Hapa nilipo,mtandao unasumbua sana.Kwahiyo,nawaomba mniruhusu niwape tu LINK HII ya makala yangu katika toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema.10 May 2008
10.5.08
Evarist Chahali
MAKALA, RAIA MWEMA
No comments
Hapa nilipo,mtandao unasumbua sana.Kwahiyo,nawaomba mniruhusu niwape tu LINK HII ya makala yangu katika toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema.3 May 2008
Hivi karibuni,eneo la Mlimani (UDSM) liligeuka Baghdad kwa muda kufuatia ghasia kubwa kati ya wanafunzi na vyombo vya dola.Hali sasa ni shwari,na majuzi walifanya uchaguzi wa viongozi wapya wa DARUSO japo inasemekana kwamba turnout ilikuwa ndogo sana.Ni kutokana na ushwari huo ndipo nami nilibahatika kuwatembelea wanazuoni flani hapo,na kufanikiwa kunyaka picha hii inayoonyesha eneo la Ubungo kama sijakosea,japo halionekani vema sana.
Miongoni mwa maeneo ya hapa jijini yanayotuwezesha kuendeleza libeneke la bloggin-japo nyakati nyingine kwa kusuasua-ni cafe moja iliyopo Millennium Tower.Kuna jamaa kanidokeza kuwa yeye huwa mwenyeji sana eneo hili kwa ajili ya kuangalia MIGONGO!Well,inawezekana alikuwa anazungumzia mgongo wa Twiga huyu,jirani na mwanga wa taa,ambaye ni kivutio mwanana!

3.5.08
Evarist Chahali
MAKALA, RAIA MWEMA, UFISADI
No comments
Sina budi kuwataka radhi wasomaji wapendwa kwa kutoweka chochote hapa kwa zaidi ya wiki sasa.Napenda sana ku-update blog hii lakini wakati mwingine mazingira ya hapa yanakuwa kikwazo.Hata hivyo,nadhani mtaburudika na makala yangu katika gazeti la Raia Mwema toleo la wiki inayoisha leo.Makala hiyo ni reaction dhidi ya wababaishaji flani ambao wanajaribu kuhoji usafi wa akina-sie tulioamua "liwalo na liwe" dhidi ya mafisadi.In fact sio kama wanahoji as such,wanachofanya ni kuwa servants wa mafisadi,nisicho na uhakika ni whether wanafanya hivyo kutokana na njaa zao au mfilisiko wa mawazo.Anyway,makala nzima inapatikana kwa kubonyeza hapa23 Apr 2008
23.4.08
Evarist Chahali
CCM, MISS TANZANIA, RAIA MWEMA, TAZARA, UFISADI
1 comment
Naamini wengi wenu mnakikumbuka kibao cha "Ingekuwa Vipi" cha wasanii Jay-Mo na Mwanafalsafa.Nakipenda,sio kwa beats zake pekee,bali pia kimebeba ujumbe mzito wenye maswali mazito.Makala yangu ndani ya toleo la wiki hii la Raia Mwema imeanza kwa kunukuu verse moja ya wimbo huo,lengo likiwa sio uchambuzi wa muziki bali kufanya tafakuri kuhusu mwelekeo wa mambo katika nchi yetu.Tangu nifike hapa nyumbani takriban wiki tatu zilizopita,nimekutana na watu kadhaa ambao wamekuwa wakidai BORA MKOLONI ARUDI KUTUTAWALA.Aliyenisukuma zaidi kujadili suala hili ni abiria mwenzangu niliyesafiri nae katika chumba cha "daraja la kwanza" cha TAZARA,ambaye nae alidai kwamba "Bora Mkoloni arudi" baada ya adha lukuki zilizotupata katika safari yetu.Mie nadhani bora Wachina warejeshewe TAZARA kwani sie Waswahili imetushinda.Hilo la Mkoloni kurudi sina hakika nalo sana,ila ni dhahiri kwamba kuna wanaharamu wanaotutesa mara 100 zaidi ya walivyofanya wakoloni.By the way,wakoloni hawakuwa Watanzania wenzetu,lakini hawa washenzi wanaotufisadi na kulimbikiza fedha (wenyewe wanaita vijisenti) huko nje ni watu tuliozaliwa nao nchi moja iitwayo Tanzania.Makala yangu hiyo imehitimishwa kwa onyo kwa CCM kwamba ikiendeleza porojo zake za Maisha Bora kwa kila Mtanzania (or did they mean "kwa kila fisadi"?) basi wasishangae wakikutana na yaliyowakuta KANU huko Kenya.Ukisikia wananchi wanatamani Mkoloni arudi basi hizo ni dalili kuwa wamechoshwa na porojo za watawala.Pamoja na habari na makala nyingine zilizokwenda shule ndani ya gazeti la Raia Mwema,bingirika na makala yangu hiyo kwa KUBONYEZA HAPAPia kuna picha kadhaa kutoka maeneo mbalimbali ya Bongo.

Nadhani kuna wanaoikumbuka joint moja ya maeneo ya Namanga kuelekea Msasani iliyokuwa ikijulikana kwa jina la Studi Becker.Sasa hivi inaitwa New Angel.Pengine kwa vile ni ya "Malaika Mpya" ndio maana toilets zao ziko kizani kama inavyoonekana (au isivyoonekana?) katika picha.

Picha hizi nzuri (hapo juu na zinazofuata chini) zimepigwa na dada mmoja mrembo wa Hoteli ya Kempinski (ameomba jina na sura yake vihifadhiwe) kutoka ghorofa ya sita ya hoteli hiyo.Dada huyo mdau wa blogu hii anadai amepatwa na wazo la kupiga na kunitumia picha hizo baada ya kuona kile "kimbembe cha zule" cha picha za matope ya barabara ya Ifakara.Picha zote zinaonyesha mandhari ya bandari ya Dar es Salaam,minus ufisadi wa Mamlaka ya Bandari na TICTS.



22 Apr 2008
NINA LUNDO LA PICHA LAKINI LEO INTERNET IKO SLOW SANA.KEEP ON VISITING THE BLOG FOR MORE PICS.PICHA TATU ZA CHINI NI KUTOKA HOSPITALI YA MTAKATIFU FRANCIS IFAKARA (KUNA SANAMU YA MTAKATIFU HUYO KATIKA PICHA YA TATU).PICHA YA NNE NI MAHINDI YALIYOANIKWA KWENYE LAMI.SIJUI NDIO TEKNOLOJIA AU VIPI LAKINI THE IDEA IS SIMPLE:LAMI INAPATA JOTO UPESI NA KWA KUANIKA MAHINDI KWENYE LAMI BASI YANAKAUKA UPESI,NA MASUALA YA UGALI YANAWEZEKANA NDANI YA MUDA ULIOPANGWA.HIKI NI KIPINDI CHA MAVUNO,KWAHIYO NADHANI VIBAKA WA MAHINDI SIO WENGI.SIDHANI KAMA KATIKA KIPINDI CHA NJAA VIBAKA WATAYANUSURU MAHINDI YALIYOANIKWA BARABARANI.



21 Apr 2008
21.4.08
Evarist Chahali
IFAKARA, TAZARA, VACATION PICS
No comments
Makala yangu katika toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema inaelezea kwa kirefu nightmare niliyokumbana nayo baada ya kuingia mkenge wa kusafiri "first class" ya Tazara.Hiyo ilikuwa wakati naelekea nyumbani Ifakara mkoani Morogoro.Baada ya mateso ya hiari huko Tazara,nikaamua usafiri wa kurudi Dar uwe kwa njia ya Barabara.Nadhani picha zifuatazo zinatosha kukueleza namna Maisha Bora kwa kila Mtanzania yanavyowezekana.Kuna jamaa aliyeziona picha hizi kabla sijaziposti amenitania kwamba heri wale ambao "nyumbani" ni Dar es Salaam na si Ifakara,et al kwani hawahitaji Tazara wala matrekta ya kuvuta mabasi.Nikamuuliza iwapo Dar es Salaam anayozungumzia ni ya Oysterbay na Upanga au ile ya Mwananyamala kwa Ali Maua au Mbagala Kibondemaji...kwani alijibu!?
21.4.08
Evarist Chahali
CHENGE, DITOPILE, VACATION PICS
No comments
Bilionea mwenye vijisenti,Andrew Chenge amejiuzulu,na Braza Ditto amefariki.Hizo ndizo habari zinazovuma hapa Dar tangu asubuhi.Hii ya kifo cha Ditto niliisikia jana.Na kama ilivyo kawaida,kila mmoja anasema lake ila kwa vile blogu hii si ya udaku,naomba nisiorodheshe conspirancy theories lukuki zinazovuma hapa jijini.Anyway,kuna picha kadhaa nilizozikamata maeneo mbalimbali.Nyingi zinajieleza zenyewe






HAPO JUU NI BUFFET COACH TAZARA

HUYO UTINGO KAZI YAKE NI KUSHUKA KWENYE FOLENI NA KUWEKA GOGO ILI LORI LISIGONGE MAGARI YA NYUMA.KWA HAKIKA UDEREVA WA BOGNO UNAHITAJI ZAIDI YA LESENI:SALA NA BAHATI NI MUHIMU PIA KUHAKIKISHA UNAMALIZA SALAMA SIKU YAKO BARABARANI.THE SAME LORRY BELOW.


HAPO JUU NA CHINI NI KIZA KWENYE PLATFORM YA TAZARA.

HAPO CHINI NI ENEO LA MIZIGO TAZARA



HUYO UTINGO KAZI YAKE NI KUSHUKA KWENYE FOLENI NA KUWEKA GOGO ILI LORI LISIGONGE MAGARI YA NYUMA.KWA HAKIKA UDEREVA WA BOGNO UNAHITAJI ZAIDI YA LESENI:SALA NA BAHATI NI MUHIMU PIA KUHAKIKISHA UNAMALIZA SALAMA SIKU YAKO BARABARANI.THE SAME LORRY BELOW.


HAPO JUU NA CHINI NI KIZA KWENYE PLATFORM YA TAZARA.

HAPO CHINI NI ENEO LA MIZIGO TAZARA


HAPO CHINI NI KITUO CHA MAFUTA MTANI.VIKO LUKUKI LAKINI BEI INAZIDI KUPAA.INAWEKEKANA ILE KANUNI YA DEMAND NA SUPPLY HAIFANYI KAZI KWENYE SUALA LA MAFUTA!

BELOW IS A LORRY TO AND FROM HELL


18 Apr 2008
18.4.08
Evarist Chahali
CHENGE, UFISADI, VACATION PICS
No comments
16 Apr 2008
16.4.08
Evarist Chahali
BT, HUDUMA, MAKALA, RAIA MWEMA, TANZANIA
No comments
Katika makala yangu ndani ya toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema,nazungumzia suala zima la huduma bora.Makala inaanza kwa kuondoa fikra za "u-tambarare" wa maisha ya ughaibuni,zinazochochewa na taswira za runinga na magazeti ya kimataifa.Ni rahisi baadhi ya wenzetu walioko nyumbani kuhisi kwamba mambo huko "majuu" ni asali na maziwa (land of honey and milk).Kilicho sahihi zaidi kuhusu maisha ya sehemu nyingi za dunia ya kwanza ni huduma inayoendana na matarajio ya mteja.Yaani mteja sio tu mfalme au malkia,bali sehemu ya familia ya watoa huduma (of course kuna exceptions...na kwa UK,tuna wahuni kama British Telecoms-BT,na wababaishaji wengine lakini ni wachache).Maudhui ya makala ni hiyo kwenye title ya post hii:TANZANIA YENYE HUDUMA BORA INAWEZEKANA.Pamoja na habari na makala nyingine za daraja la juu kabisa,binjuka na makala hiyo kwa KUBONYEZA HAPA.
Subscribe to:
Posts (Atom)



