Kama hujawahi kuhudhuria matamasha au maonyesho ya wasanii wetu huko Bongo,wala usidhani ume-miss raha pekee.Kuna karaha pia,hususan ile inayotokana na mastaa wetu kudekezwa kupita kiasi na vyombo vya dola.Kwa kifupi,huko ni bangi nje nje,wasanii hugeuka madikteta wanaoweza kufanya lolote lile hadharani ikiwa pamoja na unyanyasaji wa waziwazi dhidi ya dada zetu.Na baada ya "unga" kugeuka "kilevi cha kawaida",wengi wa wasanii hao hujitundika madawa hayo vya kutosha pasipo hofu ya kuchukuliwa hatua na vyombo vya dola.
Nadhani wapo wanaokumbuka msanii mmoja wa bongefleava aliyekamatwa na bangi katika mkoa mmoja wa nyanda za juu kusini.Ni Daz Baba wa kundi lililokuwa likijulikana kama Daz Nundaz.Iliishia kuwa amekamatwa tu,wala hakukuwa na taarifa za msanii hiyo kufikishwa mahakamani au hata kupewa onyo (si lazima kila kosa limaanishe kifungo).
Twende kwa baadhi ya marapa maarufu Msafiri Diouf na Banza Stone.
Haihitaji upelelezi kujua kuwa wanatumia kilevi haramu,lakini dola haijihangaishi kuwachukulia hatua ambazo licha ya kuwaadhibu zingesaidia pia kuokoa maisha yao kwani ni dhahiri kwamba mwisho wao sio mzuri.
Kuna msanii anaitwa Chid Benz.
Licha ya sifa yake ya kufanya vizuri zaidi anaposhirikishwa kwenye nyimbo za wasanii wengine (wanaita "kolabo" as corruption ya neno collaboration) zaidi ya nyimbo zake mwenyewe,mwanabongofleva huyo ni maarufu pia kwa vurugu na vipigo kwa wasanii wenzie.Dola imeendelea kumwangalia tu,hali inayoweza kupelekea Chid Benz kuamini kuwa yuko juu ya sheria kutoa kipondo kwa yeyote yule anapojiskia kufanya hivyo.
Licha ya sifa yake ya kufanya vizuri zaidi anaposhirikishwa kwenye nyimbo za wasanii wengine (wanaita "kolabo" as corruption ya neno collaboration) zaidi ya nyimbo zake mwenyewe,mwanabongofleva huyo ni maarufu pia kwa vurugu na vipigo kwa wasanii wenzie.Dola imeendelea kumwangalia tu,hali inayoweza kupelekea Chid Benz kuamini kuwa yuko juu ya sheria kutoa kipondo kwa yeyote yule anapojiskia kufanya hivyo.
Leo,kwenye tovuti ya Global Publishers kuna habari kwamba msaanii Khaleed Mohammed,almaaruf T.I.D,amemjeruhi mwanafunzi mmoja wa kike baada ya kumshushia kipigo cha nguvu.Kwa mujibu wa tovuti hiyo,T.I.D nasakwa na polisi na "hajulikani alipo".Nisingependa kutoa hukumu kwa vile mie si mahakama,lakini napenda kukiri kwamba nilishangazwa na habari kwamba msanii huyo alikuwa miongoni mwa waliopewa msamaha na Rais katika maadhimisho ya siku flani ya kitaifa.
Sikushangaa kwa vile aliyesamehewa ni T.I.D,bali vigezo vilivyotumika kumpa msamaha huo.Kwa tunaofahamu ukweli kuhusu kesi hiyo,yayumkinika kuwa maombi ya msahama ya mtenda kosa kwa waliotendewa kosa yalisikilizwa,na kwa vile waliotendewa kosa ni "wenye kuwezesha jua liwake au lisiwake",yaani "the powers-that-be",msanii huyo akajumuishwa kwenye msamaha wa Rais.
Tukio hili la sasa ambapo T.I.D amerejea kosa lilelile lililompeleka jela in the first place,sio tu linazidisha hisia kuwa wengi wa wasanii na mastaa wetu wanaringia ugoigoi wa wanadola wetu katika kuchukua hatua inapostahili,bali pia ni fedheha na aibu kwa suala zima la msamaha wa rais.Navyofahamu,msamaha huo huzingatia tabia ya mfungwa,afya yake,idadi ya siku zilizosalia katika kifungo chake,na pengine kikubwa zaidi,mwenendo wake pindi akipewa msamaha huo.
Ni dhahiri kwamba jinsi jeshi la Magereza "lilivyojichokea" si rahisi kwake kukamilisha vigezo hivyo vyote.Na katika jamii ambayo mwenye fedha ni mithili ya mungu-mtu huku ufisadi ukishamiri kila kukicha,yayumkinika kuamini iwamba misamaha ya rais imekuwa ikitumika ndivyo sivyo.
Hivi tunajenga jamii ya aina gani?Wkati wenzetu katika nchi zilzoendelea wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kudhibiti uvutaji wa sigara katika maoneo ya mikusanyiko,sie tunaelekea kuruhusu uvutaji wa bangi kana kwamba ni kitu halali.Nilisoma mahala flani kwamba msanii mmoja wa filamu za kibongo alichomoa bastola hadharani kisa wapita njia walimlalamikia kwa kupaki gari lake barabarani.
Hypothesis yangu ni hii: itikadi ya ujamaa iliifanya sehemu kubwa ya Watanzania kuwa wanyonge wasio na stahili ya kuwa karibu na makundi yenye nguvu au mvuto kwenye jamii hiyo e.g. wanasiasa,wasanii,nk.Japo tunadai kuwa ujamaa umekufa,mentality ya itikadi hiyo bado iko hai na inatuathiri katika namna tunavyodili na watu hao walio kwenye "makundi maalumu" kwa mfano "mastaa wetu".Polisi wa trafiki anajiuliza mara mbilimbili "kuipiga mkono" Benz au Vogue,kwa vile akilini mwake,dereva wa gari hilo ola thamani anaweza "kuhatarisha ajira yake".Mtaani,msanii anageuka "mungu-mtu",wananchi wanatamani kuwa karibu nae,angalau kugusana mabega nae,wanadola wanachelea kumchukulia hatua (pengine kwa kudhani kuwa kwa vyovyote vile msanii hiyo atakuwa na connection na mtoto wa kigogo flani),na upuuzi mwingine kama huo.
Sio kwamba ujamaa ni mbaya per se.Kuna mazuri flani,ila hapa nimezungumzia legacy ya itikadi ya ujamaa katika upande hasi.Pengine kunahitajika mjadala wa kitaifa kutafakari mambo kama haya.
UNAONAJE?