15 Jul 2016

Anaitwa Karrima Carter, mwanadada mwenye asili ya Tanzania mwenye makazi yake hapa Uingereza. Kwa miaka kadhaa amekuwa akijitolea kukusanya misaada mbalimbali kwa ajili ya kuyasaidia makundi yenye uhitaji huko Tanzania. Tayari ametoa misaada kwa shule mbalimbali za msingi na sekondari katika maeneo mbalimbali ya Tanzania, anaendesha vituo vya kulea watoto yatima na kusaidia wazee. 

Tukio hili pichani ni mfululizo wa matukio anayofanya kabla ya kuelekea Tanzania wiki ijayo kukabidhi misaada kadhaa kwa makundi mbalimbali yenye uhitaji, ikiwa ni pamoja na kuambatana na wahisani kutoka hapa Uingereza kwenye hafla kwenye kituo cha yatima huko Bagamoyo, sambamba na uzinduzi wa vyoo kadhaa katika shule ya msingi Ilala.

Blogu hii inafuatilia kwa karibu jtihada za mwanadada huyu hasa ikizingatiwa kuwa kuna makundi mengi yenye uhitaji huko nyumbani ilhali suala la kujitolea bado halijapata mwamko miongoni mwa Watanzania wengi. 

Chini ni baadhi ya picha za kikundi cha watoto wa Kiingereza walioshiriki katika shughuli hiyo kwa 'kujipaka rangi usoni' (face painting) na kuigiza tamthilia maarufu ya Simba the Lion kwa lugha mbalimbali ikiwa pamoja na Kiswahili. Licha ya kushiriki kukusanya michango, watoto hao pia wanachangia kuwasaidia watoto wenzao huko Tanzania, kwa uratibu wa Karrima.

Waweza kuangalia video mbalimbali kwenye ukurasa wake wa Facebook HAPA au kwenye akaunti yake ya Instagram HAPA.















Uchambuzi wangu wa kiintelijesnia kuhusu shambulio la kigaidi lililotokea jana usiku katika jiji la Nice, nchini Ufaransa ambapo hadi sasa watu 84 wameuawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa baada ya gaidi mmoja kuliingiza lori kwenye kundi la watu waliokuwa wakisherehekea siku ya kitaifa nchini humo. Bonyeza hapo chini kusikiliza uchambuzi huo

Check this out on Chirbit

10 Jul 2016


Check this out on Chirbit

8 Jul 2016

Ilikuwa masaa, siku, wiki, miezi na sasa mwaka. Ni vigumu sana kuamini kuwa baba umeondoka moja kwa moja. Kila siku nakumbuka, lakini kuna kitu kingine kinachonikumbusha kila wiki: makala zangu katika gazeti la Raia Mwema. Ulikuwa 'shabiki nambari wani' wa safu yangu katika gazeti hilo, na ulihakikisha unasoma kila toleo la gazeti hilo.

Pamoja na mengi uliyotuachia wanao, moja ninalofanya kila siku ni kusoma na kuandika, vitu viwili ulivyonisisitiza mno tangu nikiwa mtoto mdogo. Na kwa hakika kama ulivyopenda sana kusoma na kuandika, ndivyo ambavyo kwangu vitu hivyo vimekuwa sehemu muhimu ya maisha yangu ya kila siku.

Pia wewe na marehemu mama mlinisisitza mno kuhusu umuhimu wa elimu.Nawashukuru sana mlivyojinyima ili kuhakikisha ninatimiza ndoto zangu za kielimu. Ninasikitika kwamba wakati wewe na mama mlikuwa na kiu sana ya kuniona nahitimu shahada ya uzamifu (PhD), kwa bahati mbaya nyote mmeondoka kabla sijahitimu. Hata hivyo, nime-dedicate thesis yangu kwenye.

Nakushukuru pia wewe na marehemu mama kwa kutuhimiza mno watoto wenu kuhusu upendo, kuthamini utu na kubwa zaidi, kumtanguliza Mungu katika kila tufanyalo. Upendo wako baba ulikufilisi mapema mara baada ya kustaafu mwaka 1981, ambapo mipango yako ya kuwekeza katika kilimo ilizidiwa nguvu na moyo wako wa kuwasaidia ndugu na jamaa pale Ifakara. 

Miaka kadhaa baadae, marupurupu yako ya utumishi wako katika Jumuiya ya Afrika Mashariki nayo yaliishia kwenye kuwasaidia ndugu, jamaa na marafiki. Siku zote ulikuwa unasisitiza kuwa utu ni muhimu ziadi kuliko vitu (including pesa). 

Iliniuma mno kushindwa kuja kukuaga katika safari yako ya mwisho. Lakni nakumbuka sana maeneo yako kuwa "lolote likinitokea, hakikisha kwanza usalama wako..." Wewe baba na marehemu mama siku zote mlikuwa mnahofia kuhusu kazi niliyokuwa naifanya lakini kwa vile mlinipenda mno, mlikuwa mkiniombea kila siku ya Mungu.

Kama kuna kitu kinaniumiza mno ni mapacha Kulwa (Peter) na Doto (Paul). Kwa vile wao walizaliwa wakati umri umeshawapita mkono nyie wazazi wetu, mapacha hawa walikuwa kama wajukuu zenu. Lakini kubwa zaidi, walikuwa ndio marafiki zenu wakubwa. Kila ninapoongea nao najiskia uchungu sana kwa sababu sio tu wamepoteza wazazi lakini pia wapoteza their best friends. Ninaendelea kuwasapoti ili wasielemewe na huu uyatima tulionao.

Kama kuna kitu kimoja nilikuangusha mno ni kutofuata matakwa yako nijiunge na seminari ya Kasita baada ya kuwa mmoja wa wavulana wanne tu waliochaguliwa kujiunga na seminari hiyo. Ulitamani sana niwe padri. Hata hivyo, japo nilikuangusha, angalau mdogo wangu, Sista Maria Solana aliweza kujiunga na utawa, na yeye sasa ndio guide wetu mkuu katika sala.

Pamoja na uchungu nilionao kutokana na kifo chako baba, faraja pekee ni kuwa ninaamini muda huu upo na mkeo mpendwa, mama yetu mpendwa, marehemu Adelina Mapango a.k.a Mama Chahali. Tangu mama afariki, baba ulikuwa ukisononeka mno, kwa vile mama hakuwa mkeo tu bali pia rafiki yako mkuu. Siku zote baada ya kifo cha mama ulijisikia kuwa wewe ndo ulistahili kutangulia kabla yake kwa vile ulikuwa umemzidi umri.

Kipimo cha upendo wako baba ni kipindi kile mama alipopoteza fahamu kuanzia mwishoni mwa Januari 2008 hadi alipofariki Mei 29, 2008. Baba ulikuwa unafunga mfululizo kumwombea mama apate nafuu.Nakumbuka nilipokuja kumuuguza mama tulikushauri upunguze kufunga mfululizo hasa pale sauti yako ilipoanza kukauka na nguvu kupotea kutokana na mwili kukosa lisha na maji. Ulimpenda mno mkeo, na kwa hakika mmetachia fundisho kubwa sana.

Mwaka 2005 niliwarekodi wewe na mama, katika maadhimisho ya miaka 50 ya ndoa yenu. Bado ninayo video ile lakini nashindwa kuiangalia kwa sababu inanitia uchungu sana. Hata hivyo, kila siku ninazingatia yote mliyoniusia katika video hiyo, na ndio mwongozo wa maisha yangu.

Basi baba, nakuombea uendelee kupumzuka kwa amani na marehemu mama na mwanga wa milele uangaziwe na Bwana. Mie ninawakumbuka kwa sala kila siku kabla ya kulala. Sie tulikupenda wewe baba na mama, lakini Baba yenu wa Mbunguni aliwapenda zaidi, akawachukua. Jina lake lihimidiwe milele. AMINA



5 Jul 2016


Check this out on Chirbit

4 Jul 2016



Zaidi kuhusu kundi hilo la kigaidi, BONYEZA HAPA

CHANZO: Amor Shabbi (@amorshabbi), mwandishi  wa habari anayeripoti kuhusu eneo la Sahel na Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini (MENA). Waweza kuwasiliana nae [email protected] simu +213660376006 Constantine, Aljeria




3 Jul 2016

Mwanadada Mtanzania mkaazi wa hapa Uingereza, Karrima Carter (kushoto pichani juu) jana alifanya harambee huko Norwich kwa ajili ya kusaidia makundi mbalimbali yenye mahitaji nchini Tanzania. Karrima, amekuwa akijibidiisha kutoa misaada mbalimbali huko nyumbani ambapo kwa sasa anahudumia vituo kadhaa ya yatima jijini Dar es Salaam, sambamba na kutoa misaada ya vifaa vya elimu kwa shule mbalimbali za msingi.

Tangu aanze jukumu alilojipachika la kupeleka misaada huko Tanzania, ameshatuma makontena manane yenye vifaa anavyokusanya huku Uingereza na ambavyo vina mahitaji kwa makundi mbalimbali huko nyumbani. Cha kuvutia sana ni kuwa anafanya hivyo kwa gharama zake, akiamini katika kutumia kipato liachonacho kuwasaidia wengine wenye mahitaji.

Chini ni baadhi ya picha za kwenye tukio hilo la jana





























2 Jul 2016

Habari za wikiendi. Kila wiki, ntajitahidi kuwaletea matangazo ya kazi yanayowafaa wazungumzaji wa Kiswahili, na pengine fursa za masomo na vitu kama hivyo. Ni mwendelezo tu wa falsafa ya SHARING IS CARING. Wikiendi hii ninaanza na nafasi za kazi zifuatazo zinazohitaji waongeaji wa Kiswahili.

Idara ya Ushushushu wa Mawasiliano ya Uingereza (GCHQ) ina nafasi za Rare Languages Analysts (upcoming jobs) kwa wenye sifa stahili. Maelezo zaidi BONYEZA HAPA

Chuo Kikuu cha Edinburgh kina nafasi ya Teaching Fellow (Swahili), Edinburgh, maelezo zaidi BONYEZA HAPA

War Child wana nafasi ya Education in Emergencies Advisor, maelezo zaidi BONYEZA HAPA
Transaid wana nafasi ya Programme Assistant, London, maelezo zaidi BONYEZA HAPA

Premier Housewares Limited wana nafasi ya Export Administrator, Glasgow, maelezo zaidi BONYEZA HAPA 

Risk Advisory wana nafasi ya Junior Research Analyst, London, maelezo zaidi BONYEZA HAPA

London Borough of Honslow wana nafasi ya Swahili Mother Tongue Teacher, London, maelezo zaidi BONYEZA HAPA



30 Jun 2016


Check this out on Chirbit

24 Jun 2016

Leo nilishiriki katika mahojiano mawili kuhusu kura ya maoni iliyopigwa hapa Uingereza juzi kuhusu hatma ya uanachama wa taifa hilo kwenye Umoja wa Ulaya, ambapo matokeo yalikuwa kwa Uingereza kujitoa. Mahojiano hayo yalikuwa kati yangu na kipindi cha radio cha  Dira ya Dunia ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC na baadaye kipindi cha televisheni cha Dira ya Dunia cha kituo hicho.

Hapa chini ni video na audio ya mahojiano hayo. Karibuni





Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.