15 Sept 2014

By Masembe Tambwe

THOUGH still low, technology and communication experts in the country are seeing signs of increased cyber crimes like bullying, harassing and stalking if the use of the internet is not controlled.
Speaking exclusively to the 'Sunday News,' the Head of Corporate Communications at the Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), Mr Innocent Mungy, said that whilst there are many crimes using the internet as a platform, incidents of cyber bullying are still very small.
 
"Due to ignorance, a lot of people today think when they have been swindled online through various social media, they have been cyber bullied but this isn't so.
 
There are certain elements that qualify as bullying and evidence shows the levels are still small but will increase with time," he said. Stopcyberbullying.org website defines cyber bullying as when a child, preteen or teen is tormented, threatened, harassed, humiliated, embarrassed or otherwise targeted by another child, preteen or teen using the internet, interactive and digital technologies or mobile phones.
 
It has to have a minor on both sides or at least have been instigated by a minor against another minor. Once adults become involved, it is plain and simple cyber-harassment or cyber stalking.
 
Adult cyber-harassment or cyber stalking is never called cyber bullying. In a recent incident that left a young lady dead and that created quite a stir in many social media networks, many users christened the incident as 'cyber bullying' calling various authorities to take action.
 
Mr Mungy said that there was no law in the country that is specific to cyber bullying because the law is universal and that irrespective of where a person is insulted or degraded, whether on the sidewalk or online, it is against the law and therefore punishable.
 
"Whilst cyber bullying is seen to be at a minimal, cyber stalking and harassment is something we are increasingly seeing on social media, cases of cyber bullying can be sought at the cyber crime unit of the police," he said.
 
According to Domestic Violence Resource Centre Victoria website, cyber harassment is not just about being teased - it's repeated behaviour that is designed to humiliate, control or scare the person being targeted and is not legal or alright, while if someone keeps contacting you on Facebook or any kind of online site and it's making you scared and upset, it sounds like you're being stalked.
 
Mr Mungy said that as a country, Tanzania has leapfrogged technology and that technology advancement and development is catching up with us instead of the other way round.
 
"The challenge to stop these crimes starts with us and the media; they have to play a part in this. At the moment it is not a catastrophe because only between 17 and 20 per cent are internet users mostly aged between 18 and 25 and these are abusers," he said.
 
He cautioned users to be careful who they befriend online because one can't guarantee identity. Online, he noted, there are predators, bad people, thieves, prostitutes, con artists who use it as a platform to do what they would have done physically. "Our online presence affects our being, meaning that our character profile.
If you upload inappropriate pictures, people will harass you and later you will come to claim that you were bullied yet you caused it, let's be smart, use communication for good, it's good to make friends online because having an enemy online can be your enemy physically," he advised.
 
A cyber crime expert, Mr Sebastian Marondo, said that one advantage cyber bullies have is that they can operate under the anonymity of not being able to be seen.
 
"Cyber bullying unlike ordinary bullying is a practice that's difficult to control given the fact that it relies on the internet and like other forms of technology that require communication or sending files.
The government is supposed to enact laws protecting internet users, mobile phone subscribers from fraudsters, stalkers and in general unwelcomed callers," he urged.
 
He called on mobile phone companies to create platforms for reporting and penalising callers who misbehave in mobile communication. For instance, telecom companies can block numbers that have been identified as abusive to others.
 
The Dar Teknohama Business Incubator Chief Executive Officer, Eng. George Mulamula, told this paper that schools can be very effective brokers in working with parents to stop and remedy cyber bullying as well as educate students on cyber ethics and laws.
 
Eng. Mulamula commended TCRA for doing a good job in trying to educate the public on the correct use of digital communication technologies and have even gone on road shows around the country, educating users on best practices on the use of cell phones and the internet.
 
"Parents can help stop cyber bullying. You can start by talking to kids about the issue and teaching them the rules that will help prevent cyber bullying from happening to them or someone they know," he advised.
 
During the first ever cyber crime conference in Dar es Salaam earlier this year, the government said it is planning to enact three laws on data, internet business and cyber crime in a bid to eradicate cyber crime in the country.
 
SOURCE: Daily News

14 Sept 2014

Taarifa zilizopatikana hivi punde zinaeleza kwamba kikundi cha kigaidi cha Dola ya Kiislamu (ISIS) kimemchinja kwa kumkata kichwa, David Haines, Mwingereza mfanyakazi wa shirika la misaada, kwa mujibu wa video iliyosambazwa na kikundi hicho.

Video ya mauaji hayo ya kinyama inaanza kwa kuonyesha hotuba ya Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron kuhusu Iraki, ikifuatiwa na ujumbe kwa washirika wa Marekani dhidi ya kikundi hicho, na inahitimishwa kwa tukio la kuogofya la kukatwa kichwa kwa Davidi ambaye ni Mskochi.

Tukio hilo limetokea na kurekodia katikati ya jangwa. Baada ya hotuba ya Cameron, mtu aliyejifunga kitambaa kuficha uso huku ameshikilia kisu anaonekana amesimama mbele ya David ambaye amepiga magoti, na kuamriwa kusoma 'hotuba ya mwisho.'

Katika hotuba hiyo fupi, Mwingereza huyo anasema, namnukuu, "Ninapenda kubainisha kuwa ninakulaumu Davdi Cameron kwa kuuawa kwangu.Umeingia kwa hiari katika ushirika na Marekani dhidi ya Dola ya Kiislam, kama alivyofanya mtangulizi wako Tony Blair."

Taarifa kamili ya David ni hii

Embedded image permalink

Baada ya kusoma taarifa hiyo, Davidi anakatwa kichwa kisha Mwingereza mwingine, Alan Henning anaonyeshwa akitishiwa maisha. Mtu aliyefanya uchinjaji huo anaonekana kuwa ni yuleyule aliyewachinja watu wengine wawili kabla ya tukio hili la leo. Kadhalika, anasikika akitoa onyo, namnukuu, "Iwapo wewe Cameron utaendelea kupambana na Dola ya Kiislam, basi wewe, kama bwana wako Obama, mikono yenu itakuwa na damu ya watu walio mateka wetu."

13 Sept 2014

Happy birthday @ommydimpoz one of the most down-to-earth superstars I have ever known…his common sense always ahead of fame, his humility always infront of his celebrity status: respectful, wise and simply a good guy! God loves us all, but He loves good people even more. May Allah bless you with all the best He offers to sie viumbe wake…and keep on being the good&humble person you always are. Enjoy your big day!
Leo ni siku ya kuzaliwa ya mmoja ya wasanii maarufu kabisa huko nyumbani na hata duniani, Ommy Dimpoz. Nilifahamiana na Ommy kupitia Twitter, na tangu wakati huo sijawahi hata siku moja kujilaumu kufahamiana nae. Tofauti na hisia zilizotapakaa katika jamii kuwa watu maarufu mara nyingi huwa 'watu wa kujiskia,' kwa Ommy ni tofauti kabisa. Katika mawasiliano tuliyowahi kuwa nayo kupitia Twitter ameonyesha ni kijana mstaarabu, mwenye heshima na ni vigumu kuamini kuwa ni mmoja wa watu maarufu kabisa kwa sasa huko nyumbani na nje ya mipaka ya nchi yetu.

Na sio Ommy Dimpoz pekee. Kitu kimoja nilichojifunza katika kufahamiana na wengi wa ma-celeb wetu ni utu wao. Orodha ni ndefu lakini kwa uchache tu, nilichokutana nacho kwa Ommy Dimpoz ndicho nilichokutana nacho kwa Mwana FA, Profesa Jay, AY, Fid-Q,Solo Thang,Lameck Ditto, Cindrulz,Grace Matata,Mkoloni, Albino Fulani na hata wakongwe wa fani ya Bongoflava kama @XamiaSiku4Saa4 wa waasisi wa Bongoflava Kwanza Unit, na wengineo wengi.Tumekuwa tukiheshimiana tangu siku ya kwanza 'tulipofahamiana' mtandaoni.

Lakini si kwa Bongoflava tu kwani hata mastaa wengine kama Sinta, Flaviana Matata, Sporah Njau, Batuli, Seki, Masanja Mkandamizaji, Sheria Ngowi, Michael Mlingwa Masudi Kipanya na wengineo wengi ni watu ambao kwa hakika sijawahi kujutia kufahamiana nao kwenye mitandao ya kijamii.

Na kwenye 'anga' nyinginezo VIPs kama Mawaziri Lazaro Nyalandu, Januari Makamba, wanasiasa kama John Mnyika, Faustine Ndugulile, Halima Mdee, Hamis Kigwangalla, William Ngeleja na Lawrence Masha, sambamba na waheshimiwa wana-Afrika Mashariki Shyrose Bhanji na Abdullah Mwinyi, hali ni hiyo hiyo, unafahamiana na watu mtandaoni na wanakuwa kama 'asset' muhimu maishani kwa aidha kujifunza kutoka kupitia mafanikio yao au ustaarabu walionao mtandaoni.

Makala hii haitoshi kuwataja watu wote maarufu niliofahamiana nao kupitia mitandao ya kijamii, lakini ninachoweza kubainisha bayana ni ukweli kwamba kuwa-follow watu maarufu kunapunguza sana usumbufu kwenye mitandao ya kijamii. Pengine ni kwa sababu wanatunza heshima yao lakini pengine ni ukweli kwamba mafanikio ni mwalimu mzuri wa maisha, na wengi waliofanikiwa watakwambia kuwa moja wa mitaji mikuu ya mafanikio ni kuwaheshimu watu wengine kama wanavyokuheshimu.

Lakini ninaomba nibainishe waziwazi kwamba kama ilivyo katika maisha halisi 'mtaani' au duniani, heshima haihitaji mtu awe maarufu au wa kawaida. Kwa mantiki hiyo, ninachopigia mstari hapa si kwamba watu wote nilofahamiana nao mtandaoni nimaarufu, au watu wasio na umaarufu hawana faida. Hapana. Kuna maelfu ya watu 'wa kawaida tu' ambao kwa hakika wamenisaidia sana kuwa mtu bora zaidi ya nilivyokuwa kabla ya kufahamiana nao.

`Binafsi, moja ya vitu ninavyovithani ni mno ni utu na unyeyekevu. Kwa bahati mbaya (au pengine bahati nzuri) nilikulia katika familia isiyo na uwezo mkubwa. Sijisifu, lakini laiti nisingekuwa na akili ya darasani basi hata kuhitimu kidato cha nne ingekuwa mgogoro kwani wazazi wangu hawakuwa na uwezo wa kumudu gharama japo kiduchu za wakati ninasaka elimu maana hata ada ya elimu ya O'Level ikuwa mgogoro japo mwanzoni ilkuwa Shilingi 1,500 tu. Kubwa lililonisaidia ni kuishi na watu vizuri, unyenyekevu na heshima kwa kila mtu.

Lakini kibaya nilichojifunza katika maisha yangu mtandaoni ni ukweli usiopendeza kwamba  wengi wa wasumbufu mtandaoni ni wale wasio na moja la kujivunia: wenye umaarufu kutokana na mambo ya ovyo ovyo kama matusi na bullying, na wengine ni wenye kamera zenye IQ kubwa kuliko wao wenyewe  lakini wanahangaika kusaka umaarufu kwa kuwachafua watu waliowazidi kiakili/uwezo kuliko ukoo wao mzima.

Japo yawezekana kuwapo kwa watu maarufu wenye tabia zisizopendeza (japo sijawahi kukutana nao mtandaoni, na hata ningetakana nao ningewakwepa kwa sababu kanuni yangu kuu ni kuthamini utu wa mtu na si vitu alivyonavyo), lakini kwa hao niliofahamiana nao wamewezesha maisha yangu mtandaoni na katika dunia halisi kuwa ya amani na furaha. Uzoefu waonyesha kuwa watu wasumbufu sana, hususan mtandaoni, ni wale wasio na kitu chochote cha maana lakini wanajaribu kuihadaa dunia kuwa 'nao wamo.' Ushauri wangu mwepesi ni huu: kamwe usifuatane na mtu asiye na mwelekeo unless awe mtu anayejielewa kuwa mtaji wake mkubwa licha ya 'kutokuwa na kitu' ni utu wake.

Basi nimalizie makala hii maalum kwa ndugu yangu Ommy Dimpoz kwa kumtakia kila la kheri maishani nikitaraji watu wengine 'wenye majina' watajifunza mengi kupitia unyenyekevu wake ambao nina hakika unachangia sana katika mafanikio yake makubwa. Ninamwombea aendelee kuwa mfano kwa watu wengine maarufu kwa kujali utu kuliko vitu, kuendelea kuwa mnyenyekevu hasa kwa vile unyenyekevu una mvuto zaidi kuliko nyodo, mapozi na tabia nyingine zisizopendeza. 

Na kwa wasumbufu wanaosaka umaarufu kwa kuwasumbua wenzao, sina maneno mazuri wala ushauri wa busara wa kuwaeleza zaidi ya kuwakumbusha kuwa huwezi kumwangusha mtu mwema/bora. Kujuana na watu maarufu hakukufanyi nawe kuwa maarufu. Na hata kama watu maarufu watakuwa karibu nawe kwa 'upuuzi wako' basi ni wazi kuwa umaarufu huo utabaki kuwa kama mapovu, muda si mrefu hupasuka.

Happy birthday Ommy Dimpoz na shout out kwa kila mtu maarufu anayejali utu, mwenye heshima, mnyenyekevu na anayetambua kuwa mtaji mkubwa wa binadamu ni watu- marafiki- kuliko maadui.




Kwa ajali hizi hakuna aliye salama
KWA mara nyingine Tanzania imekumbwa na ‘msiba’ kwa ajali mbaya iliyotokea mkoani Mara na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 30.

Kama nilivyowahi kuandika hivi karibuni, kwa polepole ajali zinazogharimu maisha ya Watanzania wengi tu zinaanza kuzoeleka. Na hili linakera mno.

Kweli, nchi yetu inafahamika kwa kutoyapa uzito wa kutosha matatizo yanayotukabili, na orodha ya ushuhuda katika hilo ni ndefu, na pengine inahitaji kitabu kizima badala ya makala moja kama hii.
Tunaweza kukumbushana kuhusu matatizo mbalimbali yanayotukabili, na ambayo kwa makusudi tumekubali kuyafanya sehemu ya maisha yetu ya kila siku.

Angalia, kwa mfano, tatizo la mgao wa umeme. Hili limefanywa ngonjera na wanasiasa wetu mpaka imefika mahali wameamua kukaa kimya tu. Aidha, wamechoka kudanganya, au wameishiwa na uongo wa kudanganyia, au yawezekana wameona hakuna haja ya kuwadanganya watu wasiojali. Hatimaye mgao wa umeme umekuwa sehemu ya kawaida ya maisha ya Mtanzania, na ukiacha lawama na matusi ya hapa na pale dhidi ya Tanesco, wananchi wengi wanaonekana kulikubali tatizo hilo.

Huko nyuma zilipatikana taarifa kuwa kuna baadhi ya Watanzania wenzetu wameiba mabilioni ya shilingi na kuyaficha katika mabenki nchini Uswisi. Zikaanza porojo, mara mwanasiasa huyu adai atalazimika kuyataja majina ya ‘wezi’ hao iwapo serikali haitofanya hivyo, mara tuambiwe kuna kikosi-kazi kimeundwa kufuatilia suala hilo, mara Takukuru nao waje na ‘uzushi’ wao, na porojo nyingine za kukera kama hizo.

Kilicho bayana ni kwamba hivi sasa suala hilo ni kama limekufa kifo cha asili. Hakuna dalili zozote za watu wanaokerwa na wizi huo wala kushinikiza hatua mwafaka za angalau kurejeshwa kwa fedha hizo kama si kudai hatua za kisheria dhidi ya wahusika.

Ukifuatilia kwa karibu kuhusu tuhuma za ufisadi unaweza kuhitimisha kuwa labda tuhuma mpya huibuliwa makusudi ili kuzima tuhuma zilizotangulia.

Katika mazingira ya kawaida tu, kama wahusika wamekataa katakata hadi leo angalau kutaja jina la mmiliki wa kampuni ya Kagoda iliyokwapua fedha nyingi katika ufisadi wa EPA katika Benki yetu Kuu, iliyopo Tanzania, ni wazi kwamba kutakuwa na uwezekano mdogo kwa wananchi kufahamishwa kuhusu fedha zilizofichwa nje ya nchi.

Tukirejea kwenye janga la ajali, Inasikitisha kuona kwamba taifa limezoea ajali hadi imefika mahala hatuoni umuhimu wa kuwa na siku ya maombolezo.

Labda wahusika hawaoni haja ya kuwa na maombolezo kwa vile wanatambua kuwa kuna uwezekano wa matukio ya ajali zaidi huko mbele, na haitawezekana kuwa na siku za maombolezo kwa kila ajali.
Naam, ni ukweli mchungu lakini usiokwepeka kwamba tutaendelea kupoteza maisha ya Watanzania wenzetu kwa ajali kwa sababu hakuna jitihada zozote za kulikabili tatizo hilo.

Walisema ajali haikwepeki lakini sote tunafahamu kuwa ajali zinazosababishwa na binadamu wenyewe zinaweza kuepukika. Ni rahisi kumlaumu Mungu kwa kudai ‘ajali hizo ni mipango ya Mungu, kwa vile siku yako ikifika huwezi kukwepa kifo’ lakini tutakuwa tunamwonea tu Mungu.

Tunaporuhusu askari wetu wa usalama barabarani wahalalishe rushwa kutoka kwa madereva wanaohatarisha maisha yetu au wanaotumia magari yasiyostahili kusafirisha japo takataka, achilia mbali binadamu, hatuwezi kujidanganya kuwa ‘hiyo ni mipango ya Mungu’ pindi kukitokea ajali.
Binafsi ninaamini kuwa kati ya vyanzo vikuu vya ajali huko nyumbani ni rushwa. Rushwa inawezesha vyombo vya usafiri vibovu kuendelea na safari zake na hivyo kuyaweka maisha ya abiria hatarini, rushwa pia inawezesha madereva wasio na sifa za kuendesha vyombo vya usafiri wa abiria kufanya kazi zao kana kwamba sheria za usalama barabarani zipo likizo.

Lakini kama nilivyowahi kueleza huko nyuma, abiria nao wanaweza kubeba lawama kwa kutotumia ‘nguvu ya umma’ pindi wanapokuwa katika chombo cha usafiri kinachoendeshwa kwa mwendo wa ‘kuita ajali.’

Hivi karibuni, rafiki yangu mmoja amekiri bayana kuwa kati ya sababu zinazomfanya kupendelea usafiri wa mabasi ya kampuni fulani inayofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Dodoma ni ‘mwendo wa kasi wa mabasi hayo.’

Haihitaji kuwa na uelewa mkubwa wa kanuni za fizikia kutambua kwamba mwendo wa kasi unaweza kusababisha ajali kirahisi, na hapo hata tukiweka kando uwezekano wa ajali kutokana na mwendo wa kasi katika basi bovu.

Tuambiane ukweli, wengi wa abiria hupendezwa zaidi na usafiri unaokwenda kasi kuliko wa polepole. Si ajabu kusikia abiria wakilalamika ‘ah dereva huyu anaendesha basi utadhani tumebeba maiti.’ Na dereva akitii kilio cha abiria hao, abiria haohao wanaweza kuishia kuwa maiti!
Kwa vile lawama pekee hazijengi, ni muhimu kwa serikali kuchukua hatua za haraka kukabiliana na janga hili linalozidi kushamiri la ajali za barabarani.

Pamoja na kupambana kwa dhati na rushwa ndani ya kitengo cha usalama barabarani katika Jeshi letu la Polisi, serikali ichukue hatua za haraka za kuboresha njia mbadala za usafiri, hususan wa treni.
Kwa hali ilivyo sasa, abiria anaweza kulazimika ‘kuiweka rehani roho yake’ kwa kupanda basi bovu na linalosifika kwa mwendo wa kasi, si kwa kupenda bali kwa vile hakuna njia mbadala ya kufika aendako.

Ni muhimu kuboresha usafiri wa reli ya kati, sambamba na kuangalia uwezekano wa kufufua au kuanzisha njia mpya za treni kufikia maeneo mengi zaidi ya nchi yetu.

Mwisho, wakati tunaomboleza vifo vya wenzetu zaidi ya 30 vilivyosababishwa na ajali mkoani Mara, ninaomba kuwakumbusha Watanzania wenzangu umuhimu wa kuchukua hatua zilizo ndani ya uwezo wao, kwa mfano, kukabiliana na madereva wanaoendesha magari ya abiria kwa mwendo wa kuhatarisha maisha.

Kadhalika, japo ninatambua ugumu uliopo katika kupata ushahidi dhidi ya vitendo vya rushwa vinavyofanywa na askari trafiki, angalau Watanzania wengi sasa wanamiliki simu zinazoweza kupiga picha au kurekodi video.

Ushahidi wa picha au video pale trafiki anadai au kupokea rushwa kutoka kwa dereva aliyetenda kosa barabarani waweza kuwekwa hadharani kwa mtindo wa ‘name and shame’ au kufikisha ushahidi huo kwa mamlaka husika. Hatua ndogo kama hizo zaweza kuleta mabadiliko makubwa hata kama itachukua muda mrefu.

Tusipojali uhai wetu kwa kupuuzia janga la ajali, tusitarajie miujiza ya kutunusuru

12 Sept 2014

Judge Thokozile Masipa delivers her judgement  in court  in Pretoria, South Africa, Friday, Sept. 12, 2014. Masipa ruled out a murder conviction for the double-amputee Olympian, Oscar Pistorius, in the shooting death of his girlfriend, Reeva Steenkamp, but said he was negligent, and convicted him of culpable homicide

Mwanamama mweusi aliyeendesha kesi ya Pistorius ana historia ya kutia moyo kama ya mwanariadha huyo mlemavu.

Kesi mbili zimemalizika jijini Johannesbugh, Afrika ya Kusini: moja, ya wazi na ambayo dunia nzima ilikuwa ikiifuatilia, ya mwanariadha mlemavu, Oscar Pistorius, aliyekuwa kizimbani kwa kosa la kumpiga risasi mpenzi wake, mrembo Reena Steenkamp, na kumuua, na ya pili ni dhidi ya mwanamke mweusi mwenye miaka 66, Jaji Thokozile Masipa, aliyekuwa na dhamana ya kutoa hukumu katika kesi hiyo iliyovuta hisia za wengi duniani.

Yaliyojiri kwa upande wa Pistorius sote twayafahamu, lakini wengi hawafahamu kuhusu mwanamama Masipa, ambaye licha ya kuangaliwa kwa jicho 'kali' na familia za mwanariadha huyo na ya marehemu Reena, macho ya dunia yaliyokuwa yakifuatilia kesi hiyo nayo yalielekezwa kwake.

Ile kuwa mtu mweusi, achilia mbali uanamke wake, ilikuwa ni mtihani tosha katika nchi ambayo licha ya kumalizika kwa mfumo wa ubaguzi wa rangi bado inaugulia vidonda vya mfumo huo. Kwa mtu mweusi kuwa jaji wa kesi ya 'wazungu' wawili, ni mtihani mkubwa wenye kugusa hisia.

Lakini hata kama Afrika Kusini isingekuwa bado na makovu ya mfumo wa ubaguzi wa rangi, na pamoja na ukweli kwamba nchi hiyo imeendeleza mara kadhaa zaidi ya nchi nyingine za Afrika, bado ipo Afrika na ni nchi ya Kiafrika. Na sote twafahamu mtizamo wetu wa Afrika kwa wanawake. Tukubali, tukatae, wengi wetu tuna kasumba ya kudhani ni wanaume pekee wenye uwezo wa 'kufanya mambo makubwa.' Kwahiyo mtihani mwingine kwa Jaji huyo ulikuwa uanamke wake katika jamii inayomtizama mwanamke kwa jicho la kutokuwa na imani kuhusu uwezo wake.

Mtoto wa kwanza katika familia ya watoto 10, watano kati yao wakiwa marehemu na mmoja aliuawa wa kuchomwa kisu, Masipa alizaliwa katika nyumba ya vyumba viwili katika eneo la mafukara katika kitongoji cha Soweto. Katika utoto wake, alilala sebuleni, na wakati mwingine kulazimika kulala sakafuni jikoni pindi nyumba yao ilipopata ugeni. Japo alikuwa mwenye akili na mwenye malengo ya kimaisha tangu udogoni, alilazimika 'kupoteza muda' kwa kufanya kazi kama housegirl. Ni hadi alipotimiza miaka 20 hivi ndipo alipopata fedha za kutosha kugharamani masomo yake chuo kikuu kusoma digrii ya 'kazi za jamii' (social work).

Baadaye alikuja kuwa mwandishi wa habari, akiwekea mkazo habari za  masuala ya wanawake, na unyanyasaji dhidi wa watu weusi nchini humo.Mwaka 1977 alitiwa nguvuni wakati wa maandamano dhidi ya kukamatwa kwa mwandishi wa habari mwenzie, na mmoja wa askari alimnong'oneza "Leo unakwenda kukutana na Steve Biko," mwanaharakati aliyepigwa na polisi wa Makaburu hadi kuuawa.

Alisalimika, lakini kwa mara nyingine alijikuta akilala tena sakafuni kama alipokuwa mdogo, lakini safari hii ni katika sakafu chafu ya rumande, na kuamriwa kusafisha vinyesi vya mahabusu wengine waliokuwa humo rumande. Alikaidi amri hiyo, na hatimaye kutolewa rumande na baada ya gazeti alilokuwa akiliandikia kumlipia faini.

Baadaye alihamia kwenye taaluma ya sheria, na kuhitimu kama mwanasheria muda mfupi baada ya Nelson Mandela kutoka kifungoni. Ndani ya miaka 10 tangu muda huo, Masipa aliibuka kuwa Jaji mwanadamizi mwanamke mwenye umri mdogo kuliko wote.

Kuhusu kesi na hatimaye hukumu ya Pistorius, ukweli kwamba Afrika Kusini ni moja na nchi zinazoongoza kwa mauaji duniani uliifanya kesi hiyo na hukumu yake ivute hisia za wengi, ndani na nje ya nchi hiyo. Lakini, kama ilivyobainishwa hapo juu, Jaji Masipa pia ni mhanga wa mauaji, ambapo mmoja wa wanafamilia yake aliuawa kwa kuchomwa kisu. Yawezekana kabisa kuwa wakati anaendesha kesi hiyo, alikuwa akirejewa na kumbukumbu za nduguye huyo aliyekuwa mhanga wa mauaji. 

Na kama ilivyokuwa, baada ya hukumu hiyo dhidi ya 'mzungu' Pistorius, mijadala iliyotawala kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja na suala la 'mwanamke mweusi' kutoa hukumu kwa kutumia 'sheria ya mtu mweupe.'

Lakini ukweli unabaki kuwa hukumu aliyotoa Jaji Masipa ilikuwa ya haki, haki haina rangi', wala haibebi vinyongo dhidi ya 'mababu/ mabini makaburu' na kuihamishia kwa 'wajukuu wa makaburu' kama Pisterius. Haki katika hukumu huzingatia ushahidi na uthibitisho iwapo kosa limetendeka au la. Baada ya kuibomoa kesi iliyojengwa na waendesha mashtaka, Jaji huyo alifikia uamuzi kuwa mwanariadha huyo alimuua mpenzi wake bila kukusudia, katika lugha ya kisheria 'culpable murder' au 'manslaughter' kwa hapa Uingereza. 

Ni wazi kwamba baada ya Jaji huyo kuhitimisha kesi kwa kutamka adhabu kwa Pistorius, wengi watamsahau Jaji Masipa. Huenda kesi hiyo ikapelekea kutengenezwa kwa filamu itakayomzungumzia mwanariadha huyo huku kukiwa na uwezekano hafifu wa kuwapo filamu kuhusu kuthibitika kwa umahiri wa Jaji Masipa. 

Hata hivyo, kilicho bayana katika kesi hiyo ni jinsi mwanariadha Oscar Pistorius alivyoweza kuvuka kikwazo cha ulemavu wake na kujitengenezea jina kubwa duniani, na mwanamama mweusi Thokozile Masipa alivyoweza kuvuka vizingiti vya umaskini na mfumo wa kibaguzi na kuibuka msimamizi wa haki katika kesi hiyo ya kihistoria. Kwa hili, ni wazi laiti Mandela angekuwa hai, angejisikia fahari isiyo kifani.

Ni matumaini yangu kuwa historia ya mwanamama huyu-na hata ya Pistorius- itakuwa funzo kubwa kwa wengi wetu ambao katika safari zetu za maisha twakumbana na vikwazo mbalimbali, dhmira thabiti na jitihada zaweza kutufikisha mahala pa kuingiza majina yetu katika historia kama si kubaki katika kumbukumbu kwa jamii zetu.

PENYE NIA PANA NJIA!

Viber5 videocalls 730x608 Viber introduces videos calls to its mobile chat apps for Android and iOS
App ya mawasiliano ya meseji, VIBER, inazidi kupata umaarufu, na sasa inakuja na feature mpya na muhimu ambapo mtumiaji anaweza kumwona anayempigia kwa video, yaani sasa Viber inawezesha video calls kati ya wanaowasiliana.

App hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa 'imeifunika' app maarufu ya mawasiliano ya meseji, Skype, ilinunuliwa hivi karibuni na kampuni kubwa ya biashara za mtandaoni (e-commerce) Rakuten ya Japan  kwa dola milioni 900 imetanua mabawa yake kwa kuwezesha video calls kwa simu za Android na iOS.

Viber ilianza jaribio la video calls katika app yake kwenye desktop lakini sasa imhamishia uwezo huo kwenye app ya simu pia.

Kadhalika, toleo jipya la Viber (Viber 5.0) itamwezesha mtumiaji ku-share contacts kwa kutumia QR Code.

Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Viber Talmon Marco anasema, "Dhamira yetu haijakamilika...Sasa unaweza kupiga simu kwa video kwa kutumia Viber kwenye PC/Mac yako na kwenye simu katika namna ya kukuridhisha kabisa."

Viber sio app ya kwanza ya meseji kuwezesha video calls. Skype, Line, WeChat, Kakao na lundo la apps nyingine zina feature hiyo pia.

Downloads: Viber kwa Android, iOS, Windows Phones, Blackberry, Nokia, Windows 8 na Viber kwenye desktop yako



Nimekutana na makala hii katika gazeti la Mwananchi toleo la Jumanne Septemba 9, 2014 na nimeona ni-share nanyi
Betty Ndejembi ni msichana mrembo na mwanamitindo ambaye anatumia sana huduma za mitandao ya kijamii kwa ajili ya shughuli zake mbalimbali za kujiingizia kipato na kujitangaza zaidi. 

Siku moja alibakwa mpaka akapoteza fahamu, akaokotwa na watu akapelekwa hospitali. Alipofika hospitali aliendelea kutumia mitandao ya kijamii, kwa ajili ya kufahamisha wenzake anavyoendelea kwa nia nzuri kabisa. 

Jinsi alivyokuwa anafahamisha umma kuhusu maendeleo yake, baadhi yao walitumia fursa hiyo kumtukana, kumnyanyapaa, kutumiana picha zake na dhihaka nyingine nyingi kwa njia ya mitandao hiyo hiyo. 

Betty alifariki dunia baadaye wakati anaendelea na matibabu, lakini matusi aliyovurumishiwa, maneno aliyoambiwa na unyanyasaji mwingine, umeleta historia mpya katika matumizi salama ya mitandao ya mawasiliano. 

Jijini Arusha kijana mmoja alikutwa na mke wa mtu, akadhalilishwa huku akipigwa picha. Zile picha zikawekwa kwenye mitandao kadhaa ya kijamii, baada ya siku chache yule kijana alionekana amejinyonga chini ya daraja. 

Huko Marekani dada mmoja anayeitwa Rebecca Ann Sedwick aliamua kujitoa uhai baada ya kudhalilishwa kupitia mtandao wa kijamii. 

Kitendo alichofanyiwa Betty, kijana wa Arusha na huyo mwanadada wa Kiingereza, kinaitwa kitaalamu kwa jina la cyberbulling, yaani mtu kutumia njia za mawasiliano kwa nia ya kuumiza, kudanganya au kumdhalilisha mwingine. 

Vitendo hivi ni kama kutumia picha ambayo mwenyewe hajaruhusu, kuandika habari za uongo hasa za udaku, kuandika au kutoa maoni ambayo si ya kweli kwa nia ya kudhalilisha au kuumiza, kudanganya kuhusu bidhaa au huduma fulani kwa nia hiyo hiyo.
Mimi binafsi niliwahi kukumbana na sakata kama hili, lakini lilimkuta rafiki wa rafiki yangu mmoja. Yeye alikuwa na mpenzi wake, kumbe wakiwa kwenye starehe yule mwanaume alikuwa na tabia za kumpiga picha. 

Siku ikafika hawakuelewana ikabidi kila mtu aendelee na maisha yake, yule kijana akaingia katika mtandao wa kijamii wa facebook akatengeneza jina bandia akaweka picha za yule binti na kuwarushia watu wa karibu wa binti halafu akafuta lile jina. 

Binti alienda kituo cha polisi kutoa taarifa, polisi wakaomba ushahidi wa picha, lakini ndiyo hivyo jamaa alikuwa ameshafuta mpaka jina, kwa hiyo wakaomba msaada, nikawapeleka polisi makao makuu kitengo cha uhalifu wa mtandao. 
Polisi waliweza kupata taarifa zote zinazohusu yule kijana kwenye mitandao ya kijamii na wakaenda kumkamata alipokuwa anaishi wakakagua simu zake, kompyuta na nyaraka nyingine wakapata picha zote kama ushahidi na sasa hivi huyu kijana yuko jela. 

Huko mitaani kuna kina Betty wengi wamezushiwa, wamedhalilishwa, wamepakaziwa na kutengenezewa habari nyingi mbaya na za kuumizwa na watu wanaowajua au kutowajua, lakini wanakaa kimya. Madhara yake ni makubwa. 
Ieleweke kuwa kukaa kwao kimya hakumaanishi kitendo hiki kinakubalika. La hasha hili ni kosa kubwa la jinai ambalo hapa nchini linaanza kuota mizizi. Watu wanatumia mitandao ndivyo sivyo. 
Unachotakiwa kujua ni kwamba mawasiliano yote kuanzia simu na mitandao ya kijamii, hata kama mtu alifuta, kampuni inayotoa huduma husika huwa ina sehemu yake ya kuhifadhi mawasiliano yote. 
Tushirikiane pamoja ili kuweza kumaliza au kupunguza tatizo hili la unyanyasaji, kwa kutumia vyombo vya mawasiliano ili tuweze kuwa na jamii iliyostaarabika.
CHANZO: Mwananchi 


11 Sept 2014

Teknolojia ya kuhifadhi mafaili imetoka mbali, na kwa sasa ipo mbali pia. Zamani hizo, nyenzo kuu ya kuhifadhi mafaili ilikuwa CD-ROM,ambayo hatimaye ilipoteza umaarufu kwa USB Drives ambazo japo kimsingi bado zinatumika kwa wingi lakini umaarufu wake umepungua baada ya ujio wa kinachoitwa 'Cloud storage.' Hii ni teknolojia ya kuhifadhi mafaili 'hewani.' Uzuri wa teknolojia hii upo kwatika urahisi wa kulifikia faili lako kwani huhitaji kutembea na CD-ROM au USB Drive ili u-download faili lako. Kwa kuiba msemo wa mjini, Cloud Storage ndio 'habari ya mujini' kwa sasa.

Kimsingi, teknolojia hii ya kuhifadhi mafaili 'hewani' inahusisha ku-upload faili katika tovuti au app flani, na pili ukilihitaji faili husika basi unachofanya ni kwenda katika tovuti au app husika na ku-download faili hilo popote pale.Kwahiyo unaweza ku-save faili lako kwa kutumia simu kisha ukaweza kuli-download kwa kutumia PC au Tablet yako kwa aida kwenda kwenye tovuti husika au app yenye faili hilo.

Miongoni mwa tovuti/apps maarufu zinazotumia teknolojia ya Cloud storage ni pamoja na OneDrive ya Microsoft.OneDrive imekuwa ikichuana na tovuti/apps nyingine maarufu kama vile Google Drive,










Sasa kuna habari njema, nayo ni kwamba OneDrive imeongeza fursa ya kuhjifadhi mafaili kutoka 2 GB hadi 10GB...bure buleshi. Ifahamike kuwa nyingi  ya huduma hizo za cloud storage hutoa fursa ya wastani tu bure na iwapo mtumiaji atahitaji storage kubwa zaidi hulazimika kulipia.

Natumaini makala hii itakusaidia kupiga hatua katika teknolojia ya uhifadhi mafaili ambapo badala ya kutembea na CD-ROMs au USB Drives kila wakati, sasa waweza ku-upload mafaili yako mtandaoni au kwa kutumia apps za huduma hizo hapo juu (na zipo lukuki mtandaoni) na kuwezesha ku-access mafaili yako mahala popote pale.

10 Sept 2014

Hacked: Hackers revealed nearly 5 million Gmail account details and passwords on the Bitcoin Security site
Takriban passwords milioni tano za akaunti za email za Gmail zimekuwa hacked na kutundikwa kwenye tovuti moja ya hackers wa Russia inayojulikana kama Bitcoin Security. Kufuatia hatua hiyo, kampuni ya Google inayomiliki Gmail imewashauri wenye akaunti za Gmail kubadili passwords zao haraka iwezekanavyo kama hatua ya tahadhari.

Hackers wamesema kwamba asilimia kubwa ya passwords walizo-leak mtandaoni ni za watumiaji wa Gmail nchini Uingereza, Urusi na Hispania, na nyingi ya akaunti hizo 'ziko hai' kwa maana kwamba zinatumika.

Kwa watumiaji wa Gmail watakuwa wanafahamu kwamba mtu akijua password yako ya email anaweza pia ku-access Google Drive na apps kadhaa zinazotumia 'credentials' za ku-log in katika akaunti ya email.

Msemaji wa Google ameeleza kwamba kampuni hiyo inafahamu kuhusu tukio hilo na inawashauri watumiaji wa huduma hiyo kubadili passwords zao.

Kadhalika, Google wanashauri kutumia mbinu inayojulikana kama 'two-steps verification' ambayo kabla ya kuweza ku-access akaunti yako inabidi uingize code uliyotumiwa kwa simu yako.

CHANZO: Habari hii imetafsiriwa kutoka kwa vyanzo mbalimbali mtandaoni




Royal sources made clear that there had been no suggestion from anyone in Government or opposition for the Queen to take a public stand
Malkia Elizabeti wa Pili, mtawala wa 'Muungano wa Uingereza' (United Kingodm) ametanabaisha kuwa kamwe hatoingilia hatma ya kura itayoamua iwapo Uskochi iendelee kuwa sehemu ya 'Muungano wa Uingereza' ua iwe taifa huru.

Hatua hiyo ya nadra imetokana na maoni ya baadhi ya wabunge hapa Uingereza kwamba Malkia aingilie katik katika suala hilo.

Waziri Mkuu (First Minister) wa Uskochi anaweza kuingia matatizoni baada ya kauli yake jana kwamba alikutana na Malkia na akaambiwa kuwa mwanamama huyo yupo tayari kuwa Malkia wa Uskochi iliyo huru.

Lakini makazi ya Malkia ya Buckingham Palace yameweka bayana msimamo kwamba Malkia hajihusishi na siasa na walio katika nyadhifa za kisiasa wanapaswa kuhakikisha hali hiyo inabaki hivyo.

Vynazo vimethibitisha kuwa Malkia siku ya kupiga kura- tarehe 18 mwezi huu- Malkia Elizabeth atakuwa katika makazi yake ya faragha kwenye ukanda wa Nyanda za Juu wa Uskochi (Scottish Highlands)

Japo makazi ya Malkia yamesisitiza kuwa mtawala huyo haingilii masuala ya kisasa lakini wachambuzi wanaeleza kuwa huhitaji kuwa mtaalam wa siasa kumaizi kuwa Malkia anatamani 'Muungano wa Uingereza' uendelee, na kutumia swali la kuamsha tafakuri la 'Hivi Baba Mtakatifu (Papa) ni Mkatoliki? (kwa maana ya kuwa ili mtu awe Papa shurti awe Mkatoliki)

CHANZO: Habari hii imetafsiriwa isivyo rasmi kutoka tovuti ya gazeti la Daily Mail la hapa Uingereza

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.