26 Jun 2009


Kwa mujibu wa MZEE WA CHANGAMOTO,Hasheem Thabeet amenyakuliwa na klabu ya mpira wa kikapu ya Memphis Grizzlies katika draft ya NBA.

Hii ni miongoni mwa njia mwafaka-na nafuu-za kuitangaza Tanzania.Kila la kheri Hasheem.Mafanikio yako ni zaidi ya kufanikiwa kimichezo,umeingia kwenye orodha ya vitambulisho vya Tanzania kama vile Mlima Kilimanjaro,madini ya Tanzanite (japo mafisadi wamepania kuyamaliza kama walivyomaliza dhahabu ilivyo huko Tulawaka),Hifadhi ya Selous na vivutio vinginevyo.Kuna cha zaidi kuhusu mafanikio yako.Umevunja "utamaduni" wa Kitanzania wa ku-settle for less.Angalia timu yetu ya taifa,kwa mfano.Tumekuwa na Maximo kwa muda sasa,na wajuzi wa michezo wanatuambia tumepiga hatua.Kupiga hatua kwa kutoka sare na Senegal?Angalia Simba na Yanga,kila msimu wanahangaika na "wachezaji wa kimataifa",lakini huhitaji kuwa mtaalam wa soka kumaizi kuwa ma-pro" hao ni wababaishaji tu na hawajasaidia kuzifanya klabu hizo zitambe katika anga za soka la kimataifa (na tunaambiwa kocha wa Yanga ni profesa wa soka!Lakini msimu wa pili huu hakuna kombe la kimataifa na wana-Yanga wameridhika,sio na mafanikio ya klabu yao bali kuwa na kocha mgeni "profesa wa soka").Angalia baadhi ya mitazamo yetu.Shangwe na vigelegele tukisikia Zeutamu kakamatwa ilhali majambazi wa Kagoda bado wanapeta,na huku tukizugwa kuwa eti ufisadi wa Meremeta na Tangold ni siri za taifa! (Na kweli ni siri maana ni nadra kwa wizi kufanyika hadharani).

Mafanikio yako yanaweza kuwa chachu kwa Watanzania wengine kuondokana na unyonge wa kifikra kwamba kila baya linalotusibu ndio destiny yetu.Na ni kwa namna hiyo ndio mafisadi wanazidi kutufisadi kwa vile wanatambua unyonge na udhaifu wetu wa kukubali matokeo kirahisi.

Hongera sana,Hasheem.Sote tunajivunia jina lako.


Hili ndio "BUNGE LENYE MENO"!Juzijuzi mbunge mmoja wa CCM kaomba Mungu alilaani Baraza la Mawaziri kwa kushindwa kutimiza majukumu yake.Mwingine kadai serikali ina ugonjwa na inahitaji maombezi (na kwa kawaida magonjwa yanayohitaji maombezi ni yale yasiyotibika kama vile ukimwi,nk).Jana mbunge mwingine wa chama hicho tawala amewafananisha mawaziri na mbwa.Na pengine moja ya mambo yatakayokumbukwa zaidi katika historia ya bunge letu tukufu ni jinsi kikao hiki cha bajeti kinavyoonekana "mwiba mkali" kwa mawaziri,at least according to walio mahiri katika kuripoti pasipo kusoma kati ya mistari (reading between the lines).

Sina maneno ya huruma kwa baadhi ya wabunge hawa wa CCM.Ni wanafiki wanaohangaika kutumia vizuri nafasi hizi za mwisho mwisho kujitengenezea mazingira ya kurejea bungeni hapo mwakani.Lakini ili haki itendeke,ni vema kuwatofautisha wanafiki hawa kwa makundi.Kuna kundi la wabunge waliojitokeza mapema (kabla hata ya joto la uchaguzi wa mwakani halijaanza kupanda) kukemea ufisadi na vitendo vingine vinavyokwaza maendeleo ya taifa letu.Sio siri kwamba wabunge kama Selelii,Kimaro,Killango,Mwambalaswa,Mwakyembe na wengineo wamejitokeza kuwa sauti adimu ndani ya CCM dhidi ya ufisadi.Na tunafahamu vituko wanavyofanyiwa na watu walewale wanaopaswa kuwaunga mkono.

Kundi la pili ni la wababaishaji walio njia panda; upande mmoja hawana nia ya dhati ya kupambana na ufisadi au pengine ni sehemu ya mfumo unaodumisha ufisadi,upande mwingine wanafahamu fika kwamba miongoni mwa ajenda za uchaguzi mkuu ujao ni ufisadi na namna wawakilishi wetu walivyoshiriki katika mapambano dhidi ya ufisadi.

Pia kuna makundi mengine mawili: la kwanza linajumuisha wababaishaji wanaokwenda bungeni kwa vile tu ndio mahala pao pa kuchuma shs 7,000,000/= za mshahara kiulaini.Hawachangii hoja,hawaongei lolote japo si mabubu,wapo wapo tu.Kuwepo au kutokuwepo kwao bungeni hakutambuliki kwa vile wanaongeza tu idadi ya wabunge.Kundi la pili ni la watetezi wa ufisadi.Hawa ni wepesi wa kuomba mwongozo wa Spika kila maslahi yao au ya wadau wenzao wa ufisadi yanapoguswa.Nadhani mmesikia "Dokta" Mzindakaya alivyotumia Maandiko Matakatifu kutetea ufisadi .Ila hawa wanaocheza na vitabu vya Mungu,nadhani ndio wanaostahili kulaaniwa zaidi kwani wamevigeuza kama manifesto za usanii wao wa kisiasa!

Uzuru wa makundi haya mawili ya mwisho-la tatu na la nne-ni kwamba angalau yanajumuisha wabunge tunaofahamu wanaposimamia.Aidha ni wazembe na mabubu wasioongea (aidha kwa aibu ya kuongea,au "heri mie sijasema",au uzembe tu) au ni watetezi wa mafisadi.Hawa si wanafiki as such kwa vile wameji-identify kwetu kuwa ni viumbe wa namna gani.

Tofauti kati ya makundi hayo ni ndogo mno contrary to inavyosomeka na kusikika kwenye vyombo vya habari.Hapa nataka kuzungumzia makundi mawili ya mwanzo-la kwanza na la pili.Hawa wote ni wana CCM,na kwa namna yoyote ile hawawezi kujitenganisha na matatizo yanayosababishwa na chama hicho tawala.Na hili si la kufikirika kwa sababu tayari wengi wa wabunge wa kundi la kwanza wamekuwa wakikumbana na kadhia mbalimbali kutokana na msimamo wao dhidi ya ufisadi,na guess what,kadhi hizo ni kutoka kwa wenzao ndani ya CCM.

Mawaziri wanaolaaniwa na kufikia hatua ya kuitwa mbwa wanatoka CCM pia.Hii sio vita ya wenyewe kwa wenyewe kama inavyoweza kutafsiriwa kiuzembe.Huu ni unafiki,period.CCM isingefika hapo ilipo laiti "wapambanaji hawa" wangekuwa na mkakati wa dhati wa kuleta mabadiliko ya kweli.Wanachofanya muda huu ni cha kibinafsi zaidi kuliko kitaifa.Wanaweza kurudi bungeni hapo mwakani baada ya wapiga kura wao "kuzugika" na CVs za wawakilishi wao tangu 2005 hadi 2010.Kurudi kwao bungeni kutapelekea CCM kuendelea kuwa yenye wabunge wengi bungeni,na hivyo kupelekea kuendelea kwa haya tunayopigia kelele kila siku.

Siamini kama kuna mkakati kwa Selelii na wenzake kuleta mageuzi ndani ya CCM.So far,kelele zao hazijasaidia kukitenganisha chama hicho na ufisadi,implying that kelele zao zimebaki kuwa kelele tu.Wana options mbili: waendelee kupiga kelele lakini wabaki kuwa sehemu ya chama kinachohusishwa na ufisadi au wajondoe ndani ya chama hicho na hivyo kubainisha kuwa kuwa kwao ndani ya CCM ilikuwa ni sehemu tu ya maisha yao ya kisiasa lakini cha muhimu zaidi kwao ni Tanzania na ustawi wa Tanzania.Yes,si lazima kuwa mbunge wa CCM ili kupata fursa ya kupigania maslahi ya taifa.Mifano hai ipo;Dkt Slaa,Zitto Kabwe,nk sio wabunge wa CCM,lakini sote tunafahamu michango yao katika kupambana na ufisadi.

Unafiki wa wabunge hao wa CCM unasababishwa na kitu kimoja kisicho na msingi: UBINAFSI WA KISIASA.Ni hivi,kwa CCM,umoja na mshikamano ndani ya chama hicho ni muhimu zaidi kuliko umoja na mshikamano wa taifa.Na hilo ni matokeo ya chama hicho kuamini kwamba ni chenyewe tu kinachoweza kudumisha mshikamano na umoja wetu.Kwa lugha nyingine,kimebinafsisha uwezo,dhamira,jitihada na nguvu za Watanzania zaidi ya milioni 35 ambao si wanachama wa chama hicho (takwimu za karibuni zinaonyesha idadi ya wanachama wa CCM ni takriban milioni 4 tu).Japo ni kweli kwamba chama hicho kimetoa uongozi uliosaidia kudumu kwa amani na mshikamano huo,Watanzania wenyewe ndio waliofanya kazi ya msingi zaidi kufanikisha hilo.Upendo na upole wetu (ambao mara nyingi umeishia kutumiwa vibaya na wanasiasa walafi) ndio sababu kuu ya kwanini tumeendelea kubaki kisiwa cha amani (kwa maana ya kutokuwa vitani).

Ni ubinafsi wa kisiasa unaopelekea CCM kuweka mbele maslahi ya kisiasa badala ya maslahi ya taifa.Sote tumeshuhudia mara kadhaa wabunge wa chama hicho tawala wakiitisha vikao "vya kuwekana sawa" kila zinapojiri hoja nzito bungeni.Kuwekana sawa kwa maslahi ya nani?Hivi cha muhimu ni hoja ipite tu au ipite ili ilete mabadiliko chanya kwa wananchi?

Lakini ili upate mfano sahihi zaidi kuhusu ubinafsi wa wabunge hawa ni pale Dkt Slaa alipotamka bayana kwamba mishahara ya wabunge ni mikubwa mno kulinganisha na hali halisi ya uchumi wetu.Kwa umoja wao (huku wakipata sapoti kutoka kwa wabinafsi wengine waliojificha kwenye vyama vya upinzani) walimzomea Dkt Slaa na kumzongazonga kana kwamba kawatukana.Hivi ina maana wabunge hawa wanaotuzuga kuwa wanatetea maslahi yetu hawaelewi kuwa wakati wao wanazawadiwa takriban shilingi 7,000,000/= mwezi (wastani wa shilingi laki 230,000/= kwa siku sawa na takriban shs 10,000/= kwa saa) takriban Watanzania 36,000,000 wanaoishi kwa chini ya shilingi 3000/= kwa siku?

Hadi kufikia tamati yake na mabiloni kadhaa kutumika,kikao hiki cha bajeti kitashuhudia kila aina ya vituko kutoka kwa wanafiki hawa.Ukidhani hizo dua dhidi ya mawaziri na "matusi" ya kuwaita mbwa ndio hatua kali kabisa,subiri usikie "makombora" zaidi.Na kama kawaida ya vyombo vyetu vya habari,kurasa zitapambwa na maneno mazito kama "Bunge moto juu","Wabunge wachachamaa",na ubabaishaji mwingine kama huo.Lakini pamoja na yote hayo,makadirio ya wizara za mawaziri wanaoombewa dua mbaya na kuitwa mbwa yatapitishwa na wabunge haohao wanaotuzuga kuwa "wana hasira na mawaziri".

25 Jun 2009


Breaking News hii ni kwa mujibu wa TMZ.COM ambapo wanaeleza
Michael Jackson Dies

Posted Jun 25th 2009 5:20PM by
TMZ Staff

We've just learned Michael Jackson has died. He was 50.
Michael suffered a cardiac arrest earlier this afternoon at his Holmby Hills home and paramedics were unable to revive him. We're told when paramedics arrived Jackson had no pulse and they never got a pulse back.

A source tells us Jackson was dead when paramedics arrived. A cardiologist at UCLA tells TMZ Jackson died of cardiac arrest.

Once at the hospital, the staff tried to resuscitate him but he was completely unresponsive.
We're told one of the staff members at Jackson's home called 911.La Toya ran in the hospital sobbing after Jackson was pronounced dead.Michael is survived by three children: Michael Joseph Jackson, Jr., Paris Michael Katherine Jackson and Prince "Blanket" Michael Jackson II.

Story developing...

24 Jun 2009

Pichani,Berlusconi akijifuta jasho baada ya kutwanga swali kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga kuhusu tuhuma zinazoweza kuotesha nyasi ndoa yake na mkewe anayeonyeshwa kwenye background.

Waziri Mkuu wa Italia,Silvio Berlusconi,amekanusha madai kwamba alinunua huduma ya tendo la ndoa kwa changudoa mmoja,Patrizia D'Addario.Kiongozi huyo machachari na mwingi wa vituko,anakabiliwa na shinikizo la kisiasa kufuatia madai hayo ya kujimwayamwaya na kimada aliyekuwa miongoni mwa waliohudhuria pati iliyoandaliwa na Berlusconi.

Hadhi ya mwanasiasa huyo tajiri imekumbwa na migogoro lukuki,na hivi karibuni alikuwa na tuhuma za kuvunja amri ya sita na binti wa miaka 18,Noemi Letizia (pichani chini)


Kwa jeuri,Berlusconi amekanusha madai ya kununua ngono huku akikisitiza kwamba "Sijawahi kuona raha ya kununua ngono badala ya ujasiri wa kutongoza".
Vyama vya upinzani pamoja na Kanisa Katoliki wanamtaka Berlusconi kujieleza kuhusiana na skandali hiyo iliyoibuliwa na tume moja ya kuchunguza rushwa huko Italia ya kusini,ambapo inaelezwa kwamba kimada mhusika (kushoto,pichani chini) aliieleza tume hiyo kuwa alilipwa na Berlusconi ili kumpa huduma ya ngono na ana mkanda uliorekodi tukio hilo.

Yote haya yanajiri wakati mke wa Waziri Mkuu huyo akiwa kwenye taratibu za kuomba talaka huku akimtuhumu mumewe kwamba anapendelea sana dogodogo.

CHANZO: itn

Na sie tungekuwa na uhuru wa kuweka ishu kama hizi hadharani,sijui nani angesalimika among vingunge wetu!

Kontebo wa Polisi,Tariq Dost (pichani juu) amefungua mashtaka dhidi ya mwajiri wake na Mamlaka ya Polisi ya eneo la Midlands,hapa Uingereza, kutokana na matamshi ya mwaka 2007 kwamba anafanana na gaidi nambari wani Osama bin Laden (pichani chini).Nadhani kisa ni huo "mzuzu".Je wanafanana?
CHANZO: The Daily Mail


Slaa up in arms on 'silencing' in House
By Faraja Jube Dodoma

Karatu MP Willibrod Slaa has threatened to "go public" with what he said were issues of national interest the Parliament blocked him from tabling in the august House on Monday.

Some MPs heckled the firebrand opposition leader as he stood up in parliament on Monday to give a speech on the Prime Minister's Office 2009/10 Budget.

Dr Slaa had reportedly prepared a vitriolic attack on former President Benjamin Mkapa and the Government over alleged mismanagement of funds.

Before giving his speech, the Chadema leader was reminded to respect the Parliamentary Standing Orders and warned not to breach the law in his presentation.

But in an interview with The Citizen yesterday, Dr Slaa said the National Assembly Speaker, Mr Samwel Sitta, had no right to block debate on sensitive public issues.

He said: "I have written to the Speaker asking him why unnecessary restrictions are being imposed on MPs who want to discuss matters of public interest in parliament."

He threatened to go public with the same issues he was barred from presenting in parliament saying he had the right to let people know about matters that affected them.

"If they don't want us to speak in parliament, it will reach a point where the only reasonable thing to do is table the agenda to the people," said Dr Slaa.

CCM MPs accused the opposition legislator of attempting to use the platform to launch a verbal attack against Mr Mkapa.

Mr Mudhihir Mudhihir (Mchinga-CCM) defended the former president saying he had done "a lot of good things but people want to see the negative only".

"It was under his leadership that this country recorded significant increases in Government revenue," the MP said, praising Mr Mkapa's administration for containing inflation and opening a number of trade opportunities.

Another CCM legislator, Dr Chrisant Mzindakaya (Kwela), tried to have Dr Slaa blocked from presenting his speech at all.

But even when he finally gave his speech, the opposition leader was forced to skip tabling his prepared questions on controversial deals the Mkapa administration allegedly signed.

And in an apparent reference to Dr Slaa, Dr Mzindakaya lashed out at "jealousy hypocrites and good-for-nothing crusaders against corruption".

"Those who criticise Mr Mkapa are agents of the Devil and loafers who have done nothing in life, but are motivated by jealousy and hatred. They are themselves corrupt people," he said.

But Dr Slaa insisted he would not relent on the issues he was barred from talking about saying the Constitution and Parliamentary Immunities and Privileges Act guarantee MPs the freedom to challenge the Government in the parliament.

"I will not accept such moves by anyone any more. This is all compromising principles. But I will stand up for my principles and for justice. We all have the right voice our concerns," he said.

Dr Slaa, who had prepared his disputed speech as a shadow minister, said the Government was obliged to respond to all queries raised by MPs in parliament.

"Even if the issues are sensitive, this is the whole purpose of raising them so that people can know and be informed about what is going on," he said.

"But there has been a tendency to block all sensitive issues from being discussed in parliament," he added.

Before he gave his controversial speech, Mr Sitta told the opposition MP he had read the speech and warned him against making statements that breached parliamentary regulations.

The Speaker had also ordered Dr Slaa not to use abusive language against a former president or discuss issues that had been lined for debate during the session.

Earlier, the chairman of the Parliamentary Committee on Justice, Constitutional Affairs and Governance, Mr George Lubeleje, a CCM MP, had tabled the committee's position against Dr Slaa's speech.

However, the opposition leader retorted: "Why must I have any confidence in the committee or Speaker's office if they insist on imposing on us?"

He questioned the Speaker's application of the Parliamentary Standing Orders to the contentious issues of Meremeta, Tangold, Mwananchi and Deep Green Finance companies.

Last Friday, Dr Slaa asked the Government to respond to allegations of funds mismanagement involving the four companies that have become subjects of public debate.

"I was just questioning the Government over the embezzlement of Sh155 billion in Meremeta and not about the issues pertaining to national security," he said.

Mr Sitta postponed the debate to this Monday saying the Government should be given time to prepare its response.

But Dr Slaa also questioned the Parliament barred debate on the CAG report. "Where does the Speaker obtain the directive to block the debate?"

On the PMO's 2009/10 Budget estimates, the Chadema leader queried the allocation of billions of shillings to entertainment and hospitality, which he said had nothing to do the welfare of people.

He had to put up with sporadic interventions, mainly from Mr Philip Marmo, the minister of State in the President's Office (Good Governance), who also serves as coordinator of parliamentary activities.

Mr Marmo wanted, among other things, the Speaker to reprimand Dr Slaa for his reference to the amount of funds set aside for particular votes in the Government's Budget.

However, Mr Sitta said there was nothing wrong with the MP debating the Government's budget priorities.


SOURCE: The Citizen


Kama hujawahi kuhudhuria matamasha au maonyesho ya wasanii wetu huko Bongo,wala usidhani ume-miss raha pekee.Kuna karaha pia,hususan ile inayotokana na mastaa wetu kudekezwa kupita kiasi na vyombo vya dola.Kwa kifupi,huko ni bangi nje nje,wasanii hugeuka madikteta wanaoweza kufanya lolote lile hadharani ikiwa pamoja na unyanyasaji wa waziwazi dhidi ya dada zetu.Na baada ya "unga" kugeuka "kilevi cha kawaida",wengi wa wasanii hao hujitundika madawa hayo vya kutosha pasipo hofu ya kuchukuliwa hatua na vyombo vya dola.

Nadhani wapo wanaokumbuka msanii mmoja wa bongefleava aliyekamatwa na bangi katika mkoa mmoja wa nyanda za juu kusini.Ni Daz Baba wa kundi lililokuwa likijulikana kama Daz Nundaz.Iliishia kuwa amekamatwa tu,wala hakukuwa na taarifa za msanii hiyo kufikishwa mahakamani au hata kupewa onyo (si lazima kila kosa limaanishe kifungo).

Twende kwa baadhi ya marapa maarufu Msafiri Diouf na Banza Stone.
Haihitaji upelelezi kujua kuwa wanatumia kilevi haramu,lakini dola haijihangaishi kuwachukulia hatua ambazo licha ya kuwaadhibu zingesaidia pia kuokoa maisha yao kwani ni dhahiri kwamba mwisho wao sio mzuri.

Kuna msanii anaitwa Chid Benz.

Licha ya sifa yake ya kufanya vizuri zaidi anaposhirikishwa kwenye nyimbo za wasanii wengine (wanaita "kolabo" as corruption ya neno collaboration) zaidi ya nyimbo zake mwenyewe,mwanabongofleva huyo ni maarufu pia kwa vurugu na vipigo kwa wasanii wenzie.Dola imeendelea kumwangalia tu,hali inayoweza kupelekea Chid Benz kuamini kuwa yuko juu ya sheria kutoa kipondo kwa yeyote yule anapojiskia kufanya hivyo.

Leo,kwenye tovuti ya Global Publishers kuna habari kwamba msaanii Khaleed Mohammed,almaaruf T.I.D,amemjeruhi mwanafunzi mmoja wa kike baada ya kumshushia kipigo cha nguvu.Kwa mujibu wa tovuti hiyo,T.I.D nasakwa na polisi na "hajulikani alipo".Nisingependa kutoa hukumu kwa vile mie si mahakama,lakini napenda kukiri kwamba nilishangazwa na habari kwamba msanii huyo alikuwa miongoni mwa waliopewa msamaha na Rais katika maadhimisho ya siku flani ya kitaifa.

Sikushangaa kwa vile aliyesamehewa ni T.I.D,bali vigezo vilivyotumika kumpa msamaha huo.Kwa tunaofahamu ukweli kuhusu kesi hiyo,yayumkinika kuwa maombi ya msahama ya mtenda kosa kwa waliotendewa kosa yalisikilizwa,na kwa vile waliotendewa kosa ni "wenye kuwezesha jua liwake au lisiwake",yaani "the powers-that-be",msanii huyo akajumuishwa kwenye msamaha wa Rais.

Tukio hili la sasa ambapo T.I.D amerejea kosa lilelile lililompeleka jela in the first place,sio tu linazidisha hisia kuwa wengi wa wasanii na mastaa wetu wanaringia ugoigoi wa wanadola wetu katika kuchukua hatua inapostahili,bali pia ni fedheha na aibu kwa suala zima la msamaha wa rais.Navyofahamu,msamaha huo huzingatia tabia ya mfungwa,afya yake,idadi ya siku zilizosalia katika kifungo chake,na pengine kikubwa zaidi,mwenendo wake pindi akipewa msamaha huo.

Ni dhahiri kwamba jinsi jeshi la Magereza "lilivyojichokea" si rahisi kwake kukamilisha vigezo hivyo vyote.Na katika jamii ambayo mwenye fedha ni mithili ya mungu-mtu huku ufisadi ukishamiri kila kukicha,yayumkinika kuamini iwamba misamaha ya rais imekuwa ikitumika ndivyo sivyo.

Hivi tunajenga jamii ya aina gani?Wkati wenzetu katika nchi zilzoendelea wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kudhibiti uvutaji wa sigara katika maoneo ya mikusanyiko,sie tunaelekea kuruhusu uvutaji wa bangi kana kwamba ni kitu halali.Nilisoma mahala flani kwamba msanii mmoja wa filamu za kibongo alichomoa bastola hadharani kisa wapita njia walimlalamikia kwa kupaki gari lake barabarani.

Jeuri hii wanaipata wapi?

Hypothesis yangu ni hii: itikadi ya ujamaa iliifanya sehemu kubwa ya Watanzania kuwa wanyonge wasio na stahili ya kuwa karibu na makundi yenye nguvu au mvuto kwenye jamii hiyo e.g. wanasiasa,wasanii,nk.Japo tunadai kuwa ujamaa umekufa,mentality ya itikadi hiyo bado iko hai na inatuathiri katika namna tunavyodili na watu hao walio kwenye "makundi maalumu" kwa mfano "mastaa wetu".Polisi wa trafiki anajiuliza mara mbilimbili "kuipiga mkono" Benz au Vogue,kwa vile akilini mwake,dereva wa gari hilo ola thamani anaweza "kuhatarisha ajira yake".Mtaani,msanii anageuka "mungu-mtu",wananchi wanatamani kuwa karibu nae,angalau kugusana mabega nae,wanadola wanachelea kumchukulia hatua (pengine kwa kudhani kuwa kwa vyovyote vile msanii hiyo atakuwa na connection na mtoto wa kigogo flani),na upuuzi mwingine kama huo.

Sio kwamba ujamaa ni mbaya per se.Kuna mazuri flani,ila hapa nimezungumzia legacy ya itikadi ya ujamaa katika upande hasi.Pengine kunahitajika mjadala wa kitaifa kutafakari mambo kama haya.

UNAONAJE?

23 Jun 2009

Pichani,Mwanasoshojia akimuaga Mzaa chema.

BLOGU HII INATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKANA NA KIFO CHA MAMA MZAZI WA BLOGA MWANASOSHOLOJIA.HAKUNA MANENO MWAFAKA YANAYOWEZA KUKULIWAZA WEWE BINAFSI NA FAMILIA YENU KWA UJUMLA,LAKINI TUAMINI KUWA MUNGU AMEMPENDA MAREHEMU ZAIDI YETU,NA NDIO MAANA AMEMCHUKUA.NA KWA VILE MUNGU NI WA UPENDO,BASI TUNA HAKIKA ATAMPATIA MAREHEMU PUMZIKO LA AMANI NA RAHA YA MILELE.

POLE SANA,MWANASOSHOLOJIA.

Dunia haina dogo.Kuna wambeya wanaodai eti huyo "nzi" alikuwa ni skadi lililotumwa na Dick Cheney kwa Obama.Kuna wengine wanadai huyo wala hakuwa "nzi" bali roboti lilotengenezwa na majasusi wa Kimarekani kupeleka ujumbe kwa Kim Jong Ill na mikwara yake ya nyuklia.Wapo wanaomhusisha "nzi" huyo na uchaguzi wa Irani..... Alimradi burudani!

ELEKEZO: Neno "nzi" limetumika kama tafsiri isiyo rasmi ya "fly" (BAKITA mko wapi?)


Inakera ati!hususan kwa simu vimeo zinazokula chaji kama hazina akili nzuri.Wajuzi wa simu wanadai kwamba baadhi ya simu "zina allergy na full charge",yaani chaji haidumu.

Taarifa zinaeleza kwamba maabara ya Kampuni ya Nokia hapo Cambridge wanatafiti ujio wa simu itakayokuwa ikijichaji yenyewe.Badala ya kutumia chaja za kawaida,simu hiyo itakuwa ikijichaji kwa kugema nishati kutoka kwa mawimbi ya radio (radio waves) yanayotoka kwenye antena,milingoti ya televisheni,Wi-Fi transmitters,nk.

CHANZO: The Guardian

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.