28 Aug 2021

Tukio: Mauaji ya askari polisi watatu na mlinzi mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi
Lini: 25 Agosti 2021
Mahali: Jirani na Ubalozi wa Ufaransa, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Dar es Salaam, Tanzania
Ripoti za awali: Tamko la Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro 

Uchambuzi wa kiintelijensia:  

Dhana za awali

Dhana zilizosalia

Hitimisho la awali (provisional conclusion)

Hamza alikuwa "radicalised" na huenda lilikuwa suala la lini/wapi, na sio endapo (when/where not if) angefanya alichofanya. Lakinipia, Hamza alikuwa na kinyongo binafsi na polisi, na hiyo "radicalisation" ilirahisisha uamuzi wake wa "kuwaadhibu." 

Mwisho: 


Intelijensia sio sayansi timilifu (exact science) hasa katika mazingira haya ambapo taarifa mpya zinaendelea kumiminika. Kwahiyo, hitimisho hilo la awali lichukuliwe tu kwa mujibu wa kinachofahamika hadi muda huu. Hata hivyo, uchunguzi zaidi unaendelea.

12 Mar 2021


Rais John Pombe Magufuli amekata roho leo saa kumi na moja nusu Jioni hospitali ya Mzena Dar es Salaam. Makamu wa Rais Samiah Suluh Hassan hajaambiwa. Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Bwana Diwani Athumani na Daktari wa Rais Professor Mchembe wamekaa na Mwili wa Marehemu mpaka sasa kupanga Makamu wa Rais wanayemtaka Bwana Chamuriho. Tumlinde Samiah, tulinde Katiba. Watanzania Kesho asbh nendeni Mzena kushinikiza Katiba ifuatwe

27 Oct 2020



Network data from the NetBlocks Internet Observatory confirm widespread disruption to social media and online communication platforms via multiple internet providers in Tanzania as of Tuesday 27 October 2020. The incident comes on the eve of Tanzania’s presidential and national assembly elections and the service outages are ongoing at the time of writing.

Real-time metrics show that Twitter, WhatsApp, backend servers for Instagram and some Google services including GMail and Translate are generally or partially unavailable via Tanzania’s leading network operators Vodacom, Airtel, Tigo, Halotel and ZanTel. Meanwhile, data indicate a more generalized disruption of services on state-owned operator TTCL, the Tanzania Telecommunications Corporation. Findings are drawn from an initial set of NetBlocks Web Probe observations from 800 observation points. Twitter Inc. has also subsequently confirmed throttling of its services in Tanzania.

Authorities have not issued a statement on the disruptions as of Tuesday afternoon. A week earlier, the Tanzania Communications Regulatory Authority issued operators with a directive to suspend bulk SMS and telephony services during the election period. However, the directive does not specifically cover internet communications and relevant regulatory frameworks remain unclear.

The incident comes amid heightened concerns over election transparency and follows claims from the opposition over state interference with the accreditation process for electoral observers.

Breaking incident: article will be updated as information is processed


Methodology

This report follows the Election Pathfinder Rapid Response methodology which defines a set of core principles, workflows and benchmarks for network measurement and evaluation during elections and referenda.

Internet performance and service reachability are determined via NetBlocks web probe privacy-preserving analytics. Each measurement consists of latency round trip time, outage type and autonomous system number aggregated in real-time to assess service availability and latency in a given country. Network providers and locations enumerated as vantage point pairs. The root cause of a service outage may be additionally corroborated by means of traffic analysis and manual testing as detailed in the report.

SOURCE: NETBLOCK



Pengine umeshawahi kusikia jina la Profesa Allan Lichtman wa Marekani ambaye ana rekodi ya miaka 30 ya kutabiri kwa usahihi kabisa matokeo ya urais katika nchi hiyo. 



Pengine utabiri uliompatia umaarufu zaidi ni wa mwaka 2016 ambapo takriban kila kura ya maoni ilionyesha kuwa mgombea wa chama cha Democrats, Hillary Clinton, angemshinda mpinzani wake wa chama cha Republican, Donald Trump.

Profesa huyo anatumia vipengele 13 vinavyopatikana kwenye kitabu chake kiitwacho "The Keys To The White House" (funguo za kuingilia Ikulu ya Marekani).

Katika vipengele hivyo 13 ni kauli zenye mrengo wa ushindi kwa mgombea aliyepo madarakani. Kwa muktadha wa Tanzania, vipengele hivi hapa chini vinamhusu Rais John Magufuli wa chama tawala CCM anayechuana vikali na mpinzani wake mkuu, Tundu Lissu wa Chadema.

Endapo majibu ya SI KWELI (FALSE) ni matano au pungufu kwa vipengele hivyo, basi mgombea aliyepo madarakani anatabiriwa kushinda. Lakini endapo majibu ya SI KWELI (FALSE) yatakuwa sita au zaidi, basi mgombea huyo ataanguka kwenye uchaguzi husika.

Naomba nitahadharishe kuwa hii ni mara ya kwanza kwa kanuni hii kutumika kutabiri matokeo ya urais nchini Tanzania. Hata hivyo nimejiridhisha kuwa japo Profesa Lichtman alilenga chaguzi za rais wa Marekani, zaweza pia kutumika kwa muktadha wa Tanzania.

19 May 2020


Nimechapisha makala mbili, moja ya Kiswahili na nyingine ya Kiingereza kuhusu mustakabali wa Rais John Magufuli kutokana na anavyopuuzia janga la korona. Makala ya Kiswahili ni uchambuzi wa kiintelijensia wenye kurasa kadhaa. Ipo HAPA

Pia waweza kuisoma hapa



Makala ya Kiingereza ipo kwenye tovuti ya kimataifa ya African Arguments. BONYEZA HAPA kuisoma

1 May 2020


Kituo cha runinga cha NTV cha nchini Kenya kiliripoti jana jioni kwamba idadi ya vifo vya korona jijini Dar es Salaam pekee kwa jana vilikuwa 50. Kutokana na unyeti wa maradhi haya, yayunkinika kuamini taarifa hiyo kwa sababu sio rahisi kwa chombo cha habari cha kitaifa kama hicho kutoa taarifa nzito kama hiyo bila kujiridhisha. 

Lakini kwa upande mwingine takriban kila anayefuatilia kinachoendelea huko Tanzania anafahamu fika kwamba serikali ya Rais Magufuli sio tu inaficha takwimu kuhusiana na maambukizi na vifo bali pia inafanya mzaha mkubwa dhidi ya jana hilo.

Taarifa nilizopatiwa alfajiri hii zinaeleza kuwa serikali imetoa mwongozo wa siri kuhusu jinsi ya kuwashughulikia wagonjwa wa korona. Kwa mujibu wa mwongozo huo, mgonjwa atakaa hospitalini wak siki tatu tu. Endapo hali ya mgonjwa haitogeuka kuwa mahututi, atarudishwa akaugulie nyumbani. Mtoa taarifa ananiambia kuwa waraka huo ni sehemu ya utekelezaji wa "herd immunity," mkakati hatari ambao kwa lugha nyepesi ni kuruhusu korona iangamize maelfu hadi mamilioni ya Watanzania kwa matarajio kuwa watajenga kinga dhidi ya ugonjwa huo. 

Licha ya uwezo wake mkubwa kiuchumi, Uingereza iliamua mapema tu kuachana na wazo hilo la herd immunity ambapo japo hadi muda huu idadi ya vifo imezidi 20,000 kwa kufuata herd immunity idadi hiyo ingeweza kuwa kubwa zaidi. Kadhalika, herd immunity ni sawa na kuangamiza watu bure kwa nchi kama Tanzania ambayo ina idadi kubwa ya watu wenye magonjwa kama ukimwi, pumu, kisukaribi, shinikizo la damu, nk ambayo yamethibitika "kuwa na ukaribu na korona" ambapo wenye maradhi hayo wamekuwa waathirika wakuu wa janga hilo. 

Endelea kutembelea blogu hii mara wa mara uweze kupata updates mbalimbali hususan kuhusu janga la korona.

Chukua tahadhari, jikinge na uwakinge na wenzio. Na heri ya Mei Mosi.

29 Apr 2020


Shaka imetanda nchini Tanzania kufuatia vifo vya watu 11 mashuhuru ndani ya wiki moja yaliyopita. Muda mfupi kabla ya kuandika chapisho hili, imetangazwa kuwa Mbunge wa Sumve (CCM) Richard Ndassa amefariki.



Kifo hicho ni ni mlolongo wa vifo vya watu maarufu nchini humo ambapo Jumatano iliyopita aliyekuwa Jaji Mkuu, Agustino Ramadhan alifariki.




Kabla ya hapo, Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Ali Haji Pandu alifariki Jumanne siku moja kabla.


Jumapili usiku, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda alifariki,



na siku hiyo hiyo, Mkurugenzi wa zamani wa CTI, Hussein Kamote alifariki pia jijini Dar es Salaam.

Jumanne, Jaji Mstaafu Musa Kwikima alifariki, na siku moja baadaye Afisa mwandamizi wa Idara ya Uhamiaji mkoani Kagera, Pendo Buteghe alifariki.


 Siku hiyo pia ilishuhudia kifo cha wakili maarufu Gaudious Ishengoma.



Watu wengine maarufu waliofariki ni Ben Lowassa - mdogo wake Edward Lowassa, Mbunge wa zamani Abdulkarim Shah na Naibu Meya wa Morogoro Isihaka Sengo.



Kifo cha Ndassa  kinaweza kuhusishwa na tamko la hivi karibuni la Rais John Magufuli kwamba "mvuke unaponya korona," ambapo inaelezwa kuwa chumbani kwa marehemu Ndassa kulikutwa vifaa vya kujifukizia.



Taarifa kutoka kwa wananchi mbalimbali zinaeleza kuwa wamefiwa na ndugu,jamaa na marafiki zao ambao wamezikwa na mamlaka husika lakini hali hiyo haijionyeshi kwenye takwimu za serikali kuhusu idadi vifo.

Leo, baada ya siku kadhaa, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametangaza kuwa



Na haya yote yanajiri huku leo ni siku ya 33 tangu Rais Magufuli alipoondoka Dodoma na kwenda kijijini kwake Chato mnamo Machi 28 mwaka huu.

Awali leo, kiongozi mkuu wa Upinzani Bungeni na mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freemani Mbowe, aliongea masuala kadhaa kuhusiana na janga la korona huku akiitaka serikali kuchukua hatua stahili.




Pia jana, kada maarufu wa CCM, Wakili Albert Msando alijitokeza hadharani kueleza kuwa hali nchini Tanzania ni mbaya kuhusiana na ugonjwa wa korona, kauli iliyotafsiriwa kuwa ni uthibitisho wa hali halisi ilivyo japo serikali imekuwa ikificha ukweli huo.



31 Mar 2020


Huenda kuna watakaosema wakati huu ambapo nchi na dunia ipo kwenye kipindi kigumu kutokana na janga la krona, si muda mwafaka wa kutupiana lawama. Lakini vipi kama lawama hizo zinaweza kusaidia kuleta mabadiliko chanya katika jitihada za kukabiliana na janga hilo?

Kuna mfululizo wa matukio yanayoashiria bayana kuwa Rais Magufuli ana mapungufu ya kiuongozi kila wakati Tanzania yetu inapokumbwa na majanga. Tukio kubwa zaidi ni lile la tetemeko la ardhi Kagera ambapo kwanza alipuuza kutembelea wahanga kwa siku kadhaa, na alipoamua kuwatembelea, akaishia "kuwasemea ovyo" kwa kudai si yeye aliyesababisha tetemeko hilo.


Kwanini tukio hili ni kubwa zaidi? Si tu kwa vile liliathiri watu wengi lakini pia kwa sababu Magufuli anatokea eneo hilo. Kwa lugha nyingine, kama anaweza "kuwafanyia hivyo ndugu zake," kwaninia shindwe kwa "watu baki"?

Matukio mengine ambayo yalipuuzwa na Magufuli ni pamoja na maombolezo ya askari wetu waliouawa huko DRC walikokuwa wakishiriki operesheni za kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini humo. Licha ya kuwa Amiri Jeshi Mkuu, hakushiriki kuaga miili ya mashujaa wetu hao.


Janga jingine kwa taifa ambalo Magufuli alilipuuza nivifo vya wanafunzi kadhaa wa shule ya St Lucky huko Arusha

Kadhalika, Magufuli alipuuzia janga jingine lililotokea kanda ya Ziwa ambapo mamia walifariki katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere


Na akapuuzia pia janga la mlipuko wa lori la mafuta uliopolekea vifo kadhaa

Na kama alivyopuuzia janga la vifo vya mashujaa wetu waliouwa huko DRC, Magufuli hakutokea kwenye kuaga miili ya polisi waliouawa huko MKIRU, licha ya kuwa Amiri Jeshi Mkuu

Katika janga hili la korona, mwenendo wake tangu mwanzo umekuwa ni mwendelezo wa dharau zake kwa majanga yanapolikumba taifa letu. Baada ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kutangaza kuwa korona imeingia Tanzania, ilimchukua Magufuli siku 10 hivi kuongea lolote kuhusu janga hilo.

Na alipofungua mdomo wake, akaongea vitu vya ovyo kabisa. Akiwa Kanisani, aliweka kando uanasayansi wake na kudai kuwa "ukimwi unaua, malaria inaua, na ajali pia zinaua," na kusema kuwa "tunatishana sana (kuhusu korona). Haya si maneno ya kuyatarajia kutoka kwa kiongozi mkuu wa nchi ambaye pia ni mfariji mkuu.



Baadaye akahutubia taifa na kuendelea kutoa ujumbe usio na tija.



Baada ya ukimya wa siku kadhaa akaibukia tena huko Dodoma ambapo wakati taifa likiwa kwenye hofu na mashaka ya janga hilo la korona, mkuu huyo wa nchi akaonekana akifanya mzaha kwa kujilaza kwenye mawe.



Na majuzi alionekana akipuuza ushauri wa kitaalamu dhidi ya maambukizi ya korona unaowataka watu kuepuka mikusanyiko.

Na hii ilikuwa baada ya matukio makubwa mawili huko Dodoma yaliyosababisha mkusanyiko - kikao cha baraza la mawaziri na wakuu wa vyombo vya dola, na baadaye kupokea ripoti za TAKUKURU na CAG.
Image

Image

Kwa minajili ya kumbukumbu, mwaka juzi, mwanasiasa nguli wa upinzani Tundu Lissu alihoji kasumba hiyo ya Magufuli kujitenga na majanga ya kitaifa.

Huu sio tu ni mwaka wa tano tangu Magufuli aingie madarakani lakini pia ni mwaka wa uchaguzi mkuu mwingine (kama ataruhusu). Waweza kujiuliza "anapata wapi jeuri hiy ya kupuuzia majanga ya kitaifa miaka yote hii na hata mwaka huu wa uchaguzi?" Jibu ni kwamba anafahamu fika kuwa haitomgharimu chochote. Kwa upande mmoja wapinzani wetu wamekuwa watu wa maneno zaidi kuliko vitendo, ilhali wananchi nao wakiwa bize na ubuyu. Laiti Magufuli angehisi "kuna adhabu inamsubiri" asingefanya dharau hizi. 

Lakini hata kama wapinzani wameshindwa kushikia bango hilo, na wananchi wako bize na ubuyu, ni jukumu letu sie wachache wenye uthubutu wa kukosoa kutochoka kukemea maovu kama haya. Maana sote tukikaa kimyaatadhani tunaafiki kasumba hiyo isiyopendeza.

Nimalizie makala hii kwa ujumbe huu muhimu kuhusu janga la korona.



Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.