24 Aug 2014

Leaving: Brown is seen walking to his Lamborghini after the drama at 1Oak in Los Angeles
Chris Brown akielekea kwenye Lamborghini lake kuondoka katika klabu ya usiku palipotokea shambulio la risasi
Prodyuza Marion Suge Knight (pichani chini) amejeruhiwa kwa risasi amejeruhiwa kwa risasi katika shambuli lililotokea katika pati iliyokuwa ikiendeshwa na msanii Chris Brown.
Music producer Suge Knight has been injured during a shooting at an awards show party at a Los Angeles nightclub hosted by singer Chris Brown, it has been reported
Mashuhuda wanaeleza kuwa msanii huyo ambaye bado yupo katika msamaha wa uchungu (parole) baada ya kutoka jela hivi karibuni ndiye alikuwa mlengwa wa shambulio hilo, ambapo alikuwa MC wa pati ya utangulizi wa Tuzo za Video za Muziki (MVA) zitakazofanyika leo usiku (kwa saa za Marekani).
OK now: Brown smiled as he left the nightclub where he was reportedly targeted by a gunman
Inadhaniwa kuwa Chris hakuumia katika shambulio hilo, lakini watu wengine watatu, akiwemo Suge Knight, mwanzilishi wa lebo ya muziki ya Death Row Records iliyokuwa ikitumiwa na msanii mwingine maarufu wa nchi hiyo, Marehemu Tupac Shakur, walijeruhiwa na kupelekwa hospitali ya Cedar's Sinai. Inaelezwa kuwa mmoja wa majeruhi hao yupo taabani.
Witnesses: Partygoers talk to emergency personnel after the shooting 
Mwanamitindo na mcheza filamu Tyson Beckford na memba wa kundi la Black Eyees Peas Apple De Ap walikuwa miongoni mwa waliohudhuria pati hiyo, na walieleza kuwa walisikia sauti nne za risasi mida ya saa 7.30 alfajiri ya kuamkia leo.
Treatment: Another victim is fitted with a neck brace following the dramatic shooting
Majeruhi akitibiwa
Suge Knight ambaye kwa sasa anamiliki kampuni ya muziki ya Black Kapital Records alionekana na polisi  nje ya ukumbi baada ya shambulio hilo na akachukuliwa katika gari la kubeba wagonjwa. Inaelezwa kuwa alipigwa risasi mbili, na kujeruhiwa tumboni na mkononi na sasa anafanyiwa upasuaji.
Host: Brown enjoys the party before the alleged shooting took place
Chris Brown 'akijirusha' kabla ya shambulio
Waliofanya shambulio hilo walikamatwa na polisi ambao sasa wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Mastaa wengine waliokuwa kwenye pati hiyo ni pamoja na Justin Beiber na rapa The Game.
Guests: Justin Bieber (right) was among the guests at the VMA Pre-Party hosted by  Brown
Justin Beiber alikuwa miongoni mwa waliohudhuria pati hiyo, kama ilivyokuwa kwa rapa The Game (pichani chini)

Jayceon Terrell Taylor, aka The Game attends a VMA Pre-Party hosted by Chris Brown and Pia Mia
Iliposikika milio ya risasi hizo, Chris Brown alionekana akiruka kuelekea kwenye eneo la baa katika klabu hiyo ya usiku (nightclub), huku kwa hasira akiwaagiza watu wengine kujikinga.
Aftermath: Brown jumped on a table after the shooting, apparently furious at what had taken place
Chrsi Brown akiruka kuelekea eneo la baa baada ya milio ya risasi
Saa 12 kasorobo asubuhi ya leo, msanii huyo alitwiti


Akimaanisha 'Jamii haiwezi kustarehe au kuburudika pasipo mikwaruzo.'
Injured: Another victim is transferred into an ambulance in a stretcher
Majeruhi wakiingizwa kwenye gari la kubebea wagonjwa
Angry: Brown at first appeared to still be furious when he made his way from the West Hollywood club
Chris Brown akiwa ametahayari baada ya shambulio hilo



CHANZO : The Mail Online




Smart mannequins that ¿talk¿ to shoppers through their smartphones will go live today in branches of House of Fraser, Hawes & Curtis and the Bentalls department store

Tafsiri: 1. Duka la nguo linaingiza mtandaoni taarifa kuhusu bidhaa husika.

2. Mteja anapaswa ku-download app iitwayo Icneme katika simu yake ili kuwezesha connection ya Bluetooth.

3. Mteja akipita futi 150 karibu ya duka husika, anapata ujumbe katika simu yake, na sasa anaweza kupata taarifa kamili ya nguo husika ilivyovaliwa na mdoli (mannequin) wa maonyesho ya nguo dukani.

4. App iliyomo kwenye simu ya mteja itamwonyesha malili ilipo nguo husika ndani ya duka husika. Pia itampa kiungo (link) ya tovuti ya duka hilo kumwezesha kuinunua nguo hiyo katika muda wowote ule, iwe mchana au usiku.


Kaleem, a keen cricketer, said the teachers at his school have told him other children are 'scared' of his hands

Doctors in India have been left baffled by his growing hands and many are at a loss as to what the condition is

The youngster has difficulty eating, tying his shoelaces and carrying out other basic tasks due to his  hands

Kaleem's father Shamim, 45, (pictured together above) is worried his son will never become independent

Kaleem, from India, was born with hands twice the size of an average baby and they have continued to grow

Mtoto wa miaka minne nchini India, Kaleem (pichani) amewachanganya madaktari kufuatia mikono yake kuvimba kupita kiasi na sasa imefikia uzito wa kilo 12. Mtoto huyo kwa sasa anashindwa kutekeleza japo majukumu madogo tu kama kufunga 'kamba' (laces) za viatu vyake baada ya kuzaliwa akiwa na mikono mikubwa mno.

Kaleem anadai amekuwa akibughudhiwa mno na watoto wenzie wanaomcheka kutokana na maumbile hayo ya ajabu. "Napata mguu kuvaa nguo zangu, kufunga vifungo hata kuvaa nguo ya ndani, anasema mtoto huyo ambaye mama yake alibaini maradhi yake tangu akiwa mdogo lakini hakuwa na cha kufanya kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha. Wazazi wa Kaleem wana kipato kisichozidi Paundi za Kiingereza 15 (takriban Tsh 42,000) kwa mwezi.

Baba yake, Shamim, anahofu mwanae hatoweza kujitegemea maishani, na anajilaumu kwa kushindwa kumhudumia kutokana na uwezo duni wa kifedha. Dr Ratani, mkurugenzi wa kituo cha afya kilichomfanyia uchunguzi mtoto huyo anakiri kuwa maradhi hayo ni ya ajabu na magumu kutibika. 

CHANZO: The Mail Online



 Only men who suffered impotence as a side effect of illness or those evaluated by a specialist could be given the pills on the NHS
Mamia kwa maelfu ya wanaume hapa Uingereza wanatarajiwa kunufaika na uamuzi wa Taasisi ya Huduma za Afya (NHS) kulegeza masharti ya upatikanaji wa vidonge vya kuboresha nguvu za kiume, Viagra.

Hadi mwezi huu, watu pekee walioruhusiwa kupewa Viagra hospitalini ni wale ambao pungufu wa nguvu zao za kiume ulitokana na athari za matibabu ya maradhi mengine (side effects).

Lakini tangu taratibu za usajili na upatikanaji (patent) ya Viagra ilipoisha muda wake mwaka jana, bei ya vidonge hivyo imeshuka kwa asilimia 93 kwa vile makampuni mengine ya madawa yameruhusiwa kutengeneza aina zisizo asili (generic) za vidonge hivyo.

Kutokana na hali hiyo, NHS imeeleza kuwa watu wote wenye matatizo ya nguvu za kiume wanaruhusiwa kupata Viagra. Madaktari wengi wamefurahishwa na uamuzi huo wakiamini kuwa utasaidia kuboresha mahusiano ya kinyumba na hata kuokoa ndoa.

Hadi 'patent' ya Viagra inakwisha muda wake, Viagra ilikuwa ikiuzwa kwa Paundi za Kiingereza 21.27 (Tsh 58,567.39) kwa pakti ya vidonge vinne lakini bei hiyo sasa imeshuka hadi Paundi .1.45 (Tsh 3,992.61)kwa pakti moja ya vidonge vinne.



22 Aug 2014

Ijumaa ya leo imekuwa siku ngumu sana kwangu. Rafiki yangu mmoja wa karibu, mhamiaji kutoka Ireland ya Kaskazini aliyehamia hapa Uskochi, anajiandaa kwa ajili ya upasuaji wa moyo hapo Jumatatu. Leo tumeonana 'kwa mara ya mwisho' kwa vile atatumia wikiendi hii kujaindaa na upasuaji huo, na wiki Ijayo ndo shughuli yenyewe.

Nimepata wakati mgumu sana kuagana nae jioni hii wakati anaelekea nyumbani kwake nami narudi kwangu. Japo aliniaga kwa kujiamini kuwa tutaonana Jummatano ijayo, lakini hali ya uoga iligubika ujasiri wake, na kwa hakika almanusra niangushe chozi. 

Huyu bwana alipatwa na mshtuko wa moyo miezi kadhaa iliyopita. Naikumbuka vema siku hiyo. Tulipokutana asubuhi baada ya kuwasili kazini alionekana anatoka jasho japo siku hiyo ilikuwa ya baridi kali. Muda mfupi baadae alionekana anapumua kama mtu aliyekimbia umbali mrefu, na muda mfupi baadaye akaanguka na kupoteza fahamu. Tuliita gari ya kuhumia wagonjwa, na akakimbizwa hospitalini haraka. Kwa mujibu wa maelezo yake mwenyewe, alikuwa kama amekufa kwa masaa kadhaa. Lakini kubwa lililosaidia kuokoa uhai wake ni huduma ya kwanza tuliyompatia wakati tunasubiri gari la wagonjwa, vinginevyo moyo wake ungezimika moja kwa moja.

Alikaa hospitalini kwa wiki kadhaa na huko walimwekea mashine inayousaidia moyo wake kufanya kazi zake kwa ufanisi. 

Sasa upasuaji atakaofanyiwa Jumatatu ijayo ni kwa ajili ya uchunguzi mkubwa wa jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi.Ikumbukwe kuwa mashine hiyo inafanya kazi kuusaidia moyo, na kwahiyo moyo wake bado unafanya kazi japo ni kwa msaada wa mashine hiyo iliyowekwa juu kidogo ya moyo wake, kifuani.

Kitakachofanyika Jumatatu ni kilekile walichomfanyia wakati wanaweka mashine hiyo, yaani watatumia kompyuta kufanya kazi ya moyo, na kisha kuusimamisha moyo, na kwa wakati huo uhai wake utakuwa unategemea kompyuta hiyo. Wataitoa mashine waliomwekea mwilini na kuisafisha, sambamba na kuichunguza. Kadhalika, moyo wake nao utafanyiwa uchunguzi wa kina. Yote hayo yatatokea wakati uhai wake unategemea kompyuta inayofanya kazi ya moyo.

Japo upasuaji huo haumaanishi kifo lakini kuna uwezekano-japo si mkubwa- wa moyo kurejeshwa mwilini na ukagoma kufanya kazi kama awali. Kadhalika, ile mashine inayousaidia moyo nayo inaweza kugoma 'kuwajibika ipasavyo.' Lakini cha kutisha ni ukweli kwamba wakati upasuaji huo unafanyika, rafiki yangu huyo atakuwa kama amekufa- kwa maana ya kazi zinazofanywa na moyo wa asili kutegemea msaada wa kitu cha nje- in this case ni hiyo kompyuta. Yaani kwa lugha nyingine ni kama mtu anayepumulia mashine, ikizimwa, yaweza kuwa ndio mwisho wa uhai wake.

Wakati tunaondoka eneo la kazi, rafiki yangu huyo alisema waziwazi kuwa muda huo ndo unaweza kuwa wa mwisho kwa yeye kuwepo hapo. Japo aliongea kwa utani lakini uwezekano huo upo japo si mkubwa. Teknolojia ya matibabu ya moyo imepiga hatua kubwa sana lakini si ya uhakika wa asilimia 100.

Kwangu, nabaki kumfanyia sala, upasuaji huo ufanyie salama, na tukutane tena Jumatano kama alivyoahidi mwenyewe. Nina imani na teknolojia ya matibabu ya hawa wenzetu lakini ukweli kwamba kiungo muhimu kama moyo kitasimamishwa na kazi yake kufanywa na kompyuta inanipa msisimko wa uoga. Na hilo limeonekana hata kwa 'mgonjwa' mweyewe.'

I thought si vibaya ku-share stori hii ya kuogofya ambayo inanigusa kwa kiasi kikubwa. Kwa nman flani yanikumbusha jinsi nilivyompoteza mama yangu mpendwa, ambaye nae kama ilivyo huyo rafiki yangu alipatwa na mshtuko wa moyo, akapoteza fahamu, na fahamu hazikumrejea tena hadi anafariki Mei 29, 2008.

Natumaini msomaji mpendwa utaungana nami kumwombea rafiki yangu huyo upasuaji atakaofanyiwa uwe wa mafanikio na aendelee kuishi salama. Nitawafahamisha kilichojiri Jumatano ijayo.

Asanteni

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.


21 Aug 2014

Naomba kukiri hadharani kwamba katika mitandao yote ya jamii, Twitter ndio namba wani kwangu. Mtandao huo sio tu umeniwezesha kufahamiana na watu muhimu kabisa, bali pia ni moja ya vyanzo vyangu vikuu vya habari na uelewa. Nitaanda makala maalum ya kukufahamisha msomaji jinsi ninavyoitumia Twitter kwa ufanisi, na jinsi inavyoweza kukidhi mahitaji yangu.

Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakiilaumu kwa mapungufu wanayokutana nayo. Kwa mfano, nimesikia kwa watu kadhaa wakiilaumu Instagram kwamba imegeuka uwanja wa matusi. Jamani, tatizo sio Instagram, Twitter, Facebook au mtandao mwingine wowote ule wa kijamii bali tatizo ni mtumiaji. Kama ilivyo mtaani, ukikaa kijiweni utaambulia ya kijiweni. Ukitumia muda wako mwingi maktaba, utaweza kupata vya kupatikana maktaba. Uki-hang out na walevi, well, twajua ni utapata. Ukipendelea kuwa na watu wa Neno la Mungu, utapata Neno la Mungu. Ukijiweka karibu na wasomi, utafaidika na uelewa (knowledge). Ukifuatilia vyombo vya habari, utahabarika. 

Msanii maarufu wa muziki na filamu nchini Marekani, Tyrese Gibson, anatoa ushauri huu 

Employees hanging out with employees is just going to further your career as an employee. You start hanging out with bosses, you eventually become one. (Mwajiriwa anayetumia muda mwingi na waajiriwa wenzie wa kawaida, atadumisha ajira yake kama mwajiriwa wa kawaida tu.Ukianza 'kujichanganya na mabosi, basi nawe waweza kuishia kuwa bosi)
Naam, watu unaojihusisha nao wanachangia kukufanya kuwa mtu wa aina flani. Na kanuni hiyo ina-apply pia kwenye mitandao ya jamii. Uki-follow watu wenye kuendekeza matusi au majungu, utaishia kukutana na matusi au majungu. 

Basi hapa chini ninakupatia orodha ya maprofesa waliobobea katika fani zao ambao wapo Twitter, na waweza kuwa-follow au  kuwaingiza katika LIST yako (nitaandaa makala ya jinsi ya kutumia 


Uongozi (Leadership)
Bill GeorgeHarvard Business School, @Bill_George

Adam GrantWharton School of Finance, @AdamMGrant
Monique ValcourEDHEC, @MoniqueValcour
Karl MooreMcGill University, @ProfKJMoore
Gianpiero PetriglieriINSEAD, @GPetriglieri
Stew FriedmanWharton School of Finance, @StewFriedman
Sir Cary Cooper, Lancaster University, @ProfCaryCooper
CV HarquailHowe School of Business, @CVHarquail
Bret SimmonsUniversity of Nevada-Reno, @DrBret
Mark EspositoHarvard University, @Exp_Mark
Ian McCarthyBeedie School of Business, @Toffeemen68
Gautum MukundaHarvard Business School, @GMukunda
Thomas RouletUniversity of Bath, @ThomRoulet
Terri GriffithSanta Clara University, @TerriGriffith
Patrick J. MurphyDePaul University, @ProfPJM

Ubunifu (Innovation)

Richard FloridaRotman School of Management, @Richard_Florida
Clayton ChristensenHarvard Business School, @ClayChristensen
Calestous JumaHarvard University, @Calestous
Alf RehnÅbo Akademi University, @AlfRehn
Marcel BogersUniversity of Southern Denmark, @Bogers
Cyndi BurnettBuffalo State College, @CyndiBurnett
Diego RodriguezStanford University @Metacool
Bob SuttonStanford University, @Work_Matters
Karim R. LakhaniHarvard Business School @KLakhani
Tim KastelleUniversity of Queensland, @TimKastelle
Tor GronsundUniversity of Olso, @Tor
Frank PillerRWTH Aachen University, @MassCustom
Tina SeligStanford University, @TSeelig
Bill FischerIMD Business School, @Bill_Fischer
Gary HamelLondon Business School, @ProfHamel

Mikakati (Strategy)

Michael PorterHarvard Business School, @MichaelEPorter
Estelle MetayerMcGill University, @Competia
Ioannis Ioannou, London Business School, @iioannoulbs
Rita McGrathColumbia Business School @RGMcGrath
Teppo FelinUniversity of Oxford, @TeppoFelin
Roger Martin, Rotman School of Management, @RogerLMartin
Peter G. KleinUniversity of Missouri-Columbia, @PeterGKlein
Mislek Piskorski Harvard Business School, @MPiskorski
Kevin BoudreauLondon Business School, @KevinJBoudreau
Sheen S. LevineColumbia University, @SSLevine
Freek VermeulenLondon Business School, @Freek_Vermeulen
Marion Debruyne, Vlerick Business School, @MarionDebruyne
Robin TeiglandStockholm School of Economics, @RobinTeigland
Dan Elfenbein, Washington University, @OrgStratProf
Sydney FinkelsteinTuck School of Management, @SydFinkelstein

Watajwa wa heshima (Honorable Mentions)

Terry Linhart, Bethel College,@ TerryLinhart
Teresa AmabileHarvard Business School @TeresaAmabile
Terri ScanduraUniversity of Miami, @TerriScandura
Michael RobertoBryant University, @MichaelARoberto
Nadia KazimHigher Colleges of Technology @Nadiakazim

Wasomi hawa mahiri duniani ni visima vya uelewa (knowledge). Na kama sote tunavyoelewa, ili uweze kuchota maji kutoka katika kisima shurti uende kisimani.

Basi endelea kutembelea blogu hii kwa habari mbalimbali, ikiwa ni pamoja na hizi za teknolojia. Bonyeza TEKNOLOJIA hapo kwenye menu juu upelekwe moja kwa moja kwenye habari hizo.


Mwenyekiti wa UKAWA, Freeman Mbowe
‘UKAWA waapa kutorudi bungeni’;
‘Katiba mpya kupatikana bila UKAWA;
Safu hii haitoshi kuorodhesha vichwa vya habari vinavyotawala vyombo mbalimbali vya habari kuhusu sakata linaloendelea kuhusu Katiba mpya.
Ukifuatilia mijadala mbalimbali ya Watanzania kuhusu suala hilo, hasa katika mitandao ya kijamii, utaona masikitiko waliyonayo, hasa kwa vile mchakato mzima wa kupata Katiba mpya umeshagharimu mabilioni ya shilingi.
Lakini pengine Watanzania wengi ni watu wa kuishi kwa matumaini kuliko kuishi kwa kuzingatia hali halisi. Hakuna ubaya kuwa na matumaini lakini ni vema kuwa na matumaini yanayoendana na hali halisi.
Nisingependa kurejea jinsi Bunge Maalumu la Katiba lilivyoanza kwa ‘kwikwi’ lakini tunachoweza kukumbushana ni pamoja na sura za wateuliwa wa Rais kama wawakilishi wa makundi mbalimbali ya jamii.
Wengi wa wateuliwa walikuwa watu wenye ‘ukaribu na chama tawala, CCM,’ na hilo tu lilitosha kuonyesha kuwa hatma ya upatikanaji wa Katiba mpya ingekuwa na mushkeli.
Lakini kosa jingine lilikuwa ‘kuwahamisha’ wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuwa wajumbe ‘wa moja kwa moja’ wa Bunge Maalumu la Katiba. Nadhani hakuna Mtanzania asiyefahamu mapungufu mengi yanayolikabili Bunge letu la Muungano, na uamuzi wa ‘kuwahamisha’ wabunge wa Bunge hilo katika Bunge la Katiba ulikuwa sawa na kuhamishwa matatizo mapya.
Kwa mtizamo wangu, Bunge letu la Muungano ni miongoni mwa taasisi zisizowatendea wananchi kwa kiwango kikubwa.
Japo kila kikao cha Bunge hilo kinapoanza utakutana na vichwa mbalimbali vya habari magazetini, kama vile ‘Bunge kuwaka moto,’ ukweli mchungu ni kuwa moto pekee unaowaka ni wa kutafuna fedha za walipakodi.
Kwa kiasi kikubwa Bunge letu limegeuka uwanja wa matusi, mipasho, uhuni, na kila jambo linalokera. Badala ya kutekeleza majukumu yake muhimu kama kutunga sheria, taasisi hiyo imekuwa mstari wa mbele kuvunja sheria.
Kadhalika, Bunge letu limepoteza kabisa umuhimu wa mgawanyo wa madaraka katika ya serikali (kwa maana ya executive), Bunge na Mahakama, kwa sababu limekuwa kama muhuri wa kupitisha matakwa ya serikali.
Kwa kutumia wingi wa wabunge wa CCM, Bunge hilo likipitisha takriban kila hoja inayoletwa na serikali ya chama hicho. Pengine hiyo si dhambi bali tatizo ni ukweli kwamba kubwa lililowapeleka wabunge hao wa CCM bungeni ni kuwawakilisha wananchi pasi na kujali itikadi za vyama vyao. Katika mazingira ya kawaida tu, maslahi ya nchi (kwa maana ya wapigakura) yanapaswa kupewa kipaumbele zaidi ya maslahi ya kiitikadi.
Na tatizo hilo la wingi wa wabunge wa CCM katika Bunge la Muungano kutumika vibaya ni miongoni mwa vikwazo vya ufanisi katika Bunge Maalumu la Katiba. Badala ya kuangalia Katiba mpya kama suala lenye umuhimu mkubwa kwa Taifa, wajumbe wa Bunge la Katiba wanaotokana na ubunge wa chama hicho, wakishirikiana na wajumbe wa kuteuliwa na Rais ‘ wenye mahusiano’ na CCM, wameligeuza suala la kichama.
Sasa sijui matumaini waliyonayo Watanzania wengi kwa Bunge hilo yanatoka wapi.
Tukija kwenye sakata la Umoja wa Katiba ya Wananchi, UKAWA kususia Bunge la Katiba, binafsi ninaona tupo njia panda: wakirejea bungeni tutaendelea kushuhudia matusi, vijembe, na upuuzi mwingine na pengine tukirudi kulekule kulikosababisha UKAWA kususa.
Wakiendelea kususa kinachoendelea huko Dodoma kitakuwa ni kupoteza tu fedha za walipakodi, na hata wakifanikiwa kupata idadi ya kura zinazohitajika kupitisha vifungu vya Rasimu ya Katiba mpya, basi litakuwa ni suala la kulazimisha na linaloondoa uhalali wa zoezi hilo zima.
Hata tukiafikiana kwa minajili tu ya makala hii kwamba UKAWA wanaweza kurejea katika Bunge la Katiba, ni vigumu mno kudhani kuwa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, ataacha upendeleo wake kwa wana-CCM wenzie.
Kadhalika, ni vigumu zaidi kutarajia kwamba UKAWA wakikubali kurejea katika Bunge hilo, ghafla kutopatikana mwafaka wa kuacha matusi na vijembe na badala yake kuweka kipaumbele kwa mustakabali wa Katiba mpya na Taifa kwa ujumla.
Sana sana tutachoshuhudia ni hotuba ndefu za ‘wajumbe wa CCM’ kuwasema wenzao wa UKAWA, kutonesha majeraha ambayo hata hayajaanza kukauka, na hatimaye uwezekano mkubwa ni kwa wana-UKAWA kususa tena.
Na huko ‘mtaani’ kumeanza tetesi kwamba hata tishio la ugonjwa hatari wa ebola limeanza kutumika kwa minajili ya kufanya ‘usanii’ katika mchakato wa kupata Katiba mpya.
Tetesi nyingine ni taarifa zilizojitokeza mwishoni wa wiki iliyopita kuhusu ‘ugaidi wa CHADEMA,’ zilizotolewa na mwanachama wa zamani wa chama hicho cha upinzani, Habib Mchange.
Inasikitisha sana kuona fursa hii adimu ya kutengeneza mustakabali mwema wa Taifa inafanyiwa uhuni. Kuna wenzetu wasiotaka kabisa kuiangalia Tanzania yetu zaidi ya muda tulionao. Baadhi ya wenzetu hawa wana watoto na wajukuu lakini ubinafsi wao unawatia upofu wa kutengeneza mazingira mema kwa vizazi vijavyo.
Kwa mara ya kwanza nimejikuta nikiunga mkono ushauri uliotolewa na mwanasiasa ambaye kwa muda mrefu nimekuwa nikimwona kama kikwazo cha kupatikana ‘mwafaka wa kitaifa’ katika jambo lolote lile.
Hapa ninamzungumzia Mwigulu Nchemba, ambaye hivi karibuni alitoa wito wa kuangalia uwezekano wa kusitisha Bunge Maalumu la Katiba hadi utapopatikana mwafaka na UKAWA.
Lakini ‘sauti za busara’ za watu kama Mwigulu haziwezi kusikika wala kufanyiwa kazi, kama ilivyojitokeza kwa kiongozi mwingine wa CCM, Nape Nnauye, kupinga vikali wazo hilo la kuahirisha Bunge la Katiba, hoja yake kuu ikielemea kwenye mtizamo fyongo kuwa CCM ndio Tanzania.
Nimalizie kwa ‘kubahatisha’ kuomba busara itumike ili kumaliza sintofahamu inayoendelea kuhusu Katiba mpya.
Ni vema tukakubali kujifunza katika makosa yaliyotufikisha hapa, na pia kukubali kuwa ‘tumeliwa’ kwa maana ya gharama tulizokwishaingia kutafuta Katiba mpya, na kisha tuahirishe mchakato huo hadi mazingira yatakaporuhusu kujadili suala hilo nyeti.
Ubabe wa kulazimisha Katiba mpya waweza kuipeleka Tanzania yetu kubaya zaidi ya tulipo hivi sasa.
Ndiyo, twaambiwa na Mwanasheria Mkuu Jaji Werema kuwa Rais Jakaya Kikwete hana mamlaka ya kuvunja Bunge Maalumu la Katiba.
Lakini kwa hakika yawezekana Bunge lenyewe la Katiba kufikia mwafaka kuwa halina uhalali wa kuendelea na vikao vyake, au hata vikiendelea litaishia ‘kuzaa’ matokeo ya kulazimisha.
Ni bora tuchelewe kupata Katiba mpya lakini tutapoipata iwe kwa maslahi na hatma ya Taifa kuliko kutumia ubabe kulazimisha suala hili ambalo ni wazi limeshindikana.
Penye nia pana njia. Mungu Ibariki Tanzania

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.