22 Sept 2011


Raia Mwema Ughaibuni
Ya Usalama wa Taifa na teuzi za Rais Kikwete!
Evarist Chahali
USKOCHI
21 Sep 2011
Toleo na 204
“KATIKA kupambana na uhalifu, hakuna njia ambayo - kama inaweza kuleta ufanisi - haitotumika. Kama inazingatia sheria, maadili, na inafanywa kwa nia nzuri, nipo tayari kuifanyia kazi...tumeajiriwa na tunalipwa kupambana na uhalifu, na hicho ndicho nitakachofanya...” .
Nukuu hii inapatikana katika hotuba ya kwanza ya Mkuu mpya wa ‘kanda kuu’ ya kipolisi ya London (Metropolitan Police) Bernard Hogan-Howe.
Hogan-Howe alishinda nafasi hiyo baada ya kuwabwaga makamanda wengine watatu kujaza nafasi iliyoachwa na Sir Paul Stephenson aliyejiuzulu kufuatia kuhusishwa kwake na skandali ya kunasa kwa siri maongezi ya simu (phone hacking) kulikofanywa na baadhi ya magazeti ya Uingereza yanayomilikiwa na tajiri mkubwa kabisa wa vyombo vya habari duniani, Rupert Murdoch.
Mkuu huyo wa Metropolitan Police alitamka bayana kuwa jukumu kuu alilonalo mbele yake ni kupambana na uhalifu na kuwahudumia waathirika wa uhalifu. Na rekodi yake kiutendaji ni ya kuvutia sana.
Akiwa Mkuu wa Polisi wa kanda ya kipolisi ya Merseyside (inayojumuisha jiji lililokuwa likisifika kwa uhalifu la Liverpool), alifanikiwa kuifanya kanda hiyo itoke kwenye nafasi ya 42 kati ya 43 ya ‘ligi ya uhalifu’ hadi kufikia nafasi ya kwanza alipotoka kwenye nafasi hiyo.
Kadhalika alifanikiwa kupunguza uhalifu kwa asilimia 29 na vitendo visivyoendana na maadili ya jamii (anti-social behaviour) kwa asilimia 25 katika kile alichokiita upolisi timilifu (total policing) na vita kamili dhidi ya uhalifu (total war on crime).
Dhamira hiyo ya Hogan-Howe inashabihiana na kauli aliyotoa Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa, Rashid Othman alipoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushika nafasi hiyo mwezi Agosti mwaka 2006.
Othman, shushushu mzoefu, alitoa ole kwa majambazi akisema moja ya kazi zake kuu ni kuhakikisha kuwa anaendeleaza mapambano dhidi ya ujambazi na majambazi, kazi ambayo alisema ilikuwa imeasisiwa na Rais Kikwete.
Kadhalika, aliahidi kuwa angehakikisha anaweka utaratibu mzuri wa kukutana na vyombo vya habari ili kuwapa wananchi taarifa za kiusalama ambazo wanastahili kuzipata, na wana haki ya msingi kujua serikali yao inafanya nini katika suala zima la usalama, na hiyo ingeongeza ufanisi wa katika utendaji kazi.
Wakati sina hakika ya mafanikio katika dhamira hizo za Mkuu huyo wa Usalama wa Taifa kupambana na ujambazi ‘wa asili’ (yaani ule wa kuvunja majumba au ofisi, kupora kwa kutumia silaha, nk), yayumkinika kuhitimisha kuwa hajafanikiwa kabisa kupambana na ujambazi dhidi ya mali ya umma au kwa neno maarufu “ufisadi”.
Tangu alipotoa kauli hiyo hadi sasa, tumeshuhudia mlolongo wa matukio ya ujambazi unaofahamika kwa kimombo kama ‘uhalifu wa kola nyeupe’ (white collar crime) ambapo wahusika hawatumii silaha; bali ujuzi na madaraka yao kuliibia taifa.
Sote tunakumbuka kuhusu ujambazi wa EPA, utapeli wa kampuni ya Richmond, dili za ufisadi kwenye makampuni ya Meremeta, TANGOLD, Deep Green Finance, na uhalifu mwingineo ambao umelisababishia taifa hasara ya mabilioni ya shilingi.
Ni ukweli usiopingika kuwa baadhi ya watu wanahoji Idara ya Usalama wa Taifa iko wapi wakati haya yote yanatokea. Kuvuruga mambo kabisa, taasisi hiyo nyeti ilijikuta ikihusishwa na ufisadi wa EPA ambapo mmoja wa maafisa wake waandamizi alitajwa kuwa mnufaika wa wizi huo mkubwa.
Na hapa ndipo inapofika mahala pa kuangalia ahadi za Othman wakati anateuliwa ambapo aliahidi kuandaa utaratibu mzuri wa kukutana na vyombo vya habari ili kuwapa wananchi taarifa za kiusalama.
Kwa kumbukumbu zangu, wakati pekee ambapo Idara hiyo ilizungumza na waandishi wa habari, ni pale Naibu Mkurugenzi Mkuu wake, Jack Zoka alipokanusha madai ya mgombea kiti cha urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dkt.Willibrod Slaa, kuwa taasisi hiyo ilikuwa ikiisaidia CCM kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Hadi leo, hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa na idara hiyo kuhusu namna ilivyohusishwa na skandali ya fedha za EPA. Ilipaswa aidha wajitenganishe na afisa huyo mwanadamizi na kubainisha kuwa kampuni zilizodaiwa kumilikiwa naye hazikuwa na mahusiano na taasisi hiyo, na kutajwa kwake hakuhusiani kabisa na idara hiyo nyeti.
Kadhalika, haingekuwa vibaya kwa taasisi hiyo kuufahamisha umma ilikuwaje ikashindwa kubaini ufisadi huo, na pengine kuweka bayana mikakati yake ya baadaye ya namna ya kuzuia kurejea kwa matendo ya kihalifu kama hayo.
Naanika haya nikitambua kuwa kazi za taasisi hiyo zinafanywa kwa siri (kwa nia njema kabisa), lakini tatizo linakuja pale mambo yanapokwenda fyongo ambapo ni rahisi kwa wananchi kupata hisia kuwa utendaji kazi huo wa siri unatumika kuficha mapungufu au hata kufunika ushiriki wa taasisi hiyo katika ufisadi.
Si lengo la makala hii kumhoji kiongozi huyo mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa bali, kama nilivyobainisha mwanzoni, kauli yake siku alipoteuliwa inashabihiana na iliyotolewa na mkuu huyu mpya wa Metropolitan Police.
Na kwa vile ni nia ya kila Mtanzania kuona nchi yetu ikielekea kule inakopaswa kwenda, hakuna ubaya katika kukumbushana yale yote yanayoweza kutufikisha tuendako kwa usalama.
Lengo kuu la makala hii ni kuangalia namna teuzi zinavyofanywa na Rais, na pengine watendaji wengine wa serikali pasipo kuangalia iwapo teuzi hizo zitaleta ufanisi.
Wiki iliyopita, Rais Kikwete alitangaza wakuu wa mikoa wapya na waliobadilishiwa vituo vya kazi. Kadhalika, tulifahamishwa majina ya wakuu wa mikoa waliostaafu na ‘waliopumzishwa kwa muda’ (kwa matarajio ya kupangiwa kazi nyingine).
Kabla hata ya kujadili iwapo walioteuliwa walipaswa kupewa nafasi hizo, sijui inaleta picha gani pale Rais anapoamua kumteua mtu ambaye wapiga kura walimkataa katika ngazi ya jimbo. Hapa nazungumzia baadhi ya walioteuliwa kuwa wakuu wa mikoa lakini waliangushwa katika uchaguzi wa wabunge katika majimbo yao.
Tuwe wakweli: Hivi kama idadi ndogo tu ya wananchi katika jimbo imekosa imani na mgombea, na hivyo kutompa kura za kutosha za kumfanya awe mbunge, inawezekanaje kwa mtu huyo kukabidhiwa ‘urais wa mkoa’? Ndio, ukuu wa mkoa ni kama urais wa mkoa; kwani anayepewa dhamana hiyo ni mwakilishi wa Rais katika mkoa husika.
Sijui lengo ni kuwakebehi wapigakura waliomnyima ubunge kiongozi wa aina hiyo au ndio hadithi zile zile za kuteuana ‘kishkaji’ (kirafiki) lakini sidhani kama kuna maelezo stahili ya kuelezea teuzi za aina hii; hasa ikizingatiwa kuwa nchi yetu haina uhaba wa wazalendo wenye uwezo wa kushika nyadhifa.
Katika baadhi ya teuzi hizo zilizofanywa na Kikwete baada ya ya takriban mwaka mzima wa ‘upembuzi yakinifu’ zina walakini uliozoeleka wa watendaji ambao rekodi zao zina walakini. Hili halihitaji kutajwa majina; kwani mikoa iliyoboronga kimaendeleo inafahamika.
Kuwazawadia waharibifu wa maendeleo nafasi za ‘kujaribu tena mkoa mwingine’, ni sawa kabisa na kutothamini maslahi ya wananchi katika maeneo husika.
Lakini pia katika walioteuliwa kuna mbunge ambaye anaungana na baadhi ya wabunge wenye kofia zaidi ya moja -kwa maana ya kuwa mbunge na mkuu wa mikoa. Kitendo hiki ni kuwanyima kwa makusudi wananchi nafasi ya kuwa na kiongozi atakayeelekeza nguvu zake kwa jukumu moja.
Katika mazingira yakawaida, mbunge ana majukumu ya kuwatumikia wapiga kura wake. Kumpa jukumu jingine la kuongoza mkoa ni kumbembesha mzigo mzito wa ziada pasipo kujali matokeo yatakuwaje.
Kukosoa na kumlaumu pasipo kutoa ushauri si jambo jema. Nimalizie makala hii kwa kushauri kuangalia madaraka ya Rais katika kufanya teuzi mbalimbali, na kwa vile tupo kwenye mchakato wa marekebisho ya Katiba, basi, ni muhimu pia kuangalia  uwezekano wa ulazima wa teuzi zinazofanywa na Rais kuidhinishwa na Bunge.
Rais kama binadamu anaweza kufanya teuzi zisizo na maslahi kwa taifa. Bunge likifanya kazi yake zaidi ya kuwa ‘mhuri wa kuidhinisha kila kinacholetwa na serikali’, linaweza kabisa kuepusha teuzi fyongo au zile zinazozidi kudidimiza nchi yetu kwenye lindi la umasikini unaochochewa na ufisadi.


21 Sept 2011

Kama kuna hoja inayotawala zaidi kuliko nyingine kwenye blogu na maandiko mengi ya wengi wa mabloga wa kike wa Kitanzania ni hii ya hisia kwamba WANAUME WA KITANZANIA SI WAAMINIFU KWENYE MAHUSIANO.Ninaposema inatawala simaanishi kuwa huo ndio mtizamo wa mabloga hao bali ni kitu kinachojitokeza mara nyingi pengne zaidi ya vitu vingine,hususan kwenye sehemu za kutolea maoni (comments).

Utakuta dada mmoja anaomba ushauri kwa wenzie kuhusu mwenza wake ambaye aidha anamhisi kuwa si mwaminifu au amemsaliti kwenye uhusiano wao.Ukiweka kando ushauri atakaopewa,wengi wa wachangiaji wa kike hukimbilia kuhitimisha kuwa tatizo la msingi ni "ukweli kwamba wanaume wa Kibongo si waaminifu",huku wengine wakienda mbali zaidi na kudai "wanaume wetu wa Kibongo wanatembea wakiwa na zipu zao wazi-kwa maana ya kuwa tayari kukamata chochote kile kitakachokatiza mbele yao".

Katika hatua hii siwezi kusema hisia hizo ni sahihi au la ila nisichokubaliana na hitimisho la jumla (blanket conclusion) kwamba WANAUME WOTE WA KITANZANIA SI WAAMINIFU.Sijui kama wanaohitimisha hivi huwa wanajaribu angalau kutafakari kidogo kuhusu baba zao,maana nao pia ni wanaume wa Kitanzania.Hatari kubwa ya kuhitimisha jambo jumla jumla ni kuwaingiza hata wale wasiohusika.Wengi wetu tunafahamu jinsi baba zetu walivyo waadilifu kwa mama zetu hadi kufanikiwa kutufikisha hapa tulipo.Japo si wote lakini kwa kiasi kikubwa baba zetu-hususan wale waliokula chumvi nyingi-wamejitahidi kadri wawezavyo kuwa waaminifu kwa mama zetu.

Kwa vile mada hii ni ndefu na ili kuijadili kwa ukamilifu inahitaji kitabu kizima basi niifupishe kwa,kwanza,kuangalia sababu za kitaaluma kwanini watu wana-cheat.Naomba ieleweke kuwa hata kwenye kusaka sababu kwenye masuala mengine ni nadra kupata sababu timilifu kabisa kwa sababu kuna vigezo vingine vinavyoathiri kila sababu,kwa mfano mazingira,umri,uchumi,malezi,nk

Hata hivyo,tafiti mbalimbali za mahusiano ya kimapenzi zinataja sababu zifuatazo kuwa 'maarufu' zaidi katika kuelezea kwanini watu wana-cheat

KULIPIZA KISASI:

Sie Wakristo tunafundishwa kwenye Agano Jipya kuwa ukipigwa kofi shavu la kushoto basi geuza na shavu la kulia.Hii inapigia mstari umuhimu wa kutolipiza kisasi.Lakini hata kwenye Maandiko hayo Matakatifu haikuwa hivyo siku zote.Katika Agano la Kale,mafundisho yalikuwa ni JICHO KWA JICHO na JINO KWA JINO.Kwenye stadi za dini inafahamika kama 'sheria ya kulipiza kisasi' (law of retaliation) na 'sheria ya mapatano' (law of reconciliation).Katika poetic justice 'jino kwa jino' inaweza kulinganishwa na kile kiitwacho adhabu ya kioo (mirror punishment),yaani-kwa kifupi-malipizi kwa kutenda kosa.Msingi hapa ni kwamba tendo jema huzawadiwa na tendo baya huadhibiwa.

Kwa hiyo,kwa vile mwenza wa kiume au wa kike ame-cheat basi yule aliyekuwa cheated anaamua kulipiza kisasi kwa ku-cheat pia.Jino kwa jino,au tit-for-tat.Lakini hitimisho la kisomi ni kwamba mara nyingi kulipiza kisasi hakusaidii sio tu kuleta ufumbuzi wa tatizo bali pia hata kuondoa maumivu ya kusalitiwa kwenye penzi.

Unajua kuna tofauti kati ya kufanya jambo pasipo msukumo wowote na kufanya jambo kwa vile kuna msukumo flani.Mwanaume au mwanamke anayeamua tu ku-cheat kwa vile anajiskia kufanya hivyo ana tofauti na yule aliyelazimika ku-cheat kwa sababu tu anataka kumkomoa flani.Tofauti hii ni sawa na ile ya binti anayefanya ukahaba kama hobby na yule anayefanya kwa vile anahitaji fedha au hana njia nyingine ya kipato zaidi ya kuuza mwili/utu wake.Kufanya jambo kwa uhuru ni,well,kuwa huru (hata kama ni makosa) wakati kufanya jambo kutokana na kusukumwa ni sawa na utumwa.

Anyway,hapa tunataja sababu za ku-cheat na sio kuhukumu kuwa anaye-cheat kwa sababu flani yuko sahihi au la.Twende sababu ya pili

KAMA KIPO KITUMIE

Kuna wenzetu wanaoamini kwamba kama nyama iliyopo kwingineko ni ya kupendeza,tamu,isiyo na sumu,na inapatikana,then kwanini isiliwe?Watu wa aina hii wanaamini kuwa wanachofanya ni kula kilicho bora,na ambacho kinapatikanika (available/accessible).Hawana uchungu kwa kufanya hivyo kwa vile wanaamini kuwa maridhio ya nafsi ni muhimu zaidi kuliko uhalali au ukosefu wa uhalali wa tendo husika.

Nadhani ushaskia misemo kama 'cha muhimu ni kupata fedha,jinsi ilivyopatikana sio muhimu'.Au wengine wanakwenda mbali zaidi na kudai kuwa watu wenye kuifaidi zaidi dunia ni wale waisoongozwa na 'hiki ni halali na hiki si halali'.Ishu kama uadilifu,uaminifu,nk sio muhimu kwao.

Katika kundi hili kuna wale tunaoweza kuwaita waathirika wa Columbus Syndrome (tafsiri ya Kiswahili ni ngumu lakini turahishishe kwa kuita 'ugonjwa wa kiu ya uvumbuzi kama Christopher Columbus.Yaani tamaa ya kujua mambo zaidi ya maelezo sahihi yanavyoelezea mambo hayo).Unakuta mwanaume 'anafukuzia sketi' kwa vile tu anataka kuonja sehemu za siri za mwanamke huyo.Haijalishi kama ana mwenza au hana,bali la muhimu kwake ni kwamba A sio B,na nyama ya mbuzi si ya ng'ombe,na japo maharage na kunde zote ni mboga lakini maharage si kunde.Hawa wapo katika kile kinachoitwa kwa kimombo kama taste-testing (kujaribu ladha).

Kwenye kundi hili pia kuna wale wanaotaka kupima kama ujuzi wao wa kufukuzia sketi bado upo,licha ya ukweli tayari wana wenza nyumbani.Kwa akina dada,inawezekana ni kupima kama "kama nilimudu kum-cheat yule bwege mwaka juzi na hakujua mpaka tunaachana kwanini nisijaribu tena safari hii?"Ni sababu zinazoweza kuonekana kama za kupuuzi lakini kumbuka kuwa mara nyingi wanaofanya upuuzi hawana muda wa kutafuta sababu.Na hata ukiwahoji wakupe sababu basi majibu watakayokupa yanaweza kukutibua kuliko upuuzi waliofanya.

Kufupisha maelezo,wanao-cheat kwa mujibu wa sababu hii wanafanya hivyo kwa vile,well,kama kipo kitumie.

WASIOTOSHEKA

Unakumbuka ule wimbo wa zamani wenye maneno "ee jamani mwanadamu hatosheki,hata ukimpa nini milele hataridhika...ukimpa kumi atataka mia..."Well,si kweli kwamba kila mwanadamu hatosheki bali ukweli ni kwamba kama ilivyo kuna wenzetu ni wepesi kutosheka,wenzetu wengine kamwe hawatosheki.Tuchukulie mifano halisi.Katika kusaka ufumbuzi watatizo la rushwa katika Mamlaka ya Mapato Tanzania ikashauriwa mishahara minono na marupurupu mazuri inaweza kusaidia kuondoa vishwawisho vya watumishi wa taasisi hiyo kudai na kupokea rushwa.Seriakli ikaridhia kufanya marekebisho katika muundo wa mishahara ya watumishi wa taasisi hiyo.Sihitaji kukwambia kuwa TRA ni miongoni mwa taasisi zilizobobea kwa rushwa,pengine mara dufu ya ilivyoluwa zama za mishahara kiduchu.

Kwanini watu hawa waendelee kudai na kupokea rushwa ilhali wanalipwa mishahara minono kabisa?Well,jibu rahisi ni tamaa.Lakini jibu jingine linaweza kuwa mazowea.Kuna msemo wa Kiingereza usemao "vyovyote utakavyomtunza,mbwa mwitu hawezi kuwa mbwa".Nenda porini,kamata mbwa mwitu,mpe kila aina ya matunzo kama mbwa wa kawaida,lakini kama hatoishi kukung'ata basi atatoroka na kurejea porini.Wanasema kunguru hafugiki,na samaki yake maji.Ukimtoa samaki majini,basi umemuua.Period.

Kwahiyo kama ambavyo kuna watu hawatosheki na fedha wanazopata (kwa mfano mafisadi serikalini ambao wanalipwa mishahara mikubwa kuliko mahitaji yao) basi pia kuna watu hawatosheki na tendo la ndoa.Hata mkewe/mwenza wake ampe uroda kiasi gani bado atahitaji nyongeza.Na kuna akinadada hata apewe-ashakum si matusi- 'mabao' mangapi bado atahitaji zaidi.

Katika sababu hii kuna marejeo ya sababu iliyopita ya 'kama kipo tumia' kwa maana ya kama una njaa na chakula kipo basi kula,na kama ukienda kwingine na bado unajiskia hamu ya kula endelea kula.Ma-Tiger Woods hawa wa kike na kiume wanahitaji zaidi na zaidi just like wale wala rushwa wa TRA.

Kwa wengine hili ni kama tatizo la kiafya linalohitaji tiba za kisayansi.Kabla ya tiba hiyo,dawa pekee ya kukabiliana na 'hamu isyoisha ya kula au kuliwa uroda' ni 'kula au kuliwa uroda' zaidi na zaidi.Ni mithili ya walevi ambao njia pekee ya kumudu maisha ni pombe.

Kwa bahati mbaya,watu wa kundi hili wanaweza kujikuta matatizoni zaidi ya kuharibu mahusiano na wenza wao.Yaleyale ya simba akikosa nyama anaweza kula majani,basi si ajabu kwa watu wa kundi hili kujikuta wakiamua liwalo na liwe na kudiriki hata kufanya tendo la ndoa na watoto wadogo,watu wa jinsia moja na wao,kubaka aua hata kufanya tendo la ndoa na midoli.Kwao,tendo la ndoa ni sawa na oksijeni,pasipo hiyo ni kama wanaelekea kukata roho.

Namkumbuka kijana mmoja enzi hizo za ujana,mitaa ya Kinondoni.Kila wikiendi alikuwa anakwenda Ambassador Plaza (Gogo Hotel) 'kukamatia',na kwa vile sehemu hiyo ilikuwa inapendelewa na mashoga basi alipokuwa akikosa binti wa kulala naye basi 'anakamatia' shoga.Na huyu kijana alikuwa na girlfriend mrembo kupita maelezo.

Na kuna mama mmoja niliyewahi kufanya nae kazi sehemu fulani ambayo mshahara,posho na fedha kwa ujumla ilikuwa sio tatizo.Lakini licha ya kuwa na mume mwenye uwezo wa kifedha na mwenye haiba ya kutamanisha mwanamke yeyote yule,mama huyo alikuwa yuko radhi kulala hata na wafagizi hapo ofisini,baada ya kuwamaliza mabosi wenzie na wafanyakazi wa kada ya kati.Wambeya walikuwa wanadai kuwa mama huyo 'alipokuwa kwenye siku zake' alilazimika kufanya tendo la ndoa kinyume cha maumbile alimradi akidhi addiction yake.

KITULIZA ROHO

Wakati mwingine mwenza hujikuta anashawishika ku-cheat kutokana na mapungufu yanayozidi kuathiri mahusiano yake na mwenzie.Naomba tuelewane hapa.Sio kama nahalalisha ku-cheat bali natoa moja ya sababu zinazoweza kumfanya mtu a-cheat.Ikumbukwe kuwa wizi ni wizi tu,hakuna wizi halali.Mtu anayekutwa na hai ya kuua,kwa mujibu wa sheria zetu,adhabu yake ni kunyongwa hadi afe.Hakuna tofauti kati ya aliyeua mtu mmoja na aliyeuwa watu 10,wote ni wauaji.

Kadhalika,anaye-cheat kwa vile mumewe/mkewe hamridhishi,hana tofauti na yule wa kundi la kwanza au la pili au la tatu hapo juu.Wote wame-cheat,na kama kuna adhabu dhidi ya ku-cheat,wote wataadhibiwa kama cheaters,period!

Inaelezwa kuwa baadhi ya wanawake wanapoolewa wanaweza kujikuta wanajisahau kuhusu vitu vilivyofanya waume zao watamani kuwaoa in the first place.Matokeo yake ndoa inakuwa dull,tendo landoa linakuwa kama kutimiza wajibu tu kama sio kutokuwepo kabisa.Nasisitiza kuwa ku-cheat sio ufumbuzi lakini kwa mhusika hiyo ni excuse tosha ya kwenda nje ya uhusiano.

Wanaume pia,iwe kwenye ndoa au mahusiano tu kati ya boyfriend na girlfriend,wanadaiwa kuwa wakati mwingine wakishapata wanachohitaji wanawachulia wenza wao for granted.Zawadi za 'enzi za kutongozana'-maua,perfume,kadi,sim/sms mfululizo,nkzinaanza kufifia kadri umri wa uhusiano unavyozidi kuongezeka.

Again,naomba kusisitiza kuwa hii sio kwenye kila uhusiano bali hutokea,wewe na mimi tumeshaskia simulizi za aina hii mara kadhaa.

Mwenza anajikuta yupo kwenye uhusiano ambao ni 'uhusiano jina',hakuna mahaba,hakuna msisimko,na pengine kibaya zaidi,hakuna tendo la ndoa,au hata kama likiwepo ni la 'kizushi' tu.Kuna wanaoanza kwa kutishia ku-cheat-si kwa maneno bali vitendo.Kwa mfano,binti ambaye baada ya kuwa na mwenza wake alianza kubadilisha uvaaji wake 'wa utatanishi' (kwa lengo la kuepusha wasumbufu mtaani) anaamua kurejea kwenye uvaaji huo ili kumpelekea ujumbe mwenza wake kuwa 'kama ulinitamani uliponiona katika mavazi haya siku hizo,basi hata sasa naweza kutamaniwa na wengine'.Kwa bahati mbaya,'tisha toto' hii inaweza kupelekea madhara yasiyokusudiwa.Kwamba akajitokeza mdau akaonyesha interest ya kutosha na hatimaye mwanadada akashawishika kutembea naye 'mara moja tu' (na hatimaye mara moja hiyo kuzaa mara ya pili na kadhalika na kadhalika).

Kuna wengine hawana hata muda huo wa kufikisha ujumbe na huamua kuingia kwenye hatua ya ku-cheat moja kwa moja.Hoja ya msingi kwao ni kwamba kama huwezi kunipa ninachohitaji basi kuna wengine w3anaweza kunipa.Na kwa vile mie na wewe sio dada na kaka basi sioni umuhimu wa kuishi na mwanaume au mwanamke ambaye hanitimizii mahitaji yangu ya kimahusiano.

Kama nilivyaondika awali,ningependa sana kuingia kwa undani na kujadili njia mwafaka za kusaka suluhisho kwa kila sababu ya ku-cheat niliyotaja hapa lakini kwa leo naomba niishie kwenye kutaja sababu tu,kabla ya kuhamia kwenye mada ya msingi ambayo ni hoja ya wanawake wengi kuwa Wanaume wa Kitanzania si waaminifu.

UCHAMBUZI

Kwa kifupi kabisa,naomba nikuachie msomaji uondoe MWANAUME WA KITANZANIA kwenye kila sababu niliotaja hapo juu na uweke MWANAUME WA KIKENYA,KIMAREKANI,KIINGEREZA au MWANAUME WA NCHI YOYOTE ILE.Kisha angalia kama kuna mwanaume wa uraia flani hawezi ku-fit kwenye sababu hizo hapo juu.

Kisha jaribu tena kuondoa MWANAUME (awe wa KITANZANIA au wa nchi nyingine) na uweke MWANAMKE WA KITANZANIA.Je hakuna mwanamke wa Kitanzania anayeweza ku-cheat kwa sababu tu ANALIPIZA KISASI (at least according to her)?Je hakuna mwanamke wa Kitanzania anayeweza ku-cheat kwa sababu tu anaamini KAMA KIPO KITUMIE?Au je hakuna mwanamke wa Kitanzania anayeweza ku-cheat kwa vile tu HATOSHEKI na anachopewa na mwenza wake?Na mwisho,je hakuna wanawake wa Kitanzania wanaoweza ku-cheat kwa minajili ya KUTULIZA ROHO kutokana na mapungufu yanayokabili mahusiano na wenza wao?

HITIMISHO:

Kwa kuangalia sababu hizo za kitaaluma as to kwanini wenza wanaweza ku-cheat,ni wazi kuwa,kwanza si mwanaume tu anayeweza kuwa na sababu (hata kama haikubaliki) ya ku-cheat.Na pili,si wanaume wa Kitanzania tu wanaoweza ku-apply sababu hizo wanapo-cheat,au kwa lugha nyingine,si wanaume wa Kitanzania tu wanao-fit explanations/sababu nilizobainisha hapo juu kuhusu kwanini watu wana-cheat.

Kwahiyo basi,natumaini makala hii inaweza kutoa jibu kwa niaba ya Wanaume wote wa Kitanzania wanaotuhumiwa kuwa si waaminifu katika mahusiano.Jibu ni kwamba si wanaume wa Kitanzania pekee,na si wanaume pekee,wanaoweza kuwa nasababu moja au nyingine ya ku-cheat.Makala hii haijaribu kwa namna yoyote kuhalalisha cheating kwa vile kama nilivyobainisha hapo mwanzo,ku-cheat si ufumbuzi wa tatizo lililopelekea mtu a-cheat.Faraja ya muda mfupi-iwe ni kulipa kisasi,kukidhi utafutaji ladha mbadala nje,kutibu kiu ya ngono au kujiliwaza-haiwezi kuwa ufumbuzi wa kukarabati uhusiano unaokwenda mrama.

Siku ya siku nitajadili njia mwafaka za kuboresha uhusiano na kuondoa fursa ya ku-cheat.

Inatosha kwa leo

20 Sept 2011


Kama ilivyozoeleka,blogu hii inaelemea zaidi katika masuala ya siasa.Lakini kuna nyakati ninajaribu kuangalia nyanja nyingine za maisha katika jamii.Na kwa bahati nzuri kabla ya kuzamia kwenye Siasa kitaaluma nilikuwa mwanafunzi wa Sosholojia (ndio mchepuo niliosoma katika Shahada ya Kwanza hapo Mlimani).

Ninajaribu kuanzisha utaratibu ambapo angalau mara moja kwa wiki nitajadili mada ya kijamii,hususan masuala ambayo ni ya kibinafsi zaidi kama vile mahusiano,mapenzi,nk.Nakaribisha michango na maoni kutoka kwa wasomaji.

Leo ninaanza na jinsi mwanaume anavyoweza kukabiliana na kuvunjika kwa uhusiano kati yake na mwanamke.Karibu sana.

JINSI YA MWANAUME KUDILI NA KUVUNJIKA KWA UHUSIANO NA MWANAMKE

Pointi tatu muhimu za kuzingatia:

  • Kwanza unapaswa kufuta kumbukumbu zote za uhusiano uliovunjika
  • Jaribu kutumia muda mwingi kuwa karibu na watu 'uliowapuuza' wakati ukiwa 'bize' na mwandani wako.Watu hao wanaweza kuwa familia yako,ndugu zako au marafiki zako
  • Kisasi kikubwa dhidi ya aliyekubwaga ni mafanikio.Kwahiyo hamasika kupata mafaniko ili 'ulipe kisasi.'
Hakuna anayeweza kubisha kwamba moja ya mambo magumu kwa manaume yoyote yule (na kwa wanawake pia) ni pale uhusiano na mwenza wako unapovunjika.Mara nyingi wanaume wengi wanapokumbwa na tatizo hilo hujipa matumaini potofu kwamba maisha yataendelea kama kawaida licha ya ukweli kwamba mioyoni mwao wanaumia vya kutosha.Wengi huendelea kujifariji na matumaini 'feki' kuwa wenza waliowabwaga watarejea.

Matokeo ya matumaini hayo 'feki' ni mithili ya mkuki wa kukataliwa wenye makali pande zote (double edged sword of rejection).Kwanza ni maumivu yanayotokana na ukweli kwamba umebwagwa,na kisha ukweli mwingine unaofuatia baadaye kuwa matarajio feki kuwa mwenza atarejea,well,yalikuwa feki.Mwenza wako ndio ameondoka moja kwa moja,na hatorejea (hapa tunazungumzia kubwagana ambako hakuna dalili wala uwezekano wa suluhu).

Lakini maumivu haya yanaweza kufupishwa kwa aliyebwagwa kutambua kuwa hali ndio hiyo-ameshabwagwa na hakuna uwezekano wa kurejea katika hali ilivyokuwa awali.Kuendelea kusubiri na kutarajia miujiza ni sawa na kujifungia kwenye mzunguko wa mateso usio na mwisho (endless circle of turture).

Kwahiyo ili kumudu kuendelea na maisha yako ya kawaida baada ya kubwagwa (au hata kubwagana) jaribu kufuata njia zifuatazo:

ACHA KUJILAUMU

Mara nyingi sie wanaume tumejenga tabia ya kuwa mithili ya watoto wakubwa (big babies) ambapo hatuachi kujilaumu.Kubwagwa ni kama kunaongeza ukubwa wa tabia hii.Kuna wanaochukulia kubwagwa kama mwisho wa dunia,yaani kana kwamba kuondoka kwa mwenza wako maishani mwako ni kama ameondoka na sababu ya wewe kuendelea kuishi.

Lakini ukijaribu kidogo tu kujiuliza "Niliishije kabla sijakutana na huyu aliyenibwaga?" utagundua kuwa ulikuwa ukiishi kama kawaida,na kama binadamu wengine.Kwahiyo,huu ni ushaidi tosha kuwa kama uliwahi kuweza kuishi bila mwenza aliyekubwaga ni dhahiri unaweza kuishi pia baada ya mwenza huyo kuondoka maishani mwako.Acha kujilaumu,jipange upya,na endelea kuishi.

FUTA KUMBUKUMBU

Kama nilivyoandika hapo juu,wengi wa wanaume wanaobwagwa huendelea kuwa na matumaini 'feki' kuwa mwenza aliyeamua kuondoka atarejea.Kwamba labda ni tisha toto tu,au anatikisha kiberiti tu.Mara nyingi wanaume tunapobwagwa hatupendi kukiri hadharani kuwa inatuuma.Wengi wetu hujifanya jasiri mbele ya 'washkaji' zetu tukijigamba kuwa 'ahh yule demu anadhani mimi nitababaika kwa vile tumeachana' (actually huwa tunakwepa kutumia neno 'kanibwaga').

Kiasili,katika mahusiano wanaume wengi wanapenda kuwa ndio walioshika usukani.Kwahiyo hata wanapobwagwa bado watajaribu kudanganya umma kuwa wao ndio waliokuwa wa kwanza kubwaga.Lakini kimsingi huko ni kujidanganya kwa sababu hao unaojaribu kuwaaminisha ujasiri wao hawajali sana (na pengine nao wana ishu zao binafsi zinazowanyima nafasi ya kujihangaisha na ishu zako).

Penigne una picha za mwenza aliyekubwaga,au zawadi mbalimbali alizokupatia wakati wa uhusiano wenu.Licha ya kubwagwa,unaweza kuogopa kuzitupa kwa hofu kuwa labda atarejea na akikuta azawadi alizokupatia hazipo atakasirika na kuondoka tena.Tumia akili yako vizuri.Ameondoka jumla,hatorudi.Usijaze bure nafasi kwenye albamu yako au kwenye sehemu unapoweka zawadi/kumbukumbu zako kwa matarajio hewa.

Uwepo wa kumbukumbu hizo (picha, zawadi,nk) ni sawa na uwepo wa mwenza aliyekubwaga kiroho japo si kimwili.Kila utakapoziona utaendelea kumkumbuka na kutamani awepo au arejee maishani mwako.Ukweli ni kwamba hatorejea.Cha kufanya basi ni kuteketeza kila kumbukumbu ya huyo aliyekubwaga.Hufanyi hivyo kwa ajili ya hasira bali ni kujipa nafasi ya kuendelea na maisha yako kama yalivyokuwa kabla hujakutana naye.Kumbuka,utakapopata mwenza mwingine hutazihitaji kumbukumbu hizo,sio tu kwa vile tayari una mwingine lakini pia itamsaidia mwenza wako mpya kupata uhakika kuwa wewe ni wake peke yake.

JIREJESHE KWA ULIOWATELEKEZA

Wengi wetu tunafahamu jinsi mapenzi motomoto yanavyoweza kutuweka mbali na watu wetu wengine wa karibu.Si kwamba tukiwa kwenye mapenzi tunawasahau watu hao lakini mara nyingi ni maotkeo ya kuweka akili na nguvu zaidi kwenye mahusiano yetu na wenza wetu,na hivyo kupata fursa finyu ya kuwa karibu na watu wetu wa karibu (kwa mfano wanafamilia wenzetu,ndugu,jamaa na marafiki).

Kufanya kosa si kosa bali kurejea kosa.Na alimradi wakati uko na mwenza wako hukuwafanyia dharau watu wako wa karibu basi ni dhahiri utakaporejea kwao (na pengine kuwafahamisha bayana kuwa umebwagwa) watakuwa radhi kukupokea.Kuwa karibu na watu wako wa karibu kutakusaidia sana kukarabati maisha yako,hasa kwa vile walikuwa nawe hata kabla hujakutana na huyo aliyekubwaga.

Kumbuka,mara nyingi hawa ni watu wanaokupenda kwa dhati- aidha kwa vile ninyi ni damu moja au ni watu uliopitia nao kwenye milima na mabonde.Kwa wanafamailia na ndugu,hawa kiasili ni watu ambao tunapaswa kuwa nao kwa vile tofauti na uchaguzi tunaokuwa nao kudeti mtu fulani au la,sheria za kibinadamu hazitupi fursa ya kuchagua nani tuzaliwe naye au atuzae.Ukaribu na watu wako wa karibu utasaidia kukukumbusha nani mwenye umuhimu wa kweli katika maisha yako.

USIKURUPUKE 

Hapa unaonywa usikurupuke kutaka kuanzisha uhusiano mwingine kuziba pengo la yule aliyekubwaga.Uzoefu unaonyesha kuwa mara nyingi jitihada za haraka haraka kutaka kuziba pengo hilo huishi kwenye maumivu/majonzi zaidi kuliko mafanikio.Tatizo kubwa hapa ni kwamba katika papara ya kutaka kuziba pengo hilo,unaweza kukosa muda wa kumwelewa vyema huyo 'unayemfukuzia.' Mara nyingi jitihada hizo huelemea zaidi kwenye kupata 'demu bomba zaidi ya yule aliyenizingua.' Lakini kama wasemavyo waswahili,usione vyaelea vimeundwa.Huyo 'demu bomba' anaweza kuwa na mwenza wake au ana 'pozi nyiiingi' ambazo sana sana zitaishi kukuumiza tu.

Suluhisho ni 'kutuliza boli.' Vuta pumzi.Angalia sababu zilizopelekea ukabwagwa au mkabwagana na mwenza aliyetangulia.Ukishaelewa chanzo/sababu itakupatia nafasi nzuri ya sio tu kuepuka kurejea makosa ya awali bali pia kujenga uwezekano wa kupata mtu aliye bora zaidi ya aliyetangulia.

JIHAMASISHE

Wengi wetu tunapobwagwa tunakuwa mateka wa hasira.Na katika hasira hizo baadhi yetu hujikuta tukifanya vitu vya kitoto,kijinga na visivyo na maana kabisa.Si ajabu kuona mtu akibwagwa akakimbilia kwenye waal ya Facebook profile ya aliyembwaga na kutundika 'madudu' yenye lengo la aidha kumuumiza mhusika au kujaribu kumshawishi arejee.Unaweza kukidhi mahitaji yako kwa dakika au siku chahe lakini mara nyngi matokeo ya 'upuuzi' wa aina hiyo huwa sio mazuri hasa pale utakapobaini kuwa 'kujigonga' kwako hakujafanikiwa kubadili msimamo wake.

Kumbuka,aliyekubwaga anaweza kuwa anafuatilia kwa karibu namna unavyodili na uamuzi wake.Matarajio ya wengi wanaobwaga wenza wao ni kuwa aliyebwagwa ataumia,atakonda,atateseka au,kwa hakika,ataaanza kubembeleza.Hiyo ni attention seeking.Na hakuna dawa mwafaka kwa attention seekers kama kuwapuuza.Kuendelea na maisha yako kana kwamba hakuna lililotokea sio tu itakuwa kama kumwadhibu attention seeker aliyekubwaga (ie kuvunja matumaini yake kuwa amekuumiza na labda utambembeleza) bali pia utakuwa unajisaidia wewe mwenyewe kuendelea na maisha yako kama kawaida.

Kisasi kikubwa kabisa kwa aliyekubwaga ni kwa wewe kupata mafanikio.Yaani badala ya wewe kuonekana umekondeana kwa mawazo ya kubwagwa,siku ya siku unakutana na aliyekubwaga na kukuona ukiwa mwenye furaha na mafanikio.Na kwa vile 'what goes around always comes around' si ajabu aliyekubwaga kwa wakati ho atakuwa anajutia kwanini alichukua uamuzi huo-lakini hawezi kukubembeleza mrejeane kwa sababu yeye ndiye aliyeamua bila kulazimishwa kuwa mwachane.

Pata picha,baada ya kubwaga unaelekeza nguvu zako kwenye kujiendeleza kimaisha (kitaaluma au kikazi),unatumia muda wako kujenga mwili wako kwa mazoezi, na kwa vile Mungu humjalia kila anayejituma,unafikia mafanikio yanayoweza kugeuza shingo za watu (ya kutamanisha).Mafanikio ni sawa na sumaku,lazima yatakusaidia kuongeza nafasi zako za kupata mwenza bora,pengine bora zaidi ya yule aliyekubwaga.Sasa siki ua siku,mwenyewe umenawiri vyema kutokana na kazi inayolipa vyema,na pembeni una mwenza bora,kisha unakutana na aliyekubwaga awali akiwa kachoka kimaisha na pengine akiwa na mwenza wa ovyo ovyo.Anashindwa kujizuia na kujikuta anakuuliza "hey fulani uko wapi siku hizi...naona mambo si mabaya..."Usiwe na haraka ya kujibu bali jitahidi kadri uwezavyo kuachia kicheko cha dharau....na badala ya kujibu swali lake mkebehi kwa kurejea swali lilelile na pigiria msumari kwa "hata wewe naona mambo si mabaya"...na kicheko kingine..Hiyo inaitwa kushinda vita bila kwenda vitani.

AMKA NA ENDELEA NA SAFARI

Vyovyote utakavyofanya huwezi kumzuia mwenza aliyedhamiria kukubwaga.Pengine amepata mtu aliye bora zaidi yako,pengine ameamua tu.Kama binti anatamani kuwa na mtu mwenye uwezo mkubwa kifedha kuliko wewe,kuendelea kumbembeleza mwendelee kuwa pamoja kutakuingiza kwenye vishawishi vya ufisadi,au matendo mengine mabaya ambayo si ajabu badala ya kukusaidia kumridhisha mwenza wako yakaishia kukupeleka jela.Naamini umeshaona au kuskia stori kibao za watu waliolazimika kujiingiza kwenye uhalifu ili kupata fedha za kuwaridhisha wenza wao.

Of course,mwenza wako ana haki ya kutaka kilicho bora.Lakini hiyo sio sababu ya kutaka uurefushe mkono wako zaidi ya uwezo wake.Mwneza wako ana haki ya kukupa changamoto za koboresha maisha yako/yenu lakini sio kwa namna ya kukusukuma uhatarishe maisha yako kwa ajili yake.Kumbuka,kama maisha yake ni muhimu,yako ni muhimu pia.Kama anakupenda kwa dhati atakubaliana na hali yako alimradi isiwe hali yako ni matokeo ya uvivu au uzembe wako au uoga wako kijituma.

Kwa hiyo badala ya kuendelea kuifanya hali ngumu (kubwagwa) kuwa ngumu zaidi,futa machoz yako,amka na endelea na maisha yako.Katika saikolojia kuna imani kwamba mengi ya tunayoyaita matatizo ni matokeo ya fikra zetu tu.Njaa,kwa mfano,si lazima imaanishe mahitaji ya mwili (tumbo) bali ni fikra kuwa tumbo linahitaji kitu fulani.Tamaa ni hali ya kutamani usichokuwa nacho hata kama si cha muhimu.Badala ya kujipa moyo kuwa mwenza wako atarudi aua atajilaumu kukubwaga,kwanini usielekeze fikra zako kwenye masuala mengine ya muhimu katika maisha yako?Kumbuka wewe ndiye nahodha ya maisha yako,kumkabidhi mtu mwingine jukumu hilo sio tu kunaondoka uhuru wako wa kukufikisha unakotaka kwenda bali pia kuna hatari ya kupotezwa.

Kwa leo inatosha!

MAKALA HII IMEANDALIWA KUTOKANA NA VYANZO MBALIMBALI MTANDAONI HUSUSAN MTANDAO WA AskMen 

MAKALA IJAYO ITAZUNGUMZIA IMANI ILIYOJENGEKA MIONGONI MWA MABINTI/WANAWAKE WENGI WA KITANZANIA KUWA WANAUME WA KITANZANIA NI MAHIRI KWA KU-CHEAT,AU KUNUKUU KIUSAHIHI, "OVYO KABISA", "BURE KABISA", "CHU*I MKONONI", NA KAULI KAMA HIZO.KICHANGAMSHA UBONGO: JE TABIA YA MWANAUME (AU MWANAMKE) INA MAHUSIANO YOYOTE NA URAIA WAKE?

HADI MUDA HUO,NAKUTAKIA SIKU NJEMA




Mdau mmoja mkubwa wa blogu hii amenitumia ujumbe ufuatao,nami naomba niuwasilishe kama ulivyo 


20/09/2011 09:00 kaka chahali.....naheshimu sana kazi zako za uandishi....ila kwahili nahisi umekosea

nikweli magamba wanafanya kila wawezalo huko igunga ila kutumia picha isiyo na uhalisia juu ya tukio hilo ni jambo la kudhalilisha taaluma yako ya uandishi.....

Picha ya kwanza ni imepigwa morogoro na si igunga na tena ilikuwa ni mashindano ya kula .....verify it here http://issamichuzi.blogspot.com/2011/07/mashindano-ya-kula-yafana-sana-mkoani.html

chonde ni heri kutoa habari bila picha kuliko kucopy and paste picha za matukio mawili tofauti....

ningefurahi kama utalitolea ufafanuzi jambo hili....

Regards,KM
mdau ninayefatilia kazizako twitter,facebook na kwenye hii blog yetu tuk


Baada ya kufuatilia kiungo (link) kilichobainishwa na mdau huyo nimegundua kuwa chanzo cha picha husika (ambacho ni jukwaa la mtandaoni la Jamii Forums) hakikuwasilisha picha husika kwa usahihi.

Naomba kutumia fursa hii kuomba radhi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wote walioguswa na picha husika.Kuna nyakati waandishi hujikuta katika wakati mgumu kuthibitisha uhalisia wa kila habari,picha au chanzo cha habari/picha husika.

Lakini ni matumaini yangu makubwa kuwa kila msomaji wa blogu hii ataiga mfano wa mdau MK pindi kunapojitokeza mapungufu au makosa ya aina yoyote ile.Kwangu,kukosolewa ni miongoni mwa njia za kujifunza na kujirekebisha.Naomba kumshukuru sana mdau MK kwa ujumbe wake,na ninatumini tutazidi kushirikiana.


Kikwete mtegoni tena
• Asaini tangazo la serikali lililochakachuliwa

na Waandishi wetu

RAIS Jakaya Kikwete amedanganywa tena na baadhi ya watendaji wake, akasaini tangazo lililochakachuliwa.

Septemba 5 mwaka huu, Kikwete alisaini tangazo la kusudio la uanzishaji wa wilaya mpya ya Butiama, lakini katika namna ya kushangaza, sasa inaonekana eneo la wilaya mpya ni Nyamisisi.

Hali hiyo inayotia fedheha kwa Rais wa nchi, imebainika juzi wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipofika Butiama kuzuru kaburi la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Pinda alilazimika kuwatuliza wakazi wa eneo hili waliotaka kujua sababu za msingi za Rais kubadili msimamo wake na kuhamishia makao mapya yaliyotakiwa kuwa Butiama na kuyapeleka Nyamisisi.

Pinda alikiri bayana kuwa Rais alisaini tangazo hilo akijua kuwa kilichoandikwa ni makao makuu kuwa Butiama bila kujua eneo lililoandikwa ni Nyamisisi.

“Hata kama kuna mtu alitaka makao makuu yawe Nyamisisi, kwa kweli haikupaswa hiyo Nyamisisi kuchomekwa hivyo. Hata mngeniuliza mimi makao makuu yawe wapi, ningesema lazima yawe Butiama tu,” alisema Pinda na kushangiliwa.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema tangazo hilo lilikuwa na makosa kutokana na kutaja eneo la makao makuu tofauti na lile lililopendekezwa.

Pinda alisema mpango wa serikali ulikuwa ni makao makuu ya wilaya hiyo yawe katika kijiji cha Butiama ili kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Akijibu malalamiko ya wakazi wa Butiama, walioingia katika eneo la nyumba hiyo, wakimtaka atamke kuwa makao makuu yatakuwa Butiama, Pinda alisema:

“Hili la Butiama kwa kweli linaleta manenomaneno. Sisi serikalini tulidhani ukiwa na wilaya ya Butiama na makao makuu ni lazima yawe Butiama, ili tumuenzi Baba wa Taifa.

Hata hivyo, alisema pamoja na tangazo hilo kuchomekwa neno Nyamisisi, bado mtu aliyefanya hivyo hajafanikiwa, kwani tangazo hilo sio uamuzi wa mwisho wa kuhusu suala hilo.

Aliwataka wananchi wa Butiama kulichukulia tangazo hilo kuwa ni pendekezo tu ambalo wanapaswa kulitolea maoni yao kuhusu kulikubali au kulikataa na kwamba maamuzi ya mwisho kuhusu wapi yawe makao makuu ya wilaya hiyo yatatokana na maoni ya wananchi wenyewe.

Alisisitiza kuwa Butiama ikiwa wilaya sio tu huduma za msingi zitaboreshwa na kuwapa watu sababu ya kwenda wilayani hapo, bali pia itawapa sababu ya kwenda kuzuru nyumbani kwa Hayati Baba wa Taifa.

Pinda pia alimpa fursa mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, kutoa kauli yake kuhusu suala hilo, ambaye alisema yeye asingependa kuliingilia suala hilo.

“Hili suala halina tatizo, ninyi na wananchi wote mtakavyoamua ndivyo iwe hivyohivyo,” alisema Mama Maria.

Maswa watishia kuandamana

Katika hatua nyingine, hatua ya Rais Kikwete kuunda mikoa mipya, imezua balaa baada ya mamia ya wananchi wa wilaya ya Maswa, mkoa wa Shinyanga kuandaa maandamano iwapo serikali itaamua kuyaweka makao makuu ya mkoa mpya wa Simiyu katika wilaya ya Bariadi.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Uwanja wa Nguzo Nane na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa wilaya hiyo, wananchi hao wamedai kuwa hawako tayari kutendewa hivyo na wataandamana hata ikilazimu kupigwa risasi.

Katika mkutano huo ulioitishwa kwa ajili ya kutoa maoni ya mapendekezo juu ya nia ya serikali ya kupeleka makao makuu ya mkoa mpya wa Simiyu mjini Bariadi, wananchi hao wamesema uamuzi huo ni dharau kwao na unataka kufanywa kwa ajili ya manufaa ya viongozi wachache.

“Sisi wana Maswa tutaandamana bila kujali itikadi za vyama kama hatutasikilizwa na tuko tayari kupigwa risasi. Hatuwezi kunyang’anywa haki yetu kwa ajili ya ubinafsi wa viongozi wachache,” alisema mkazi mmoja wa Maswa, Thomas Nkola, na kushangiliwa na umati wa wananchi.

Walisema kuwa viongozi wa mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Bariadi wamekuwa na desturi ya ubinafsi katika masuala yenye maslahi ya umma kitendo kilichodhihirika katika ujenzi wa barabara ya lami ya Mwigumbi –Maswa-Lamadi.

“Viongozi wetu wa mkoa wa Shinyanga na wa Bariadi wametuona sisi wa Maswa watulivu sana hivyo wanatumia mwanya huo kutuchezea.

“Mfano ujenzi wa barabara ya lami ya Mwigumbi-Maswa-Lamadi ilitakiwa ianzie Mwigumbi kuja Maswa lakini kutokana na ubinafsi wao imeanzia Bariadi kwenda Lamadi,” alisema mwananchi mwingine, Samwel Kidima.

Walisema licha ya mapenzi mema aliyonayo Rais Jakaya Kikwete ya kuanzisha mkoa huo, ni vizuri mchakato wa kupata makao makuu yake ukaanza upya kwani wa awali haukupitia katika vikao halali kama vile baraza la madiwani na kamati za ushauri za wilaya (DCC) hali ambayo imezua mgogoro mkubwa na kufanya kutokuwepo kwa mahusiano mazuri kati ya wananchi wa wilaya hizo.

“Rais Kikwete alipoamua kuanzisha mikoa na wilaya mpya alikuwa na nia nzuri sana lakini jambo la kushangaza mchakato wa kutoa mapendekezo ya makao makuu ya mkoa wa Simiyu hayakufuata utaratibu kwani ilitakiwa uanzie katika vikao vya baraza la madiwani na kamati za ushauri za wilaya ndiyo maana jambo hili limezua mgogoro mkubwa na sasa mahusiano kati ya wananchi wa wilaya ya Maswa na Bariadi si mazuri hivyo mchakato uanze upya,” alisema Edward Bunyongoli.

Walisema iwapo serikali itabaki na msimamo wake huo basi wao wataendelea kubaki katika mkoa wa Shinyanga lakini hawako tayari kukubaliana na uamuzi huo uliofanywa kwa ajili ya maslahi ya watu wachache wabinafsi.

“Kama serikali itabaki na msimamo kuwa Bariadi ndiyo makao makuu ya mkoa wa Simiyu sisi tutabaki katika mkoa wa Shinyanga kwani hatuko tayari kukubali uamuzi huo uliotawaliwa na vitendo vya kifisadi,” alisema Kulwa Nangale.

Hii si mara ya kwanza kudanganywa kwa Rais kwani ameshadanganywa zaidi ya mara 12 miongoni mwa mambo aliyodanganywa ni pamoja na ile ya kuzindua mradi wa Bwawa la Manchira lililoko wilayani Serengeti wakati tayari wananchi wamekwishafungua kesi Mahakama Kuu ya Mwanza wakidai fidia.

Kesi hiyo iliyofunguliwa ni matokeo ya viongozi wa serikali wilayani humo kuhusika kuwalipa fidia watu wasiohusika na kuwaacha walengwa waliofanyiwa tathmini.

Pia aliwahi kudanganywa kwamba daraja la Mkenda lililoko Ruvuma ambalo ni njia muhimu kuelekea Msumbiji, lilikuwa limekamilika.

Katika tukio jingine, Rais aliwahi kupewa taarifa zisizo sahihi kuhusu tuhuma za rushwa zilizokuwa zikimkababili Anatory Choya kisha akamteua kuwa mkuu wa wilaya, lakini siku siku chache baadaye akafunguliwa mashtaka na TAKUKURU.

Mwaka juzi, akiwa ziarani Mbeya msafara wa Rais ulishambuliwa kwa mawe na watu, lakini wasaidizi wake wakaja kutoa taarifa kwamba watu hao walikuwa ni wahuni na walikuwa wakimsubiri Rais kwa muda mrefu bila mafinikio.

Hata hivyo, baadaye uchunguzi huru ulibainisha kwamba tukio hilo lilikuwa na mafungamano ya kisiasa na makovu ya mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM kwa mwaka 2005.

Mlolongo huo mrefu wa upotoshaji taarifa kwa Rais uliibuka tena katika utoaji wa magari ya misaada ambapo badala ya kupewa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Longido alipewa wa Ngorongoro.

Tukio hilo lilimfanya mkuu huyo wa nchi kukasirika na kumzodoa mkurugenzi huyo, lakini baadaye ikabainika mkurugenzi huyo alikwenda kutokana na makosa ya maafisa wa Ikulu.

Katika mlolongo huo, tukio kubwa kabisa ni Rais kutia saini kwa mbwembwe Sheria ya Gharama za Fedha za Uchaguzi ambayo ilichomekwa vipengele nje ya Bunge kitu ambacho ni kinyume cha sheria.

Tukio hilo ambalo ni la uvunjifu wa Katiba, liliibuliwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, ambaye awali, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fedrerick Werema, alikanusha.

Hata hivyo, baadaye sheria hiyo ilirudishwa bungeni na kukarabatiwa kwa mgongo wa mabadiliko ya sheria mbalimbali.

Mei mwaka jana, Rais alipewa taarifa za upotoshaji kuhusu mazungumzo ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) na serikali, kwa kuelezwa shirikisho hilo halikuhudhuria mkutano wa saa 4:00 asubuhi kama ilivyopangwa.

Hata hivyo, TUCTA wakatoa ushahidi wa barua za mwaliko wa mkutano huo wa Aprili 22 mwaka jana, ambazo zilikuwa mbili, moja ikionyesha walitakiwa kufika katika mazungumzo Hazina saa 4:00 asubuhi na nyingine saa 8:00 mchana.

Katika kuonyesha upotoshaji kwa Rais, wasaidizi hao walimpa barua iliyokuwa ikionyesha walipaswa kukutana saa 4:00 asubuhi huku ile ya saa 8:00 wakawa wameificha.

Rais akizungumza na wazee wa mkoa wa Dares Salaam aliwashambulia viongozi wa TUCTA hasa Naibu Katibu Mkuu, Nicolas Mgaya, akimwita mnafiki, mzandiki, na mchochezi.

19 Sept 2011

 
SALAM,
Habari zenu wadau wote popote Duniani Tunapenda kuwasalimu wakubwa Shikamoo na tulio Umri sawa Mambo zenu!, Baada ya salamu hizi tunapenda kuwaletea habari njema sana kwa wazazi na wanafunzi ambao walikuwa wamefanya mtihani kidato cha sita lakini hawakufanikiwa kuyaona majina yao wakati wa Selection ya kwanza, Lakini muda sio mrefu sana yametoka majina mapya ya Second Selection ambapo utaweza Bahatika kuliona jina lako, la ndugu yako, rafiki ama mwanao. Tunawaomba mkipata taarifa hii muwape na wengine pia ili wapate kutazama majina hayo. mwisho tunawapa hongera sana wale walio chaguliwa kwa mala ya kwanza na hawa ambao mmechaguliwa kwa mala ya pili. Web site ya Matukio na wanavyuo itaendelea kuwaletea habari zaidi za vyuo mbali mbali Tanzania. 

Nyongeza: Tunaomba sana ushirikiano wenu uongozi wa vyuo mbali mbali Tanzania, ikiwa ni kututumia matukio mbali mbali ambayo yanatokea katika vyuo vyenu, mfano mikutano,mahafari na mambo kama hayo, pia kama mna applications za kutaka wanafunzi wajiunge na vyuo vyenu pia tunakaribisha sana na matangazo mengine. Kwa wanafunzi wa vyuo mbali mbali Tanzania pia tunawaomba ushirikiono wenu wa ukaribu wa kututumia matukio mbali mbali sisi ni wasimamizi tuu wa kupost habari lakini mshiriki mkuu ni wewe msomaji na mtumaji wa matukio. Lengo ni kuwaunganisha wanafunzi wote wa vyuo Tanzania. Pamoja tunaweza 

Matukio yote ama kitu chochote tutumieni kupitia Barua pepe: [email protected]
Asanteni sana
Matukio na wanavyuo Crew


BOFYA HAPA CHINI KUONA MAJINA HAYO
 

BEFFTA Founder Pauline Long with Frank from Urban Pulse
Beutiful ladies in the house
Dj Abbas with Miss Jestina George
Live perfomance
 
 
Urban Pulse and Miss Jestina George who's blog www.missjestinageorge.blogspot.com has been nominated as Blog of the Year, had the pleasure of attending the 3rd BEFFTA AWARDS nomination party at the London Hilton on Park Lane on Friday 16 September 2011.
URBAN PULSE CREW with Entrepreneurs
 
The party was awesome full glamour and excitements with Celebrities guests, Enterpreneurs, Shakers & Movers in showbiz.
Sola Oyebade from MAHOGANY PRODUCTION adressing to the invited guests during the launch party at Hilton Park lane Hotel, London
 
BEFFTA Awards is a distinctly special awards ceremony honouring the best showbiz and entertainment personalities in the black and ethnic communities in the UK, USA and globally. BEFFTA Awards is the first of its kind rewarding under one roof outstanding achievements and contributions from Africans, Caribbeans and Asians in entertainment, film, fashion, television and arts. This international prestigious ceremony celebrates an all round accomplishments of a hard working community within entertainment and showbiz especially the unknown talent that need exposure. The awards ceremony founded by Pauline Long also aims to inspire black and ethnic personalities worldwide to achieve at the highest levels.
 
The nomination categories were as follows:
 
MusicDance
Comedy
Radio
Newspapers
Magazines
Blogs
Events
DJ
Photographers
Fashion Category:
Fashion Designers
Stylists
Make-up Artists
Fashion Choreographers
Models
Beauty Pageants
Film Category
TV Category
ART Category
 
 
BEFFTA  Awards – Black Entertainment Film Fashion Television and Arts will be on the 22.10.2011
Thanks,
 

One of this year's BEFTA Award nominee Jestina George from Miss Jestina George Blog posing for the camera during the lauch party

URBAN PULSE CREATIVE In Association with MISS JESTINA BLOG

18 Sept 2011

Umoja Wa Bloggers Wa Kitanzania
September 17, 2011

Dear Tanzanian Bloggers,

Do you guys have a union? Why don't you create a Tanzania bloggers union? Haya ni maswali nimekua nikiulizwa na watu mara kwa mara…Kila muda kidogo huwa napokea email inayohusu hili jambo. Nimejitahidi sana kukaa mbali na hii topic lakini kila ninavyofunga macho ndio emails zinazidi kuuliza lini umoja utaanzwisha? Je upo umoja wa watanzania.

Mimi kukaa mbali na hili suala na kuwajibu watu ni kuwa mimi naamini umoja wa kitu chochote unaanzishwa na watu kwa mapenzi yao. Na umoja huo ni lazima uwe na malengo na faida za kuwa mwanachama katika umoja huo. Bila hilo kutakua hakuna maana ya kuwa na umoja au hata ukiwepo hautadumu. Halafu lingine lililokua linanifanya mimi niwe mbali na hii issue ni kuwa mimi sina blog. Ni hivi karibuni tu ndio nimefufua blog yangu ambayo nilikua nayo zamani lakini sikuiendelezaga baada ya kupokea email ya kijana wa miaka 14 akiniambia huwa anafuatilia sana Tanzanian blog awards site na ameona kuwa ninahamasisha sana watu wawe na moyo wa kupenda kuwa na blogs lakini hajaona blog yangu. Hiyo ndio ilikua aha moment yangu. Nikakumbuka ule msemo unaosema “Talk the talk and walk the walk.”.

Anyway baada ya kufikiri sana nimeona kwa vile sasa hivi technology inaweza kuwakutanisha watu kwa urahisi kutoka pande zote za ulimwengu hivyo inaweza kuwa rahisi kwa wale watakaopenda kujiunga kuweza kuwasiliana na kujadili mambo yao kwa urahisi. Na kwa vile kama tunavyofahamu muda sio mrefu Google+ itakua inapatikana kwa kila mtu na itakua inaweza kuwaunganisha watu 10 kwa wakati mmoja hivyo nikafikiria labda kwa kutumia technology hii kuna kitu cha maana kinaweza kufanyika.

Kwa muda huu mfupi nimepata experience kubwa sana kuhusu blogs za watanzania walioko ndani na nje ya Tanzania. Kuna baadhi ya bloggers nimeweza kufahamiana nao katika personal level. Ila baada ya kuongea na wengi ni kuwa sasa hivi nikiwa nasoma blog yeyote ambapo mwandishi wake yupo Tanzania nasoma na kuiangalia tofauti na kama nilivyokua naangalia hapo nyuma. Well, blog yeyote ni lazima kuipa heshima kwa blogger anayeiandika bila kujali yupo wapi lakini baada ya kuongea na bloggers wengi nimegundua mazingira na vitendea kazi wanavyotumia kuili kuweza kufanya blog zao ziwe nzrui ni taabu sana. Blogs nyingi ni nzuri na zina idea nzuir lakini hao bloggers wakiulelezea jinsi wanavyofanya kuweza kupost chochote unakaa chini na kujiuliza WHY and always don't take things for granted.

Hivi mnafahamu kuna bloggers wengine mpaka leo wanatumia internet cafés kumaintain blogs zao. Just imagine mtu anaacha kuingia kwenye internet café ajisomee kwenye net mambo anayotaka anakalia kuweka blog ili mimi na wewe tusome yale anayoyapost. Kuna watu wengine bado wanatumia computers za kazini kublog na watu hao wameniambia kuwa huwa wanawahi kazini mapema ili watumie computer za kazi kabla muda wa kazi haujaanza. Wengine wanaskip lunch breaks zao ili watumie huo muda kublog. Na kuna baadhi wameniambia wao wanaruhusiwa kwenda na nyumbani na laptop za kazini lakini huyo mmoja alinichekesha…It is not a a laughable issue lakini alisema laptop battery charge yake ni ndogo sana sometimes akiwa kwenye daladala anatumia kidogo by the time akifika nyumbani battery imeisha na nyumbani hakuna umeme. Hivyo anakua yupo na laptop lakini hawezi kufanya chochote nayo.

Yaani kuna mambo mengi sana ambayo nimekaa nikajiuliza how can we help? Ndio nikasema once tukishajua watu wangapi wanapenda au watajiunga then agenda inayofuata ni kuweka fundraising. Siku hizi kuna online fundraising sites nyingi tu ambazo huwa tunaweza kuanzisha na zinaonyesha how much watu wamecontribute na baada ya hapo…Kuna off lease laptop very reasonable price zinaweza kupatikana na kusaidia bloggers wa kitanzania who are really in need. Kuna mambo mengi sana kama sio hawa bloggers wa kawaida kuweka wengine wetu wala tusingeweza kuona wala kufahamu. Sasa what is our appreciation? Kama tusipotafuta njia ya kusaidiana nani atakuja kutusaidia? Hata tukiweza kukusanya na kununua moja ni better than nothing. Ni bora kulikokukaa tu na kusema kila mtu atajisaidia mwenyewe.

That is why I am presenting this to you guys …Email me for any suggestions and how we can do and then we will start from there….

Mimi nilichokua nafikiria kwa kuanza kila bara atokee mtu mmoja takayependa kuwa mwenyekiti wa bloggers walioko huko..Hao watu watawasiliana ana kuchagua mwenzyekiti wa wate..Na kama watu watakua wengi basi kuwe na msaidizi na katibu katika kila bara..Kama ni wachache basi itajulikana baadaye jinsi ya kufanya. I don't think kutahitajika cashier mpaka huko mbele kukishaundwa kitu cha maana. Na nadahani itakua fair hao viongozi wawe at least wamekua na blog kwa zaidi ya miaka miwili.

Mimi nipo willing to organise and help to put together this baada ya hapo nitawaachia wanaochagulia na kubakia as a just mwanachama. Hivyo nimeweka hiyo form hapo ili nione ni watu wanagapi wanataka kujiunga. Kwa sababau hatakwenye hii newsletter kuna mambo naona hayanihusu mimi kuyatuma na hayo mambo yangekua vizuri yakitumwa kwa bloggers kma wangekua na umoja.

Na labda niweke clear kama watu wakipatikana huo umoja sio lazima Kwa kila blogger kujiunga. Na pia kujiunga au kutojiunga haitasababisha mtu kuingia katika mashindano yetu au la. This will be two separate things as I said before nikishaweza kusaidia kuput together kama kuna vitu vya kuforward kwa viongozi I will do that and step aside.

Kuna vitu vingi vitaweza kufanyika kwa bloggers vikiwa under umoja wa bloggers.

Okay nasubiri kusikia kutoka kwenu.. Na form ya kutaka kufahamu ni watu wangapi watapenda kujiunga nimeiweka kwenye hiyo site...

Pauline
Founder, Tanzanian Blogs Awards



PRESS RELEASE
BEN TELEVISION
25 ASHLEY ROAD
TOTTENHAM
LONDON, N17 9LJ

09/Sept/2011

RE: PRESS RELEASE
RE: BEN TV DIPLOMATIC AWARDS 2011
This to announce that The Tanzania , Uganda and Kenya High commissions in London have been nominated to receive awards in the following categories:

· Diaspora growth, development and involvement

· Good customer service at the High commission/embassy

· Positive projection of country’s image abroad

· Economic and Cultural diplomacy

· Country’s Human Development


Other categories to be awarded are:
Diplomat of the year from Africa, Caribbean and Pacific 2011
Diplomat of the Year from the Americas
Deputy Head of mission of the year
Distinguished contribution to diplomacy

The night will recognise and celebrate the diplomatic achievements made within the African, Caribbean and Pacific regions on the 4th November 2011 at the Hilton park lane Hotel

Which category do you think fits your High commission? Please send your entries, comments and nominations to [email protected], or [email protected]

The BEN TV DIPLOMATIC AWARDS will be adding glamour to Africa’s Golden Jubilee celebrations with:

* Top Nollywood stars & the best of African film stars
* UK celebrities and crème de la crème
* Diplomats and professionals


For further information: email [email protected],newdealafrica.co.uk

Signed.
Ayoub mzee
Public/current Affairs Desk
BEN TV SKY 184
TEL + 44 7960811614/+442088088800

Notes
Africa is truly a great nation with great people. We celebrate Africa at 52. We celebrate you and other great people like you as an inspiration to the next generation of leaders.

BEN TV is a Black and ethnic oriented ,urban , diverse and cosmopolitan Family channel ,established to provide a whole some mix of entertainment ,educative and informational programmes suitable for family viewing .It also includes a range of cultured programming to empower ,transform and challenge the conventional perception of Africa, Caribbean and African Diaspora


Ajali Ya Boat Ya Zanzibar

Kama wote tunavyofahamu taifa limepatwa na msiba mkubwa sana kutokana na ajali ya boat iliyotokea huko Zanzibar. Tunaomba Mwenyenzi Mungu awape faraja wale wote waliopoteza ndugu, jamaa au marafiki katika ajali hii na pia tunaomba Mwenyenzi Mungu awaweke mahali pema wale wote waliopoteza maisha yao katika ajali hii. Katika kipindi hiki kigumu tumeweza kuona kwa mara nyingine tena jinsi social medias zilivyo na mchango mkubwa katika jamii zetu. Kwa vile ajali hii ilitokea mwisho wa week blogs zilisaidia sana kutoa habari kwa haraka sana kuhusu ajali hii kuliko hata vyombo vya habari. Watu wengi waliweza kufuatilia na kuelewa mambo mengi kuhusu ajali hii kwa urahisi kuliko kusubiri vyombo vya habari kutangaza au kuchapisha katika magazeti. Mchango wa bloggers ni mkubwa sana katika jamii zetu hasa kama nchi yetu ambazo hazina centralized alert system. Tunawashukuru sana wale wote waliojitahidi kutupatia updates za habari hii kila mara..


Campaign Ya Kupunguza Ajali Nchini
Kuna watu wameniandikia na kuniuliza ni nini kinaweza kufanyika ili tuanzishe campaign ya kuwapa watu awareness ya kusaidia kupunguza ajali Tanzania? NImefurahishwa na moyo wa watu hawa kwa vile baadhi yao sio watanzania lakini wameweza kufuatilia habari za ajalii hii na kugundua kuwa ajali ni tatizo sugu nchini Tanzania. Bado nina brainstorming vitu ambavyo vinaweza kuanzishwa katika campain hii lakini kama kuna watu wana ideas please naomba mzitume ili tuangalie ni zipi zitaweza kufanyika na kuwafikia watu wengi na kwa budget gani. Ili tuangalie jinsi tutakavyoanza kufanya fundraising ya kusupport campain hiyo. Tukumbuke leo kwa mwenzio kesho kwako. Hizi ajali hazichagui jinsia, umri, kisomo wala kipato. Zinakuja kutoka kila pande. Tusipojisaidia wenyewe nani atakuja kutusaidia?

Campain itahusika na:-
1. Kuhamasisha madereva kujifunza sheria za barabarani
2. Kuhamasisha madereva kupima macho mara kwa mara.
3. Kuhamasisha watu wawe responsible kwa maisha yako eg don't drink and drive, follow the speed limit, wear seat belt, wear a helmet etc.
4. Kuhamasisha watu kwa wale wanaotumia public transportation kufuata sheria za usalama.

Kama mtu ana idea yeyote basi msisiste kututumia.



follow on Twitter | friend on Facebook | forward to a friend
Copyright © 2011 Tanzanian Blog Awards, All rights reserved.
You are receiving this email because you are in our Tanzanian bloggers' list ...If you wish to be removed from our list please email us...
Our mailing address is:

Tanzanian Blog Awards
122 Laurel Ave Suite 3
Maplewood, NJ 07040

15 Sept 2011

EMPOWER | EDUCATE | ENTERPRISE women in TANZANIA 
 

TWENDE

Copyright © 2011 Tanzania Women Entreprenuers Network & Development Exposition, All rights reserved.
You are receiving this email because we Believe in Empowering, Educating and Enterprising Women. Together We Can.
Our mailing address is:
Tanzania Women Entreprenuers Network & Development Exposition
105 Kilimani road
Dar Es Salaam 10684

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.