CHANZO: Daily Mail
CHANZO: Daily Mail
![]() |
| Picha kwa hisani ya Je Unajua Hii |
| JK: Nawajua wala rushwa kwa majina | |
By Richard Williams | Published 02/22/2006 | Habari za Kitaifa |Rating:![]() ![]() ![]() ![]() ![]() | |
Richard Williams .Asema tabasamu lake lisipotoshe watu .Maamuzi yake si nguvu ya soda RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amesema anawajua kwa majina wala rushwa katika wizara na kwamba nguvu anayokwenda nayo siyo ya soda. Alikuwa akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika jana katika uwanja wa michezo wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga, mkutano ambao lengo lake lilikuwa ni kuwashukuru wananchi wa mkoa huo kwa ushindi wa kishindo waliompatia yeye na Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa Desemba 14, mwaka jana. Rais Kikwete ambaye mkoa wa Rukwa ulikuwa ni wa nne katika ziara zake za kuwashukuru wananchi, amesisitiza kwamba kauli mbalimbali ambazo amekuwa akizitoa katika ziara zake za kutembelea wizara mbalimbali na idara za serikali ni kauli ambazo hazitoi kwa kutania, bali ni kauli za mambo anayoyafahamu vyema na kwamba mengine ameyaweka akiba. "Sizungumzi kwa utani nayajua ninayoyasema. Nilichoweka akiba ni kuwataja watu kwa majina, wasidhani nikienda wizarani nikasema watu hawa wanakula rushwa wasidhani siwajui kwa majina, ninawajua, bali kwa sasa ninatoa muda kwa watu hao wajisahihishe. Mwenye masikio nadhani atakuwa amesikia," alisisitiza. Katika mazungumzo yake na wananchi hao ambayo mara kwa mara yalikuwa yakikatishwa na vigelegele na nderemo; Rais alirudia tena kauli yake kwamba Mwenyezi Mungu amemuumba akiwa na sura ya tabasamu jambo alilosema kuwa hawezi kulibadili, lakini tabasamu hilo lisiwapotoshe watu, kwani yanapokuja mambo ya msingi huwa hana mchezo na mtu. Alisisitiza kuwa kila kiongozi katika nafasi wajibu wake ni kuwatumikia wananchi na kwamba wananchi wanayo haki ya kupata huduma kutoka kwa kiongozi huyo. "Ikifika mahali Mtanzania akitaka huduma kutoka kwa mtumishi wa serikali anayelipwa mshahara, basi ni lazima kwanza kabla ya kupewa huduma hiyo, amlipe mtumishi yule, tukifika huko basi huo ni ukiukwaji wa maadili ya kazi na mtu kama huyo hastahili kuwa mtumishi wa umma. "Tumejipanga vizuri ndani ya serikali katika kuwatumikia wananchi, na hii siyo nguvu ya soda, ukisimama mbele yetu utasukumwa," alisema na kushangiliwa na wananchi. Rais amebainisha kuwa wale watumishi ambao wamekuwa wakidhani kuwa kutokana na unyeti wa taaluma zao basi hata wakinyanyasa wananchi hawataondolewa katika nafasi zao, wakidhani hivyo wanajidangaya. "Anayedhani kuwa ataendelea kuharibu kwa sababu katika taaluma yake itachukua muda kuwafundisha watu wengine, anajidanyaganya, tuko tayari kuanza upya. Bora tabu kuliko kuwa na mtu wa aina hiyo ambaye badala ya kuwatumikia wananchi yeye anawatesa," alisema. Alisema maamuzi mbalimbali ambayo serikali inayachukua hivi sasa na hapo baadaye yanalenga katika kuurejesha utumishi wa umma katika mstari ulionyooka na kwa sababu hiyo amewataka watumishi wa serikali kuu na serikali za mitaa kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia maadili ya kazi na viapo walivyokula Alisema mfanyakazi atakayetekeleza kazi zake kwa kuzingatia maadili ya kazi yake, hata nishani anaweze kupewa na serikali, lakini kwa yule ambaye atafanya kinyume chake serikali haitakuwa na muda naye. "Hatuna ugomvi na mtu wala hatuna chuki na mtu, tunachotaka kutoka kwako ni utumishi wako uliotukuka kama ulivyoapa kufanya kazi kwa kuzingiatia maadili," alisisitiza Rais na kuufanya umati wa wananchi wa Sumbawanga kumshangilia. Alisema kuwa anachotoa ni ilani na kukumbushana kama gari lilikuwa linapita kwenye majani, basi sasa lirejee barabarani ili kule lilikokuwa linapita lisije kuwakanyaga watu. Kikwete alisema uwajibikaji huo wa watumishi wa serikali kuu na mitaa unawahusu vilevile wakuu wa mikoa ambao tayari alishazungumza nao, na atarudia tena kwa wakuu wa wilaya na wakuregenzi wakati atakapokutana nao mara baada ya kukamilisha kazi ya kuwateua. Akiwashukuru wananchi wa mkoa huo kwa kumpatia ushindi wa asilimia 86, Rais alisema kuwa ahadi ya serikali ya kuwajengea barabara ya lami kutoka Sumbawanga hadi Tunduma, iko palepale na kwamba kazi ya uchoraji imekwisha kamilika na zabuni za kutafuta kandarasi ili kazi ianze inaendelea. Kuhusu mvua zinazoendelea kunyesha katika mkoa huo, Rais amewaomba wananchi hao kuzitumia vizuri ili waweze kuzalisha chakula cha kuwatosha wao na ziada itumike kuwalisha Watanzania wengine ambao mikoa yao imekosa mvua. Rais Kikwete alishindwa kuhutubia jana mjini Iringa kwa sababu ya mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na radi na hivyo atahutubia leo na baadaye atakwenda kutembelea mabwawa yanayotoa umeme ya Kihansi na Mtera. Mikoa ya Rukwa na Mbeya ambayo hivi sasa mvua zinanyesha, ingawa zilichelewa kuanza, hali ya mashamba na mazao ni ya kuridhisha hali inayoashiria kuwa kama mvua hizo zinataendelea basi kuna uhakika wa kupata chakula kwa wingi. Mkoa wa Rukwa hauna matatizo ya njaa isipokuwa katika wilaya ya Mpanda ambako bei ya mahindi imepanda hadi kufikia sh. 10,000 kwa debe, kupanda kwa bei huko kumetoka na wananchi wa maeneo hayo kuuza kwa wingi mahindi yao za ziada katika nchi jirani ambako kuna njaa. Mkoa huo wa Rukwa unatarajia kuzalisha tani milioni 1.2 za mahindi wakati mahitaji halisi ya mkoa ni tani 500,000. ISSN 0876-3896 NA.19240 Na Maura Mwingira, Sumbawanga | |
![]() |
| HUU NDIO UBUNIFU WA DARAJA LA JUU KWA WATEMBEA KWA MIGUU WA JIJI LA MBEYA ENEO LA MWANJELWA MIAKA MIWILI IJAYO KAMA ULIVYOBUNIWA NA TAASISI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA |
Taswira ya karibu inayo onesha Soko la Mwanjelwa jijini Mbeya |
Dk Slaa ang’ara urais
Wednesday, 03 August 2011 23:11
0
digg
NI IWAPO UCHAGUZI MKUU UNGEFANYIKA SASA ANGESHINDA.
Leon BahatiMATOKEO ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Synovate yanaonyesha kwamba iwapo Rais Jakaya Kikwete angeamua kujiweka kando na ukaitishwa Uchaguzi Mkuu sasa, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa angeibuka mshindi wa nafasi hiyo.Ripoti ya Synovate iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana ambayo inawapa wapinzani fursa ya ushindi kwa mara ya kwanza, wagombea kutoka vyama vya upinzani wana uwezo wa kupata asilimia 67 iwapo uchaguzi ungefanyika sasa.
Dk Slaa anaongoza kwa kupata asilimia 42, akifuatiwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (asilimia 14), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (asilimia 12) na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe asilimia tisa.
Synovate inaeleza kwenye ripoti hiyo kwamba matokeo ya utafiti huo yanatokana na watu mbalimbali wenye umri zaidi ya kuanzia miaka 18 walioulizwa maswali ya ana kwa ana vijijini na mijini.
Katika kupata maoni juu ya mtu ambaye wangependa awe rais waliuliza: “Mbali na Rais Jakaya Kiwete, ni mtu gani ungeweza kumchagua kuwa Rais iwapo atakuwa miongoni mwa wagombea?”Kwa mujibu wa matokeo hayo, iwapo uchaguzi ungefanyika sasa, Pinda angeambulia nafasi ya tatu licha ya kwamba CCM ndicho chama kinachoongoza kwa kuaminika mbele ya umma ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa.Katika utafiti wake huo uliofanywa kati ya Mei 2 hadi 29, mwaka huu, jumla ya watu 1,994 walihojiwa.
CCM wamtaka Dk SlaaUtafiti huo unaonyesha kuwa wanachama wengi wa CCM walionyesha kuvutiwa na Dk Slaa ikilinganishwa na viongozi wengine ndani ya chama hicho tawala.Hii inatokana na takwimu kuonyesha kuwa kati ya waliohojiwa katika utafiti huo, wengi wanatokana na CCM, lakini wakamchagua Dk Slaa.
Takwimu za ripoti hiyo zinaonyesha kuwa kati ya waliohojiwa, walipoulizwa kuhusu vyama vyao asilimia 51 walisema ni CCM, asilimia 35 wakasema Chadema, 10, CUF na TLP asilimia moja.
Mbali na Dk Slaa, Profesa Lipumba, Pinda na Zitto wanasiasa wengine wanne wanaofuatia ambao asilimia walizopata zimo kwenye mabano ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli (4), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (2) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (2).
Kadhalika, vigogo tisa waliofungana kwa kupata asilimia moja ya kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo ni Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe na Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya.
Katika utafiti huo, Synovate iliegemea nyanja tatu za utafiti ambazo ni siasa, uchumi na masuala ya kijamii na utamaduni.
Mgombea urais CCM 2015Ndani ya CCM, anayepewa nafasi ya kwanza kuwa mgombea urais kwa mwaka 2015 ni Pinda aliyepata asilimia 35 akifuatiwa na Dk Magufuli asilimia 14.
Wanaofuatia kwa mvuto pamoja na asilimia walizopata kwenye mabano ni Membe (8), Sitta (3), Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye (3), Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa (3) na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi (2).
Vigogo tisa ndani ya CCM walifungana kwa kupata asilimia moja nao ni Makinda, Dk Mwakyembe, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Magembe na Waziri Mkuu wa zamani, Dk Salim Ahmed Salim.Wengine ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk Asha-Rose Migiro, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba.
Uvuaji gamba CCMUtafiti huo wa Synovate unaonyesha kuwa Watanzania wengi wanatofautiana juu ya uelewa wa mpango wa CCM wa kujivua gamba.
Katika mpango huo ripoti hiyo inasema asilimia 41 walisema ni mpango wa kuwataka watu kujiuzulu kwenye uongozi wakati asilimia 29 walisema ni mpango wa kutaka kukisafisha chama.
Inaonyesha kuwa asilimia 15 ya waliohojiwa walielezea kujivua gamba kuwa ni mabadiliko ya uongozi kwa kuondoa viongozi wabovu na asilimia tano wakasema ni mpango wa kuondoa viongozi wote watuhumiwa wa ufisadi.
Asilimia mbili walisema ni mpango wa kukifanya chama hicho cha siasa kiwe na mfumo wa wazi na unaoeleweka wakati asilimia moja walisema ni suala la kujizuzulu, kutafuta viongozi wachapakazi na wenye tija. Kuna wanaouchukulia kuwa ni mkakati wa kisanii wa kuwadanganya wananchi.
Kwa ujumla, taarifa hiyo ilisema ni asilimia 45 tu ambao wana taarifa kuwa kuna Sekretarieti ya CCM ilijiuzulu na Mwenyekiti wake, Rais Kikwete amekwishateua wengine kushika nafasi hizo.
Kero kubwa nchiniAsilimia 56 walisema tatizo kubwa linalowakumba ni kupanda kwa bei ya vyakula, gharama za maisha na umaskini na asilimia 46 walisema njaa na tatizo kwenye kilimo.Tatizo la ufisadi nchini lilichukua nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 36, ukosefu wa ajira (31), tatizo la nyumba, barabara na umeme (27), elimu (23), afya (21), maji (16), uharibifu wa mazingira (12), taasisi za siasa (10), haki za binadamu, uhalifu (6) ubeberu na usafirishaji wa dawa za kulevya (3).
Katiba MpyaMiongoni mwa mambo ambayo yanatajwa kuwa ni vikwazo kwa Tanzania kupata Katiba Mpya ni rushwa (26), kukosekana kwa umoja (19), maslahi ya kisiasa (18), ufahamu mdogo (11) na kukosekana kwa msukumo wa kisiasa (9).
Hata hivyo, asilimia 78 walisema wanataka yawepo mabadiliko ya katiba nchini wakati asilimia 21 hawaoni umuhimu wake.Lakini asilimia 42 walisema wana uhakika kwamba mpango wa Katiba Mpya utafanikiwa.Lakini pia makosa ya Katiba iliyopo yalielezwa kuwa ni kupitwa na wakati, kuandikwa kwa Kiingereza zaidi kuliko Kiswahili, kukosekana kwa utawala bora, kutokuwepo kwa sheria za haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari.
![]() |
| Chuwit kama kuwadi kubwa lao (master pimp) |
![]() |
| Wanaposema siasa ni mchezo mchafu hawaongopi: Bango la Chuwit wakati wa kampeni za uchaguzi |