4 Aug 2013
3 Aug 2013
2 Aug 2013

HATIMAYE PINDA KUWA
WA KWANZA KUBURUZWA MAHAKAMANI ...
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimemfungulia mashtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutokana na kauli yake aliyoitoa bungeni hivi karibuni kwamba wanaokaidi maagizo ya dola wapigwe.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimemfungulia mashtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutokana na kauli yake aliyoitoa bungeni hivi karibuni kwamba wanaokaidi maagizo ya dola wapigwe.
Hatua hiyo ya LHRC imepingwa vikali na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), Dk Elieza Feleshi akisema hakuna uhalali wa mashtaka yoyote dhidi ya kiongozi huyo sababu kauli ya Pinda kuwa pigeni haikuwa piga ua.
Mkurugenzi wa LHRC, Dk Hellen Kijo Bisimba alifungua mashtaka hayo katika Mahakama Kuu jana akisema kuwa wanamshtaki Waziri Mkuu kwa maelezo kuwa amekiuka kifungu cha Katiba Ibara 13 (1). Pinda ametajwa kuwa ni mdaiwa wa kwanza katika kesi hiyo namba 24.
Mkurugenzi wa Maboresho na Utetezi wa LHRC, Harold Sungusia alisema jana kwamba, mwingine aliyeunganishwa katika kesi hiyo ya kikatiba iliyofunguliwa na LHRC na Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.
Alisema katika kesi hiyo, kuna jopo la mawakili wasiopungua 20 na kwamba wamepata saini za wananchi 2,029 wanaopinga kauli hiyo ya Pinda na kuunga mkono kufunguliwa kwa kesi hiyo.
Mjumbe wa Bodi ya LHRC, Wakili Dk Ringo Tenga alisema katika kesi hiyo wameangalia zaidi sheria na hasa haki za msingi za binadamu na kwamba kauli hiyo ya Waziri Mkuu Pinda inahatarisha haki hizo.
Kauli yenyewe
Wakati wa Kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu bungeni, Juni 19, mwaka huu, Waziri Mkuu akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu aliyeuliza: “Serikali ipo tayari kiasi gani kubainisha na kuchukua hatua stahiki, badala ya kusakama makundi fulani, tujue chanzo halisi cha vurugu hizi na matatizo haya na jinsi gani vyombo vya dola vinavyoshughulikia kwa sababu yapo malalamiko katika baadhi ya maeneo kama Mtwara kwamba wananchi wanapigwa na vyombo vya dola?”
Waziri Mkuu alijibu: “Ni lilelile nililosema... mwishowe unaona anasema vyombo vya dola vinapiga watu. Ukifanya fujo, umeambiwa usifanye hiki, ukaamua kukaidi, utapigwa tu... hamna namna nyingine, maana wote tukubaliane kwamba nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria.
“Sasa kama wewe umekaidi, hutaki unaona kwamba ni imara zaidi... wewe ndiyo jeuri zaidi watakupiga tu.... Mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine... maana tumechoka.” Kesi hiyo itakayosikilizwa na majaji watatu, haina uhusiano na kesi nyingine ambazo wajibu maombi hupewa siku 90 kujibu hoja zilizowasilishwa. Kesi hiyo imefunguliwa kwa mujibu wa Katiba Sura ya Tatu.
Akizungumza juzi kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma baada ya kufungwa kwa Warsha ya Wapelelezi na Waendesha Mashtaka wa Serikali ngazi ya mikoa, Dk Feleshi alisema hakuna uhalali wa mashtaka hayo kwa sababu kauli ya Pinda kuwa pigeni haikuwa piga ua.
“Hii haikuwa kuchochea apige watu, alichosema ni kupiga wale wasiotaka kutekeleza amri halali na zaidi alisema piga lakini si kupiga na kuua,” alisema.
Mkutano huo uliendeshwa chini ya ulinzi mkali huku kukiwa na udhibiti wa kuvuja siri kwa kiwango cha juu. Pamoja na mambo mengine, ulikuwa ukijadili mbinu za kisasa katika kuendesha kesi pamoja na kujiuliza sababu za Serikali kushindwa katika kesi nyingi.
“Kwa sababu lile neno kupiga ni lazima lipewe maana pana huwezi kumpiga tu mtu hivihivi ambaye hakuvunja sheria lakini nilivyoelewa, ilikuwa ni hivyo, ni sawa na mtu ambaye anamshambulia askari,” alisema Dk Feleshi.
Alisema kuna sheria ya kutumia nguvu pale ambako kuna mkusanyiko usiokuwa wa halali pindi raia wanapokaidi kutawanyika kwa hiari hivyo hakuna shaka kauli ya Waziri Mkuu ililenga hivyo.
Hata hivyo, alisema hajapata taarifa za LHRC kumshtaki Waziri Mkuu kimaandishi na kwamba akizipata atatoa ufafanuzi baada ya kuona lengo la mashtaka.
Msimamo
Akizungumza baada ya kufungua mashtaka hayo, Dk Bisimba alisema Waziri Mkuu anaweza kushtakiwa kwa kuwa alizungumza kwa nafasi yake ya Waziri Mkuu na si mbunge na kusisitiza kwamba hakuna aliye juu ya sheria na kudai kwamba kauli hiyo ni kinyume cha Katiba.
Alisema kuwa kila anayevunja Katiba lazima ashughulikiwe kisheria na kwamba mahali pake ni mahakamani tu. Alisema kwa mujibu wa hati hiyo ya madai, kauli na amri kama hizo zinapotolewa na kiongozi mwenye hadhi kama ya mdaiwa wa kwanza (Waziri Mkuu) huchukuliwa kama sheria inayopaswa kutekelezwa na wakala wa utekelezaji wa sheria kama vile polisi. Wadai hao wanadai kuwa kwa ufahamu wao polisi wanaweza kuchukulia kauli hiyo kama amri halali kutoka kwa mkubwa wao na hivyo kuwapiga na kuwatesa watu wasio na hatia, kinyume cha Katiba.
Pia wanadai wanatambua kuwa Ibara ya 100 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa kinga kwa wabunge na uhuru wa maoni bungeni. Hata hivyo, wanatambua kuwa Ibara ya 100 (2) ya Katiba hiyo inawawajibisha wabunge wote chini ya masharti ya Katiba na kwamba kauli aliyoitoa Waziri Mkuu Pinda inakiuka Ibara ya 12(12).
Hivyo wanaiomba Mahakama hiyo itamke kuwa kauli na amri hiyo aliyoitoa Pinda inavunja Katiba.
Mkurugenzi wa taasisi inayofuatilia Mwenendo wa Bunge (Watch), Marcos Albania alidai kwamba wamegundua kuwa kauli hiyo ya Pinda ni moja kati ya matamko makubwa yanayovunja Katiba.
Alisema mbali na shtaka hilo, kuna la pili dhidi ya Waziri Mkuu Pinda, ambalo hawajalifikisha mahakamani ambalo pia linatokana na kauli hiyo aliyoitoa bungeni kwamba: “Sasa wamechoka.”
1 Aug 2013
1.8.13
Evarist Chahali
RAIA MWEMA
No comments

TANGU niwasili kwa mara ya kwanza hapa Uingereza zaidi ya miaka 10 iliyopita, nimejijengea tabia moja ambayo ni mithili ya ‘ibada’ yangu kila asubuhi, kusoma habari za huko nyumbani katika vyanzo mbalimbali vya habari mtandaoni.
Na ni katika mwendelezo wa tabia hiyo, Oktoba 2006 nilikutana na habari moja iliyohusu ‘sakata la Richmond.’ Katika habari hiyo ndani ya gazeti moja la kila siku huko nyumbani (Tanzania), ilielezwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alikuwa anafanya jitihada za kuhamasisha wabunge wa CCM wawe na msimamo mmoja katika mjadala bungeni kuhusu sakata hilo.
Wakati huo nilikuwa nikituma makala katika gazeti moja la kila wiki huko nyumbani (sio hili), na kutokana na kuguswa na habari hiyo ambayo iliashiria uwepo wa harakati za kukwaza mjadala wa maana kuhusu skandali ya Richmond, niliifanya habari hiyo kuwa mada kwenye makala ya wiki iliyofuatia.
Makala hiyo ilinisababishia matatizo makubwa. Kwanza, mwandishi wa habari wa Waziri Mkuu (wakati huo) aliandika makala kali ya kunijibu, pamoja na mambo mengine aliniita mpotoshaji, huku akikanusha kwa nguvu mtizamo wangu kuwa ‘Lowassa alikuwa anajaribu kuwafumba mdomo wabunge wa CCM wasijadili suala la Richmond bungeni kwa ufanisi.’
Siku chache baadaye, nilipata simu kutoka kwa kiongozi mmoja wa juu wa taasisi niliyokuwa nikiitumikia wakati huo. Katika simu hiyo, bosi huyo alihoji iwapo nipo hapa Uingereza kimasomo au kisiasa. Alikwenda mbali zaidi na kunituhumu kuwa huenda wakati huo nilikuwa nikiitumikia Serikali ya Uingereza, kosa ambalo kwa mujibu wa kanuni za sehemu niliyokuwa mtumishi wakati huo ni sawa na kosa la uhaini (treasonable offence).
Kadhalika, kiongozi huyo, alinishambulia kuwa makala zangu zilikuwa zikiwapa hoja wapinzani wa CCM, na kisha kuniamuru niache mara moja kuandika makala zinazohusu masuala ya siasa za huko nyumbani. Nilijaribu kutii amri hiyo kwa muda mrefu lakini baadaye nikashindwa baada ya kuja huko nyumbani mwaka 2008 na kushuhudia jinsi mafisadi walivyokuwa wakiitafuna nchi yetu.
Kosa lililosababisha bosi huyo kufikia hatua ya kinipigia simu ya karipio ni makala hiyo niliyobainisha hapo awali, ambayo kimsingi ililenga kushauri uwepo wa mjadala huru na wa wazi kuhusu sakata la Richmond. Katika makala hiyo nilitahadharisha kuwa jitihada zozote za ‘kulifunika suala hilo chini ya kapeti’ zinaweza kuzua madhara huko mbele.
Miaka miwili baadaye, nilichobashiri katika makala hiyo kikatokea. Hatimaye Lowassa alilazimika kujiuzulu kutokana na skandali hiyo ya Richmond. Kama nilivyoitarajia, yule bosi aliyenikaripia mwaka 2006 hakunipongeza, na sidhani kama hadi leo (bado yupo madarakani) anatambua umuhimu wa nilichoandika wakati huo.
Kimsingi, tukio hilo ndio lilikuwa mwanzo wa uhusiano mbaya na mwajiri wangu, na picha iliyozidi kujengeka ni ya mie kuonekana msaliti kwa ‘kuisema vibaya’ CCM na serikali yake. Japo kimsingi nyingi ya makala zangu kuhusu siasa ziliendana na wajibu wa taasisi hiyo kwa umma, vitisho na manyanyaso mfululizo hatimaye vilisababisha ajira yangu katika taasisi hiyo ‘kutowezekana.’
Lengo la makala hii sio kumlaumu mtu au taasisi fulani. Pamoja na misukosuko kadhaa niliyopitia kutokana na dhamira yangu kunituma kujadili masuala mbalimbali yanayokwaza maendeleo ya nchi yetu, hususan ufisadi, bado ninaamini kwa asilimia 100 kuwa ninafanya jambo stahili, hata kama limeshanigharimu katika maisha.
Nilichokuwa ninafanya nilipokuwa mwajiri wa taasisi hiyo ndicho hasa kilichopaswa na kinachopaswa kufanywa na kila mwajiriwa na kiongozi wa taasisi hiyo ya umma, sambamba na kila Mtanzania mwenye upendo wa kweli kwa nchi yetu. Hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania, na tusipoilinda na kuienzi hatutokuwa na pa kukimbilia (hasa tukizingatia hivi sasa tuna uhusiano wa shaka na baadhi ya majirani zetu).
Kilichonisukuma kurejea mkasa huo ulionikumba miaka kadhaa iliyopita ni mawasiliano niliyofanya majuzi na mwalimu wangu mmoja wa zamani hapo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Binafsi, mwalimu huyo ni kama mzazi wangu kielimu kwani ameniongoza tangu nikiwa mwanafunzi wake hapo ‘Mlimani,’ na kuniunga mkono kitaaluma hadi nikamudu kupata shahada nyingine mbili (licha ya niliyoipata UDSM), na ameendelea kuwa nguzo yangu muhimu wakati huu ninaposaka shahada ya nne – ya uzamivu (licha ya vikwazo mbalimbali vya kimaisha nilivyokumbana navyo).
Mwalimu huyo (ambaye ninaomba nihifadhi jina lake) alinieleza kuwa amekuwa akizungushwa na serikali kuongezewa mkataba wake kama mhadhiri katika kitivo kimoja chuoni hapo. Pengine msomaji unaweza kudhani nimeguswa na suala hili kwa vile tu mhadhiri huyo amekuwa na msaada katika maisha yangu kitaaluma. Ukweli ni kwamba takriban kila mwanafunzi aliyefundishwa na mhadhiri huyo atakubaliana nami kuwa mwanataaluma huyo ni mfano wa kuigwa kwa jinsi anavyojibidiisha kuhakikisha wanafunzi wake wanafaulu.
Na kujibidiisha huko hakumaanishi kuwapatia wanafunzi njia za mkato bali ni pamoja na kutumia muda wake binafsi hata katika siku za mapumziko kuwafundisha wanafunzi wake, iwe ni katika majengo ya chuo au nyumbani kwake.
Uzuri mwingine wa mhadhiri huyo ni ukweli kwamba yeye si muumini wa hizi dini zetu za ‘mapokeo’ yaani Ukristo na Uislamu. Ninasema ni ‘uzuri’ kwa sababu pamoja na mazuri ya dini zetu, kuna aina fulani ya ‘ubaguzi uliofichika’ unaotokana na mafunzo ya dini hizo, hususan katika kipengele cha ‘imani yangu ndio sahihi kuliko nyinginezo.’ Asiye muumini wa Ukristo au Uislam, kama ilivyo kwa mhadhiri huyo, ana ‘faida’ ya kuelezea mambo pasi kukwazwa na ‘sheria kali za kiimani’ zinazotawala dini zetu.
Katika kubobea kwenye taaluma ya Sosholojia (elimu-jamii), mwongozo mkubwa wa kitaaluma na kimaisha kwa mwalimu huyo ni jamii. Na ndio maana, kama ilivyo katika masuala ya dini, yeye amekuwa ‘neutral’ (asiyefungamana na upande wowote) katika itikadi za kisiasa. Kwake, jamii ndio nyanja muhimu zaidi katika maisha ya mwanadamu.
Mhadhiri huyo anashangaa kwa nini serikali imekuwa ikisuasua kumwongezea mkataba wake hasa ukizingatia kuwa utendaji kazi wake ni wa hali ya juu hadi amefikia hatua ya kupata Uprofesa. Na kwa kila anayemfahamu, kusita kwa serikali kumwongezea mkataba mwanataaluma huyo kunaashiria jambo moja tu; kutothamini michango ya Watanzania wenzetu wanaojitolea kwa maslahi ya taifa letu.
Bahati nzuri amefanikiwa kupata chuo kikuu cha kufundisha katika nchi moja barani Afrika, lakini hata hivyo anajisikia uchungu kuona anakwenda kutoa mchango wa kielimu katika nchi nyingine ilhali taifa letu lina mahitaji makubwa ya wataalamu katika nyanja mbalimbali, hususan elimu ya juu.
Sitaki kujifananisha na mwanataaluma huyo mahiri, lakini kwa kiasi flani, yanayomsibu yanashabihiana na kilichonikumba huko nyuma. Unatumikia umma kwa nguvu na moyo wako wote lakini wenye mamlaka wanakuona kama surplus to requirements (ziada isiyohitajika)
Athari kubwa ya kutothamini wenzetu wanaojitolea kwa ajili ya taifa letu ni ile hisia kuwa “ah, bora ujali tu maisha yako...mbona fulani alijiweka kimbelembele na angalia yaliyomfika.” Kwa lugha nyingine, uzalendo unakwazwa na vitimbi vinavyowaandama wenzetu wanatanguliza maslahi ya umma mbele ya maslahi yao binafsi.
Kwa mwenendo huu, basi tutazidi kushuhudia wataalamu mbalimbali wakiamua aidha kukimbilia kwenye ‘ulaji’ katika siasa au, kama ilivyo kwa mhadhiri huyo, kwenda kutumia utaalamu wao nchi nyingine, na kuliongezea taifa letu uhaba wa wataalamu katika sekta mbalimbali.
- See more at: http://raiamwema.co.tz/imebaki-kazi-moja-tu-kuipigania-tanzania#sthash.QVeXmYgZ.dpuf

Ahadi za JK kwenye kampeni za kusakaurais 2010
1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria- Igunga
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
7. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi- Kagera
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba- Bukoba Mjini
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu- Kagera
15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba- Kagera
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika- Mwanza
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
21. Kulinda muungano kwa nguvu zote- Pemba
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa- Mbeya mjini
24. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
31. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)- Hydom Manyara
35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa-Musoma
36. Kulinda haki za walemavu- Makete
37. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
38. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40. Kujenga barabara ya lami Manyoni- Kigoma– Kaliua,Tabora
41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi- Arusha Mjini
42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
43. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido
44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo- Busekera, Wilaya ya Musoma, .
47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
50. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
52. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
53. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania- Iringa
54. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
55. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
56. kuwapa wanawake nafasi zaidi- Kilolo ,Iringa
57. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
58. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa- Kabandamaiti mjini Zanzibar
59. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
60. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
61. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
62. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa- Kibaha66. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha
31 Jul 2013
WARAKA MZITO WA PAPII KOCHA KWA JK
Na Mwandishi WetuULE waraka wa mwanamuziki aliyefungwa gerezani kifungo cha maisha sambamba na baba yake mzazi, Nguza Viking ‘Babu Seya’, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ umeibua mjadala tena huku Naibu Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiombwa na kukubali kuufikisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
MIAKA 10 GEREZANI
Hivi karibuni wasanii hao walitimiza miaka kumi tangu walipofungwa katika Gereza la Ukonga, Dar mwaka 2003 hivyo kusababisha waraka huo aliouandika Papii Kocha Februari mwaka 2010 kusababisha mjadala upya.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Julai 21, mwaka huu waraka huo ulikuwa gumzo kubwa juu ya ombi la Papii Kocha kwa Rais Kikwete kuwa amhurumie atoke gerezani kwa kuwa bado ni kijana mdogo huku nyuma yake watu wakituhumiana bila ushahidi.
Hivi karibuni wasanii hao walitimiza miaka kumi tangu walipofungwa katika Gereza la Ukonga, Dar mwaka 2003 hivyo kusababisha waraka huo aliouandika Papii Kocha Februari mwaka 2010 kusababisha mjadala upya.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Julai 21, mwaka huu waraka huo ulikuwa gumzo kubwa juu ya ombi la Papii Kocha kwa Rais Kikwete kuwa amhurumie atoke gerezani kwa kuwa bado ni kijana mdogo huku nyuma yake watu wakituhumiana bila ushahidi.
OMBI KWA WAZIRI NYALANDU
Mwandishi Mtanzania aishie Uskochi, Evarist Chahali aliutundika waraka huo katika ukurasa wake wa Twitter na kusababisha msigano wa kimawazo.
Chahali aliusindikiza waraka huo na maneno akimuomba Waziri Nyalandu kwa kuwa ni mmoja wa ‘memba’ wake mtandaoni aufikishe kwa Rais Kikwete kwa kuwa ulimlenga yeye moja kwa zote.
Alimwandikia Waziri Nyalandu: “Nina imani sana kwako, mheshimiwa waziri na kwa vile Rais Kikwete yupo katika swaumu, natumaini kilio hicho kitasikilizwa.”
Kukawa mchana, kukawa usiku, siku hiyo ikaisha.
Mwandishi Mtanzania aishie Uskochi, Evarist Chahali aliutundika waraka huo katika ukurasa wake wa Twitter na kusababisha msigano wa kimawazo.
Chahali aliusindikiza waraka huo na maneno akimuomba Waziri Nyalandu kwa kuwa ni mmoja wa ‘memba’ wake mtandaoni aufikishe kwa Rais Kikwete kwa kuwa ulimlenga yeye moja kwa zote.
Alimwandikia Waziri Nyalandu: “Nina imani sana kwako, mheshimiwa waziri na kwa vile Rais Kikwete yupo katika swaumu, natumaini kilio hicho kitasikilizwa.”
Kukawa mchana, kukawa usiku, siku hiyo ikaisha.
WAZIRI NYALANDU AKUBALI
Kesho yake, yaani Julai 22, mwaka huu, Waziri Nyalandu alimjibu Chahali kwa kumwandikia: “Chahali copy that (nimepokea), asante kaka.”
SEHEMU YA MANENO YA KUCHOMA YA WARAKA WA PAPII KOCHA
Baada ya salamu kwa mkuu huyo wa nchi, Papii Kocha aliyekuwa nyota wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ aliandika: “Naanguka na kushika miguu yako mitukufu mheshimiwa rais.
“Nakuomba msaada (msamaha) kwako mheshimiwa rais kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani, niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu (Kisutu).
“Mhe. Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mhe. Rais.
“Naomba huruma yako mheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninayehitaji huruma yako wewe mzazi.
“Natumaini kauli yako ya mwisho ndiyo itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu.
“Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu. Mungu akubariki.”
Kesho yake, yaani Julai 22, mwaka huu, Waziri Nyalandu alimjibu Chahali kwa kumwandikia: “Chahali copy that (nimepokea), asante kaka.”
SEHEMU YA MANENO YA KUCHOMA YA WARAKA WA PAPII KOCHA
Baada ya salamu kwa mkuu huyo wa nchi, Papii Kocha aliyekuwa nyota wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ aliandika: “Naanguka na kushika miguu yako mitukufu mheshimiwa rais.
“Nakuomba msaada (msamaha) kwako mheshimiwa rais kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani, niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu (Kisutu).
“Mhe. Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mhe. Rais.
“Naomba huruma yako mheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninayehitaji huruma yako wewe mzazi.
“Natumaini kauli yako ya mwisho ndiyo itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu.
“Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu. Mungu akubariki.”
WAKIKUBALIWA WATAREJEA URAIANI?
Baada ya Waziri Nyalandu kukubali kuupeleka waraka huo ikulu na habari hiyo ikasambaa mitandaoni, baadhi ya watoa maoni walikwenda mbele zaidi wakidai huenda ombi lake litakubaliwa na kumfanya Papii Kocha na baba yake kurudi kula bata uraiani.
Wanamuziki hao walifungwa gerezani kwa tuhuma za kunajisi watoto 10 wa Shule ya Msingi Mashujaa, Sinza jijini Dar.
Mbali na kuachiwa kwa baadhi ya watoto wa familia ya Babu Seya waliokuwa wakitumikia kifungo cha maisha, Papii na baba yake bado wanaendelea kutumikia kifungo hicho hadi sasa.
Baada ya Waziri Nyalandu kukubali kuupeleka waraka huo ikulu na habari hiyo ikasambaa mitandaoni, baadhi ya watoa maoni walikwenda mbele zaidi wakidai huenda ombi lake litakubaliwa na kumfanya Papii Kocha na baba yake kurudi kula bata uraiani.
Wanamuziki hao walifungwa gerezani kwa tuhuma za kunajisi watoto 10 wa Shule ya Msingi Mashujaa, Sinza jijini Dar.
Mbali na kuachiwa kwa baadhi ya watoto wa familia ya Babu Seya waliokuwa wakitumikia kifungo cha maisha, Papii na baba yake bado wanaendelea kutumikia kifungo hicho hadi sasa.
29 Jul 2013
29.7.13
Evarist Chahali
Mihadarati
No comments
Ukisoma habari hii utabaini kwanini biashara ya madawa ya kulevya inazidi kushamiri. Ni kwamba, wauza unga wanafahamika,sio kwa polisi tu bali hata kwa Rais Jakaya Kikwete, na hakuna uthibitisho mzuri kama huu uliomo katika habari hii.
Zingatia tarehe ya habari hii,18 SEPTEMBA 2006, les than mwaka mmoja tangu JK aingie madarakani.Sasa kama alikabidhiwa majina tangu wakati huo na hakuchua hatua, hivi waliotajwa katika orodha hiyo wamesha-multiply mara ngapi?
Vigogo dawa za kulevya watajwa
Written by Mwananchi
Monday, 18 September 2006
*Majina yao yapelekwa kwa Rais Kikwete
*Ni orodha ndefu ya majina ya watu 58
*Wamo wafanyabishara, wanasiasa, viongozi wa dini
*Mbinu wanazotumia nazo zaanikwa hadharani
WITO wa Rais Jakaya Kikwete wa kutaka wananchi wajitokeze kutaja majina ya wahalifu nchini, umepata mwitikio mpya, safari hii watu kadhaa wakijitokeza kutaja majina ya vigogo wanaoongoza kwa biashara ya dawa za kulevya nchini.
Majina hayo yako katika barua iliyoandikwa na wananchi 15 kwenda kwa Rais Kikwete, ambamo wanadai kwamba walikuwa wakitumiwa na vigogo hao kufanya biasharahiyo, lakini sasa wameamua kuachana nayo. Barua hiyo iliandikwa Septemba 8, mwaka huu na wahusika wanadai wamekwisha kuiwasilisha Ikulu.
Kwa mujibu wa barua hiyo, majina 58 yameorodheshwa yakiwa katika makundi matatu makubwa, la kwanza likiwa ni waagizaji wakubwa wa dawa hizo; la pili niwafadhili ambao majina yao hutumika kusafirisha dawa hizo; na la tatu ni wauzaji walioko Dar es Salaam, Tanga, Mwanza, Mbeya na Zanzibar.
Katika orodha ya waandishi wa barua hiyo wanaodai kusukumwa na uzalendo na uchungu kwa nchi yao, yamo majina ya wafanyabiashara maarufu nchini na wanasiasa,wakuu wa taasisi nyeti, baadhi ya viongozi wa dini na maafisa wa juu serikalini.
Kundi la kwanza lina majina 12, miongoni mwao ni wafanyabiashara maarufu katika miji ya Dar es Salaam, Morogoro, Zanzibar, Arusha na Bagamoyo na baadhi ya viongozi wa dini wa madhehebu fulani.
Kundi hili linadaiwa kuwa linaingiza dawa za kulevya kwa njia mbalimbali zikiwamo, kutumia mipira ya kondomu, majokofu, vifaa vya hospitali, meli na marobota ya mitumba.
Katika kundi la pili kuna watu 19, miongoni mwao wamo wanasiasa wakubwa nchini wakiongoza kundi hili, kutoka taasisi ya fedha nchini na wafanyabiashara maarufu waDar es Salaam na Zanzibar.
Kundi la tatu lina majina 27, ambao si ya watu wenye majina makubwa, lakini ndio wanaotumika kusambaza mitaani kwa watumiaji wa dawa za kulevya.
Mbali ya kushiriki katika kusambaza dawa za kulevya, kundi hili pia lina baadhi ya majina ya watu waliotajwa kushiriki katika kuingiza silaha nzito zinazotumika kwa ajili ya ujambazi kutoka nchi jirani.
Ufukwe wa Pwani ya Bahari ya Hindi eneo la Muhoro wilayani Rufiji inaelezwa kuwa linatumika kuingizia silaha hizo kutoka nchi jirani pamoja na dawa za kulevya chini ya ufadhili wa mmoja wa wanasiasa nchini.
Uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere unatajwa kuwa unatumiwa na watu hawa kuingiza dawa hizo nchini kutokea nchi za nje, huku baadhi ya maafisa wa polisi watatu wakitajwa kuwa ndio wanaotoa ulinzi kwa watu wanaopitisha dawa hizo.
Nyumba ya afisa wa juu mstaafu katika idara nyeti iliyopo jijini Dar es Salaam inatajwa kuwa inatumika katika kuhifadhi vijana wanaoingiza dawa za kulevya nchini, huku nyumba ya mfanyabiashara mmoja iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam ikitajwa kuwa ndiyo inayotumika kama kituo cha kutolea pipi tumboni kwa vijana wanaotumika kuingiza dawa hizo kutoka nje ya nchi.
Vile vile, katika kundi hili mwanamke mmoja anayefanya kazi katika taasisi moja ya fedha anatajwa kuwa anashiriki katika kuhujumu uchumi wa nchi kwa kusafirisha kwenda nje fedha nyingi za kigeni akitumiwa na mfanyabiashara mmoja maarufu wa dawa za kulevya nchini.
Mipaka ya Tunduma mkoani Mbeya, Horohoro mkoani Kilimanjaro na Namanga mkoani Arusha, nayo imetajwa kuwa inatumika kupitisha dawa za kulevya kwa kutumia mabasi na magari mengine. Kuna kampuni mbili za mabasi nchini zinazotajwa kuongoza kutumika katika usafirishaji.
Barua hiyo ya kurasa 10, pia inamtaja mwanamke mmoja ambaye anatumika kupitisha dawa za kulevya uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere kuwa ni sugu; aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 35 jela kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya, lakini hivi sasa yupo mitaani kifungo chake akitumikia mtu mwingine.
Alipoulizwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Utawala Bora), Philip Marmo, alisema hajapata barua hiyo na kwamba atalizungumzia baada ya kuipata.
Naye Waziri wa Usalama wa Raia, Bakari Mwapachu, alisema hana taarifa za kuwako kwa barua hiyo. Hata hivyo, alisema kuna tume ya dawa za kulevya iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ndiyo inayoshughulikia zaidi suala hilo.
Alisema Jeshi la Polisi linafanya kazi za kukamata watu wanaojihusisha na dawa hizo na kwamba mikakati mingine ya kupambana na watumiaji inafanywa na tume hiyo.
Mwanzoni mwa mwaka huu, Rais Kikwete aliagiza Jeshi la Polisi liongezewe uwezo wa kupambana na uhalifu, ikiwa ni pamoja na kuwahamisha vituo vya kazi askari waliokaa kituo kimoja kwa muda mrefu.
Pia alilitaka Jeshi hilo lijisafishwe lenyewe kutokana na madai kwamba polisi wanahusika na baadhi ya matukio ya uhalifu nchini.
Rais alitoa wito kwa wananchi wenye taarifa zozote za uhalifu, na wanaojua waliko majambazi wazipeleke taarifa hizo kwake kama wanaogopa kuzipeleka polisi.
Katika kuitikia wito huo, wananchi kadhaa waliandika barua iliyooroshesha majina ya polisi 20, wakiwamo baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa na kuikabidhi kwa Waziri wa Usalama wa Rais, Bakari Mwapachu.
Tangu wakati huo, mabadiliko makubwa yameshuhudiwa yakifanywa kwenye jeshi hilo, hata hivyo hii ni mara ya kwanza kwa watu kujitolea kuandika barua yenye majina na maelezo ya kina kama hii kuhusu biashara ya kulevya na kuipeleka kwa Rais.
Subscribe to:
Comments (Atom)









































