25 May 2011

Askari wa Kikosi cha Kuzuwia Ghasia (FFU) wakiwa tayari kuvunja haki za binadamu nchini Tanzania.Picha hii haihusiani na habari ifuatayo.

Tanzania yetu inaelekea wapi?Tangu lini kupiga picha jeneza imekuwa kosa linalopelekea polisi kukamata waandishi wa habari waliopiga picha majeneza?

Kwa kweli Jeshi la Polisi linafanya kila jitihada kuhakikisha amani na utulivu vinaondoka nchini.Jeshi hilo limekuwa likiendeshwa kibabe pasipo kujali haki za binadamu.Inachukiza kuona polisi wanakurupuka kumkamata mtu yeyote yule wanapojisikia lakini wanakuwa wagumu kuchukua hatua dhidi ya wabaka uchumi wanaotenda uhalifumkubwa kwa taifa kuliko raia wema hao wasio na hatia.

Kadhalika,jeshi hilo limekuwa halina heshima yoyote kwa wanasiasa na wanachama wa vyama vya upinzani ambapo polisi wanawakamata ovyo ovyo.Wito wa tovuti hii ni kwa wanaokamatwa kufungua kesi za madai wanapoachiwa bila kufunguliwa mashtaka.Tkuwaacha wahuni hawa waliokabidhiwa jukumu la usalama kwa raia lakini badala yake wanapelekea adha kwa raia wasio na hatia tutaishia kujilaumu huko mbeleni.Violence begets violence,wananchi watafika mahala wakaamua liwalo  na liwe na hao polisi waonevu hawatakuwa salama.

Ubabe sio ufumbuzi wa matatizo kwani kama tumeshuhudia tawala kadhaa za kibabe zikiondoka madarakani pale wananchi wanapoamua kuwa imetosha,enough is enough.Soma habari ifuatayo na utaelewa ninacholalamikia hapa

Polisi wadaiwa kupora maiti Tarime 
Tuesday, 24 May 2011 22:44

WADAIWA KUVAMIA MOCHWARI USIKU,
WABUNGE CHADEMA WATUPWA RUMANDE
Waandishi Wetu
POLISI Kanda Maalumu ya Tarime, wanadaiwa kuvamia chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime, Mara kuchukua maiti za watu wanne waliouawa katika tukio la uvamizi wa Mgodi wa Nyamongo na kuziweka chini ya ulinzi.Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa tukio hilo lilikwenda sambamba na kukamatwa kwa watu 12 wakiwemo wabunge wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Waliokamatwa katika tukio hilo ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Matiko. Wengine ni kada wa Chadema, Waitara Mwita na wakazi wengine sita wa Tarime ambao majina yao hayakupatikana mara moja.

Chanzo kimoja cha habari kilisema jana kwamba watu hao walikamatwa majira ya saa 3:23 juzi usiku baada ya polisi kupiga mabomu ya machozi eneo la chumba cha kuhifadhia maiti kuwatawanya watu waliojitokeza kuzuia polisi kuchukua miili ya marehemu usiku huo.

Taarifa zilisema kuwa mbali na watu hao kukamatwa juzi, jana majira ya saa 4:30 asubuhi waandishi wa habari watatu; Anthony Mayunga (Mwananchi), Beldina Nyakeke (The Citizen) na Anna Mroso (Nipashe), walikamatwa.

Waandishi hao walikamatwa jana na mbunge huyo wa viti maalumu wa Chadema katika Kijiji cha Nyakunguru na kuhojiwa kwa muda katika Kituo cha Polisi Nyamwaga kabla ya kupelekwa kwa Kamanda wa Operesheni Maalumu, Paul Chagonja. Waliachiwa kwa kujidhamini wenyewe saa 9:30 jioni.

Hata hivyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema alipotafutwa kuzungumzia suala hilo simu yake ya mkononi ilipokewa na msaidizi wake ambaye alisema anayeweza kulitolea ufafanuzi ni msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso.

Senso alipotafutwa naye alisema hawezi kulizungumzia akimtupia mpira Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Tarime, Constantine Massawe.

Hata hivyo, Massawe alikanusha madai hayo ya kupora maiti akisema kwamba walipata taarifa kutoka kwa ndugu wa marehemu kwamba kuna baadhi ya watu waliokuwa wakiwazuia kuchukua miili ya ndugu zao.

"Jana baada ya kufanyika uchunguzi kama walivyotaka, miili yote ilikuwa chini ya familia. Sasa uamuzi wa kuzika ulikuwa juu yao, lakini majira ya saa mbili usiku tulipata taarifa kuwa kuna watu wako mochwari wamezuia ndugu wanaotaka kuzika wasichukue miili ya jamaa zao," alisema Kamanda Massawe na kuongeza:

"Tulipofika tulikuta wapo watu wanane, wanne walikuwa ni wakazi wa Singida na wengine wanne wakiwa ni wakazi wa Tarime. Tuliwakamata na kusimamia ulinzi wa ndugu waliotaka kuchukua miili ya jamaa zao wakachukua."

Alisema baada ya miili hiyo kuchukuliwa, polisi ililitoa msaada wa kuwasafirishia ndugu hao hadi majumbani kwao na walikuwa wanaishusha kadri walivyokuwa wameambiwa na ndugu hao.

‘Sasa asubuhi hii (jana), tumeelezwa kuwa kuna kundi la watu wengine lilikuwa likipita nyumba hadi nyumba kuwahamasisha wafiwa kutokubali kuzika maiti za ndugu zao baada ya kufuatilia tuliwakamata na hawa waandishi wakiwa wanapiga picha jeneza," alisema Kamanda Massawe.

Awali, Katibu wa Chadema Tarime Mjini, Paschal Warioba alidai kuwa polisi walipora maiti hizo na kwamba viongozi wa chama chake walikamatwa juzi usiku majira ya saa nne.

"Lissu yuko 'lockup' (rumande) hapa Nyamongo, walikuwa wakifuatilia maiti za watu waliouawa katika vurugu mgodini ili leo (jana) ziende kuzikwa, lakini kabla ya kufanikisha zoezi hilo jana (juzi), polisi walizipora maiti hizo kwa kuwadanganya baadhi ya ndugu kwa kuwapa fedha ili waende kuzizika," alisema.

Warioba alidai kuwa baadhi ya maiti tayari wamezikwa, lakini wengine wameonekana katika maeneo karibu na walipokuwa wakiishi.

Juzi alasiri, maiti hao walifanyiwa uchunguzi wa mwisho tayari kwa ajili ya maandalizi ya mazishi yaliyokuwa yamepangwa kufanyika jana chini ya uratibu wa Chadema kabla ya vurugu kubwa kuibuka katika chumba cha maiti baada ya polisi kufika na kukuta umati wa watu uliokuwa tayari umekusanyika kuanzia saa 1:30 jioni ili kuchukua miili hiyo kwa ajili ya mazishi yaliyokuwa yamepangwa kufanyika leo.

Hata hivyo, Chadema kinadai kwamba baadhi ya ndugu wa wafiwa waliona maofisa wa polisi wakinunua majeneza manne na kuyapakia katika gari lao kabla ya kufika hospitali hapo kuchukua miili hiyo.

Kutokana na taarifa hiyo, Lissu, Waitara na makada wengine wa Chadema wakiwa na wananchi wengine waliamua kufika katika eneo la mochwari na muda mfupi baadaye, idadi ya watu iliongezeka kwa lengo la kuzuia Polisi kubeba miili hiyo.

"Wakati tukio hilo hapo mochwari polisi walifika majira ya saa mbili usiku na kukuta timu kubwa ya watu ambao walikuwa wamejitolea kulinda maiti hao wasichukuliwe," alisema mkazi wa Tarime aliyejitambilisha kwa jina la Mwita Nyankaira na kuongeza:

"Walianza (polisi) kupiga mabomu ya machozi kuwatawanya watu na ndipo walipowakamata kina Lissu na wengine. Sisi tulifanikiwa kukimbia."

Alisema baada ya polisi kuwasambaratisha wananchi, walirudi hospitalini hapo na kuchukua maiti hao na kuanza kuwapeleka usiku huohuo kwenye familia za wafiwa.

Habari zimeeleza maiti ya Chawali Bhoke ilipelekwa katika Kijiji cha Bonchugu, wilayani Serengeti na Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mwikwabe Makena alisema kulikuwa na vurugu kubwa jana asubuhi kijijini hapo baada ya polisi kuwalazimisha ndugu kupokea mwili huo kwa ajili ya kuuzika.

"Kumekuwa na vurugu kubwa iliyoambatana na polisi kurusha mabomu ya machozi," alisema mwenyekiti huyo.

Maiti nyingine ilipelekwa katika Kijiji cha Nyakunguru, Kata ya Kibasuka. Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyamanche kilichoko kwenye kijiji hicho, Isaack Marara alisema jana saa 12:00 asubuhi, alifuatwa na mkazi wa eneo hilo, Kisabo Ghati na kumweleza kuwa kuna jeneza limewekwa barabarani lakini hawajui kuna nini ndani yake.

"Watu walishtuka sana kwani hawajawahi kuona tukio hilo. Baba mdogo wa marehemu Emmanuel Magige, Ambrose Nyabwanya alidai kuwa saa 6:00 usiku wa juzi, magari mawili ya polisi yalisimama na kushusha jeneza mita 200 kutoka nyumbani kwao kisha magari hayo yakaondoa haraka.”

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, Mwanasheria na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabere Marando alisema kitendo cha polisi kuchukua kinguvu miili ya watu hao wanne kwa lengo la kwenda kuizika ni kinyume na walivyokubaliana.

Marando alisema walikubaliana na polisi pamoja na ndugu wa marehemu Jumapili iliyopita kwamba shughuli za mazishi zifanyike leo katika Uwanja wa Sabasaba.

“Chadema siyo kama tumeshikilia kidedea msiba huu. Tunafanya hivi kwa kuwa waliouawa ni makada wa Chadema na hiyo ndiyo siasa."

Ripoti ya uchunguzi wa miili yawekwa hadharani

Uchunguzi wa miili ya maiti wanne waliopigwa risasi na askari polisi katika Mgodi wa African Barrick North Mara uliofanywa na daktari bingwa kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Makatta imebaini kuwa marehemu wote walipigwa risasi maeneo ambayo hayakulenga kujeruhi, bali kuua.

Uchunguzi huo uliochukua saa 4:27 ulianza saa 5.20 asubuhi hadi saa 9.47 alasiri. Upande wa familia za wafiwa ulisimamiwa na Dk Greyson Nyakarungu kutoka Hospitali ya Wilaya ya Tarime na askari wawili. Taarifa hiyo itakabidhiwa kwa hospitali

Dk Nyakarungu alisema Emmanuel Magige mwenye jalada la uchunguzi wa kidaktari namba za PM1/5/2011 (TGH), alipigwa risasi katika nyonga ya kushoto ambako kulikuwa na tundu la duara llilokuwa na upana wa sentimita 0.5 ilipoingilia na sentimita 2.5 ilipotokea.

“Mishipa ya damu iliharibiwa, kibofu cha mkojo, mishipa ya fahamu, mfupa wa nyonga ulisagika, damu ikavia ndani ya tumbo, lakini chini ya mgongo karibu na risasi ilipotokea kulikuwa na tundu linaloonyesha kuwa alichomwa na kitu chenye ncha kali kama singa ya bunduki,” alisema na kuongeza:

“Tumebishana sana kwa hilo wenzangu wakidai huenda aliangukia kitu kikamchoma, ikumbukwe kuwa alipigwa kwa nyuma akikimbia hivyo asingeweza kuanguka chali zaidi ya kifudifudi,” alisema.

Kuhusu Chacha Ngoka mwenye jalada la uchunguzi wa kidaktari PM 2/5/11 (TGH), uchunguzi ulibaini kuwa alipigwa risasi mgongoni karibu na kiuno na kutokea katikati ya mbavu chini ya titi, tundu la kuingilia likiwa ni sentimita za duara 0.3 na ukubwa wa tundu pa kutokea ikiwa ni sentimita tano.

Mishipa mikubwa ya damu iliharibiwa, ini likasagwasagwa, damu iligandia kwenye mfumo wa upumuaji hali ambayo inadhihirisha kuwa alipumua kwa nguvu, damu ilikwisha mwilini na kuwa alipigiwa risasi kwa mbali.

Alisema marehemu Bhoke mwenye jalada la uchunguzi wa kidaktari PM/3/5/11(TGH) alipigwa risasi ya kichwani karibu na sikio na kidonda chake pakuingilia ni sentimita za duara 0.2 ,pa kutokea sentimita tano za duara kwenye paji la uso hivyo kuharibu ubongo, fuvu na mifupa yote kubomolewa.

Kuhusu uchunguzi wa Mwikwabe Marwa Mwita mwenye jalada la uchunguzi wa kidaktari PM/4/11 (TGH) alisema alipigwa risasi karibu na nyonga na kuacha tundu la sentimita za duara 3,5 na risasi haikutoka nje na kuharibu mifupa yote ya nyonga, misuli ikawa imeharibiwa na kipande cha risasi kilikutwa katikati ya misuli (PSOAS), damu ikiwa imevia tumboni.

“Kilichoonekana hapo ni kuwa walipigwa risasi kwa mbali tena kwa nyuma maana wote zimeingilia kwa nyuma na maeneo waliyopigwa risasi ni yale ya kuua si kuwapunguza nguvu kama walikuwa wamegoma kusalimu amri,” alisema daktari huyo.

Kuzuiwa kwa maziko ya pamoja

Awali, Chadema kilipanga kuendesha ibada ya maziko katika Uwanja wa Sabasaba leo kuanzia saa 2:00 asubuhi kabla ya kupelekwa katika vijiji vyao kwa ajili ya mazishi ya kifamilia.

Lissu alisema juzi usiku kuwa licha ya kukubaliana na wanafamilia na Kamishina wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, jeshi la polisi lilibatilisha kibali hicho baadaye.

"Tumekuwa katika maandalizi ya mazishi hayo tangu jana jioni. Hata hivyo, jioni hii tumeletewa barua ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Tarime kututaarifu kwamba haturuhusiwi tena kuwaaga marehemu wetu kama ilivyokubaliwa jana," alieleza Lissu.


Waandishi waeleza walivyokamatwa

Baadhi ya waandishi waliokamatwa katika sakata hilo walieleza kuwa walikuwa kazini kutekeleza majukumu yao.

Mmoja wa waandishi waliokamatwa, alisema baada ya kusikia taarifa juzi usiku juu ya polisi kupiga mabomu na kuchukua miili ya marehemu aliamua kuingia kazini kufuatilia tukio hilo.

“Tulipofika hapo kijijini tulikuta pia kuna mbunge wa viti maalum wa Chadema, sasa wakati tukiwa tunamhoji, polisi wakafika na kutukamata wakieleza kuwa tumekuwa tukichochea ndugu wasizike miili ya marehemu," alisema

Alisema kitendo cha polisi kuwahoji jana kuanzia saa 5:10 asubuhi hadi saa 6:20 mchana kimewafanya washindwe kuwajibika ipasavyo jambo ambalo linapaswa kulaaniwa na wadau wote wa habari.

“Tulihojiwa hapa kwa zaidi ya saa moja na ilipofika saa 6:20 mchana walituambia tusubiri maelekezo kutoka kwa kamanda wa polisi…" alisema.

Mei 16, mwaka huu polisi wilayani Tarime iliwaua kwa kuwapiga risasi watu wanne kati ya zaidi ya watu 1,000 waliovamia mgodi wa Nyamongo wilayani humo kwa lengo la kupora mchanga wa dhahabu.

Tukio hilo lililotokea katika Kijiji cha Matongo, lilizua msuguano baina ya polisi, Chadema na wananchi wa eneo hilo ambao juzi waligoma kuzika miili ya marehemu hao na kukataa rambirambi ya polisi.

Habari hii imeandaliwa na Antony Mayunga, Tarime,
Frederick Katulanda, Mwanza na Fidelis Butahe Dar


CHANZO: Mwananchi

24 May 2011

Mwangalie kwanza.Hivi abiria watasafiri kwenye hilo lijinembo lisilo na mvuto?Au anamaanisha wapande kwenye mkono wake alioinua?Hovyoooo!!!!

Unajua,baadhi ya viongozi nchini Tanzania wanatuona sie kama machizi vile.How come mtu anayeamua kuondoka katika shirika mfu ajigambe kwa kubadilisha nembo?Huu ni uhuni wa hali ya juu.Lakini uhuni huu unasababishwa na anayeteua wahuni wa aina hii,I mean Rais Jakaya Kikwete.
Hivi Kikwete anajisikiaje kumsikia rafiki yake Mattaka akiwatusi Watanzania kwa kujivunia mafanikio ya nembo mpya ilhali ATC haina ndege hata moja inayoruka?Majuzi tu,Kikwete kaendelezakulialia kuhusu wasaidizi wake anaodai ni mzigo-kana kwamba walimshikia mtutu wa bunduki awateue,na wameendelea kumshikia mtutu wa bunduki asiwatimue.Hii misemina elekezi ya kila kukicha inasaidia nini katika mazingira haya ya mchezo wa kuigiza wa kisiasa ambapo watu wanaosifika kwa tabia zao chafu kuliko ufanisi wao wanaruhusiwa kula fedha za walipa kodi,only kuondoka kwa matusi dhidi ya walipa kodi hao hao?

It's sooo disgusting.Enewei,soma kichekesho hiki kinachoudhi

Mattaka ang'oka ATCL 
Monday, 23 May 2011 21:56

Fredy Azzah

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka ametangaza kustaafu kazi huku akijivunia kubadilisha nembo, ingawa ameliacha likiwa halina hata ndege moja inayoruka.

Mattaka aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa alistaafu rasmi Mei 11, mwaka huu baada ya kufika umri wa miaka 60 na kwamba alishindwa kulifufua shirika hilo la umma kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wa menejimenti. Alitaja moja ya sababu hizo kuwa ni mzigo wa madeni.

“Naondoka lakini najivunia kuiondoa ATCL chini ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) waliokuwa wameingia ubia, pia najivunia kuleta nembo mpya ambayo inatumika sasa,” alisema Mattaka.

Desemba 2002, Shirika la Ndege Tanzania (ATC), lilibinafsishwa kwa kuingia ubia na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) na kubadilisha jina lake kuwa “Air Tanzania Company Limited” (ATCL). “Wanasema najiuzulu.

Hii siyo kweli, nastaafu kwa mujibu wa sheria, ingetakiwa nistaafu kuanzia Mei 11, lakini ni barua tu ndiyo ilichelewa kuja, nimeomba kustaafu na nimekubaliwa,” alisema Mattaka. Mattaka alisema tangu kuteuliwa kwake kuliendesha shirika hilo mwaka 2007, walikuwa na nia ya kulifufua lakini sababu zilizokuwa nje ya uwezo wao zilikuwa kikwazo.

“Shirika lolote la ndege linahitaji mtaji ili liweze kujiendesha, sisi tumechukua shirika likiwa na mtaji hasi wa Sh43 bilioni na madeni yaliyofikia Sh23 bilioni,” alisema Mattaka.

Alisema katika kujitahidi kulifufua shirika hilo, kuanzia mwaka 2007 mpaka mwishoni mwa 2008, walifanya kazi nzuri ikiwa ni pamoja na kununua ndege moja yenye uwezo wa kubeba abiria 50 na kukodi nyingine aina ya Air Bus, shughuli ambayo alisema waliifanya katika mazingira magumu.

Alisema baada ya mwaka huo, mafuta ya ndege yalipanda kwa zaidi ya asilimia 50, jambo lililoyafanya mashirika mengi ya ndege yaliyokuwa yakiendeshwa bila ruzuku ya serikali kuanguka.

“Mwishoni mwa 2009 ndipo serikali ikaanza kutoa fedha kidogo kidogo ambazo hata hivyo, ilizielekeza kwenye kulipa madeni. Napenda tu kusema kuwa sasa serikali inatakiwa kuwa na shirika lake la ndege,” alisema Mattaka na kuongeza: “Unapokuwa katika shirika la umma ukastaafu bila matatizo ni jambo la kumshukuru Mungu, kwa hiyo kwa sasa napenda tu kumshukuru Mungu kwa kunifikisha hapa.”

Amlaumu Mkapa
Awali, Mattaka alisema katika uongozi wake ndani ya mashirika ya umma, kamwe hatamsahau Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ambaye alimsimamisha alipokuwa Mkurugunzi wa Mfuko wa Jamii wa (PPF) kutokana na kashfa mbalimbali, ikiwamo ya rushwa na ubadhirifu wa fedha.

Anasema kitendo cha kusimamishwa kwake ghafla kilimuumiza sana, ingawa anadai kuwa baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Usalama wa Taifa kuchunguza, walibaini kuwa hapakuwa na ukweli wowote wa kashfa zilizomfanya asimamishwe kazi.

“Unajua bwana siku zote mti wenye matunda ndiyo hurushiwa mawe, waliona majengo yanaibuka tu, mara PPF House, PPF Tower na kile Kijiji cha PPF kule Arusha, wakasema lazima hizi ni 10 percent.” “Walichunguza wakakuta yote yale hayana ukweli wowote na wakanilipa stahili zangu ambazo ndizo zilinifanya nikae takribani miaka ninne mpaka nilivyokuja tena huku ATCL.”

Alisema ameondoka ATCL na kuliacha likiwa halina hata ndege moja inayoruka akidokeza kwamba moja ipo Afrika Kusini ikifanyiwa matengenezo ambayo anasema yamekamilika na kinachosubiriwa ni Serikali kulipa fedha za matengenezo.

Alisema ndege nyingine ipo nchini lakini haifanyi kazi kutokana na kuhitaji matengenezo ya lazima. Mattaka alisema, serikali imemteua William Haji, kukaimu nafasi anayoiacha.

CHANZO: Mwananchi

23 May 2011




BONYEZA PICHA HAPO JUU KUSOMA HABARI KAMILI






CHANZO : Daily Mail

22 May 2011



URBAN PULSE CREATIVE Ilipata fursa ya kufanya mahojiano maalum na MH Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokuja katika Ziara yake hapa nchini Uingereza siku chache zilizopita. Mahojiano hayo maalum yalilenga zaidi kuelemisha jamii yetu ya kitanzania, vile vile kutoa Msimamo kutoka katika serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusiana na mambo mbalimbali yanayomhusu Mtanzania .

Mahojiano hayo yaligusa maeneo tofauti yakiwepo majukumu pamoja na changamoto anazokumbana nazo Mh waziri mkuu, Suala la katiba, Uchumi, Rushwa na Ufisadi, Miundo Mbinu, Maendeleo, Chakula, Nishati, Jumuiya ya Africa mashariki pamoja na mambo mengine mengi.Mahojiano yalifanywa na Baraka Baraka Kutoka URBAN PULSE CREATIVE MEDIA na yatarushwa hewani mda sio mrefu.

MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU IBARIKI TANZANIA

Asanteni,

URBAN PULSE CREATIVE MEDIA



For you guys who Swahili is a foreign language,the happy dude in the middle is a Bishop.Seen in the picture on the left is him preaching the Gospel of Jesus.Joined by the two ladies in a pool,the Bishop couldn't resist flashing a RAPTURous smile...

 The same Bishop,Jamal Ally Hussein,who converted to Christianity from Islam,is seen posing romantically with a young girl...RAPTURE!!!!

Photo credit: Global Publishers

20 May 2011


CCM Arusha kwachafuka

Thursday, 19 May 2011 22:42

CHATANDA ATAKIWA KUNG'OKA, GARI LAKE NUSURA LICHOMWE MOTO NA UVCCM
Moses Mashalla, Arusha
HALI si shwari chama tawala mkoani Arusha mara baada ya gari la Katibu wa CCM hapa, Mary Chatanda kunusurika kuchomwa moto na baadhi ya wanachama wa Umoja wa Vijana wa chama hicho(UVCCM).Wanachama wa umoja huo kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Arusha waliandamana katika Jengo la Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Arusha, wakishinikiza Chatanda pamoja na Mjumbe wa Baraza la Vijana mkoani Arusha, Mrisho Gambo "wajivue gamba".

Hali hiyo ilijitokeza jana katika jengo la makao makuu ya chama hicho wakati Kikao cha Kamati ya Siasa Mkoa kikiendelea ambapo, hali iliyosababisha dereva wa gari la katibu huyo wa CCM kulitoa nje ya jengo hilo na kisha kulikimbiza mahali kusikojulikana.

Vijana hao walikuwa wameshika mabango yenye ujumbe mbalimbali huku wakipaza sauti zilizokuwa zikimtaka Chatanda kuondoka katika nafasi yake ya uongozi kwa madai kwamba amekuwa akikivuruga CCM mkoani Arusha.

Wakizungumza na waandishi wa habari, wanachama hao kutoka wilaya za Monduli, Longido, Arusha, Arumeru, Karatu na Ngorongoro walisema pamoja na wao kutoa malalamiko mbalimbali juu ya Chatanda na Gambo, lakini uongozi wa CCM taifa umekuwa ukiwakumbatia viongozi hao na kudai sasa wamechoka.

Walisema malaliko yao kuwa Chatanda amekuwa akikivuruga chama chao ikiwa ni pamoja na kusababisha kukosa ushindi wa Jimbo la Arusha Mjini lililoenda kwa Chadema huku wakisema kwamba ikiwa atakataa kung'oka watajua cha kufanya.

“Hatumtaki Chatanda na hatumtaki Mrisho Gambo hawa watu kwanza ni wasaliti, lakini pia wamechangia sisi kushindwa kuchukua jimbo hili kwani walikuwa wanaiunga mkono Chadema tunataka waondoke mara moja hadi kieleweke,” ilisikika sauti ya mmoja wa vijana hao.

Miongoni mwa jumbe ambazo zilikuwa zimeandikwa kwenye mambango hayo ni "Chatanda umehujumu uchaguzi kwa siasa zako za makundi zilizojaa chuki, ubinafsi na ubabe usio na manufaa kwa Chama Cha Mapinduzi", "Chatanda kwa siasa zako za ubabe umetuchonganisha na viongozi wa dini”, na nyingine kadha wa kadha.

Hali hiyo ilisababisha Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Arusha, James Ole Millya aliyekuwa kwenye kikao cha kamati ya siasa kutoka nje na kwenda ukumbini kuwatuliza wanachama hao, lakini juhudi zake ziligonga mwamba.

Akizungumza na wanachama hao, Milya aliwataka wapunguze jazba na kusema kuwa yeye ni mjumbe ametumwa kusikiliza madai yao hivyo wampatie na kisha taufikisha ujumbe huo.

“Jamani ninawaomba mtulie sidhani kama mtafanya fujo ninaomba mnipatie ujumbe mnitume niufikishe jamani nami nitaufikisha tulieni jamani,” alisema Milya

Hata hivyo, ushawishi wa Milya haukuzaa matunda na kuamua kurudi kikaoni kwani wanachama hao waliendelea kupaza sauti zao kwa wakidai kuwa wanamtaka katibu huyo aondolewe mkoani Arusha kwa kuwa amekuwa akiingilia uamuzi wa umoja wao na kuendelea kumkubatia Gambo.

“Mheshimiwa tunakipenda sana chama chetu na tunakuheshimu sana, tunaomba Chatanda aondoke la sivyo tutachoma gari lake, tukikutana nalo tutamondoa kwa nguvu,” alisema kwa jazba mmoja wa vijana hao.

Vijana wavamia kikao cha kamati ya siasa
Wakati hayo yakiendelea wanachama hao walikosa uvumilivu na kisha kuvamia ofisi ambapo Kikao cha Kamati ya Siasa mkoa kilipokuwa kikifanyika huku wakitishia kubomoa mlango kitendo kilichosababisha viongozi mbalimbali wa CCM mkoani hapa kuhaha kutuliza tafrani hiyo.

Maafisa usalama wakiwemo askari kanzu walikuwa wametanda katika maeneo ya jengo hilo huku wengine wakionekana wakizungumza na viongozi wa UVCCM kujua chanzo cha vurugu hizo.

Chatanda ajifungia ukumbini
Hadi tunakwenda mitamboni, Chatanda alikuwa bado amejifungia ndani ya ukumbi wa mkutano na hakuna taarifa yoyote ya CCM Mkoa aliyotolewa kuhusiana na tukio hilo.

Tuhuma dhidi ya Chatanda kutoka ndani ya chama chake zimekuja siku chache tangu ashutumiwe kuwa mmoja wa waliosababisha mgogoro mkubwa wa kisiasa mkoani Arusha baina ya vyama vya CCM na Chadema.

Mgogoro huo unafuatia Chadema kupinga katibu huyo wa CCM wa Mkoa wa Arusha kushiriki katika vikao vya Baraza la Madiwani na kupiga kura ya kumchagua meya wa Jiji la Arusha, hali Iliyosababisha maandamano makubwa ambayo yalisababisha vifo vya watu watatu.

Wakati CCM wakidai kuwa Chatanda ni mjumbe halali wa vikao vya baraza hilo, Chadema wamekuwa wakipinga kwa maeleo kwamba mwanamama huyo ni mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tanga hivyo hana sifa ya kushiriki vikao vya Arusha.
CHANZO: Mwananchi



Mauaji Tarime yalikoroga taifa
• Mbunge Lema apambana na kamishna wa polisi

na Mwandishi wetu

MAUAJI ya watu watano waliouawa na polisi, Tarime mkoani Mara kwa madai walikuwa ni wahalifu waliotaka kuvamia mgodi wa North Mara Barrick sasa ni dhahiri yameikoroga serikali na taifa kwa ujumla.

Jana Jeshi la Polisi pamoja na kutuma timu ya maofisa waandamizi kutoka makao Makuu ya Jeshi hilo, lilishindwa kuwashawishi ndugu wa marehemu hao ambao walikataa kusitisha mgomo kususia miili hiyo hadi serikali itoe tamko la kukomeshwa mauaji hayo na wahusika kuchukuliwa hatua.

Timu ya maofisa waandamizi kutoka makao makuu ya jeshi hilo ikiongozwa na Mkuu wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi, Kamishna Paul Chagonja walilazimika kuondoka pasipo kufikia muafaka katika eneo la chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya wilaya baada ya mamia ya waombolezaji waliopiga kambi tangu Jumatatu kukataa mapendekezo yao.

Awali Kamishna Chagonja aliwahutubia wananchi hao akiwataka waridhie miili hiyo ifanyiwe uchunguzi na kuchukuliwa kwa ajili ya mazishi yatakayogharamiwa na serikali lakini juhudi zake ziligonga mwamba baada ya ndugu wa marehemu kukataa mapendekezo hayo, kwanza wakitaka taarifa ya serikali kulaani mauaji hayo.

“Sisi tumekuja hapa kushirikiana nanyi kwa lengo la kutafuta ufumbuzi sasa tunawaomba mridhie kufanyika uchunguzi halafu taratibu nyingine za mazishi zifuatwe ambapo pia tumejitolea kama jeshi la polisi kushiriki kwa kutoa msaada wa hali na mali ili tufanikishe zoezi hili, tunaomba mkubali kufanyika uchunguzi na tume huru itaundwa kuchunguza tukio hilo,” alisema Changonja.

Kauli yake hiyo ilipingwa vikali na waombolezaji hao ambao walishikilia kuwa kwa vyovyote vile ilivyotokea hakukuwa na sababu ya kuhalalisha vifo hivyo kwa sababu polisi ndio wahusika na walitumia nguvu nyingi kupita kiasi kukabiliana na raia wasiokuwa na silaha za moto.

Wakiongozwa na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema (CHADEMA) aliyepiga kambi katika eneo hilo, wana ndugu hao walidai ingawa hawakupinga kuendelea na zoezi la mazishi lakini wasiwasi wao ulitokana na uharaka wa jeshi hilo kutaka kupoteza ushahidi kwa kulazimisha kufanyika mazishi.

Lema apambana na kamishna wa polisi

Katika eneo la chumba cha kuhifadhia maiti, mbunge wa Arusha mjini, ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Lema alilazimika kumhoji Kamishna Changoja kwa maswali mazito akitaka kujua uharaka wa Jeshi la Polisi kufanya maziko tena ya watu waliowaita kuwa ni wahalifu.

“Kwa nini mnaharakisha maziko bila kuwepo kwa mtu anayewafanyia postmotem? Wewe unasema umetumwa na serikali umetoka makao makuu kuja kuiwakilisha serikali ni serikali ipi unayoiwakilisha?

“Asubuhi Waziri Kagasheki amesema waliouawa ni wahalifu… umekuja hapa huna mkuu wa mkoa, wilaya wala mbunge unamwakilisha nani kwenye serikali iliyokutuma? Ninatilia mashaka uharaka wa serikali kuwazika watu hawa. Ina maana serikali inazika majambazi? Umeanza lini utaratibu huu?” alihoji Lema.

Alisema polisi na serikali yao kuamua kutoa sh milioni tatu kwa kila marehemu kwa ajili ya maziko haijawahi kutokea.

Akizungumza na gazeti hili Lema alisema; “Wakati namuuliza chagonja anasema nisilete siasa kwenye jambo hilo hivi nani sio mwanasiasa? Huyo waziri aliyesema waliokufa ni wavamizi naye mwanasiasa.

“Kwa niaba ya chama changu tumefanikiwa kushwawishi ndugu wote wa marehemu na wameshawishika tukaondoka kwa pamoja pale chumba cha kuhifadhi maiti tukamuacha Chagonja na polisi wenzake, tumemwambia tunaahirisha maziko haya hadi postmotem itakayosema marehemu waliuawa kwa kupigwa risasi wapi kama ni mguuni au kichwani tujue,” alisema Lema.

Kauli nyingine ya Kagasheki

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamis Kagasheki, amemtuhumu mbunge mmojawapo wa chama fulani cha siasa (hakukitaja) kuhusika katika tukio la kushambuliwa kwa Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwile (CCM), aliyedai kufika katika eneo la Nyamongo kwa ajili ya kuwafariji ndugu wa marehemu waliouawa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, katika uzinduzi wa sera ya ukimwi eneo la kazi kwa jeshi la polisi nchini, Waziri Kagasheki alisema mbunge wa chama hicho cha siasa alitoka jimboni kwake na kufika kwenye jimbo lingine kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kufanya fujo.

“Suala la Nyamongo sitaki kulizungumzia kwa kina, ila niseme kwamba kuna mbunge mmoja wa chama fulani cha siasa, alisafiri kutoka jimboni kwake na kwenda jimbo hilo kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kufanya fujo….

“Kitendo kama hicho na vingine vinavyowiana kamwe haviwezi kuvumiliwa ndani ya nchi…,” alisema Waziri Kagasheki.

Alipoulizwa ni hatua gani serikali itazichukuliwa dhidi ya mbunge huyo, Waziri alishindwa kuweka wazi.

“Nimeshasema sitaki kulizungumzia kwa kina suala hilo, na kuliweka wazi mbele ya umma….” alimaliza na kuondoka.

Ngeleja naye azungumza

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja, ameeleza kusikitishwa na vurugu zilizotokea katika mgodi wa dhahabu wa North Mara. Ngeleja alieleza hayo jana alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua tamko la wizara yake kuhusu vurugu hizo mgodini.

“Tumesikitishwa na taarifa hizo pamoja na vifo vilivyotokea tunatoa salamu za pole kwa wafiwa, kwa sasa vyombo vya usalama vinashughulikia hali hiyo,” alisema Waziri Ngeleja baada ya kuzindua bodi ya wakala wa ukaguzi wa madini.

Alisema pamoja na mambo mengine, serikali kupitia wizara yake imekuwa ikifanya juhudi kuhakikisha katika eneo hilo kunakuwa na mahusiano mazuri kati ya wawekezaji na wananchi wa eneo hilo.

Alieleza pamoja na changamoto mbalimbali zilizopo katika eneo hilo tayari serikali na wawekezaji wamebuni mradi wa uchimbaji mdogo wa madini ambao utaanza baadaye mwaka huu ili kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi.

Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 23 wameuawa kwa vipindi tofauti kwenye mgodi huo. Hata Barrick wenyewe wanasema nia yao si kuua raia hivyo hawakubaliani na kitendo kilichofanywa na polisi.

CHANZO: Tanzania Daima

19 May 2011


JINA LA BLOG: KONA YA MATUKIO

Tunapenda kulitambulisha wadau wote libeneke jipya la KONA YA MATUKIO ambapo nia na lengo kubwa ni kuleta matukio yanayotokea kila siku katika Jamii yetu na Duniani kwa Ujumla..pia kutakuwa na Matukio ya papo kwa hapo yani Breaking News Endelea kuwepo kila muda kujua nini kitatokea

Kama unatukio la aina yoyote tutumie kupitia [email protected] 
Karibuni nyote na asanteni kwa kututembelea.

Pamoja Tunaweza



Alfajiri ya leo nilikutana na comment ya msomaji mmoja aliyejitambulisha kama Andrew Blasio.Msomaji huyo alianza kwa kuhoji kama sijawahi kuona zuri lililofanywa na CCM.Mie nikamjibu kwa kifupi, "You tell me,sir" kwa maana kama yeye anayajua mema ya CCM basi anieleze badala ya kutegemea mie niyataje.

Akanijibu kuwa yeye haamini kuwa hakuna jema la CCM.HAAMINI.So what?Kwa vile yeye haamini kuwa hakuna jema la chama hicho basi imekuwa nongwa kwa mie kuandika yasiyo mema ya CCM.Akaendelea kunishutumu kuwa eti niko biased katika uandishi wangu,na pengine ni propaganda.Akadai mwandishi sharti awe fair na balanced,na kuhitimisha kuwa hajaona mwandishi anayehubiri uvumilivu wa kisiasa.KWA VILE YEYE HAJAONA BASI INAMAANISHA HAKUNA KITU KAMA HICHO!!!

Nikamjibu

 Sasa mbona wewe unayejua mema ya CCM hutaki kuyaweka hadharani?Na hiyo political tolerance kwako unaitafsiri vipi?Mafisadi wasikemewe?

Nikaongeza 

Unakosoa kuwa niko biased kwa vile hujaona nikiandika "mema" ya CCM.Je bado utaniona biased nikikwambia sijaona jema la kuandika?Na kwanini wewe mwenyewe usijione uko biased kwa kutarajia mema hata kama hayapo?Kukosoa ni rahisi kuliko kutenda jambo.Why not start writing objective,unbiased articles preaching all the good stuff CCM wanafanya?

Naye akanijibu 

Usinishambulie bosi! I'm trying to read " black and white"! kama huoni jema lolote lililofanywa na serikali ya CCM then that is your problem maana "Mwenye macho haambiwi tazama!". Being fair and balanced comes from "journalistic ethics & standard". it doesn't matter whether you are reporting news or you are penning opinions!

Nikahitimisha mjadala kwa kumwambia, 

To be honest with you,I dont write to please whoever reads my articles.I speak my mind supported with facts.As for "journalistics ethics&standards",I'm not a journalist by profession.Tell you what my friend,if you dont like what I write,or it's contrary to what you believe,best I could advise you is to avoid reading them.I dont take issues with constructive criticism,but I hardly pay attention to "people who are not happy with what I wrote just because it's contary to their points of view

Kimsingi,Bwana Blasio hapendezwi na msimamo wa makala zangu kuikosoa CCM,na angependa kuona ikipongezwa.Lakini kama ulivyoona kwenye malumbano yetu hapo juu,yeye mwenyewe hajaongea japo suala moja ambalo lingeweza kuifanya CCM ipongezwe.It doesnt make any sense kumshutumu mtu anayekemea jambo flani lakini wakati huohuo mtoa shutuma anashindwa kutoa japo mfano mmoja wa kuonyesha kuwa kukemea huko sio kwa haki.

Kwa Bwana Blasio na watu wengine wenye mtizamo kama wake,napenda kuwafahamisha kuwa siandiki makala kwa minajili ya kujikomba au kumpendeza mtu.Ninachoandika ni mawazo yangu binafsi,ambayo kama kawaida yangu hayatoki tu pasipo utafiti wa kutosha na wa kusapoti nisemacho.

Lakini la msingi zaidi ni hili.Kama kuna mtu anaona ninachoandika hakimpendezi,kwanini basi apoteze muda wake kukisoma?Si kwamba sipendi kukosolewa bali ninachoafiki ni constructive criticism na sio baseless and unfounded criticism.

Ni rahisi kulaumu makala ninazoandika lakini si rahisi kuandika makala mbadala.Na pengine njia mwafaka ya kupambana na hoja "potofu" kama zangu (kwa mujibu wa Bwana Blasio) ni kuandika makala inayoweza sio tu kujibu au kupinga hoja zangu bali pia kukata mzizi wa fitina kwa kuorodhesha mema ya CCM ambayo hayapatikani kwenye maandiko yangu.

NAREJEA TENA.SIANDIKI KUMFURAHISHA MTU BALI NINA-EXPRESS MAWAZO YANGU NILIYOYAFANYIA KAZI KWA UMAKINI KABLA YA KUYAWEKA HADHARANI.ASIYERIDHISHWA NAYO ANAWEZA KUYAPUUZA KWA KUKAA KIMYA AU KUTOYASOMA.MAWAZO MBADALA RUKSA LAKINI SHUTUMA ZISIZO NA KICHWA WALA MIGUU HAZINA FURSA.


Makala yangu katika toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema inazungumzia "usanii" wa CCM kujivua magamba,na kuwaingiza mkenge watu kama Nape Nnauye walioamini kuwa chama hicho kimeamua kufanya kweli,kabla ya "moto wa karatasi" haujazimika wenyewe.

Kadhalika,katika makala hiyo nimejaribu kuwashauri CCM watambue kuwa kamwe ugonjwa hautibiki kwa kuukwepa bali kuutambua na kuutibu.Kwa chama hicho,tatizo la msingi ni mwenyekiti wake wa taifa,Rais Jakaya Kikwete,ambaye aliletwa madarakani kwa nguvu za "magamba" na aliposhika hatamu za madaraka akayalea "magamba" hayo.The so-called magamba ni sehemu muhimu ya uhai wa kisiasa wa Kikwete.Kwahiyo kama CCM ina dhamira ya kweli ya kuondokana na ufisadi (magamba) hawana budi kuanza na Kikwete.

Pamoja na makala hiyo ni habari moto moto na makala nyingine zilizokwenda shule ndani ya jarida hili mwanana la Raia Mwema.BONYEZA PICHA HAPO JUU KUSOMA MAKALA HIYO.

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.