4 Sept 2010

Kwa mujibu wa blogu ya Utakapojua Hujui Ndipo Utakapojua (mwanahabari mahiri Ansbert Ngurumo),Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwa alionekana Ikulu siku ya Alhamisi majira ya saa 9 alasiri ambapo inaelezwa alikutana na Rais Jakaya Kikwete,mgombea wa CCM ambaye amelalamikiwa na Chadema kwa kukiuka Sheria y Gharama za Uchaguzi.Awali,Tendwa alisema kuwa angetoa "hukumu" keshokutwa (Jumatatu).

Kwa hakika,haihitaji utaalam wowote kuhusisha tukio hilo (la Tendwa kukutana na Kikwete) na pingamiz la Chadema.Na haihitaji ujuzi wa sheria kubashiri matokeo ya "hakimu kukutana faragha na mshtakiwa" siku chache kabla ya hukumu.

Wengi wetu tunafahamu Tendwa atasema nini hiyo Jumatatu.Most likely,ameshafanya maamuzi ila kinachoshughulikiwa sasa ni usanii wa lugha ya utoaji wa maamuzi hayo.Na ni katika hilo ndio maana inamlazimu awasiliane na JK ili "ajenge mazingira ya hukumu ya haki".Katika mazingira tuliyonayo ambapo Msajili wa vyama vya siasa ni kama kibaraka wa CCM,haiwezekani kabisa kiongozi huyo kutoa maamuzi ya haki yatakayokiathiri chama hicho.

Na dalili za "usanii" zimeonekana tangu Chadema wawasilishe malalamiko yao.Hivi Tendwa anaweza kuwaambia Watanzania kwanini imchukue takriban wiki nzima kutoa maamuzi kuhusu malalamiko ya Chadema?Je hiyo pekee sio dalili ya uzembe na kutowajibika ipasavyo?Awali aliwaeleza waandishi wa habari kuwa angetoa maamuzi Jumatatu lakini hakueleza kwanini itachukua muda wote huo kutoa maamuzi hayo muhimu kwa mustakabali wa demokrasia nchini mwetu.Jibu jepesi ni kwamba hana ubavu wa kutoa maamuzi kabla ya kupata ridhaa ya CCM.Na kwa vile CCM ndio watuhumiwa,ni dhahiri maamuzi ya Tendwa yataelemea kuipendelea CCM.

Nafahamu kuna wataosema "aah,sasa kelele za nini wakati maamuzi hayajatolewa?" Wana haki ya kusema hivyo lakini wanapaswa pia kutambua vema mapungufu ya Katiba yetu yanayomfanya mgombea wa chama tawala kuwa na advantage kubwa dhidi ya wagombea wengine kutokana na ukweli kwamba Katiba inampa rais nguvu kubwa mno.

Kikwete ameendelea kupuuza malalamiko ya Chadema kwa kuzidi kutoa rushwa ya ahadi katika mikutano yake ya kampeni.Sote tumemsikia akiwazuga wapigakura huko Mbagala kuhusu daraja la Kigamboni na ahadi nyingine hewa ya huduma ya uhakika kwa maji jijini Dar es Salaam.Huyu mtu hana aibu kwa sababu ahadi anazotoa sasa zinatoa picha ya mgombea anayeomba idhini ya kuingia madarakani kwa mara ya kwanza na sio aliyekuwa rais wetu kwa miaka mitano iliyopita.Kama tangu 2005 hadi leo ameshindwa kuwezesha ujenzi wa daraja hilo la Kigamboni,kwanini tumwamini kuwa ataweza katika mhula wake wa mwisho (2010-2015) hasa ikizingatiwa kuwa kipindi hicho cha pili kitatumika zaidi kwa yeye kujitengenezea mazingira ya "kustaafu kwa amani"?

Jeuri ya Kikwete inasababishwa na ufahamu kuwa Chadema,na vyama vingine vya upinzani,havina mahala pa kukimbilia pindi wasiporidhishwa na mwenendo wa kampeni za Kikwete na CCM kwa ujumla.Anafahamu kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa,Mahakama na taasisi nyingine za kusimamia uchaguzi na sheria nza nchi kwa ujumla,ziko mikononi mwa CCM.Hata hivyo,wapinzani hawapaswi kukata tamaa kwa vile nchi yetu kama masikini wa kutupwa inategemea sana misaada ya wafadhili.Japo kuwapigia magoti wafadhili kunaweza kutafsiriwa kama "kuegemea kwenye ukoloni" lakini tufanyeje kama nchi yetu inaendeshwa kiholela.Binafsi,nina matumaini makubwa kuwa nchi wafadhili zinafuatilia kwa karibu mwenendo wa kampeni za vyama vya siasa nchini na hazitasita kuchukua hatua mwafaka pale CCM itakapotumia ubabe wake kulazimisha ushindi.

Hata hivyo,wakati we keep on hoping for the best and expecting the worst,Tendwa afahamu kuwa he wont get away with this issue as easily as he might think.Blogu hii inaamini kuwa Chadema ni chama makini na chenye rekodi nzuri ya ufuatiliaji mambo.Ni katika mantiki hiyo basi blogu hii inatarajia kuwa Chadema hawatamruhusu Tendwa kufanya uhuni wa aina yoyote ile katika maamuzi yake.Ni heri uchaguzi uvurugike lakini haki ipatikane.Kutoa fursa ya sheria za nchi kupindishwa kwa namna watawala wanavyotaka ni hatari sana hasa tukizingatia ulevi wa madaraka unaowakabili viongozi wengi wa "dunia ya tatu".

Kama alivyoandika Ngurumo katika blogu yake,nami narejea kumkumbusha Tendwa kuwa HATUDANGANYIKI!




Brought to you by Urban Pulse Creative

3 Sept 2010


CHANZO: Jamii Forums

Wenye busara zao wanatuusia kuwa pindi ukiwa unaishi kwenye nyumba ya vioo then sio wazo jema ku-entertain kurusha mawe.Mantiki ya msemo huo ni kwamba kama una ishu zenye utata katika maisha yako then sio wazo jema kuanza kushupalia ishu za watu wengi lest flani akakugeuzia kibao.

Lakini usemi huo umeonekana hauna maana kwa Katibu Mkuu wa CCM,Yusuph Makamba,ambaye kwa siku kadhaa sasa ameamua "kuvalia njuga maisha binafsi ya Dokta Wilbroad Slaa" na kuligeuza suala la ndoa ya mgombea huyo wa Chadema kuwa ajenda ya uchaguzi.

Pengine ni dharau au ujinga,Makamba alijisahau kuwa wakati anamnyooshea kidole Dkt Slaa,yeye mwenyewe (Makamba) alikuwa na doa linaloweza kabisa kumpeleka jela.Kwa mujibu wa taarifa zilizozagaa mtandaoni,Makamba anatuhumiwa kumbaka mwanafunzi wakati akiwa mwalimu mkuu wa shule moja na hatimaye kufukuzwa ualimu.

Hizi ni tuhuma nzito sana kwani licha ya kumtia doa Makamba kama mwanasiasa,ni suala linaloweza kumpeleka jela endapo victim wake atajitokeza hadharani,na kupatiwa msaada wa kisheria.Lakini tukiweka ishu za kisiasa kando,hapa kuna suala la binti asiye na hatia ambaye inadaiwa alibakwa na mtu aliyekabidhiwa dhamana ya kumpatia elimu na mwongozo katika maisha yake,mwalimu wake,lakini akaishi kubakwa.

Blogu hii inatoa ombi maalum kwa yeyote yule anayeweza kuipatia taarifa za uhakika kuhusu binti huyo anayedaiwa kubakwa na Makamba.Lengo si kumkomoa mtuhumiwa bali kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake as well as kutoa reminder kwa watu wengine wanaotumia vibaya dhamana walizokabidhiwa,iwe mashuleni,makazini au hata katika ngazi ya familia.

Je unamfahamu binti anayedaiwa kubakwa na Makamba?Kama jibu ni ndiyo basi tafadhali sana tuwasiliane kwa barua pepe kwa anuani hii [email protected].

1 Sept 2010

Kama waliweza kuchakachua kadi zao wenyewe kwenye kura za maoni watashindwaje kufoji za Chadema?Na wameshamgeuza sehemu ya kufanyia mazoezi kuzuga kama anavyotabasamu hapo chini kwa kupewa "two hundred thousand USD za $300,000/="!!!!


31 Aug 2010





Mwezi Juni mwaka huu tuzo maarufu ya kimataifa iitwayo Ashden Awards iilitolewa kwa wahusika kadhaa duniani zikiwepo nchi za Afrika Mashariki. Tuzo hiyo hutolewa na shirika maalum lililoundwa na duka maarufu la matajiri wa Uingereza yaani Sainsbury Kutoka katika Ashden Trust Charity ambapo mlezi wake akiwa ni Prince Charles. Lengo lake ni kusaidia kurekebisha na kuboresha mazingira duniani . Tuzo ya mwaka huu ilitolewa kwa watafiti na wabunifu waliotengeneza zana za kutengeneza umeme kutokana na nguvu asilia za jua yaaani Solar Energy.
Ingawa wabunifu walitoka mataifa mbalimbali ya Marekani, Asia na Afrika washindi pia walihusisha Kenya, Uganda na Tanzania.
Umeme Jua, Bio gas( Gas Itokayo kwenye kinyesi cha ng'ombe) ni zana ambayo itawasaidia watu maskini hasa wanaotoka nchi kama yetu Bongo vijijini.
Baada Ya Mafanikio makubwa la movie ya £ovely Gamble Urban Pulse wakishirikiana na Msanii/ Mhariri Freddy Macha Wamepewa mzigo mwingine wa kutengeneza documentary ambayo itakuwa hewani tarehe 2 sept 2010 na kurushwa katika tv za hapa ukerewe na mabara mengine ya ulaya.
Hivyo basi utawala wa Urban Pulse Unawaletea trailer ya documentary hiyo hapo juu.

Baada ya uzinduzi tutawapatia kipindi chote
Asanteni sana
Urban Pulse Creative

30 Aug 2010

Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kimewasilisha rasmi pingamizi dhidi ya mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Jakaya Kikwete kwa madai ya kukiuka Sheria ya Gharama za Uchaguzi (iliyosainiwa na Kikwete kama Rais).Imedaiwa kuwa Kikwete amenongeza mishahara ya watumishi wa umma kinyume cha taratibu,na inatafsiriwa kuwa ni rushwa.

Stay tuned!

Kwa mujibu wa mwana-Jamii Forums

Nimekutana na habari hii huko Jamii Forums,nami naiwasilisha kama ilivyo:

Dola kuishughulikia CHADEMA
DAWATI LA HATUDANGANYIKI limepokea taarifa za kuaminika kutoka vyanzo vyake kuwa kuwa mara tu baada ya mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CHADEMA, siku ya Jumamosi tarehe 28 Agosti 2010 wakuu wa Idara ya intelejensia walikutana na timu ya Kampeni ya CCM kwa ajili ya kutoa mlisho nyuma, na kupanga mikakati ya kuikabili CHADEMA, na yafuatayo yalijiri:-
a)Idara ililazimika kutolea ufafanuzi sababu zilizopelekea shauri wake wa kutaka matangazo ya TBC ya mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za CHADEMA kurejeshwa mara moja baada ya kukatizwa. Walieleza kuwa ilitokana na maelfu ya wananchi waliohudhuruia mkutano huo kuwa wa kwanza kugundua kukatishwa kwa matangazo hayo na kuamua wenyewe, bila ya kushawishiwa na kiongozi yeyote kuchukua hatua kali sana dhidi ya TBC. Viongozi wa CHADEMA walistukia tuu mkutano ukitaka kuvurugika kwa wananchi kudai vikali kurejeshwa kwa matangazo hayo. Ilielezwa kuwa kuvurugika kwa mkutano ikwa sababu ya kukatishwa kwa matangazo ya chombo cha umaa kama TBC iimeelezwa kuwa ingekuwa ni aibu kubwa kwa Serikali na TBC.
b)Idara ilitoa taarifa kuwa licha ya umati wa watu waliohudhuria kutofikia ule wa mkutano wa uzinduzi wa CCM, lakini kwa kuwa umati huo kila mtu alijinyanyua kutoka atokako na kuja Jangwani kwa ajili ya CHADEMA tofauti na maandalizi makubwa ya usafiri, fedha, burudani za kila aina, viburudisho n.k yaliyofanywa na CCM kuwafikisha watu kwa maelfu Jangwani. Hizo ni dalili mabaya na ni tishio kubwa kwa CCM. Na ikaamuliwa kuwa iandaliwe mikakati ya kuwakatisha tamma wananchi wenye mapenzi na CHADEMA.
Mkakati :- Ilamuliwa kuwa upandikizwe mgogoro baina ya viongozi wa CHADEMA na mgombea wake Dr W. Slaa; na kuwachonganisha na wapiga debe wao akina Marando, Shibuda, Mpendazoe n.k kwa nia ya kuwakatisha tamaa wenye mapenzi na CHADEMA na wote wanaotarajia kuwapigia kura wagombea wa CHADEMA.
Iliamualiwa kwa kuwa wananchi wanampenda sana Dr W Slaa, zisambazwe habari kuwa aelewani na Mwenyekiti wake Ndg Freeman Mbowe kwa sababu Dr Slaa sio kutoka kabila la wachagga. Ilikubaliwa kuwa taarifa hizo zianze kusambazwa wiki inayoanzia Jumatatu ya tarehe 30 Agosti 2010. Na tathmini ifanyike kujua mafanikio yake wakati zinatungwa mbinu mpya.
Iliamuliwa kuwa magazeti ya New Habari Corporation ikiwemo Mtanzania, Rai n.k yaanze kutumika kwa kazi hiyo wakati waandishi zaidi wa kufanya kzai hiyo wakitafutwa.
Ili wananchi wenye mapenzi mema na CHADEMA waweze kusadiki taarifa zitakazosambazwa ilikubaliwa kuwa magazeti yatakayotumika yaanze kwanza kwa kipindi kifupi kuandika habari njema kuhusu CHADEMA na wagombea wake; na baada ya mashabiki wake kuyaamini magazeti na vyombo hivyo vya habari ndipo kazi ya kuisamabaratisha CHADEMA ianze rasmi.
Ili kutekeleza mipango hiyo waandishi wa gazeti la Mtanzania walipatiwa maelekezo ya kurekebisha kichwa cha habari na maudhui ya habari za uzinduzi wa CHADEMA zilizochapishwa tarehe 29/8/2010, kwa lengo hilo.
Vyombo vya habari vya Serikali ya ikiwemo magazeti ya Daily News na Habari Leo na TBC na redio za TBC vilielekezwa kuanza mara moja kazi ya kuipamba CHADEMA kama chama na watu wa fujo mbele ya jamii makakati amabo unadaiwa kufanikiwa sana kuisambaratisha CUF mwaka 2005, wakati Mkuu wa chombo kimoja cha dola alipodai siku moja kabla ya upigaji kura wamekamata shehena ya majambia yenye rangi za bendera za CUF
c)Pingamzi la CHADEMA dhidi ya Jakaya Kikwete mkutano ulikubaliana kuwa kuaniza sasa idara ihakikishe kuwa inamgeuzia kibao Dr Slaa na kusambaza habari kwa wafanyakazi na umma kuwa DR Slaa anapinga wafanyakazi kuongezwa mishahara ndio maana CHADEMA inamuwekea pingamizi mgombe wa CCM Jakaya Kikwete kwa kitendo cha kuwaongezea mishahara watumishi wa umma katika kipindi hiki cha kampeni.
Dawati litaendelea kuwahabarisha!!!!!!!

If it's true,hivi hii sio local version yetu ya Watergate?

From Lt. Gen. Peter Olu
From:

NATIONAL SECURITY ADVISER 
Add to Contacts
OFFICE OF THE NATIONAL SECURITY ADVISER
TO THE PRESIDENT FEDERAL REPUBLIC OF NIGERIA
GET BACK TO ME AT YOUR EARLIEST CONVENIENCE

Dear Sir/Madam,

I am Lt. Gen. Peter Olu, National Security Adviser to the New President Dr Goodluck Jonathan Federal Republic of Nigeria. I decided to contact you because of the prevailing security report reaching my office and the intense nature of policy in Nigeria. This is to inform you about our plan to send your fund to you via cash delivery. This system will be easier for you and for us. We are going to send your contract part payment of US4.1 Million to you via diplomatic courier service.

Note: The money is coming on two security proof boxes. The boxes are sealed with synthetic nylon seal and padded with machine. This fund was brought to us from America; it was meant for our Local AFEM market. But since the money was not used, I will use my position as the National Security Adviser to the President to send this fund to you.

The boxes are coming with a Diplomatic agent who will accompany the boxes to your house address. All you need to do now is to send to me

Your full name
Your house address
Your age
Your marital statue
Your identity such as, international passport or driver license
Your contact phone and fax numbers,

The Diplomatic attached will travel with it. He will call you immediately he arrives your airport. I hope you understand me.

I will let you know by the special grace of God when the boxes are airlifted.

Note: The diplomatic does not know the original contents of the boxes. What l declared to them as the contents is Sensitive Photographic Film Material. I did not declare money to them please. If they call you and ask you the contents please tell them the same thing OK, I will let you know how far I have gone with the arrangement. I will secure the Diplomatic immunity clearance certificate that will be tagged on the boxes to make it stand as a diplomatic consignment.

This clearance will make it pass every custom checkpoint all over the world without hitch. Confirm the receipt of this message and send the requirements to me immediately you receive this message. If you need more information about this, I will give you the details how to contact the diplomat for more information on how to carry out the plan.

I need you response because the boxes are schedule to leave as soon as we hear from you. Reply me immediately you receive this message via Email ([email protected]) Call me on my direct phone: (+234-8063619571) or Fax: (234-8029402741)

Best Regards,
Lt. Gen. Peter Olu

28 Aug 2010

Bonyeza HAPA kupata up-to-the-minute updates za uzinduzi wa kampeni za Chadema katika viwanja vya Jangwani.

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.