27 Jul 2014


DSC01188
DSC01189
DSC01190
DSC01191
DSC01192
DSC01193
DSC01194
DSC01195
DSC01196
DSC01197
DSC01198
DSC01199
DSC01200
DSC01201
DSC01202
DSC01203
DSC01204
DSC01205
DSC01206
DSC01207
DSC01208
DSC01210
DSC01211
DSC01212


Spy central: The MI5 headquarters near Vauxhall Cross on the River Thames
Jengo la makao makuu ya Idara ya ushushushu ya Uingereza,jijini London
Kuna ukweli mmoja usiofichika wala kupingika kwamba watu wengi sana wanapenda kazi ya ushushushu, yaani Uafisa Usalama wa Taifa.Hiyo sio kwa Tanzania pekee bali sehemu nyingi duniani. Ukiingia mtandaoni utakutana na watu wengi wanaozungumzia taaluma ya intelijensia au/na wahusika katika hali ya kutamani kuifahamu taaluma hiyo nyeti  au kuwa mhusika.

Leo nitaanza mlolongo (series) wa makala kuhusu taaluma hiyo adimu. Hata hivyo ni vema nikatahadharisha mapema kwamba nitakachoandika ni kile tu kinachoruhusiwa kuandikwa hadharani. Kimsingi,taaluma ya ushushushu inatawaliwa na usiri,na mengi ya yanayohusiana na taaluma hayo yanabaki kuwa siri. Hata hivyo,kuna maelezo ambayo yapo wazi japo inahitaji uelewa wa aina flani kuchora mstari kati ya kipi ni siri na kipi ni ruksa kuwa hadharani.

Kwa tafsiri rahisi, ushushushu ni taaluma inayohusu ukusanyaji wa taarifa za kiusalama kwa njia za siri (clandestine methods). Japo kwa kiswahili ushushushu ni intelijensia, kiundani kuna tofauti kati ya ushushushu unaofanyika ndani ya nchi na unaofanyika nje ya nchi.Kwa hapa Uingereza, Idara ya ushushushu inayoshughulika na masuala ya ndani inajulikana kama MI5 na inayohusiska na ushushus nje ya nchi ni MI6.Kwa huko nyumbani, tofauti hizo zipo ndani ya muundo wa taasisi husika, kwa maana kwamba kuna taasisi moja tu lakini ndani yake kuna mgawanyo wa kimajukumu ya ndani na ya nje.

Kadhalika, japo mashushushu wamekuwa wakifahamika pia kama spies, ukweli ni kwamba spy ni shushushu anayefanya kazi nje ya nchi yake,kitu kinachojulikana kiusalama kama ujasusi au espionage kwa Kiingireza.

Japo mataifa mbalimbali yana miundo tofauti ya Idara zao za Usalama wa Taifa,lengo na kazi kuu ni ukusanyaji wa taarifa hizo.Kwa minajili ya makala hizi, nitazungumzia zaidi mazingira ya huko nyumbani Tanzania. Kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1996, Idara yetu ya Usalama wa Taifa ni idara ya serikali iliyo chini  ya Ofisi ya Rais,ambayo ina jukumu la kukusanya na kuchambua taarifa za usalama na kuziwasilisha 'mahala kunakohusika' katika namna ambayo Mkurugenzi Mkuu wa Idara hiyo ataona inafaa.

Kimsingi, mkuu'halisi' wa Idara hiyo ni Rais mwenyewe,ambaye kwa lugha ya kiusalama anafahamika kama 'sponsor.' Wakuu wa Idara za usalama popote pale duniani hufahamika kama spymaster.

Maeneo makuu ya kazi za Idara ya Usalama wa Taifa ni kukusanya na kuchambua habari za kiusalama zinazohusiana na ujasusi (espionage),uzandiki (subversion),uhujumu (sabotage) na ugaidi (terrorism). Lakini jukumu la Idara hiyo si kukusanya taarifa hizo na kuzichambua tu bali pia kuzuwia matukio hayo yanayofahamika kama matishio ya usalama wa taifa.

Ni kwa vile utendaji wa kazi wa Idara yoyote ile ya Usalama wa Taifa unaegemea katika usiri mkubwa ndio maana kwa 'mtaani' kuna hisia tofauti kuhusu umuhimu wa taasisi hiyo. Ukweli ni kwamba laiti umma ungefahamu nini kinafanywa (au kinapaswa kufanywa) na Idara hiyo basi kwa hakika ingethaminiwa zaidi ya kuogopwa tu. Ni muhimu hapa nisisitize kuwa ninazungumzia 'hali mwafaka' yaani kwa Kiingereza ideal situation. Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi miongoni mwa wananchi wakiishutumu Idara yetu ya Usalama wa Taifa kuwa imeleemea mno kwenye siasa hasa kuibeba CCM,imezembea mno kiasi cha kuruhusu ufisadi kushamiri, na imekuwa ikilaumiwa pia kutokana na matukio mbalimbali yanayotishia usalama wa Taifa kama vile ugaidi.

Wanaotoa lawama hizo wapo sahihi kwa kiasi flani,kwani  kushamiri kwa maovu katika jamii sambamba na mwendelezo wa matukio yanayotishia usalama wa taifa ni viashiria kuwa Idara ya Usalama ya nchi husika ina mapungufu kiutendaji.

Hata hivyo,ni muhimu kutambua kanuni moja muhimu ya ufanisi au kushindwa kimajukumu kwa Idara ya Usalama wa Taifa popote pale.Ni kwamba wakati Idara husika inapaswa kuwa macho katika kila sekunde kuzuwia matendo ya kidhalimu, wanaopanga kufanya matendo hayo wanahitaji mara moja tu kufanikisha azma yao.Mfano halisi ni kwenye matukio ya ugaidi. Wakati gaidi anahitaji fursa moja tu kufanikisha tukio la kigaidi, Idara ya Usalama inahitaji kila fursa- kila sekunde,dakika,saa,siku,wiki,mwezi,mwaka-kuhakikisha gaidi hafanikiwi.

Kadhalika, wakati inaweza kuwa rahisi kuilaumu Idara ya Usalama wa Taifa inaposhindwa kuzuwia tukio flani, kwa mfano shambulio la kigaidi nchini Kenya, kiuhalisi suala zima la ukusanyaji wa taarifa za kiusalama ni gumu mno. Hebu pata picha: unaletewa tetesi kuwa kuna mtu anataka kulipua bomu kanisa au msikiti. Mara nyingi tetesi hizo huwa hazibainishi jinsia ya mtu huyo,wajihi wake,ni mwenyeji au mgeni na vitu vingine muhimu vya kuweza kumtambua japo kwa ugumu. 

Kutokana na ugumu wa zoezi la kukusanya taarifa za kiusalama,ndio maana wahusika-mashushushu/maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa-wanapaswa kuwa watu wenye akili isiyo ya kawaida, au angalau wenye uwezo mkubwa wa kutumia akili.Neno lenyewe intelijensia linahusiana na matumizi ya akili.Lakini si akili tu, bali pia maafisa usalama wa taifa hupaswa kujifunza na kuendeleza hisia ya sita (6th sense). Mwanadamu wa kawaida ana hisia 5: HARUFU  kwa kutumia pua; LADHA kwa kutumiamdomo/ulimi, KUGUSWA (touch) kwa kutumia ngozi, KUONA kwa kutumia macho, KUSIKIA kwa kutumia masikio. Lakini kwa mashushushu wanapaswa kuwa na hisia ya ziada ya kutambua kitu zaidi ya kutumia hisia hizo 5 kuu. Si kazi rahisi hata kidogo.

Basi kwa leo niishie hapa.Nitaendelea na mfululizo wa makala hizi angalau kila wiki. Usikose kutembea blogu hii kupata habari na makala zaidi kuhusu taaluma hii nyeti ya ushushushu kwa kubonyeza hapo juu ya blogu kwenye seksheni ya INTELIJENSIA 



Pengine umeamua kufuta SMS baada ya kuona SMS Inbox yako inajaa au pengine umefuta SMS kwa bahati mbaya. Katika mazingira ya kawaida, ukisahfuta SMS ndio 'imetoka hiyo.' Lakini kimsingi waweza kuzirejesha kwenye inbox japo kitu cha muhimu kabisa na muda. Uwezekano wa SMS ulizozifuta kurejea inbox kunategemea sana uharaka: kadri unavopokea SMS mpya au updates za apps zako ndivyo fursa ya kuzirejesha inavyozidi kuwa ndogo.

Kuna nyenzo kadhaa za PC au Mac za kuweza kukuongoza katika zoezi la kurejesha SMS zako kwenye simu yako.Nyingi ya nyenzo hizo ni za bure, na hata zinazohitaji malipo,zinakupa fursa ya majaribio kabla ya kununua (free trial). Aina gani ya nyenzo uitumie,yategemea mapendezeo yako,lakini zote zafanya kazi moja ku-scan memory ya simu yako,kutambua na kuokoa SMS zilizofutwa. Zitakuongoza katika hatua nne muhimu za zoezi hili: kuunganisha, ku-scan, ku-review na kuziokoa (recover).

Baadhi ya zana za PC au Mac zinazoweza kukusaidia ni pamoja na Coolmuster Android SMS+Contacts Recovery, Wondershare Dr Fone for Android (hii inahitaji simu yako iwe rooted) na Android Data Recovery

Hatua zifuatazo zinaweza kuwa tofauti kutegemea na zana ya PC/Mac utakayoamua kutumia hapa imetumika Wondershare Dr Fone kwa minajili ya maelezo kwa picha).

1. Download moja ya nyenzo nilizotaja hapo juu kwenye PC/Mac yako,kisha iwashe (launch)
2. Unganisha simu yako na PC/Mac kwa kutumia waya wa USB

drfone android sc01
3. Wezesha 'USB Debugging' katika simu yako kwa kwenda kwenye 'Developer Options' katika 'Setting.' Vinginevyo, waweza kwenda kwenye 'About Phone' kisha 'Build Number,' piga eneo hilo na kidole chako mfululizo (tap repeatedly) na hatimaye utapelekwa kwenye 'Developer Options.' Kutoka hapo,nenda kwenye 'USB Debugging' (au Android Debugging kutegemea aina ya simu yako) kisha tiki kiboksi husika.
drfone android sc02
4. Fuata maelekezo kama yanavyoonyeshwa katika zana unayotumia kwenye PC/Mac yako
drfone android sc05
5. Ukishamaliza, sasa utaweza kuona data zilizopo kwenye memory ya simu yako, na SMS ulizofuta kwa bahati mbaya au makusudi-kutegemea kama hakuna SMS mpya au updates za apps,maana kitu chochote kipya kwenye memory kitaondoa uwezekano wa kuokoa SMS ulizofuta.
drfone android sc09

6. Tafuta folder ya SMS,chagua SMS unayotaka/unazotaka kuzirejesha inbox,na aidha tumia option ya 'Recover' kwenye PC/Mac yako au 'save' kwenye kompyuta yako.

Natumaini makala hii itakuwa na msaada na manufaa kwako. Usikose kufuatilia makali nyinginezo za teknolojia katika blogu hii.Bonyeza TEKNOLOJIA hapo juu na utapelekwa moja kwa moja katika makala hizo.



Je wafahamu kwamba unaweza ku-print document kutoka katika simu yako ya Android kwenda kwenye printer? Makala hii inakuelekeza jinsi ya kufanya hivyo.

Baadhi ya simu za kisasa zaidi kwa mfano Samsung Galaxy S5 tayari zina app hiyo, na hakuna haja ya ku-download upya.

androidpit cloud print one

Hatua ya kwanza ni ku-download Google Cloud Print  kisha 'add new printer'

androidpit cloud print two

Baada ya kuchagua 'add new printer' utapalekwa kwenye ukurasa wa Google wa Cloud Print, au kwenye akaunti yako ya Google iwapo hujasaini.

androidpit cloud print three

Japo ukurasa wa Cloud Print haupo bayana sana kimatumizi, zoezi la ku-'set up' si gumu. Fata maelekezo kutoka kwa printer yako,iwe ni offline model au Cloud ready model.
androidpit cloud print four

Sasa nenda kwenye faili unalotaka ku-print kutoka katika simu yako, na utaona chaguo la kulichapisha.

Iwapo unahitaji ku-print SMS,njia nyepesi ni kutumia app iitwayo SMS Backup& Restore. App hii ina-backup SMSzako kwenye simu yako,email au huduma za 'cloud' kama vile Dropbox na Google Drive. Ukisha-backup,nenda mahala ulipohifadhi SMS hizo,kisha chagua 'print'

androidpit cloud print five

CHANZO: Andoidpit
Natumaini makala hii itakuwa na msaada na manufaa kwako pindi utapohitaji kuchapisha dokumenti au SMS zako. Usikose makala nyingine za teknolojia katika blogu hii,ambazo utazipata kirahisi kwa kubonyeza hapo juu kwenye blogu palipoandikwa TEKNOLOJIA


26 Jul 2014




 Mara ngapi unakutana na tweet, au post kwenye Facebook, au picha Instagram ikiambatana na maneno 'I am happy'? Nina hakika ni takriban kila siku. Si dhambi kutamka hadharani kuwa una furaha, lakini uzoefu waonyesha kuwa wenye furaha za dhati wala hawahitaji kuishawishi dunia kuwa wana furaha: ukiwa na furaha ya kweli itaonekana tu bila hata kuitangaza.

Hebu tuangalie tabia 20  za watu wenye furaha ya dhati lakini wala hawana muda wa kujitangaza kuwa wana furaha, kwa vile furaha hujionyesha nyenyewe pasi haja ya matangazo.

1.  Hawana muda na drama za watu wengine: Kamwe usianzishe drama, na kamwe usiruhusu drama za watu wengine zikuhusu. Wengi wa watu wenye furaha hawajali nini kinachosemwa dhidi yao na watu 'wasio muhimu' kwao. Kwa hakika, watu wenye furaha huwashukuru wanaowasema vibaya kwani ni fundisho kwao kuhusu wasivyostahili kuwa ,yaani kutostahili kutokuwa na furaha.

2. Hupendelea kutoa/kusaidia kila wanapoweza: Nadhani ushaskia usemi 'kutoa ni moyo si utajiri. Watu wenye furaha ni wepesi kutoa/kusaidia, lengo kuu likiwa kusambaza furaha waliyonayo.

3. Wanathamini mahusiano yao muhimu: Mara nyingi watu wenye furaha wana marafiki wengi kwa sababu wanathamini marafiki, na marafiki hao in return wanatambua kuthaminiwa kwa urafiki wao.Hata hivyo, umuhimu wa marafiki hao hutegemea mchango walionao kwa furaha ya wenye furaha hao.Ni vema kuepuka watu watakapa mawazo fyongo.

4. Wanatenga muda kwa ajili ya kujipenda wenyewe pia: huwezi kupenda wengine wakati hujipendi mwenyewe. Ushakskia msemo 'charity begins at home.' Na Maandiko Matakatifu yanausia kuwa huwezi kumpenda Mungu usiyemuona ilhali huwapendi wanadamu unaowaona. Kadhalika,huwezi kuwapenda wengine ilhali wajichukia mwenyewe.Tenga muda ujipende.And by the way, kama mwenyewe hujipendi nani atakuwa na muda wa kukupenda?

5. Huthamini ufanisi kuliko umaarufu: Kamwe usi-confuse ufanisi na umaarufu.Kuwa maarufu kwamaanisha unapendwa kwa kipindi flani tu,lakini kuwa na ufanisi kunamaanisha unaleta tofauti chanya katika maisha ya wengine, na kuleta tofauti chanya katika maisha ya wengine kunamfanya mtu kuwa na furaha zaidi kwani inatambulisha umhimu wake kwa wengine.

6. Wanasema 'hapana' pale inapobidi: kuna msemo wa Kiswahili kwamba mkono hujikuna pale unapofiki.Huwezi kutaka kumridhisha mtu kwa kujiumiza mwenyewe. Na ni vema kusema 'hapana' ya dhati kuliko 'ndio' ya uongo. Kumbuka,kuwa mkweli ni kiungo muhimu cha kukufanya uwe mwenye furaha.

7. Wanajua kushukuru/kuthamini: Shukrani ni mfalme wa furaha, wanasema Waingereza (gratitude is the king of happiness).Watu wenye shukrani huwa na furaha maishani kwani ni nadra kwao kuwa na kinyongo au hasira. Shukrani ninayoonglea hapa ni pamoja na kuridhika na yale tuliyojaaliwa au tulofanikiwa kuwa nayo. Kwa mfano rahisi kabisa ni kumshukuru Mungu kwa kuamka ukiwa hai.

8. Hujenga matumaini: Watu wenye furaha huyaangalia maisha kwa mtizamo chanya. Kisaikolojia,ukiliangalia jambo kwa mtizamo hasi waweza kufanya matokeo ya jambo hilo kuwa hasi pia.Kumbuka kwamba mtizamo wetu ni sehemu muhimu ya kinachotusukuma au kutuzuwia kufanya/kutofanya vitu katika maisha yetu.

9. Hawajihusishi na kila fanikio au anguko: Watu wenye furaha hawachukulii kila anguko kuwa ndo mwisho wa kila kitu na kamwe hawavimbishwi vichwa na mafanikio. Hawaruhusu anguko (failure) kuwakaa moyoni na hawaruhusu mafanikio/sifa kuwalevya kichwani.

10. Hujenga mikakati ya kukabiliana na nyakati ngumu: Sote twatambua kuwa si kila leo ni kama jana, na si kila kesho ni kama juzi. Siku huwa tofauti,na ndo maana leo kuna mvua kesho kuna jua kali. Cha muhimu ni kuwa na mikakati madhubuti ya kukabiliana na matatizo.Na moja ya njia nzuri ni kujifunza kutoka kwa wengine.Twaweza kujifunza kwa kujali experiences za wengine ma kusoma pia.

11. Huchukulia kukataliwa kama kinga dhidi ya mabaya: Kuna namna njema ya kudili na kukataliwa- kuangalia kukataliwa kama kinga ya kukuepusha na jambo bayana. Sio kila kukataliwa kunamaanisha wewe si bora,wakati mwingine kunamaanisha kwamba alokukataa ameshindwa kutambua jinsi gani ulivyo bora.Ukikataliwa, amini kwamba kuna jema zaidi lipo njiani kwa ajili yako.

12. Wanaweka mkazo katika wakati uliopo: Kuendelea kunung'unika kuhusu mabaya yaliyopita hakusaidii kubadili hali ilivyo sasa. Cha muhimu ni kujifunza kutoka kwa mabaya hayo na kujitahidi kuhakikisha kuwa hakujitokezi tena. Kwa kujifunza kutokana na mabaya yaliyopita,watu wenye furaha wanatengeneza mazingira bora ya muda uliopo na kuweka 'bima' kwa ajili ya wakati ujao. 

13. Wanawekeza nguvu na muda kwa mambo ya msingi: Ukipanda upupu utavuna upupu. Mawazo chanya huzaa matokeo chanya, mawazo hasi huzaa matokeo hasi.Hilo halina ubishi. Kesho ni matokeo ya bidii za leo, na kwa kuwekeza nguvu na muda kwa mambo bora sasa, kehso ina uhakika wa kuvuna matokeo bora ya jitihada hizo za leo.

14. Wanaji-commit katika vipaumbele vyao: Ushaskia msemo'mshika mawili moja humponyoka.' Huwezi kuchanganya shule na mapenzi na ukafainikiwa katika vyote viwili.Lakini ili uweze kuwa na mafanikio ni muhimu kutambnua vipaumbele vyako, na si kutambua tu bali pia kufahamu mbinu za kuvifikia. Na ukishavitambua na kufahamu namna ya kuvifikia,yalazimu kuwekeza mtaji wa kutosha (sio lazima fedha bali nguvu, akili na muda) kuhakikisha unavifikia.

15. Wanaangalia kutopendezwa kama sehemu ya kuboresha uwezo wao: Kuna nyakati utafanya hili lakini huotfanikiwa. Lakini badala ya kubaki na hasira au manung'uniko ni vema kutumia fursa hiyo kujiuliza kipi kilikwenda mrama hadi ukashindwa kufanikiwa.Na kwa kufanya hivyo,unatengeneza mazingira mazuri ya kupata matokeo bora kwa kitu kilekile kilichoshindikana hapo awali.

16. Wanajali afya zao: Mwili wenye afya ni kama koti la akili yenye afya: Pasipo afya bora ni vigumu mno kuwa na furaha.Na katika hali ya kawaida tu, ukiwa unaumwa na kichwa, huwezi kuwa na furaha. Watu wenye furaha huwekeza vya kutosha katika kula vizuri,kufanya mzoezi,kuepusha vitu vinavyoweza kuathiri afya zao na pia kujali mapumziko.

17. Hutumia fedha kupata uzoefu badala ya vitu wasivyohitaji: Watu wenye furaha wapo makini katika matumizi yao, hasa kuepuka manunuzi ya vitu wasivohitaji na badala yake kufanya manunuzi ya vitu muhimu kwa maisha yao. Kuna kitu kinaitwa manunuzi ya uzoefu (experiential purchase),yaani kununua uzoefu, kwa mfano kutumia fedha kwenda likizo ya kujifunza kitu flani kinachoweza kukubailishia maisha yako, au kutumia fedha kujiunga na kozi flani itakayokuongezea ujuzi, na vitu kama hivyo.

18. Wanathamini furaha japo kidogo: Ili uweze kuwa na furaha kubwa shurti uweze kuthamini furaha ndogo,kwani hata wahenga walisema haba na haba hujaza kibaba.Kidogo unachopata katika dakika moja,kitakuwa kingi kikipatikana katika saa nzima,na kingi zaidi katika siku,na kwa mwezi,mwaka au miaka kitakuwa kingi kabisa. Furaha ni ku-enjoy vitu vidogo wakati tunafukuzia vitu vikubwa.

19. Wanatambua hali ya vitu kutodumu milele: Ni hivi, kwa vile kitu kizuri hakikudumu, haimaanishi kuwa kilikuwa kibaya. Kila kitu kina muda na wakati wake.

20. Huishi maisha wanayotaka kuishi: Tatizo la watu wengi wasio na furaha ni kuhangaika kuishi maisha ya wengine.Hakuna ubaya katika kutamani jinsi flani anavyoishi lakini ni vema kutambua wewe sio yeye, na kinachompa furaha yeye si lazima kukupe furaha wewe pia.Ndege wanaweza kuruka angani, na pengine nawe ungependa kuwa na uwezo huo,lakini wewe si ndege. Wanachofokiria watu wengine kuhusu wewe,hususan usiowajua- hakijalishili. cha muhimu ni ndoto zako,malengo yako na matarajio yako. Jitahidi kuzungukwa na watu ambao sio wanaotaka uwe wao wanavyotaka bali wanaojali na kuthamini wewe unavyota kuwa au ulivyo.Tengenezeza marafiki wa kweli na dumisha mawasiliano nao. Na la muhimu kabisa ni kutambua kwamba furaha ni chaguo lako mwenyewe, kama ilivyo kwa kutokuwa na furaha.





DSC01171
DSC01162
DSC01163
DSC01175
DSC01176
DSC01164
DSC01165
DSC01167
DSC01168
DSC01169
DSC01170

DSC01173
DSC01174
DSC01179
DSC01180
DSC01181
DSC01182

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.