11 Nov 2013
7 Nov 2013
7.11.13
Evarist Chahali
RAIA MWEMA
No comments
.jpg)
KATIKA moja ya makala zangu huko nyuma nilitaja kitabu fulani ambacho kwa muda mrefu kimekuwa kikinipa mwongozo katika mazingira tofauti. Kitabu hicho kinaitwa ‘48 Laws of Power’ (Kanuni 48 za nguvu, kwa tafsiri isiyo rasmi).
Robert Greene, mwandishi wa kitabu hicho ambacho miongoni mwa ‘waumini’ wake wasanii Will Smith na Jay-Z, ambao ni maarufu nchini Marekani na duniani kwa ujumla, anakanusha vikali madai kuwa kitabu hicho ni ‘Biblia ya mwendawazimu.’
Anasema tofauti na Biblia Takatifu ambayo inategemea zaidi kwenye upendo na mambo mema, hali halisi duniani ni tofauti: kuna maadui na watu wenye roho mbaya; kuna maharamia ambao ukifuata mafundisho ya Biblia kuwa “mtu akikupiga kofi shavu la kushoto, mgeuzie na shavu la kulia” watakumwagia tindikali uso wako kama si kung’oa meno na kucha.
Kwa kifupi, kitabu hicho kinatoa mwongozo wa jinsi ya kupata nguvu, kutathmini nguvu, na jinsi ya kujikinga dhidi ya nguvu za wengine.
Kwa nini nimeanza makala hii kwa kukumbushia kuhusu Kanuni 48 za Nguvu? Jibu ni kwamba dhima ya makala hii ni kujadili harakati za kusaka nguvu ndani ya chama kikuu cha upinzani huko nyumbani (Tanzania), yaani CHADEMA.
Kanuni ya 4 ya Nguvu (4th Law of Power) inaonya: “ Usiongee sana zaidi ya inavyopaswa: kadri unavyojaribu kuridhisha watu kwa maneno, ndivyo kadri utakavyoongea zaidi, na kuonekana ‘mtu wa kawaida’... Watu wenye nguvu hujenga heshima na kuogofya kwa kuongea maneno machache. Kadri unavyoongea maneno mengi ndivyo kadri unavyokuza uwezekano wa kuonekana mpumbavu.”
Kanuni ilipaswa kuzingatiwa na Mbunge wa CHADEMA, Godbless Lema ambaye kwa siku za hivi karibuni amekuwa katika malumbano makali na mbunge mwenzie kutoka chama hicho, Zitto Kabwe, kuhusu suala la posho kwa wabunge.
Kilichonikera kuhusu Lema ni ukweli kwamba alipotoa taarifa katika mtandao wa Jamii Forums kuwa kesho yake angeandika makala kuhusu ‘Unafiki wa Zitto kuhusu suala la posho’ nilimjibu kwa kumtafadhalisha kutofanya hivyo, nikimkumbusha kuwa malumbano hayo hayana manufaa kwa chama chao. Kwa bahati mbaya au makusudi alipuuza ushauri wangu.
Labda nimuulize Lema, baada ya kuandika makala hiyo ya ‘kumsuta’ Zitto, CHADEMA imejipatia wapiga kura wangapi kwa minajili ya kukiingiza chama hicho Ikulu mwaka 2015? Kwa kuutangazia umma kuwa Naibu Katibu wake Mkuu (Zitto), Lema ameisaidiaje CHADEMA kujenga dhana kwa Watanzania kuwa ni chama kilicho tayari kuwa mbadala wa CCM pindi chama hicho tawala kiking’oka madarakani?
Hivi kulikuwa na ugumu gani kwa Lema kumtafuta Zitto baada ya vikao vya Bunge au kwenye simu na kujadili tofauti zao ‘ki-utu uzima’? Pamoja na kuthamini mchango wake katika siasa za upinzani huko nyumbani, ninaomba kuhitimisha kuwa alichofanya Lema ni dalili za ‘utoto wa kisiasa’ (political immaturity).
Kanuni ya 9 ya Nguvu (9th Law of Power) inausia: “Ushindi unaopatikana kupitia malumbano una madhara yake. Chuki itakayozalishwa kutokana na ‘ushindi’ huo itadumu kwa muda mrefu...Ni vema kuwafanya watu waafikiane nawe kutokana na matendo na sio maneno yako.” Yawezekana Lema akahisi ameshinda katika hoja yake ya kujenga picha kuwa ‘Zitto ni mnafiki,’ lakini kwa gharama ipi, kwa manufaa ya nani na hatma ya ‘ushindi’ huo ni ipi?
Hivi baada ya malumbano hayo ya mitandaoni kati ya Lema na Zitto kuna uwezekano wowote wa wanasiasa hao kusimama jukwaa moja kunadi mgombea wa chama chao? Je, wanaweza kukaa pamoja kujenga hoja yenye maslahi kwa chama chao au wapigakura wao?
Kanuni ya 19 ya Nguvu (19th Law of Power) inafundisha; ‘Kuna aina mbalimbali za watu ulimwenguni na kamwe usidhani kuwa kila mtu atafanya mambo kulingana na matarajio yako. Msaliti au mwajibishe mtu wa aina fulani basi mtu huyo atatumia uhai wake wote akisaka fursa ya kulipa kisasi...Chagua maadui zako kwa makini, na kamwe usimkosee mtu asiyestahili kukosewa.”
Hata kwa mie ambaye si ‘shabiki wa Zitto,’ aliyoyaandika Lema huko mitandaoni yangeweza kuniacha na kinyongo dhidi yake. Pengine Zitto ni ‘malaika’ ambaye atachukulia kauli za Lema kama sehemu tu ya maisha ya kisiasa, lakini kuna mashabiki wake (Zitto) ambao huenda si ‘malaika’ kama yeye. Je, vinyongo vyao havina madhara kwa mustakabali wa CHADEMA?
Na tutarajie nini iwapo hata Zitto si ‘malaika’ (kwa maana kwamba akifanyiwa jambo baya analea kinyongo)?
Lakini kosa jingine la Lema ni kupuuzia Kanuni ya 43 ya Nguvu (43rd Law of Power) inayofundisha “Ubabe hupelekea matokeo yatakayokuwa dhidi yako. Ni lazima uwashawishi watu watake kufuata mwelekeo wako. Mtu aliyeshawishika kufuata mwelekeo wako anakuwa mfuasi wako mtiifu...Lainisha upinzani kwa kufanyia kazi hisia zao, kwa ‘kucheza’ na kile wanachokithamini na wanachokiogopa. Puuza matamanio ya wengine, basi nao watakupuuza.”
Mpende au mchukie, Zitto ana turufu kubwa zaidi ya Lema katika ajenda kuu ya CHADEMA ya kupambana na ufisadi. Kuna Watanzania wengi tu wanaomwona kama ‘mpiganaji halisi’ wa maslahi yao: kuanzia ‘ishu’ ya Buzwagi hadi kwenye kufuatilia ‘mabilioni yaliyofichwa Uswisi’ sambamba na ‘vita yake mpya’ dhidi ya ukwepaji kodi.
Kwa Lema kutumia ‘ubabe’ kwenye mitandao ya kijamii ilhali hana ‘kete muhimu’ ya kuwafanya Watanzania wengi zaidi wampende, anaweza kuwa amewapa sababu baadhi yao kumchukia kwa ‘kumwandama shujaa wao Zitto.’
Kadhalika, Lema angeweza kabisa kusaka kuungwa mkono na Watanzania katika hoja yake ya ‘unafiki kuhusu posho za wabunge’ kwa kuwashawishi Watanzania (badala ya kumwandama Zitto) kuwa tatizo sio posho bali mantiki yake (yaani kuwajali wabunge na kuwapuuza watumishi wengine wa umma).
Vile vile Lema alipaswa kutambua kuwa ajenda zinazompa umaarufu Zitto sio kususia posho huko bungeni bali masuala muhimu zaidi kama kufuatilia mabilioni ya Watanzania yaliyoibwa na kufichwa huko Uswisi. Iwe Zitto amedhamiria kwa dhati ‘kufa na mafisadi wa mabilioni hayo’ au anatumia suala hilo kama mtaji tu wa kisiasa, ukweli unabaki kuwa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa ‘kulainisha’ upinzani kwa kufanyia kazi hisia zao, kwa kucheza na kile wanachokithamini (stahili zao) na wanachokiogopa (ufisadi).”
Kwa Lema ku-“puuza matamanio ya wengine (walalahoi wanaotamani kuona Zitto anapambana na mafisadi), basi nao watampuuza (hasa kwa vile utetezi wowote kwa posho za wabunge unatafsiriwa kuwa ni usaliti kwa walalahoi).”
Huko nyuma, kiongozi mmoja wa vitengo vya CHADEMA aliniomba msaada wa kusaidia kukijenga chama hicho huku Ughaibuni. Niliafiki ombi hilo kwa vile ninaunga mkono ajenda za CHADEMA dhidi ya mafisadi. Hata hivyo ningefanya hivyo kama Mtanzania mwenye mapenzi kwa nchi yake lakini sio mwanachama wa chama hicho. Sijui hakupenda msimamo wangu au vipi, akapotea moja kwa moja.
Baadaye akajitokeza kijana mmoja aliyepo kwenye kitengo fulani nyeti cha chama hicho. Kwa kuridhishwa na utendaji kazi wake, nikatoa ‘ofa ya msaada wa kitaalamu.’ Nikampatia ‘jukumu fulani,’ na huo ndio ukawa mwisho wa mawasiliano yetu.
Mifano hiyo miwili, ukijumlisha na ushauri wangu kwa Lema kumsihi asibandike ‘post’ ya kumkosoa kiongozi mwenzie wa CHADEMA (Zitto) mtandaoni kisha akapuuza, inanifanya nikitazame chama hicho kama ambacho aidha kinajiamini sana kiasi kwamba hakioni umuhimu kwa kujijenga au kinadhani kimekamilika katika nyanja zote kiasi kwamba misaada japo ya ushauri tu haina umuhimu kwake.
Nihitimishe makala hii kwa Kanuni nyingine ya Nguvu (5th Law of Power) inayotahadharisha “Kila kitu kinategemea hadhi yako: ilinde kwa nguvu zako zote maishani...Hadhi ni msingi wa nguvu. Hadhi peke yake inaweza kukufanya ushinde au uogopwe, lakini ikiponyoka itakudhoofisha na utaandamwa kila upande...” Kinachoendelea ndani ya CHADEMA sasa hivi sio tu kinakishushia hadhi chama hicho bali pia kinawafanya Watanzania walioanza kukiamini chama hicho wajione kama ‘wameingizwa mkenge’ (wamesalitiwa). Usipoziba ufa utajenga ukuta
6 Nov 2013
4 Nov 2013

Makala hii iliandikwa kwa minajili ya kuchapishwa katika jarida la Raia Mwema toleo la Oktoba 23. Hata hivyo haikuchapishwa kwa madai kuwa ilikuwa inapromoti msanii Fid Q na wimbo wake mpya wa Siri ya Mchezo. Whether uamuzi wa jarida hilo ni sahihi au la, nimeonelea ni vema kuichapisha makala hiyo hapa bloguni
MAKALA YA RAIA MWEMA
TOLEO LA OKTOBA 23, 2013
Nianze makala hii
kwa kuomba radhi kutokana na kuadimika kwangu katika toleo lililopita. Hali
hiyo ilitokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu.
Uandishi wa makala
zangu umekuwa sehemu muhimu ya maisha yangu, na pindi ikipita wiki pasi
kuandika chochote (kama ilivyokuwa wiki iliyopita) huwa najisikia kama
nimepungukiwa na kitu flani.
Pamoja na kiu yangu
kubwa ya kuhamasisha mijadala mbalimbali, kukemea maovu na hata kuhabarishana
tu, moja ya hamasa kubwa zinazonifanya niendelee na jukumu hili ni mapokeo ya
wasomaji mbalimbali.
Na wiki iliyopita
nilipata hamasa kubwa kutoka kwa msanii maarufu wa muziki wa Bongofleva, Fareed
Kubanda, au 'Fid Q' kwa jina la kisanii.
Msanii huyo ametoa
kibao chake kipya kinachofahamika kama ‘Siri ya Mchezo’ (unaweza kukisikiliza
na kusoma mashairi yake hapa).
Kilichonivutia kuhusu wimbo huo ni ujumbe mzito wa kisiasa, ambapo ni kitu
adimu kwa wasanii wetu kuzungumzia masuala ya kisiasa kwenye tungo zao.
Niliongea na Fid Q kwa
kutumia mtandao wa kijamii wa Twitter, ambapo pamoja na mambo mengine
alinieleza kitu kimoja kilichonigusa sana. Namnukuu, “Believe or not, nilijaribu kujivisha viatu vyako wakati ninaandika hii
track.”
Ni nani hatofarijika
kuambiwa na msanii mwenye jina kubwa kama Fid Q kuwa alipata hamasa kutoka kwao
wakati anaandika mashairi ya wimbo ambao kwa hakika utavuma?
Lakini licha ya
hamasa, furaha na heshima hiyo kutoka kwa msanii huyo, kuna kitu cha ziada
ambacho kimsingi ndicho kinabeba dhima ya makala hii: nafasi ya wasanii wetu
katika kuhamasisha mabadiliko chanya kwa jamii.
Kwa muda mrefu
wasanii wetu, hususan wa muziki ‘wa kizazi kipya’ (Bongofleva) wamekuwa
wakilaumiwa kwa aidha kutumika vibaya na wanasiasa au kutotilia maanani
matatizo mbalimbali yanayoikabili Tanzania yetu.
Imezoeleka kwamba
ukifika wakati wa uchaguzi ndipo wanasiasa wetu hukumbuka kuwa kuna vijana
wanaendesha maisha kwa kujishughulisha na sanaa ya muziki. Kama ilivyo kwa
makundi mengine ya jamii, wanasiasa hao pasi haya huwavuta karibu wasanii na
kisha kuwatumia kwenye kampeni zao. Wakishapata madaraka, wanawatelekeza kama
inavyotokea kwa wengi wa wapigakura majimboni.
Lakini wakati ni
rahisi kuwalaumu wasanii kwa kile kinachotafsiriwa na wengi kama ‘kutojali
matatizo yanayoikabili Tanzania yetu,’ Fid Q alinieleza kuwa tatizo mojawapo ni
ukiritimba wa vyombo vya habari ‘vya asili’ (yaani traditional media, kwa maana
ya radio, televisheni na magazeti). Sio siri kwamba wamiliki wa vyombo hivyo
huchelea sana kuwaudhi watawala kiasi kwamba si ajabu kwa wimbo unaokemea maovu
flani yanayowahusu watawala ukanyimwa fursa radioni au kwenye runinga.
Tukirejea kwenye
wimbo huo wa Siri ya Mchezo, yayumkinika kubashiri kuwa Fid Q anafungua mlango
wa kile kinachofahamika kimuziki kama ‘political rap’ yaani muziki wa
kufokafoka uliobeba ujumbe wa kisiasa. Aina hiyo ya muziki ilikuwa maarufu sana
huko Marekani kwenye miaka ya 1970 hadi 1980, ambapo ulilenga kuzungumzia
masuala mbalimbali ya kisiasa na kijamii. Kimsingi, muziki huo ulikuwa ni kama
nyenzo ya wasanii kupambana na udhalimu, sambamba na kuhamasisha jamii, hususan
vijana, kushiriki katika harakati za kujenga jamii bora.
Katika wimbo huo,
Fid Q anamkumbuka mmoja wa wasomi lulu kwa taifa letu, marehemu Profesa
Chachage Chachage ambaye wakati wa uhai wake alijitahidi sana kutuelimisha
kuhusu soko huria na athari zake. Kadhalika, msanii huyo anasononeka kuhusu
hatma ya taifa letu akidadisi “tutarithi
nini...” katika zama hizi ambapo utajiri wetu unanufaisha wachache (hususan
wageni na vibaraka wao) huku mamilioni ya Watanzania wakibaki masikini.
Kadhalika, msanii
huyo anawanyooshea kidole wahujumu wa uchumi, kabla ya kutoa angalizo muhimu
kuwa “taifa la kondoo huendeshwa na
serikali ya dubu/mbwa mwitu wenye siri...”
Vilevile, Fid Q
anatahadharisha kuhusu siasa inavyotumika kama kitega uchumi, na kusikitishwa
na jinsi ukoloni mamboleo ulivyotupatia uhuru wa bendera huku ukituonyesha “kufuru za wenye hela.”
Katika lugha ya
kisanii, msanii huyo analalamika kuwa Tanzania imegeuka kama mwanamke
asiyefuata maadili, ‘anayetembea’ na kila mtu, mpaka wanamwita “cha wote,” na ambaye anatumia pombe kama
njia ya kukimbiza matatizo yake. Kimsingi, hapa anazungumzia jinsi nchi yetu
ilivyogeuka ‘shamba la bibi’ ambapo kila mwenye ‘fursa’ anajichumia.
Msanii huyo
anakwenda mbali zaidi na kukemea dhana kuwa wawekezaji wa kigeni watatuletea
maendeleo, na anasema “maendeleo ni
ndoto, ile mwekezaji ashaipuuza,” na kutahadharisha kwamba uwepo wa
wawekezaji hautufanyi tufikie viwango vya maendeleo katika nchi zao, akihoji “je kukaa karibu na moto ni kuota au
kujiunguza?”
Fid Q pia anazilaumu
taasisi za kisiasa kwa ‘kuwafelisha’ wananchi, kama ambavyo tunashuhudia vyama
vyetu vya kisiasa vikiwa ‘bize’ kulumbana huku walalahoi wakizidi kutaabika.
Pia anakumbusha kuwa “hakuna utumwa mbaya kama kujiona uko huru” na kutahadharisha kuwa
jitihada za kusaka ukweli zitakumbwa na vizingiti, akisema, “Kuusaka ukweli ni sawa na
kumenya kitunguu/
kila ganda litakutoa machozi na utabaki macho juu/
Ukishafika kwenye kiini niambie nini utagundua..?”
kila ganda litakutoa machozi na utabaki macho juu/
Ukishafika kwenye kiini niambie nini utagundua..?”
Anahitimisha tungo
hiyo aliyomshirikisha msanii mwingine maarufu Juma Nature kwa kutahadharisha
kuhusu wanasiasa matapeli ambao “wamejivisha
u-Noah, safina zao zikatoboka; wakajivisha u-Mussa, fimbo zao hazikugeuka
nyoka; sasa wamejivisha u-Mungu mtu...” Kadri tunavyoelekea kwenye uchaguzi
mkuu wa mwaka 2015 tutashuhudia kila aina ya utapeli wa kisiasa ambapo baadhi
ya wanaosaka urais wataahidi mambo ambayo hata wenyewe hawayaamini.
Lengo la makala hii
sio kuchambua wimbo huo bali kupigia mstari umuhimu wa alichofanya msanii Fid Q
kutumia kipaji chake cha muziki kuuzindua umma hasa katika kipindi hiki cha
mchakato wa kupata Katiba mpya, sambamba na hekaheka za uchaguzi mkuu ujao wa
mwaka 2015.
Nimalizie makala hii
kwa kumpongeza msanii huyo, na kutoa wito kwa kila Mtanzania kutumia nafasi
aliyonayo kuwa chachu ya mabadiliko stahili kwa nchi yetu. Hatuwezi kuendelea
kuwa watu wa kulalamika tu ilhali tuna uwezo wa kubadilisha yote yanayokwaza
ustawi wa taifa letu.
Inawezekana, timiza
wajibu wako
1 Nov 2013
1.11.13
Evarist Chahali
AD, Sintah
No comments

tuna vibanio tofauti ,cheni etc
sexy Sintah
sexy Sintah

Usimuudhi Padre/Mchungaji
vikoti vinApatikana
hili gauni kwa mtu mwembamba
linakuhusuuu
vikoti vinApatikana
hili gauni kwa mtu mwembamba
linakuhusuuu

| Wajawazito sasa mmepata solution hasa kama magauni haya |

| Kwa wale wanaoficha ficha ujauzito humu unaingia na halionekani lolest |

Come n shop wit us
Happy pipooo
Happy pipooo

Tuna different sizes za Veil
fupi, size ya kati na ndefuu kabisa
fupi, size ya kati na ndefuu kabisa

Usimuudhi Padre narudia tena njoo
ujipatie kikoti chako mapema
vipo aina tofauti
ujipatie kikoti chako mapema
vipo aina tofauti

Kwa mtu mwembamba kidogo
linakuhusu hili eeeh
linakuhusu hili eeeh

Umeona hio veil ilivyo ndefu hio ni
size ya kati tuna ndefu mpaka chini
kwa wale wasiopenda magauni ya mikia
inawahusu
pendeza mtoto wa kike huwa
haijirudii
usisahau ku smile
karibuniiii
size ya kati tuna ndefu mpaka chini
kwa wale wasiopenda magauni ya mikia
inawahusu
pendeza mtoto wa kike huwa
haijirudii
usisahau ku smile
karibuniiii
Lovies mambo mapya yameingia njoo ujipatie Size yako wewe mjamzito, mtu mnene maana watoto wa Dar sasa hivi sijui mnalishwa nini mnafutuka tu usijali size yako ipo, bila kusahau portables easy to carry, pia utapata accessories aina tofauti, viatu na pia veil za kila size kwaajili ya siku yako hiyo maalumu usihangaike kwenda sehemu nyingine karibu ukaribie Sintah's wedding lounge.For more info call 0652 112071
From C.E.O Sintah
1.11.13
Evarist Chahali
CCM, CHADEMA, RAIA MWEMA
No comments

NIANZE makala hii kwa kuomba radhi kutokana na kuadimika kwangu katika matoleo mawili yaliyopita. Hali hiyo ilitokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu.
Uandishi wa makala katika gazeti hili maridhawa umekuwa sehemu muhimu ya maisha yangu, na pindi ikipita wiki pasi kuandika chochote (kama ilivyokuwa wiki mbili zilizopita) huwa najihisi kupungukiwa kitu fulani maishani mwangu.
Pamoja na kiu yangu kubwa ya kuhamasisha mijadala mbalimbali, kukemea maovu na hata kuhabarishana tu, moja ya hamasa kubwa zinazonifanya niendelee na jukumu hili ni mapokeo ya wasomaji mbalimbali.
Katika wiki hizi mbili, nimepokea lundo la barua-pepe kutoka kwa wasomaji wakihoji kulikoni. Baadhi walikwenda mbali zaidi na kuhoji iwapo “nimenyamazishwa.” Ni katika mazingira kama haya ambapo ninaendelea kutambua kuwa jukumu hili la uandishi wa makala katika gazeti hili ni muhimu kwa jamii ninayoitumikia.
Katika mazingira ya Tanzania yetu ya sasa, ni rahisi kwa mtu kufika mahala akaamua “kubwaga manyanga,” kwamba hizi “kelele” za kila wiki ni kupoteza muda tu hasa kwa vile mambo yanazidi kwenda mrama badala ya kurekebishika. Lakini Waingereza wana msemo “hope is the last thing to lose” (yaani ‘kamwe usipoteze matumaini) kwa tafsiri isiyo rasmi). Inabidi tuendelee hivyo hivyo licha ya vikwazo tunavyokumbana navyo.
Na katika wiki mbili hizi nimejikuta nikikabiliwa na swali moja la msingi: pamoja na Watanzania wengi kuchoshwa na CCM, je CHADEMA ipo tayari kuiongoza Tanzania? Nimetaja CHADEMA kwa vile kila anayefuatilia kwa karibu siasa za huko nyumbani anatambua kuwa kwa sasa chama hicho ndicho pekee ambacho angalau kinaweza kuing’oa CCM.
Swali hilo limeniijia baada ya kauli ya majuzi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete kwamba CCM inaweza kuanguka kwenye Uchaguzi Mkuu ujao, na mwenendo wa CHADEMA.
Kwamba Mwenyekiti wa Taifa wa CCM ambaye pia ni Rais wa nchi yetu anahisi kuwa chama chake kinaweza kuondoka madarakani si jambo dogo. Lakini kubwa zaidi ni ukweli kwamba kauli hiyo ya Rais Kikwete inaakisi mawazo ya wachambuzi wengi wa siasa wanaoegemea kwenye uhalisia, badala ya hisia au itikadi za kisiasa.
Awali, mmoja wa wanasiasa wakongwe wa CCM, Mzee Peter Kisumo alitoa kauli kama hiyo ya Kikwete kwamba CCM inaweza kung’oka madarakani kutokana na kunyamazia vitendo vya ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za umma.
Mwanasiasa huyo alitoa onyo hilo wakati wa kumbukumbu ya miaka 14 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. “Chama kimebaki kuwa cha walalamikaji, kila mtu amekuwa mlalamikaji. Hata Waziri Mkuu amegeuka mlalamikaji. Sijaona watu wanaowajibishwa kwa ufisadi,” alisema Kisumo na kutolea mfano sakata la mabilioni ya fedha za umma zilizotoroshwa na kuhifadhiwa kwenye benki mbalimbali nchini Uswisi.
“(CHADEMA) wakijitokeza na kuwataja majina wahusika, wakasema fulani na fulani ndiyo wenye mabilioni haya Uswisi, na serikali ikasita kuwachukilia hatua, wakasema tukiingia madarakani tutawakamata, wananchi wanaweza kuwaamini na kuwachagua,” alisema.
Lakini pengine kwa kutolielewa kwa undani tatizo la ufisadi, Rais Kikwete alitahadharisha uwezekano wa CCM kuanguka katika uchaguzi ujao akisema; “kama rushwa haitakomeshwa ndani ya chama hicho.” Kwa mtizamo wangu, japo ninampongeza Rais Kikwete kwa angalau kuwa na ujasiri wa kutoa tamko hilo, lakini ameendeleza siasa katika suala hili nyeti.
Ni hivi, kitakachoiangusha CCM (si lazima iwe mwaka 2015 japo ni muhimu) sio rushwa ndani ya chama hicho pekee bali katika taifa kwa ujumla. Kuwanyooshea vidole viongozi wa CCM pekee ilhali rushwa ni janga la kitaifa ni moja ya kasoro za kauli hiyo ya Kikwete. Wakati kila Mtanzania anafahamu jinsi rushwa ilivyoshamiri kwenye kila chaguzi za chama hicho tawala, ufisadi mkubwa na wa kutisha unaowahusisha watendaji wa serikali kwa kushirikiana na wafanyabiashara wahalifu wanaolindwa na CCM na taasisi za dola.
Japo kushamiri kwa rushwa ndani ya CCM kumechangia kulea na kukuza ufisadi nchini Tanzania, kuna idadi kubwa tu ya watendaji wa serikali ambao si viongozi wa kisiasa na wanajihusisha na ufisadi. Ningetamani endapo Rais Kikwete angekwenda mbali zaidi na kutangaza ufisadi kuwa ni janga la kitaifa, hasa ikizingatiwa kuwa uhai wa Tanzania sio tu ni muhimu zaidi ya uhai wa CCM, bali pia ukweli kwamba madhara ya rushwa yanamgusa kila Mtanzania bila kujali itikadi yake ya kisiasa.
Lakini angalau kwa Rais Kikwete kuwa na ujasiri wa kulizungumzia suala hilo bayana inaleta matumaini kuwa huenda katika miezi kadhaa iliyosalia kabla ya yeye kumaliza muhula wake wa urais, anaweza kulivalia njuga janga hilo la ufisadi ndani na nje ya CCM.
Hata hivyo, kama CCM itaanguka kwenye Uchaguzi Mkuu ujao na CHADEMA kufanikiwa kushika madaraka, je chama hicho cha upinzani kipo tayari ‘kuikomboa’ Tanzania kutoka katika lindi la umasikini unaochangiwa kwa kiasi kikubwa na ufisadi?
Japo nimekuwa nikiunga mkono harakati za chama hicho (pasi kuwa mwanachama) katika kuiletea nchi yetu ‘ukombozi wa pili’ (wa kwanza ulikuwa kumng’oa mkoloni, wa pili kung’oa mfumo wa kifisadi) bado nina wasiwasi kwamba vita ya chini kwa chini inayoendelea ndani ya CHADEMA inaweza sio tu kukinyima ushindi chama hicho katika Uchaguzi Mkuu ujao, bali pia inaweza kuzalisha ‘CCM-B.’
Ninaandika haya nikitambua hujuma kubwa zinazofanyika dhidi ya chama hicho kutoka nje yake lakini pia kuna hujuma zinazofanyika ndani ya chama hicho, ambazo zinaweza kuwa na madhara makubwa pasipo kuchukuliwa hatua haraka.
Lakini hata tukiweka kando hujuma hizo, kwa mtizamo wangu ninaiona CHADEMA kama imeridhika na uungwaji mkono inaopata kutoka kwa wananchi na kwa namna fulani, wameanza kubweteka. Je, chama hicho hakiwaelewi Watanzania vizuri au ni uzembe tu?
Tujiulize swali hilo tukizingatia ukweli mchungu kwamba, sehemu kubwa ya wapigakura huko nyumbani (Tanzania) ni rahisi mno kughilibiwa kwa vitu vidogo tu (pishi za sukari na mchele, doti za khanga na vitendo vingine kama hivyo).
CHADEMA kinaelekea kutegemea huruma ya umma, kitu ambacho hakipo, kwa tunaozifahamu siasa za Tanzania yetu. Sio kama ninawakashifu Watanzania wenzangu, lakini ukweli ni kwamba kuna wenzetu wengi tu wanaoendeshwa na ‘matukio ya kupita.’ Likitokea jambo kubwa, litashika moto mkubwa kwa saa kadhaa, kisha ‘life goes on.’ Kuna idadi kubwa tu ya Watanzania ambao yayumkinika kuhitimisha kuwa wanaona matatizo yanayoikabili nchi yetu ni hatima yetu na si jambo ‘la kujitakia’ au linaloweza kurekebishika.
Ili CHADEMA iweze kuingia Ikulu inapaswa kujibadili kutoka kikundi cha harakati na kuwa chama kamili kilicho tayari kushika dola. Na sio kushika dola kwa minajili ya kuwa Ikulu tu bali kuhakikisha kuwa sababu zinazowafanya baadhi ya Watanzania kutamani CCM iondoke madarakani haziendelei kuwepo.
Ni rahisi kwa mwananchi anayetaka mabadiliko kuvunjika moyo akishuhudia jinsi harakati za uchaguzi tu ndani ya CHADEMA zikitishia amani na hata hatma ya chama hicho.
Baadhi ya wachambuzi wa siasa wanabashiri kuwa iwapo chama hicho kitaitupa mkono demokrasia ndani yake na kuingia katika Uchaguzi Mkuu katika hali hiyo, basi kisahau ndoto za kwenda Ikulu. Na kana kwamba CHADEMA wapo kwenye majaribio ya siasa, wanapiga danadana kufanya uchaguzi wao mkuu ikiwa ni chini ya mwaka mmoja kabla ya Uchaguzi Mkuu wa nchi. Tufanye tafakari fupi kwa kujiuliza; hao watakaochaguliwa kuongoza chama hicho baada ya uchaguzi, watakuwa na muda wa kutosha kukiingiza chama hicho Ikulu?
Lakini tishio jingine linaloendelea hivi sasa dhidi ya CHADEMA ni mfumuko wa nyaraka kadhaa zinazosambazwa kielektroniki (nimebahatika kuzisoma) zinazomhusu kiongozi mmoja mwandamizi wa chama hicho. Ziwe ni hujuma zinazofanywa na maadui wa nje ya chama hicho au ni sehemu ya vita ya wenyewe kwa wenyewe, au ni tuhuma za kweli, madhara yake yanaweza kuwa makubwa kwa chama hicho kikuu cha upinzani.
Nihitimishe makala hii kwa kubainisha kuwa mjadala huu ni endelevu, nitauendeleza. Kwa sasa, ni muhimu kwa kila Mtanzania anayeitakia mema nchi yetu kutumia muda huu kutafakari kwa makini nafasi yake binafsi katika ‘mapambano ya kupata ukombozi wa pili.’
Tanzania yetu ni muhimu kuliko vyama vya siasa, na wakati vyama vya siasa huzaliwa na kufa, nchi yetu ni lazima ibaki hai kwa gharama yoyote ile.
Inawezekana, timiza wajibu wako.
24 Oct 2013
23 Oct 2013
23.10.13
Evarist Chahali
New Music, Prezzo
No comments
Submitted by Arthur, Manager Unity Entertainment Tanzania
Subscribe to:
Comments (Atom)
























































