Showing posts with label NIGERIA. Show all posts
Showing posts with label NIGERIA. Show all posts

15 Oct 2014

Oktoba 20 mwaka huu itakuwa siku muhimu kwa Nigeria kwani siku hiyo taifa hilo litaadhimisha siku 42 tangu mtu wa mwisho kuthibitishwa kuwa na maambukizi ya Ebola. Idadi hiyo ya siku ni mara maradufu ya muda ambao Ebola yaweza kujitokeza hadharani (incubation period). Kwa maana hiyo, siku hiyo, Nigeria itakuwa na haki ya kujitangaza kuwa ipo huru dhidi ya ugonjwa huo hatari.

Hata hivyo, jana, Nigeria iliadhimisha tukio jingine ambalo pengine isingependa kulikumbuka: miezi sita kamili tangu kikundi cha kigaidi cha Kiislamu cha Boko kilipowateka wanafunzi wa kike 276 na kupelekea kelele takriban kila kona ya dunia kwa kampeni ya #BringBackOurGirls (Warejesheni Mabinti zetu).

Hata hivyo, licha ya kampeni hiyo, mabinti 219 bado wanaendelea kuwa mateka wa magaidi hao tangu walipotekwa katika eneo la Chibok. Licha ya tukio hilo la kinyama kuvuta hisia na sapoti ya watu wengi duniani, magaidi hao wanaendelea kufanya unyama wao uliopelekea maelfu ya mauaji, hususan katika majimbo ya kaskazini mwa nchi hiyo.

Maadhimisho hayo mawili yanazua swali linalokanganya: imewezekanaje kwa Nigeria kumudu kuidhibiti Ebola lakini imeshindwa kuidhibiti Boko Haram? Kwanini taifa hilo limeweza kulishughulikia tatizo moja kwa ufanisi mkubwa ilhali ikilishughulikia jingine kwa udhaifu mkubwa?

"Ebola inamgusa kila mtu."

Moja ya sababu ni jiographia ya kisiasa (political geography) ya Nigeria.ambayo tangu nchi hiyo kupata uhuru wake imekabiliwa na machafuko. Taifa hilo lenye watu milioni 170 ambao wamegawanyika katika makabila lukuki, limeshindwa kwa kiasi kikubwa kujenga umoja,mshikamano na maelewano kati ya wengi wa Wakristo wanaojiweza kwa upande wa kusini mwa nchi hiyo na wengi wa Waislamu wanaokabiliwa na ufukara upande wa kaskazini mwa nchi hiyo.

Boko Haram ambayo maana yake ni ni 'elimu ya kimagharibi ni dhambi,' inautumia mwanya huo.Kundi hilo linafanya zaidi shughuli zake katika majimbo matatu ya kaskazini mashariki, yote yakiwa chini ya uongozi wa chama cha upinzani cha All People's Party (APP), na ambako imani kwa Rais wa nchi hiyo, Goodluck Jonathan, ni haba.

"Watu wengi kaskazini mwa Nigeria wanaichukia Boko Haram," anaeleza Rudy Atallah wa taasisi ya The Atlantic Council na mtaalam wa masuala ya nchi hiyo. "Lakini kwa vile idadi kubwa ya watu wa kaskazini mwa nchi hiyo wanaona kama wametelekezwa na wenzao wa kusini kwa muda mrefu, wengi wanaiona Boko Haram kama chombo kinachoweza kuambana na serikali," anatanabaisha mtaalam huyo.

Katika hali tofauti, Patrick Swayer, Mwamerika mwenye asili ya Liberia alipogundulika kuwa na Ebola alipowasili Lagos, alijikuta katika jiji lililosheheni miundominu ya kisasa ya huduma za afya na makao makuu ya taasisi nyingi za kimataifa, Na tofauti na mapambano dhidi ya Boko Haram, mapambano dhidi ya Ebola yanavuka mipaka ya ukabila, siasa na dini.

"Ebola inamgusa kila mtu," anasema Atallah. "Haina madhehebu wala kundi maalum."

'Kasheshe' nyingine nchini humo yatarajiwa Februari mwakani wakati taifa hilo litakapofanya uchaguzi wa Rais. Baada ya mhula mmoja madarakani, Rais Jonathan anaruhusiwa kugombea tena. Ushindi kwa chama chake cha People's Democratic Party, ambacho kimeitawala Nigeria kwa miaka 14, na ambacho kina sapoti kubwa kusini mwa nchi hiyo, waweza kuchochea mgawanyiko zaidi nchini humo, sambamba na ugumu wa kuwaokoa mateka waliosalia mikononi mwa Boko Haram.

CHANZO: Makala hii imetafsiriwa kutoka hifadhi yangu ya habari muhimu, ninazokutana nazo mtandaoni na kuzihifadhi katika app ya Instapaper. App nyingine ninayoitumia kwa hifadhi ya habari ninazozitumia kama reference ni Pocket. Kadhalika, app nyingine muhimu ninayoitumia kuhifadhi vitu mbalimbali ninavyokutana navyo mtandaoni au hata mtaani ni Evernote

26 Feb 2012


Kwa Waafrika wengi,na pengine kwingineko ulimwenguni,Wanigeria wanatamba kwa sifa kuu mbili;moja mbaya  na nyingine nzuri.Mbaya ni tabia yao ya utapeli ambapo ni bora kulala na chatu mwinye njaa kuliko kumwamini Mpopo.Wenye uzoefu nao wanajua ninamaanisha nini.Sifa yao nzuri-hasa kwa wanaume ni kutamba katika soka takriban kila kona ya dunia.Inayoambatana na hiyo ni mfaniko makubwa waliyonayo wengi wao-hasa nje ya nchi (usiulize wameyapataje).

Katika hili la mafanikio,juzi juzi tu tumesikia wanamuziki kadhaa wa Kipopo wakivamia anga za muziki nchini Marekani ambapo tayari majina makubwa kama Snoop Dogg na Akon wameshafanya kazi nao.D'Banj kwa sasa anafanya kazi kwenye lebo ya G.O.O.D Music ya Kanye WestKwa upande mwingine,wanamuziki maarufu wa Kinigeria P.Square, 2Face Idibia na Whizkid wamesaini kwenye lebo ya Konvict ya Akon.Na wiki hii,gazeti maarufu la nchini Marekani la New York Times lina makala ndefu kuhusu kiwanda cha filamu za Nigeria kinachojulikana kama Nollywood.Unaweza kusoma makala hiyo ndefu HAPA.

Maendeleo haya ya wasanii wa kipopo yanaweza kuwa changamoto kubwa kwa wasanii wetu huko nyumbani.Japo kuna dalili kidogo za kutia matumaini baada ya wasanii AY na Jay Mo kushirikiana na wasanii wa kimataifa,kimsingi wengi wa wasanii wetu wanaendelea kutafsiri mafanikio kwa kigezo cha umaarufu ndani ya Tanzania (na kidogo kwa Afika Mashariki) na kuendekeza zaidi shoo za hapa na pale.
1 Dec 2008


Over 300 people have died in Muslim-Christian clashes in the worst sectarian violence in Nigeria since 2004.
Angry mobs burned homes, churches and mosques on Saturday in the central state of Plateau, according to The Associated Press.

Initially a clash between supporters of the region’s two main political parties, the violence was soon divided along ethnic and religious lines.

Tension began when electoral workers did not post the results in ballot centers, causing many locals to assume the election was going to be another fraudulent political event. After riots broke out, a curfew was declared and the governor of Plateau state ordered troops to shoot on sight to enforce the curfew in neighborhoods affected by the violence.

About 7,000 people in conflict areas have left their homes and are seeking refuge in government buildings and religious centers, the Red Cross reported.

Sectarian violence is not new in Plateau, with more than 1,000 people killed in Jos – the state’s capital – in September 2001 due to Christian-Muslim hostility.

This weekend’s sectarian violence was the worst clash in the West African nation since 2004, when as many as 700 died in Plateau and over 100 churches were destroyed. The 2004 violence was said to have been sparked by land disputes between members of the predominantly Christian Tarok tribe and Muslim Hausa-Fulani farmer.

Nigeria is split nearly evenly between a predominantly Muslim north and a Christian south. According to Compass Direct, religious conflicts between Muslims and Christians have claimed more than 10,000 lives since 1999.

SOURCE: EURWEB

WAKATI HAYO YAKIENDELEA HUKO NIGERIA,INAELEKEA BADO KUNA WENZETU HUKO NYUMBANI TANZANIA WANGEPENDA TUONJE HAYO YANAYOWAKUTA WENZETU WA NIGERIA.HEBU SOMA KWANZA STORI HII HAPA CHINI

Waislamu, Wakristo waishika pabaya CCM
NI KATIKA SUALA LA MAHAKAMA YA KADHI, OIC

Na Geofrey Nyang’oro

WAUMINI na dini mbili kuu nchini za Kiislamu na Kikristo wameiweka pabaya serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika kufanya maamuzi kutokana na mvutano mkali unaoendelea, huku pande hizo zikiwa zimeshikilia misimamo mikali kuhusu hoja ya Mahakama ya Kadhi na nchi kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC).

Mjadala kuhusu masuala hayo mawili ulikuwa umepoa, lakini uliibuka hivi karibuni baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk Bernard Membe, kuzungumzia suala la OIC wakati akizungumza na waandishi kuhusu ziara ya rais nje ya nchi.

Baada ya maaskofu kuitahadharisha serikali ya CCM kuwa hawatafanya nayo kazi iwapo itashikilia msimamo huo wa kujiunga na OIC, jana Waislamu nao waliipa serikali mwezi mmoja iwe imeshatoa tamko rasmi kuhusiana na hoja hizo, vinginevyo wataing'oa CCM madarakani kwa kuwa imeshindwa kutekeleza suala hilo, wakidai suala la Mahakama ya Kadhi limo kwenye ilani ya chama hicho tawala.

Kauli hiyo ilitolewa na Waislamu kwenye kongamano la "Hatima ya Elimu ya Uislamu na Urejeshwaji wa Mahakama ya Kadhi," lililofanyika kwenye Ukumbi wa PTA jana jijini Dar es Salaam jana.

Pia kwenye kongamano hilo, Waislamu walimtaka Waziri Membe kuomba radhi au kujiuzulu kutokana na kauli yake ambayo walidai kuwa, inakashifu fedha kutoka OIC kwa madai kuwa ni ya shetani.

Walitoa msimamo huo wakati waumini wa makanisa mbalimbali yaliyo chini ya CCT, KLPT wakiwa wameshatoa tamko lao la nguvu kupinga hatua ya serikali kudhamiria kujiunga na OIC, wakieleza athari ambazo serikali itapata iwapo haitakuwa makini.

"Tuna uhakika kuwa yaliyomo ndani ya OIC ni hatari kabisa, kwani endapo yakikubalika katiba, nchi itakuwa imevunjika na Watanzania watakuwa wameingia katika migogoro itakayoua maridhiano, mshikamano, utengemano na umoja wa kitaifa, " walisema maaskofu hao katika tamko lao.

Rais Jakaya Kikwete pia alitaka waumini wa Kiislamu kuwa na subira na kuiachia serikali itafakari kwa utulivu ili ifanye uamuzi ya hekima utakaojenga na kulihakikishia taifa umoja, amani, utulivu na upendo miongoni mwa raia.

"Tujiepushe na vitendo au kauli ambazo zitawatia watu hofu na kujenga chuki miongoni mwa raia wa nchi yetu wanaopendana na kujenga chuki na kutoaminiana baina ya raia na serikali yao inayowapenda na kuwathamini," alisema Rais Kikwete mwezi uliopita.

Lakini Waislamu jana wakawa na kauli kali wakati wakijadili masuala hayo kwenye kongamano hilo, ambalo pia lilihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Kikristo na kufikia hatua ya kutoa tamko hilo na wameazimia kufanya maandamano makubwa jijini Dar es Salaam ambayo yatakwenda sambamba na mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika kesho kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Akizungumza kwenye kongamano la jana, Katibu Mkuu wa Baraza la Habari la Kiislamu Tanzania (Bahakita), Sheikh Sadiki Godigodi alisema suluhisho la uwepo wa haki na usawa kwa wote hapa nchini ni urejeshwaji wa Mahakama ya Kadhi pamoja na upatikanaji wa haki ya kielimu kwa Waislamu.

Alisema ukimya wa serikali ya CCM kuhusu Mahakama ya Kadhi unaonyesha kuwa serikali hiyo, ambayo walidai inaongozwa na Jumuiya ya Kikristo (CCT), kutokana na kuonyesha kuipinga dhana hiyo, haina nia ya kutekeleza ilani yake licha ya kwamba suala hilo halina madhara kwa Watanzania wote na ni muhimu kwa dini ya Kiislamu na Uislamu kwa ujumla.

Godigodi alisema kwa sasa Uislamu hapa nchini hautakuwa tayari kudhulumiwa haki zake na hautakuwa tayari kuona mtu yeyote anajitokeza kukwamisha jitihada za kudai haki zao ambazo ni urejeshwaji wa Mahakama ya Kadhi na nchi kujiunga na OIC na kudai kuwa mtu yeyote atakayejitokeza kupinga jitahada hizo, atakuwa anatangaza uadui kati yake na Uislamu.

Sheikh Mustafa Lema kutoka Arusha alisema anashangazwa na serikali ya CCM licha ya kuliweka suala la Mahakama ya Kadhi kwenye ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005, imeamua kukaa kimya katika utekelezaji wake.

Alisema Mahakama ya Kadhi ni suala la kiimani katika dini ya Uislamu na wala si la dini ya Kikristo wala serikali, hivyo jambo la msingi linalotakiwa kufanywa na serikali ni kurudishwa kwa chombo hicho.

“Ukimuuliza Mkristo anajua nini kuhusu dini atakupa habari kuhusu maaskofu, mashemasi na wachungaji na mambo yote yanayofanyika ndani ya imani yao, ukimuuliza Mwuislamu yeye atakueleza habari za masheikh, OIC na Mahakama ya Kadhi, hiyo ndiyo imani yao iweje leo Wakristo waje kuipinga Mahakama ya Kadhi ambayo siyo suala la imani yao?” alihoji Godigodi.

“Sisi tunataka Mahakama ya Kadhi ili tuweze kutetea haki zetu, hatuwezi kushughulikia mambo yahusuyo Uislamu ikiwa ni pamoja na mirathi, talaka na mali za Uislamu kama kiwanja cha Chang’ombe,” aliongeza.

Walisema kutokana na serikali ya CCM kuendelea kudhulumu haki za Uislamu na kuwachezea mara kwa mara kwa kushindwa kushughulikia masuala hayo, hawatakuwa tayari kukichagua chama hicho na badala yake watafanya kila linalowezekana kuhakikisha Waislamu wanakitosa chama hicho kwenye chaguzi zijazo.

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema suala la Mahakama ya Kadhi linapaswa kuanzishwa, lakini akasisitiza uwepo wa elimu ya kutosha katika suala hilo.

Alisema tatizo lililopo ni watu kutojua nini maana ya Mahakama ya Kadhi na kazi zake na kwamba kama watapatiwa elimu ya kutosha na kueleweshwa vema, itaanzishwa kwa amani na utulivu.

Alisema elimu pekee ndiyo itakayokwenda sambamba na mijadala ya uso kwa uso kati ya makundi yote mawili na hivyo kuwezesha uanzishwaji wa mahakama hiyo kuwa wa amani.

“Tatizo linalosababisha watu kupinga ni kutoelewa Mahakama ya Kadhi nini na kazi zake. Hapa inatakiwa elimu kwa wananchi wote kuhusu mahakama hiyo ili kuwaondoa hofu," alisema.

Hata hivyo Mbatia aliwataka Waislamu kuiachia serikali ifanye kazi zake katika kushughulikia hilo kutokana na ukweli kuwa iliahidi kulishughulikia.

Katika kongamano hilo, Waislamu hao walianzisha mchango wa hiari ili kupata Sh2 milioni kwa kwa ajili ya kuendesha zoezi la kufanya kampeni ya kuzunguka nchi nzima kutangaza azma yao ya kukusanya kadi na kuzirudisha kwa CCM kama serikali haitatekeleza suala hilo.

CHANZO: Mwananchi

TATIZO LETU NI KUKURUPUKA KWA WANASIASA AMBAO WAKATI WA CHAGUZI HUTOA AHADI KAMA ZILE ZA KWENYE WIMBO NDIO MZEE WA PROF JAY ILHALI WANAJUA KABISA HAWANA UWEZO WA KUZITEKELEZA.KULIKUWA NA HAJA GANI KWA CCM KUINGIZA KWENYE MANIFESTO YAKE YA 2005 AHADI YA KUPATIA UFUMBUZI SUALA LA MAHAKAMA YA KADHI IWAPO HAIKUWA INAJUA NAMNA YA KUITEKELEZA?NA NANI ALIMTUMA MEMBE KUROPOKA HUKO DODOMA KUHUSU OIC WAKATI MAMBO BAADO KABISA?KAMA ILIVYO RAHISI KWA DEREVA ASIYE MAKINI KUSABABISHA AJALI NDIVYO WANASIASA WASIO MAKINI WANAVYOWEZA KUINGIZA NCHI KATIKA MATATIZO AMBAYO YANAWEZA KABISA KUEPUKIKA.NA KAMA ILIVYO KAWAIDA,WALIOWASHA MOTO HUO WAKO KIMYA KWA SASA KANA KWAMBA SIO WAO WALIOTUFIKISHA HAPA.

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.