23 Mar 2008

Wakati tunasherehekea sikukuu ya Pasaka ni vema tukifanya tafakuri ya mambo ambayo machoni yanaweza kuonekana madogo lakini yenye uzito mkubwa katika hali halisi.Ni muhimu kumshukuru Mungu kwa mengi au machache aliyo/anayotujalia.Hivi kuna zawadi kubwa kutoka kwa Mungu zaidi ya UHAI?Sambamba na uhai ni uzima/ukamili wa miili yetu.Tuliozaliwa tukiwa kamili (yaani bila ulemavu) tunaweza kujisahau kuuliza maswali magumu kama "ingekuwa vipi kama ningezaliwa nina mkono nusu,au pua iliyozama ndani,au hata jicho lililokaa kisogoni" hadi pale tunapowaona wenzetu kama huyu mtu-tembo (elephant man-sio yule wa dancehall),ambaye stori yake inapatikana HAPA

22 Mar 2008

NAWATAKIENI NYOTE HERI NA BARAKA ZA SIKUKUU YA PASAKA.UFUFUKO WA BWANA YESU KRISTO ULETE AMANI,UPENDO,AFYA NJEMA NA MAFANIKIO KWA KILA MMOJA WETU.PAMOJA NA SALAMU HIZI NI SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWENU NYOTE MNAOTEMBELEA BLOGU HII NA KUSOMA MAKALA ZINAZOTOKA KATIKA BAADHI YA MAGAZETI YA NYUMBANI.BWANA AWABARIKI SANA,AMEEN.

Jana nilishuhudia kituko cha mwaka.Mwanzoni nilidhani ni porojo tu lakini asubuhi hii nimeona tukio hilo limekuwa gumzo mtandaoni.Ilikuwa takriban saa 6 mchana za hapa (hapa saa zitabadilika mwishoni mwa mwezi huu),nikaamua kupoteza muda kwa kuangalia kipindi cha Fox&Friends.Nasema kupoteza muda kwa vile waendesha kipindi hicho huwa wananikera sana kutokana na kauli zao za upendeleo wa wazi kwa wahafidhina na upinzani wao mkubwa dhidi ya Democrats na liberals.Sikujutia uamuzi wa "kupoteza muda" kwani huku watangazaji Steve Doocy na Gretchen Carlson wakishikia bango kauli ya Obama kwamba grandmom wake ni like typical White person,mwenzao Brian Kilmeade aliamua kuondoka kwa muda studioni kutokana na kukerwa na namna wenzie walivyokuwa wakimsakama Obama.Kama hiyo haitoshi,muda mfupi baadaye,mtangazaji mwandamizi wa kituo hicho,Chris Wallace,alionekana hewani wakati Fox&Friends inaendelea ambapo alielezea waziwazi kwamba alikuwa akiangalia kipindi hicho na hakupendezwa na namna kauli ya Obama kuhusu bibi yake ilivyokuwa ikipotoshwa.Wallace alieleza wazi kwamba yeye si msemaji wa kambi ya Obama lakini angependa kuona kipindi hicho kinazungumzia suala hilo ndani ya context,na kwenda mbali zaidi kwa kuwashauri wana-Fox&Friends kuangalia pia habari nyingine za muhimu kuhusu Obama kama vile endorsement ya Bill Richardson na hotuba zake mbili kuhusu uchumi na vita ya Irak.





19 Mar 2008

Makala yangu katika toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema inajaribu kudadisi chanzo cha ufisadi huko nyumbani.Je tatizo ni mfumo unaozaa na kulea ufisadi au tatizo ni watu wanaosabaisha ufisadi na kuishia kutengeneza mfumo haramu wa maovu?Lakini kabla ya kuingia kwenye mjadala huo,makala hiyo imeanza kwa discussion fupi kuhusu kipindi cha BET cha Hip-Hop vs America.Binafsi,nimetafsiri dhima ya kipindi hicho kuwa ni jamii ya Black Americans kujiuliza adui yao halisi ni nani: wao wenyewe au mfumo dhalimu uliotawaliwa na ubaguzi na nguvu za Corporate America.Basi,pamoja na habari na makala nyingine zilizokwenda shule,bingirika na makala hiyo kwa KUBONYEZA HAPA.

18 Mar 2008

Gazeti la Los Angeles Times lina habari kwamba rapa tajiri na maarufu,Sean "P.Diddy" Combs alikuwa na taarifa za ndani kuhusu mpango wa mauaji ya Tupac Shakur aliyepigwa risasi na hatimaye kufariki Novemba mwaka 1994.
Kwa mujibu wa taarifa za kiuchunguzi za gazeti hilo,watu mbalimbali wamethibitisha tuhuma hizo ambazo zimekanushwa vikali na P.Diddy.Itakumbukwa kwamba kifo cha Tupac kinahusishwa pia na mauaji ya rapa mwingine maarufu Christopher Wallace a.k.a. Notorious B.IG. ambacho kinadhaniwa kuwa ni kisasi cha washirika wa Tupac.


                
              Uchunguzi huo wa L.A.Times unadai kwamba sababu kubwa iliyopelekea kuuawa kwa Tupac ni "adhabu" kwa nguli huyo wa rap kukataa kuwa mshirika wa kibiashara wa lebo ya Bad Boy inayomilikiwa na P.Diddy.

Kwa habari zaidi soma habari hiyo ya kusisimua kwa KUBONYEZA HAPA.Hapo chini ni clip ya B.I.G katika track Mo Money Mo Problems akimshirikisha Puff Daddy na Mase


Pia waweza kuangalia track hii hapo chini ya Tupac  f/t The Outlawz (Caution: Very Explicit Lyrics) Hit Em Up ambapo rapa huyo na vijana wake wanatupa "madongo" makali kwa P.Diddy (enzi hizo akijulikana kama Puff Daddy),B.I.G,Lil' Kim,Lil' Cease,Mobb Deep na lebo nzima ya Bad Boy.Ni dhahiri kuwa track hii ilichangia sana kukuza beef kati ya mahasimu hao wa Pwani ya Mashariki na ya Magharibi huko Marekani.



17 Mar 2008

Hebu toa hukumu mwenyewe katika MAKALA HII

16 Mar 2008

Nawazungumzia wahafidhina.Wanafikiri siku zote wao wako sahihi,lakini licha ya fikra hizo mufilisi,wanataka ku-monopolize haki ya kuwa on the right of the political spectrum.And for that matter,Jeremiah Wright,yule livewire cleric wa Barack Obama yuko wrong ilhali right-wing lunatics like Bill O'ReillySean Hannity,Ann Coulter,Rush Limbaugh,ambao wanasifika kwa maneno machafu kupita kiasi,siku zote wako sahihi...according to them.Anyway,that's politics.Soma makala hii kuhusu uhusiano wa Obama na Rev Wright.

15 Mar 2008



OBAMA:On My Faith and My Church. (CLICK THE LINK TO READ THE ARTICLE)

12 Mar 2008

Makala yangu katika toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema inatanua wigo wa uchambuzi kuhusu suala la ufisadi na kuangalia eneo jingine nyeti la ufisadi wa ngono.Umeshawahi kujiuliza ma-miss wangapi wanaletwa jijini Dar kutoka vijijini,wilayani au mikoani kisha kushirikishwa kwenye mashindano ya ulimwende na hatimaye kuachwa mikononi mwa fisi-maji wa ngono?Pamoja nahabari na makala nyingine zilizobobea,bingirika na makala yangu hiyo kwa KUBONYEZA HAPA

11 Mar 2008























Kufuatia Gavana wa New York,Elliot Spitzer,au "Client 9", kukumbwa na skandali la kujihusisha na makahaba,The Huffington Post wametoa wanachokiita (kwa tafsiri yangu) Mwongozo wa Kutumia Huduma ya Makahaba (Prostitution:A User's Manual).Soma Mwongozo huo HAPA (you never know when it might become handy!)

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.