22 Apr 2009
21 Apr 2009
Shule ya Sekondari ya kutwa ya Marambo yenye wanafunzi 253 ya kidato cha Kwanza hadi cha Nne , iliyopo Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi ina mwalimu mmoja. Mkuu wa shule hiyo, Saidi Mbutuka ndiye pekee aliye shuleni hapo anayelazimika kushika nyadhifa zote.Mbutuka aliliambia gazeti hili kuwa hali hiyo inatishia mustakabali wa elimu kwa wanafunzi shuleni hapo kwa kukosa elimu inayostahili. ''Mimi ndiye mkuu wa shule, ndiye mwalimu wa zamu, mwalimu wa taaluma, kila siku za kazi natakiwa kuingia katika madarasa yote manne, kwa siku ninakuwa na vipindi zaidi ya 10'', alisema.
Aliongeza, ''kwa hali hiyo hata kama ningekuwa mwalimu mzuri, kuna kila sababu ya kutilia mashaka na ubora wa elimu, mimi ni mwalimu wa masomo ya Sanaa, lakini nalazimika kufundisha Sayansi,'' alisema Mbutuka.
Alifafanua kuwa tatizo hilo limejitokeza mwaka huu baada ya walimu wanne waliokuwa shuleni hapo kwenda kusoma. 'Tunao wanafunzi wa kidato cha Nne ambao wanahitaji wafanye mtihani wa kuhitimu elimu yao, hivi tujiulize nini watavuna wanafunzi hawa kwa kufundishwa na mwalimu mmoja ambaye pia ndiyo nguzo kwa wanafunzi wa vidato vingine,'' alihoji.
Kwa mujibu wa mwalimu huyo, akiondoka kwenda mjini hulazimika kuwatawanya wanafunzi au kuwaacha chini ya uangalizi wa wanafunzi wenzao ambao ni viongozi.
Mbutuka alibainisha kuwa pamoja na tatizo hilo shule hiyo inakabiliwa na tatizo sugu la mdondoko wa wanafunzi unaotokana na wanafunzi hao kukimbilia katika machimbo ya madini ya Miruwi, Nachianji na Mituguru yaliyopo jirani na shule hiyo.
Alisema mwaka 2006, wanafunzi 53 waliripoti shuleni hapo hata hivyo waliobakia ni 31, wakati mwaka 2007 wanafunzi walioripoti walikuwa 111 waliopo 73. Mwaka 2008 wanafunzi 80 waliripoti na waliopo ni 50. Ofisa Elimu Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Nachingwea, Bakari Mussa, alikiri kuwapo kwa tatizo hilo na kuongeza kuwa halmashauri inashindwa kuwahamishia walimu shuleni hapo kutoka shule zingine ili kupunguza ukubwa wa tatizo kutokana na kukosa fedha za uhamisho.
''Kuna waraka wa serikali unaomtaka mwajiri kutomhamisha mtumishi yeyote bila kumlipa stahiki zake, kwa sababu halmashauri haina pesa tunashindwa namna ya kuiisaidia shule hiyo, lakini uwapo wa tatizo hilo sote tunautambua'' alisema Mussa.
CHANZO:Habarileo
HALAFU 2010 CCM WATAKUJA KUTUIMBIA MAFANIKIO KATIKA SEKTA YA ELIMU,NA KUDAI WAPEWE TENA MUDA WA KUIPELEKA NCHI YETU WANAKUJUA WAO.MIAKA ZAIDI YA 40 BAADA YA UHURU BADO TUNAKUWA NA SHULE YENYE MWALIMU MMOJA?WATETEZI WATASEMA SIE MASIKINI.MASIKINI GANI ANAYEWALIPA WABUNGE ZAIDI YA 300 SHS MILIONI 7 KWA MWEZI?MASIKINI GANI ALIEIBIWA BILIONI 40 NA KAGODA LAKINI ANAMWONEA AIBU HATA KUMTAJA HADHARANI?

Baraza la Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) limepitisha uamuzi wa kuishirikisha Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) kuhakiki vyeti vya wote wanaoomba kuwania nafasi za kisiasa ili sifa zao kielimu zitambulike.
Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Mayunga Nkunya, aliwaambia waandishi wa habari jana Dar es Salaam, TCU imewasiliana na NEC kwa barua, ili utaratibu huo uanze kutumika katika uchaguzi mkuu ujao mwakani.
Nkunya alitoa taarifa hiyo wakati akizungumzia maonyesho ya vyuo vikuu yaliyoandaliwa na TCU yatakayoanza kesho hadi Aprili 24, mwaka huu. “Baraza letu limepitisha uamuzi ili watu wanaotaka kugombea nafasi za kisiasa, vyeti vyao vihakikiwe, ili akipita sifa ijulikane rasmi kama ni daktari basi awe daktari na si daktari feki,” alisema Profesa Nkunya.
Hatua hiyo ya tume inatokana na kilichoelezwa na Nkunya kuwa ni kukithiri kwa vyuo na vyeti bandia nchini, jambo ambalo alisema wamejipanga kulivalia njuga kwa kushirikiana na wadau ili kuhakikisha Tanzania haiangamii kitaalamu na kitaaluma.
Alisema orodha ya vyuo visivyotambulika vya nje ambavyo Watanzania wengi wakiwamo mawaziri na wabunge wamesoma, ni ya kweli na kwamba kama kuna mtu anahisi kuonewa ruhusa kwenda mahakamani...ENDELEA

CHANZO: Habarileo.
TAMKO ZURI LAKINI LINALOSTAHILI UMAKINI KATIKA KULIAMINI.HAWA TCU WAKATI WANAZUNGUMZIA UCHAGUZI WA 2010,WANATAKA KUTUMBIA HAWAKUWEPO 2005?AU WATAPATA NGUVU HIYO 2010?JE KAMA SASA WANASHINDWA KUWASHUGHULIKIA HAO "MADAKTARI WA FALSAFA" WALIOKWAA SHAHADA ZAO MTANDAONI TUTAAMINI VIPI KUWA WATAWEZA HIYO 2010?
TATIZO LA NCHI YETU SIO SHERIA,KWANI ZIMEKUWEPO TANGU TUNAKABIDHIWA UHURU NA MKOLONI.TATIZO NI UTEKELEZAJI WA SHERIA HIZO.KUNA MBUNGE ALIKUWA NA TUHUMA ZA KUFOJI ELIMU (SIO YA CHUO KIKUU) BALI YA SEKONDARI.CHA AJABU HADI LEO "ANAPETA".JE HII HAILETI USHAWISHI KWA VIHIYO WENGINE KUJARIBU BAHATI ZAO?
TATIZO LA PILI LA NCHI YETU SIO SHERIA BALI UTEKELEZAJI WAKE UNAOELEMEA ZAIDI AINA YA MKOSAJI.YALEYALE YA ANAEIBA KUKU KWA NJAA KUITWA MWIZI LAKINI ANAYEFUJA MABILIONI ANAOTWA M-BADHIRIFU (NA SANASANA BADALA YA KWENDA JELA ATAHAMISHWA KITUO CHA KAZI).KUNA SHERIA KWA AJILI YA VIGOGO (KAMA AKINA CHEYO WANAOUA KWENYE AJALI LAKINI WANAUNDIWA TUME BADALA YA SHERIA KUCHUKUA MKONDO WAKE) NA SHERIA NYINGINE NI KWA AJILI YA MAKABWELA.
21.4.09
Evarist Chahali
KIWIRA, MKAPA, UFISADI
No comments

SAKATA la mgodi wa Kiwira kufikishwa bungeni, limeendelea kugubikwa na wingu zito, kutokana na ratiba za bunge kutoonyesha kama serikali itatoa ripoti.
Mgodi wa Kiwira, ambao unamuhusisha Rais wa Serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati, Daniel Yona umejaa utata kutokana na madai kuwa kampuni ya Tan Power Resources Limited iliununua kwa Sh70 milioni badala ya thamani yake halisi ya Sh4 bilioni.
Hadi sasa serikali haijatoa ufafanuzi wowote kuhusu utata huo licha ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuahidi katika mkutano wa 13 wa bunge kwamba,ingetoa taarifa bungeni.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja alisema tu kwa kifupi "vuta subira".
Iwapo serikali haitatoa ripoti hiyo katika mkutano unaoendelea itakuwa ni mara ya tatu kupigwa tarehe suala hilo.
Katika mkutano wa 13, wakati mjadala wa mgodi wa Kiwira na Meremeta ukiwa umepamba moto, Pinda alisema serikali ilikuwa ikiandaa taarifa lakini akasema ni bora asulubiwe kuliko kutaja wamiliki wa Meremeta kwa maelezo kuwa inahusu usalama wa taifa.
Lakini, hadi mkutano huo unamalizika hakukuwa na ripoti yoyote ya serikali na hata ulivyokuja mkutano wa 14 hakukuwa na ripoti kama hiyo.
Tayari ratiba ya bunge imetoka na kuonyesha kwamba, hoja nzito inayotarajiwa kutikisa bunge hadi sasa ni ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambayo imepangwa kuwasilishwa bungeni Aprili

20 Apr 2009
20.4.09
Evarist Chahali
KATUNI
No comments
18 Apr 2009
Na Leon BahatiSAKATA la Halmashauri ya Karatu, kugomea kulipia malazi ya Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein na ujumbe wake limechukuwa sura mpya, baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Celina Kombani kuunga mkono uamuzi wa halmashauri ni sahihi.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili, Kombani alisema halmashauri za wilaya haziwajibiki kuchangia ziara za mawaziri, rais au makamu wake, wanapotembelea katika maeneo yao.
Kombani alibainisha kuwa kama ingekuwa utaratibu huo upo, halmashauri nyingi zingefilisika hasa ambazo mawaziri wanatoka, kwa sababu wana utaratibu maalumu wa kutembelea zaidi ya mara tano kwenye maeneo yao, kwa mwaka.
"Kwa mfano kwa mwaka mimi hufanya ziara mara sita katika wilaya yangu ya Ulanga (Morogoro). Tukisema wanigharamie basi ingefilisika pamoja na halmashauri nyingine ambazo zina mawaziri," alisema Kombani ambaye ni Mbunge wa Ulanga Mashariki.
Akielezea kuhusu taratibu za matumizi ya fedha kwenye halmashauri, alisema kwa kawaida matumizi yote hupitishwa kwenye vikao vya madiwani.
Alibainisha kuwa gharama za msafara wa rais, makamu wa rais na mawaziri hugharamiwa na serikali kuu, kulingana na taratibu zilizowekwa.
"Ndiyo maana rais anapokuwa kwenye ziara huenda na vyakula vyake," alisema Kombani lakini akafahamisha kuwa halmashauri zinaweza kutenga fungu kwa ajili ya kuuandalia ugeni kwenye maeneo yao chakula cha jioni.
Iwapo halmashauri itaamua kufanya hivyo, alisema kuwa ni lazima fungu hilo liwe limepitishwa na halmashauri kupitia vikao vyake halali na si mkurugenzi na watendaji wake.
Alipoulizwa juu ya adhabu ya kiongozi wa halmashauri atakayetoa fedha pasipokufuata taratibu; alisema kila halmashauri ina taratibu zake za kuwajadili viongozi au maofisa waliokiuka taratibu na kuwachukulia hatua.
Suala la Halmashauri ya Karatu, kugomea kulipia malazi ya Makamu wa Rais pamoja na ujumbe wake liliripotiwa na gazeti la Mwananchi Jumatano iliyopita likionyesha kuwa Mkuu wa wilaya hiyo, Mathew Sedoyeka alimjia juu na kumtaka aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Majid Myao, aandike barua ya kujieleza kwanini alikataa kutoa fedha za kulipia ziara ya makamu wa rais wilayani humo.
Sedoyeka hakufurahishwa na kitendo cha halmashauri hiyo kugoma kulipa kiasi cha Sh2 milioni ambazo ni malipo ya kulala siku moja pamoja na chakula kwa ujumbe huo wa makamu wa rais, katika hoteli ya Bougain Villea ya mjini Karatu.
Kwenye barua ya kujieleza iliyoandikwa Machi 3, 2009 yenye kumbukumbu namba kdc/ded/cv.3/1/121, Myao amejitetea kuwa uamuzi wa kutolipiwa ziara hiyo, umetokana na kamati ya fedha ya madiwani kukataa kuidhinisha fedha hizo.
Alisema kutokana na kutoidhinishwa malipo hayo, aliona angekiuka Sheria namba tisa ya mwaka 1982 ambayo inahusu masuala ya matumizi ya fedha za halmashauri na maamuzi ya kamati ya fedha.
“Kama mimi ningetoa malipo hayo ni wazi ningekiuka sheria za serikali za mitaa hasa ikizingatiwa madiwani katika kikao chao halali ndio waligomea,” alieleza Myao.
Akizungumzia sakata hilo, Mbunge wa Jimbo la Karatu, Dk Willibrod Slaa alisema alichofanya ofisa huyo wa serikali ilikuwa halali kwa sababu walikuwa hawana bajeti ya malipo hayo.
Dk Slaa alitoa wito kwa serikali kutomuadhibu mtendaji yoyote wa halmashauri hiyo kutokana na uamuzi uliochukuliwa, ambao ulizingatia maadili ya kazi na utekelezaji wa utawala bora.
CHANZO: Mwananchi

Riyadh, April 16 - Saudi investors have asked Tanzania if they can lease 500,000 hectares of farmland mainly for rice and wheat farming as part of a plan to secure food supplies for the desert kingdom, officials said.
Senior officials from the Saudi capital's chamber of commerce made the request on the sidelines of a meeting with visiting Tanzanian President Jakaya Kikwete.
"Tanzania is ready to do business with you ... There is 100 million acres (40.5 million hectares) of good arable land," Kikwete told Saudi businessmen.
Samir Ali Kabbani, head of the chamber's agriculture committee, said: "We had very positive feedback."
"He (Kikwete) told us that Tanzanian authorities can lease us plots each of which covers up to 10,000 hectares for a 99-year period," he told Reuters after the meeting.
The Saudi government has joined private operators to invest in farm projects abroad after a long and costly food sufficiency plan threatened to deplete the desert kingdom's water supplies.
Saudi businessmen and officials will visit Tanzania in the next few weeks.
"They can lease the land from the government," January Makamba, an aide to President Kikwete, told Reuters.
"But we have to make sure we don't end up in a situation similar to that of Nigeria: Huge oil reserves but long queues in front of petrol stations," Makamba said.
Saudi officials are particularly interested in Tanzania because of its geographic proximity, political stability and the availability of water resources and farmland.
Several Saudi firms have already started investing in agricultural projects from Indonesia to Ethiopia.
Indonesia said in August that Saudi BinLadin Group would invest $4.3 billion on 500,000 hectares for rice farming.
Saudi Arabia's annual wheat needs are estimated at about 2.5 million tonnes and it imported a little over 1 million tonnes of rice in 2008, according to the U.S. Department of Agriculture.

SOURCE: Reuters
"TANZANIAN AUTHORITIES CAN LEASE THE SAUDIS PLOTS EACH OF WHICH COVERS UP TO 10K HECTARES FOR A 99-YEAR PERIOD!?"
"TANZANIAN AUTHORITIES CAN LEASE THE SAUDIS PLOTS EACH OF WHICH COVERS UP TO 10K HECTARES FOR A 99-YEAR PERIOD!?"
DID I QUOTE THAT RIGHT? YES I DID.
CALL ME ONE OF THE DOUBTING THOMASES BUT IF THIS STORY IS TRUE,THEN PERHAPS THE LIKE OF CHIEF MANGUNGO WERE NOT SO DUMB WHEN THEY WERE DUPPED INTO SIGNING SOME CRAZY LAND CONTACT WITH KARL PETERS&co..AT LEAST THE CHIEFS COULD HAVE AN EXCUSE...IT'S DURING THE "DARK AGES" AND THE FORE-RUNNERS OF COLONIALISM TOOK OF ADVANTAGE OF THE CHIEFS' ILLITERACY AND LACK OF SUFFICIENT KNOWLEDGE IN GOVARNANCE OF THEIR PEOPLE AND PROPERTY.
BY THE WAY,INSTEAD OF BEGGING THE SAUDIS,WHY SHOULDNT THE PRIORITY BE IN EMPOWERING THE LOCAL FARMERS IN A COUNTRY WHERE THE ECONOMY DEPENDES HEAVILY ON AGRICULTURE THAT ACCOUNTS FOR MORE THAN 40% OF GDP?
HIVI HAWA WAHINDI WAMETUROGA HADI KUFIKIA HATUA YA KUBADILISHA MAJINA YA MITAA YETU KWA MINAJILI TU YA KUKIDHI LADHA ZAO!HUYU ABUU JUMA,MEYA WA MANISPAA YA ILALA SI ALIAHIDI KUFANYIA KAZI TABIA HII CHAFU YA KUBADILISHA MITAA PASIPO KIBALI?FOR THAT MATTER,INAELEKEA CITY FATHERS WAMEAMUA "KUKUBALI MATOKEO" NA HATIMAYE KUWAACHA HAO WAHINDI WAJIBADILISHIE MAJINA YA MITAA KWA NAMNA WANAVYOTAKA!
NA KAMA DESTURI ILIVYO,YAYUMKINIKA KUAMINI KWAMBA "KUKUBALI MATOKEO" HUKO HAKUKUFANYIKA HIVI HIVI TU,KUNA FISADI "KADIKISHWA KITU" KURIDHIA UCHAFUZI WA HISTORIA.OLE WAO WANAOENDEKEZA TAMAA ZAO ZA FEDHA NA KUPUUZA URITHI WETU WA KIHISTORIA.IPO SIKU MAKABURI YAO YATABOMOLEWA KWA HASIRA YA VIZAZI VIJAVYO.WHY NOT?MTU YEYOTE MWENYE AKILI TIMAMU ANAPASWA KUKASIRISHWA NA UPUUZI WA NAMNA HII.
17 Apr 2009
17.4.09
Evarist Chahali
CCM, JK, RUSHWA TANZANIA, YUSUPH MAKAMBA
No comments
KWA MUJIBU WA GAZETI LA Uhuru,KATIBU MKUU WA CCM,YUSUPH MAKAMBA,AMEAGIZA UONGOZI WA CCM NA JUMUIYA ZAKE NGAZI ZA MIKOA KUANDAA MAPAMBANO YA KUMPONGEZA JK NA SERIKALI KWA KAZI NZURI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA.....Nadhani muda si mrefu kutakuwa na tangazo jingine la kuagiza maandamano ya kupongeza mafanikio ya kutimizwa kwa ahadi ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA sambamba na pongezi za kuwabainisha wamiliki wa Kagoda.
CCM HOYEEEE!!!!!
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!!!!
That's all I can say!
Habari nyingine ndani ya gazeti hilo ni pamoja na "UFISADI MALIASILI:Sh Bil 2.4 zayeyuka kiutatanishi;Mil 790 zatumika kununua pikipiki hewa;Watumishi watimuliwa,wachunguzwa"
Subscribe to:
Posts (Atom)