24 Aug 2011



PICHA ZOTE HIZI ZIMEPIGWA KATIKA KIKAO CHA BUNGE KINACHOENDELEA HUKO DODOMA.HIVI WAZIRI MZEMBE KAMA HUYU ANAYEDIRIKI KULALA OVYO OVYO HADHARANI  (BUNGENI) AKIWA OFISINI KWAKE SI NDIO ANAJIFUNIKA NA SHUKA KABISA.JE CHANZO CHA KULALA LALA OVYO KAMA TEJA NI UCHOVU NYAKATI ZA USIKU (ATUELEZE ANAKESHA AKIFANYA NINI),MARADHI KAMA SLEEPING SICKNESS AU "TEJA"?

JE INAWEZEKANA WASSIRA ALIKWENDA KWA BABU WA LOLIONDO KUSAKA TIBA YA SLEEPING SICKNESS?


KIONGOZI MCHOVU KAMA HUYU ANAPASWA KUSTAAFISHWA KWA MANUFAA YA UMMA.LAKINI INAELEKE KULALA HADHARANI NI TATIZO LINALOANZIA NGAZI ZA JUU KABISA

 NA LIMESAMBAA MIONGONI MWA VIGOGO,KAMA PICHA ZIFUATAZO ZINAVYOONYESHA (MAJI HUFUATA MKONDO)








ENEWEI,HEBU PATA UHONDOMWINGINE WA WACHAPA USINGIZI HAWA.WANASEMA RAHA YA USINGIZI IPATE MLALAJI









22 Aug 2011


Imetumwa na mdau Kato Lukaija

Wapo watu wanoamini kwamba pakipatikana suluhisho la matatizo ya biashara na uchumi kati ya bara na Zanzibar, basi kero za muungano zitakua zimekwisha. Hawa wanafanana na viongozi wetu wanaoamini kwamba muungano wa kiuchumi wa Afrika mashariki ni atua itakayotosheleza kuleta muungano wa kisiasa na kiutamaduni .Kwa mtazamo huu, uchumi ndio msingi wa kila jambo, liwe la kitamaduni,kisiasa au kitaifa. Na ndio maana nguvu zinaelekezwa zaidi kwenye diplomasia ya uchumi.

Lakini Muungano wetu,pamoja na kuunganisha uchumi wetu kwa matumizi ya sarafu moja,bado umegubikwa na hali ya kutosikilizana.Hali imekua hivyo kwa muda mrefu. Kwa hiyo kero zake,kama mijadala mingi inavyoonesha,haisababishwi na matatizo ya uchumi peke yake. Kuna tatizo la utata wa historia yenyewe ya muungano.

Kuna historia mbili za Muungano. Watu wa bara wanaona Muungano ni matokeo ya Mapinduzi ya Zanzibar yalioundoa utawala wa kitumwa wa Waarabu. Lakini nje ya madarasa rasmi ya historia hiyo,wapo vijana wanaharakati wa Zanzibar, kama Harith Ghasany,mwandishi wa KWAHERI UKOLONI,KWA HERI UHURU. Wanaharakati hawa wanadai kwamba Mapinduzi ya Zanzibar ni tunda la usuda ya Nyerere na kanisa dhidi ya waislamu na waarabu wa Zanzibar.Hivyo Muungano unaonekana kama ukoloni.

Hali hii inahitaji Wazee wakae na kukubaliana kuandika historia moja.  Wafanye kama Rais Kagame. Pamoja na kuangaikia uchumi,Kagame amehakikisha kwamba historia ya kweli ya mauaji ya 1994 ndio inayofundishwa na watu wote.Kagame anajua kwamba mtu haishi kwa mkate tu,ila kwa kila neno litokalo kwa bwana. Kwa hiyo vijana tunaomba wazee waandike historia moja tu. Wazee  wakisimamia historia moja tu, Muungano wetu utapona.

                             ------Kato Lukaija,  P.O.BOX 10351, DAR ES SALAAM.
                                         



Taarifa ifuatayo imetumwa na mwananchi aliyejitambulisha kama Msemakweli.Naiwasilisha kama ilivyo:
 Uvamizi wa wanajeshi dhidi ya wanakijiji Kimbiji ! Polisi kigamboni wamekua BUBU!hawajakubali kupokea malalamiko ya wanakijiji ! nani ? wa  kumfunga simba kengele? 
MALI NA MAKAZI YA WANAKIJIJI WAPATAO 200 Kimbiji zimeharibiwa.
 Uvamizi uliofanyika 16.08.2011 jumatano saa 4.00 hasubui wakazi kijiji cha Kimbiji,nje kidogo ya jiji la Dar,wamekuwa na mashaka ya maisha baada ya makazi na mazao yao kuharibiwavibaya na wanajeshi (JWTZ) ambao walivamia kijiji hiko na kuvunja vunja makazi ya raia..kinyume cha sheria. 
Hata hivyo baadhi ya wanakijiji walipereka taarifa katika vya  vituo vya polisi vya Kigamboni na mji mwema,havijakubali kupokea malalamiko ya wanachi walioharibiwa mali zao na kutishiwa usalama wao,hadi sasa inaonekana kuwa wanachi wa Kimbiji hawana wa kuwalinda wao na mali zao,kama inavyoeleza katiba ya nchi kuwa kila raia ana haki ya kupewa ulinzi wa maisha yake na mali zake! 
Katika Sakata hili la wanajeshi (JWTZ) kuvamia makazi ya raia na kuharibu mali za raiabado lina utata  wa nani ? kumfunga kengengele simba?


AFISA UBALOZI "USTAADH" IDRISA ZAHARANI AKIKARIBISHA WAGENI


Add caption






Salam,

Ubalozi wa Tanzania Hapa London Leo uliwaalika watanzania wote kutoka madhehebu na dini mbalimbali kuja kupata futari ya pamoja walioandaa ikiwa ni ishara njema ya kuonyesha amani,upendo, ukarimu kwa watanzania wote. Vyakula vya aina mbalimbali viliandaliwa  na vilipikwa katika hadhi ya kitanzania. Naibu Balozi Mh Chabaka aliwashuru wadau wote ambao waliweza kuja na kujumuika na kufuturu kwa pamoja. Aidha Mh Balozi aliahidi kushirikiana na watanzania kwa ukaribu zaidi katika hali na mali pia kuwaomba kutoa ushirikiano wao na ubalozi katika kuboresha mawasiliano na utendaji wa kazi ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo. Aliendelea kwa kusema Ubalozi upo kwa ajili yetu hivyo tuutumie ipasavyo.

Kwa niaba ya URBAN PULSE CREATIVE Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa ubalozi wetu kwa namna walivyojitolea kutengeneza futari na kuwakaribisha wadau kuja kufuturu.

Asanteni Sana,

MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU IBARIKI TANZANIA

URBAN PULSE CREATIVE



BENDI ya mziki ya msondo ngoma imepata TUZO ya the Best Rhumba Group katika East Africa Music Awards mashindano yariyofanyika Nairobi Kenya na kukusanyika kwa bendi za Afrika Mashariki na bendi ya msondo kuibuka Kidedea katika mashindano hayo akisibitisha ushindi uho meneja wa bendi Saidi KIbiriti alipokuwa akiongea na Msemaji wa Bendi hiyo, Rajabu Mhamila , Super D (pichani)

Alisema wameshinda tuzo hiyo na watahakikisha wanaionesha kwa mashabiki wa bendi hiyo ili kudhirisha kuwa bendi ipo ng'ang'ari popote duniani mana bendi imekamilika kila idara alisema Super D
(pichani)

Bendi hiyo itanza mazoezi siku ya jumatatu kwa ajili ya kujiandaa na sikukuu ya Iddi inayotarajia kufanyika wiki ijayo ambapo wanaingia kambini kusuka vibao vipya ikiwemo na kuvifanyia kazi vile vya Zamani

Super D alisema bendi hiyo siku ya Iddi Mosi itapiga katika viwanja vya TTC Chang'ombe ambapo mashabiki watapata kuona tuzo hiyo ya Afrika Mashariki walioitwaa hivi karibuni na kupata fursa ya kupiga nayo picha katika viwanja hivyo

Bendi hiyo inayotamba na vibao vyake vipya vya Suluu uliotungwa na Shabani Dede na Nadhili ya Mapenzi uliotungwa na Juma Katundu

Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times [email protected] www.burudan.blogspot.com
 Mob;+255787 406930
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania




Bondia YOhana Robart wa kambi ya Ilala akioneshana ufundi wa kutupa masumbwi na mtoto, Zainabu MHamila 'IKOTA' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi hiyo juzi.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com )

kondo

Kocha wa mchezo wa ngumi kondo Nassoro (kulia) akimwelekeza mtoto Zainabu Mhamila 'IKOTA' jinsi ya kutupa masumbwi wakati wa mazoezi ya kambi ya Ilala yanayoendelea katika ukumbi wa Amana CCM Dar es salaam.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com )
--
Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times [email protected] www.burudan.blogspot.com
 Mob;+255787 406930
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

20 Aug 2011




Thank you so much from the bottom of my heart to all my fans.

LAST NIGHT THE SPORAH SHOW WON AN AWARDS FOR THE FACE OF 2012  SPECIAL RECOGNITION AWARDS ON WORLD HUMANITARIAN DAY 19TH AUGUST 2011 AT  THE ROYAL BOROUGH OF KENSINGTON & CHELSEA.

Sporah Sporah in the building.


The World Humanitarian Day is a celebration of people helping people. Every day humanitarian aid workers help millions of people around the world no matter who they are or where they are. The day recognizes the sacrifices and contributions of those who risk their lives to give others help and hope.


 WALKING THE ROOM..!


YES! WE WON IT..!

Sporah Accepting The Award from Dorothy.!

 All thanks goes to our adoring fans who watch The Sporah Show on TV, follow us on Twitter, Facebook, Blog etc day in and day out.

Special thanks goes to all my entire team who work tirelessly on this production.


RECOGNITION IS GREAT WHEN IT COMES FROM ANYONE.!



 SPORAH ON INTERVIEW WITH OTHER PRESS AFTER RECEIVING THE AWARD.!

 The Sporah show would like to thank Dorothy and the Team for Organising the Awards, and of course to YOU, You Guys make The Sporah Show What It Is..! Thanks for your continuing support, we could't have done this without you..!  

I LOVE YOU, I LOVE YOU, I LOVE YOU ALL XOXO



19 Aug 2011




Raia Mwema Ughaibuni
Walalahoi Uingereza, sawa na wa Tanzania, ni ‘bomu’
Evarist Chahali
Uskochi
17 Aug 2011
Toleo na 199
  • Lisipoteguliwa na watawala hulipuka
  • Ghasia za Tottenham ni kengele ya uamsho
KATIKA makala ya wiki iliyopita, nilizungumzia vurugu zilizotokea katika kitongoji cha Tottenham, jijini London, hapa Uingereza. Kadhalika nilijaribu kuzihusisha vurugu hizo na mazingira yalivyo sasa huko nyumbani na kutoa wito kwa watawala wetu kufanya kila wawezalo kutatua matatizo yanayowakabili Watanzania ambayo yanaweza kusababisha vurugu kama hizo.
Hata hivyo, wakati naandaa makala hiyo vurugu hizo zilikuwa zimetawala Tottenham pekee. Lakini kwa takriban siku tano tangu zianze, ziliweza kusambaa maeneo mbalimbali ya London na hatimaye kuvuka mipaka hadi miji ya Liverpool, Birmingham, Manchester na mingineyo.
Kwa bahati nzuri sie huku Scotland tumenusurika. Na katika kile kinachoweza kutafsiriwa kama uhusiano wa ‘paka na panya’ kati ya Scotland na England, Waziri Mkuu (First Minister) Alex Salmond, alitahadharisha watu walioziita vurugu hizo ‘za Uingereza’ (UK riots) na kuwakumbusha kuwa hazijaigusa Scotland, Wales au Ireland ya Kaskazini; bali England pekee. Kwa hiyo, Salmond alitaka vurugu hizo ziitwe ‘za England’ (English riots).
Baada ya takriban siku tano zilizoshuhudia uharibifu mkubwa na vifo vya angalau watu watano, hatimaye polisi walifanikiwa kuzizima japokuwa hadi sasa bado hali haijarejea kuwa shwari kabisa.
Zaidi ya watu 1,000 wameshafikishwa mahakamani na wengine kuhukumiwa. Mahakama zinazoendesha kesi dhidi ya washiriki wa vurugu hizo zimelazimika kufanya kazi hadi usiku kukabiliana na msongamano wa watuhumiwa.
Waziri Mkuu wa Uingereza (nzima), David Cameron, alilazimika kukatisha likizo yake ili kutoa tamko na kuendesha mjadala Bungeni kuhusu vurugu hizo. Takriban kila mwanasiasa aliyezungumzia vurugu hizo aliwalaani wahusika na kuhitimisha kuwa hakuna maelezo mengine zaidi ya uhalifu mtupu (sheer criminality).
Licha ya Kamisheni Huru ya Malalamiko dhidi ya Polisi (Independent Police Complaint Commission) kukiri bayana kuwa taarifa za awali kwamba kulikuwa na kurushiana risasi kati ya Mark Duggan (Mwingereza Mweusi aliyeuawa na polisi kwa risasi na hatimaye kusababisha vurugu hizo) na polisi si sahihi (marehemu alikutwa na silaha lakini hakuwafyatulia risasi polisi), ‘makosa’ hayo ya polisi yalifunikwa na shutuma na laana zilizoelekezwa kwa waliohusika kwenye vurugu hizo.
Kimsingi, vurugu hizo zilipoanza katika kitongoji cha Tottenham zilihusisha zaidi Weusi. Na hata ziliposambaa kwenye maeneo mengine ya jiji hilo bado wahusika wengi walikuwa Weusi. Hata hivyo, kadri zilivyosambaa ndivyo tulivyozidi kushuhudia picha kwenye vyombo vya habari zikiwaonyesha Weupe kadhaa wakishiriki kwenye uporaji ulioambatana na vurugu hizo.
Kwa baadhi yetu, licha ya kutopendezwa na vurugu hizo, uwepo wa Weupe ulileta ahueni kidogo; kwani ni siri iliyo wazi kwamba kila baya linalofanywa na asiye Mweupe (Non-Whites) ‘linaongeza shehena ya silaha kwenye ghala la chuki dhidi ya kila asiye Mweupe.’ Mifano ni mingi lakini hapa nitaonyesha machache.
Kwa mfano, huko Marekani ambapo mtikisiko wa uchumi unaisumbua nchi hiyo vilivyo, kuna wanaoamini kuwa tatizo ni rais Mweusi, Barack Obama. Lakini ukweli ni kwamba matatizo ya kiuchumi ya nchi hiyo yalianza zama za mtangulizi wa Obama; yaani ‘Mweupe’ George W. Bush.
Na mfano unaoweza kutoa picha halisi ya double standards (viwango vinavyokinzana) ni tukio la kinyama kabisa la kigaidi lililotokea mwezi uliopita nchini Norway ambapo mhusika, ‘Mweupe’ Anders Behring Breivik, aliwaua kinyama zaidi ya watu 70. Mara baada ya kupatikana kwa habari za kusikitisha kuhusu tukio hilo, wachambuzi walikurupuka na kubashiri kuwa wahusika wangekuwa “Waislamu wenye msimamo mkali.”
Wachambuzi hao wakajitahidi kadri wawezavyo kubainisha sababu mbalimbali zinazowafanya kuamini kuwa kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwa wahusika ni “magaidi wa Kiislamu.”
Wakajaribu kuhusisha hasira za Waislamu dhidi ya mchora katuni wa Kidenishi aliyechora kikaragosi cha kumkashifu Mtume Muhammad S.W.A na kusababisha maandamano sehemu mbalimbali duniani. Kwa nini tukio lililotokea Udenishi lisababishe shambulizi ‘la kigaidi’ Norway? Jibu wanalo wachambuzi hao.
Wakajaribu pia kuhusisha uwepo wa majeshi ya nchi za Magharibi huko Afghanistan, na sababu nyingine kadha wa kadha; alimradi kuongeza nguvu kwenye ubashiri wao.
Bahati nzuri, kama wasemavyo Waswahili, Mungu hamfichi mnafiki. Baada ya muda si mrefu ikafahamika kuwa mhusika wa ugaidi huo alikuwa sio tu Mnorway; bali pia ni Mweupe, na tena ni muumini wa Ukristo wenye mrengo mkali (Christian Fundamentalism) na mfuasi wa siasa za mrengo mkali wa kulia (far-right politics).
Pamoja na majonzi yaliyowakumba wengi kutokana na mauaji hayo ya watu wasio na hatia, lakini taarifa kwamba mhusika hakuwa Muislamu zilileta ahueni kubwa.
Lakini kama ilivyo katika matukio mengine ya kigaidi yaliyofanywa na Weupe, ukajitokeza ‘utetezi’ kuwa Breivik (muuaji) “alikuwa ni chizi tu, na wala hakusukumwa na Ukristo wake wala itikadi yake ya siasa za chuki dhidi ya wageni na Waislamu.”
Licha ya gaidi huyo kuchapisha mtandaoni ‘ilani’ yake yenye kurasa 1,500 (siku chache kabla ya mashambulizi yake ya kigaidi) ambapo alibainisha chuki aliyonayo dhidi ya wageni na Waislamu na kuweka wazi kuwa ‘angefanya kitu fulani kikubwa kuleta ufumbuzi’, bado watetezi wake wameendelea kumtenganisha na siasa za mrengo mkali wa kulia na Ukristo wa msimamo mkali.
Tukirejea kwenye vurugu za Uingereza, tayari dalili zimeanza kujitokeza kuwa wa ubaguzi wa rangi watafanya kila wawezalo kumhusisha mtu Mweusi na vurugu hizo.
Ni kweli kuwa vurugu zilichipuka kutoka katika maandamano ya amani ya baadhi ya watu kwenye Jumuiya ya Weusi katika baadhi ya vitongoji vya London. Lakini kila aliyeshuhudia vurugu hizo zikipamba moto aliona wahusika wa rangi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Weupe.
Majuzi, mwanahistoria maarufu wa hapa, David Starkey, aliwachefua watu wengi alipodai kuwa vurugu hizo ni matokeo ya ‘Weupe kugeuka Weusi.’ Kimsingi, hoja yake ni kwamba vurugu ni kasumba ya mtu Mweusi, na Weupe wanaojihusisha na vurugu ni matokeo ya ‘maambukizo’ ya kasumba hiyo kutokana na mwingiliano wa kijamii kati ya Weusi na Weupe. Inachefua!
Kwa upande mwingine, ‘majibu’ ya watawala wa hapa wakiongozwa na Waziri Mkuu Cameron yanaonekana kuelemea zaidi kwenye kukabiliana na matokeo badala ya chanzo. Cameron amekuwa akizungumza kwa ukali dhidi ya ‘wahalifu’ waliosababisha vurugu hizo; huku akinuia kupambana nao kwa nguvu zote.
Lakini Profesa wa Historia ya Wakati Huu (Modern History), Robert Gildea wa Chuo Kikuu cha Oxford anabainisha kuwa “wanasiasa na vyombo vya habari wameongoza msafara wa kulaani walioshiriki vurugu kama wahalifu, wendawazimu na wasio na maadili. Hii ni lugha ya matabaka tawala yanapokabiliwa na vurugu za kijamii, kuwaharamisha wanaonyanyaswa kama wahalifu wa anasa dhidi ya jamii yenye amani, lengo likiwa kuwaadhibu wanyanyaswa hao na kuwatenga zaidi.
Cameron na Wahafidhina wenzake wana kila sababu ya kuwabebesha lawama ‘wahalifu’ hao; kwani baadhi ya wachambuzi wanazihusisha vurugu hizo na hatua ya serikali kubana matumizi kutokana na mtikisiko wa uchumi wa dunia, ambapo wahanga wakubwa wameendelea kuwa tabaka la walalahoi.
Kwa kuaminisha umma kuwa vurugu hizo ni uhalifu tu, Cameron na serikali yake atakuwa amefanikiwa kuepusha lawama dhidi ya hatua zinazochukuliwa na serikali yake kubana matumizi na madhara yake kwa jamii.
Kadhalika, kwa bahati mbaya au makusudi watawala wameamua kufumbia macho tatizo la ubaguzi wa rangi ambalo ndio kilio kikubwa cha jamii za Wasio Weupe, na kwa wengi ni sababu kuu ya kuibuka kwa vurugu hizo.
Vilevile, uwezekano kwamba baadhi ya walalahoi wa Uingereza wanaona kama wamesahauliwa na tabaka tawala, na hivyo kusubiri kwa hamu fursa za kuonyesha hasira zao, pia unaelekea kupuuzwa.
Kama nilivyoeleza wiki iliyopita, kuna mengi ambayo watawala wetu huko nyumbani wanaweza kujifunza kutoka kwenye vurugu hizi na jinsi watawala walivyozishughulikia.
Historia inatufundisha kuwa amani inayotawala licha ya uwepo wa lindi la ubaguzi, ukandamizwaji na umasikini, ni sawa na bomu la muda linalosubiri tu wakati lilipuke. Kama tabaka tawala Uingereza litapuuzia vyanzo halisi vya vurugu hizo (ubaguzi, umasikini, nk), basi, ni suala la muda tu kabla hatujashuhudia vurugu nyingine.
Katika mtizamo huo huo, iwapo watawala wetu huko nyumbani wataendelea kuamini katika amani ya kukosekana vurugu; ilhali kuna mamilioni ya Watanzania wasio na amani matumboni na mifukoni mwao (kutokana na umasikini), basi, nasi tunaweza kujikuta katika hali mbaya kama hii iliyojiri hapa.
Tunaweza kusema ‘Mungu aepushie mbali’, lakini tukumbuke kuwa mara nyingi Mungu huwasaidia wale wanaojisaidia wenyewe kwanza.

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.