Showing posts with label BBC. Show all posts
Showing posts with label BBC. Show all posts

24 Jan 2011

Makao Makuu ya MI6 jijini London
Makao Makuu ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) jijini London

Mashirika ya ushushushu ya Uingereza,MI5 na MI6,leo yalitarajiwa kuieleza Mahakama Kuu ya hapa kwamba siku zijazo  taarifa za kiusalama zitazokusanywa nje ya nchi hazitawekwa hadharani kortini hata kama zimepatikana kwa kuwatesa watuhumiwa (torture).

Mwaka jana,mahakama ya rufaa ilitupilia mbali kesi kwa kile ilichokiita jaribio la kudhoofisha kanuni ya msingi ya sheria: mshtakiwa lazima aone na kusikia ushahidi uliotumiwa kujenga kesi dhidi yake.

Sasa mashirika hayo ya usalama wa ndani (security) na ujasusi (intelligence) yanapambana na uamuzi huo.Baadhi ya vyombo vya habari vya hapa,magazeti ya The Guardian na The Times,na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC)-chombo cha umma hicho kama TBC1,Daily News na Habari Leo-pamoja na vikundi vya haki za binadamu vya Liberty na Justice,vilitarajiwa kutoa hoja mbele ya majaji waandamizi kabisa wa hapa kuwa kama hoja ya mashirika hayo ya kishushushu ikikubaliwa,itabomoa nafasi ya kesi kuwa ya haki na kumomonyoa  imani ya umma kwa maamuzi ya mahakama.Mawakili wa taasisi hizo za habari na haki za binadamu walitarajiwa kudai kuwa kanuni hizo ni muhimu hasa panapokuwa na madai ya maafisa wasiomudu majukumu yao ipasavyo (incompetent) au kutenda makosa.

Shauri hilo linatokana na madai ya raia (citizens) sita na mkazi (resident) mmoja wa Uingereza waliokuwa wakishikiliwa katika jela ya kuhifadhi watuhumiwa wa ugaidi ya Ghuba ya Guantanamo,kwa kile wanachodai ushirika wa siri kati ya MI5 na MI6 na mamlaka za Marekani.Watuhumiwa hao waliyataka mashirika hayo ya ushushushu kuonyesha ushahidi wa nyaraka kuhusu ufahamu wa  mashirika hayo katika uamuzi wa siri wa Marekani kuwapeleka jela hiyo,na ushiriki wa MI5 na MI6 katika suala hilo.

Japo watuhumiwa hao wameshafikia makubaliano ya fidia inayokisiwa kuwa mamilioni ya pauni za Kiingereza  (baada ya kuachiwa kutoka Guantanamo),mashirika hayo ya kishushushu yanataka kuanzisha kanuni mpya kwamba hakuna taarifa ya kiusalama itakayowekwa hadharani kwenye kesi yoyote ile ya madai au ya jinai.Tayari MI5 na MI6 wameshaonyesha wasiwasi wao katika mgogoro wa kitambo sasa kati yao na majaji wa mahakama kuu juu ya shinikizo kwa mashirika hayo kuonyesha ushahidi wa kuhusika kwao katika mateso aliyopewa (mmoja wa watuhumiwa hao) Binyam Mohamed,mkazi wa Uingereza aliyeshikiliwa kwa siri katika jela nchini Pakistan na Morocco kabla ya kupelekwa Guantanamo.Majaji waruka pingamizi la aliyekuwa 'Waziri wa Mambo ya Nje' (Foreign Secretary) wa hapa ,David Miliband,na kuweka hadharani muhtasari wa taarifa za (Shirika la Ujasusi la Marekani) CIA kwa MI5 na MI6.

Kama mashirika hayo ya usalama na ujasusi yakishinda madai yao,taarifa yoyote ya kiusalama na/au kijasusi inayohusu kesi ya madai au jinai itaonyeshwa kwa majaji na waendesha mashtaka pekee na sio washtakiwa au hata mawakili wao.Badala yake,taarifa hizo zitaonyeshwa kwa "mawakili maalumu" waliohakikiwa kiusalama (vetted).

Mwaka huu, Serikali ya Uingereza inatarajiwa kuchapisha muswada kupendekeza kipengele cha sheria kinacholitaka Bunge kuzuwia ushahidi wa uliopatikana kwa njia za ushushushu kuwekwa hadharani kortini,hatua ambayo inapingwa na majaji.  

Habari hii nimeitafsiri (kadri nilivyoweza) kutoka toleo la jana la gazeti la The Guardian la hapa Uingereza.Lengo la kutafsiri na kuiweka habari hiyo hapa bloguni ni kutoka changamoto kwa vyombo vyetu vya habari-hususan vya umma-kusimamia haki za jamii.Wengi wetu tumekuwa tukihudhunishwa na namna TBC,Daily News na Habari Leo,taasisi za habari zinazoendeshwa kwa fedha za walipakodi (pasipo kujali itikadi zao za kisiasa) wanavyoendesha shughuli zao kana kwamba ni vyombo vya habari vya CCM.Ikumbukwe kuwa vyombo vya habari ni mhimili  wa nne wa utawala wa nchi (pamoja na Bunge,Mahakama na Serikali),na hivyo kuwa na wajibu wa kutopendelea au kuegemea upande wowote dhidi ya maslahi ya umma.
    

13 Dec 2008

Watanzania wengi wanapenda habari.Na siku hizi vyombo vya habari viko vya kumwaga.Hata hivyo,upatikanaji wa habari za uhakika bado ni tatizo.Kwanza,wanahabari wengi wa huko nyumbani wanapendelea zaidi kuripoti habari badala ya kuleta habari iliyochunguzwa.Leo hii ukitoka ughaibuni na vizawadi viwili vitatu kisha ukaitisha press conference na kudai unataka kuanzisha mradi flani,kesho yake habari hizo zitaripotiwa kama ulivyotaka.Na kama hiyo press conference itaambatana na makulaji na vinywaji basi si ajabu habari hiyo ikawa ukurasa wa kwanza.Of course,kuna exceptions kwenye magazeti kama This Day,Kulikoni,Raia Mwema,Mwanahalisi na mengine machache.

Tatizo la pili katika upitakanaji wa habari liko katika mafungu mawili.Kwanza,japo magazeti ni mengi,wenye uwezo wa kununua bado si wengi sana.Bei ya wastani ya gazeti ni shilingi 400.Ukizingatia ugumu wa maisha,ni vigumu kutoa kiasi hicho kwa gazeti ambalo ukishasoma linakuwa halina matumizi mengine ya muhimu.Pili,upatikanaji wa habari kwa njia ya runinga na redio bado ni mgumu katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.Nilipokuwa Ifakara hivi karibuni,nilibaini kwamba ili uweze kukamata matangazo ya vituo vyote vya televisheni ni lazima uwe na "ungo".Sasa unaweza ku-imagine ni watu wangapi wenye uwezo wa kumudu gharama za kununua na ku-install satellite dish.

Pamoja na "chengachenga" za hapa na pale,redio imeendelea kuwa tegemeo la wengi hasa vijijini.Na ukipta hapa na pale utakuta wazee wetu nyakati za jioni wakisikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC au Deutsche Welle.Na kupitia matangazo hayo ndipo mzee wangu mmoja niliyeongea nae kwa simu jioni ya leo alipata habari kwamba kuna wawekezaji kadhaa "walioingizwa mkenge" na tapeli mmoja,Bernard Madoff,katika kile kinachofahamika kama Ponzi Scheme.Mzee huyo aliniuliza inakuwaje "wazungu" wenye uelewa mkubwa wa mambo waliweza kuhadaika na kushiriki "upatu" huo?Sikua na jibu kwa vile habari yenyewe ilikuwa bado ngeni kwangu.Kama mwenzangu nawe hujaipata,BONYEZA HAPA kuisoma kwa undani.

12 Nov 2008


A BBC Radio presenter has been sacked following a 'racist' call to a taxi firm, in which she requested a 'non-Asian' driver.

Sam Mason told the operator that 'a guy with a turban would freak her daughter out' insisting they send an English driver instead.

The ex-glamour girl, 40, called the firm to order a taxi for her 14-year-old daughter off-air, while presenting her BBC Bristol radio show.

After the operator branded her request 'racist', Mason insisted, claiming it wasn't the first time she had made the request.

She said: 'A guy with a turban is going to freak her out. She's not used to Asians.'
When the operator said it would not be possible to carry out her wishes, she said: 'You've managed it before.'

Mason, who has previously battled alcohol addiction, claimed she wasn't racist but insisted she was looking out for her daughter's interest.

Mason said: 'If it were me I wouldn't care if it had two heads, but it's my little girl we are talking about.'

After the operator refused to book a car, Mason complained before hanging up.

The operator said: 'We would class that as being racist. We can't just penalise the Asian drivers and just send an English one.'

She later called back before a manager accepted the booking.

Mason said: 'I work at the BBC. I'm far from racist and that uneducated woman has no right to call me one.'

The BBC were alerted to the conversation after it was recorded and sent to the Sun newspaper. 
The mother-of-one was subsequently suspended and fired 24 hours later.

A BBC spokesman said: 'Although Sam Mason's remarks were not made on-air, her comments were completely unacceptable and, for that reason, she has been informed that she will no longer be working for the BBC with immediate effect.'

SOURCE: Daily Mail

1 Feb 2008

Makala yangu hii ilitoka katika toleo la jana la gazeti la Mtanzania

Miongoni mwa adha za kumiliki runinga hapa Uingereza ni kuilipia ada ya leseni (TV Licence Fee).Ada hiyo kwa kiasi kikubwa hutumika kuendesha BBC ambalo ni shirika la utangazaji la nchi hii.Wananchi wengi wamekuwa wakilalamika kwamba baadhi ya vipindi vya BBC havina ladha inayoweza kuhalalisha shirika hilo kuendelea kupewa ruzuku inayotokana na ada ya leseni za runinga.Hata hivyo,BBC imeendelea kuwa shirika la habari maarufu na lenye mtandao mkubwa sio tu ndani ya Uingereza bali duniani kwa ujumla.Na miongoni mwa vipindi maarufu vya shirika hilo la habari ni Newsnight,kipindi kinachoonyeshwa siku za wiki kuanzia saa 4.30 usiku.

Kipindi hicho huchambua habari muhimu zilizojitokeza katika siku husika ndani na nje ya nchi hii.Hivi karibuni,Newsnight ilizungumzia machafuko yanayoendelea nchini Kenya.Kwa hakika ilikuwa inatia uchungu kuona namna watu wanavyotaabika nchini humo.Moja kati ya mambo yaliyolinisikitisha zaidi ni mahojiano mafupi kati ya mtangazaji wa BBC aliyeko nchini Kenya na mwanamama mmoja ambaye wakati wa mahojiano hayo alikuwa kamanda wa polisi wa eneo flani (jina la afande huyo na mahala alipokuwa anaongoza vimenitoka kidogo).

Kamanda huyo alianza mahojiano hayo kwa kukanusha madai kwamba jeshi la polisi la Kenya limekuwa likiuwa raia wasio na hatia katika kutekeleza sera ya “piga risasi kuua” (shoot-to-kill policy).Alidai kuwa wanachofanya wanausalama ni kudhibiti machafuko na uhalifu.Mwishoni mwa mahojiano,afande huyo alieleza uchungu alionao kuona nchi yake ikiteketea.Alisema kwamba ameshatembelea sehemu nyingi duniani na kuona watu wa nchi hizo wakiwa na fahari na nchi zao,jambo ambalo lilimwongezea mapenzi kwa nchi yake.Aliwalaumu wanasiasa wa Kenya kwa kuzorotesha jitihada za kuleta amani.

Cha kusikitisha ni kwamba kamanda huyo aliyeonekana kuguswa sana na madhila yanayowakumba Wakenya wenzie aliondolewa kwenye usimamizi wa operesheni za mitaani na kukabidhiwa majukumu ya kiofisi (desk job).Yaani aliadhibiwa kwa kusema ukweli wa moyoni mwake kuhusu namna wanasiasa wanavyoendekeza maslahi yao kuliko ya nchi na wananchi.Naamini mwanamama huyo ni mmoja tu kati ya askari wengi ambao wanalazimika kupiga na hata kuua Wakenya wenzao katika kutekeleza amri “halali” za serikali.

Ilielezwa katika kipindi hicho cha Newsnight kwamba licha ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge mwezi Desemba mwaka jana kuwa chanzo kikuu cha machafuko hayo yasiyoonyesha dalili ya kupungua,msingi wa matatizo ulijengwa miaka kadhaa iliyopita.Kwa mujibu wa uchambuzi wa wajuzi wa siasa za Kenya,kwa muda mrefu kumekuwa na manung’uniko miongoni mwa baadhi ya makabila kuhusu umiliki wa njia za uchumi ambapo inadaiwa Wakikuyu wamekuwa na upendeleo zaidi.

Tofauti za kikabila na kidini ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vya machafuko sehemu mbalimbali duniani hususan barani Afrika.Lakini tofauti hizo hustawi vizuri zaidi mahala ambapo kuna manung’uniko kuhusu haki na usawa hasa katika uchumi.Ni rahisi kumshauri fukara aingie mtaani “kujikomboa” kuliko kumshawishi mtu afunge biashara zake akashiriki maandamano.Pia ni vigumu kwa watu wa makabila au dini tofauti wanaoshirikiana katika ajira na utoaji au upokeaji huduma kuanzisha vurugu ambazo kwa vyovyote zitapelekea kuathiri mahusiano yao (kwa mfano, mahusiano kati ya mfanyabiashara na mteja au mwajiri na mwajiriwa).

Tofauti na nchi kama Uingereza ambapo mvuto wa kisiasa miongoni mwa wapiga kura uko chini hasa kwa vijana,wengi wetu tulishuhudia namna kampeni za uchaguzi nchini Kenya zilivyogusa karibu kila sehemu ya maisha ya Wakenya,kama ambavyo chaguzi zetu huko nyumbani zinavyokuwa na mvuto mkubwa.Ni dhahiri kwamba amani ingeshapatikana iwapo nguvu nyingi zilizotumiwa na wanasiasa wa Kenya na vyama vyao kushawishi wapiga kura zingeelekezwa pia kwenye kutafuta mwafaka katika vurugu zinazoendelea.

Ni vigumu kubashiri namna gani vurugu hizo zitadhibitiwa na kumalizwa kwa vile Kibaki na Raila wanaonekana kutokubaliana katika njia sahihi za kuleta amani.Yayumkinika kusema kwamba hakuna uwezekano wa Kibaki na serikali yake kukubali mapungufu yaliyojitokeza kwenye uchaguzi huo kwa vile kwa kufanya hivyo watakuwa wameongeza nguvu kwenye hoja za Raila na wafuasi wake kwamba matokeo ya uchaguzi huo ni feki.

Kwa upande mwingine,Raila anafahamu gharama kubwa ya maisha na mali wanayoipata wafuasi wake kwa kupinga matokeo ya uchaguzi huo,na kukubali kushirikiana na Kibaki pasipo makubaliano ya kutengua ushindi wa rais itakuwa ni sawa na usaliti wa daraja la kwanza.Historia nayo haitoi matumaini ya amani kwa jirani zetu wa Kenya kwani hakuna rais yeyote (hasa barani Afrika) anayeamini alishinda uchaguzi kwa njia halali aliye tayari kukubali uchaguzi urejewe kwa minajili tu ya kuridhisha wapinzani wake au kutuliza machafuko nchini mwake.

Madhara ya muda mrefu ya kinachoendelea nchini Kenya ni kuzaliwa kwa kizazi chenye kinyongo.Ni kipi kinachoweza kufuta kinyongo cha mtoto aliyepoteza wazazi wake katika machafuko hayo?Kibaya zaidi ni kwamba kadri machafuko yanavyoendelea ndivyo kizazi hicho cha kinyongo kinavyozidi kuongezeka.

Miezi michache iliyopita Watanzania walitoa maoni kuhusu wazo la kuunda muungano wa nchi za Afrika Mashariki,na wengi wao walipinga uharakishaji wa muungano huo.Ni kama walifahamu kwamba kelele za kuwa na muungano zilikuwa za kisiasa zaidi kuliko kuzingatia hali halisi ndani ya nchi husika. “Mikoa” ambayo ingeunda “nchi” hiyo (yaani sie na Uganda,na pengine Burundi na Rwanda) imeshindwa kuwa na mchango wa maana wakati “mkoa mwingine” (Kenya) unazidi kuteketea.Sijui ingekuwaje iwapo haya yangekuwa yanatokea ndani ya muungano huo!

Baadhi ya wapinzani wa muungano huo walieleza bayana kwamba japo wanafahamu umuhimu wa ushirikiano,au hata kuungana kisiasa,ukweli unabaki kwamba nchi husika zina matatizo yake lukuki ambayo yanapaswa kushughulikiwa kwanza kabla ya kuyakuza kwa kuunda “nchi” kubwa zaidi iliyojaa vipande vyenye matatizo binafsi.

Jeuri za wanasiasa wa Kenya kutosikiliza vilio vya wananchi wao na kupuuza jitihada mbalimbali zinazofanywa na wasio Wakenya ni onyo muhimu kwa wenye ndoto za ya muungano wa Afrika Mashariki kwamba kama wanashindwa kuweka mbele maslahi ya nchi yao na wananchi wao watajali vipi maslahi ya Watanzania au Waganda.

Kubwa la kujifunza katika sakata hili ni jinsi ilivyo amani iliyojengwa kwa miaka miongo kadhaa inavyoweza kuyeyuka ndani ya kipindi kifupi kabisa.Harakati za kumfukuza mkoloni nchini Kenya zilichukua miaka mingi na kugharimu maisha mengi.Wakenya walikuwa bado wako katika harakati za kupata uhuru wa kweli hadi wakati machafuko yanaanza nchini humo.Kinachoendelea sasa ni sawa na kusigina jitihada na damu za mashujaa waliopigania uhuru wa nchi hiyo.

Kwa Watanzania,wakati tunaendelea kuwaombea jirani zetu amani (yaelekea hakuna la ziada tunaloweza kufanya zaidi ya hilo) ni muhimu kutambua kwamba amani na utulivu tulionao unaweza kudumu milele iwapo tu jitihada za makusudi zitafanyika kuondoa umasikini,kuhakikisha pato la taifa linatumika kwa maslahi ya wote na “haki” kuwa haki ya kweli kwa kila Mtanzania bila kuangalia tabaka.Kelele dhidi ya ufisadi na mafisadi ni sehemu muhimu ya harakati za kuhakikisha amani na utulivu nchini inadumu milele.

13 Jan 2008Muda mfupi uliopita nilikuwa naangalia documentary moja ya Louis Theroux kuhusu maisha ndani ya San Quentin State Prison,one of the toughest and most dangerous in the U.S. of A.Katika documentary hiyo iliyoonyeshwa BBC2 Louis alipewa access ya wiki mbili ndani ya jela hiyo,na kwa hakika simulizi na mandhari ya humo ni ya kutisha na kuogopesha.It's such a moving documentary that I decided to share with you,msomaji mpendwa wa blogu hii,assuming that you have 60 minutes to spare.WATCH IT HERE

Locked Up ya Akon ft Styles P inaweza kuwa mwafaka kwa post hii fupi


17 Apr 2006

KULIKONI UGHAIBUNI


Asalam aleykum waungwana.

Nadhani kabla ya kubwabwaja mengi ingekuwa ni vema tukatambuana. Lakini kabla ya hapo, ngoja nikunong’oneze kitu kimoja kuhusu gazeti hili mwanana la KULIKONI.Hili sio gazeti la kawaida. Japokuwa hili ni toleo la pili tu, lakini nimeshuhudia kwa macho na masikio yangu maelfu kwa maelfu ya wapenda habari wakisema kwamba gazeti hili tayari limeshakidhi kiu ya wasomaji japo ndio kwanza linaanza. Na nawahakikishia wenye mtizamo huo kuwa hawajakosea. Ama kwa hakika huu ni mwanzo wa tofauti na mazoea. Japokuwa yapo baadhi ya magazeti yanayotoka mara moja kwa wiki ambayo ukilikosa linapotoka usitarajie kulipata siku inayofuata, kwa KULIKONI ukilikosa Ijumaa basi uwezekano wa kulipata kesho yake ni finyu sana. Kwa kifupi, ni gazeti linalokidhi matakwa ya kila aina ya msomaji: mtu mzima kwa kijana, kinababa kwa kinamama, waliojiajiri kwa walioajiriwa, na kadhalika na kadhalika.

Nirejee kwenye kujitambulisha. Mimi ni Mtanzania mwenzenu, na hadi naandika makala haya nipo hapahapa nchini, lakini nitakuwa nikiwaletea makala kutoka huko Ughaibuni ninakoishi. Naamini kuna mengi yanayotokea huko Ughaibuni ambayo ninyi wasomaji watukufu mngependa kuyapata sio kwa mtizamo wa CNN, Newsweek au Times, bali kwa mwenzenu ambae anayaona katika macho ya ki-Tanzania. Labda nifafanue. Mara ya kwanza nilipoombwa sigara na Mzungu nilidhani ni utani. Nilipompatia alinishukuru nusura anilambe miguu.Kumbe yule Mzungu alikuwa ombaomba kama rafiki yangu Matonya (japo ile staili ya Matonya inaweza kuwa kali kuliko zote ulimwenguni).Nilipokutana kwa mara ya pili na jamaa yule alieniomba sigara ,ambapo safari hii aliniomba pauni moja,ndipo nilipogundua huenda akawa ni ombaomba kweli.Uthibitisho niliupata nilipokutana nae kwa mara ya tatu lakini safari hiyo nikiwa na rafiki yangu mmoja Mghana ambae alikuwa hapo Ughaibuni kabla yangu.Huyo muumuu wa Came Nkrumah die alienithibitishia kuwa hapo Uingereza kuna ombaomba lukuki.Niliposimulia hadithi hiyo kwa jamaa zangu hapa baadhi walinibishia.Na walikuwa na hoja.”Mbona tunaangalia BBC kila siku na tunaowaona ni wazungu wanaoonekana kuwa hawana shida hata kidogo”,ilikuwa hoja ya mmoja wao.Ukweli ni kwamba hawa wenzetu wanapenda zaidi kuonyesha yale wanayoyaona kuwa yanaleta picha nzuri ya nchi zao.Angalau balaa la Katrina lilisaidia kuwafumbua macho watu kwamba hata huko kwa George Bush kuna masikini kama hapa kwetu,na wamesahaulika.

Kwa hiyo basi,makala hii itawasaidia Watanzania wenzangu kujua mambo mbalimbali-mazuri kwa mabaya-yanayojiri huko Ughaibuni ambayo ni nadra kwa mtu wa kawaida kuyapata.Naahidi wasomaji watukufu kwamba kama ambavyo hamtopenda kukosa nakala za KULIKONI basi ndivyo hamtotaka kukosa uhondo nitakaokuwa nawaandalia kutoka huko nje.Kama azma ya gazeti hili ilivyo-kuupatia umma chakula cha kila wakati-nami nitahakikisha nawapatia mlo wa kila wakati.Labda tofauti itakuwa ni kwamba mlo huo unaandaliwa kutoka nje.Lakini ugali si ugali tu.Ukitoka Uingreza au ukipikwa Manzese si bado ni ugali.Cha msingi upikwe kwa kuzingatia kanuni za upishi wa ugali.Pengine kingine ni kwamba mapishi haya ya kutoka nje yatakuwa tofauti ni yale uliyoyazowea.Haya yatamlenga mlaji wa kawaida.Kwa ufafanuzi,ni kwamba utofauti wa makala hii ni kwamba kama lilivyo gazeti lenyewe,itakuwa tofauti ni makala mlizozizowea katika baadhi ya magazeti ya kila wiki.Na tofauti yenyewe ni kwamba kipaumbele kitawekwa kwa watu wa kawaida na mambo ya politiki yatakuja tu pale yanapowagusa watu wa kawaida.

Basi hadi Ijumma ijayo,nawaomba make mkao wa Kula ambapo makala motomoto zitaanza kuwajia kutoka Ughaibuni.Ahadi yangu na ya timu nzima ya KULIKONI ni kubeba sauti za watu wa kawaida,na kwahakika hilo linawezekana.

Alamsiki

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.