16 Aug 2012


Kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu,makala yangu katika jarida la Raia Mwema toleo la Jumatano iliyopita (Agosti 8, 2012) haikuwekwa mtandaoni japo ipo gazetini.Kwa faida ya wasomaji,nimelazimika kuiweka hapa (inaweza kuwa na tofauti chache na iliyopo gazetini ambayo imehaririwa)


MAKALA YA RAIA MWEMA TOLEO LA AGOSTI 8
Kwa zaidi ya wiki moja sasa kumekuwepo habari zisizopendeza kuhusiana na tatizo la muda mrefu la mpaka kati ya Tanzania na Malawi.

Ningependa kukiri hadharani kwamba pamoja na kiu yangu kubwa ya ufahamu wa masuala mbalimbali sikuwahi kujibidiisha kufuatilia kwa undani chanzo cha tatizo hilo. Na pengine kuliita suala hilo ‘tatizo’ ni kulipunguzia uzito kwani ukichambua kwa makini kauli mbalimbali kutoka kwa baadhi ya viongozi wetu na wenzao wa Malawi, kinachoendelea hivi sasa kinaweza kabisa kuitwa ‘mgogoro wa mpaka kati yetu na Malawi.’

Katika baadhi ya mitandao ya jamii, ambayo baadhi yetu inatusaidia sana kufuatilia mambo mbalimbali huko nyumbani kumeanza kujitokeza hofu ya vita kati ya nchi hizi ambazo licha ya ujirani zina ukaribu mkubwa kwa sababu ya mwingiliano wa makabila.

Hata hivyo, wakati hofu hiyo ya vita kati yetu na Malawi ikianza kukua, kuna mambo kadhaa yanayopaswa kujadiliwa kwa uwazi. Lakini pia ningependa kuweka wazi msimamo wangu kuwa ninaamini ufumbuzi pekee na wenye manufaa katika mgogoro huu ni kwa njia za amani.

Na moja ya sababu kubwa ya kutaka mgogoro huu utatuliwe kwa njia za amani ni kumbukumbu niliyonayo ya vita pekee nilivyowahi kushuhudia katika uhai wangu hadi sasa. Bado nina kumbukumbu nzuri ya vita ya Kagera kati yetu na Uganda, ambapo wakati huo nilikuwa mtoto mdogo ninayeishi na wazazi mkoani Kigoma.

Moja ya kumbukumbu zinazoniogofya hadi leo ni pale wakazi wa mji huo walipotakiwa kuchimba mahandaki kama hatua ya kujilinda. Kulikuwa na taarifa kwamba ‘swahiba’ wa nduli Idi Amin wa Uganda, aliyekuwa Rais wa ‘Zaire’ (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo-DRC) dikteta Mobutu, alikuwa na mpango wa kumsaidia Amin kushambulia Kigoma hasa kwa vile mkoa huo unapakana na DRC.

Ninakumbuka hofu tuliyokuwa nayo kila tuliposikia mlio wa ndege angani, tukidhani ni ndege za Mobutu zimekuja kutuangamiza. Bahati nzuri hadi vita hiyo inamalizika hakukuwa na shambulio lolote kwa mji huo.

Kwa kuzingatia kumbukumbu hizo, nisingependa kuona Watanzania wenzangu wakirejea kwenye hofu kama hiyo iliyotukumba sie wakati wa vita hiyo kati yetu na Uganda.

Lakini kuna jambo jingine linalonipa hofu zaidi. Katika moja ya shahada zangu za Uzamili nimesoma Stadi za Vita (War Studies), na katika kozi hiyo tulitumia muda mwingi mwanafilosofia mahiri wa masuala ya vita, Mchina Sun Tzu. Moja ya mambo yanayousiwa na Sun Tzu kuhusu maandalizi ya vita ni hili

Sanaa ya vita inatufundisha sio kutarajia kuwa adui hatotuvamia bali maandalizi yetu katika kukabiliana nae, na sio katika uwezekano kuwa (adui) hatoweza kutuvamia bali uimara wa nafasi yetu ‘kutohujumika’ (unassailable).”

Licha ya sote kuwa na mapenzi kwa nchi yetu, tukiangalia mwenendo wa mambo huko nyumbani kwa sasa, jambo tusilotaka kabisa kusikia kwa sasa ni vita. Mmoja wa ukweli mchungu ni kwamba hadi sasa tumeshindwa kukabiliana na maadui kadhaa wa ndani ambao hawana silaha bali fedha na porojo zao. Hapa ninawazungumzia mafisadi na maharamia wengine wanaoifanya Tanzania yetu kuwa katika umasikini tusiostahili.

Lakini pia uimara wetu kukabiliana n adui si wenye kutoa matumaini. Katika siku za karibuni tumeshuhudia migomo ya madaktari na baadaye walimu, wote wakidai kuboreshewa maslahi yao. Wakati watawala wetu wanadai serikali haina fedha za kuboresha maslahi ya watumishi wake, imemudu kupandisha mishahara ya wabunge hadi kufikia shilingi milioni 11 kwa kila mmoja wao.

Je inawezekana chokochoko kutoka Malawi zinachangiwa na uelewa wa nini kinachoendelea nchini mwetu? Lakini hata kama hiyo si sababu, je katika mazingira haya ya kuendekeza anasa kwa tabaka dogo huku wengi wa wananchi wakizidi ‘kupigika’ kutokana na uchumi dhaifu unaozidi kudhoofeshwa na majambazi wanaopora raslimali zetu kila kukicha, tunaweza kweli kukabiliana na adui huku tukiwa na uhakika wa kumshinda?

Ninatambua kuwa ninaweza kuonekana msaliti kwa nchi yangu kwa kubainisha hoja hizo hapo juu lakini kama nilivyotanabaisha hapo awali, ningependa, na ninataraji, mgogoro huu utamalizwa kwa njia za amani.

Nimeeleza hapo mwanzo kuwa sikuwahi kujishughulisha kufuatilia chanzo cha mgogoro ‘wa muda mrefu’ wa mpaka kati yetu na Malawi. Lakini jitihada kidogo tu ziliniwezesha kukutana na makala ya kitaaluma, ambayo licha ya kuwa ilichapishwa mwezi Disemba mwaka 1973, bado ina maelezo muhimu kuhusu mgogoro huo.

Katika makala hiyo, The Malawi-Tanzania Boundary Dispute (mgogoro wa mpaka wa Malawi na Tanzania) iliyoandikwa na James Mayall, na ambayo ni mapitio ya kitabu (book review) kuna taarifa ambazo kwa namna flani zinatoa taswira ya ‘msimamo wa kukanganya’ kwa baadhi ya viongozi wetu, ikiwa ni pamoja na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

Kwa mujibu wa makala hiyo, awali viongozi wetu wakiongozwa na Nyerere waliridhia kuwa Ziwa si letu bali la Malawi. Kwa kiasi kikubwa msimamo huo ulionekana kuchagizwa na dhamira ya nchi yetu katika umoja wa nchi za Afrika.

Japo sitaki kuchukulia makala hiyo kama ukweli halisi kuhusu chanzo cha mgogoro huo, mwandishi alijitahidi kwa kiasi kikubwa kubainisha jinsi suala hilo lilivyochukuliwa kuwa la kiutawala zaidi kuliko la kisheria.

Inavyoelekea, kwa mujibu wa Mayall, moja ya sababu zilizopelekea nchi yetu kubadili msimamo wake wa awali kuwa Ziwa hilo si letu ni uhusiano wa karibu kati ya aliyekuwa Rais wa Malawi, dikteta Kamuzu Banda na utawala wa makaburu. Kama ambavyo inaelezwa kuwa moja ya vipaumbele vilivyopelekea Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ni sababu za kiusalama, umuhimu wa sehemu ya Ziwa hilo kumilikiwa nasi unaelekea kuchangiwa na sababu kama hizo.

Kadhalika, makala hiyo inajenga picha moja ambayo yayumkinika kuhisi kuwa inaweza kurandana na sababu za sasa za kurejea kwa mgogoro huo. Mwandishi Mayall alieleza kuwa katika wakati flani huko nyuma kulikuwa na hisia kwamba hoja ya Malawi kumiliki Ziwa lote ilihamasishwa na utawala wa Makaburu (waliokuwa wakitawala baadhi ya nchi za kusini kabisa mwa Afrika) na Wareno (waliokuwa wakitawala Msumbiji).

Kisichopendeza kwa Mtanzania yeyote kuhusu makala hiyo ni ukweli kwamba msimamo wa awali wa nchi yetu ulikuwa ni pamoja na kuwaachia Wamalawi waamue wenyewe ‘kutuachia’ sehemu ya Ziwa Nyasa na pia kauli mbalimbali zilizoonyesha kuafiki kuwa Ziwa hilo si sehemu ya nchi yetu, japo baadaye msimamo huo ulibadilika.

  Ningependa sana kuitafsiri makala hiyo nzima kwa Kiswahili lakini nafasi hairuhusu, na pengine kufanya hivyo kunaweza kuwavunja moyo baadhi ya Watanzania wenzangu na pengine kuanza kuamini kuwa sie ndio chanzo cha chokochoko zilizopelekea mgogoro huo kufikia hatua ya sasa. Hata hivyo, iwapo kuna msomaji atahitaji nimsaidie kutafsiri makala hiyo ya Kiingereza, nipo tayari kufanya hivyo.

Wakati ninajipa matumaini kuwa mgogoro huo utamalizwa kwa amani, ninajikuta nikikabiliana na maswali kadhaa ambayo ninachelea hata kudadisi majibu yake. Kwa mfano, itakuwaje iwapo Malawi watapuuza onyo lililotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe kuwa makampuni yanayojihusisha na uchimbaji raslimali katika Ziwa hilo yasitishe kazi mara moja?

Wakati viongozi kadhaa huko Malawi wametoa kauli za kuleta matumaini kuwa kilichopo si mgogoro kwa vile nchi zetu zipo katika mahusiano mazuri, takriban wote wanaonekana kuwa na msimamo unaorandana kwamba Ziwa Nyasa lote ni la nchi hiyo.
Hapo huhitaji uelewa wa mambo ya diplomasia kuhitimisha kuwa kinachoongelewa na viongozi hao ni kupunguza tu hofu kwa wananchi lakini pasipo kurudi nyuma katika msimamo kuwa Ziwa hilo ni lao lote na hawapo tayari kuliachia.

Lakini kuna swali jingine la msingi zaidi. Je jeuri ya Malawi inatoka wapi? Je inachangiwa na makampuni yanayochimba raslimali katika Ziwa hilo? Je inachangiwa na uelewa kuwa nchi yetu kwa sasa inakabiliwa na ‘mizigo mikubwa’ kiasi cha kuiaminisha nchi hiyo kuwa hatuna uwezo wa kuwakabili? Na swali ambalo pengine ni gumu zaidi, je tuna uwezo wa kurejea ‘tulichomfundisha Nduli Idi Amin mwaka 1978-79?

Ili uingie vitani ni lazima uwe na taarifa sahihi dhidi ya adui yako. Je taasisi zetu zinazoonekana kama zimesalimu amri kwa mafisadi wanaotafuna nchi yetu zina uwezo wa kukusanya taarifa muhimu za kiusalama ili pindi tukiamua ‘liwalo na liwe’ dhidi ya Malawi tusiishie kujilaumu?

Vyovyote itakavyokuwa (huku tukiamini kuwa hakutokuwa na haja ya matumizi ya nguvu kutatua mgogoro huo) suala moja muhimu ni kuutumia mgogoro huu kama fursa ya kusaka suluhisho la kudumu.Kama ambavyo matatizo ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unavyoendelea kuzalisha matatizo hususan kutokana na kukosekana utashi wa kisiasa kumaliza matatizo yaliyopo, mgogoro huu kati yetu na Malawi ambao umedumu kwa takriban nusu karne sasa unahitaji kumalizwa. Lakini ili hilo liwezekane ni muhimu kwa watawala wetu kuelewa vipaumbele vya taifa letu.

Na kwa vile katika mazingira tuliyonayo tunalazimika kuwa kitu kimoja (na kuweka kando ukweli kuwa baadhi ya wenzetu wameigeuza nchi yetu kuwa kitegauchumi chao) na tunalazimika pia kuwaamini watu walewale ambao ‘wanadai hawajui chanzo cha umasikini wetu’, basi ni muhimu Tuweke kando tofauti zetu na tuwe tayari kulinda na kutetea kile tunachoamini ni halali yetu.

Nimalizie kwa kutoa wito kuwa suala hili nyeti lisigeuzwe turufu ya kisiasa kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2015.Tusiruhusu wababaishaji wakurupuke na kauli za kusaka umaarufu pasipo kuwa na mikakati ya namna ya kutatua mgogoro huu kwa njia za amani.

Kwa jirani zetu wa Malawi na hususan Rais Banda, wito wangu kwao ni huu: amani ni muhimu kwetu sote, lakini wakati mwingine inalazimu kutumia mabavu ili kuleta amani ya kudumu. Pamoja na matatizo yetu, mie na pengine kila Mtanzania anaamini kuwa kamwe hatutoruhusu Ziwa Nyasa ligeuzwe ‘uwanja wa kutupima ubavu.’ Tulimsambaratisha Nduli Amin kwa sababu nia tulikuwa nayo, sababu tulikuwa nazo, na uwezo pia tulikuwa nao. Hata kama itaonekana kwa Wamalawi kuwa nia, sababu na uwezo wetu ni hafifu kwa sasa, hakuna Mtanzania aliye tayari kuona ardhi ya nchi yake ikimegwa au mipaka yetu ikichezewa.

Mwanafalsafa Sun Tzu anaonya; “gharama ya vita ni kubwa kuliko ushindi wowote utakaopatikana”   na “wanaoingia vitani hufanya hivyo wakiongozwa na ‘miscalculations’ hasa imani kuwa watashinda...lakini vita ikimalizika hujikuta wana hasara kubwa kuliko kabla hawajaingia vitani.

Mungu Ibariki Afrika

Barua-pepe: [email protected] Blogu: www.chahali.com   





9 Aug 2012




Picha zote mbili zinamwonyesha Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta alipotembelea maonyesho ya kilimo ya Nane Nane mkoani Morogoro.Katika picha zote,Waziri Sitta ameambatana na mlinzi (BODIGADI) kutoka Idara ya Usalama wa Taifa.Ninakumbuka,uamuzi wa kumpatia Sitta ulinzi ulifanywa na Serikali wakati waziri huyo alipokuwa Spika wa bunge lililopita,na alidai anatishiwa maisha.Je matishio hayo bado yanaendelea?Ikumbukwe,gharama za kutoa ulinzi kwa kiongozi ni kubwa sana,na kimsingi,kiprotokali,Sitta hastahili kuwa na bodyguard....unless tumembiwe kuwa tishio dhidi ya maisha yake bado lipo hai 



Picha kwa hisani ya AudifaceJackson Blog


8 Aug 2012

 


JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALI ASILI NA UTALII
 
 





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI – (PRESS RELEASE) ILIYOTOLEWA NA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. BALOZI KHAMIS .S. KAGASHEKI LIWALE
TAREHE 8/8/2012


NDUGU WAANDISHI WA VYOMBO VYA  HABARI:

1.0    SALAMU ZA JUMLA:
NACHUKUA NAFASI HII KUWAKARIBISHA NA KUWAPONGEZA KWA JINSI MNAVYOSHIRIKIANA NA WIZARA HII KUPIGA VITA UHALIFU / UJANGILI WA RASILIMALI ZA TAIFA. AIDHA NATAMBUA JINSI MLIVYOTENGA MUDA WENU  NA KUFIKA HAPA ILI TUPEANE TAARIFA ZA KIUTENDAJI HUSUSANI OPERESHENI INAYOENDELEA KATIKA WILAYA YA LIWALE MKOA WA  LINDI.

NDUGU WANAHABARI:
2.0           UTEKELEZAJI WA  OPERESHENI:
KUMEKUWA NA ONGEZEKO LA VITENDO / WIMBI LA UHALIFU / UJANGILI WA NYARA ZA SERIKALI AMBAO UNAATHIRI RASILIMALI ZA TAIFA HUSUSANI WANYAPORI TEMBO, VIBOKO, SIMBA, MAMBA, TWIGA, NYATI NA WANYAMA WENGINE PAMOJA NA UVUNAJI HARAMU WA MAZAO YA MISITU. KUTOKANA NA HALI HIYO, WIZARA YA MALI ASILI NA UTALII ILIOMBA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI KUPITIA WIZARA YA MAMBO NDANI YA NCHI KUANDAA OPERESHENI MAALUM WILAYANI LIWALE KUDHIBITI HALI HIYO. JESHI LA POLISI LILIKIAGIZA KITENGO CHA KUPAMBANA NA UHALIFU MKUBWA NCHINI (NATIONAL AND TRANSNATIONAL SERIOUS CRIME INVESTIGATION UNIT – NATIONAL TASK FORCE) AMBACHO KINAVISHIRIKISHA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VYA (POLISI, JWTZ, TISS, MAGEREZA, UHAMIAJI NA OFISI YA DPP) KUTEKELEZA MAJUKUMU YA OPERESHENI MAALUM KAMA ILIVYOELEKEZWA. OPERESHENI HII ILIANZA TAREHE 22/07/2012  NA NI ENDELEVU. KATIKA OPERESHENI HIYO MAOFISA WAKUU WAANDAMIZI, MAOFISA WA KATI, WAKAGUZI NA ASKARI WA KAWAIDA KUTOKA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA TAJWA HAPO JUU WANASHIRIKI UTEKELEZAJI WA OPERESHENI HIYO.  

MATOKEO YA AWALI YA UTEKELEZAJI WA OPERESHENI HII NI KAMA IFUATAVYO;
v WATUHUMIWA 101 NA KESI 101 ZIMEFUNGULIWA KITUO CHA POLISI LIWALE KATI YA HIZO:

i.                     KESI  15 ZIMEFIKISHWA MAHAKAMANI NA MIONGONI MWAKE KESI MOJA (1) IMETOLEWA HUKUMU NA ZILIZOBAKI ZIKO KWENYE HATUA MBALIMBALI MAHAKAMANI,

ii.                  KESI 20 ZIMESIKILIZWA NA KUPATA HUKUMU YA “BINDING OVER”, MIONGONI MWAKE KESI 7 ZIMEPATA MAAMUZI NA 13 ZINASUBIRI MAAMUZI YA MAHAKAMA. MASHARTI YA “BINDING OVER” YALIYOTOLEWA YAMETOLEWA DHIDI YA WATUHUMIWA;
a.                 KUTOTOKA NJE YA WILAYA YA LIWALE BILA KIBALI CHA HAKIMU MKAZI WA WILAYA

b.                KURIPOTI KWA OC CID KITUO CHA POLISI LIWALE  KILA MWISHO WA MWEZI

c.                 KUITWA KUHOJIWA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA WAKATI WOWOTE KADRI ITAKAVYOONA INAFAA
d.                KUTOFANYA KOSA LOLOTE NDANI YA MIAKA MIWILI YA MATAZAMIO

e.                 KWA WALIOKUWA WAMILIKI WA SILAHA, SILAHA ZAO ZIMEHODHIWA POLISI LIWALE KWA MUDA WA MIAKA MIWILI NA MMILIKI ATAWAJIBIKA KUANZA TARATIBU ZA MAOMBI YA KUMILIKI SILAHA HIYO / HIZO UPYA PINDI UTEKELEZAJI WA HUKUMU HIYO ITAKAPOMALIZIKA

f.                  KUWEKA DHAMANA YA MALI ISIYOHAMISHIKA YENYE THAMANI YA TSH. 5,000, 000.00 NA MALI HIZO ZIWE NDANI YA WILAYA YA LIWALE


II.        KESI 66 ZINAENDELEA KUFANYIWA UCHUNGUZI ILI WAHUSIKA WAFIKISHWE MAHAKAMANI
v AIDHA KATIKA OPERESHENI HII VIJIJI 27 VYA WILAYA YA LIWALE VINGI VIKIWA VIMEPAKANA NA HIFADHI YA SELOUS VIMEHUSIKA. MATOKEO YAKE NI KUPATIKANA KWA SILAHA 80, RISASI 674 NA MAGANDA YA RISASI 289 KAMA IFUATAVYO;
v BUNDUKI 79 ZILIZOKAMATWA NI;
i.                    SAR - 1,
ii.                RIFLE - 16
iii.             SHOT GUN  - 63

v JUMLA YA RISASI 645 ZIMEKAMATWA NI;
i.                    SAR - 20,
ii.                RIFLE - 8
iii.             SHOT GUN – 647

v MAGANDA YA RISASI 289 YALIYOKAMATWA NI  ;
i.                   RIFLE - 99
ii.                 SHOT GUN – 190

v NYARA ZA SERIKALI;
SN
AINA YA NYARA ZILIZOKAMATWA
KIASI
THAMANI TSH
1
MENO YA KIBOKO,
80
18,892,500.00
3
MENO YA TEMBO
14
164,075,000.00
5
BANGILI MOJA YA USINGA WA MKIA WA TEMBO
1
23, 625, 000.00, 
6
NGOZI  ZA SIMBA,
2
15,435,000.00
7
NGOZI YA CHUI,
1
5,505,500.00
9
MIKIA MIWILI YA NGEDERE
2
378,000.00
10
KICHWA CHA NYATI CHENYE PEMBE 2,
1
2,992,500.00
11
NYAMA YA  NYATI ,
KG
2,988,700.00
12
KICHWA CHA POFU CHENYE PEMBE 2,
1
2,677,500.00
JUMLA KUU
212,944,700.00

v VIELELEZO VINGINEVYO
o       GARI NDOGO AINA YA  TOYOTA CORONA NO. T. 836 ADV 

o       PIKIPIKI MBILI ZA SANLG T. 901 BXQ NA T. 772 BSD

o       MSUMENO WA MBAO NA MBAO 149



3.0    LENGO LA OPERESHENI;
OPERESHENI HII MAALUM INALENGA KUZUIA, KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA UHALIFU / UJANGILI KATIKA MAENEO MBALIMBALI NCHINI WILAYA YA LIWALE IKIWA KAMA ‘ROLE MODEL’.

4.0           MAFANIKIO;
I.                  KWA KUWA OPERESHENI HII IMEPANGWA NA KUENDESHWA KITAALAM NA KISAYANSI (INTELLIGENCE LED OPERATIONS), MAFANIKIO YAFUATAYO YAMEJIDHIHIRISHA;

a.                 IMEUNGWA MKONO NA KUSIFIWA NA RAIA NA WANANCHI KWA UJUMLA KWA MAELEZO KUWA HAKUNA MTUHUMIWA ALIYEKAMATWA KWA KUONEWA.

b.                 KUMEKUWEPO NA MAPOKEO CHANYA (POSITIVE IMPACT) KUTOKANA NA WANANCHI KUTAMBUA KUWA MWENENDO WA OPERESHENI HII UNAIPA HESHIMA KUBWA SERIKALI

c.                 HAKUKUWA NA RAIA MWEMA ALIYEBUGHUDHIWA AU KULALAMIKIA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA OPERESHENI HII

ii.                MTANDAO WA UHALIFU WA UJANGILI UNAVUNJWA NA WAHUSIKA WOTE SASA WANAFAHAMIKA NA UCHUNGUZI MAKINI NA WA KINA UNAENDELEA DHIDI YAO NA WATAFIKISHWA MBELE YA MAHAKAMA NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE

iii.             BAADHI YA WAZEE WENYE UMRI MKUBWA NA AMBAO AFYA ZAO ZILIONEKANA KUTOMUDU MASHARTI YA KUENDELEA KUMILIKI SILAHA WALIZISALIMISHA WENYEWE NA KUOMBA ZIHIFADHIWE KATIKA KITUO CHA POLISI LIWALE MPAKA MAAMUZI YATAKAPOTOLEWA NA MAHAKAMA DHIDI YA SILAHA HIZO.

iv.             WALE AMBAO MAHAKAMA ITAONA WAMEPOTEZA SIFA ZA KUMILIKI SILAHA ZITAHODHIWA KITUO CHA POLISI KUSUBIRI UTEKELEZAJI WA MAAMUZI YA MAHAKAMA


5.0           CHANGAMOTO:
i.                   BAADHI YA WAMILIKI WA SILAHA SIO WAAMINIFU    KWA KUWA WANATUMIA SILAHA ZAO KUFANYA UJANGILI AU KUZIAZIMISHA KWA MAJANGILI. 

ii.                BAADHI YA WAMILIKI WA SILAHA WAMEPOTEZA SIFA ZA UMILIKI KUTOKANA NA MATATIZO YA KIAFYA; MFANO KUKABILIWA NA UPOFU, UGONJWA WA KIHARUSI N.K JAMBO AMBALO LINACHANGIA WAO KUSHINDWA KUZINGATIA NA KUTEKELEZA TARATIBU ZA UMILIKI WA SILAHA

6.0           MUONO WA MBELE (WAY FORWARD);
i.                   WIZARA YA MALI ASILI NA UTALII ITAENDELEA KUTOA ELIMU KWA JAMII ZINAZOISHI KANDOKANDO YA MAPORI YA AKIBA /  HIFADHI KUHUSU UMUHIMU WAO WA KUTOJIHUSISHA NA UJANGILI NA WAWE VYANZO VYA TAARIFA ZA KIINTELIJENSIA KUFUATIA MKAKATI MADHUBUTI WA KUDHIBITI MTANDAO WA UJANGILI NCHINI.

ii.                UTAKUWEPO MWENDELEZO WA KUBORESHA NA KUIMARISHA DORIA, MISAKO NA HATUA NYINGINE ZA KIOPERESHENI KWENYE MAPORI YA AKIBA NA HIFADHI ZA TAIFA MARA KWA MARA KUFUATIA MUONGOZO WA TAARIFA ZA KIINTELIJENSIA KADRI ITAKAVYOONEKANA INAFAA KATIKA KUFANYA OPERESHENI ZA PAMOJA (JOINT OPERATIONS INVESTIGATIONS & INTELIGENCE –JOII)  KWA KUTUMIA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUPITIA “TASK FORCE” YA KITAIFA .

7.0    MWISHO
NAWAPONGEZA MAOFISA WAANDAMIZI, MAOFISA WA KATI, WAKAGUZI NA ASKARI WA VYEO MBALIMBALI WANAOSHIRIKI UTEKELEZAJI WA OPERESHENI HII INAYOENDELEA. KWA UJUMLA NAMALIZIA KWA KUWASHUKURU TENA NYINYI WANAHABARI MLIOFIKA HAPA KWA USHIRIKIANO MNAOUTOA KATIKA KUPAMBANA NA UHALIFU HUU.


ASANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA
//////////////////////////////////////////MWISHO///////////////////////////////////////

IMETOLEWA TAREHE  08/08/2012  NA

MHE. BALOZI KHAMIS .S. KAGASHEKI (MB)
WAZIRI


NAKALA KWA:
VYOMBO VYA HABARI

6 Aug 2012

Champion again: Jamaica's Usain Bolt crosses the finish line to win gold in the men's 100-metre final in the Olympic Stadium in London
BOLT AKIVUKA MSTARI NA KUSHINDA


Outright winner: Usain Bolt streaks clear of the field to claim gold from lane seven in one of the most eagerly awaited Olympic events ever
USAIN BOLT AKIMALIZA MBIO NA KUSHINDA 



Showman: Usain Bolt celebrates his victory by striking his customary lightning bolt pose in the Olympic Stadium in London
USAIN BOLT AKIONYESHA POZI YAKE MAARUFU YA 'RADI' (LIGHTNING BOLT) BAADA YA KUSHINDA


Points ahead: Usain Bolt proved his doubters wrong and retained the Olympic 100m title he first won in Beijing in 2008
USAIN BOLT AKIWEKA POZI YAKE BAADA YA KUSHINDA


Taking a bow: Jamaica's Usain Bolt kneels and rests his head against the track in the Olympic Stadium after recording the second-fastest time ever
USAIN BOLT AKIINAMISHA KICHWA ARHDINI BAADA YA KUSHINDA


Star attractions: Jamaican sprinters Usain Bolt (right) and Yohan Blake (left) are mobbed by fans after winning gold and silver in the race
USAIN BOLT NA YOHAN BLAKE WAKISHANGILIA NA MASHABIKI


Golden boy: The Olympic champion in typical pose with the Olympic mascot
USAIN BOLT AKIWA NA MDOLI (MASCOT) WA OLIMPIKI


They're off: Usain Bolt (third left) did not start well in lane seven but he was comfortably leading the field as the athletes entered the final 20 metres
USAIN BOLT HAKUANZA VIZURI SANA KWENYE MSTARI (LANE) WA SABA LAKINI AKAMUDU KUSHINDA KWA KISHINDO


Effort: The world's fastest men - Usain Bolt (second left), Justin Gatlin (left), Yohan Blake (second right) and Tyson Gay (right) - strive to reach the line first
BINADAMU WENYE KASI KULIKO WOTE DUNIANI


Storming in front: Bolt (second left) crosses the finish line first, ahead of fellow Jamaican Yohan Blake (second right) and bronze medallist Justin Gatlin (centre)
NI USAIN BOLT TENA


Global appeal: Some 80,000 spectators in the Olympic Stadium watched the 100-metre race, as well as an estimated worldwide television audience of up to two billion
USAIN BOLT AKIMALIZA MBIO KWA KISHINDO


Picture perfect: Cameras flash as spectators capture the moment that Usain Bolt left his competitors in his wake
BINADAMU MWENYE KASI ZAIDI USAIN BOLT AKIWEKA REKODI MPYA YA OLIMPIKI HUKU PATNA WAKE  WA MAZOEZI ,MJAMAIKA YOHAN BLAKE (WA TATU KULIA) AKISHIKA NAFASI YA PILI NA MMAREKANI JUSTIN GATLIN (WA TATU KUSHOTO) AKISHIKA NAFASI YA TATU


Number one: Usain Bolt raises a finger after clinching victory, with the time reading 9.64 seconds on the electronic board behind. The time was later officially rounded down to 9.63 seconds
USAIN BOLT AKIWEKA REKODI MPYA 


Rapid results: Bolt ran the second-fastest time ever - an Olympic record of 9.63 seconds. Yohan Blake won silver with a time of 9.75 and Justin Gatlin took bronze in 9.79. Seven men clocked a time below 10 seconds
MATOKEO


World order: American bronze medallist Justin Gatlin (left) can only look on with envy as Jamaica's Usain Bolt (right) rewrites Olympic history once again
MWANARIADHA WA MAREKANI JUSTIN GATLIN ALIYESHIKA NAFASI YA TATU AKIMWANGALIA USAIN BOLT



On fire: Usain Bolt runs past the Olympic flame after winning the sprint final for Jamaica in scintillating fashion
USAIN BOLT AKIPITA PEMBENI YA 'MWENGE WA OLIMPIKI'  BAADA YA KUSHINDA MBIO ZA MITA 1OO WANAUME


Out of contention: Usain Bolt's Jamaican team-mate Asafa Powell, who pulled up injured during the race, looks forlorn after finishing eighth
MWANARIADHA WA JAMAIKA ASAFA POWEEL AKIWA AMESHIKA TAMA BAADA YA KUMALIZA WA MWISHO KUFUATIA MATATIZO YA MISULI


Bolt's our boy: Fans in Brixton watch Usain storm to victory in the 100m
MASHABIKI KATIKA KITONGOJI CHA BRIXTON JIJINI LONDON WAKISHANGILIA USHINDI WA USAIN BOLT


Fans who watched the race at the O2 Arena salute their hero with his 'Lightning Bolt' pose
MASHABIKI WAKISHANGILIA KWENYE UWANJA WA O2 HUKU WAKIONYESHA POZI YA USAIN BOLT


By Royal appointment: The Duke and Duchess of Cambridge and Prince Harry, sitting in front of the Culture Secretary Jeremy Hunt, were among the 80,000 spectators inside the Olympic Stadium
DUKE NA DUCHESS WA CAMBRIDGE NA PRINCE HARRY WAKIWA NA 'WAZIRI' WA UTAMADUNI JEREMY HUNT (NYUMA YA DUKE)



Behind Bolt: Prince Harry wore Jamaican colours as he accompanied his brother and sister-in-law at the athletics
DUKE NA DUCHESS WA CAMBRIDGE (PRINCE WILLIAM NA MKEWE KATE MIDDLETON-WA KWANZA NA WA PILI KUSHOTO) WAKIFUATILIA KASI YA USAIN BOLT HUKU PRINCE HARRY AKIWA AMEJITUNDIKA BENDERA YA JAMAIKA


Psyched: Jamaica's Yohan Blake, pictured gesturing prior to competing in his semi-final, was one of the favourites for the Olympic title as he came into the race in excellent form
YOHAN BLAKE, PATNA WA MAZOEZI WA USAIN BOLT ALIKUWA AKITARAJIA KUTOA UPINZANI MKALI LAKINI AKAISHIA KUWA WA PILI


Fighting fit: Usain Bolt, who had been troubled by a hamstring injury, claimed he was only 95 per cent fit but he looked in fine condition before the eagerly awaited final
USAIN BOLT AKIFANYWA MBWEMBWE KABLA YA MCHUANO


Fervour: Spectators from the Jamaican community in Brixton, south London, watch their heroes in action on television on the 50th anniversary of the Caribbean island's independence from Britain
JUMUIYA YA WAJAMAIKA KATIKA KITONGOJI CHA BRIXTON,JIJINI LONDON WAKIFUATILIA USHIRIKI WA WANARIADHA WAO 


CHANZO: Daily Mail

5 Aug 2012


Makada wa CCM wakiwa na kadi za  uwanachama kwa wanachama wapya  katika futari ya pamoja ilioandaliwa na tawi la CCM DMV Jana Ijumaa Aug 3, 2012 katika ukumbi wa Hillandale Park iliyopo Silver Spring, Maryland Nchini Marekani.

Mwenyekiti wa tawi la CCM DMV Loveness Mamuya akipata picha na tikiti maji lililochongwa kwa longo ya Chama cha CCM, katika futari ya pamoja ilioandaliwa na tawi la CCM DMV Jana Ijumaa Aug 3, 2012 katika ukumbi wa Hillandale Park iliyopo Silver Spring, Maryland Nchini Marekani.

Tikiti maji lililochongwa kwa longo ya Chama cha Mapenduzi CCM

  
Baadhi ya waTanzania mbali mbali waliohudhuria kwenye futari hiyo ilioandaliwa na tawi la CCM DMV

Baadhi ya waTanzania waliovalia rangi za chama cha CCM wakiwa kwenye futari ya pamoja ilioandaliwa na tawi la CCM DMV, Jana Ijumaa Aug 3, 2012 katika ukumbi wa Hillandale Park iliopo Silver Spring, Maryland Nchini Marekani.

  Makada wa CCM Tawi la DMV shoto Mbunifu wa Ma Winny Casey Khanga Wrap Designer, pamoja na Peter Ligate (Picha ya kulia) wakiwa katika mpango mzima wa futari ya pamoja ilioandaliwa na wanatawi la CCM DMV

Watanzania  waliojumuika  kwenye futari ya pamoja ilioandaliwa na tawi la CCM DMV, Jana Ijumaa Aug 3, 2012 katika ukumbi wa Hillandale Park iliopo Silver Spring, Maryland Nchini Marekani.

  
Mwenyekiti wa tawi la CCM DMV Loveness Mamuya akiwakaribisha rasmi  wageni walikwa  kwenye futari ya pamoja ilioandaliwa na tawi la CCM DMV, Jana Ijumaa Aug 3, 2012 katika ukumbi wa Hillandale Park iliopo Silver Spring, Maryland Nchini Marekani.


Baadhi ya wanachama wa  CCM Tawi la DMV wakipata picha ya pamoja baada ya futari walioiyanda 


Wanachama wa  CCM Tawi la DMV na baadhi ya wageni wawili kutoka Londan Uingereza

Wageni wawili majirani wapendanao kutoka jijini London pia walihudhuria katika futari hiyo ilioandaliwa na  ilioandaliwa na tawi la CCM DMV Jana Ijumaa Aug 3, 2012 katika ukumbi wa Hillandale Park iliyopo Silver Spring, Maryland Nchini Marekani


Katibu wa CCM DMV Jacob Kinyemi, kushoto akipata picha ya pamoja na  Halima baada ya kumkabidhi rasmi kadi ya uwanachama wa CCM, Jana Ijumaa  na kuwa mwanachama rasmi wa CCM



Chanzo: SWAHILIVILLA

4 Aug 2012

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.