1 Dec 2008


Over 300 people have died in Muslim-Christian clashes in the worst sectarian violence in Nigeria since 2004.
Angry mobs burned homes, churches and mosques on Saturday in the central state of Plateau, according to The Associated Press.

Initially a clash between supporters of the region’s two main political parties, the violence was soon divided along ethnic and religious lines.

Tension began when electoral workers did not post the results in ballot centers, causing many locals to assume the election was going to be another fraudulent political event. After riots broke out, a curfew was declared and the governor of Plateau state ordered troops to shoot on sight to enforce the curfew in neighborhoods affected by the violence.

About 7,000 people in conflict areas have left their homes and are seeking refuge in government buildings and religious centers, the Red Cross reported.

Sectarian violence is not new in Plateau, with more than 1,000 people killed in Jos – the state’s capital – in September 2001 due to Christian-Muslim hostility.

This weekend’s sectarian violence was the worst clash in the West African nation since 2004, when as many as 700 died in Plateau and over 100 churches were destroyed. The 2004 violence was said to have been sparked by land disputes between members of the predominantly Christian Tarok tribe and Muslim Hausa-Fulani farmer.

Nigeria is split nearly evenly between a predominantly Muslim north and a Christian south. According to Compass Direct, religious conflicts between Muslims and Christians have claimed more than 10,000 lives since 1999.

SOURCE: EURWEB

WAKATI HAYO YAKIENDELEA HUKO NIGERIA,INAELEKEA BADO KUNA WENZETU HUKO NYUMBANI TANZANIA WANGEPENDA TUONJE HAYO YANAYOWAKUTA WENZETU WA NIGERIA.HEBU SOMA KWANZA STORI HII HAPA CHINI

Waislamu, Wakristo waishika pabaya CCM
NI KATIKA SUALA LA MAHAKAMA YA KADHI, OIC

Na Geofrey Nyang’oro

WAUMINI na dini mbili kuu nchini za Kiislamu na Kikristo wameiweka pabaya serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika kufanya maamuzi kutokana na mvutano mkali unaoendelea, huku pande hizo zikiwa zimeshikilia misimamo mikali kuhusu hoja ya Mahakama ya Kadhi na nchi kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC).

Mjadala kuhusu masuala hayo mawili ulikuwa umepoa, lakini uliibuka hivi karibuni baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk Bernard Membe, kuzungumzia suala la OIC wakati akizungumza na waandishi kuhusu ziara ya rais nje ya nchi.

Baada ya maaskofu kuitahadharisha serikali ya CCM kuwa hawatafanya nayo kazi iwapo itashikilia msimamo huo wa kujiunga na OIC, jana Waislamu nao waliipa serikali mwezi mmoja iwe imeshatoa tamko rasmi kuhusiana na hoja hizo, vinginevyo wataing'oa CCM madarakani kwa kuwa imeshindwa kutekeleza suala hilo, wakidai suala la Mahakama ya Kadhi limo kwenye ilani ya chama hicho tawala.

Kauli hiyo ilitolewa na Waislamu kwenye kongamano la "Hatima ya Elimu ya Uislamu na Urejeshwaji wa Mahakama ya Kadhi," lililofanyika kwenye Ukumbi wa PTA jana jijini Dar es Salaam jana.

Pia kwenye kongamano hilo, Waislamu walimtaka Waziri Membe kuomba radhi au kujiuzulu kutokana na kauli yake ambayo walidai kuwa, inakashifu fedha kutoka OIC kwa madai kuwa ni ya shetani.

Walitoa msimamo huo wakati waumini wa makanisa mbalimbali yaliyo chini ya CCT, KLPT wakiwa wameshatoa tamko lao la nguvu kupinga hatua ya serikali kudhamiria kujiunga na OIC, wakieleza athari ambazo serikali itapata iwapo haitakuwa makini.

"Tuna uhakika kuwa yaliyomo ndani ya OIC ni hatari kabisa, kwani endapo yakikubalika katiba, nchi itakuwa imevunjika na Watanzania watakuwa wameingia katika migogoro itakayoua maridhiano, mshikamano, utengemano na umoja wa kitaifa, " walisema maaskofu hao katika tamko lao.

Rais Jakaya Kikwete pia alitaka waumini wa Kiislamu kuwa na subira na kuiachia serikali itafakari kwa utulivu ili ifanye uamuzi ya hekima utakaojenga na kulihakikishia taifa umoja, amani, utulivu na upendo miongoni mwa raia.

"Tujiepushe na vitendo au kauli ambazo zitawatia watu hofu na kujenga chuki miongoni mwa raia wa nchi yetu wanaopendana na kujenga chuki na kutoaminiana baina ya raia na serikali yao inayowapenda na kuwathamini," alisema Rais Kikwete mwezi uliopita.

Lakini Waislamu jana wakawa na kauli kali wakati wakijadili masuala hayo kwenye kongamano hilo, ambalo pia lilihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Kikristo na kufikia hatua ya kutoa tamko hilo na wameazimia kufanya maandamano makubwa jijini Dar es Salaam ambayo yatakwenda sambamba na mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika kesho kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Akizungumza kwenye kongamano la jana, Katibu Mkuu wa Baraza la Habari la Kiislamu Tanzania (Bahakita), Sheikh Sadiki Godigodi alisema suluhisho la uwepo wa haki na usawa kwa wote hapa nchini ni urejeshwaji wa Mahakama ya Kadhi pamoja na upatikanaji wa haki ya kielimu kwa Waislamu.

Alisema ukimya wa serikali ya CCM kuhusu Mahakama ya Kadhi unaonyesha kuwa serikali hiyo, ambayo walidai inaongozwa na Jumuiya ya Kikristo (CCT), kutokana na kuonyesha kuipinga dhana hiyo, haina nia ya kutekeleza ilani yake licha ya kwamba suala hilo halina madhara kwa Watanzania wote na ni muhimu kwa dini ya Kiislamu na Uislamu kwa ujumla.

Godigodi alisema kwa sasa Uislamu hapa nchini hautakuwa tayari kudhulumiwa haki zake na hautakuwa tayari kuona mtu yeyote anajitokeza kukwamisha jitihada za kudai haki zao ambazo ni urejeshwaji wa Mahakama ya Kadhi na nchi kujiunga na OIC na kudai kuwa mtu yeyote atakayejitokeza kupinga jitahada hizo, atakuwa anatangaza uadui kati yake na Uislamu.

Sheikh Mustafa Lema kutoka Arusha alisema anashangazwa na serikali ya CCM licha ya kuliweka suala la Mahakama ya Kadhi kwenye ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005, imeamua kukaa kimya katika utekelezaji wake.

Alisema Mahakama ya Kadhi ni suala la kiimani katika dini ya Uislamu na wala si la dini ya Kikristo wala serikali, hivyo jambo la msingi linalotakiwa kufanywa na serikali ni kurudishwa kwa chombo hicho.

“Ukimuuliza Mkristo anajua nini kuhusu dini atakupa habari kuhusu maaskofu, mashemasi na wachungaji na mambo yote yanayofanyika ndani ya imani yao, ukimuuliza Mwuislamu yeye atakueleza habari za masheikh, OIC na Mahakama ya Kadhi, hiyo ndiyo imani yao iweje leo Wakristo waje kuipinga Mahakama ya Kadhi ambayo siyo suala la imani yao?” alihoji Godigodi.

“Sisi tunataka Mahakama ya Kadhi ili tuweze kutetea haki zetu, hatuwezi kushughulikia mambo yahusuyo Uislamu ikiwa ni pamoja na mirathi, talaka na mali za Uislamu kama kiwanja cha Chang’ombe,” aliongeza.

Walisema kutokana na serikali ya CCM kuendelea kudhulumu haki za Uislamu na kuwachezea mara kwa mara kwa kushindwa kushughulikia masuala hayo, hawatakuwa tayari kukichagua chama hicho na badala yake watafanya kila linalowezekana kuhakikisha Waislamu wanakitosa chama hicho kwenye chaguzi zijazo.

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema suala la Mahakama ya Kadhi linapaswa kuanzishwa, lakini akasisitiza uwepo wa elimu ya kutosha katika suala hilo.

Alisema tatizo lililopo ni watu kutojua nini maana ya Mahakama ya Kadhi na kazi zake na kwamba kama watapatiwa elimu ya kutosha na kueleweshwa vema, itaanzishwa kwa amani na utulivu.

Alisema elimu pekee ndiyo itakayokwenda sambamba na mijadala ya uso kwa uso kati ya makundi yote mawili na hivyo kuwezesha uanzishwaji wa mahakama hiyo kuwa wa amani.

“Tatizo linalosababisha watu kupinga ni kutoelewa Mahakama ya Kadhi nini na kazi zake. Hapa inatakiwa elimu kwa wananchi wote kuhusu mahakama hiyo ili kuwaondoa hofu," alisema.

Hata hivyo Mbatia aliwataka Waislamu kuiachia serikali ifanye kazi zake katika kushughulikia hilo kutokana na ukweli kuwa iliahidi kulishughulikia.

Katika kongamano hilo, Waislamu hao walianzisha mchango wa hiari ili kupata Sh2 milioni kwa kwa ajili ya kuendesha zoezi la kufanya kampeni ya kuzunguka nchi nzima kutangaza azma yao ya kukusanya kadi na kuzirudisha kwa CCM kama serikali haitatekeleza suala hilo.

CHANZO: Mwananchi

TATIZO LETU NI KUKURUPUKA KWA WANASIASA AMBAO WAKATI WA CHAGUZI HUTOA AHADI KAMA ZILE ZA KWENYE WIMBO NDIO MZEE WA PROF JAY ILHALI WANAJUA KABISA HAWANA UWEZO WA KUZITEKELEZA.KULIKUWA NA HAJA GANI KWA CCM KUINGIZA KWENYE MANIFESTO YAKE YA 2005 AHADI YA KUPATIA UFUMBUZI SUALA LA MAHAKAMA YA KADHI IWAPO HAIKUWA INAJUA NAMNA YA KUITEKELEZA?NA NANI ALIMTUMA MEMBE KUROPOKA HUKO DODOMA KUHUSU OIC WAKATI MAMBO BAADO KABISA?KAMA ILIVYO RAHISI KWA DEREVA ASIYE MAKINI KUSABABISHA AJALI NDIVYO WANASIASA WASIO MAKINI WANAVYOWEZA KUINGIZA NCHI KATIKA MATATIZO AMBAYO YANAWEZA KABISA KUEPUKIKA.NA KAMA ILIVYO KAWAIDA,WALIOWASHA MOTO HUO WAKO KIMYA KWA SASA KANA KWAMBA SIO WAO WALIOTUFIKISHA HAPA.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.