC,AL-Jazeera,etc pekee?Hii ni live and direct from Ifakara:maji katika mto Lumemo yamevunja kingo za mto huo dakika chache zilizopita na hivi sasa yanakuja kwa kasi huku mjini-kati.Wazoefu wananiambia nikisubiri ili nipate picha za kuweka hapa bloguni basi si ajabu huko Scotland likarudi jina tu na hii blog ikaishia kufa kifo cha asili (bloga akisombwa na mafuriko si inamaanisha blogu nayo imekufa,au sio?).Hayo mambo ya kuwa embedded na jeshi huko Comoro wanayaweza wenyewe lakini sidhani if it's a healthy idea kuwa embedded na mafuriko.Let me pack my things and run,guys.I can smell death in the air!Run blogger,run!
15 Apr 2008
15.4.08
Evarist Chahali
IFAKARA, TAZARA, VACATION PICS
No comments
MASHABIKI WA SOKA WA IFAKARA WAKIFUATILIA MECHI KATI YA TAIFA STARS NA HARAMBEE STARS YA KENYA
HUYU NYAU ANAJARIBU KU-GOOGLE NENO "UFISADI"
UFISADI KUTOKA CHINA: HII NI PIRACY YA DARAJA LA KWANZA (ZAIDI YA LILE LA TAZARA).MOVIES TAKRIBAN 40 ZIMELUNDIKWA KWENYE DISC MOJA.BEI MAELEWANO.HI SAMPLE NILINUNUA KWA SHS 5000.NAOMBA KUSISITIZA KUWA NILINUNUA ITEM HII KWA AJILI YA KUKUONYESHA WEWE MSOMAJI WA BLOG HII,NA SIO KUWANUFAISHA MAFISADI.TRUST ME!
UFISADI,CHINESE STYLE
HIVI UNAWEZA KU-GUESS HAPO NI WAPI?I DONT THINK SO.NI RAHISI ZAIDI KU-EXTRACT DAMU KUTOKA KWENYE JIWE KULIKO KUPATA JIBU SAHIHI KWENYE KIJISWALI HIKI.ANYWAY,HAPO NI KWENYE PLATFORM YA KUONDOKEA,STESHENI KUU YA TAZARA DAR ES SALAAM,NA HILO DUDE KULIA NDIO TRENI LA KWENDA ZAMBIA.MWANGA HAPO NI HAFIFU ZAIDI YA ZILE DISCO LIGHTS ZA KIZAMANI.NDANI YA HILO DUDE LIITWALO TRENI NI ADHABU FROM THE MOMENT UNAINGIA TILL UPOTEREMKA UENDAKO ("KUTEREMKA" IS A POLITE WORD,"KURUKA" WOULD BE MORE PRECISE)
ANGALIA KWA MAKINI "TAIFA LA KESHO" (WATOTO) WAKIFUATILIA MECHI YA TIMU YETU YA TAIFA HUKUWAKIWA WAMEKAA CHINI.HAPA NI IFAKARA.RUNINGA ZIPO MADUKANI LAKINI NI AFFORDABLE KWA WATU WACHACHE.UNYANYASAJI WA WATOTO HAPA NYUMBANI UNAPASWA KUTANGAZA JANGA LA KITAIFA.NOBODY SEEMS TO CARE JAPO KUNA WIZARA INAYOHUSIKA NA MASUALA HAYA.NA HAKUNA SEHEMU NZURI YA KUPIMA POROJO ZAMAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA KAMA HUKU UPCOUNTRY.MORE PICS LATER,STAY TUNED!
10 Apr 2008
10.4.08
Evarist Chahali
HUDUMA, MAKALA, RAIA MWEMA, TANZANIA
No comments
Huduma za afya hapa nyumbani ni duni na hazileti matumaini ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania (by the way,tangu nifike hapa sijaona ile hamasa niliyoikuta 2005 kuhusiana na kauli-mbiu hiyo.Sijui imekufa kifo cha asili au imepotea kama Gavana Daudi Ballali!).Hospitali za umma zinaweza kujitetea kuhusu huduma zao mbovu,na utetezi unaweza kuwa ule uliozoeleka:serikali haitengi fungu la kutosha kwenye sekta ya afya,mishahara ya watumishi ni midogo,na mlolongo wa sababu ambapo mlengwa mkuu ni serikali.Lakini haitarajiwi hospitali binafsi,ambazo gharama zake ni za juu sana,zitoe huduma ya chini ya kiwango.Nimeelezea kwa kirefu kuhusu suala hilo katika makala yangu ndani ya toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema.Pamoja na makala nyingine na habari motomoto,bingirika na vyote hivyo kwa KUBONYEZA HAPA6 Apr 2008
Pata burudani ya picha zaidi kutoka Bongo
Wakati unasubiri batch nyingine ya picha kutoka hapa,hebu pata burudani kutoka kwa Common featuring Dwelle katika track ya The People
Kempinski kwa ndani,kwa hakika wanastahili pongezi kwa namna palivyoboreshwa.
Msikiti wa Kichangani Magomeni.Jirani na msikiti huuu,kuna makutano ya barabara za Morogoro na Kawawa.Eneo hilo ni maarufu sana kwa vibaka wababe wanaopora madereva.Ni zaidi ya kosa la jinai kusimamisha gari eneo hilo huku kioo kikiwa chini au nusu.


Kasi ya majengo mapya ni kubwa katika maeneo mengi ya Dar.Hata hivyo,wananchi wengi wanalalamika kuwa hali ya maisha inazidi kuwa ngumu.
Sehemu hii inapendeza.Kwa muda nilijiskia kama niko Scotland vile.Hapa ni Kilimanjaro Hotel Kempinski.


Kempinski
Hakuna sheria muhimu ya uendeshaji gari mitaa ya Kariakoo zaidi ya ubabe.Ukifuata taratibu za usalama barabarani utaishia kugongwa,kuporwa au kulala hapohapo.


Msikiti wa Kichangani Magomeni
Millennium Towers.Eneo hili kuna internet cafe ambayo ni kimbilio la wengi wanaotegemea wireless connection.Pia ni mahala unapoweza kugongana na jamaa mbalimbali mliopoteana kutokana na kwenda nje kusaka hili au lile


Hii joint inaitwa "SAMAKI SAMAKI".The name tells it all...it's all about fish,fish and even more fish...Jana tulipewa ofa ya bure ya dagaa wa kukaanga.Yaani.... ndio mambo ya home sweet home hayo!However,dont let these nice pics fool you,mapambano ya maisha hapa yanataka ujasiri...na ukiwa jijini hapa inaweza kuwa rahisi kufahamu kwanini UFISADI unashamiri.The going seems to be getting tougher and tougher,forcing some folks to try to make the tough get going.


Mitaa ya Kariakoo
Wakati unasubiri batch nyingine ya picha kutoka hapa,hebu pata burudani kutoka kwa Common featuring Dwelle katika track ya The People
5 Apr 2008
Zoezi la kuleta picha za Bongo linaendelea.I'm not trying to become a photoblogger of some sort,hiyo wanaiweza magwiji WA FANI kama rafiki yangu HAKI.Hapa chini kuna kiji-collection kidogo ca picha nilizodhani zinaweza kukupendeza wewe msomaji. Zote zimepigwa kwa kutumia Samsung Armani,na naamini quality ya picha inaridhisha.If not,let me know,plz!


Foleni za magari bado ni tatizo sugu kama Ufisadi.Hapa ni junction ya maeneo ya Namanga.Halafu jana kulikuwa na mvua si utani.Breaking news niliyopata jana mchana ni kuwa maji yalikuwa yanalazimisha kuingia ndani ya "mansion yetu" huko Ifakara (well,kwa level ya kijiji chetu,nyumba ikipigwa lipu nje,na vikorombwezo flani na geti la kizushi basi inapata hadhi ya kuitwa "mansion")


Hapa ni HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI.Jana nayo ilikuwa imeelemewa na maji.Tatizo la Hospitali hii ni kwamba mazingira ya nje hayaridhishi,ya ndani ni ya kusikitisha na huduma ndani ni za kuvunja moyo. It's like a hospital from hell.
Niliamua kuwanasa kwa picha hawa wageni waliokuwa wanafanya nini sijui hapo Mbuyuni,barabara ya Ali Hassan Mwinyi.Lilikuwa sio kundi kubwa as such lakini kama ujuavyo Bongo hakuna jambo dogo,muda si muda kukawa na lundo la watu wanawashangaa hao jamaa...I could swear I saw someone cancelling his trip to work just ku-join the party ya kushangaa... More pics hapo chini


STAY TUNED FOR MORE PICS.
2 Apr 2008
Dar kuna tatizo kubwa sana la foleni.Na kwa kasi magari yanayoingizwa kila siku jijini hapa,nadhani kimeo cha foleni kitaebndelea kwa muda mrefu sana.Na inavyoonekana,hakuna mipango ya kuboresha barabara ili ziweze kumudu wingi wa magari.Sijui quality ya picha hizi ikoje.Ni majaribio ya Samsung Armani kwenye poor light (mida ya saa 12).Location ni Millennium Towers.Will keep on bringing more pics for you guys.




31 Mar 2008
31.3.08
Evarist Chahali
No comments
KWA MUDA SASA BLOGU HII IMEKUWA KIMYA.HIYO NI KUTOKANA NA SAFARI YA KUJA HAPA NYUMBANI BONGO.LIBENEKE LITAENDELEA PINDI MAMBO YAKISHATULIA.WILL DO MY BEST TO KEEP YOU GUYS POSTED ABOUT WHAT'S HAPPENING KIPANDE HII
23 Mar 2008
23.3.08
Evarist Chahali
PASAKA
No comments
Wakati tunasherehekea sikukuu ya Pasaka ni vema tukifanya tafakuri ya mambo ambayo machoni yanaweza kuonekana madogo lakini yenye uzito mkubwa katika hali halisi.Ni muhimu kumshukuru Mungu kwa mengi au machache aliyo/anayotujalia.Hivi kuna zawadi kubwa kutoka kwa Mungu zaidi ya UHAI?Sambamba na uhai ni uzima/ukamili wa miili yetu.Tuliozaliwa tukiwa kamili (yaani bila ulemavu) tunaweza kujisahau kuuliza maswali magumu kama "ingekuwa vipi kama ningezaliwa nina mkono nusu,au pua iliyozama ndani,au hata jicho lililokaa kisogoni" hadi pale tunapowaona wenzetu kama huyu mtu-tembo (elephant man-sio yule wa dancehall),ambaye stori yake inapatikana HAPA22 Mar 2008
22.3.08
Evarist Chahali
PASAKA
No comments
NAWATAKIENI NYOTE HERI NA BARAKA ZA SIKUKUU YA PASAKA.UFUFUKO WA BWANA YESU KRISTO ULETE AMANI,UPENDO,AFYA NJEMA NA MAFANIKIO KWA KILA MMOJA WETU.PAMOJA NA SALAMU HIZI NI SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWENU NYOTE MNAOTEMBELEA BLOGU HII NA KUSOMA MAKALA ZINAZOTOKA KATIKA BAADHI YA MAGAZETI YA NYUMBANI.BWANA AWABARIKI SANA,AMEEN.
Jana nilishuhudia kituko cha mwaka.Mwanzoni nilidhani ni porojo tu lakini asubuhi hii nimeona tukio hilo limekuwa gumzo mtandaoni.Ilikuwa takriban saa 6 mchana za hapa (hapa saa zitabadilika mwishoni mwa mwezi huu),nikaamua kupoteza muda kwa kuangalia kipindi cha Fox&Friends.Nasema kupoteza muda kwa vile waendesha kipindi hicho huwa wananikera sana kutokana na kauli zao za upendeleo wa wazi kwa wahafidhina na upinzani wao mkubwa dhidi ya Democrats na liberals.Sikujutia uamuzi wa "kupoteza muda" kwani huku watangazaji Steve Doocy na Gretchen Carlson wakishikia bango kauli ya Obama kwamba grandmom wake ni like typical White person,mwenzao Brian Kilmeade aliamua kuondoka kwa muda studioni kutokana na kukerwa na namna wenzie walivyokuwa wakimsakama Obama.Kama hiyo haitoshi,muda mfupi baadaye,mtangazaji mwandamizi wa kituo hicho,Chris Wallace,alionekana hewani wakati Fox&Friends inaendelea ambapo alielezea waziwazi kwamba alikuwa akiangalia kipindi hicho na hakupendezwa na namna kauli ya Obama kuhusu bibi yake ilivyokuwa ikipotoshwa.Wallace alieleza wazi kwamba yeye si msemaji wa kambi ya Obama lakini angependa kuona kipindi hicho kinazungumzia suala hilo ndani ya context,na kwenda mbali zaidi kwa kuwashauri wana-Fox&Friends kuangalia pia habari nyingine za muhimu kuhusu Obama kama vile endorsement ya Bill Richardson na hotuba zake mbili kuhusu uchumi na vita ya Irak.
Subscribe to:
Posts (Atom)












