HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE,KWA WANANCHI KUHUSU HALI YA UCHUMI NCHINI NA MCHAKATO WA KATIBA MPYA, TAREHE 17 NOVEMBA, 2011
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa,Mstahiki Meya,Viongozi wa Serikali,Wazee wangu,Ndugu Wananchi,
Nakushukuru Mkuu wa Mkoa na viongozi wenzako wa Jiji la Dar es Salaam kwa kuniandalia fursa hii ya kukutana na Wazee wa Dar es Salaam. Nawashukuru sana wazee wangu kwa kuitikia wito wangu huu wa kukutana nanyi. Nimefarijika sana kwa mahudhurio yenu makubwa pamoja na taarifa kuwa ya muda mfupi.Nimewaiteni wazee wangu nizungumze nanyi na kupitia kwenu nizungumze na wananchi wote wa Tanzania. Mwisho wa mwezi uliopita sikuweza kufanya hivyo kupitia utaratibu wetu wa kawaida kwa sababu nilikuwa kwenye Mkutano wa Jumuiya ya Madola nchini Australia. Mwisho wa Mwezi huu nitakuwa Bujumbura kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, hivyo sitaweza kuongea na wananchi wakati huo. Lakini, yapo masuala kadhaa ambayo ni muhimu watu kupata ufafanuzi kutoka kwangu. Kwa ajili hiyo nimeona nitumie fursa hii kuzungumza nanyi siku ya leo. Leo nataka kuzungumzia hali ya uchumi na mchakato wa kupata Katiba Mpya.
Hali ya UchumiNdugu Wananchi;Katika kuelezea hali uchumi nchini, naomba nianze kwa kuelezea hali ya uchumi duniani kwani yanayotokea nchini yana uhusiano mkubwa na yanayotokea duniani. Hali ya uchumi duniani siyo shwari. Ukweli ni kwamba hali katika uchumi wa mataifa ya Marekani, Ulaya Magharibi na Japan haijatengemaa kufuatia machafuko ya masoko ya fedha na mdororo wa uchumi wa miaka miwili iliyopita. Hivi sasa uchumi wa mataifa tajiri ya Ulaya , wanachama wa Umoja wa Ulaya na hasa wanachama wa Umoja wa Sarafu ya Euro unapita katika kipindi kigumu na mashaka. Thamani ya sarafu hiyo inashuka na hata kuaminika kwake ni kwa mashaka. Mfumuko wa bei umepanda, ukosefu wa ajira umeongezeka na ipo hofu kubwa ya uchumi wa nchi hizo kudorora tena. Lakini nchi hizi ndiyo masoko makubwa ya bidhaa zetu, watalii na bidhaa za viwandani. Hivyo, athari zao zinatugusa na sisi. Kuongezeka kwa mfumuko wa bei kunaongeza bei ya bidhaa tunazonunua kutoka kwao. Aidha, kutetereka kwa uchumi wao nako kumepunguza masoko ya bidhaa zetu.Lakini kulegalega kwa sarafu ya Euro kumesaidia kuimarika kwa sarafu ya dola ambayo kabla ya hapo ilikuwa imepungua nguvu. Kwa sababu hiyo thamani ya sarafu ya dola imepanda duniani ikilinganishwa karibu na sarafu nyingine zote pamoja na yetu. Wakati huo huo bei ya mafuta imeendelea kupanda duniani kutoka dola 76.1 kwa pipa Septemba,, 2010 hadi dola 100.5 Septemba, 2011. Jumla ya yote haya ni kuongezeka kwa mfumuko wa bei kutoka asilimia 4.2 Oktoba, 2010 hadi asilimia 17.9 Oktoba, 2011.Ndugu Wananchi;Serikali na vyombo husika vimekuwa vinachukua hatua mbalimbali kukabiliana na matatizo ya kushuka kwa thamani ya shilingi, bei ya mafuta, bei ya sukari na matatizo ya umeme. Kuhusu kushuka kwa thamani ya shilingi Benki Kuu imeendelea kuchukua hatua zilizopo ndani ya mamlaka yake hususan kubana ulanguzi wa fedha za kigeni, kudhibiti matumizi ya fedha kigeni kufanyia malipo hapa nchini na kuongeza fedha za kigeni katika masoko ya fedha. Kwa kweli uwezo wao una ukomo. Jawabu la uhakika lipo kwenye uchumi wa mataifa makubwa kuchukua hatua thabiti kuimarisha uchumi wao ili thamani ya dola irejee mahali pake stahiki na bidhaa zetu zipate masoko ya uhakika na bei nzuri ili mapato yetu ya fedha za kigeni yaongezeke.Kwa upande wa mfumuko wa bei, ni vyema tukatambua kuwa Asilimia 75 ya ongezeko hili imetokana na kupanda kwa bei ya chakula na mafuta. Asilimia 25 iliyobaki imechangiwa na sera za fedha. Kwa upande wa mafuta, tunaamini utaratibu wa kuagiza mafuta kwa pamoja utasaidia kudhibiti bei za ndani za bidhaa hiyo. Aidha, itsaidia kupunguza makali ya athari ya bei za dunia zinazopanda. Kwa upande wa bei za vyakula, tatizo kubwa ni uhaba wa chakula katika nchi jirani unaosababisha wote kututegema sisi na hivyo kupandisha bei nchini. Tunaendelea kudhibiti magendo ya chakula na wakati huo kutengeneza taratibu rasmi za kuziuzia chakula nchi jirani.Kwa upande wa sukari tumeamua kuruhusu tani 120,000 ziagizwe ili kupunguza uhaba wa bidhaa hiyo na kushusha bei yake.
Hatuko Peke Yetu
Ndugu Wananchi;Ni vizuri tukafahamu kuwa, matatizo ya mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya fedha yetu siyo yetu peke yetu. Nchi zote za Afrika Mashariki zinakabiliana na matatizo haya. Kwa mfano, mfumuko wa bei kwetu ni asilimia 17.9, Kenya wako asilimia 18.9 na Uganda asilimia 30.5. Wakati mwaka wa jana sote tulikuwa kwa watani karibu asilimia 5. Kwa upande wa kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola sote tumeathirika. Shilingi ya Tanzania imeshuka kwa asilimia 9.4, Kenya kwa asilimia 6.8 na Uganda kwa asilimia 17.4. Randi ya Afrika Kusini kwa asilimia 18.7, Rupia ya India kwa asilimia 9.8, Pauni ya Uingereza kwa asilimia 6.6. na Euro kwa asilimia 9.7.Ndugu Wananchi;Katika kukabiliana na tatizo la umeme, Serikali inaendelea kutekeleza mpango wa dharura wa kuongeza uzalishaji wa umeme. Serikali imewawezesha TANESCO kukodi mitambo ya kuzalisha umeme kutoka kwenye makampuni ya Symbion (112 MW) na Aggreko (100 MW) na kununua mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL (100 MW).Napenda niwahakikishie wananchi kuwa, ifikapo Desemba, 2011 hali ya upatikanaji wa umeme itakuwa nzuri na mgao utapungua sana baada ya kufunga mitambo mingine mipya ya kuzalisha umeme ya TANESCO (160 MW) na Symbion (60 MW). Mikakati tuliyonayo ya muda mrefu ni kuongeza mitambo zaidi na kuongeza upatikanaji wa gesi ya kuendeshea mitambo kwa kujenga bomba kubwa la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.Mchakato wa KatibaNdugu Wananchi;Kama mtakavyokumbuka tarehe 31 Desemba 2010 katika hotuba yangu ya kuuaga mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka 2011 nilizungumzia maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika ambayo sasa ni Tanzania Bara tarehe 9 Desemba, 2011. Miongoni mwa mambo ambayo niliyataja kuwa tutayafanya katika kusherehekea siku hiyo adhimu ilikuwa ni kuanzisha mchakato wa kuitazama upya Katiba ya nchi yetu kwa nia ya kuihuisha ili hatimaye tuwe na Katiba mpya.Nilifafanua siku ile kwamba tunataka kufanya hivyo si kwa sababu Katiba yetu ya sasa ni mbaya, la hasha! Nilieleza kwamba Katiba yetu ya sasa ni nzuri na imelilea vyema taifa letu. Tuna nchi yenye amani, utulivu na umoja pamoja na watu wake kuwa wa rangi, makabila, dini na itikadi mbalimbali za kisiasa. Tunayo nchi ambayo imepiga hatua kubwa sana ya maendeleo ukilinganisha na ilivyokuwa miaka 50 iliyopita. Pamoja na hayo tunataka kuihuisha Katiba yetu ili tuwe na Katiba inayoendana na Tanzania ya miaka 50 baada ya Uhuru wa Tanzania Bara, Tanzania ya miaka 47 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na Tanzania ya miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.Kwa ajili hiyo nilielezea dhamira yangu ya kuunda Tume Maalum ya Katiba yaani Constitutional Review Commissionitakayojumuisha Watanzania wa makundi mbalimbali katika jamii yetu na kutoka pande zetu mbili za Muungano. Aidha, nilifafanua kuwa jukumu la msingi la Tume hiyo litakuwa ni kuongoza na kuratibu mchakato wa kupata maoni ya Watanzania kuhusu nini wanachokitaka kiwemo katika Katiba yao.Tume itasikiliza maoni hayo na baadaye kutengeneza rasimu ya Katiba mpya ambayo baada ya kukubaliwa na Bunge itafikishwa kwa wananchi kutoa ridhaa yao kwa kupiga kura. Nilisisitiza kuwa mchakato huo utawahusisha Watanzania wote wa ngazi zote na popote walipo mijini na vijijini. Hapatakuwa na aina yoyote ya kuwabagua watu kwa itikadi zao za siasa, shughuli wazifanyazo, dini zao, rangi zao au jinsia zao.Ndugu Wananchi;Nilifarijika sana na kauli za pongezi kwangu na kwa Serikali kwa uamuzi wa kuanzisha mchakato wa kupata Katiba mpya. Miongoni mwa waliotoa pongezi alikuwa Ndugu Freeman Mbowe, Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA ambaye wakati akichangia hotuba yangu ya kufungua Bunge Jipya, tarehe 11 Februari, 2011; nanukuu Hansad ya Bunge aliposema “Mheshimiwa Spika, ninapenda kwenye hili, nimpongeze Rais kwa kuwa msikivu, na Rais anapofanya jema tutampongeza, Serikali yake inapofanya jema tutaipongeza na Chama chochote kitakapofanya jambo jema kwa Taifa letu, tutakipongeza. Napenda kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa sababu moja ya msingi sana, kuridhia mabadiliko au kuitafuta upya Katiba ya nchi yetu.” mwisho wa kunukuu. Lakini siku chache baadaye Chama chake kikaja na msimamo tofauti, wakawa wanalalamikia kunyang’anywa hoja yao na kukataa Rais asiunde Tume ya Katiba na wala asihusike kabisa na mchakato huu. Tangu wakati huo wameendesha kampeni kubwa ya kutaka Rais asihusishwe kwenye mchakato wa kubadili KatibaKwa kweli watu wengi wanaoitakia mema nchi yetu walishangazwa na madai hayo na vitendo vya ndugu zetu hao. Hii si mara ya kwanza kwa nchi yetu kufanya zoezi la marekebisho ya Katiba au hata kuandika upya Katiba tangu Uhuru na Muungano. Mara zote hizo iliundwa Tume ya kukusanya maoni ya wananchi ambayo iliundwa na Rais. Ndivyo ilivyokuwa wakati wa Rais wa Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Rais wa tatu Mzee Benjamin Mkapa. Mwalimu Julius Nyerere alifanya hivyo mara tatu. Mara ya kwanza mwaka 1963 wakati wa kubadilisha mfumo wa vyama vingi kwenda Chama kimoja, Rais aliunda Tume ya Mheshimiwa Rashid Kawawa, Amon Nsekela. Mara ya pili wakati wa kutengeneza Katiba ya Kudumu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 aliunda Tume ya Mzee Sheikh Thabit Kombo.Mwaka 1984 Mabadiliko ya Katiba ya 1977 yaliyoweka ukomo wa Urais na kuingiza katika Katiba Haki za Binadamu, yaliyotokana na mchakato uliokuwa ni wa Kichama, ambapo CCM ilikusanya maoni kupitia mtandao wa kichama kuanzia Matawi hadi kufikia Makao Makuu. Wakati wa Rais Ali Hassan Mwinyi wa Awamu ya Pili, kulikuwa na Tume ya Jaji Mkuu Francis Nyalali iliyotuletea mabadiliko ya nane ya Katiba yaliyoruhusu vyama vingi vya siasa. Wakati wa Rais wa Awamu ya Tatu, mzee Benjamin Mkapa kuliundwa Tume ya Jaji Kisanga iliyoleta mabadiliko ya 13 na 14 ya Katiba ya nchi.Hivyo la ajabu lipi kwa Rais wa sasa kuunda Tume ya Katiba? Amepungukiwa nini Kikatiba na Kisheria ambacho Marais wenzake walikuwa nacho katika madaraka yao? Hakipo hata kimoja! Madaraka waliyokuwa nayo Marais waliomtangulia ndiyo aliyonayo Rais wa sasa. Hajapungukiwa chochote kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi. Kwa kweli hakuna hoja yoyote ya msingi ya kumuengua Rais katika mchakato wa kutengeneza Katiba ya nchi. Haipo hoja ya Kikatiba wala ya Kisheria. Hivi Rais asipounda Tume, nani aiunde Tume hiyo? Na huyo atakayeunda atapatikanaje?Juzi Bungeni msemaji wa kambi ya upinzani, katika mjadala wa Muswada wa Kuunda Tume ya Kukusanya Maonialisema Rais ni dikteta. Ama kweli “akutukanae hakuchagulii tusi” kama ulivyo msemo wa Kiswahili. Hivi mimi kweli ni dikteta? Kwa jambo lipi? Hivi ndugu zangu Rais dikteta anatoa uhuru mkubwa kama uliopo sasa wa vyombo vya habari na wa watu kutoa maoni yao? Kama mimi ningekuwa dikteta kweli nina hakika hata yeye asingethubutu kusema hivyo na kama angethubutu basi mpaka sasa asingekuwa anatembea kwa uhuru. Mimi ninachofahamu ni kuwa nasemwa kwa kuwapa watu, vyama vya siasa na vyombo vya habari uhuru mkubwa mno ambao watu wanaona unatumika vibaya kusema maneno yasiyokuwa na staha au hata matusi, fitina na kupandikiza chuki katika jamii. Labda, nijaribu kuwa dikteta kidogo watu waone tofauti yake. Naamini kungekuwa na malalamiko makubwa zaidi ya haya.Ndugu Wananchi;Mimi na wenzangu Serikalini tumefanya yote ambayo Katiba ya nchi na Sheria vinaruhusu. Ndivyo Marais walionitangulia na Serikali zao walivyofanya tena sisi tumefanya zaidi ya wao. Wote waliunda Tume za kukusanya maoni ya Katiba na wakati wa Mwalimu Julius Nyerere liliundwa Bunge Maalum la Katiba lililojumuisha Wabunge na wananchi wengine kama tulivyoamua kufanya sisi. Ilifanyika hivyo wakati wa kutengeneza Katiba ya Tanganyika kuwa Jamhuri na Katiba ya Kudumu ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977. Sisi tulichofanya cha ziada ni kulihusisha Bunge kutunga Sheria ya Kuunda Tume ya kusimamia mchakato wa Katiba mpya na vile vile kuwapa wananchi wote ridhaa ya kuamua kwa kuipigia kura Katiba inayopendekezwa. Ni kutokana na nyongeza hii ndipo tukaona busara ya kuwepo kwa Sheria maalum ya kuongoza mchakato wa kupata Katiba mpya. Tumepanua demokrasia na kuwahusisha wananchi wenyewe siyo tu katika kutoa maoni bali pia kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu Katiba ya nchi yao, badala ya kuwaachia Wabunge na viongozi wengine Serikalini peke yao. Kwa kweli tunastahili pongezi badala ya shutuma na lawama zisizokuwa na msingi.Pia inasikitisha kuona au kuwasikia watu wanaojua wakijifanya ukweli huu hawaoni au hawajui. Baya zaidi ni pale wanapojihusisha na kupotosha ukweli na kuipaka sura isiyokuwa ya kweli kuhusu kinachofanywa na Serikali. Mimi hujiuliza kwa nini wanafanya hivi. Kwa nini wanafanya hiyana ya upotoshaji wote huu? Kwa kweli sipati majibu ya uhakika. Labda ndiyo ile dhamira ya kutaka nchi isitawalike. Au ndiyo pengine ni ile nia ya kutaka kwenda Ikulu kwa njia ya mkato. Ati kwa kutumia nguvu ya umma. Basi hata hiyo nguvu unaitumia bila ya kuwa na hoja za kweli?Ndugu Wananchi;Nayasema haya kwa sababu kumekuwepo na upotoshaji mkubwa wa jambo hili tangu baada ya hotuba yangu ya tarehe 31 Desemba, 2010 mpaka wakati wa kuwasilishwa kwa Muswada wa Sheria wa Kuunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliomalizika leo Bungeni. Upotoshaji wa kwanza ulikuwa ni ule wa kujenga dhana kana kwamba Serikali imewasilisha Muswada wenyewe wa Katiba mpya. Wapo watu wamefanywa waamini hivyo wakati si kweli hata kidogo. Huu ni Muswada ambao ukipitishwa, itaundwa Tume ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu nini wanachokitaka kijumuishwe katika Katiba yao mpya. Kwa maneno mengine, maoni yenu mtakayoyatoa wananchi kwa Tume ndiyo yatakayotumika kutengeneza Katiba mpya.
Ndugu Wananchi;Katika Muswada huu kuna mambo tuliyotaja kuwa ni ya msingi ambayo yamewekewa wigo wa kuhakikisha yanalindwa. Mambo hayo ni yale ambayo yanalitambulisha taifa letu na tunu zake kuu. Mambo yenyewe ni haya yafuatayo: Kuwepo kwa nchi yetu na mipaka yake; kuwepo kwa Serikali, Bunge na Mahakama; kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; kuwepo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; umoja wetu, mshikamano wetu na usalama wetu; Mfumo wa uchaguzi kwa kura unaotoa fursa kwa wote; Hifadhi ya haki za Binadamu; Haki za watu; Usawa mbele ya sheria na haki; Uhuru wa kuabudu na kuvumiliana kwa imani zetu.Kumekuwepo na upotoshaji ati huko ni kuwaziba watu midomo. Siyo hivyo hata kidogo. Mambo hayo yanajadiliwa, lakini siyo kwa nia ya kuyaondoa bali kuboresha. Kwa mfano, kuhusu Muungano, tunachosema ni kwamba hatujadili kuwepo au kutokuwepo kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bali namna bora ya kuendesha shughuli za Muungano wetu. Lakini, tulichokifanya siyo kitu kigeni, hata Rais wa kwanza alifanya hivyo mwaka 1963 alipounda Tume ya Mfumo wa Chama Kimoja cha Siasa iliyoongozwa na Mheshimiwa Rashid Kawawa. Alitoa mwongozo na aliyataja mambo ya kulinda. Sisi tulichokifanya ni kuyataja kwenye sheria badala ya kuwa Mwongozo wa Rais.Ndugu Zangu, Watanzania Wenzangu;Kwani Katiba ya Nchi ni kitu gani. Katiba hutaja nchi na mipaka yake. Kwetu sisi nchi yenyewe ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotokana na kuungana kwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika. Pili, Katiba inaelezea jinsi nchi hiyo itakavyoendeshwa kwa maana ya mihimili mikuu mitatu ya dola ya Utawala/Serikali, Bunge na Mahakama. Katiba inafafanua jinsi Serikali inavyopatikana, muundo wake na inavyofanya kazi.Aidha, inaeleza jinsi Bunge linavyopatikana, jinsi linavyofanya kazi ya kutunga sheria na mahusiano yake na mihimili mingine. Vile vile, Katiba inaeleza jinsi Mahakama inavyofanya kazi ya kutoa haki, muundo wake na jinsi Majaji na Mahakimu wanavyofanya kazi. Kwa kweli mchakato wote huu unahusu hayo. Tunatakiwa kutoa maoni juu ya namna gani bora zaidi na ikiwezekana namna mpya ya kuendesha shughuli za Muungano wetu na jinsi mihimili yetu inavyopatikana na kufanya shughuli zake.Ndugu Wananchi;Jambo lingine lililopotoshwa ni dhana ya muswada kusomwa mara ya kwanza. Kwa mujibu wa utaratibu wa kutunga sheria, Miswada, husomwa mara tatu Bungeni. Muswada kusomwa mara ya kwanza ni pale unapogawiwa kwa Wabunge baada ya kuchapishwa katika gazeti la Serikali siku 21 kabla ya kuwasilishwa Bungeni. Baada ya kuchapishwa, hugawiwa kwa Wabunge. Muswada husomwa mara ya kwanza Bungeni ili kutoa fursa kwa Mheshimiwa Spika kuwasilisha Muswada huo kwenye Kamati iuchunguze na kuutolea maoni. Mheshimiwa Spika anaweza pia kuielekeza Kamati kutafuta maoni ya wananchi.Baada ya Kamati kukamilisha kazi yake, Muswada husomwa mara ya pilli ambapo Muwasilishaji atatoa hoja kwamba Bunge liujadili Muswada pamoja na kutoa maelezo ya Muswada. Mjadala huanza kwa Kamati ya Bunge kutoa maoni yake ikifuatiwa na maoni ya Kambi ya Upinzani. Wakati Kamati ya Bunge inapojadili Muswada, Waziri mhusika huwepo na mara nyingi maoni ya Kamati ya Wabunge na wadau hujumuishwa wakati Waziri anapowasilisha hoja Bungeni ya Muswada unaposomwa mara ya pili. Baada ya mjadala, Bunge hukaa kama Kamati ya Bunge zima ambapo hupitia Muswada kifungu kwa kifungu.Katika hatua hii Wabunge huweza kupendekeza mabadiliko mahsusi kwenye kila kifungu. Aidha, Waziri nae anaweza kutetea marekebisho ya Muswada. Baadaye Bunge hurejea, taarifa ya Kamati ya Bunge zima hutolewa kwamba Muswada umepitiwa kifungu kwa kifungu na kukubaliwa. Kisha Muswada husomwa mara ya tatu kuashiria kwamba Muswada umepitishwa. Mara nyingi Muswada hutokana na majadiliano katika hatua hizi zote, mabadiliko hufanywa na wakati mwingine mabadiliko huwa makubwa kiasi kwamba kufanya Muswada uliochapishwa na kusomwa mara ya kwanza na ule uliokubaliwa mwishoni uwe tofauti kabisa.Ndugu Wananchi;Muswada huu ulisomwa mara ya kwanza mwezi Aprili na kupelekwa kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala mwezi Aprili, 2011. Tangu wakati huo Kamati imekuwa ikiufanyia uchunguzi Muswada huo na kukusanya maoni ya wadau. Walisikiliza wadau Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar pamoja na kufuatilia maoni ya makongamano, magazetini na kwenye mitandao. Kisha Kamati ikayajadili na kutoa mapendekezo yake ambayo Serikali iliyasikiliza na kuyajumuisha wakati uliposomwa mara ya pili. Muswada huu haukuwahi kuondolewa Bungeni. Kwa sababu hiyo, hakuna sababu ya kurudia kusomwa mara ya kwanza kwa mujibu wa taratibu za kuendesha Bunge.Tukumbuke kwamba baadhi yao waliahidi kwamba wangetoa Katiba Mpya katika siku mia moja tu. Serikali imechukua miezi kumi na mmoja na wanalaumu kwamba eti inawahisha mchakato!! Hiyo Katiba ya siku mia moja sijui wangeipataje bila kuwashirikisha wananchi?Ndugu Wananchi;Ni kutokana na hoja hizo Spika akaamua Muswada uendelee kujadiliwa na Bunge na leo Bunge limeupitisha Muswada huo. Baadae Muswada utaletwa kwangu kwa ajili ya kutiwa saini uwe Sheria. Baada ya hapo itabakia kazi yangu na Rais wa Zanzibar kuunda hiyo Tume ili mapema mwakani kazi ya kukusanya maoni ya wananchi ianze. Lengo letu ni kuwa ifikapo mwaka 2014 zoezi zima liwe limekamilika ili mwaka 2015 tufanye uchaguzi tukiwa na Katiba mpya. Itapendeza tukisherehekea miaka 50 ya Muungano na Katiba mpya. Ni matumaini yangu kwamba wananchi wote watashiriki kwa ukamilifu kutoa maoni yao kwa Tume hiyo.
Ndugu Wananchi;Nimechukua muda wenu mwingi kuyafafanua masuala haya kwa umuhimu wake. Nia ni kutaka watu waelewe maoni ya upande wa Serikali. Matatizo ya kiuchumi yanayotukabili tunaendelea kuyashughulikia. Yale yaliyo kwenye uwezo wetu tutayamaliza na yale yaliyo nje ya uwezo wetu tutaendelea kuchukua hatua za kupunguza makali. Aidha, tutaendelea kutoa wito kwa mataifa husika kuchukua hatua thabiti kutatua matatizo yao kwani tunaoumia ni wengi.Ndugu Wananchi;Kwa upande wa mchakato wa kupata Katiba mpya nawasihi Watanzania tujiandae kwa maoni ya kutoa kwenye Tume ya Katiba mara itakapoanza kazi. Kwa wale ambao hawatapata walichokitaka nawaomba warudi kundini, sote tuungane kwa hatua inayofuata. Najua wanayo maoni mengi mazuri wayatayarishe na kuyawasilisha kwa Tume itakayoundwa. Njia ya maandamano na vurugu si ya busara kufuata. Haijengi bali inabomoa, haina faida bali hasara nyingi, haina faraja bali machungu kwa pande zote. Busara ituongoze sote kuchagua njia inayojenga, yenye faida, furaha na faraja kwa wote. Tutofautiane bila kupigana. Serikali itaendelea kutekeleza wajibu wake wa kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa nchi ya amani na utulivu.
Mwisho
Ndugu Wananchi,Naomba nimalizie kwa kuwashukuru wananchi kwa kuwa na subira kwa kipindi chote hiki toka tutangaze nia yetu ya kuanza mchakato wa kupata Katiba mpya. Kwa mara nyingine tena nawaomba mjiandae kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kupata Katiba mpya mara utakapoanza ili tuendelee kuijenga na kuiendeleza nchi yetu na vile vile tuendelee kuithamini na kuitunza amani ya nchi yetu.
Mungu Ibariki Afrika!Mungu Ibariki Tanzania!Asanteni sana kwa kunisikiliza!
18 Nov 2011
18.11.11
Evarist Chahali
JAKAYA KIKWETE
1 comment
16 Nov 2011
16.11.11
Evarist Chahali
Siasa za Kijambazi
No comments
Mishahara mipya kwa wabunge ni ujambazi
Uskochi
AWALI, nilitaraji wiki hii ningeendelea na uchambuzi wangu kuhusu changamoto mbalimbali zinazovikabili vyama vyetu vya siasa nchini kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao, mwaka 2015. Lakini wakati najiandaa kuingia kwenye mada hiyo nikakutana na habari ambayo siyo tu ilinitia hasira bali pia ilinichefua.
Habari yenyewe inahusiana kwa namna fulani na mada niliyozungumzia wiki iliyopita katika safu hii, yaani suala la unafiki. Wakati unafiki niliouchambua ulihusu sakata la ushoga (kufuatia tamko la Waziri Mkuu wa Uingereza kwamba nchi yake inafikiria kuzikatia misaada nchi zinazominya haki za mashoga), unafiki ninaouzungumiza leo unahusu baadhi ya wabunge wetu.
Wiki iliyopita, vyombo mbalimbali vya habari huko nyumbani viliripoti kwamba baadhi ya wabunge wetu wamekumbushia “kilio chao cha siku nyingi” wakidai posho na mishahara yao viongezwe. Naomba nitamke mapema kuwa huu ni ujambazi wa mchana kweupe (daylight robbery).
Ninatambua kuwa waheshimiwa wetu wamezoea kusifiwa tu hata pale wanapoongea masuala yasiyo na msingi na sitashangaa iwapo hitimisho langu kwamba madai yao ya kuongezewa posho na mishahara ni ujambazi, likaibua malalamiko makali kutoka kwao.
Lakini kwa vile Tanzania haiwezi kuendelea kufanywa shamba la bibi la walafi wachache (ambao zama za Mwalimu Nyerere tuliwaita kupe wanaoishi kwa kutegemea jasho la wengine) ni lazima tuwakemee watu hawa pasipo uoga wala aibu.
Ili kuelewa kwa nini nimeandika kuwa wanachofanya wabunge wanaodai nyongeza ya posho na mishahara ni unafiki wa hali ya juu (na kuufananisha na ujambazi) ni muhimu kusikia hoja zao za ovyo ovyo zinazojaribu kuhalalisha wanachodai.
Mbunge wa Rombo kupitia CHADEMA, Joseph Selasini, alinukuliwa na gazeti moja akidai kuwa eti “uwakilishi umekuwa mzigo kwani wakati mwingine amekuwa akitumia fedha anazopata kwenye vyanzo vyake binafsi kuwatumikia wananchi.”
Gazeti hilo liliendelea kumnukuu mbunge huyo akisema kwamba “Hapa nina mialiko 26 ya kwenda kuchangia ujenzi wa shule na shughuli nyingine za maendeleo kule Rombo, zote hizi zinanihitaji kama mbunge nitoe fedha, sasa jamani fedha hizi zinatoka wapi?”
Swali analopaswa kuulizwa Selasini na wabunge wenzie wenye mawazo kama yake ni hili: “kama uwakilishi ni mzigo, nani alimshikia mtutu wa bunduki kwamba lazima agombee uwakilishi huo? Na kama wakati anagombea ubunge hakufahamu kuwa kutumikia umma ni jukumu linalohitaji kujitoa muhanga kwa nini basi asitue mzigo huo?
Haihitaji japo kozi ya saa chache ya jinsi ya kutumia busara zetu ipasavyo kutambua kuwa kama umewania nafasi fulani na kuipata lakini hatimaye unagundua kuwa nafasi hiyo ni mithili ya mzigo mzito wa gunia la misumari, kinachopaswa kufanywa siyo kudai (tena kwa ubabe badala ya unyenyekevu) usaidiwe bali kuacha nafasi hiyo kwa wenye uwezo wa kuimudu.
Kwa hiyo kama Selasini anaona jukumu la uwakilishi linamfilisi basi kuna shughuli nyingi tu za kufanya ambazo hazitamfanya alalamikie “mshahara na posho kidogo.” Anaweza kabisa kuachana na ubunge na akabaki na jukumu dogo la kuhudumia familia yake pasipo kutaka kuwabebesha walipakodi wa Kitanzania mzigo mkubwa zaidi ya wanaoubeba sasa kuhudumia maisha ya kitajiri ya wabunge wetu.
Lakini katika kuonesha kuwa tuna tatizo kubwa na baadhi ya watu tuliowakabidhi dhamana ya kutuwakilisha, Selasini ananukuliwa na gazeti hilo akikiri kwamba “...wabunge hukutana na kero ya wananchi kuomba fedha ili wakatatue matatizo yao mbalimbali na kwamba ni vigumu kukwepa jukumu hilo kutokana na hali ya maisha ilivyo sasa nchini.”
Ahaa, kumbe wakati anaomba kuongezewa posho na mshahara anafahamu fika kuwa wanyonge anaotaka wakamuliwe zaidi ili posho na mishahara ya wabunge iongezwe si tu wana matatizo mbalimbali bali pia wanakabiliwa na hali ngumu kutokana na hali ya maisha ilivyo sasa nchini.
Sijui tatizo la wabunge kama Selasini ni kuishi katika sayari nyingine ambayo wenye haki ya maisha ya anasa ni wao tu au ni ulafi tu wa kutaka kila kidogo tulichonacho kikusanywe na kukabidhiwa wao wenye mahitaji muhimu kuliko wanyonge “wanaopigika” tangu mawio hadi machweo.
Naye Mbunge wa Mtera kwa tiketi ya CCM, Livingstone Lusinde alinukuliwa akiitaka Ofisi ya Spika, Anne Makinda, kufanya jitihada za kuwaelimisha wananchi kuhusu wajibu wa mbunge ili wafahamu kazi nyingine wanazofanya wawakilishi hao wa wananchi ni nyongeza nje ya majukumu yao ya msingi.
Lusinde alidai kwamba “Malipo yetu ni kidogo sana, hayatoshelezi kabisa lakini wananchi tunaowawakilisha hawatuelewi katika hili, maana wanadhani tuna fedha nyingi, sasa hapa kuna tatizo. Nadhani kuwapo utaratibu wa kuwaelimisha, wajue hata kazi nyingine tunazofanya siyo wajibu wetu ila tunajitolea na nyingine hizi zina gharama kubwa.”
Huu ni zaidi ya unafiki. Ni matusi kwa Watanzania masikini. Hivi Lusinde anafahamu pato la Mtanzania wa kawaida ni kiasi gani? Hivi kigogo huyu ana taarifa zozote kuhusu kuporomoka kwa kasi thamani ya shilingi yetu? Na anaposema hayo mamilioni wanayolipiwa ni kidogo anataka kutuambia kiasi gani ndio stahili kwa mbunge wa nchi yetu masikini kabisa duniani?
Ni hivi, Lusinde sio kwamba wananchi mnaowawakilisha hawawaelewi kwa nini mnadai marupurupu zaidi ya hayo makubwa kabisa mnayopata sasa. Wasichowaelewa ni mnaishi sayari gani? Hivi mnapolalamika kuwa mamilioni mnayolipwa hayawatoshi, watumishi wengine wa umma kama vile walimu, madaktari na wengine waseme nini?
Tatizo la waheshimiwa hawa wakishapata kura wanageuka viumbe tofauti kabisa na wale waliokuwa wakijifanya wana uchungu kweli na wapiga kura wao. Wanasahau kuwa wengi wa wananchi waliowapigia kura waheshimiwa hao kuingia bungeni ni masikini wa kutupwa na hawana wa kumlalamikia (na hata wakilalamika ni kazi bure maana wawakilishi wao nao wapo ‘bize’ kulalamikia mishahara na posho).
Labda msomaji mpendwa unaweza kuwa unajiuliza ninapoandika waheshimiwa hawa wanapata mishahara ya mamilioni ninazungumzia kiasi gani hasa. Kwa hesabu za haraka haraka, mshahara wa mbunge ni Sh milioni 2.3 kwa mwezi na pamoja na posho kiwango cha juu anachopokea kwa mwezi kinafikia takriban shilingi milioni saba.
Hivi mtu anayelipwa shilingi milioni saba kwa mwezi lakini bado “analilalia” kuwa fedha hizo hazitoshi tumwite jina gani? Binafsi nimehitimisha hapo awali kuwa huu ni ujambazi wa mchana kweupe kwa sababu wanachofanya wabunge wanaodai maslahi zaidi ya hayo lukuki wanayopewa ni matusi kwa mamilioni ya Watanzania ambao, wastani wa pato la kila mmoja wao kwa mwaka ni dola za Marekani 500 (takriban shilingi 870,000). Kwa maana hiyo, kwa wastani, pato la Mtanzania kwa mwezi ni shilingi 70,000.
Sasa kuna uhalali gani kwa wabunge kutoridhika na mshahara ambao ni takriban mara 100 ya “mshahara” wa Mtanzania wa kawaida (yaani pato la wastani kwa mwezi)? Ninafahamu kuwa waheshimiwa wabunge hawatopenda kusikia nikihitmisha kuwa neno pekee mwafaka la kuelezea hali hii ni ujambazi lakini huo ndio ukweli wenyewe.
Kwa lipi hasa wanalofanya huko bungeni hadi wadai kuwa malipo mara 100 zaidi ya Mtanzania wa kawaida hayawatoshi? Kama ubunge umekuwa mzigo basi waachie ngazi. Kuna haja gani ya kuwa na watu zaidi ya 300 wanaolipwa mamilioni ya fedha huku nchi ikizidi kuwa masikini tena siyo kwa bahati mbaya bali ni matokeo ya wengi wa wabunge hao kutanguliza mbele maslahi ya chama (na matumbo yao) badala ya yale ya walalahoi waliowatuma kuwawakilisha?
Nimalizie kwa kutoa rai kwa Watanzania wenzangu kufuatilia kinachoendelea hivi sasa kwenye nchi tajiri kama Marekani, hapa Uingereza na kwingineko ambapo umma umeamua kuingia mtaani katika kile kilichoanza kama “Occupy Wall Street” na sasa kinaelekea kusambaa sehemu mbalimbali duniani. Lengo la harakati hizo ni kupinga tamaa na ulafi wa taasisi za fedha hususani benki. Lakini lengo kubwa zaidi ni kupambana na mfumo wa kiharamia ambao mwenye nacho si tu anaongezewa bali anafanya ujambazi kuwapora wale wasio nacho.
Nanyi wabunge nawasihi muache matusi dhidi ya mamilioni ya walalahoi wa Kitanzania ambao licha ya mzigo mkubwa mnaowabebesha kumudu kuwalipa ninyi posho na mishahara yenu ya kufuru, muda huu hawajui watamudu vipi mlo ufuatao, achilia mbali mlo wa siku inayofuata.
Msipoacha kebehi zenu kuwa mamilioni mnayolipwa hayatoshi na mnataka zaidi, ipo siku mtashitukia mkipita mitaani mkiwa ndani ya magari yenu ya kifahari mnakumbana na makelele ya “mwizi, mwizi...” Labda hiyo ndio itawashitua mtambue kuwa ninyi ni wabunge wa nchi masikini kabisa duniani na mishahara na posho mnazopewa sasa haziendani hata chembe na umasikini wetu.
16.11.11
Evarist Chahali
CHADEMA, MBEYA
No comments
![]() |
| Miraj Kikwete (kushoto) |
MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Miraj Jakaya Kikwete, amekitetea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akipinga chama hicho kuhusishwa na vurugu mbalimbali zinazotokea nchini, zikiwemo zile za Wamachinga, zilizotokea jijini Mbeya hivi karibuni.
Mtoto huyo wa Rais alionyesha kukerwa na watu wenye mtazamo wa kukisingizia chama hicho kikuu cha upinzani kwa kukihusisha na vurugu, wakati hali halisi inaonyesha wazi kuwa wananchi wenyewe hawaridhishwi na hali ya mambo ilivyo na hivyo kuamua kuwa mstari wa mbele kupigania haki zao.
Miraj aliweka wazi msimamo wake huo kupitia mtandao wake wa facebook akichangia mjadala mzito uliohoji kwa nini CHADEMA inasingiziwa vurugu Mbeya?
Mtoto huyo wa Rais, aliweka wazi ujumbe wake huo baada ya mchangiaji mmoja, kuchangia kwa jazba akitabiri machafuko kutokea kabla ya 2015.
Mchangiaji huyo alisema yeye si mtabiri, lakini kwa hali ilivyo nchini, tunaelekea kwenye vita na haina hata mpito wa chaguzi mbili mbele kwa maana ya 2015 na 2020.
Mchangiaji mwingine, Gallus Mpepo, ambaye ndiye aliyekuwa akijadiliana na Miraj, alianza kwa kumrushia lawama Mkuu wa Mkoa mpya wa Mbeya, Abbas Kandoro, kwamba kila mkoa anaokwenda, amekuwa ukikumbwa na vurugu za Wamachinga.
Mpepo alisema anashangaa kuona baadhi ya wachangiaji wa mjadala huo, wanahusisha vurugu za Mbeya na maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), licha ya kwamba chanzo chake kiko wazi kwamba wafanyabiashara hao walikuwa wakipinga kuondolewa kwenye maeneo yao ya biashara bila kupewa maeneo mbadala.
Alisema hii inatokana na hali ya kutaka kuficha makosa yaliyofanywa na uongozi wa mkoa huo chini ya Kandoro, kutoongoza kwa busara katika kutatua kero za wananchi.
Katika ujumbe huo, Mpepo alieleza kufurahishwa na ujumbe wa mtoto wa Rais Kikwete na kwamba ameupenda ufafanuzi wake kuhusu mjadala huo.
Akichangia mjadala huo, Miraj ambaye ni nadra kujihusisha na masuala ya siasa, alihoji nani anayedai haki Mbeya kati ya CHADEMA na wananchi hadi kusababisha vurugu hizo.
Mtoto huyo wa Rais Kikwete alisema ni makosa kuihusisha CHADEMA na vurugu hizo kwani CHADEMA si nchi.
“CHADEMA si nchi ni chama na si kwamba wanachama wa CHADEMA ndio pekee wenye shida na matatizo, ni Watanzania wote,” alisema mtoto huyo wa Rais.
Miraj alienda mbali kwa kusema ni fikra potofu kufanya kama vile kuna Tanzania na CHADEMA.
“Maana serikali ndiyo Tanzania na CHADEMA ni chama ndani ya Tanzania, ni chama cha Watanzania kwa ajili ya Watanzania, kama kilivyo Chama cha Mapinduzi (CCM), NCCR-Mageuzi na kadhalika.
“Tofauti ni harakati na sera... tupendane Watanzania, tutafika mbali kwa umoja na mshikamano wetu na wala si kwa kejeli na matusi…, wenye haki tuwasimamie wote na penye haki tusimame sote,” alisema Miraj
CHANZO: Tanzania Daima
12 Nov 2011
02. Mgonjwa aliyekuwa akitibiwa Zahanati hapo akiwa amezirai baada ya bomu la machozi lililopingwa na Jeshi la polisi kutua ndani ya Wadi. |
03. Mganga Mkuu wa zahanati ya Ipinda jijini Mbeya Dk. Lute Kibopile ambaye pia ni mmiliki wa zahanati hiyo akionesha Bomu la machozi lililopigwa na Jeshi la polisi na kuingia ndani ya Wadi. |
04. Mganga Mkuu wa zahanati ya Ipinda jijini Mbeya Dk. Lute Kibopile ambaye pia ni mmiliki wa zahanati hiyo akielezea jinsi bomu la machozi lilivyopingwa. |
05. Muuguzi akionesha eneo ambalo bomu la machozi lilipotua katika Zahanati ya Ipinda, eneo la Mwanjelwa jijini Mbeya. |
CHANZO: www.mbeyayetu.blogspot.com
:
11 Nov 2011
11.11.11
Evarist Chahali
RAIA MWEMA, USHOGA
1 comment
Tatizo ni unafiki wetu, si ushoga
Uskochi
MOJA ya mambo yaliyonishitua sana nilipofika hapa Uingereza kwa mara ya kwanza ni jinsi Ukristo ulivyopoteza nguvu yake (hususan mahudhurio kanisani na watu wanaofuata Ukristo). Kilichonishitua ni ukweli kwamba Ukristo uliletwa huko nyumbani na “wazungu” hawa na nilitarajia wangekuwa wacha Mungu wakubwa.
Dalili za Ukristo kupoteza nguvu yake zinaonekana katika namna makanisa yanavyoishia kugeuzwa kumbi za starehe baada ya kukosa waumini. Kadhalika, asilimia kubwa ya waumini makanisani ni wageni kutoka nje ya nchi hii. Na japo Malkia wa Uingereza ni Mkuu wa Kanisa la Anglikana na Askofu Mkuu wa Canterbury ni mithili ya Baba Mtakatifu (Papa) kwa Kanisa hilo, idadi kubwa ya Waingereza inajitambulisha kama watu wasiofuata dini. Na kuna kundi kubwa tu la wanaojitambulisha kama Wakristo lakini wasiotia mguu kanisani.
Hakuna jibu jepesi kuhusu kwa nini Ukristo unazidi kupoteza nguvu nchini hapa lakini baadhi ya watu niliowahoji wanadai huenda maendeleo katika nyanja mbalimbali ni chanzo kwa baadhi ya watu “kupuuza” umuhimu wa imani katika maisha ya mwanadamu.
Lakini pamoja na Ukristo kupoteza nguvu yake miongoni mwa Waingereza, kwa kiasi kikubwa uadilifu katika nyanja mbalimbali za maisha umeendelea kuwa wa kiwango cha juu. Na hapa ndipo unaweza kubaini tofauti kubwa kati ya Waingereza “wanaopuuza dini” na akina sie huko nyumbani ambao dini inaonekana kuwa sehemu muhimu kwa maisha yetu.
Neno mwafaka linaloweza kuelezea tofauti hiyo ni UNAFIKI. Ni hivi, ni bora kuwa na watu wasio na dini au wasioabudu uwepo wa Mungu lakini wakaishi na kutenda mambo kiadilifu kuliko kuwa na ‘washika’ dini wasiokosekana makanisani au misikitini lakini uadilifu wao ni haba kama sio sifuri kabisa.
Na suala la unafiki linaweza kuchukua nafasi muhimu katika mjadala mkali uliosababishwa na kauli ya Waziri Mkuu wa Uingereza kuwa nchi yake itasitisha misaada kwa nchi zinazokiuka haki za mashoga. Tayari Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ameweka bayana msimamo wa Serikali kwamba Tanzania ipo tayari kukosa misaada ya Uingereza kuliko kubadilisha sheria za nchi zinazopiga marufuku ushoga.
Kuonyesha kuwa tamko la Membe halikuwa la kukurupuka tu, Rais Jakaya Kikwetealinukuu kauli hiyo ya Waziri wake na kuirusha hewani (Retweeted) kwenye ukurasa wake (Kikwete) kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.
Lakini kabla sijaingia kwa undani katika kujadili suala hili ni vema nikaweka wazi msimamo wangu. Imani yangu kama Mkristo wa madhehebu ya Katoliki (ambaye almanusura ningekuwa padre iwapo nisingeghairi kujiunga na seminari mwaka 1986) sio tu inapinga ushoga bali pia inauona kama dhambi. Kwa hiyo, naomba ifahamike kuwa lengo la makala hii si kuunga mkono ushoga.
Kwa upande mmoja, Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, alikuwa na haki ya kuweka masharti katika misaada wanayotoa. Ifahamike kuwa misaada hiyo inatokana na fedha za walipa kodi wa Uingereza na inatarajiwa ielekezwe kwa nchi zinazoonekana machoni mwa Waingereza kama zinazoendana na maadili yao. Na moja ya masuala yanayopewa kipaumbele na nchi hii ni haki za binadamu (ikiwa ni pamoja na haki za mashoga).
Kwa hiyo basi si kwamba Cameron alikurupuka tu na tamko hilo ambalo baadhi ya wenzetu wamelitafsiri kama ajenda ya kueneza ushoga, bali anawakilisha hisia za wananchi wake ambao kimsingi ndio chanzo za fedha tunazopatiwa kama misaada.
Ni wazi kuwa kiongozi yeyote yule anayejua anachofanya atahakikisha anasimama upande wa wananchi wake. Kwa mantiki hiyo wananchi wake wanapotaka fedha yao wanayotupatia kama msaada ielekezwe tu kwa nchi zinazojali haki za binadamu (ikiwa ni pamoja na haki za mashoga) tu basi hana budi kufanya hivyo.
Japo siungi mkono ushoga lakini ninaelewa mantiki ya Cameron kutoa tamko hilo linaloakisi matakwa ya wananchi wake. Lakini kwa vile matakwa ya Waingereza kuhusu haki za binadamu hayaishii kwa mashoga pekee, ingeleta maana zaidi iwapo tishio la kukata misaada lingeelekezwa pia kwenye tatizo sugu la rushwa (na ufisadi kwa ujumla) ambalo si tu linakwaza haki za binadamu za masikini (ambao ni wengi kuliko mashoga) bali pia linaweza kusababisha wanyonge kupoteza maisha (kwa mfano rushwa inayowezesha vyombo vya usafiri vyenye hitilafu kuendelea na kazi na hatimaye kusababisha ajali).
Sasa nigeukie unafiki unaoandamana na jinsi tamko la Cameron lilivyopokelewa. Haihitaji utafiti wa kina kubaini kwamba si tu Tanzania (na nchi nyingine zinazolengwa na tishio hilo la kukatiwa misaada) ina mashoga lakini pia ushoga unazidi kuongezeka. Hivi nani anayesoma magazeti ya burudani au blogu hajamwona shoga mmoja aliyejipachika jina Seduction ambaye ni kama yupo kwenye kila shughuli za mabinti maarufu jijini Dar?
Nilipokuwa huko nyumbani mwaka 2005 na niliporejea tena mwaka 2008 nilishuhudia idadi kubwa tu ya mashoga katika maeneo mbalimbali ya burudani jijini Dar es Salaam. Na uchunguzi usio rasmi ulionesha kuwapo kwa mashoga kwenyekitchen parties ni kama suala la kawaida tu. Nilibaini kwamba kumbi za muziki wa mwambao zilikuwa ni chaguo kubwa la mashoga.
Lakini jambo moja la wazi ni kwamba hakukuwa na upinzani, chuki au hasira dhidi ya mashoga hao. Na sijawahi kusikia kuna shoga amekamatwa na polisi, kupelekwa mahakamani na hatimaye kufungwa kwa “kosa” la kuwa shoga. Na ukidhani hilo la kutokamatwa kwa mashoga ni la kushangaza sana, basi kubwa zaidi ni uteuzi wa kigogo mmoja (mstaafu sasa) wa shirika la umma ambaye kila aliyemjua alikuwa anafahamu tabia yake ya ushoga (kwa maana ya tendo la ndoa na watu wa jinsia yake).
Nina hakika aliyemteua alikuwa anafahamu hilo lakini haikuzuia kigogo huyo kupewa nafasi ya kufisadi shirika hilo hadi alipoondoka huku akijimwagia sifa za vichekesho.
Tuache unafiki, hivi maadili tunayodai ni haya ya wengi wa vigogo wetu kutumainia waganga wa kienyeji katika kila wanalofanya? Maadili haya ya “wachunga kondoo wa Bwana” kuishi maisha ya kifahari kama matajiri wakubwa ilihali waumini wao hohehahe wakihimizwa kuongeza kiwango cha sadaka? Au maadili haya ya Wakristo na Waislamu wasiokosekana kwenye nyumba za ibada lakini ndio wahusika wakuu wa ufisadi? Au haya ya ushirikina kuwa muhimu kuliko kumtumainia Mungu?
Au maadili tunayodai kuwa nayo ni haya ya majambazi wanaotupora utajiri wetu kisha kuibukia makanisani au misikitini na kutoa sadaka au zaka kubwa (iliyotokana na fedha ileile waliyotuibia)? Au maadili tunayodai Waziri Mkuu Cameron anayapuuza ni haya ya wengi wa wasanii wetu wa kike kwenye fani ya filamu ambao licha ya kupendelea kuvaa nusu uchi, hawana mishipa ya aibu kutangazia umma uchafu wanaofanya katika maisha yao? Maadili haya ya wasanii wa Khanga Moja na Kitu Tigo wanaoigiza u-Sodoma na Gomora hadharani kwa kisingizio cha burudani lakini hakuna wa kuwachukulia hatua?
Ni maadili gani anayozungumzia Kikwete na Waziri wake Membe ilihali katika hotuba yake iliyogusia mafisadi wa EPA alikumbushia umuhimu wa haki zao za binadamu (na ikambidi aliyekuwa Spika, Samuel Sitta, amkumbushe Rais kuwa haki za wananchi ni muhimu kuliko za mafisadi)?
Mbona hakukuwa na maandamano ya kumlaani Kikwete kwa kutetea haki za binadamu ambao ni mafisadi lakini leo tunawalaani Waingereza kwa kutishia kutunyima fedha zao kama tusipofuata matakwa yao?
Lakini unafiki mkubwa zaidi ni huu: viongozi hawa hawa ambao licha ya kukiri hadharani kuwa hawajui kwa nini nchi yetu ni masikini (labda pia hawajui kwa nini waliamua kutuongoza) pia ni washiriki wakubwa wa ufisadi unaotufanya tuishi kwa kutegemea fadhila za wafadhili kama Uingereza, wanatuhadaa kuwa ni bora tunyimwe misaada kuliko kukiuka maadili yetu. Lakini wababaishaji hawa hawatuambii jinsi watakavyofidia pengo litakalotokana na kukatwa misaada hiyo.
Na hawatuambii kwa sababu hajui watafidia vipi na hawajali kwa vile wao hawataathiriwa na kukatwa misaada hiyo. Na kama ambavyo tatizo la umeme linavyodumishwa na mafisadi ili kujaza akaunti za vijisenti huku nje, si ajabu tukikatiwa misaada mafisadi watapata kisingizio kipya cha “imebidi mabilioni haya ya shilingi yatumike kufidia pengo lililotokana na uamuzi wa Uingereza kutukatia misaada.”
Nimalizie makala hii kwa kutamka bayana kuwa kama ambavyo sipingi uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi kwa vile hainihusu mie Mkristo, sina tatizo na kurekebisha sheria za ushoga kwa vile si tu mashoga wapo na wanazidi kuongezeka (na hakuna anayewachukulia hatua kwa kuvunja sheria) lakini pia sheria hizo hazinihusu mimi au yeyote yule asiye shoga.
9 Nov 2011
9.11.11
Evarist Chahali
Heavy D, HIP-HOP, Music
No comments
Sad news out of Los Angeles this evening, as TMZ reports that rapper Heavy D has died.
The 44-year-old star, who found fame with his 1991 hit Now That We Found Love and appeared in several movies, was reportedly rushed to a hospital this afternoon after a 911 call was made from his
Officials tell TMZ that no foul play is suspected, and they are investigating the death.
Heavy D, whose real name is Dwight Arrington Myers, had just performed at two special events last month: the Michael Jackson tribute concert in Wales and the BET Hip Hop Awards in Atlanta. He also has a minor role in the new Eddie Murphy comedy Tower Heist.
The overweight star tweeted a simple final message earlier today: "BE INSPIRED!"
Famous fans from throughout Hollywood are taking to Twitter to remember Heavy D and express shock at his sudden death. A roundup of who's saying what:
-Samuel L. Jackson: "Ahhh man! Heavy D?! Dwight wz a dear friend. Fond memories of a truly cool brutha."
-Usher: "This is too heavy, I can't believe it. HEAVY D was just here. Truly gone too soon. My heart and support goes out to his family. R.I.P HEAVY"
-Ne-Yo: "Man. I was just with Heavy D recently in London. Had I known it'd be the last time I'd see him, I woulda told him he was truly great. RIP..."
-LL Cool J: "May GOD embrace the soul of Heavy D and Bless his family. I respected you Heavy and I always will."
-Fred Savage: "Rest in Peace Heavy D. You provided the soundtrack to some of the best times of my teenage years. Your music will always make me smile."
-Eve: "RIP HEAVY D... Sending my prayers and condolences to family and friends"
-Joel Madden: "Heavy D was a truly positive and uplifting man. Rest in peace Heavy. Its a very Sad day today."
-Keyshia Cole: "When I met Heavy D.. He said 'believe U have a good soul, Sing with always having Something to say'"
-Big Boi: "R.I.P Heavy D a true pioneer may god bless your soul"
-Sinbad: "It is a sad day today .. My younger yellow brother from another mother 'heavy D' passed away today. I loved that brother. He was a good man"
-Alyssa Milano: "Heavy D gave me advice when I was pregnant. He said, 'Cherish every single moment. It goes by way too fast.' Rest in peace, Heavy D."
-Jill Scott: "Oh my heart aches!! In shock. Can't believe Heavy D is gone. Such a positive sweet hearted man. Please pray for his daughter."
-Wilmer Valderrama: "We have lost another member of Hip Hop's legacy, a TRUE Rap legend... 'Heavy D' RIP...... WV"
-Missy Elliott: "U will be missed Heavy D so many laughs we've shared but your Music is Timeless and will Always be Around 4ever Love u Heav..."
7 Nov 2011
7.11.11
Evarist Chahali
No comments

So homosexuality is unAfrican? What about living on handouts?
For a country that once had ambitions of becoming a self-reliant nation, Tanzania is a surprisingly donor-dependent place.
The Arusha Declaration, Julius Nyerere’s blueprint for socialism and self-reliance, argued that dependency on external economic assistance would be detrimental to the country’s independence.
In a brief but closely argued document, a strong case was made for reliance on our own resources and treating foreign aid with care, especially shunning financial grants, for whereas loans and credit lines impose the responsibility of repayment, free money makes the recipient a virtual beggar and keeps him beholden to the donor.
And yet Tanzania, even under the old man himself, went ahead and accepted foreign money, loans and grants, in huge sums, especially in sectors such as education, health and water and sanitation.
The dependency grew so great that when Olof Palme, the Swedish social democrat who had underwritten Nyerere’s education programme, lost power, Tanzanians felt the impact probably more acutely than the Swedes.
The rightwing government that came in scrapped the whole aid package to Tanzania, declaring, rather cruelly, that we had become a bottomless pit.
Since then our education programmes have struggled, our schools have staggered along, and our rulers have remained largely clueless as to what we need to do to liberate ourselves from the mire of growing dependency.
Indeed, a few years ago we reached some benchmark that convinced our donor countries that we had become a highly indebted poor country (HIPC). And we celebrated with a beggar’s dance, bowl in hand.
Our government has continued to borrow and to receive cash handouts in what has come to be known as general budget support (GBS) that gives it unfettered licence to place those monies wherever it pleases.
At some stage in the past, our beggar practices were streamlined in such a way that we could only borrow or beg to meet capital, or development programmes.
Now we can borrow to pay government employees and other charges (OT), which gives dependency a new and menacing dynamic.
This has meant that when a donor government decides to withdraw its GBS grant, the beggar government finds itself in an awkward situation, for whereas a road construction programme can easily be put off or postponed, civil service pay and running the government cannot.
So, when the Brits announced, a couple of weeks ago, that they intend to cut their GBS handouts, the Tanzanian government put on a brave face, making it appear like it was a small matter. But it’s likely to hurt.
All this was, of course, before David Cameron made his remarks about his intention to cut aid to governments that suppress homosexual rights, so we don’t know what the real motive for the aid cut was.
African men are a macho lot, and for many the very idea of a man-on-man sexual partnership is anathema.
Woman-on-woman also. A man was created specifically to have liaison with a woman, and a woman was created as a tool, exclusively to serve the man, in both productive and reproductive pursuits.
It is inconceivable that two such tools would dream of having a liaison other than with the man.
Rather like the tractor dating the combine harvester on the farm.
Apart from the viewpoint of a woman being a centre for economic and biological production, I do not have much against those who claim that homosexuality is un-African.
But let us push this macho thing to its logical conclusion.
No self-respecting African man would let another man pay for his and his wife’s and his children’s upkeep.
Indeed, a man who allows that to happen would be considered as having been married by the provider man, call them economic homos. Rejecting the one, reject the other too.
SOURCE: The East African
6 Nov 2011
6.11.11
Evarist Chahali
RAIA MWEMA
No comments
CCM dhaifu mtaji imara wa urais CHADEMA, CUF
Uskochi
NIANZE makala hii kwa kutoa salamu za pongezi kwa jarida hili la Raia Mwemaambalo limetimiza miaka minne tangu kuanzishwa Oktoba 30, 2007. Binafsi, jarida hili limekuwa sehemu muhimu ya maisha yangu tangu nilipopewa fursa ya kuandika safu hii.
Lakini kubwa zaidi ni jinsi jarida hili lilivyosimama imara na kuwa sauti ya wasio na sauti (wanyonge), likifukua ufisadi na kuhabarisha umma pasipo upendeleo.
Pasi na shaka yoyote, Raia Mwema linastahili kuitwa gazeti la rekodi, yaani unaloweza kulitumia kunukuu chochote kile bila hofu kuwa huenda kimekosewa au kimeandikwa kwa unazi. Sitoi sifa hizi kwa vile ni mwandishi wa makala gazetini humu lakini ninaamini kila anayependa kuhabarishwa kwa ufasaha na umakini ataafikiana nami kuwa Raia Mwema limeonyesha njia sahihi ya uandishi wa habari na makala.
Baada ya pongezi hizo za dhati nielekee kwenye mada ya wiki hii. Mada hii ni mwendelezo wa ile ya wiki iliyopita ambayo iliangalia mazingira yanayotarajiwa ya chama tawala katika kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao hapo mwaka 2015.
Wiki hii ninajaribu kuangalia hali ilivyo katika vyama viwili, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF), ambavyo kwa sasa vinastahili kuitwa vyama vikuu vya upinzani.
Urais ndani ya CUF
Kuna msemo mmoja wa Kiingereza ambao katika tafsiri yake ya Kiswahili ni kama hivi: “Jambo zuri si lazima liwe jambo sahihi.” Kwa mfano, kumpatia chakula kingi mtu mwenye njaa kali kunaweza kusababisha kumuua mtu huyo bila kukusudia.
Mantiki ya usemi huo ni kwamba kuna nyakati tunafanya mambo kwa kuamini ni vizuri kufanya hivyo, lakini matokeo yake yanaweza kuwa mabaya kuliko matarajio. Kwa kurejea msemo huo wa Kiingereza, sote tunafahamu kuwa mtu mwenye njaa kali anahitaji chakula.
Lakini kabla ya kumpatia chakula ni vema kumpatia kinywaji cha moto kama vile chai au uji (kama wanavyofanya watu waliofunga). Kumpatia mtu huyo ugali mwingi kunaweza kusababisha akavimbiwa na pengine kuishiwa pumzi au hata kumpotezea uhai.
Chama cha CUF kililazimika kukaa meza moja na wapinzani wao wa CCM huko Zanzibar na hatimaye kufikia mwafaka na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Hilo lilikuwa jambo zuri (kama kumpatia chakula mtu mwenye njaa kali).
Lakini matokeo ya uamuzi huo wa busara yameiacha CUF huku Bara (na pengine hata huko Zanzibar) ikiwa haina mwelekeo. Kimsingi, chama hicho ni nusu ya serikali inayotawala kwa vile kimetoa Makamu wa Kwanza wa Rais kuongoza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Na katika kutekeleza kanuni ya uwajibikaji wa pamoja, CUF hawawezi kuinyooshea kidole CCM huko Zanzibar pindi mambo yakienda kombo.
Naomba ieleweke kuwa si kama ninailaumu CUF kwa kukubali mwafaka na CCM bali ninachoonyesha hapa ni madhara yasiyokusudiwa ya uamuzi huo. Ni vigumu kubashiri chama hicho kitaendeshaje kampeni “za maana” mwaka 2015.
Katika mazingira ya siasa za Zanzibar ni dhahiri kuwa kutakuwa na umuhimu wa kuendelea na serikali ya umoja wa kitaifa baada ya Uchaguzi Mkuu ujao.
Lakini ili hilo liwezekane itabidi kampeni katika uchaguzi huo ziwe za “kistaarabu” (ambalo ni jambo zuri isipokuwa tu linaweza kupunguza hamasa ya kisiasa kwa baadhi ya wapigakura).
Hoja hapa ni kwamba kama CCM itashinda na kisha kuunda serikali ya pamoja na CUF kuna haja gani basi ya kufanya kampeni za nguvu ambazo hazitabadili picha ya matokeo ya uchaguzi huo?
Na hata kama CUF wataamua waendeshe kampeni za nguvu ili kupata ushindi mkubwa, watawezaje kuonyesha kuwa CCM haistahili ushindi ilhali vyama vyote viwili vilikuwa madarakani (na hivyo kustahili sifa kwa mema au lawama kwa mabaya waliyofanya katika muhula wa 2010-2015)?
Kwa nini mazingira ya Zanzibar ni muhimu kwa hatima ya CUF kwa nchi nzima? Kwa sababu kila anayefahamu siasa za nchi yetu anatambua kuwa nguvu kubwa ya chama hicho ipo huko Visiwani. Lolote linalotokea huko linakigusa chama hicho kwa upande wa Bara na Muungano kwa ujumla.
Urais ndani ya CHADEMA
Sote tunakumbuka yaliyoikumba NCCR-Mageuzi baada ya mgombea wake Augustine Mrema kubwagwa na mgombea wa CCM, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, katika uchaguzi wa mwaka 1995.
Licha ya kushindwa katika chaguzi mbili mfululizo (mwaka 2005 na mwaka jana), CHADEMA imeendelea kuwa imara huku mgombea wake katika uchaguzi uliopita Dk. Willibrod Slaa akiendelea kuwa na hadhi ileile aliyokuwa nayo kama mgombea urais.
Kulikuwa na hofu kuwa laiti Dk. Slaa angeshindwa kwenye uchaguzi uliopita basi angepotea kabisa kwenye ulingo wa siasa za nchi yetu lakini hali imekuwa tofauti kabisa. Licha ya kubaki Katibu Mkuu tu wa CHADEMA (wadhifa aliokuwa nao kabla ya kugombea urais na kushindwa), mwanasiasa huyo ameendelea kuwa na mvuto mkubwa huku mikutano anayohutubia ikiendelea kupata wasilikizaji.
Lakini si Dk. Slaa pekee ambaye ameendelea kuwa na umaarufu na mvuto bali hata chama chake kimemudu kubaki tishio kwa chama tawala CCM.
Ukifuatilia kwa karibu malumbano ya kisiasa yanayoendelea nchini, unaweza kudhani kuwa bado tupo kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita au uchaguzi mwingine utafanyika hivi karibuni tu.
Moja ya mitaji mikubwa ya CHADEMA ni msimamo wake kuhusu mustakabali wa taifa. Chama hicho kimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kujitambulisha na kukubalika kama kitovu cha harakati za mapambano dhidi ya ufisadi.
Bahati nzuri kwa CHADEMA ni namna CCM inavyoshindwa kujiondoa kwenye utando wa ufisadi, ambapo pamoja na mambo mengine suala la kujivua magamba ni kama kuafikiana na CHADEMA kuwa CCM ni kichaka cha mafisadi na hivyo chama hicho kikongwe hakina budi kujisafisha.
Mtaji mwingine wa CHADEMA ni mshikamano miongoni mwa viongozi wake wakuu na wa kada ya kati. Sina hakika sana hali ipo vipi katika ngazi za chini lakini kwa kiasi kikubwa CHADEMA inainyima usingizi CCM.
Kama mazingira yatabaki jinsi yalivyo sasa, kuna uwezekano wa CHADEMA kumteua tena Dk. Slaa kuwa mgombea wake hapo 2015. Mwanasiasa pekee anayeweza kubadili hali hiyo ni Naibu Katibu mkuu wa chama hicho, Kabwe Zitto, ambaye aliwahi kunukuliwa akisema kuwa angegombea urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Mtaji mwingine mkubwa kwa CHADEMA ni hali ya mambo ndani ya CCM na mazingira yanavyotarajiwa kuwa katika mchakato wa chama hicho tawala kupata mgombea wake katika Uchaguzi Mkuu ujao (ambayo niliyaelezea kwa kirefu katika makala iliyopita).
Kama kuna nafasi yoyote kwa CHADEMA au chama kingine cha upinzani kuindoa CCM madarakani ni mwaka 2015 kwani kuna kila dalili kuwa sokomoko linaloendelea ndani ya chama hicho tawala litadumu hadi kitakapofanikiwa kupata mgombea wake. Laiti CHADEMA wakiafikiana mapema kuhusu mgombea wao katika uchaguzi huo basi watakuwa na muda wa kutosha kuandaa mazingira ya ushindi huku CCM wakiendelea kupigana vikumbo.
Lakini kuna busara moja ya kuzingatia katika msemo ufuatao: “Siasa si kama fumbo la hesabu ambapo siku zote 2 kujumlisha 2 jibu ni 4. Katika siasa jibu linaweza kuwa 100 au kwa kukatisha tamaa zaidi jibu likawa 0.” Licha ya kuwa siasa ni mchezo mchafu, kipindi cha miaka minne kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao ni kirefu sana katika siasa na lolote linaweza kutokea kinyume kabisa cha uchambuzi huu.
Katika moja ya makala zijazo nitaingia kwa undani kujadili mambo yanayoweza kuikwamisha CHADEMA (au chama kingine cha upinzani) kuing’oa CCM kwenye Uchaguzi Mkuu ujao. Lakini kwa leo tuishie hapa
Subscribe to:
Comments (Atom)












