16 Jan 2009





Pichani,ni KEZIA OBAMA-mama wa kambo wa Barack Obama-akiwa uwanja wa ndege wa Heathrow,London hapa Uingereza tayari "kukwea pipa" kuelekea Marekani kuhudhuria kuapishwa kwa mwanae hapo Jumanne ijayo.Kezi,ambaye kwa sasa anaishi Bracknell, Berkshire,aliwahi kuolewa na marehemu baba yake Rais Mteule Obama.Mama huyo aliondoka siku ambapo sanamu (waxwork) ya mwanae ilizinduliwa katika musemum ya Madame Tussaud jijini London.





14 Jan 2009

WARNING: Very Graphic

Osama bin Laden has called for Muslims to wage a holy war against Israel over the invasion of Gaza. Skip related content

The al-Qaeda leader called for jihad in an audio tape that appeared on Islamist websites. In response, the US said it demonstrated bin Laden's isolation and it was merely an effort to raise money.

The news came as United Nations Secretary-General Ban Ki Moon visited the Middle East to press for an immediate ceasefire in the Gaza Strip.

The Hamas-run Health Ministry in Gaza has said 1,010 Palestinians - including over 670 civilians - have been killed in the offensive which began on December 27. Around 4,700 people have been wounded.

t
Ten Israeli soldiers and three civilians hit by rockets fired from the Gaza Strip have been killed in the violence. Israel has continued to drop bunker-busting bombs on around 35 smuggling tunnels under the Gaza-Egypt border in a bid to halt Hamas re-arming.

Meanwhile, in Cairo, Mr Ban renewed his call for "an immediate and durable ceasefire" between the warring sides. An unnamed Israeli official has said Egypt, which is trying to broker a truce, is pushing for a deal by the weekend.

The official said "there has been progress" on talks over border controls to prevent Hamas from replenishing its arsenal. But he said Israeli leaders were non-committal about the prospect of reaching a ceasefire accord in the next few days. Elsewhere, three rockets launched from Lebanon hit fields outside
the Israeli town of Kiryat Shmona, the second such attack in less than a week.
SOURCE: ITN



13 Jan 2009

Venance George, Morogoro
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limesema kauli iliyotolewa juzi na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kupinga oparesheni Sangara inayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), si kauli ya waislamu wote.
Akizungumza mjini Morogoro kwa niaba ya Kaimu Mufti wa Tanzania,
Shekhe Suleiman Gorogosi, mratibu wa habari wa Bakwata, ustadhi Issa Mkalinga alisema kauli hiyo ni ya waislamu wachache ambao wamekuwa wakitumiwa na viongozi wa kisiasa kwa manufaa binafsi.
Ustadhi Mkalinga pamoja na Mkurugenzi wa Utawala, ustadhi Karim Mataliwa, aakizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kaimu mufti huyo ya kutembelea mikoani kuhamasisha uhai wa baraza, alisema baraza halitambui kauli hiyo na wala halijihusishi na mambo ya siasa.
"Ujue tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu hapo mwakani, hivyo wako baadhi ya wanasiasa wanatumia mwanya wa majukwaa ya dini kupeleka ujumbe wao," alisema.
Akizungumzia ziara ya kaimu mufti mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa Utawala alisema kuwa ziara hiyo ni sehemu ya utaratibu aliyojiwekea kaimu mufti ya kutembelea baraza katika mikoa yote Tanzania na kwamba kaimu mufti ametembelea Dodoma na Morogoro na atatembelea mikoa mingine.
Ustadhi Mataliwa alisema lengo la ziara hizo ni kutaka kujua uhai wa baraza na matatizo yanayolikabili baraza katika ngazi hizo ikiwa ni pamoja na kuhimiza kufanya maandalizi ya uchaguzi wa viongozi kuanzia ngazi ya msikiti hadi taifa utakaoanza kufanyika mwezi April mwaka huu.
Wakati huo huo, katika mahojiano na baadhi ya waumini wa dhehebu hilo, mkoani Morogoro wameunga mkono kauli ya Bakwata na kudai kuwa viongozi wa dini ni vema wakafanya shughuli zao za kiroho na kuwaacha wanasiasa kufanya kazi zao za siasa.
Mmoja wa waumini hao, Ismael Rashid, alisema tamko lililotolewa na waislamu katika kongamano la jijini Dar es Salaam la kudai kuwa Chadema haina manufaa na msaada wowote kwa uislamu si maneno ya kiungwaana na si vema kukipakazia chama hicho kwamba ni kikabila na cha kibinafsi.
Rashid ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Jahazi asilia mkoani Morogoro alisema hatua iliyochukuliwa na Chadema ya kuacha kuunga mkono vyama vya CUF na Sauti ya Umma (SAU) ilikuwa ni sahihi kwa sababu chadema walisimamisha mgombea ubunge katika jimbo la Mbeya vijijini lakini vyama hivyo vilimwekea pingamizi mgombea huyo na kuenguliwa.
"Pingamizi hilo lilisababisha mgombea ubunge wa Chadema akaenguliwa kugombea
nafasi hiyo, sasa iweje chadema iwaunge mkono?" alihoji Rashid .
Alisema chama cha Chadema hakiungi mkono kampeni za mgombea wa CUF kwa mdai kuwa chama hicho, mwakani inakusudia kusimamisha mgombea wake katika jimbo hilo kwa hiyo kama Chadema ikiunga mkono CUF itashindwa kusimamisha mgombea wake hapo mwakani.


CHANZO:Mwananchi

12 Jan 2009

KWANZA,SAMAHANI KWA KUPOTEA ANGANI GHAFLA.HIYO NI KUTOKANA NA SABABU ZILIZOKUWA NJE YA UWEZO WANGU.PILI,NIMEKUTANA NA HABARI IFUATAYO KATIKA GAZETI LA MWANANCHI,NA IMEVUTA HISIA ZANGU.ISOME KWANZA KISHA TUIJADILI KIDOGO


WAUMINI wa dini ya kiislam wamepinga oparesheni sangara
inayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai kuws
chama hicho na operesheni hiyo, haina manufaa kwa uisalam kwa kuwa imejaa
ukabila, ubinafisi na udini
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye
kongamano la kiisilamu, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam, walisema
oparasheni Sangara imekuwa ikimchafua rais Jakaya Kikwete bila sababu licha ya
mambo mengi mazuri, aliyoyafanya kwa taifa.
Shekhe Saidi Mwaipopo aliwataka
waisalamu kutambua kuwa chama hicho, hakina msaada wowote wa maendeleo ya
uislamu kutokana na chama hicho kujaa ukabila udini na ubinafisi.
"Napenda
waislamu muelewe kuwa chama cha Chadema hakina msaada wowote juu ya uislamu na
kimekumbatia udini, ukabila na ubinafisi kutokana na sababu hiyo, tutatembea
nchi nzima kuwaeleza wanachi ukweli wa jambo hili na kuwataka wasikiunge mkono
chama hicho,"alisema Mwaipopo...
ENDELEA


HISIA ZANGU ZA HARAKA NI KWAMBA KUNA KUNDI LA MAFISADI AMBAO KATIKA KUTAPATAPA KWAO WAMEAMUA KUTUMIA TURUFU YA UDINI.KUNA VUGUVUGU LA UDINI LINALOENDELEA KIMYAKIMYA HUKO NYUMBANI.KUNA WATU WANATUMIWA KUTETEA MASLAHI YA MAFISADI,AIDHA WAKATI WANAFAHAMU KUWA WANATUMIWA AU HAWAFAHAMU KABISA.




HIVI INAINGIA AKILINI KWELI KWA WAUMINI WA DINI INAYOSIMAMIA HAKI (UISLAM) KUPINGA HARAKATI ZA KUSIMAMIA HAKI?JE IWAPO OPERESHENI SANGARA ITAZAAA MATUNDA KWA KUFANIKISHA UDHIBITI DHIDI YA MAFISADI,WAISLAMU NCHINI HAWATONUFAIKA?HAPA KUNA MIKONO YA WATU WANAOMWAGA FEDHA ZXAO ZA KIFISADI KWA WALE WALIO TAYARI KUSEMA LOLOTE ALIMRADI MKONO UENDE KINYWANI.




TUSIPOKUWA MAKINI,UFISADI UTAIFIKISHA TANZANIA MAHALA PABAYA ZAIDI YA HAPA TULIPO.

7 Jan 2009

Padre Privatus Karugendo amekuwa akisimulia mkasa ulisababisha yeye kusimamishwa,na hatimaye kuvuliwa,daraja la upadre.Kma nilivyoeleza katika post hii,japo sifahamiani personally na Mtumishi huyu wa Bwana,alikuwa columnist mwenzangu katika jarida la Raia Mwema hadi nilipolazimika kuchukua "sabbatical leave" ya uandishi wa makala.Pia,maandiko mbalimbali ya Padre Karugendo yalinipa changamoto kubwa hadi nikaamua kujiingiza katika anga za uandishi wa makala kwenye magazeti mbalimbali huko nyumbani.

Unaweza kusoma SIMULIZI kuhusu chanzo cha mkasa uliopelekea Padre huyo kusimamishwa na hatimaye kuvuliwa upadre kwa KUBONYEZA HAPA (Sehemu ya Kwanza) na HAPA (Sehemu ya Pili) na HAPA (latest).Blogu hii itaendelea kuwaletea simulizi hizo kadri zinavyochapishwa gazetini.Mkasa uliomkumba Padre huyu unanigusa sio tu kwa vile napenda makala zake au kwa sababu tuliwahi kuandikia gazeti moja,bali pia kwa vile kwa namna flani yeye,kama mie,ni majiruhi wa mfumo uliozowea kupongezwa na kunyenyekewa lakini usiotaka kusikia criticism au mawazo mbadala.
NYONGEZA: Nimekutana na post katika blogu ya Pambazuko ambapo Askofu (anayetajwa kwenye Simulizi za Karugendo) ANADAIWA KUWA NA MTOTO NA ANATAKIWA AKAMCHUKUE. (Bonyeza link kuisoma)




MWANGALIE MZAZI HUYU ASIYE NA AIBU KATIKA PICHA HII ILIYOPATIKANA KWA HISANI YA Father Kidevu.AMEJAWA NA TABASAMU WAKATI ANAMPELEKEA BIA MWANAE AMBAYE KWA MAKISIO HAZIDI MIAKA MITANO.TENA BIA YENYEWE NI SAFARI,AMBAYO HATA WANYWAJI SUGU WANAELEWA INAVYOMPELEKESHA MNYWAJI.INGEKUWA KWENYE NCHI ZINAZOJALI HAKI YA MTOTO NA WAJIBU WA WAZAZI,HUYU FISADI WA MALEZI ANGESHACHUKULIWA HATUA.KWANINI AMRITHISHE MWANAE ULEVI BADALA YA VITU VYA MUHIMU ZAIDI KWA FUTURE YA DOGO HUYO?HEBU ANGALIA VIDEO HII HAPO CHINI YENYE HABARI KUHUSU MZAZI ALIYECHUKULIWA HATUA KWA KILICHOELEZWA KUWA NI KOSA LA KUMPA SAPOTI MWANAE APIGANE.
KAMA WENZETU WANAWEZA,WHY NOT US?




CLICK HERE to read more about Orgasmic childbirth


Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.