6 Feb 2023


 


28 Aug 2021

Tukio: Mauaji ya askari polisi watatu na mlinzi mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi
Lini: 25 Agosti 2021
Mahali: Jirani na Ubalozi wa Ufaransa, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Dar es Salaam, Tanzania
Ripoti za awali: Tamko la Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro 

Uchambuzi wa kiintelijensia:  

Dhana za awali

Dhana zilizosalia

Hitimisho la awali (provisional conclusion)

Hamza alikuwa "radicalised" na huenda lilikuwa suala la lini/wapi, na sio endapo (when/where not if) angefanya alichofanya. Lakinipia, Hamza alikuwa na kinyongo binafsi na polisi, na hiyo "radicalisation" ilirahisisha uamuzi wake wa "kuwaadhibu." 

Mwisho: 


Intelijensia sio sayansi timilifu (exact science) hasa katika mazingira haya ambapo taarifa mpya zinaendelea kumiminika. Kwahiyo, hitimisho hilo la awali lichukuliwe tu kwa mujibu wa kinachofahamika hadi muda huu. Hata hivyo, uchunguzi zaidi unaendelea.

12 Mar 2021


Rais John Pombe Magufuli amekata roho leo saa kumi na moja nusu Jioni hospitali ya Mzena Dar es Salaam. Makamu wa Rais Samiah Suluh Hassan hajaambiwa. Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Bwana Diwani Athumani na Daktari wa Rais Professor Mchembe wamekaa na Mwili wa Marehemu mpaka sasa kupanga Makamu wa Rais wanayemtaka Bwana Chamuriho. Tumlinde Samiah, tulinde Katiba. Watanzania Kesho asbh nendeni Mzena kushinikiza Katiba ifuatwe

27 Oct 2020Network data from the NetBlocks Internet Observatory confirm widespread disruption to social media and online communication platforms via multiple internet providers in Tanzania as of Tuesday 27 October 2020. The incident comes on the eve of Tanzania’s presidential and national assembly elections and the service outages are ongoing at the time of writing.

Real-time metrics show that Twitter, WhatsApp, backend servers for Instagram and some Google services including GMail and Translate are generally or partially unavailable via Tanzania’s leading network operators Vodacom, Airtel, Tigo, Halotel and ZanTel. Meanwhile, data indicate a more generalized disruption of services on state-owned operator TTCL, the Tanzania Telecommunications Corporation. Findings are drawn from an initial set of NetBlocks Web Probe observations from 800 observation points. Twitter Inc. has also subsequently confirmed throttling of its services in Tanzania.

Authorities have not issued a statement on the disruptions as of Tuesday afternoon. A week earlier, the Tanzania Communications Regulatory Authority issued operators with a directive to suspend bulk SMS and telephony services during the election period. However, the directive does not specifically cover internet communications and relevant regulatory frameworks remain unclear.

The incident comes amid heightened concerns over election transparency and follows claims from the opposition over state interference with the accreditation process for electoral observers.

Breaking incident: article will be updated as information is processed


Methodology

This report follows the Election Pathfinder Rapid Response methodology which defines a set of core principles, workflows and benchmarks for network measurement and evaluation during elections and referenda.

Internet performance and service reachability are determined via NetBlocks web probe privacy-preserving analytics. Each measurement consists of latency round trip time, outage type and autonomous system number aggregated in real-time to assess service availability and latency in a given country. Network providers and locations enumerated as vantage point pairs. The root cause of a service outage may be additionally corroborated by means of traffic analysis and manual testing as detailed in the report.

SOURCE: NETBLOCKPengine umeshawahi kusikia jina la Profesa Allan Lichtman wa Marekani ambaye ana rekodi ya miaka 30 ya kutabiri kwa usahihi kabisa matokeo ya urais katika nchi hiyo. Pengine utabiri uliompatia umaarufu zaidi ni wa mwaka 2016 ambapo takriban kila kura ya maoni ilionyesha kuwa mgombea wa chama cha Democrats, Hillary Clinton, angemshinda mpinzani wake wa chama cha Republican, Donald Trump.

Profesa huyo anatumia vipengele 13 vinavyopatikana kwenye kitabu chake kiitwacho "The Keys To The White House" (funguo za kuingilia Ikulu ya Marekani).

Katika vipengele hivyo 13 ni kauli zenye mrengo wa ushindi kwa mgombea aliyepo madarakani. Kwa muktadha wa Tanzania, vipengele hivi hapa chini vinamhusu Rais John Magufuli wa chama tawala CCM anayechuana vikali na mpinzani wake mkuu, Tundu Lissu wa Chadema.

Endapo majibu ya SI KWELI (FALSE) ni matano au pungufu kwa vipengele hivyo, basi mgombea aliyepo madarakani anatabiriwa kushinda. Lakini endapo majibu ya SI KWELI (FALSE) yatakuwa sita au zaidi, basi mgombea huyo ataanguka kwenye uchaguzi husika.

Naomba nitahadharishe kuwa hii ni mara ya kwanza kwa kanuni hii kutumika kutabiri matokeo ya urais nchini Tanzania. Hata hivyo nimejiridhisha kuwa japo Profesa Lichtman alilenga chaguzi za rais wa Marekani, zaweza pia kutumika kwa muktadha wa Tanzania.

19 May 2020


Nimechapisha makala mbili, moja ya Kiswahili na nyingine ya Kiingereza kuhusu mustakabali wa Rais John Magufuli kutokana na anavyopuuzia janga la korona. Makala ya Kiswahili ni uchambuzi wa kiintelijensia wenye kurasa kadhaa. Ipo HAPA

Pia waweza kuisoma hapaMakala ya Kiingereza ipo kwenye tovuti ya kimataifa ya African Arguments. BONYEZA HAPA kuisoma

1 May 2020


Kituo cha runinga cha NTV cha nchini Kenya kiliripoti jana jioni kwamba idadi ya vifo vya korona jijini Dar es Salaam pekee kwa jana vilikuwa 50. Kutokana na unyeti wa maradhi haya, yayunkinika kuamini taarifa hiyo kwa sababu sio rahisi kwa chombo cha habari cha kitaifa kama hicho kutoa taarifa nzito kama hiyo bila kujiridhisha. 

Lakini kwa upande mwingine takriban kila anayefuatilia kinachoendelea huko Tanzania anafahamu fika kwamba serikali ya Rais Magufuli sio tu inaficha takwimu kuhusiana na maambukizi na vifo bali pia inafanya mzaha mkubwa dhidi ya jana hilo.

Taarifa nilizopatiwa alfajiri hii zinaeleza kuwa serikali imetoa mwongozo wa siri kuhusu jinsi ya kuwashughulikia wagonjwa wa korona. Kwa mujibu wa mwongozo huo, mgonjwa atakaa hospitalini wak siki tatu tu. Endapo hali ya mgonjwa haitogeuka kuwa mahututi, atarudishwa akaugulie nyumbani. Mtoa taarifa ananiambia kuwa waraka huo ni sehemu ya utekelezaji wa "herd immunity," mkakati hatari ambao kwa lugha nyepesi ni kuruhusu korona iangamize maelfu hadi mamilioni ya Watanzania kwa matarajio kuwa watajenga kinga dhidi ya ugonjwa huo. 

Licha ya uwezo wake mkubwa kiuchumi, Uingereza iliamua mapema tu kuachana na wazo hilo la herd immunity ambapo japo hadi muda huu idadi ya vifo imezidi 20,000 kwa kufuata herd immunity idadi hiyo ingeweza kuwa kubwa zaidi. Kadhalika, herd immunity ni sawa na kuangamiza watu bure kwa nchi kama Tanzania ambayo ina idadi kubwa ya watu wenye magonjwa kama ukimwi, pumu, kisukaribi, shinikizo la damu, nk ambayo yamethibitika "kuwa na ukaribu na korona" ambapo wenye maradhi hayo wamekuwa waathirika wakuu wa janga hilo. 

Endelea kutembelea blogu hii mara wa mara uweze kupata updates mbalimbali hususan kuhusu janga la korona.

Chukua tahadhari, jikinge na uwakinge na wenzio. Na heri ya Mei Mosi.

29 Apr 2020


Shaka imetanda nchini Tanzania kufuatia vifo vya watu 11 mashuhuru ndani ya wiki moja yaliyopita. Muda mfupi kabla ya kuandika chapisho hili, imetangazwa kuwa Mbunge wa Sumve (CCM) Richard Ndassa amefariki.Kifo hicho ni ni mlolongo wa vifo vya watu maarufu nchini humo ambapo Jumatano iliyopita aliyekuwa Jaji Mkuu, Agustino Ramadhan alifariki.
Kabla ya hapo, Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Ali Haji Pandu alifariki Jumanne siku moja kabla.


Jumapili usiku, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda alifariki,na siku hiyo hiyo, Mkurugenzi wa zamani wa CTI, Hussein Kamote alifariki pia jijini Dar es Salaam.

Jumanne, Jaji Mstaafu Musa Kwikima alifariki, na siku moja baadaye Afisa mwandamizi wa Idara ya Uhamiaji mkoani Kagera, Pendo Buteghe alifariki.


 Siku hiyo pia ilishuhudia kifo cha wakili maarufu Gaudious Ishengoma.Watu wengine maarufu waliofariki ni Ben Lowassa - mdogo wake Edward Lowassa, Mbunge wa zamani Abdulkarim Shah na Naibu Meya wa Morogoro Isihaka Sengo.Kifo cha Ndassa  kinaweza kuhusishwa na tamko la hivi karibuni la Rais John Magufuli kwamba "mvuke unaponya korona," ambapo inaelezwa kuwa chumbani kwa marehemu Ndassa kulikutwa vifaa vya kujifukizia.Taarifa kutoka kwa wananchi mbalimbali zinaeleza kuwa wamefiwa na ndugu,jamaa na marafiki zao ambao wamezikwa na mamlaka husika lakini hali hiyo haijionyeshi kwenye takwimu za serikali kuhusu idadi vifo.

Leo, baada ya siku kadhaa, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametangaza kuwaNa haya yote yanajiri huku leo ni siku ya 33 tangu Rais Magufuli alipoondoka Dodoma na kwenda kijijini kwake Chato mnamo Machi 28 mwaka huu.

Awali leo, kiongozi mkuu wa Upinzani Bungeni na mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freemani Mbowe, aliongea masuala kadhaa kuhusiana na janga la korona huku akiitaka serikali kuchukua hatua stahili.
Pia jana, kada maarufu wa CCM, Wakili Albert Msando alijitokeza hadharani kueleza kuwa hali nchini Tanzania ni mbaya kuhusiana na ugonjwa wa korona, kauli iliyotafsiriwa kuwa ni uthibitisho wa hali halisi ilivyo japo serikali imekuwa ikificha ukweli huo.Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.