29 Mar 2009

(Picha kwa hisani ya KENNEDY)

Gazeti la Majira limepotea mtandaoni kwa muda mrefu sasa,na kwa akina sie tunaotegemea habari za nyumbani kupitia nakala za kielektroniki za magazeti husika mkombozi wetu mkuu amebaki Mr Kennedy.Na ni kwa kupitia tovuti yake ndipo nilikutana na version isiyopendeza ya habari kuhusu ajali iliyomhusisha Mzee wa Vijisenti,Andrew Chenge,na kupelekea vifo vya akinadada wawili.

Gazeti la Majira lilidai kuwa marehemu hao ni "machangudoa waliokuwa wanatokea Maisha Club".Sijui vyanzo (sources) vyao vya habari husika ni vipi lakini mwandishi yeyote mwenye busara angepaswa kujiridhisha kuhusu identity halisi ya marehemu hasa kwa vile tunazungumzia watu waliopoteza maisha.Hivi mwandishi huyo atajisikiaje iwapo baada ya uchunguzi itagundulika kuwa marehemu hao hawakuwa machangudoa?In fact,magazeti kadhaa yameripoti maelezo ya ndugu za marehemu yanayoeleza kwamba mmoja wao alikuwa mfanyabishara na mwingine mfanyakazi wa hoteli jijini Mwanza.

Pengine haikuwa nia ya mwandishi kuwa-describe marehemu hao kama changudoa (labda kutokana na haraka ya kuwahisha habari kwa mhariri) lakini taswira ya haraka iliyopatikana kutoka katika habari hiyo ni ujenzi wa matabaka:kigogo (mzee wa vijisenti) kagonga fukara (changudoa).By the way,hata hata kama hao mabinti wangekuwa machangudoa as suggested by the Majira reporter bado haiondoi haki yao ya kuwa hai muda huu!

Kingine ambacho hakihusiani na uandishi japo kinahusu tukio hilo la kusikitisha ni namna Jeshi la Polisi linavyoonekana "kubabaika" katika kushughulikia ajali hiyo.Kwa mujibu wa vyombo vya habari,Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova,ameunda TUME MAALUM ya kuchunguza ajali hiyo eti kwa "kuzingatia uzito wa tukio hilo".Chenge ni Mtanzania kama mie na wewe,na kama amehusika na ajali basi sheria za uslama barabarani zifanye kazi yake.Sijui ni madereva wangapi walalahoi wanaopata "bahati" kama ya Chenge ya kuundiwa tume!

Kamanda Kova anadai kuwa tume hiyo imeundwa ili "kusiwepo mwanya wowote ,taratibu zote zitafuatwa bila kujali nani na wala nafasi aliyonayo....na kuleta uwazi na utawala bora" (kwa mujibu wa gazeti la Majira) na pia amenukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema kuwa "hapa bwana hakuna mchezo wala hakuna kuangalia vyeo wala nani ni nani...".Hivi matamshi kama hayo (iwapo kesi itapelekwa mahakamini) hayawezi kutumiwa na wakili wa Chenge kudai "ameonewa kwa vile Kamanda Kova alishadai hawataangalia vyeo-which directly points to Chenge ambaye licha ya kuwa ex-minister,pia ni munge na kigogo wa CCM?"

Kama nilivyoandika jana,tuendelee kuwapa polisi benefit of doubt kwa matarajio kwamba wanafahamu bayana kuwa tukio hilo linaangaliwa na Watanzania wengi kama kipimo cha haki sawa kwa wote (huku wakiwa na kumbukumbu ya kesi ya marehemu Ditto).

2 comments:

  1. ajali ngapi zilizowahi kutokea bila kuundiwa tume ya uchunguzi kwani hii ina nini? tena watu walikufa ni wawili tu! kule arusha,Tanga watu wangapi walikufa katika ajali na hatukusikia tume? kuna nini kinataka kufichwa hapa? kwanza kabisa inabidi chenge awe jela kwa kuendesha gari bila bima ya gari kwa miaka 2! ebu fikiria ungekuwa wewe unaedesha bila bima ya gari wacha kupata ajali? nahisi bado tanzania hatuna usawa!mbona yule kijana aliyemuua chacha wangwe hakupewa dhamana? au tuseme hao marehemu ndiyo walioua chenge katika ajili hiyo wangepewa dhamana? jamani lazima tutenda haki kwa kila mtanzania kwa vile ni haki ya mtanzania kuwa na haki katika nchi yake.kumwachia mzee chenge huru ni kuendeleza matabaka ya walionacho na wasio nacho.

    ReplyDelete
  2. Zipo dalili kwamba haki ya kweli kwenye vyombo vyetu vya sheria bado ni jambo lisilowezekana.

    Wapo wenzetu wanahesabiwa haki kwa gharama ya haki za wanyonge.

    Mfumo uliopo unaanza kujenga picha kuwa walio kwenye 'system' wanaweza kujiona juu ya sheria na wakatamba wapendavyo na asiwepo wa kuwagusa as long as wapo ndani ya mtandao. Wanapata haki isiyo yao kwa matumizi ya sheria hizi hizi zinazowakaanga walio 'nje' ya system.

    Mifano iko mingi katika hili. Na huu wa Chenge unaleta hofu hiyo hiyo.

    Kwa namna Polisi walivyoonekana kubehave katika tukio hili, mashaka yanakuwa mengi kuliko matumaini. Tunafika mahali pa kukosa imani nao. Tunakata tamaa kiwango cha ubeuzi. Na matokeo yake hayawezi kuwa mazuri.

    Huu uandishi wa siku hizi ni zao la haya yanayoendelea. Wapo waandishi wanaoamua kupiga teke maadili ili ama kuyakandamiza haya mapapa mpaka wanapitiliza, ama kuyasaidia mapapa kupora haki ya wananchi.

    Kwa hiyo tumefika mahali kwa jinsi kashfa zilivyo nyingi, serikali haiaminiki. Mahakama nayo inashakiwa kutumika kama mtaji wa kisiasa na Checheme. Bunge afadhali, nako huenda ni kwa sababu fulani fulani.


    Ndio maana nilipokuwa najaribu kuchangia maoni kwenye ile article ya Chadema na mtaji wa kashfa za ufisadi (nafikiri kuna tatizo lilizua kupublish siku ile), nilijaribu kuonyesha kwa vipi ni afadhali kupiga kelele nje ya mahakama, kuliko kwenda mahakamani hali wakijua ni kupoteza muda?
    Na kwa kufanya hivyo, hata kama hawataikomboa ile nyumba pale Magogoni, lakini kelele hizo zinaweza kabisa kupunguza usingizi wa pono kwa wananchi na kuwashawishi kujiunga nao na hatimaye kuongeza nguvu Bungeni.

    Kama nje ya mahakama kunalipa, bora!

    Ninachojaribu kusema ni kwamba waandishi ni sehemu ya jamii. Na kwa vile jamii inaumwa ubeuzi, na kujikuta ikifanya mambo yasiyotarajiwa, waandishi ni nani hata kikombe hicho kiwaepuke?

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.