19 Nov 2008

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeendelea kusisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinahusika na wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

Hayo yalibainishwa juzi na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, alipohutubia wananchi wa Manispaa ya Iringa, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mwembe Togwa.

Alisema CCM inahusika na wizi wa fedha hizo, kwani chama hicho ndicho kilichotoa maelekezo kwa makampuni yanayotuhumiwa kuiba fedha hizo.

Alisema CCM ilitumia makampuni hewa yaliyoanzishwa kughushi na kujipatia fedha hizo kwa ajili ya kugharamia kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, uliomwingiza Rais Jakaya Kikwete madarakani kwa ushindi wa asimilia 80.

Akitoa mfano Zitto alisema, kutokana na rekodi za kibenki za Benki Kuu ya Tanzania (BoT), CHADEMA ilibaini CCM iliitumia kampuni hewa ya Deep Green Finance, kuchota sh bilioni 10.4, katika kipindi cha miezi minne kati ya Agosti mosi na Desemba 10 mwaka 2005, na kisha kampuni hiyo kutoweka katika faili la Msajili wa makampuni nchini (BRELA).

Alisema katika kipindi hicho CCM pia iliitumia Kampuni ya Tangold Ltd ambayo haikuwa imesajiliwa kisheria, kujichotea kiasi kingine cha sh bilioni 9 kwa madhumuni hayo hayo ya kugharamia kampeni zake.

Aidha, alisema baadhi ya viongozi wa CCM wana uhusiano wa moja kwa moja na Kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd, ambayo ni moja ya kampuni kadhaa zinazodaiwa kuhusika na wizi huo, na kujipatia fedha kwa ajili ya kampeni, lakini vigogo wa CCM waliohusika na wizi huo hawajafikishwa mahakamani.

Alisema, CCM ilimtumia pia mfanyabiashara mmoja maarufu mwenye asili ya Kiasia (jina tunalo) kujipatia kiasi kingine cha fedha, na licha ya mfanyabiashara huyo kurejesha fedha alizochukua bado alifikishwa mahakamani kwa sababu ya kukataa kurejesha kiasi kingine cha fedha.

Alisema mfanyabiashara huyo aliikatalia serikali ya CCM, kurejesha sehemu ya fedha alizochukua kwa sababu kiasi hicho cha fedha ndicho alichokitumia kuwanunulia viongozi wa CCM magari aina ya Mahandra.

“Kama CCM inabisha kwamba haikufadhiliwa wala kununuliwa magari na mtuhumiwa huyo wa EPA, itoe vielelezo vyote vinavyothibitisha kwamba walinunua wenyewe magari hayo. Itoe risiti zote za usajili wa ....na iseme ilitumia fedha kiasi gani wakati wa kampeni. Iseme ilizipata wapi fedha hizo,” alisema Zitto huku akishangiliwa.

Alisema Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati, hajui chochote kuhusiana na jinsi chama chake kilivyopata fedha za kampeni ndiyo maana amekuwa akitetea.

Alisema Chiligati hajui kwa sababu kampeni za CCM wakati wa uchaguzi mkuu 2005, hazikuratibiwa na viongozi wa makao makuu ya chama hicho, bali ziliratibiwa na kundi maarufu la wanamtandao lililokuwa mstari wa mbele kumuunga mkono Rais Kikwete, tangu katika hatua za awali za uteuzi wa mgombea wa chama hicho.

Alisema kwa mara ya kwanza, sakata la wizi wa fedha za EPA, liliibuliwa bungeni na Mbunge wa Karatu, Dk. Willbrod Slaa, lakini wabunge na viongozi wa CCM walisema Slaa alitumia nyaraka za kughushi na hoja yake ilikuwa ya uongo.

Aliendelea kufafanua kwamba, sakata hilo lilipozidi serikali ililazimika kutumia kampuni kufanya ukaguzi ambayo ilithibitisha kwamba ilikuwa ni kweli.

Alisema suluhisho la msingi la kushughulikia kwa haki watuhumiwa wote wa EPA na kuhakikisha kwamba wizi huo hautokei tena, ni kwa serikali kuanzisha Mahakama Maalumu ‘Tribunal’ itakayohusisha wanasheria na majaji wastaafu wanaoheshimika na kuaminika nchini pamoja na wataalamu wazoefu wa masuala ya fedha, kwa ajili ya kushughulikia tuhuma zote za EPA.

Alisema bilioni 133 zilizoibwa ni fedha za umma na wala wananchi wasikubali kudanganywa kwamba fedha hizo si za serikali.

Katika mkutano huo, aliyekuwa kada maarufu wa Chama cha Wananchi CUF katika manispaa hiyo, Mlaki Mdemu, alitangaza kujiunga na CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama na Zitto.

Wananchi waliohudhuria mkutano huo, waliichangia CHADEMA, takriban sh 300,000 na kukitaka chama hicho kiende kwenye Jimbo la Mbeya Vijijini, ambalo liko wazi kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wake, Richard Nyaulawa, kilichotokea hivi karibuni.

Hata hivyo, Zitto aliwaambia wananchi hao kwamba CHADEMA inakusudia kusimamisha mgombea katika jimbo hilo, lakini kwa sasa haiwezi kufanya lolote, kwa kuwa bado inaomboleza msiba huo.

IWAPO MADAI HAYA YA CHADEMA YANA UKWELI (AND CIRCUMSTANTIAL EVEDIENCE SEEMS TO BACK THEM) BASI HUENDA HATA KESI ZINAZOENDELEA MAHAKAMANI NI CHANGA LA MACHO TU.CCM NEEDS TO COME CLEAN ON THIS.

UONGOZI wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) umekifunga chuo hicho kwa muda usiojulikana kutokana na mgomo wa wanafunzi.

Uongozi wa chuo hicho umefikia uamuzi huo, baada ya wanafunzi katika chuo hicho kufanya mgomo kuishinikiza serikali kuwarudisha vyuoni wanafunzi waliofungiwa.

Kabla ya kufungwa kwa chuo hicho jana, bodi ya chuo hicho ilifanya kikao, ili kujua wachukue uamuzi gani.

Awali, akizungumza na Tanzania Daima jana chuoni hapo, Rais wa DIT, Cleophace Maharangata, alisema mgomo wao bado unaendelea lakini bodi ya chuo inafanya kikao kuamua kama chuo kifungwe ama la.

“Sisi tunasubiri tamko baada ya kikao…uamuzi wowote utakaotolewa sisi tupo tayari,” alisema.

Naye mwalimu wa chuo hicho ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini alisema mgomo huo upo kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza, huku wanafunzi wa astashahada (diploma) wakiendelea na masomo kama kawaida.

Awali Rais wa wanafunzi hao, alisema mgomo huo ulianza rasmi juzi baada ya wanafunzi kutoingia madarasani huku wakiwa wameshika mabango yaliyobeba ujumbe mbalimbali.

Kufungwa kwa chuo hicho kunafanya idadi ya vyuo vilivyofungwa kufikia saba. Vyuo vingine ambavyo vimeshafungwa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), Chuo Kikuu cha Elimu Mkwawa (MUCE), Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Moshi Ushirika.

18 Nov 2008

Picha hii inayoonyesha adha ya usafiri wa wanafunzi Dar (haihusiani na habari ifuatayo) kwa hisani ya Zenjidar
Wakati Gazeti la Serikali HABARI LEO linaripoti  

WALIMU kote nchini jana walianza mgomo usio na kikomo wa kuishinikiza serikali kuwalipa madai yao ya zaidi ya Sh16 bilioni, katika siku ambayo ilijaa matukio mbalimbali, yakiwemo ya kuchapwa viboko kwa walimu waliokataa kugoma, jitihada za serikali kukwamisha mgomo, walimu kuripoti kazini na kuanza kupiga soga na wengine kuanza kulipwa madai yao.

Waandishi wetu kutoka mikoa mbalimbali wanaripoti kuwa mgomo huo, uliotakiwa kuanza Oktoba 15 lakini ukakwamishwa, ulifanikiwa kwa asilimia 70 ikiwa ni pamoja na baadhi ya wanafunzi kushindwa kuanza mitihani ya kumaliza mwaka, lakini katika baadhi ya shule walimu walifundisha kama kawaida.

Katika ufuatiliaji uliofanywa na Mwananchi katika sehemu kadhaa, walimu ama hawakwenda kabisa kazini ama walienda na kufanya vikao, vilivyoonekana kuwa vya kupoteza muda. Walimu wakuu, wakurugenzi wa halmashauri na wakuu wa wilaya wengi walidai kuwa hali ilikuwa shwari kwenye maeneo yao, lakini waandishi wetu walipoenda kwenye shule walikuta migomo ikiendelea kwa mikutano hiyo ya soga maofisini, huku wengine wakipata kinywaji kwenye baa jirani.

Mgomo huo ni matokeo ya serikali kushindwa kuwatimizia walimu madai yao nane tangu walipotangaza mgomo na kutoa siku 60 kwa serikali kuhakikisha inatatua matatizo hayo. Madai hayo ni pamoja na malimbikizo ya Sh6.6 bilioni, masomo (Sh1.01 bilioni), likizo (Sh1.07 bilioni), matibabu (589.9 milioni), posho za kujikimu (Sh565.8 milioni) na mirathi (72.9 milioni), kwa mujibu wa serikali.

Pia walimu wanadai kupandishwa daraja na kuundwa kwa baraza la maridhiano.

Serikali imekuwa ikidai kila mara kuwa inaendelea na zoezi la uhakiki na kuwataka walimu kuvuta subira, lakini baada ya Mahakama ya Rufaa kubatilisha amri ya muda ya kuzuia mgomo, kasi ya kushughulikia madai hayo ilionekana kuongezeka na jana baadhi ya walimu walianza kulipwa madai yao, huku Chama cha Walimu (CWT) kikisitiza kuwa mgomo utaisha baada ya walimu kulipwa senti ya mwisho.

Mwandishi wetu, Shija Felician anaripoti kutoka Kahama, Shinyanga kuwa walimu waliotii uamuzi wa kugoma, jana walitembeza viboko kwa wenzao walioingia darasani kufundisha.

Katibu wa CWT Kahama, Said Mselem alisema asilimia 70 ya walimu wote walioko wilayani hapa waligoma, lakini wale wachache ambao waliandikisha majina kuonyesha wamehudhuria kazini, walijikuta kwenye hali ngumu baada ya kuondolewa madarasani kwa viboko na wenzao waliogoma.

Sakata hilo lilitokea kwenye shule za msingi za Kilima "A" na "B", Nyashimbi na Mbulu, ambako walimu wachache walioamua kuingia darasani waliondolewa kwa viboko.

Baadhi ya shule zilizotembelewa na waandishi wa habari jana zilikuwa zimefungwa wanafunzi walikuwa wamezagaa nje wakicheza. Viongozi wa serikali ngazi ya wilaya, tarafa, kata na vijiji walikuwa wakizunguka kila shule kufuatilia walimu waliogoma baada ya Wizara ya Serikali za Mitaa (Tamisemi) kuagiza hivyo juzi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kahama, Theresia Mahango alisema amepokea Sh34,300,000 kwa ajili ya kulipa madai ya walimu. Walimu wilayani Kahama wanadai zaidi ya Sh300 milioni, lakini Mahango alisema fedha hizo ni kwa ajili ya malipo yaliyoonekana kuwa ni halali tu.

Awali jana, Katibu Tawala wa Kahama, Bulla Gwandu alisema walimu walikuwa darasani wakifundisha, lakini mashuleni hali haikuwa hivyo.

Jijini Dar es salaam, Hussein Kauli anaripoti kuwa walimu walianza mgomo wao wakifananisha ahadi za serikali na ahadi za kuku kwa vifaranga kuwa atavinyonyesha wakati ni jambo lisilowezekana.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Pwani, Method Rugambarala alisema walimu wake walianza mgomo asubuhi na walimueleza kuwa wanafanya hivyo kuunga mkono tamko la CWT, lakini akasema watafika maeneo ya kazi kuhofia vitisho vya serikali.

Naye mmoja wa walimu wakuu wa shule za msingi Temeke ambaye hakutaka kutajwa gazetini, aliilalamikia serikali kuwa inatafuta ugomvi na walimu kwa kuwa haina sababu ya kutowalipa madai yao.

"Serikali haina sababu inayowafanya wasitulipe madai yetu kwa kipindi kirefu kiasi hiki. Upole wetu kwa watu hawa umefikia kikomo na tutashindwa kufanya kazi hali ambayo itawaathiri watoto wetu," alisema.

Walimu wengi wa shule za msingi za Kunduchi na Pius Msekwa hawakuhudhuria shuleni jana, hatua iliyofanya kushindwa kuanza kwa mitihani ya mwisho wa mwaka.

Walimu wengine waliounga mkono mgomo huo ni wa shule za msingi za Bunge, Uhuru Mchanganyiko, Boma na Diamond za Wilaya ya Ilala, hali iliyowafanya baadhi yao kuandamana kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro kufikisha kilio chao.

Naye, Patricia Kimelemeta anaripoti kuwa, zaidi ya asilimia 75 ya walimu wa Manispaa ya Kinondoni walifika shuleni kama kawaida, lakini hawakufundisha.

Mkuu wa Wilaya ya Kindondoni, Kanali Fabian Massawe alisema kuwa alipata taarifa kuwa baadhi ya walimu hawakufika shuleni na kuelezea kitendo hicho kuwa ni kiburi kwa serikali ambayo tayari imeanza kutoa fedha kulingana na madai yao nchi nzima.

Naye Aziza Nangwa, anaripoti kuwa shule za msingi za Ubungo Kibangu na Ubungo Kisiwani hakukuwepo na mgomo.

"Sisi bwana tunaendelea na kazi kama kawaida na suala la kugoma kwetu halipo. Si unaona tunavyochapa kazi au huoni watoto wanaingia madarasani kama kawaida kwahiyo tunafuata selikali inasemaje," alisema Mwalimu Kilimba.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ubungo, Kibangu Juma Abdallah alisema kuwa suala la kugoma ni la mtu binafsi kwa hiyo wanaendelea na kazi.

Mwandishi wetu, Angela Mwakilasa anaripoti kuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Air Wing, Devota Stambuli alisema kuwa, taarifa za mgomo alizisikia kwenye vyombo vya habari na kwamba ataendelea kufundisha hadi apate barua ya CWT.

Kutoka Morogoro, Samuel Msuya anaripoti kuwa asilimia 70 ya walimu waliitikia wito wa kugoma.

Katibu Mkuu wa CWT Morogoro, Issa Ngayama alisema walimu katika wilaya za Ulanga, Kilombero, Kilosa na Mvomero hawakuingia darasani, lakini wa Manispaa ya Morogoro waliendelea kufundisha.

Ngayama alidai kuwa walipata taarifa kutoka Ulanga na Kilombero kuwa, polisi walikuwa wakipita sehemu kadhaa kuhakikisha kuwa mgomo unadhibitiwa.

"Lakini sisi tunaona kuwa mgomo umefanikiwa kutokana na viongozi wa serikali kuacha kazi zao na kuzunguka katika shule kuhakikisha wanauzima mgomo huu," alisema.

Hata hivyo, uchunguzi katika shule mbalimbali za Manispaa ya Morogoro na Ulanga unaonyesha kuwa walimu waliripoti kwenye vituo vya kazi, lakini hawakuingia darasani kwa madai ya kuandaa ripoti za mwaka.

Katibu wa CWT Kilombero, Maswi Mudani alisema walimu wamefuata maelekezo ya chama chao ya kugoma hadi walipwe haki zao, wakati wilayani Kilombero, Mkurugenzi Mtendaji, Alferd Luanda alisema wamepokea Sh63 milioni kwa ajili ya malipo hayo.

Naye Juddy Ngonyani wa Sumbawanga anaripoti kuwa, walimu wa shule za sekondari na msingi walianza mgomo na kufanya wanafunzi wa shule nyingi kupata fursa ya kucheza nje tangu asubuhi.

Mwananchi ilishuhudia hali hiyo katika shule za msingi Mwenge A na B, Chanji, Kizwite, Chemechem, Majengo, Jangwani, Kanda, Mazwi na Shule ya Kutwa Sumbawanga, wakati walimu wengi wa shule za sekondari hawakwenda kabisa kazini .

Katika Shule ya Msingi ya Jangwani, Mwalimu Mkuu Morris Kibona alisema kuwa walimu wameripoti kazini kama kawaida asubuhi, lakini hawakuingia darasani isipokuwa wale wa darasa la kwanza.

Mmoja wa walimu hao, Mary Kameme alisema: "Hatufurahishwi na kitendo cha kugoma kwa kuwa kinawaathiri wanafunzi, lakini ni lazima serikali itambue kuwa kama walimu wamefikia hatua ya kugoma, inamaanisha wamechoshwa na hali iliyopo."

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwenge "A", Gilbert Mwangosi alisema: "Leo nimechelewa kwa sababu nimekuja kwa mguu... sikuona sababu ya kuchoma mafuta yangu ya pikipiki ili kuwahi shule wakati leo walimu tunaanza mgomo nchi nzima."

Kutoka Arusha, Hemed Kivuyo anaripoti kuwa kulikuwa na walimu waliogoma na walioamua kuingia darasani.

Uchunguzi uliofanywa jana katika shule za msingi na sekondari umebaini kuwa pamoja na walimu wengi kukataa kushiriki mgomo, wengi walikaa kwenye vikundi kujadili hatima yao.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Uhuru ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema hakukuwepo na mgomo isipokuwa baadhi ya walimu wapo katika majadiliano na kwamba, anawasubiri ili waweze kusimamia mitihani.

"Hakuna mgomo kama unavyoona walimu wapo ofisini na wengine wale kule nje wapo katika majadiliano na ninawasubiri waje kusimamia mitihani," alisema mwalimu huyo.

Lakini walimu walioongea na Mwananchi walisema hawawezi kuingia madarasani kwa kuwa, kufanya hivyo ni kusaliti msimamo wa wenzao.

"Hatuingii darasani; huyo mwalimu aliyekueleza hakuna mgomo yeye ndiye hayupo katika mgomo, lakini sisi tunagoma," alisema mmoja wa walimu hao ambao hawakutaka kuandikwa majina yao gazetini.

Katika shule ya msingi Ungalimited, baadhi ya walimu waliingia madarasani kama kawaida huku baadhi yao wakiwa katika baa ya jirani iliyoandikwa `NARA` wakinywa bia, wakidai kuwa wameamua kujiburudisha kwa kuwa kwa sasa wanasimamia mitihani.

Katibu wa CWT Arusha, Nuru Shenkalwa alisema mpaka sasa chama hicho hakina tamko lolote na kwamba wanasubiri maelekezo toka juu, wakati Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Evance Balama alisema kuwa amefanya ziara ya ghafla katika baadhi ya shule na hapakuwepo na mgomo wowote kwa walimu.

Mwandishi wetu wa Mbeya, Brandy Nelson anaripoti kuwa baadhi ya walimu waliamua kuendelea na kazi, ikiwa ni pamoja na kusimamia mitihani ya kumaliza mwaka, wakidai kuwa hawajapata taarifa ya maandishi ya kuwataka wagome.

"Taarifa za mgomo tumezisikia kwenye vyombo vya habari, lakini hatujapata barua yoyote kutuarifu kuhusu mgomo kutoka CWT mkoa," alisema Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Sisimba, Ephata Mbisemmoja.

Naye Afisa Elimu wa Mbeya, Juma Kaponda alisema kuwa tayari Sh 636,507,743 zimeshafika kwa ajili ya kulipa walimu madai yao na kwamba zimeanza kufanyiwa utaratibu wa kuingizwa katika akaunti za halmshauri kwa ajili ya kuanza kuwalipa walimu.

Katibu wa CWT Mbeya, Tweedsmur Zambi alikiri kupata taarifa kuwa katika baadhi ya shule walimu waliamua kuendelea na kazi.

"Lakini si kweli kwamba hawana taarifa ya mgomo. Naomba uelewe kuwa mgomo kwa Mkoa wa Mbeya upo kama ulivyo mikoa mingine,"alisema.

Jijini Tanga walimu waliochelewa vituoni walitumiwa ujumbe mfupi wa simu (sms) kubembelezwa wafike vituoni, anaripoti Burhani Yakub.

Walimu kadhaa walitumiwa ujumbe kwenye simu zao wakiombwa kufika shule na kuhakikishiwa kuwa fedha zao zimeshawasilishwa na kwamba, ziko kwenye akaunti ya halmashauri.

Mwananchi ilionyeshwa ujumbe uliokuwa kwenye simu ya mwalimu mmoja wa shule ya msingi iliyo katikati ya Jiji la Tanga ikisema: “Unoambwa kufika shuleni kwako, usifanye mgomo fedha zimeshaingia na mtaanza kulipwa leo.”

“Hata wenzangu wa shule mbalimbali wametumiwa ujumbe kama huu hivyo tukaamua kuja shuleni baada ya kuhakikishiwa kuwa, fedha zetu zimeshawasilishwa,” alisema mwalimu huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwajuma.

Kutoka mkoani Mwanza, Frederick Katulanda anaripoti kuwa walimu waliendesha mgomo baridi, baadhi wakiripoti kazini na wengine kutoripoti kabisa huku wakisubiri taarifa za malipo yao.

Karibu katika shule zote za msingi kulikuwa na walimu wachache na hivyo kushindwa kufundisha na kuachia wanafunzi waendelee na michezo nje.

Katika shule za Nyamagana, Buhongwa, Kitangiri, Mirongo, Mbugani na Nyamanoro, walimu walikuwepo, lakini hawakuweza kufundisha.

Mmoja wa wanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya Kitangiri, Zelaida Filbert alisema ingawa baadhi ya walimu wamefika shuleni hapo, hakuna aliyefundisha na kuongeza: “Tumekaa darasani kwa muda mrefu sasa nimeamua kuondoka tu kwenda nyumbani, walimu hawafundishi wapo tu. Alikuja mwalimu wa Hisabati na kutupatia mitihani yetu halafu akaondoka.”

Mwanafunzi mwingine, Charles James wa shule ya Nyanza alisema leo hatahudhuria shule kutokana na ukweli kuwa, walimu wanaendelea na mgomo.

Mwenyekiti wa CWT Mwanza, Benedicto Raphael alisema jana walikuwa na mgomo baridi kutokana na taarifa kuchelewa kuwafikia walimu wengi na kutangaza kuwa mgomo rasmi ni leo.

“Serikali imetimiza madai mawili kati ya nane, tunaendelea na mgomo wetu. Tunaiomba serikali kutekeleza madai yetu badala ya kututolea vitisho na napenda itambue hatutaogopa vitisho... tutaendelea kudai haki yetu mpaka ilipwe,” alisema na kubainisha kuwa walimu wa Mwanza wanadai Sh1.1 bilioni.

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya jiji alisema wamelipa jumla ya madai 67 kiasi cha Sh 37 ml. kuanzia majira ya saa 3:00 asubuhi. Kuna madai 195 ya walimu, lakini madai 128 yamebainika kuwa na kasoro.

Julieth Ngarabali anaripoti kutoka mkoani Pwani kuwa, wanafunzi walishindwa kufanya mitihani ya kumaliza mwaka kutokana na mgomo wa walimu.

Habari ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa shule nyingi za msingi katika wilaya za Kibaha Vijijini, Bagamoyo, Kisarawe na Kibaha Mjini mitihani haikuanza kama ilivyopangwa.

Katika shule kadhaa ikiwemo Msangani, Nyumbu, Umoja, Mwendapole na Chalinze walimu walikiri kuwa mitihani haikufanyika, lakini wakasema kuwa hiyo ilitokana na kutokamilika kuchapishwa na kwa sababu ya mgomo, lakini katika shule za Mkuza, Mkoani, Maili Moja, Nyumbui na Soga wanafunzi waliendelea na mitihani.

Baadhi ya walimu walisema mitihani itaanza Jumatano.

Mwenyekiti wa CWT, Pwani Kelvin Mahundi alisema walimu waliingia darasani kutokana na kuogopa vitisho vya serikali, lakini si kwamba hawana nia ya kugoma, wakati mwenyekiti wa Kibaha, Donald Machapula alikiri kuwepo kwa shule ambazo walimu waligoma kusimamia mitihani.

"Sidhani hapa kuna la maana linaloendelea; naishauri Serikali iharakishe malipo ya walimu maana hakuna kitakachokuwa kinafanyika huko kwa watoto mashuleni," alisema Mahundi.

Mkurugenzi wa Wilaya ya Kibaha, Festo Kang'ombe alisema wamepokea hundi ya Sh55 milioni kwa Wilaya ya Kibaha Vijijini na Sh51,818,107 kwa Kibaha Mjini na kwamba wahasibu jana walikuwa wakihaha kuandika malipo kwa walimu.

Hali ya mgawanyiko pia ilionekana mkoani Singida, ambako baadhi ya walimu waliingia darasani na wengine kutoenda kabisa kazini, anaripoti Jumbe Ismaily.

Katika Shule ya Msingi ya Kindai, wanafunzi wake walihudhuria shuleni, lakini hawakuweza kusoma kutokana na mgomo huo, hali iliyokuwa pia katika shule za msingi za Bomani, Sabasaba, Ukombozi na Chief Senge Sekondari ambako wanafunzi walitakiwa kurudi nyumbani.

Katika shule za Utemini na Singidani, walimu wote walihudhuria kazini na kusimamia mitihani ya mwisho wa mwaka.

Waandishi wetu walio Babati, Iringa na Handeni wanaripoti kuwa hakukuwepo na mgomo na zoezi lililotawala jana lilikuwa ni malipo.

Gazeti la MWANANCHI kwa upande wake linahabarisha kwamba

HABARI LEO LIMEFANYA KAZI YAKE KAMA YALIVYOKUWA YANAFANYA MAGAZETI YA SERIKALI YA KIKOMUNISTI YA MUUNGANO WA KISOVIETI (USSR),KUTOA TAARIFA ZINAZOASHIRIA UDOGO AU KUTOKUWEPO KABISA KWA TATIZO (KATIKA HABARI HII,MGOMO WA WALIMU UMEDORORA,HAIJALETA ATHARI ZILIZOKUSUDIWA,MAMBO YOTE "POA",NK).UKISOMA MWANANCHI UTAGUNDUA KUWA HALI NI TOFAUTI NA INAYOZUNGUMZIWA NA HABARI LEO.IFAHAMIKE KWAMBA HAKUNA ANAYENUFAIKA KWA KUPEWA TAARIFA ZA KUPENDEZESHA MACHO.SUALA HAPA SIO UKUBWA AU UDOGO WA MGOMO HUO BALI ATHARI ZAKE KWA WADOGO,WATOTO NA WAJUKUU ZETU.IKUMBUKWE PIA KWAMBA TUKIO HILI LINATOKEA WAKATI SUALA LA MIGOMO LINAANZA KUWA KAMA "FASHENI" FLANI.

HILI TATIZO LINGEWEZA KUEPUKWA ZAMANI HIZO LAITI WAHUSIKA WASINGEENDEKEZA PRIORITIES ZAO BADALA YA ZA WALE WANAOPASWA KUWATUMIKIA.UTARATIBU WA KUTATUA MATATIZO KWA NJIA YA ZIMAMOTO NI HATARI SANA,YAANI MPAKA TATIZO LITOKEE NDIO ZIANZE JITIHADA ZA KUTAFUTA UFUMBUZI.HIVI SIKU ZOTE HIZI WALIKUWA WAPI HAO WANAOPASWA KUHAKIKI MADENI YA WALIMU?HIVI HAKUNA WATU WANAOLIPWA MISHAHARA KWA AJILI YA KAZI HIYO YA KUHAKIKI NA KUHAKIKISHA MASLAHI YA WALIMU NA WATUMISHI WENGINE WA UMMA?

KUKIMBILIA MAHAKAMANI KUZUIA MIGOMO NI SULUHISHO LA MUDA TU,UFUMBUZI WA KUDUMU NI KUWAJIBIKA IPASAVYO KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU (UWAJIBIKAJI).TATIZO LA WALIMU NI SEHEMU NDOGO TU YA MATATIZO KADHAA AMBAYO KWA HAKIKA YANGEWEZA KUEPUKIKA LAITI WAHUSIKA WANGEWAJIBIKA IPASAVYO.WALIMU WATALIPWA KWA ZIMAMOTO,INAWEZA KUZIMA MGOMO LAKINI KESHO TRL NAO WATAGUNDUA KUWA WAKIGOMA WATAFANYIWA MALIPO YA ZIMAMOTO,KESHOKUTWA MADAKTARI,MANESI,NK NK NK.

WAHUSIKA WATEKELEZE WAJIBU WAO.PIA,SISI NI MASIKINI NA TUNAPASWA KUISHI KIMASIKINI KAMA TUNATAKA KUMUDU GHARAMA ZA MAISHA YETU.UNUNUZI WA VITU VYA FAHARI NA MATUMIZI MENGINE YASIYO YA LAZIMA YANAATHIRI KWA KIWANGO KIKUBWA UWEZO WETU WA  KUJIHUDUMIA NA KUJIENDESHA WENYEWE.HIVI NI LAZIMA KILA MHESHIMIWA ATUMIE "SHANGINGI" LA MAMILIONI KADHAA?JE GHARAMA ZA GARI HILO ZINGEKATWA JAPO ROBO ZISINGEWEZA KUWALIPA WATUMISHI WENZETU WANAODAI MALIMBIKIZO YAO?

Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara mkoani Kilimanjaro (MUCCoBS) kimewatimua wanafunzi 595 wa mwaka wa kwanza kutokana na kuanzisha mgomo chuoni hapo. 

Aidha wanafunzi hao pamoja na mgomo huo,wametuhumiwa pia kuhatarisha maisha ya baadhi ya wanafunzi wenzao wa mwaka wa pili na wa tatu sambamba na wahadhiri chuoni hapo baada ya kuwamwagia mchanga na kuwarushia mawe wakiwa darasani. 

Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Suleiman Chambo alisema jana kuwa kutokana na mgomo huo, menejimenti iliamua kuwasimamisha masomo wanafunzi hao kwa muda usiojulikana na umewataka wawe wameondoka chuoni hapo hadi kufikia jana saa 10 jioni. 

"Wanafunzi wa mwaka wa kwanza walipoona wenzao wa mwaka wa pili na tatu hawawaungi mkono waliamua kuwafuata madarasani na kuwamwagia mchanga na kuwarushia mawe huku mhadhiri mmoja akiwa darasani, Profesa Temba, ambaye alinusurika kipigo na ilimbidi kuingia chini ya meza ili kujinusuru," alisema. 

Aliongeza kudai kuwa wanafunzi hao hawana madai ya msingi na kwamba moja ya madai yao ni kuishinikiza Serikali kuwalipia mikopo kwa asilimia 100 huku madai mengine ni kuwaunga mkono wanafunzi wenzao katika vyuo vikuu vilivyofungwa. 

"Tumeamua kuwarudisha nyumbani kwa muda usiojulikana, na wakirudi waandike barua wathibitishe kulipa ada kwa asilimia 100, waombe kurudi chuoni na kufuata taratibu za chuo na walete vyeti vya kuonesha kwamba wana sifa za kurudia shahada wanayosomea," alisema. 

Alidai kuwa wanafunzi hao pia walitishia maisha ya Rais wa Serikali ya wanafunzi chuoni hapo, Zamu Mlimila ambaye alilazimika kuokolewa na polisi baada ya wanafunzi kumzonga kwa lengo la kumshinikiza atangaze mgomo chuoni hapo.

CHANZO: Majira

17 Nov 2008

Picha (ni kielelezo tu,haihusiani na habari) kwa hisani ya MJENGWA

WALIMU wanaofundisha katika shule zilizopo wilayani Monduli mkoani Arusha ambao waliajiriwa toka Julai mwaka huu, wapo katika hali mbaya kimaisha kiasi cha kufikia hatua ya kufanya kazi za kugonga kokoto ili kujikimu kimaisha.

Hali hiyo imetokana na walimu hao kutolipwa mishahara yao ya miezi zaidi ya minne toka waajiriwe, licha ya kusaini mkataba wa miaka mitano.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na Tanzania Daima, umebaini kuwa walimu walioathirika kwa kiasi na hali hiyo ni waliopo katika maeneo ya Loolkisare, Moita, Meserani Juu, Mto wa Mbu, Losomingo na Lepulko ambapo inadaiwa walimu hawana hata nauli ya kuwafikisha katika Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.

Akizungumza na Tanzania Daima, mmoja wa walimu hao, Goodluck Namoyo, alisema hali zao ni mbaya kifedha na wanajiandaa kukutana leo ili kujadili hatma yao.

Katika maeneo mengine ya Loolkisare na shule zilizopo vijiji vya mbali walimu wanaingia darasani kwa muda mfupi na muda mwingi wanatumia kufanya kazi za vibarua kwa kugonga kokoto ili kuwawezesha kupata angalau fedha za kujikimu.

Kaimu Afisa Elimu wa wilaya ya Monduli Emanueli Maundi, alikiri kuwepo kwa hali hiyo na kuongeza kuwa walimu 40 hawajalipwa mishahara yao mpaka sasa na wao kama idara ya elimu, wamefanya jitihada kunusuru hali hiyo.

''Ndugu yangu mwandishi hivi tunavyoongea licha ya mweka hazina kuwasilisha majina ya walimu hao wizarani kwa muda mrefu sasa, hali bado ni tete na imemlazimu afisa elimu hiyo kwenda jijini Dar- es- salaam kushughulikia mishahara ya walimu hao kwani wana hali mbaya sana hivi sasa,'' alisema Maundi.

Naye katibu wa chama cha walimu wilaya za Monduli na Longido Godwin Mushi, alisema hali ya walimu hao inadhihirisha ni jinsi gani walimu hawathaminiwi kwani toka waajiriwe, hawajalipwa.

''Sidhani kama mwalimu huyo anaweza kumshauri ndugu yake yoyote apende kuwa mwalimu kutokana na hali aliyokumbana nayo yeye hivi sasa na hali hiyo ni hatari zaidi kwa siku za baadaye juu ya mustakabali wa elimu nchini, ''alisema Mushi.

Akizungumzia hali hiyo Mkaguzi wa Elimu wa Wilaya ya Monduli, Ernest Mwende, alisema kazi ya walimu kwa sasa ni ngumu kutokana na kupungua kwa thamani ya mwalimu.
CHANZO: Tanzania Daima

CLICK HERE to read the story.

Universities are being asked to set up surveillance units to monitor the movements of international students in a government-led crackdown on bogus student immigration scams, academics say. New rules to force universities to report overseas students who miss too many lectures to immigration officers will harm the academic-student relationship because lecturers are being asked to act in a "police-like" manner, according to a group of 200 academics and activists opposing the moves.

A letter to the Guardian, organised by Ian Grigg-Spall, academic chair of the National Critical Lawyers Group and signed by leading academic lawyers, the head of the lecturers' union and Tony Benn, claims that the rules could breach the European convention on human rights, which guarantees the individual's right to privacy. "This police-like surveillance is not the function of universities and alters the educational relationship between students and their teachers in a very harmful manner," it says. "University staff are there to help the students develop intellectually and not to be a means of sanctioning these students."

The rules will require all universities to obtain a licence to admit students from outside the EU. They will then have to sponsor students, who will be required to have their fingerprints taken and be issued with ID cards. Lecturers will have to report any student who misses 10 or more lectures or seminars. Students will also have to prove they have funds to cover fees plus £800 a month for the duration of their courses. Universities have separately raised concerns that the system of registering overseas students, which is planned to take place at six centres around the country, will struggle to cope.

About 350,000 overseas students attend British universities every year. Universities are heavily dependent on the £2.5bn a year they pay in fees.

Almost 300 bogus colleges have been uncovered in the past three years, many involved in immigration scams.

Sally Hunt, general secretary of the University and College Union, said: "We have grave concerns that new rules on monitoring foreign students have been pulled together without any consultation with the people who would implement them. We do not believe it is appropriate or effective to task colleges and universities with the policing of immigration."

A Home Office spokesman said: "Those who come to Britain must play by the rules and benefit the country. This new route for students will ensure we know exactly who is coming here to study and stamp out bogus colleges who facilitate the lawbreakers.

"International students contribute £2.5bn to the UK economy in tuition fees alone. The student tier of the points system means Britain can continue to recruit good students from outside Europe."

SOURCE: The Guardian

*Wajipanga kuanika siri zote hadharani
*Vocha za malipo kwa CCM kuanikwa
*Kapt. Chiligati awakana, naye awatisha
*Asisitiza hakuna kikao kilichowatuma

Na Mwandishi Wetu 

BAADHI ya watuhumiwa wa ufisadi kwenye Akaunti ya EPA iliyokuwa Benki Kuu (BoT) sasa wameamua kuitisha Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, uchunguzi wa Majira umebaini. 

Kitisho hicho kimekuja kufuatia baadhi yao kukamwatwa na kufunguliwa kesi mbalimbali za jinai huku ikionekana kuwa wao walikuwa mawakala tu katika kupitisha fedha hizo na vigogo husika wakiwa nje. 

Chanzo chetu kilicho karibu na baadhi ya watuhumiwa hao kilieleza kuwa kukamatwa, kufunguliwa mashitaka kumewadhalilisha sana baadhi yao huku wakiumia zaidi kwa kusota rumande, kwenye gereza la Keko na wale wanawake wakiweka Gereza la Wanawake Segerea. 

"Jamaa ameumia sana rohoni, hata kuhangaikia dhamana alisita mwanzo baada ya kuona kwa nini ahangaike kutoa mali zake, wakati alikuwa wakala tu," kilisema chanzo chetu kilicho karibu ni mmoja wa watuhumiwa waliokwisha funguliwa kesi na akasota sana kwenye gereza la Keko. 

Ingawa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa kikikana mara kadhaa kuhusika kunufaika na fedha hizo katika chaguzi mbalimbali, duru za uchunguzi, zinawakariri baadhi ya watuhumiwa hao wakilalamika 'kutolewa kafara.' 

Ndugu mwingine wa mtuhumiwa ambaye ameshafanikiwa kwa kiasi kikubwa kulikwepa sakata la EPA, ingawa taarifa za kiuchunguzi bado zinaamini huenda akaburutwa naye kortini, aligusia kuwa kwa sababu yeye alitumiwa tu, ameandaa faili la utetezi ambalo pamoja na nyaraka nyingine, limeheheni kile alichokitaja kuwa vocha za malipo kwenda kwa baadhi ya vigogo wa CCM. 

"Hapa ndipo Serikali itakapoumbuka. Kila kitu kipo. Hajakamatwa bado, ameshahojiwa na kubanwa katika shughuli zake, anasubiri tu afikishwe kortini atoe vielelezo vyake, yeye si fisadi, aliombwa asaidie shughuli halali akafanya hivyo, kwa namna anavyojiheshimu, asingeweza kusaidia akakubali wizi," kilisema chanzo chetu kilicholiona faili hilo la utetezi. 

Wakati watuhumiwa hao wa EPA wakijipa 'kujiondoa katika ukafara,' Mwandishi Wetu Eckland Mwaffisi anaripoti kuwa uongozi wa juu wa CCM, umeendelea kusisitiza kuwa hawahusiki na ufisadi wa EPA. 

Akitoa tamko kwa niaba ya Chama chake Dar es Salaam jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Bw. John Chilligati, alisema CCM haikuhusika na wizi huo kama ilivyodhibitishwa na ripoti ya kamati ya wanasheria. 

Alisema pamoja na madai yanayotolewa na viongozi wa vyama vya upinzani, pasipo kuthibitisha madai hayo, CCM haikuchukua fedha hizo wala haikumtuma mwanachama wake au mkereketwa yoyote kwenda kuchukua fedha hizo katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT). 

Bw. Chilligati alisema pamoja na orodha ya watuhumiwa wa EPA kuhusisha majina ya wanachama wa CCM ama Wakereketwa, Chama hakijahusika kumtuma bali ni kitendo cha mtu binafsi. 

Hadi sasa miongoni mwa waliokamatwa kwa tuhuma za wizi wa fedha za EPA wanaohusishwa na ukaribu na vigogo wa CCM au kuwa makada ni Bw. Rajabu Maranda na mfanyabiashara, Bw. Jeetu Patel. 

"Kwenye ukweli, uongo hujitenga, madai yote ya kuihusisha CCM na ufisadi wa EPA ni uongo wenye nia ya kukivunjia heshima chama chetu machoni mwa jamii pamoja na hila za kuchafua jina la chama zinazofanywa na wapinzani ambazo kamwe, hazitafanikiwa," alisema Bw. Chilligati. 

Kutokana na hali hiyo, Bw. Chilligati aliongeza kuwa, baadhi ya wanachama wanaokiuka maadili hayo, isichukuliwe kwamba wanatumwa na vikao vya chama bali ni vitendo vyao binafsi na watachukuliwa hatua za kisheria na vyombo vya dola kama ilivyo kwa wahalifu wengine. 

Alisema CCM, inapongeza Rais Jakaya Kikwete kwa hatua alizozichukua katika kushughulikia sakata hilo. 

Hadi wiki inayoanza leo, ambapo zipo tetesi za watuhumiwa zaidi kuanza kufikishwa kortini huku Mkurugenzi wa Mashitaka ya Umma (DPP), Bw. Eliezer Feleshi akikiri kuwa bado kuna mafaili yanapitiwa, idadi ya watuhumiwa waliokwishafikishwa kortini ni 20. 

Baadhi ya makampuni ambayo yameshafikishwa mahakamani ni pamoja na Money Planners, Kiloloma & Brothers, Njake Hotel, Rashhas, Mibare Farm, Changanyikeni, Bencon International, Kernel, Malta Mining, Navy Cut Tobacco na BC Grassel & Company. 

Makampuni yanayosubiriwa kwa hamu na wananchi katika Mahakama ya Kisutu ni pamoja na kampuni ya Kagoda ambayo inadaiwa kuchota fedha nyingi kulikoni kampuni nyingine.

CHANZO: Majira

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.