9 Aug 2011
8 Aug 2011
8.8.11
Evarist Chahali
Big Boi, Outkast
No comments
Patton, half of the platinum-selling, Grammy-winning group Outkast, was charged with three counts of possession of a controlled substance and one count of possession of drug paraphernalia — all felony charges, according to the Miami-Dade County Corrections Department website.
The 36-year-old was caught by drug-sniffing dogs while getting off a cruise ship.
Patton was carrying Viagra, which he didn’t have a prescription for, Ecstasy pills and MDMA powder, the main ingredient in Ecstasy.
"While Big Boi was traveling with his group and friends, a small amount of contraband was found in the collective luggage," the rapper's attorney Daniel Kane said in a statement. "I am confident when the entire facts are aired Big Boi will be completely exonerated."
He's being held on a $16,000 bond at the Pre-Trial Detention Center in Miami.
SOURCE: Los Angeles Times
8.8.11
Evarist Chahali
Tangazo
No comments
|
CHANZO: Daily Mail
CHANZO: Daily Mail
7 Aug 2011
7.8.11
Evarist Chahali
Didas Masaburi, UDA, UFISADI
1 comment
![]() |
Picha kwa hisani ya Je Unajua Hii |
Masaburi awatusi wabunge
• ATISHIA KULIPUA UFISADI WAO HADHARANI
na Ramadhani Siwayombe, Arusha
MEYA wa jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi, ambaye ametakiwa na wabunge wa jiji la Dar es Salaam kujiuzulu kupisha uchunguzi kutokana na kashfa ya uuzaji kifisadi Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam (UDA), amewajibu wabunge hao na kusema kuwa kuna baadhi yao wanashindwa kufikiri kwa kutumia vichwa na badala yake wanafikiri kwa kutumia 'makalio'.
Masaburi alitoa kauli hiyo nzito jana mjini hapa alipozungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Naura Spring ambapo anahudhuria mkutano wa pamoja wa kamati za uongozi za serikali za mitaa za nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EACLAT).
Alisema wabunge katika kuchangia hoja ya suala la UDA wamegawanyika katika mafungu matatu ambao alisema katika mafungu hayo moja halijui lolote kuhusiana na sakata hilo na limedandia tu hoja na kuwataja miongoni mwao ni mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi, na mbunge wa Mafia, Abdukarim Shah.
Alitaja kundi la pili kuwa ni la wabunge wa jiji la Dar es Salaam ambao ni mbunge wa Ubungo, John Mnyika, na mbunge wa Kawe, Halima Mdee, ambao alisema wanatafuta umaarufu wa kisiasa kupitia sakata la UDA.
Alisema Mnyika aliweza kuhoji hata katika vikao rasmi, lakini Mdee hajui chochote kwa kuwa hajawahi kuhudhuria vikao vya jiji mpaka sasa.
Aidha, kundi la tatu ambalo ndilo alilituhumu zaidi kufikiri kwa kutumia makalio badala ya kichwa ni la wabunge Abasi Mtemvu (Temeke), Musa Azzan 'Zungu'(Ilala) na Makongoro Mahanga (Segerea) ambao alidai kuwa wanajua ukweli wa jambo hilo lakini wanapotosha ili kuficha madhambi yao ambayo alisema yataibuliwa muda si mrefu ya ufisadi ndani ya jiji hilo.
"Hawa wabunge ambao wana nyadhifa toka kipindi kilichopita ndio wanaohusika na kulifilisi shirika hilo na mashirika mengine ya jiji kwa kuwa mchakato wa kuuzwa kwa shirika hilo ulianza toka mwaka 2008 ambapo mimi nilikuwa hata sijawa diwani," alisema Masaburi.
Alieleza kuwa toka kipindi hicho kwa mujibu wa madokezo yaliyopo kuhusiana na uuzwaji wa shirika hilo, yanaonyesha maamuzi yalipitishwa na vikao halali hadi kuuzwa kwake mapema mwaka huu ambapo yeye hajashiriki kwa lolote mpaka wanauziana.
"Mimi ndiye niliyeibua hii tuhuma ya kuuzwa kwa UDA wakati nikihoji mali zinazomilikiwa na jiji na kuambiwa UDA imeishauzwa; nilipofuatilia nikakuta imeuzwa shilingi milioni 285! Nilipofuatilia hizo fedha kama zipo nikakuta milioni 200 zimeshaliwa; nikaamua kumsimamisha meneja wa shirika hilo na mhasibu. Sasa leo nageuziwa kibao kuwa mimi ndiye nimeuza inashangaza sana!" alisema Masaburi.
Aliendelea kusema wabunge hao wanang'ang'ania ajiuzulu kutokana na hofu iliyotanda baada ya kuanza kazi ya kuibua ufisadi ndani ya jiji hilo kwa kuanzia na UDA.
"Baada ya kuibua ufisadi UDA sasa nimepanga nihamie shirika la DDC ambako Mtemvu ni mwenyekiti wa bodi; shirika ambalo nalo kuna ufisadi mkubwa umefanyika ikiwemo kuuza mashamba ya shirika hilo na baadhi ya nyumba," alisema.
Alisema akimaliza suala hilo atahamia kuhakiki matumizi ya ujenzi wa Machinga Complex ambapo alidai inashangaza kusikia zimetumika bilioni 1.2 kujenga zile nyavu za vizimba ambavyo alifananisha na nyumba za wanyama wafugwao.
Alisema kutokana na mkakati wake huo anaomba wabunge wampe muda wa kutekeleza hayo.
Masaburi alisema hawezi kujiuzulu kwa shinikizo la mafisadi na kudai endapo akifuatilia mashirika yote hayo na kubaini yapo sahihi yuko radhi kujiuzulu kama itahitajika.
"Naomba wanipe muda kidogo nisafishe ufisadi ndani ya jiji la Dar es Salaam kutokana na mikataba ya ajabu iliyoingiwa baina ya viongozi waliokuwepo madarakani kipindi cha nyuma wakishirikiana na wabunge na kulitia umaskini jiji ili kama kuna hoja za msingi wabunge wapate hoja za kujadili bungeni," alijinasibu Masaburi.
Alifafanua kuwa kuhusu suala la malipo ya mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo, Iddi Simba, kutoka kwa wanunuzi wa shirika hilo yeye hatambui kwa kuwa hakuna risiti yoyote ya UDA inayoonyesha malipo hayo.
Aliongeza kuwa hata baada ya yeye kupata barua za kuwepo kwa malipo ya sh milioni 320 zilizofanywa kupitia akaunti ya Iddi Simba alimfuata mwenyekiti huyo na kuhojiana naye na alikiri kupokea malipo hayo, lakini alisema hayahusiani na mauzo ya UDA na kusema yanahusiana na biashara zao binafsi.
Alisema kutokana na majibu hayo ya Iddi Simba hakuwa na mamlaka ya kung'ang'ania kuwa malipo hayo ni sehemu ya malipo ya UDA hivyo vyombo kama Takukuru ndio nafasi yao ya kuchunguza suala hilo.
Akizungumzia tamko la Waziri Mkuu kuviagiza vyombo vya Takukuru, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na ofisi ya DCI kushughulikia suala hilo, aliunga mkono uamuzi huo kwani ndio utabainisha wazi wote waliohusika katika kuliuza shirika hilo.
Sakata la kuuzwa kwa UDA lilichukua nafasi katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Uchukuzi ambapo ilifikia wakati wabunge kutishia kutoipitisha bajeti hiyo na kutaka wote waliohusika katika uuzaji wa shirika hilo wawajibishwe ikiwemo Masaburi kwamba ajiuzulu kabla ya Waziri Mkuu kuingilia kati na kuunda tume kuchunguza suala hilo.
CHANZO: Tanzania Daima
6 Aug 2011
Nimekutana nayo huko Jamii Forums.Habari hii imenikumbusha mbinu iliyotumiwa na utawala wa mkoloni kuendeleza utawala wake dhalimu.Wakoloni walitugawanya kwa misingi mbalimbali,hususan rangi,na kwa kiasi kikubwa walifanikiwa kuchelewesha jithada za ukombozi wetu.Lakini kama zilivyo mbinu nyingine za ujanja ujanja,mbinu hiyo haikuweza kudumu milele.Kwa hakika hakuna mbinu yoyote inayoweza kuzuwia kiu ya mwanadamu kuleta mabadiliko bora kwake.
Kinachonisikitisha katika habari hii ni namna baadhi ya wanablogu wenzetu wanavyokubali kuuza utu wao (na kuwasaliti mamilioni ya walalahoi) kwa ajili tu ya maslahi binafsi.Wosia wangu kwao ni mwepesi tu: waangalie namna CCM ilivyowatumia wanahabari katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010,na mara baada ya Wanamtandao kufanikiwa kumwingiza Kikwete Ikulu wakawatosa wengi wa wanahabari hao.Kuna wanahabari walibembelezwa kuacha vibarua vyao nje ya nchi,wakawatumikia wanamtandao na baada ya umuhimu wao kwisha,wakatoswa.Ni vema mabloga walioingia mkenge huu wakatambua kuwa nafasi yao walionayo ni mhimili wa nne wa dola.Lakini la muhimu zaidi,wakae wakielewa kuwa,ashakum si matusi watatumika kama kondomu: MUHIMU SANA KABLA NA WAKATI WA TENDO LA NDOA LAKINI HUONEKANA UCHAFU USIOVUMILIKA BAADA YA TENDO HILO.
Soma habari husika hapa chini
CCM yaanzisha Mtandao wa Friendly Media to CCM
Wana JfCHANZO: Jamii Forums
JK: Nawajua wala rushwa kwa majina | |
By Richard Williams | Published 02/22/2006 | Habari za Kitaifa |Rating:![]() ![]() ![]() ![]() ![]() | |
Richard Williams .Asema tabasamu lake lisipotoshe watu .Maamuzi yake si nguvu ya soda RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amesema anawajua kwa majina wala rushwa katika wizara na kwamba nguvu anayokwenda nayo siyo ya soda. Alikuwa akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika jana katika uwanja wa michezo wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga, mkutano ambao lengo lake lilikuwa ni kuwashukuru wananchi wa mkoa huo kwa ushindi wa kishindo waliompatia yeye na Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa Desemba 14, mwaka jana. Rais Kikwete ambaye mkoa wa Rukwa ulikuwa ni wa nne katika ziara zake za kuwashukuru wananchi, amesisitiza kwamba kauli mbalimbali ambazo amekuwa akizitoa katika ziara zake za kutembelea wizara mbalimbali na idara za serikali ni kauli ambazo hazitoi kwa kutania, bali ni kauli za mambo anayoyafahamu vyema na kwamba mengine ameyaweka akiba. "Sizungumzi kwa utani nayajua ninayoyasema. Nilichoweka akiba ni kuwataja watu kwa majina, wasidhani nikienda wizarani nikasema watu hawa wanakula rushwa wasidhani siwajui kwa majina, ninawajua, bali kwa sasa ninatoa muda kwa watu hao wajisahihishe. Mwenye masikio nadhani atakuwa amesikia," alisisitiza. Katika mazungumzo yake na wananchi hao ambayo mara kwa mara yalikuwa yakikatishwa na vigelegele na nderemo; Rais alirudia tena kauli yake kwamba Mwenyezi Mungu amemuumba akiwa na sura ya tabasamu jambo alilosema kuwa hawezi kulibadili, lakini tabasamu hilo lisiwapotoshe watu, kwani yanapokuja mambo ya msingi huwa hana mchezo na mtu. Alisisitiza kuwa kila kiongozi katika nafasi wajibu wake ni kuwatumikia wananchi na kwamba wananchi wanayo haki ya kupata huduma kutoka kwa kiongozi huyo. "Ikifika mahali Mtanzania akitaka huduma kutoka kwa mtumishi wa serikali anayelipwa mshahara, basi ni lazima kwanza kabla ya kupewa huduma hiyo, amlipe mtumishi yule, tukifika huko basi huo ni ukiukwaji wa maadili ya kazi na mtu kama huyo hastahili kuwa mtumishi wa umma. "Tumejipanga vizuri ndani ya serikali katika kuwatumikia wananchi, na hii siyo nguvu ya soda, ukisimama mbele yetu utasukumwa," alisema na kushangiliwa na wananchi. Rais amebainisha kuwa wale watumishi ambao wamekuwa wakidhani kuwa kutokana na unyeti wa taaluma zao basi hata wakinyanyasa wananchi hawataondolewa katika nafasi zao, wakidhani hivyo wanajidangaya. "Anayedhani kuwa ataendelea kuharibu kwa sababu katika taaluma yake itachukua muda kuwafundisha watu wengine, anajidanyaganya, tuko tayari kuanza upya. Bora tabu kuliko kuwa na mtu wa aina hiyo ambaye badala ya kuwatumikia wananchi yeye anawatesa," alisema. Alisema maamuzi mbalimbali ambayo serikali inayachukua hivi sasa na hapo baadaye yanalenga katika kuurejesha utumishi wa umma katika mstari ulionyooka na kwa sababu hiyo amewataka watumishi wa serikali kuu na serikali za mitaa kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia maadili ya kazi na viapo walivyokula Alisema mfanyakazi atakayetekeleza kazi zake kwa kuzingatia maadili ya kazi yake, hata nishani anaweze kupewa na serikali, lakini kwa yule ambaye atafanya kinyume chake serikali haitakuwa na muda naye. "Hatuna ugomvi na mtu wala hatuna chuki na mtu, tunachotaka kutoka kwako ni utumishi wako uliotukuka kama ulivyoapa kufanya kazi kwa kuzingiatia maadili," alisisitiza Rais na kuufanya umati wa wananchi wa Sumbawanga kumshangilia. Alisema kuwa anachotoa ni ilani na kukumbushana kama gari lilikuwa linapita kwenye majani, basi sasa lirejee barabarani ili kule lilikokuwa linapita lisije kuwakanyaga watu. Kikwete alisema uwajibikaji huo wa watumishi wa serikali kuu na mitaa unawahusu vilevile wakuu wa mikoa ambao tayari alishazungumza nao, na atarudia tena kwa wakuu wa wilaya na wakuregenzi wakati atakapokutana nao mara baada ya kukamilisha kazi ya kuwateua. Akiwashukuru wananchi wa mkoa huo kwa kumpatia ushindi wa asilimia 86, Rais alisema kuwa ahadi ya serikali ya kuwajengea barabara ya lami kutoka Sumbawanga hadi Tunduma, iko palepale na kwamba kazi ya uchoraji imekwisha kamilika na zabuni za kutafuta kandarasi ili kazi ianze inaendelea. Kuhusu mvua zinazoendelea kunyesha katika mkoa huo, Rais amewaomba wananchi hao kuzitumia vizuri ili waweze kuzalisha chakula cha kuwatosha wao na ziada itumike kuwalisha Watanzania wengine ambao mikoa yao imekosa mvua. Rais Kikwete alishindwa kuhutubia jana mjini Iringa kwa sababu ya mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na radi na hivyo atahutubia leo na baadaye atakwenda kutembelea mabwawa yanayotoa umeme ya Kihansi na Mtera. Mikoa ya Rukwa na Mbeya ambayo hivi sasa mvua zinanyesha, ingawa zilichelewa kuanza, hali ya mashamba na mazao ni ya kuridhisha hali inayoashiria kuwa kama mvua hizo zinataendelea basi kuna uhakika wa kupata chakula kwa wingi. Mkoa wa Rukwa hauna matatizo ya njaa isipokuwa katika wilaya ya Mpanda ambako bei ya mahindi imepanda hadi kufikia sh. 10,000 kwa debe, kupanda kwa bei huko kumetoka na wananchi wa maeneo hayo kuuza kwa wingi mahindi yao za ziada katika nchi jirani ambako kuna njaa. Mkoa huo wa Rukwa unatarajia kuzalisha tani milioni 1.2 za mahindi wakati mahitaji halisi ya mkoa ni tani 500,000. ISSN 0876-3896 NA.19240 Na Maura Mwingira, Sumbawanga |
HABARI HII ILICHAPIHSWA KWENYE MTANDAO WA HABARI TANZANIA
Kwanza nitoe ufafanuzi wa neno "Dola ya Kiusalama", ambalo ni tafsiri yangu isiyo rasmi ya security state.Kwa kifupi,dola ya kiusalama inaruhusu bughudha na unyanyasaji kwa wananchi wasio na hatia kwa kisingizio cha maslahi ya usalama wa taifa.
Kwa makusudi,Tanzania yetu inaelekea kurejeshwa kwenye zama hizo za wanausalama kupewa ruhusa ya kumbughudhi mwananchi yoyote yule kwa kisingizio cha "kusaka taarifa za kiusalama." Of course,sheria za nchi zinavipatia mamlaka vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wao katika namna inavyoweza kutafsiriwa kama unyanyasaji wa wananchi,lakini hilo si tatizo kubwa iwapo uchunguzi huo unafanyika kwa maslahi ya umma.
Taarifa nilizonazo ni kwamba wanausalama wetu wameanza kuwasumbua baadhi ya wananchi wasio na hatia wakishinikiza kufahamu "chanzo cha tetesi za ufisadi mkubwa huko JWTZ".Usidhani kuwa wanasaka chanzo hicho kwa minajili ya kusaidiana nacho katika uchunguzi wa suala hilo (kama upo).Wanataka kumfunga mdogo.
Huu ni uhuni wa kitaaluma.Kama huyo anayetuhumiwa kukibwa fedha za umma anaona amekashifiwa,kwanini asiende mahakamani?Nini kinafichwa katika suala hili?Natambua kuna wanaodai kuwa suala hili ni nyeti sana na linaweza kupelekea uasi huko jeshini (ambapo asilimia kubwa ya askari wanaishi maisha magumu kulinganisha na makamanda wao).Lakini hoja hiyo haina uzito kushinda ukweli kwamba fisadi ni fisadi,awe raia au kamanda wa jeshi,na hatua za kisheria lazima zichukuliwe dhidi yake.
Watawala wanataka kulificha suala hili chini ya zulia.Lakini itambulikwe kuwa tunaishi zama tofauti na huko nyuma.Iwapo suala hili halitashughulikiwa kikamilifu na kiuadilifu,basi wahusika wakae wakijua kuwa kuna siku litalipuka upya.
Na nyie mnaojaribu kunyanyasa wananchi kuwashinikiza wawaambie vyanzo vya tetesi za ufisadi jeshini ACHENI MARA MOJA.Hatupendi kuharibu hadhi ya nchi yetu kwa nchi na taasisi wafadhili lakini mkiendeleza uhuni huu tutashawishika kuweka hadharani jinsi mnavyojaribu kufunika ufisadi kwa kuwanyanyasa wanaoibua taarifa hizo.
Nimechukua hatua zaidi kwa kum-tweet Rais Jakaya Kikwete (@jmkikwete) kama invyoonekana mwanzoni mwa makala hii.
Subscribe to:
Posts (Atom)