19 Jan 2013



THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIADIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone:


255-22-2114512,2116898

E-mail:
[email protected]

[email protected] Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,THE STATE HOUSE,P.O. BOX 9120,DAR ES SALAAM
.
Tanzania
.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa JakayaMrisho Kikwete anaanza ziara rasmi ya Kiserikali nchini Ufaransa leo, Jumamosi, Januari 19, 2013, kwa mwaliko wa Rais wa Ufaransa,Mheshimiwa Francois Hollande.Rais Kikwete na ujumbe wake aliondoka nchini usiku wa kuamkialeo, Jumamosi, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uswisi kuelekea Ulayakwa ajili ya ziara hiyo.Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja waNdege wa Charles DeGaul mjini Paris leo jioni, Rais Kikwete ambaye anafuatana na MamaSalma Kikwete atapokelewa rasmi katika Ufaransa kwa gwaride nakupokelewa na Waziri wa Misaada ya Maendeleo wa Ufaransa,Mheshimiwa Paschal Canfin.Kwa mujibu wa ratiba, kesho, Rais Kikwete atakutana na kufanyamazungumzo na Mama Frannie Leautiera mbaye ni Mtendaji Mkuu waMfuko Private Fund na baadaye atakutana na Mama Marie ChristineSaragosse, Mtendaji Mkuu wa
Redio France International (RFI).
Mkutano huo utafuatiwa na kikao kati ya Rais Kikwete na Jumuiya yaWatanzania wanaoishi nchini Ufaransa.Keshokutwa, Jumatatu, Rais Kikwete atakutana na kufanyamazungumzo na Mheshimiwa Francois Hollande, Rais wa Ufaransakwenye Kasri ya nchi hiyo ya Elysee Palace.Mazungumzo kati ya Rais Kikwete na Rais Hollande yatafuatiwana chakula cha mchana ambako Rais Kikwete atakaribishwa naWaziriwa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mheshimiwa Laurent Fabius. Baada yachakula hicho cha mchana, Rais Kikwete atakutana na kuzungumza na

Bwana Yves Louis Darricarere, Rais wa Kampuni ya Mafuta yaKimataifa ya Total.Mazungumzo hayo yatafuatiwa na mazungumzo mengine kati yaRais Kikwete na Kiongozi wa Madhehebu ya Ismailia Duniani H.H TheAga Khan na baada ya hapo, Rais Kikwete atakwenda Kasri laLuxemburg kukutana na kuzungumza na Rais wa Bunge la Seneti laUfaransa, Mheshimiwa Jean Pierre Bel.Usiku wa Jumatatu, RaisKikwete atakula chakula cha usiku naRais wa zamani wa Ufaransa, Mheshimiwa Valery Giscard d’Estaingambaye ni Mwenyekiti wa
Tanzania Wildlife Conservation Foundation
. Jumanne, Rais Kikwete atakuwa na siku nyingine yenye shughulinyingi ambako miongoni mwa mambo mengine atakutana na kufanyamazungumzo na mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zaokatikaUfaransa, na atakutana na Mheshimiwa Abdou Diouf, KatibuMkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Nchi Zinazongumza Lugha yaKifaransa na Rais wa zamani wa Senegal.Rais Kikwete pia atashiriki majadiliano kuhusu masuala yakimataifa yaliyoandaliwa na Taasisi ya Mahusiano ya Kimataifa yaUfaransa – Institute Francais Des Relations International (IFRI) naatakutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika laMaendeleo ya Kimataifa la Ufaransa (AFD).Rais Kikwete ataondoka nchini Ufaransa Jumatano, Januari 23,2013, kwenda Uswisi ambako atatembelea Makao Makuu ya Shirikishola Soka Duniani (FIFA) mjini Zurich na baadaye kwenda Davoskuhudhuria mkutano wa mwaka huu wa Shirika la Uchumi Duniani –
World Economic Forum (WEF).
Imetolewa na
:Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
.Dar es Salaam.19 Januari, 2013
Kuna mambo mawili  ya msingi yanayohusiana na taarifa hii:

 KWANZA, Ziara hii ya Rais Kikwete huko Ufaransa inazidi kuthibitisha kuwa Rais ameamua kuziba masikio kwa kelele kuwa ANASAFIRI MNO.Na kelele hizo si za chuki wala hazimaanishi 'Rais aote matende kwa kwa kutotoka nje ya Ikulu.' Ukweli ni kwamba safari hizi za mfululizoni mzigo mkubwa kwa nchi yetu ambayo inakabiliwa na jumla ya wastani ya deni la nje na ndani la takriban shilingi 40,000,000,000,000 (TRILIONI 40)! 

 PILI, ni fedheha kwa Rais Kikwete kupokelewa na Waziri wa Misaada ya Maendeleo wa Ufaransa.Hii inaonyesha kuwa ziara hiyo si muhimu kwa nchi hiyo,japo Rais Kikwete baadaye atakutana na Rais Hollande wa Ufaransa.Mkuu wa nchi anapozuru nchi nyingine shurti apokelewe na mwenyeji wake,yaani mkuu mwenzie wa nchi.

18 Jan 2013
















*Serikali yadaiwa kuchakachua bei halisi ya ujenzi
*Gharama za mradi huo zimeongezwa maradufu
*Zitto Kabwe adai kuwa viongozi wamehongwa 



KASHFA mpya ya ufisadi wa mamilioni ya Dola za Kimarekani zilizokusudiwa kutumika katika ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, imeanza kutokota serikalini, Rai limedokezwa.


Habari zilizolifikia gazeti hili kutoka vyanzo vyake mbalimbali serikalini, zimeeleza kuwa kufichuliwa kwa ufisadi huo, ni jitihada za kuwaunga mkono wananchi wa Mtwara, ambao kwa takribani wiki mbili sasa, wamekuwa katika mgogoro na Serikali wakishinikiza uvunaji wa gesi hiyo uwanufaishe wao kwanza, badala ya kuipeleka jijini Dar es Salaam, jambo ambalo Serikali imekuwa ikiliita ni usaliti na uhaini.



Maofisa kadhaa walioko Wizara ya Nishati na Madini waliozungumza na Rai kuhusiana na sakata hilo, wameeleza kuwa, baadhi ya viongozi wa Serikali, waliosimamia upatikanaji wa mkopo wa Dola za Kimarekani bilioni 1.2 kutoka Benki ya Exim ya China, na wale walioandaa gharama za ujenzi wa bomba hilo, walishtushwa na hatua ya wananchi wa Mtwara kuandamana kupinga mpango wa ujenzi huo, kutokana na hofu ya kubainika kwa ufisadi mkubwa ulioughubika mradi huo.



Wamesema kutokana na hofu hiyo, viongozi mbalimbali wanaoguswa na walio katika hatari ya kuguswa na sakata hilo, walianzisha uchunguzi, ili kubaini iwapo maandamano hayo yalikuwa na shinikizo la wanasiasa waliobaini kuwapo kwa ufisadi kwenye mradi huo.



Ili kuzima jitihada za aina yoyote za kuukwamisha, walilazimika kutumia maneno makali na yenye vitisho kwa waandamanaji na kuwatuhumu wanasiasa waliokuwa wakiunga mkono hatua ya wananchi wa Mtwara.



Kwa mujibu wa taarifa hizo, gharama zilizoongezwa katika ujenzi wa bomba hilo ni Dola za Kimarekani milioni 532, kiasi kinachoelezwa kuwa kinaweza kulingana na gharama halisi ya ujenzi kwa mradi mzima.



Baadhi ya wahandisi waliobobea katika fani hiyo, wamelieleza Rai kuwa gharama halisi ya ujenzi wa bomba hilo ambalo litatandazwa urefu wa kilomita 532 kutoka Mtwara hadi eneo la Kinyerezi, Dar es Salaam, ni Dola za Kimarekani milioni 638, hivyo kiasi kilichokopwa na Serikali kwa ajili ya kazi hiyo ni kikubwa zaidi.



Wamefafanua kuwa, gharama za kimataifa za ujenzi wa mabomba ya aina hiyo kwa kilomita moja, ni Dola za Kimarekani milioni 1.2 na kwamba kiasi hicho hutumika kwenye maeneo magumu kiujenzi yakiwemo maeneo ya milima na kweenye miamba.



Kiasi hicho kinazidi karibu maradufu ya kile kinachotumika hapa nchini, ambapo kilomita moja inajengwa kwa gharama ya Dola za Kimarekani milioni 2.2. Kwa gharama hiyo, kukamilika kwa ujenzi wa kilimota 532, kutagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani bilioni 1,170,400,000.



Mchanganuo wa gharama za bei za kimataifa zinazotumika sehemu mbalimbali kwa ujenzi wa njia za mabomba na gharama inayotumika Tanzania uliofanywa na watalaamu wa uhandisi waliozungumza na Rai, unaonyesha kuwa zaidi za Dola za Kimarekani milioni 500 zimeongezwa, jambo linaloashiria kuwapo kwa ufisadi katika mradi mzima.



Akizungumza na Rai kuhusu sakata hilo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, amesema analifahamu kwa undani suala hilo na kwamba kinachoitesa sasa Serikali, ni kubainika kwa ufisadi mwingine ilioufanya ambao utawaumiza Watanzania kwa kiwango kikubwa.



Zitto amesema anazo taarifa za kutolewa rushwa kubwa kwa baadhi ya viongozi wa Tanzania na wale wa China, ambao walihusika kuidhinisha na kupokea mkopo wa Dola za Kimarekani bilioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa bombahilo, madai ambayo ameanza kuyachunguza kutokana na historia ya China kuonyesha kuwa imekuwa ikijihusisha na vitendo vya rushwa katika kupata zabuni kubwa kubwa katika mataifa mbalimbali duniani.



“Kuna ufisadi wa kutisha katika mradi huu, ukiangalia fedha zilizotolewa, gharama halisi ya ujenzi wa bomba la gesi na gharama inayotumiwa kujenga hili la hapa nchini, utabaini kuwepo kwa ufisadi. Tunapaswa kujiuliza uhalali wa gharama hizi. 



“Ni kweli Serikali imekopa dola bilioni 1.2 kutoka Benki ya Exim ya China kwa ajili ya ujenzi wa bomba hilo. Gharama za kimataifa za ujenzi wa kilomita moja ni dola milioni 1.2, lakini sisi tunajenga kilomita moja kwa dola milioni 2.2, mara mbili ya gharama za kimataifa. 



“Kwanini? Watanzania wanapaswa kujiuliza hili, kwanini gharama hizi? Sasa kwa sababu ya hofu ya kugundulika kwa ufisadi huu, Serikali inapoona wananchi wanadai haki yao ya msingi, kwa sababu ya hofu ya kubainika kwa ufisadi, ilioufanya inahamanika kwa sababu madudu yake yatabainika.



“Taarifa nilizonazo zinaeleza kuwa kuna dola milioni 220 zilitumika kuhonga viongozi, ili mkopo upatikane na gharama za ujenzi ziwe juu. Sasa China inasifika kwa rushwa kwenye miradi mikubwa, kwa sababu hiyo tu, utaona kuna kila sababu ya suala hili kuchunguzwa vizuri. Wabunge wanapaswa kuhoji hili,” alisema Zitto.



Zitto ameeleza zaidi kuwa, mazingira ya utoaji wa mkopo huo yamejaa utata, kwa sababu Benki ya Exim haijautoa serikalini, bali imeelekeza fedha zote kwa kampuni iliyopewa zabuni ya ujenzi, hivyo Watanzania hawataambulia chochote katika mkopo huo.



Amesema maeneo mengine yenye utata katika utekelezaji wa mradi huo, ni namna mzabuni alivyopatikana bila kufuata taratibu za utoaji zabuni, na kwamba hata mkataba wa ujenzi uliosainiwa na Wizara ya Fedha na Shirika la Maendeleo ya Petrol (TPDC) kwa upande wa Tanzania na Benki ya Exim kwa upande wa China, umeghubikwa na usiri, ambapo kabla na baada ya kusainiwa, Bunge limekuwa likifichwa kufahamu chochote kilicho katika mkataba huo.



Akieleza kushangazwa na jinsi mkopo huo ulivyopatikana, amesema imekuwa kawaida kwa China inapotoa mkopo, kuweka sharti kwa mkopaji na kutoa kitu kitakachoinusha na kutoa mfano wa nchi ya Angola, ambayo ilipewa mkopo kwa sharti la kupatiwa visima vya gesi, hivyo ni lazima Serikali ya Tanzania imetoa sehemu ya maliasili zake kwa mkopo huo, ambazo amesisitiza kuwa ni lazima zitajwe ili Watanzania wafahamu.



Jitihada za Rai kumpata Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuhusu suala hilo, hazikuweza kufanikiwa, baada ya simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa kwa muda mrefu.



Kuibuka kwa madai ya kuwapo ufisadi katika mradi wa ujenzi wa bomba la gesi, kunazidi kuyapa nguvu madai ya wananchi wa Mtwara ya kutaka rasilimali hiyo isitumike vibaya, bali iwanufaishe wananchi, tofauti na ilivyopata kutokea katika maeneo ya madini ambako kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuwa madini yamekuwa yakiwanufaisha zaidi vionghozi wachache na wawekezaji badala ya wananchi.

CHANZO: Rai





IMG-20130118-00363 64950

IMG-20130118-00364 91725

IMG-20130118-00365 11a3a

IMG-20130118-00366 de3fa


IMG-20130118-00360 6853c

IMG-20130118-00361 9060f

IMG-20130118-00362 c1e74


Picha kwa hisani ya MJENGWA


17 Jan 2013


MIONGONI mwa matokeo ya kuyumba kwa uchumi wa Uingereza, ni mfumuko wa kampuni za mikopo ya muda mfupi ambayo hulipwa pindi mkopaji anapopata mshahara (payday loans).
Kushamiri kwa kampuni zinazotoa mikopo ya aina hiyo, kumechangiwa na ukweli kwamba taasisi nyingi zinazotoa mikopo ya ‘asili’ (traditional lenders), zimekuwa na masharti magumu ya kutoa mikopo kwa wateja wao.
Ingawa kampuni hizo za ‘payday loans’ zimekuwa kama mkombozi kwa wananchi wasioweza kupata mikopo kwingineko, viwango vyao vikubwa vya riba vimepelekea mjadala mkubwa huku baadhi ya taasisi za kutetea maslahi ya wateja zikiitaka Serikali kuongeza udhibiti wa taratibu za mikopo hiyo.
Kwa wastani, viwango vya riba vinavyotozwa na wakopeshaji hao ni kati ya asilimia 1,000 hadi 4,000. Mengi ya kampuni zinazotoa mikopo hiyo, hutoza riba kila siku, na matokeo yake ni kwamba mkopaji hujikuta akilazimika kukopa tena mara baada ya kumaliza kulipa deni la awali.
Kadhalika, wakopeshaji hao hufanya kila jitihada kuhakikisha kwamba mteja wao anaendelea kuwa ‘mtumwa’ wa kudumu wa mikopo yao ambapo humwandama kwa ofa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ‘likizo’ ya malipo ambayo kimsingi hukuza kiwango cha riba hata maradufu ya kiwango cha awali.
Lengo la makala haya si kuzungumzia kuhusu kuyumba kwa uchumi wa Uingereza, ‘payday loans’ au kampuni zinazotoa mikopo ya aina hiyo yanavyonufaika na riba kubwa wanazotoza wateja wao, bali habari niliyoisoma katika gazeti moja la huko nyumbani, zikisema kwamba Shirika la Fedha Duniani (IMF) linaridhishwa na mwenendo wa uchumi wa Tanzania, na kwamba nchi yetu inaweza kukopa zaidi.
Mara baada ya kusoma habari hiyo ‘nilitwiti’ katika mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa ‘hivi sasa IMF imegeuka kuwa kama kampuni ya kimataifa ya ‘payday loans.’
Niliandika hivyo kwa sababu ni mwendawazimu pekee anayeweza kudai kwamba mwenendo wa uchumi wetu ni mzuri. Haihitaji japo kozi ya saa chache ya uchumi kutambua kwamba licha ya Tanzania kuwa moja ya nchi masikini zaidi duniani, pia hali za maisha ya Watanzania zinazidi kuwa ngumu siku hadi siku.
Lakini kwa vile IMF ni ‘wahuni’ kama kampuni za ‘payday loan’ ya hapa Uingereza, ambayo kwao cha muhimu ni faida bila kujali mzigo wanaombebesha mkopaji, pasi aibu, shirika hilo linanishawishi nchi yetu kukopa zaidi, kutokana na msingi wa kwamba ‘tunakopesheka’ ingawa tuna mzigo wa deni la ndani linalofikia Sh trilioni 22.
Niwarejeshe nyuma kidogo. Nimeshaandika mara kadhaa katika makala zangu kadhaa katika matoleo yaliyopita kwamba wakati mkoloni alikuwa na ‘excuse’ isiyokubalika ya kutuibia raslimali zetu, hakuna hata Mtanzania mmoja mwenye sababu ya kuihujumu nchi yetu.
Katika mtizamo huo huo, wakati ninaelewa kwanini IMF haijali kabisa kuchambua kwa undani hali halisi ya uchumi wetu, kwa vile kimsingi sera za IMF haina tofauti na zile za mkoloni, nilikerwa mno na kauli za wasomi wawili wa Kitanzania; Profesa Delphin Rwegasira na Profesa Humphrey Moshi.
Wakati Profesa Rwegasira alidai kuwa kuridhishwa huko kwa IMF kuhusu uchumi wetu kunaonyesha kwamba taasisi hiyo ina imani na mwenendo wa uchumi wetu, lakini akatahadharisha kuwa tunaweza kuishia kuwa na madeni makubwa zaidi. Kwa upande wake, Profesa Moshi alidai kuwa hiyo ni hatua nzuri kwa nchi kama Tanzania kwani inatoa fursa zaidi kwa sera na uhuru wa kuchagua sera.
Ingawa ninawaheshimu wasomi hawa, na ninatambua kwamba wanatumia haki yao ya kitaaluma na kikatiba kutoa mtizamo wao, lakini licha ya mimi kuwa si msomi kama wao, ninashindwa kuwaelewa wanapozichukulia porojo hizo za IMF kama hatua ya msingi kwa nchi yetu.
Kauli za wasomi hao, hazitofautiani na zile tunazosikia mara kwa mara kutoka kwa baadhi ya viongozi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), na hasa Gavana, Profesa Benno Ndulu, na viongozi wetu serikalini, na hasa Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk William Mgimwa, ambazo huambatana na takwimu za kuleta matumaini huku zikikinzana kabisa na hali halisi ya maisha mtaani.
Binafsi, ninaamini kwamba matumizi bora ya elimu si tu kuzingatia kanuni (theories) zilizopo vitabuni, ambazo mara nyingi hupuuza hali halisi ya jamii zisizo za kimagharibi, bali kutafsiri kanuni hizo kwa kuzingatia hali halisi katika jamii husika.
Ndiyo. Fedha za mikopo kutoka IMF na taasisi nyingine za fedha na nchi wafadhili, zinachangia kwa kiasi kikubwa katika bajeti yetu na miradi mbalimbali ya maendeleo. Lakini kanuni nyepesi na isiyo ya kitaaluma ya uchumi wetu, ni kwamba sehemu ya fedha za mikopo hiyo ndizo hizo zilizoko Uswisi kwenye akaunti za mafisadi.
IFM wanafahamu bayana kwamba nchi yetu ina mabilioni ya Shilingi yaliyofichwa na mafisadi huko Uswisi, na jinsi fedha hizo zingeweza si tu kupunguza haja ya nchi yetu kuendelea kukopa, bali pia zingeweza kuchangia kupunguza deni la ndani la Serikali na nakisi kwenye bajeti yetu.
Kwanini IMF inapuuza ukweli kuhusu uchumi wetu uliowekwa rehani mikononi mwa wafadhili wa nje na mafisadi wa ndani? Jibu jepesi ni kama lile la kwanini kampuni za ‘payday loans’ za hapa Uingereza, zinaendelea kuwabebesha mzigo wa madeni yenye riba kubwa wateja wake, hali inayowafanya waendelee kuwa mateka kwa kukopa na kulipa ili waendelee kukopa zaidi. Kwa lugha nyingine, ni kuendelea kwa mzunguko katili wa umasikini (vicious circle of poverty).
Kimsingi, kauli ya IMF haina tofauti na ile iliyotolewa na Waziri Mgimwa kuhusu deni letu la ndani la Sh trilioni 22, ya wamba ‘bado tunakopesheka.’ Busara kidogo tu zinapaswa kubainisha kwamba suala si kuendelea kuwa na uwezo wa kukopesheka, bali uwezo wa kulipa madeni hayo na hatimaye kuondokana na utumwa kwa kuishi kwa matakwa ya wanaotukopesha.
Nihitimishe makala haya kwa kuwakumbusha watawala wetu kwamba pamoja na ukweli kuwa hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kujiendesha pasipo kukopa kutoka taasisi za ndani na nje ya nchi, deni la takriban Sh 500,000 (Sh trilioni 22 kugawanya kwa idadi ya sasa ya Watanzania-takriban milioni 45) analobeba kila Mtanzania, haliwezi kulipwa, achilia mbali kupunguzwa, kwa kukopa zaidi.
Njia pekee ni kutanguliza mbele maslahi ya taifa kwa kupambana na majambazi wanaohujumu uchumi wetu, kukubali kuishi kimasikini kwa maana ya matumizi ya Serikali kuendana na uwezo wetu, na pia kutohadaika na porojo za wakopeshaji kama IMF ambao kimsingi ustawi wao unatutegemea sisi kuendelea kuwa wateja wao.
Na kwa upande wa wasomi wetu, wito wangu kwao ni kujaribu kutafsiri yaliyoandikwa vitabuni kwa kuzingatia hali halisi ya nyanja mbalimbali katika Tanzania yetu. Uchumi wetu kwa mfano, ni zaidi ya takwimu, bali ni mamilioni ya Watanzania wasio na uhakika wa mlo ujao, raslimali zetu zinazotoroshwa kila kukicha, utashi wa kisiasa na kisera dhidi ya porojo za kibabaishaji katika kuikwamua nchi yetu kimaendeleo, na uelewa wa mfumo wa kinyonyaji unaotaka kuziona nchi masikini zikiendelea kuwa tegemezi daima.



.

.

.

.

.

.

.

.


15 Jan 2013



.

.

.

.

.

.

.


100 5309 e0e77


Kwa hisani za Millard Ayo na Mjengwa
.


Haya ndio matokeo ya kumkabidhi mtu mbabaishaji kuongoza nchi.Naam,namzungumzia Rais Jakaya Kikwete.Wengi wanaomfahamu vizuri wanatambua kwanini nchi yetu inazidi kupoteza mwelekeo.Majambazi waliojivika joho la uongozi wanazidi kufilisi nchi yetu, Na sasa kila Mtanzania amebebeshwa deni la takriban shilingi laki tano kila mmoja kutokana na zigo zito la misumari la deni la ndani la taifa la shilingi 22,000,000,000,000 (TRILIONI 22). Na hilo ni deni la NDANI TU.

Wakati tunakabiliwa na mzigo huo wa deni hilo kubwa,serikali ya Kikwete imelipa takriban SHILINGI MILIONI 100 kugharamia makazi ya Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt CHARLES TIZEBA (Ni muhimu kujikumbusha Waziri KAMILI wa Uchukuzi ni yule anayetajwa kama kuwa mfano wa viongozi safi wachache ndani ya CCM, Dkt Harrison Mwakyembe).

Uchunguzi wa gazeti la Kiingereza la Guardian umefukua uhuni huo unaotokea katika Hoteli ya Kitalii ya New Africa jijini Dar,ambapo gharama za makazi ya Dkt Tizeba zimeendelea kuchajiwa hata pale anapokuwa nje ya jiji la Dar.

Gharama za malazi katika hoteli hiyo zinaangukia katika makundi matatu: vyumba vya kawaida dola 160 kwa usiku mmoja; vyumba vya klabu dola 180 kwa usiku mmoja; na vyumba maalumu (suites) dola 300 kwa usiku mmoja.Dkt Tizeba anaishi kwenye chumba maalumu (suite) lakini hoteli hiyo imekubali kupunguza gharama hadi dola 250 kwa usiku mmoja.

Hadi kufikia Jumamosi iliyopita (Januari 12, 2013) Naibu Waziri huyo angekuwa ameishi hotelini hapo kwa sangalau siku 247,na hivyo kufanya gharama za malazi yake hotelini hapo kufikia dola 61,750 (sawa na SHILINGI MILIONI 98.8)

Hata hivyo jumla hiyo ni ya malazi na kifungua kinywa tu ( bed and breakfast), ikimaanisha kuwa gharama za jumla zinaweza kuwa kubwa zaidi ikijumlishwa na zile za mlo,ambapo mlo mmoja (buffet) unagaharimu angalau shilinhi 21,000.

Kadhalika,kwa vile Naibu Waziri huyo ana familia,gharama hizo zinaweza kuwa kubwa zaidi.Hivi karibuni Naibu Waziri Tizeba alitembelewa na wanawe wawili walioishi hotelini hapo kwa zaidi ya wiki kwa gharama ya dola 100 kwa kila usiku.

Alipotafutwa na gazeti hilo,Dkt Tizeba ambaye ni Mbunge wa jimbo la Buchosa kupitia CCM, alishauri suala hilolielekezwe kwa mamlaka zinazohusika na makazi ya mawaziri na viongozi wengine wa umma.

"Siwezi kujipangia makazi mie mwenyewe...kuna mamlaka zenye jukumu hilo,kwahiyo tafadhali ongea nao na upate tamko rasmi.Hata hivyo,vyanzo vya gazeti hilo vimeeleza kuwa gharama za makazi ya Naibu Waziri huyo hotelini hapo zinabebwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Hta hivyo,Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Paniel Lyimo alikataa kuzungumzia suala hilo,hususan haja ya kupunguza gharama kwa kumpatia Dkt Tizeba makazi ya kudumu badala ya kuishi hotelini na hivyo kuongeza gharama.

Katibu huyo Mkuu alimtaka mwandishi kumtumia ujumbe mfupi wa maneno (SMS), akidai maongezi kwenye simu hayakuwa sawia.Lakini masaa mawili baadaye,mwandishi alipokea ujumbe kutoka kwa mtu aliyedai kuwa ni Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo akisema:

"Kuhusu taarifa ulizokuwa ukisaka kutoka kwa Lyimo,Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, ningependa kukufahamisha kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri wa Uchukuzi ameshapangiwa nyumba kitambo sasa."

Hata hivyo kuna taarifa kuwa Dkt Tizeba amekataa kuhamia kwenye nyumba hiyo,ambayo awali ilikuwa ikitumiwa na mtangulizi wake, Athuman Mfutakamba. kwa madai kuwa "haiendani na hadhi yake."

Lakini alipotakliwa kutoa msimamo wake, Dkt Tizeba 'aliponda' tuhuma hizo akidai zinasambazwa na maadui zake.ambao walikuwa wakipambana na harakati za Wizara yake kuweka mambo sawa (kupambana na ufisadi).

Gazeti hilo limepata taarifa kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, naye aliishi hotelini hapo kwa angalau miezi miwili baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.

HII NDIO SERIKALI YA RAIS KIKWETE AMBAYO IAN DENI LA NDANI LA SHILINGI TRILIONI 22 NA DENI LA NJE (HADI KUFIKIA AGOSTI MWAKA JANA) LA DOLA BILIONI 10.35 (SHILINGI 16,050,000,000,000),YAANI ZAIDI YA SHILINGI TRILIONI 16.KWAHIYO KIMSINGI JUMLA YA DENI LA NDANI NA LA NJE NI TAKRIBAN SHILINGI TRILIONI 40 (40,000,000,000,000) AMBALO LINAMFANYA KILA MTANZANIA KUDAIWA TAKRIBAN SHILINGI MILIONI MOJA KILA MMOJA (NI WASTANI WA SHS 888,888,.89 )

LAKINI LICHA YA UZITO WA DENI HILO BADO SERIKALI YA KIKWETE HAIJALI KUMLIPIA NAIBU WAZIRI TAKRIBAN SHILINGI MILIONI 100 KWA MAKAZI YA HOTELINI (MNAZIKUMBUKA ZILE NYUMBA ZA MAWAZIRI PALE VICTORIA JIRANI NA KAMBI YA USALAMA WA TAIFA NA HOSPITALI YA KAIRUKI?)

SIJUI HALI YA NCHI YETU ITAKUWAJE HAPO 2015 KIKWETE ATAKAPOONDOKA MADARAKANI.ILA MOJA LILILO WAZI NI KUWA DENI HILI LA MATRILIONI YA SHILINGI LITAKUWA LIMEZALIANA KWA KASI PENGINE ZAIDI YA KASI YA KUZALIANA KWA MAFISADI HUKO NYUMBANI.





Mmoja amshangaa mwenzake kuwakamata machangudoa
*Asema anawakamata kwa sababu hana elimu ya madanguro
*Mwenzake ajibu, huyu ana miezi sita hapa, haya anayatoa wapi?

MAKAMANDA wawili wa polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam, wamekwaruzana. Makamanda hao, Charles Kenyela wa Mkoa wa Kinondoni na Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo, wamekwaruzana na kurushiana maneno yasiyofaa kuhusu namna ya utendaji kazi wa Jeshi la Polisi.


Kutofautiana huko kumeibuka baada ya wiki iliyopita, Kamanda Kenyela kufanya operesheni ya kuwakamata wanawake wanaofanya biashara ya ukahaba, maarufu kama machangudoa na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Baada ya Kamanda Kenyela kuendesha operesheni hiyo, Kamanda Kiondo wa Temeke, alinukuliwa na vyombo vya habari jana, akikosoa zoezi hilo na kusema hakuna sheria nchini inayozuia mwanamke kujiuza.

Katika maelezo yake, Kamanda Kiondo alisema, operesheni hiyo ilifanywa kwa kukurupuka na kwamba kamanda huyo hajasomea elimu ya jamii juu ya madanguro.

Kwa mujibu wa Kamanda Kiondo, kama Kamanda Kenyela angekuwa anaielewa vizuri elimu hiyo, kamwe asingedhubutu kuwakamata wanawake hao bali angewapatia elimu na ushauri dhidi ya maradhi wanayoweza kuambukizwa.

Pamoja na hayo, alihoji kuna umuhimu gani wa kuwakamata machangudoa wakati hakuna sheria inayomtaka awafikishe mahakamani badala yake anayetakiwa kushitakiwa ni mtu anayetoa nyumba ili itumike kama danguro.

Naye, Kamanda Kenyela alipozungumza na MTANZANIA jana juu ya kauli za kejeli zilizotolewa na mwenzake huyo, alisema amestushwa na taarifa ya Kamanda Kiondo kwa kuwa amemdhalilisha kupitia vyombo vya habari.

“Yaani mwandishi sipati picha kama Kamanda Kiondo ambaye hana miezi sita kwenye nafasi hiyo tangu ateuliwe, anaweza kunidhalilisha juu ya utendaji wangu wa kazi, kwanza inakuwaje azungumzie mambo ya Kinondoni wakati mimi nipo?

“Kama alijua nimekosea, alipaswa kunipigia simu kwanza tushauriane kabla ya kusema kwenye vyombo vya habari au angenisema kwa wakubwa wetu ambao wangeniita na kunishauri ili nisitishe operesheni hiyo, kama kweli ninakwenda kinyume.

“Amenidhalilisha sana na unajua ni vigumu kwa kamanda kama yule kutoka kwenye himaya yake na kuzungumzia himaya ya kamanda mwingine wakati mhusika yupo.

“Kibaya zaidi anasema eti mimi sina elimu ya jamii juu ya madanguro, lakini binafsi siwezi kuona vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani au usumbufu kwa raia wengine, halafu nikakaa kimya, sitaacha kuchukua hatua.

“Ninachoweza kumwambia Kamanda Kiondo ni kwamba, sina ugomvi naye na pia sitaki malumbano naye, kazi ya kudhibiti uhalifu haihitaji mpango mmoja lazima tutumie njia mbadala kuhakikisha tunatimiza majukumu yetu ya kulinda raia na mali zao, nafikiri suala hilo linazungumzika tuache litapata suluhisho,” alisema Kamanda Kenyela akionyesha kukerwa na kauli za Kamanda Kiondo.

Kova aingilia kati 
Kutokana na malumbano hayo, Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, aliliambia MTANZANIA kwa simu kwamba atawakutanisha makamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ili kupata ufumbuzi wa suala hilo.

“Ni kweli suala hili limenifikia na kwa kuwa kesho (leo) kuna kikao, basi litawekwa katika ajenda ili lipate kuondoa malumbano hayo.

“Lazima tuangalie sheria zinasemaje juu ya machangudoa, sasa tutajadiliana ili kupata msimamo wa kudhibiti biashara hiyo, kwani kuna matukio mengi ya namna hiyo yapo yanafanyika lakini kwa upande wetu polisi lazima tuwe na sheria ya kudhibiti vitendo hivyo.

“Kikao cha kesho (leo) kitaangalia sana sheria kuliko maoni ya watu, tutaangalia upande wa mahakama kama sheria zipo za kuwatia hatiani wahusika wa biashara hiyo, nakuhakikishia tofauti hizi za ma RPC wawili zitakwisha na wote tutapata msimamo wa pamoja.

“Si kwamba kikao cha kesho (leo) kimeitishwa kwa sababu ya mzozo huo wa ma RPC hao, hapana, kilipangwa tangu siku nyingi lakini tushukuru mzozo huu umeibuka wakati tunatarajia kukutana,” alisema Kamanda Kova.

Kamanda Kiondo alipozungumza na MTANZANIA kwa simu, alisema alitoa kauli hiyo baada ya kupigiwa simu na waandishi wa habari wakitaka atoe ushauri juu ya operesheni inayofanywa na Kamanda Kenyela.

“Nilichokifanya ni kutoa ushauri na uzoefu wangu nilioupata wakati nikiwa masomoni nchini Afrika Kusini, ambako Serikali ya nchi hiyo ilipambana kisheria na machangudoa lakini ikashindwa kwani hata soko liliongezeka.

“Hata huku kwangu eneo la Sokota kuna machangudoa na kila ninapojaribu kuwakamata, ndipo soko linapoongezeka. Hivyo hivyo na gongo, ukiikamata inapanda bei.

“Kwa hiyo, nilichokifanya mimi ni kutoa ushauri ili itolewe elimu kwa wanawake na wanaume ili wajue madhara wanayoweza kupata pindi wanapojihusisha na biashara hiyo.

“Sasa basi ninachosema hapa ni kwamba, nguvu ya Kenyela haitaleta mafanikio bali itaongeza soko, kwani ukiwakamata wahusika maana yake unawafanya waliobaki waongeze bei na pia ieleweke kwamba, wanaokamatwa ni machangudoa wa Kinondoni tu wala siyo Dar es Salaam nzima.

“Kwa hiyo, sina maana ya kutaka kumchafua Kamanda Kenyela, niliyasema kwa nia nzuri kabisa, sina tatizo naye, naomba anielewe hivyo,” alisema Kamanda Kiondo.

 CHANZO: Mtanzania



14 Jan 2013


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
 CHANZO: Millard Ayo

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.